Nguvu walizokuwa nazo wale watu waliomvamia Liam zilitokana na kiapo cha kale cha giza kilichoitwa “The Veil of Umbros” — agano la kale la wachache waliotamani nguvu za haraka kwa gharama ya nafsi zao.
The Evil Umbros ilikuwa ni mkataba wa kipepo uliosainiwa na roho zao mbele ya mwanazuoni wa giza aitwaye Kael’Thun, zaidi ya miaka 300 iliyopita. Agano hilo lilitoa nguvu zisizo za kibinadamu — nguvu za kasi, uzito wa miguu mithili ya chuma, na uwezo wa kushambulia kwa moshi wa giza,, moja kati ya kanuni za nguvu zao
"Wakishindwa kupambana au kujeruhiwa vibaya, mwili wao huzuiwa kurudi kuwa wa kawaida.
Pia Wakifa, mwili wao unageuka kuwa jiwe la kipekee — liitwalo “Garnyx Stone” — ambalo linahifadhi sehemu ya nguvu za agano hilo.
Kwa hiyo, wale watu waliomvamia Liam walikuwa ni watu kutoka kundi linalo tokea Korea liitwalo “The Covenant of Nyx,” kundi la giza lililoingia agano la The Veil of Umbros, wakitumika kama watendaji wa kazi chafu za kutafuta vitu vya kale— ili wapeleke kwa mabwana wao.
Sababu ya wao kugeuka mawe: Agano hilo liliwalinda dhidi ya kifo cha kawaida, lakini pia liliwatia laana ya milele: wakifa, roho zao hushikwa ndani ya mwili uliogeuka kuwa jiwe, ili wasiweze hata kuingia kuzimu au kuishi tena.
Na kwa vile miili hiyo ya mawe huhifadhi chembechembe za nguvu, makundi ya giza hujaribu kuyachukua tena na kuyatengeneza upya kwa uchawi wa kale.
Liam alikua na uzoefu na watu wa aina hiyo kwani sio mara yake ya kwanza kukutana na watu wa aina hiyo hivyo alijua namna ya kudili nao kilahisi ndio maana hawakumpa.shida pia alijua njia ya kuharibu kabisa Garnyx Stone — kwa kutumia maneno ya kale ya Nadharia ya Mwisho (Final Doctrine), ambayo huharibu chembechembe zote za uchawi zilizobebwa na miili ile baada ya kugeuka mawe
Ila watu kama hao pindi wanapo kutana na watu wa kawaika ata kama wanamafunzo ya kimapigano kiasi gan ningumu sana kuwashinda
Usiku huo Liam aliludi Hotel akiwa ametulia kimya. Walinzi wa lango walimfungulia bila kuuliza chochote. Mvua ndogo ilikuwa imenyunyiza barabara za Masaki, ikiacha sakafu ya vioo kwenye maegesho ya magari.
Alipofika ukumbini, akajielekeza moja kwa moja kwenye mgahawa wa hoteli. Alikaa kwenye kona ya ndani, karibu na dirisha lililotoa mwanga mwepesi wa taa za barabarani. Alijitakia sahani ya wali wa nazi na samaki
Wakati akila, hakuwa na wasiwasi tena. Moyo wake ulionekana kuwa katika hali ya utulivu wa ajabu, licha ya yote yaliyotokea masaa machache kabla.
Alipomaliza kula, akapanda juu chumbani kwake. Akajimwagia maji ya moto bafuni, kisha akavaa tracksuit na kujilaza kitandani. Mwili wake ulikuwa umechoka, lakini akili yake ilikuwa bado inachakata. Licha ya kelele za maisha za Dar es Salaam nje ya dirisha lake, yeye aliishi ndani ya kimya chake.
“Dar es Salaam… ni jiji linalocheka, lakini lina mengi linayoficha,” alijinong’oneza kabla ya macho kufunga.
----------
Siku iliyofuata, jua lilipoanza kupenya kwenye mapazia ya chumba chake, Liam aliamka mapema. Alioga, akavaa fulana nyeupe safi, suruali ya kitambaa laini, na viatu vyepesi vya ngozi.
Alishuka chini kwa kifungua kinywa,alikutana na Edina — msichana wa mapokezi — alimsalimia kwa tabasamu pana.
“Habari za asubuhi, Liam,” alisema Edina kwa sauti yenye uzuri wa kawaida.
“Habari nzuri Edina. Sijui kama ni wewe au kahawa zenu, lakini kila nikikuona nahisi siku yangu inaanza vizuri,” alisema Liam kwa utani.
Edina alicheka, akatikisa kichwa.
“Utaanza kunibebesha majivuno sasa.”
“Majivuno yanastahili mrembo kama wewe mwenye tabasamu la dhati,” alisema Liam huku akimkazia macho, lakini kwa namna ya utulivu.
Baada ya kifungua kinywa, Liam aliamua kutoka nje, kutembea kidogo katikati ya Masaki. Aliingia kwenye maduka kadhaa, akanunua miwani ya jua, fulana mbili, na kikombe cha kahawa katika duka moja dogo la pembeni ya barabara.
Alitembea hadi Coco Beach, akakaa kwenye mnazi, akatazama bahari. Alizungumza na vijana wawili waliokuwa wanauza mishikaki.
Liam alikua kashaanza kulizoea jiji — si kwa macho ya mgeni tena, bali kwa moyo wa mtu anavyojitafuta. Siku nzima aliimalizia akiwa Beach
Jiji lilimzoesha, lakini hakuweza kuzoea kukaa bila kufanya jambo lolote. Licha ya ukweli kwamba alikuwa na pesa ya kutosha kuendelea kuishi maisha ya kifahari katika Lush Bay Hotel ya Masaki, moyoni alihisi shimo tupu — kama roho yake ilikua inahitaji kitu zaidi ya starehe: kitu cha kufanya. Kitu kitakachomfanya ahisi tena.
Aliporudi hotelini usiku mmoja baada ya kutoka matembezini, aliingia moja kwa moja chumbani, akafungua laptop yake kuangalia habari za hapa na pale. Wakati huo, hakutafuta chochote maalum. Lakini kama kawaida ya ulimwengu wa leo — kila mtu hufuatiliwa — tangazo moja lilijitokeza upande wa kulia wa skrini yake, kwa sauti isiyoandikwa bali inayoonekana kusema: “Looking for something real?”
Tangazo hilo lilionyesha picha ya walinzi waliovaa sare nadhifu, wakiwa na nembo iliyoandikwa “ Royal Shield Security” — kampuni ya ulinzi binafsi. Chini yake, maandishi yalisomeka:
> “Do you have what it takes to stand between danger and safety? Join Royal Shield Security.. We’re not just guards, we’re guardians.”
Liam alicheka kimya kimya.
"Guardians? Mko mbali sana na ninacholinda mimi." Alisema Liam kwa kejeli ya taratibu, lakini alihisi mvuto wa ajabu kuelekea tangazo hilo.
Aliibonyeza link. Tovuti ilifunguka. Kulikuwa na fomu rahisi ya maombi ya kazi, maelezo mafupi kuhusu kampuni, na kigezo cha kuwa “mwenye uwezo wa kipekee wa kutambua hatari na kushughulika nayo kwa weledi na usiri.”
Alikaa kimya kwa sekunde kadhaa, macho yake yakisoma mistari ile bila kuyumbisha.
"Inaonekana dunia hii haiko tofauti sana na ile niliyozoea... watu bado wanahitaji kulindwa." Alisema kwa sauti ya kutafakari.
Hata hivyo, hakuwa tayari kujiingiza haraka. Kama kawaida yake, Liam hakufanya maamuzi ya papara.
Aliifunga laptop na kulala kifudifudi kitandani, macho yakitazama dari huku masikio yake yakisikiliza sauti ya kiyoyozi na kelele za mbali za magari ya barabarani.
Ilikua ni Asabuh, jua la Dar es Salaam lilichomoza taratibu likiangaza kuta nyeupe za Lush Bay Hotel. Kwenye ghorofa ya tano, Liam Carter alikuwa tayari ameshaamka. Akiwa amevaa t-shirt nyeupe na suruali fupi ya kijani kibichi, alikaa kwenye meza ya kona ya chumba chake, kikombe cha kahawa mkononi na laptop mbele yake.
Aliikumbuka tovuti aliyoiangalia usiku uliopita — Royal Shield Security. Bila kusita tena, aliiwasha laptop na kufungua ukurasa ule ule. Safari hii hakusita. Akaingia moja kwa moja kwenye fomu ya maombi.
Aliandika jina lake:
Liam Carter.
Tarehe ya kuzaliwa?
Akaleta tarehe ya kubuni — iliyomfanya aonekane kama kijana aliyekomaa lakini bado mwenye nguvu.
Uraia?
Tanzania
Uzoefu?
Hapo ndipo alipotulia kidogo, macho yake yakikodolea sehemu ya "Experience in Security or Military Background."
"Kwa kuwa huu ni mchezo wa kivuli, ni lazima nivae kivuli hicho sawasawa." Alisema Liam kwa sauti ya kujinong’oneza.
Liam kutokana na kuanmtaalam aliamua kufoji vitu vingi kupitia koneshen zake aliweza kufoji kua aliwahi kua mwanajeshi wa nchi ya malekani
Aliendelea kuandika kwa ufasaha kana kwamba alikuwa ameishi hayo maisha. Kwa namna alivyoandika, hata mtu mwenye akili ya kuchambua wasifu angeamini. Alimalizia fomu kwa kuambatanisha picha ya pasipoti (ambayo pia ilikua ya bandia lakini yenye uhalisia wa hali ya juu), kisha akabonyeza SUBMIT.
Kompyuta ilitoa mlio wa “Ping!” na ukurasa mpya ukajitokeza:
> Thank you for your application, Mr. Carter. Our recruitment team will review your submission and contact you shortly.
Liam alicheka kidogo.
"Wakijua ukweli, watanitaka zaidi — si kunikataa." Alisema Liam huku akiinyanyua kahawa yake na kunywa kwa utulivu.
Aliinuka, akafungua pazia na kuangalia bahari kwa mbali, macho yake yakimetameta kwa utulivu wa mtu asiyeeleweka kiurahisi. Hakuwa amejaza fomu ya kazi kwa sababu ya pesa. Alikuwa anatafuta kivuli kipya cha kuishi ndani yake — na kwa sasa, kazi ya mlinzi ilimfaa kwa kuendelea kuzugia na angalau itamfanya kua bize
Baada ya kutuma maombi ya kazi ya ulinzi, Liam Carter alijiegemeza kwenye kiti chake akitazama skrini ya laptop kwa muda. Akavuta pumzi ndefu, kisha akakunja vidole vya mikono yake kama mtu anayefikiria jambo zito.
"Kama nataka kuishi maisha ya kawaida... siwezi kuendelea kuishi hotelini milele Alinong’ona
Alichukua simu yake na akaingia mtandao pedwa wa Instagram nakuamua kutafuta dalali wa nyumba lakinai aliwezq kukutana na kampuni inayo jihusisha na uuzaji wa nyumba hivyo Alifungua programu ya WhatsApp Business ya kampuni ile, akaandika ujumbe moja kwa moja kwa wakala:
> Hello. I’m looking for a luxurious house to purchase in Dar es Salaam. Preferably private, spacious, and secure. Budget is flexible. Contact me as soon as possible.
Dakika tatu baadaye, akajibiwa:
> Karibu sana Haraka Realty. Tunaweza kukusaidia bila tatizo. Tutahitaji baadhi ya taarifa zako na pia kukutumia chaguo chache za nyumba kulingana na vigezo vyako. Tuanze na location gani unapendelea?
Liam akaandika:
> Somewhere serene but close enough to the city. Masaki, Oysterbay, or even Bahari Beach if the property is right.
Simu yake ikatoa mlio wa video na picha — nyumba tatu za kifahari zenye uzio wa kisasa, mabwawa ya kuogelea, maegesho ya magari manne, na bustani za kijani kibichi. Moja yao ilikuwa ya kuvutia hasa. Ghorofa mbili, mlango wa mbele wa glasi nzito, na veranda iliyoangalia bahari.
Aliitazama kwa makini.
“Hii inaweza kuwa ngome yangu kwa muda.” Alisema kwa sauti ya chini.
Kisha akaandika:
> That third one. I want to view it in person. Can we schedule it for tomorrow morning?
> Absolutely. We’ll send one of our agents to pick you up from your location. Just share the details.
Liam alitabasamu. Hatua kwa hatua, alianza kujenga kivuli kipya cha maisha. Sehemu ya kuishi. Kazi (angalau kwa jina). Na taratibu, mizizi ya historia mpya ilianza kuchomeka katika ardhi ya joto ya Dar es Salaam.
**********************
Kesho yake, Liam aliamka mapema kabla hata ya jua kuchomoza vizuri. Alivaa shati nyeupe safi na suruali ya khaki, akavaa miwani yake meusi na viatu vya ngozi vilivyoonekana kama vile havijawahi kukanyaga vumbi. Saa moja kamili, ujumbe uliingia kwenye simu yake kutoka kwa wakala wa Haraka Realty:
> Good morning Mr. Carter. Our agent is on the way to pick you up. ETA: 10 minutes.
Liam aliteremka chini ya Lush Bay Hotel akiwa mtulivu. Edina alikuwa zamu ya mapokezi, akamtazama kwa macho ya udadisi.
“Una safari ya mapema leo?” Aliuliza kwa tabasamu.
“Kidogo tu. Nataka kuona kama Dar inaweza kuwa nyumbani,” alisema Liam kwa sauti ya utulivu, kisha akaondoka bila kuongeza neno.
Gari jeusi aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilimsubiri nje. Mtu mmoja wa kiume, mwenye suti nyeusi, akashuka na kumfungulia mlango.
“Mr. Liam? I’m Raymond from Haraka Realty. Karibu.” Alisema kwa sauti ya kutolidhidhwa na liam
Safari haikuchukua muda mrefu. Kwa maana seemu ambayo nyumba hiyo ilikuepe ni masaki hapo hapo. Mwisho walifika kwenye geti kubwa la kijani, lililokuwa na alama ya metali: “Villa Nyota.”
Geti lilipofunguliwa kwa rimoti, gari likaingia taratibu ndani.
Nyumba aliyokuta... haikuwa ya kawaida.
Ilikuwa ni gorofa la ghorofa mbili lililosimama kwenye ekari moja ya ardhi. Juu ya paa lake palikuwa na balcony pana inayoangalia bahari. Mlango wa mbele ulikuwa wa mbao nzito ya mninga, ukifunguka kwa mzunguko mlegevu wa kisasa. Sakafu ya ndani ilikuwa ya marumaru meupe yaliyong’ara, ukuta ukiwa na uchoraji wa sanaa ya Kiafrika na viti vya kifahari vya ngozi.
Kulikuwa na vyumba vitano vikubwa, kila kimoja kikiwa na bafu lake binafsi. Kulikuwa pia na studio ndogo ya ndani, ofisi, chumba cha mazoezi, na basement ndogo ya starehe.
"Nimewahi kulala hotelini, lakini hapa... hapa panapumua." Alisema Liam kwa utulivu, macho yake yakizunguka chumba kikuu cha wageni.
Raymond akacheka. "Ni mojawapo ya nyumba bora tulizonazo. Imejengwa kwa mteja aliyeghairi kununua dakika ya mwisho. Unaweza kuichukua kwa urahisi."
"Sijawahi kupenda nyumba ya mtu mwingine hivi." Alisema Liam. "Nipe siku mbili. Nikimaliza mambo yangu mengine, nitatoa jibu."
Raymond akatikisa kichwa kwa heshima"Tunaweka pending kwa ajili yako mr liam"
*******
Siku mbili baada ya kutembelea nyumba hiyo ya kifahari katika eneo la masaki, Liam Carter aliamua kuichukua. Alikutana na Raymond, wakala wa Haraka Realty, katika ofisi yao iliyopo Ostabei. Baada ya kusaini makubaliano na lasmi liam kua ndio mmiliki wa jumba hilo liam alitumia takriban dola laki 5 kununua nyumba hiyo
Liam, akiwa na utulivu wake wa kawaida, wakati wa kukamilisha makubaliano ya nyumba. Alijua kuwa ili kuendelea na maisha yake mapya, alihitaji kuwa makini na kila hatua anayochukua, kuhakikisha kuwa anadhibiti taarifa zinazomhusu na kudumisha taswira ya mtu wa kawaida
Will continue
Comments