Hamza aliona ni kama Dina anaonngea kimafumbo mafumbo na alitaka aende moja kwa moja.
“Unakumbuka nilimwambia Prisila leo kuna tukio la ufunguzi wa Albam ya msanii mmoja mkubwa hapa nchin na niende nae?”Aliongea Dina na Hamza hapo hapo alikumbbuka ndio.
“Nakumbuka vizuri?”
“Basi huyu msanii ni mkubwa mno na huyo mtu ambae namzungumzia lazima atakuwa mmoja wa wageni wa heshima wa tukio hili , nina uhakika hata mstaafu Mgweno atakuwepo , unaonaje tukishiriki wote watatu?”Aliongea Dina na Hamza hapo hapo aliona ni pendekezo zuri.
“Itakuwa vizuri nikishiriki, nitaenda kumpitia
Prisila nije nae”
“Vizuri , mimi nitatangulia na kukuwekea utaratibu wa kupata kadi ya mwaliko”Aliongea Baada ya Hamza kukata simu alimtumia ujumbe Prisila kwamba atampitia kwa ajili ya kwenda kwenye sherehe za ufunguzi wa Albamu na Prisila alijibu dakika hio hio kwamba atamsubiri.
Muda alikuwa nao wa kutosha na alitamani kurudi kwenye kampuni lakini aliona sio chaguo sahihi hivyo alipeleka gari mpaka fukwe ya Coco na kisha alishusha kiti na kusinzia.
Saa kumi na mbili hivi aliwasiliana na Prisila na alimtajia anapoishi na Hamza mara baada ya kuijua Anuani inaelekeza wapi alichoma mafuta kwenda huko na ilimchukua dakika kama kumi na tano mpaka kufika nje ya nyumba kubwa yenye ukuta na Geti jeusi lililonakshiwa na rangi ya shaba.
Lakini sasa muda ambao Hamza anasimamisha gari pembeni kwa ajili ya kugonga geti , gari nyingine ilisimama kando yake, ilikuwa ni moja ya gari ya kifahari na ilionekana pia uelekeo wake ni ndani ya nyumba hio.
Hamza mara baada ya kufungua mlango na kutoka na gari ile aina ya Cadillac S series toleo jipya ya rangi ya bluu ilifunguliwa mlango na palepale Hamza alimfahamu bwana huyo ambae alionekana kupendeza mnno.
Alikuwa amevalia suti ya Armani na suruali ya Zegna , mtu yoyote angemuona kwa macho ya haraka angeweza kumfahamu ni mtu muhimu kwenye jamii.
“Bosi Side naona ni bahati nyingine tunakutana”Alisalimia Hamza huku akikunja ndita “Hamza!, unafanya nini hapa?”Aliuliza Side huku akikunja sura kama amelishwa pilipili.
Kabla hata ya Hamza kujibu hilo swali mlango wa geti ulifunguliwa na alitoka Prisila ambae alionekana ameshavaa makeup lakini mavazi bado , urembo wake uliongezeka maradufu.
“Hamza umewahi mno , nilikuambia uchelewe chelewe”Aliongea Prisila huku akitoa tabasamu. , lakini alionyesha mshangao mara baada ya kumuona Side , ilionekana alifika hapo bila taarifa.
“Side unafanya nini na wewe hapa ?”Aliuliza.
Muda ule Side hakumjali tena Hamza na alitoa tabasamu lake la kimauaji huku akitoa ua la Rose kutoka kwenye gari.
“Prisila najua wewe ni shabiki kindaki ndaki wa msanii Almasi na leo ni siku ya kuzindua rasmi albamu yake , nina mwaliko nataka tutangulizane wote”Aliongea kwa swaga nyingi mno kama vile ni mwanamfalme.
Prisila alijikuta akiyaangalia maua na kisha bila hata ya kujielewa macho yake aliyaelekeza kwa Hamza huku akionyesha hali ya kusita.
Baada ya kujifikiria kwa sekunde aliishia kupokea lile ua kwa ajili ya kutoonyesha ujeuri.
“Asante sana Saidi , lakini umejuaje namshabikia Almasi na sio King?”
“Nimekufollow instagram na mara nyingi naona maoni yako ya kumkubali Almasi” “Oh kumbe “Aliongea huku akionyesha kutofikiria sana isitoshe hata yeye alikuwa akiona maoni ya Saidi mtandaoni.
“Saidi nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya kuelekea huko ndio maana Hamza yupo hapa kwa ajili ya kunichukua”
“Ulikuwa na mwaliko , wewe na Hamza!!?”Aliongea Saidi huu akionyesha mshangao.
Lakini side muda huo alikuwa akijiuliza inamaana Lea hakumwambia Prisila juu ya Hamza kujihusisha na magenge ya kihalifu.
Aliishia kumwangalia Prisila kwa namna anavyomwangalia Hamza na kila kitu kilijionyesha na ukauzu ulimvaa palepale lakini alijitahidi kujionyesha kuwa kawaida , alitamanni bora hata angekuwepo Chriss kidogo angeweza kuonyesha ukichaa wake waziwazi lakini aliupotezea mara moja.
“Prisila nataka leo uwe partner wangu usinikatae, sikukutaarifu moja kwa moja maana nilijua huna wa kwenda nae”Aliongea .
“Side kama nilivyosema nishakubaliana na Hamza kwenda nae na tuna mwaliko , ni kosa lako kuchelewa, Hamza naenda kuchukua mkoba wangu tutapitia Malkia Stylish nivae gauni langu”Aliongea Prisila na bila ya kusubiri alirudi ndani na hazikuchukua sekunde nyingi aliweza kutoka na kumpa ishara waondoke.
“Bosi Side naomba utuwie radhi tutatangulia wa kwanza”Aliongea Hamza na muda ule Saidi alijihisi ni kama atapasuka kwa hasira.
“Prisila fikiria mara mbilimbili , ukienda na mimi utakutana na watu wazito na itakuwa faida kwako”
“Asante Side naenda kumshuhudia msanii ninaemshabikia na sio kukutana na watu wazito” “Prisila kwanini hutaki kunielewa tokea tukiwa shuleni mpaka sasa najitahidi kukuonyeshea ninavyojisikia , lakini kwanini hujawahi kunisikiliza”
“Saidi kwanini ghafla tu unaongea yote hayo..”Aliongea Prisila huku hasira zikianza kumvaa na Saidi hakutaka kumsababishia hasira zaidi.
“Usikasirike Prisila , sijaja kwa ajili ya kukasirisha hivyo naondoka, Hamza hakikisha
Prisila anakuwa salama”
“Usiwaze bosi , Prisila ni mwanafamilia , hawezi kupatwa na tatizo lolote chini ya himaya yangu”Aliongea Hamza lakini kauli ile ilimfanya Side kumwangalia Hamza kwa macho makali bila kuongea neno.
Upande wa Hamza alijikuta akikunja ndita , sekunde hio kuna kitu ambacho alihisi na sio cha kawaida ni msisimko wa ajabu ambao ulimtoka Saidi.
Lakini sekunde kadhaa tu msisimko ule ulipotea na hakuweza kuhisi kitu chochote tena na alijikuta akijiuliza nini kimetokea au amehisi vibaya.
“Hamza hakuna kinachoendelea kati yangu na Saidi na haitokuja kutokea hivyo usije kunidhania vibaya , nimepokea zawadi yake ya ua kwasababu sikutaka kuonekana nina jeuri”
“Usiwe na wasiwasi , mwanamke kama wewe kufuatiliwa na wanaume wengi inamaanisha ni mzuri , sio jambo baya”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu huku akijiuliza kwanini rafiki yake huyo wa utotoni anajitetea mno kwake au ashampenda.
Prisila aliishia kutoa tabasamu baada ya kuona Hamza hana ishara yoyote ya kumdhania vibaya na muda huo huo walianza safari.
“Hamza vipi ile siku walikutoa saa ngapi?”Aliuliza Prisila.
“Ukweli nilienda kama kutalii tu na kurudi , sikukaa muda mrefu”Aliongea Hamza na Prisila alitingisha kichwa kukubali.
“Vipi Regina anaendeleaje , sijawasiliana nae muda mrefu?” “Kama kawaida yake , nadhani unamjua rafiki yako alivyo”
‘”Wee unaongea kama vile una ukaribu nae sana siku hizi”
“Ndio ukaribu wetu ni mkubwa”Aliongea Hamza na kumfanya Prisila kutoa tabasamu lililojaa maswali.
Dakika chache tu Hamza alisimamisha katika moja ya duka kubwa la nguo za kike na ilionekana wauzaji walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kumhudumia , licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda lakini walionekana uwa na ari kubwa.
Dakika chache tu lilitolewa gauni la rangi nyeupe na nyeundu kama main tone , ambalo limedariziwa shingoni na Velvet , Chiffon na vitambaa vingine vya rangi ya dhahabu na kutengeza shingo yenye upo la Almasi.
Baada ya Prisila kwenda kulivaa na kurudi wahudumu wa duka hilo walitoa macho kutokana na kupendeza kwake.
“Jamani hilo gauni limekupendeza , ni kama vile limetengenezwa kwa ajili yako pekee”Aliongea muhudumu huku akimuonea Prisila wivu kwa urembo wake.
“Prisila nakukumbusha hili gauni ni kwa ajili ya matangazo ya duka letu”Aliongea mdada mmoja mweupe hivi mwenye uso wa duara na mwanya.
“Hilda mbona unakumbushia sana wakati naelewa , isitoshe hata kama nataka kulinunua ni bei kubwa sana”Aliongea Prisila na Hamza mara baada ya kusikia kauli ile alitoa simu yake na aliingia kwenye internet na kupiga simu kwenda nje ya nchi na ndani ya dakika chache tu alianza kuongea Kifaransa.
Na kitendo kile kilimfanya Prisila kumshangaa Hamza kwani licha ya kwamba hakuwa akijua lugha ya kifaransa lakini kwa kusikia tu alikuwa akiijua lugha hio , sasa alishangaa kuona Hamza anaongea tena kwa ufanisi mkubwa.
“Hamza hicho ni kifaransa?”Aliuliza Prisila. “Ndio ni kifaransa”Aliongea na Prisila alionyesha ushangaa.
“Kumbe unajua kuongea kifaransa tena unaonekana unaongea kwa usahihi kabisa , ulikuwa ukiongea na nani?”
“Nitakuambia baadae”Aliongea Hamza huku akionyesha tabasamu , ndani ya dakika chache tu walitoka ndani ya eneo hilo na kurudi kwenye gari kwani kila kitu kiliuwa kimekamilika kwa upande wa Prisila.
Kutoka Malkia EmpireStylish mpaka Mlimanni City tukio linakofanyikia iliwachukua dakika kumi na mbili hivi na baada ya Hamza kuiingiza Maybach ndani ya eneo hilo Kamera za waandishi zilianza kumulika upande wao.
Hamza akiwa kwenye gari aliweza kumuona Dina akiwa ameshafika na alikuwa juu ya redcapert.
Watu walionekana kuwa wengi ndani ya eneo hilo na ulinzi pia ulikuwa sio wa kawaida na haraka haraka ilionyesha kuna kiongozi mkubwa ambae anakwenda kuhudhuria hilo tukio.
Hata Prisila licha ya kwamba alikuwa na hamu zote za kushiriki tukio hilo lakini baada ya kuona idadi hio kubwa ya watu maarufu mabimbali pamoja na Kamera za Redcarpet wasiwasi ulianza kumwingia , kwake ilikuwa ni mara ya kwanza kuhudhuria tukio kubwa la namna hio.
Comments