SEHEMU YA 82.
Waandishi wa habari walianza kujiuliza maswali wao kwa wao wakitaka kujua mwanamke alieshuka kwenye gari ya kifahari na kupendeza sana ni nani.
Prisila hakuzoea maisha ya Kamera hivyo aliishia kuinamisha kichwa chake chini kwa namna ya kutotaka sura yake kuonekana.
Hamza hata yeye hakujua ndani ya eneo hilo kungekuwa na vyombo vya habari namna hio ,lakini yeye hakuwa na wasiwasi hata kidogo , kama ni matukio makubwa alikuwa ashashiriki mara kibao hivyo alitembea kwa kujiamini.
Hamza na Prisila hawakusimama kwenye Zulia jekundu, Dina aliishia kuwakabidhi kadi zao mwaliko na kisha kuzionyesha na kuruhusiwa.
Baada ya kuingia kwenye ukumbi Prisila mwili ulimsisimka , kulikuwa na watu wengi ndani ya eneo hilo wengine wakiwa ni watu wazito ambao aliwajua lakini hakuwahi kuwa na ukaribu nao huku eneo lilkiwa limependeza mno.
Wanaume kwa wanawake walimwangalia Prisila kwa macho ya matamanio na wivu , licha wanawake wengi kupendeza waliona wivu kufunikwa na Prisila mrembo ambae sio maarufu.
Muda huo kabla hawajaelekea kwenye sehemu zao kukaa sauti ililiita jina la Prisila.
“Kwaho wewe ndio Prisila?”Ilikuwa sauti ya mwanamke
Kauli ile ilimfanya Hamza na Prisila wote kugeuka na macho kwa macho waliweza kukutana na Salma , Hamza alikuwa akimjua ila upande wa Prisila alionekana kutomfahamu.
“Ni wewe tena?”Aliongea Hamza huku akikunja sura.
“Hamza huyu ni nani , ananijua lakini mimi simjui”Aliuliza Prisila.
“Jina lake anaitwa Salma ni mpenzi wake Saidi”
“Oh kumbe! , mambo Salma”Alisalimia Prisila kwa upole lakini upande wa Salma alionekana kutompenda waziwazi Prisila.
“Sitaki salamu yako , nakupa onyo kaa mbali na Saidi”Aliongea Salma huku akiweka mwonekano wa kejeli mbele ya Prisila
“Hakuna kinachoendelea kati yangu na Saidi , hakikisha taarifa zako”Aliongea Prisila huku akishindwa kuamini siku yake inaingia dosari kwa kuanza kusingiziwa.
“Kwahio uaniona mjinga , Saidi ametokea nyumbani kwenu kwa ajili ya kukuchukua na ameenda mbali mpaka kukuandalia gauni . halafu unasema sina taarifa, huna aibu kuchanganya wanaume wawili kwa wakati mmoja?”Aliongea Salma akimjumuisha na Hamza na kauli yake ilimfanya Prisila kupaniki.
“Sina mahusiano yoyote na Saidi, ni ukorofi kuwaza kitu ambacho huna uhakika nacho”Aliongea Prisila huku akianza kutokufurahishwa na tabia ya Salma , lakini alijizuia maana eneo hilo lilikuwa na watu wengi ambao walionekana kusikiliza mazungumzo yao.
“Salma unafanya nini?”Aliongea Saidi ambae alionekana kusogea eneo hilo kwa spidi na alimwangalia Salma kwa macho makali mno kiasi cha kumfanya kuingiwa na wasiwasi kidogo
“Saidi naomba unisamehe , najua nilikukosea usinifanyie hivi , huyu mwanamke hajui kipi ni kizuri kwake na hana thamani ya kukupoteza muda wako”
“Sikia Salma usinikasirishe , nishawambia mimi na wewe basi , ondoka”Aliongea kwa hasira.
Salma uso wake ulikuwa na hasira mno , ijapokuwa Salma hakuwa maarufu sana lakini alikuwa akitokea familia ya matajiri kuliko hata Saidi ambae ni Mkurugenzi tu ndani ya shirika la mitandao ya simu.
Lakini licha ya mwanamke huyo kufokewa na Saidi hakukasirika zaidi alimwangalia Prisila kwa macho ya hasira mno.
Hamza mara baada ya kuona tukio hilo alijiambia siku zote matajiri hawakosi cha kuchukia kwa watu waliowazidi kipato.
“Saidi mimi na wewe hayajaisha bado”Aliongea Salma kwa hasira na kisha aliondoka na kuwaacha.
“Prisila umependeza sana”
“Asante sana Saidi”
Hamza hakutaka kuendelea kusimama na Saidi maana ashaanza kumchoka hivyo mara baada ya kuangalia upande ambao Dina yupo alimpa ishara ya kusogea.
Saidi licha ya kuonyesha kutoridhishwa na Prisila kuwa karibu na Hamza lakini hakuwa na chakufanya kwa usiku huo.
Dina ndio ambae alionekana kufahamiana na watu wengi mno na ndio pekee aliekuwa bize huku Hamza na Prisila wakiwa wametulia wakisubiria ratiba nzima kuanza.
Saa tatu kamili karibia wageni wote walioalikwa walikuwa wamekwisha kufika mpaka wale wa muhimu zaidi ambao walikaa viti vya mbele , upande wa Hamza wao walikaa mstari wa tatu kutoka vilipo viti va VIP.
Hamza hakuwa hapo kwa ajili ya uzindunduzi huo wa albamu kabisa , alichokuwa akitaka ni kumuona huyo mwanaume ambae inasemekana anajihusisha na shirika la Utatu Giza.s
Dina upande wake alitaka kumsaidia kwa namna yoyote Hamza lakini mpaka uzinduzi unaanza Dina hakuonyesha ishara yoyote ya kumuona mtu ambae alimtarajia na aliishia kumtingishia kichwa Hamza kumuashiria hayupo jambo ambalo lilimfanya kidogo kutoyafurahia matokeo maana alitaka kumaliza swala hilo usiku huo huo.
Prisila upande wake hakuwa akijua hata kinachoendelea kutokana na umakini wake kuuelekezea jukwaani.
Wakati Hamza akijishawishi kuangalia uzinduzi huo muda uleule simu yake ilianza kunguruma ikiashiria ilikuwa ikiita , Hamza aliitoa haraka haraka na kuangalia nani anapiga na namba ilionekana ngeni na kumfanya akunje ndita.
“Prisila naenda msalani mara moja”Aliongea Hamza na Prisila aliekuwa amenogowa aliishia kutingisha kichwa.
Hamza mara baada ya kuingia msalani hakuchelewa kupokea simu ile .
“Hello”
“You are Hamza?”Sauti ya kingereza iliojaa lafudhi ya kizungu ilisikik.
“It’s me”Alijibu Hamza akimaanisha ni yeye.
“Not bad , its took me so long to find out what the hell you are”
“Unataka nini kwangu na wewe ni nani?”
“Niite Van Bridge , najua una mahusiano na mwanamke anaeitwa Eliza na upo ndani ya huo ukumbi kwa ajili ya kutafuta watu wanaohusika na Utatu , nimekupigia kukurahisishia misheni yako”Sauti ya majigambo ilisikika na kumfanya Hamza kukunja sura huku akitoa tabasamu la kifedhuli.
“Ongea unachokitaka?”
“Kama unataka kumuona baba mkwe wako akiwa hai , ndani ya msaa mawili yajayo nikuone mjini Morogoro”
“Morogoro!”
“Ndio Morogoro ndani ya masaa mawili”Sauti hio iliongea na palepale simu ilikatwa.
Hamza aliishia kusimama kwa sekunde kadhaa akififikiria cha kufanya , lakini alionekana kupatwa wazo hivyo alirudi alipomuacha Prisila na Dina.
“Prisila mimi nitatangulia , utaondoka na Dina”Aliongea Hamza na Prisila alishangaa kidogo.
“Hakuna shida , mimi nishanogewa hapa”Aliongea na Hamza alitabasamu huku akimwangalia Dina.
“Nenda , usijali kuhusu Prisila nitahakikisha anarudi nyumbani salama”Aliongea Dina bila ya kuuliza Hamza anaenda wapi ila tu alijua atakuwa na haraka.
Hamza haraka haraka hakusubiri kuendelea kukaa ndani ya eneo hilo , baada ya kutoka nje alimpigia Eliza simu wakutane kituo cha Treni ya Mwendokasi Posta, Eliza aliuliza kuna nini ila Hamza alimwambia atamwambia akifika.
Baada ya kumaliza kuongea alimtumia Regina ujumbe wa meseji akimwambia ana dharula na hatorudi nyumbani na upande wa Regina licha ya meseji kupokelewa haikujibiwa , ikionekana bado ana hasira juu ya kilichotokea mchana, ila Hamza aliona sio kipaumbele kumbembeleza Regina kwa wakati huo , alihitaji kumsaidia Eliza kadri awezavyo ili asiwe na mawazo ya kukimbilia nnje ya nchi.
Nusu saa baadae Hamza aliweza kukutana na Eliza akiwa tayari amekwisha kukata tiketi na kwa bahati nzuri walipata treni hio ya mwendokasi inayoelekea Dodoma.
“Kuna nini Hamza?”Aliuliza Eliza akiwa na wasiwasi huku akiangalia tiketi zilizokuwa kwenye mikono yake.
“Inaonekana baba yako hayupo hapa Dar kama ulivyofikiria , bali yupo Morogoro”
“Baba yupo Morogoro!!?”
“Ndio , waliomshikilia wamenipigia simu ,sijajua hata namba yangu wametoa wapi, tuingie kwanza tutaongea mbele ya safari”Aliongea Hamza maaana ndio waliokuwa wa mwisho mwisho na Treni inataka kuondoka.
Kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro ulikuwa mwendo wa dakika sabini pekee.
Hamza na Eliza mara baada ya kutoka katika kituo hicho cha Treni vijana watatu waliokuwa wamevalia suti waliwasogelea na kuwaziba kwa mbele , kitendo kile kilimfanya Eliza kumwangalia Hamza.
“Mr Hamza tupo hapa kukuchukua kwa maelekezo ya bosi”
“Bosi wenu ndio Van Bridge sio?”Aliuliza Hamza na wale wanaume ambao walionekana ni mabodigadi walitingisha kichwa bila kuongea neno na kuwapa ishara Hamza na Eliza wawafuate.
Mita kama miatatu mbele walikuja kusimama pembeni ya gari nyeusi Toyota Landcruiser na kumpa ishara Hamza kuingia.
“Hamza tunajiendea tu bila kuchukua tahadhari?”Aliuliza Eliza akiwa na wasiwasi.
“Usiwe na wasiwasi, lazima tufanye hivi kama tunataka kumuokoa baba yako”Aliongea na Eliza alitingisha kichwa kukubali.
Gari ile iliondolewa ndani ya maeneo hayo bila ya kuwa na maongezi yoyote kutoka kwa wale waliowachukua na safari ilitembea kwa muda mrefu mno na kwakua Hamza hakuwa mzoefu sana wa mji huo hakuwa akijua ni ueleko gani wanaelekea , kitu pekee alichokuwa akijua wamekwisha kutoka mjini tayari na muda huo walikuwa kwenye mashamba ya mikonge ambayo barabara yake ilikuwa ni ya lami pia
Baada ya dakika kumi na tano mbele hatimae Hamza alielewa kinachoendelea, ilionekana walikuwa wameletwa hotelini.
Ilikuwa ni hoteli ya hadhi ya nyota tatu iliofahamika kwa jina la Troitsa na mara baada ya Hamza kusoma jina hilo alijikuta akitoa tabasamu na kumfanya hata Eliza kushangaa kwanini Hamza anatabasamu.
Baada ya kushushwa nje ya gari waliingia ndani ya hoteli hio wakitangulizana na wale mabodigadi mpaka eneo la mapokezi.
“Mtapumzika hapa kwa usiku na kesho tutakuja kuwachukua na kuwapeleka kwa bosi”Aliongea mmoja ya wale mabodigadi huku akimkabidhi Hamza ufunguo wa chumba.
“Kama alikuwa na mpango wa kuonana na sisi kesho, kwanini ametuharakisha kuja kote huku usiku usiku?”Aliuliza Hamza huku akionyesha hali ya kukasirika kutokana na kuchezewa na watu hao ilihali wenyewe ndio walionekana kuwa wagomvi, ila Hamza aliona avumilie tu aone nini kinaendelea.
“Hamza hatuwezi kulala kwenye chumba kimoja , tuchukue chumba kingine ili nikalale”Aliongea Eliza mara baada ya kuingia ndani ya chumba walichopewa , Eliza alidhania kutakuwa na angalau vitanda viwili lakini kilikuwa chumba cha kitanda kimoja pekee
“Eliza tunapaswa kulala pamoja, unajua kabisa tupo kwenye misheni hivyo unapaswa kuwa karibu yangu kwa usalama ,isitoshe hii hoteli nina mashaka nayo”Aliongea Hamza huku akimshika Eliza mkono.
Kwa kuona usiriasi aliokuwa nao Hamza , Eliza alishindwa kujua kama kuna nia nyingine ambayo Hamza anakusudia au ni sababu tu ya kutaka kumlinda.
“Eliza unapaswa kuniamini?”Aliongea.
“Hapana nakuamini”Aliongea Eliza huku bado akionyesha kuwa na wasiwasi na hali ya hewa ilionekana kuwa ya ubaridi hivyo hakuna ambae alienda kuoga na waliishia kupanda kitandani na kulala.
Lakini licha ya muda kuwa umeenda, Eliza alikosa usingizi kutokana na kuwa na mambo mengi kichwani kwake, hata Hamza hakutaka kulala moja kwa moja , aliona atumie hio nafasi kuongea na Eliza.
“Eliza sikupata nafasi ya kukuuliza , ulijuaje kuhusu ndoa yangu na Regina?”
“Ni Madame , bibi yake Regina alieniambia ..”Alijibu Eliza kwa sauti ya chini na Hamza aliweza sasa kuamini kile alichokuwa akifikiria ni kweli.
Ilionekana Bibi Mirium alikuwa akifanya yote hayo kwa ajili ya Regina hivyo hakutaka kuongeza neno.
“Wakati tunaingia ulionekana kutabasamu , sababu ilikuwa nini?”Aliuliza Eliza.
“Ah!,mliniambia waliomkopesha baba yako ni shirika linaoitwa Utatu , hii hoteli pia inaitwa Utatu ila wameamua kutumia lugha ya Kirusi ya Troitsa”Aliongea Hamza.
“Unamaanisha Utatu kwa kirusi ni Troitsa?”
“Ndio”
“Kwanini mchana uliongezea neno Black Trinity , maana mimi ninavyojua Utatu ni kama sehemu ya mafundisho ya kikristo?”
“Ndio , ila kama ninachodhania ni sahihi ni tofauti na unavyofikiria , Black Trinity ni shirika la ulimwengu wa Giza , lilianzia kama Band ya mziki na baadae likakua na kujitransform”Aliongea Hamza.
“Kwanini unaamini hawa waliomchukua baba ni hili shirika , kuna sababu yoyote ya kuamini hivyo?”Aliuliza Eliza.
“Labda nikuambie kwa njia hii pengine utaelewa ,katika dunia ya kawaida kuna sababu nyingi za mtu kufanya mapenzi lakini katika ulimwengu wa giza kuna sababu kuu nne, Burudani , biashara, kuzaa na kisha inakuja sababu ya kuvuna nguvu za kiroho”Aliongea Hamza.
“Kuvuna nguvu za kiroho inakuwaje kuwaje?”Aliuliza Eliza akionekana kushangaa.
“Muunganiko wa ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa nyama ni kupitia hisia, kwa lugha nyepesi unaweza kusema hisia ni mlango wa kuingia kwenye ulimwengu wa kiroho, kitendo cha mwanaume na mwanamke kukutana kimwili kuna matokeo mengi yanatokea katika nafasi zao kwenye ulimwengu wa kiroho , kuna mafunzo maalumu ya kuvuna nguvu za kiroho , ziwe nguvu za giza ama za nuru kupitia kufanya mapenzi”
“Kwahio unaamini kama ni huyu mbaba aliefanya haya yote kwa ajili ya kunitaka , unamaanisha ni kati ya hizi sababu unazoongelea?”Aliongea Eliza akiwa na mshangao.
“Ndio”
“Lakini wanawake wapo wengi tena wazuri zaidi yangu , kwanini mimi ?”
“Katika ulimwengu wa kiroho kigezo cha uzuri wa mwanamke sio muonekano ni ile nguvu ya kike unayozaliwa nayo , kuna majina mengi sana jinsi ya kuiita hii nguvu, Wewe ita ukike na Ukiume ,sasa kila mwanamke anakuwa na kiwango tofauti , kuna wanaozaliwa na kiwango kikubwa cha nguvu hii ya Ukike na aina hii ya wanawake unaweza kuwatambua katika ulimwengu wa kawaida kwa bahati zao na mvuto, hujawahi kuona mwanamke ni wa kawaida lakini wanaume wanapanga foleni au mwanake ni mzuri lakini hana mvuto mkubwa?”Aliuliza Hamza na Eliza alitingisha kichwa kuitikia kama ni kweli.
“Hivyo kwa upande wako wewe , umezaliwa na kiwango kikubwa cha nguvu ya kiroho na pia nguvu yako haijapotea kwa kukutana na wanaume wengi kimwili?”
“Kwahio nguvu unazaliwa nayo lakini inapungua kadri unavyokutana na mwanaume kimwili?”Aliuliza Eliza huku akionyesha kushangaa mno maana ni kama anajifunza kitu kipya.
“Sio lazima lakini ni kweli nguvu inapungua , inategemea unakutana kimwili na mwenza kwa malengo yapi , kama unakutana nae kwa ajili ya kunyonya nguvu zake basi wewe utafaidika kwa kuimarisha nguvu zako , kama mnafanya kwa ajili ya kujinufaisha wote wawili basi nguvu zenu zinabakia palepale ,ila kama unaefanya nae ana malengo ya kunyonya nguvu yako ya kiroho basi za kwako zinapungua, mwanamke hata ajiweke msafi vipi , hata afanye upasuaji mara ngapi kuongeza urembo kama amekutana na wanaume wengi na wakamtumia kwa ajili ya kujiimarisha kiroho mvuto wake utapotea na ataishia kukosa soko , umoja huu wa siri wa Black Trinity wanachama wake wanafanya mapenzi kwa ajili ya kujiimarisha kiroho na wanawake hao wanapimwa kiasi cha nguvu wanachokibeba kabla ya kuwa shabaha , hivyo kama huyo mbaba ni mshirika basi moja kwa moja anakutaka kimapenzi kama host , hii haipo kwa mwanamke ipo , yote niliokuelezea yanatokea pia kwa upande wa wanaume
Eliza wewe licha ya kuwa mrembo una mvuto mkubwa mno wa nguvu ya kiroho ndio maana wanaume wanakuwinda , ikitokea ukiwa na ukaribu na mwanaume mwenye nguvu za ukiume hafifu itaonekana ni kama umemuwekea Limbwata..”Aliongea Hamza huku akicheka.
“Hee! , Kumbe dunia ina mambo mengi namna hii?”
“Dunia ina mambo mengi sana Babe ,Unadhani watu mashuhuri wanaoandamwa na kesi za kulawiti watoto na kubaka ni kwasababu wamekosa wanawake , kila kitu kinatokea kwasababu maalumu, zipo ‘organisation’ nyingi za kiroho kama hii ambazo zinalea watu mashuhuri ikiwemo viongozi wakubwa wa kidini”Aliongea Hamza na Eliza alijikuta mwili ukimsisimka , alijifikiria maisha yake ni kama kila alichoongea Hamza kina ukweli ndani yake.
“Vipi kama ukipendana na mtu bila ya kufanya mapenzi?”
“Unaongelea True love , au love with no reason , unajikuta mnapendana sana lakini hakuna sababu yoyote kati yenu ya kufanya mpendane , huu muunganiko wa kiroho wa namna hii ni ngumu kuuvunja katika ulimwengu wa kiroho , penzi hili linaweza kupitia misuko suko na hata wenza kutengana na kuendelea na maisha mengine lakini kama mmefungwa na Nira za kihisia ,mkitakana tena ni ngumu sana kujizuia”
“Wewe na Regina penzi lenu ni la aina gani?”Aliuliza Eliza.
“Babe Eliza ya Regina yamekujaje hapa , hebu sogea karibu kidogo nikukumbatie basi”Aliongea Hamza huku akisogea lakini Eliza alimkwepa.
“Sitaki , wewe ni mume wa bosi wangu , hatuwezi kukumbatiana , sitaki unitumie kiroho mimi?”Aliongea Eliza na kumfanya Hamza kutamani kulia na kujiambia umbea wake unamkosesha fursa.
“Kama Bibi yake ndio aliekuambia kuhusu swala la ndoa yetu , basi utakuwa unajua pia tumeandikisha ndoa mimi na Regina kwa ajili ya hisa za kampuni , sikatai ni kweli nampenda Regina lakini hata wewe nakupenda”
“Kama umemuoa bosi Regina huwezi kunipenda na mimi”
“Kwanini , unataka kusema binadamu anaweza kuuzuia moyo wake uliongezeka ukubwa kwasababu ya mtu?”
“Huo moyo unaemuongezekea ukubwa ndio unaemuoa , ipo hivyo”Aliongea Eliza huku akijikunyata kwenye ukingo wa kitanda.
“Labda iwe hunipendi ila sitokukatia tamaa , nishakuambia kuhusu hili au umesahau?”Aliuliza Hamza lakini Eliza hakujibu kitu zaidi ya kukaa kimya.
Hamza aliwaza namna ya kumsogeza karibu Eliza bila ya kutumia nguvu na baada ya kupata mbinu alitoa tabasamu.
“Ngoja nikusimulie simulizi moja ya kusisimua”
“Simulizi gani?”
“Wewe sikiliza itakufanya ulale kwa haraka”Aliongea Hamza huku akijiambia ngoja tuone baada ya hii simulizi utaendelea kujikunyata au utakuja kwenye kifua changu.
“Kuliwahi kutokea wanandoa wawili ambao walikuwa wakigombana kila siku kwa kufokeana , siku moja ugomvi wao ulikuwa mkubwa mno kiasi cha kuanza kupigana, mume alichukua kisu na bila kudhamiria alijikuta akimuua mke wake kwa kumchoma nacho tumboni , baada ya tukio hilo ili mume kuficha kile alichokifanya alimbeba mke wake kimya kimya na kwenda kumzika msituni , lakini hata bado alikuwa akiogopa mtoto wake wa kiume atauliza ni wapi alipo mama yake akisharudi nyumbani hivyo hakujua ni namna gani atamjibu mtoto , lakini sasa baada ya yule baba kurudi nyumbani siku ya kwanza ilipita , hatimae siku ya pili mpaka ya sita yule mtoto hakuwahi kuuliza mama yake yuko wapi , kitu kilichompelekea yule mume kuona kuna kitu hakipo sawa , hivyo alichukua jukumu la kumuuliza mtoto wake”
“Mtoto wangu hujamuona mama yako kwa muda mrefu , kwanini huulizi alipoenda?”Aliuliza yule baba lakini ajabu yule mtoto alimwangalia baba yake kwa namna ya kushangaa lakini alijibu.
“Baba kwanini unaniuliza mama alipoenda wakati umembeba mgongoni na hutaki kumshusha…”Kitendo cha Hamza kufikia hapo Eliza alijipeleka mwenyewe kwenye mwili wa Hamza kwa kuanza kuhisi woga.
Hamza aliishia kutoa tabasamu la ushindi kana kwamba ameokota embe chini ya mparachichi.
“Hehe .Eliza najua unanipenda sana..”Aliongea huku akinusa harufu ya marashi kutoka kwenye nywele zake.
“Umenifanyia makusudi kunisimulia simulizi ya kutisha..”Aliongea Eliza kwa sauti nyororo.
Hamza aliishia kuinamisha kichwa chake na kumbusu kwenye paji la uso, kitendo kilichomfanya Eliza ajihisi yupo kwenye mikono salama na hakuna kitu ambacho kinaweza kuuogopesha tena.
“Lala sasa , nitahakikisha baada ya kesho kila kitu kinakuwa sawa na utaishi kwa amani”Aliongea Hamza huku akimpeti peti na hatimae mrembo huyo alipotelea usingizini muda mchache tu.
Asubuhi kulivyokucha bwana alieitwa Van Bridge hakutuma watu kuja kwa haraka jambo ambalo lilimfanya kuona ni kama anacheleweshwa , hivyo bila ya kujifikiria mara mbili mbili alitumia ile namba iliompigia jana na kupiga.
“Hamza wewe ni kijana jasiri sana mpaka kukikipigia kifo simu , yaani mimi hata sitaki kukuua lakini wewe unanipigia?”
“Mmekuja, mmeniweka kwenye hoteli yenu bila maelekezo ya kutosha kwanini nisipige , kama unaniogopa kuwa muwazi”Aliongea Hamza.
“Unaongea ujinga , yaani nikuogope wakati nazungukwa na mabodigadi zaidi ya mia, kama nisingekuwa bize ningeshatuma watu kukuua”
“Wewe sema uko wapi?”
“Unataka kujileta kwenye mdomo wa mamba?”
“Wewe sema unapatikana wapi , mimi nitakuja na kukutafuta , kama unaniogopa basi chukulia sijaongea chochote , nitatumia njia nyingine za kukupata”
“Afraid! , I, Van Bridge have been out here for thirty years and I don’t know how to write word ‘fear’, kama unakitaka kifo fanya uone”Aliongea kwa ubabe na simu ilikatwa palepale.
Hamza alijikuta akishangaa , inamaana hao watu wamemleta hapo kumchoresha, lakini hata hivyo hakutaka kuwaza sana.
Muda huo huo mlango wa chumba chao uligongwa na Hamza mara baada ya kwenda kufungua alikuwa ni mhudumu aliemwagiza kifungua kinywa.
Lakini bila kutarajia yule mhudumu wa kike alimpatia Hamza kikatarasi mkononi na baada ya kukifungua aliweza kusoma neno ambalo hakulielewa mara moja na ilimfanya na Eliza kuwa na shauku.
“Kimeandikwa Shamba la Mzungu”Aliongea Hamza na Eliza alionekana kuelewa neno lile mara moja.
“Ninavyojua mimi Shamba la Mzungu ni hospitali ya kuhudumia wagonjwa wa muda mrefu wasiojiweza”Aliongea Eliza.
“Unamaanisha ni Sanatorium?”
“Ndio , miaka kadhaa iliopita sehemu hio ilivuma kwa kashfa ya kuiba viungo vya wagonjwa waliofariki , lakini serikali ilikuja kukanusha baadae”
“Umesema kuiba viungo?!!”Aliongea Hamza na swali lile lilimfanya Eliza na yeye akili kumkaa sawa.
“Baba..!!!”
Eliza alishituka huku akiamini kinachoendelea huko pengine ni baba yake kuondolewa figo au moyo kulipia deni.
Hamza na yeye ni kama sasa anaamka , mwanzoni akili yake ilijua pengine ni mchezo wa kumfanya Eliza akubali kutumika lakini hisia zingine zilimwingia mara baada ya kujua pengine mchezo uliochezwa ni kwa ajili ya Mzee Mlowe kuuza kiungo cha mwili kulipia deni.
“Eliza usiwe na wasiwasi , ngoja tuwahi”Aliongea Hamza akimtuliza Eliza na kwa haraka sana walichukuana na kutoka nje ya hoteli hio na kisha waliita taksi iwapeleke Shamba la Mzungu
Hamza alijiambia kama wamevuna viungo vya baba mkwe wake atalipua eneo lote.
Baada ya kupanda taksi iliwachukua saa moja na dakika kadhaa kufika , ilikuwa ni sehemu ambayo ipo ndani ndani, licha ya barabara yake kuwa nzuri
Kwa mbali tu Hamza aliweza kuona majengo mengi ya ghorofa yaliokuwa ni kama chuo hivi na mazingira kusogelea eneo hilo yalikuwa safi kabisa na kulikuwa hadi na kibao kiliochoandikwa Bridge Sanotarium.
Comments