Reader Settings

Ilikua ni siku ya jumamosi jion Jua lilikuwa limeanza kupinduka wakati Liam Carter alisimama mbele ya mlango mkuu wa nyumba yake mpya iliyoko Masaki. Hii ilikuwa ni siku ya kihistoria kwake—siku ya kuhamia rasmi kwenye makazi aliyoyanunua siku chache zilizopita.

Nyumba hiyo ilikua na kila kitu na baadhi ya sehemu ambazo liam hakuvutiwa nazo aliwaambia wamlekebishie sikuile wanafanya makubaliano ya kuinunua

Hakuwa na msafara, wala hakukuwa na kelele za wajakazi au magari ya mizigo. Alikuwa yeye peke yake, na begi moja tu la mgongoni. Kwa mtu mwingine, hili lingeonekana kama maigizo au ufukara wa ghafla. Lakini kwa Liam, kila kitu kilikuwa kimetulia kwenye mpango alioujua yeye mwenyewe.

Mlinzi aliyekuwa langoni alimsalimia kwa heshima kubwa.

“Karibu tena bwana mkubwa. Tumekamilisha kila kitu kama ulivyoagiza.” Alisema mlinzi huyo, akifungua geti la kisasa lililokuwa limepambwa kwa alama ya kifahari ya L.

“Vizuri. Na zile kasoro nilizotaja?” Alisema Liam kwa sauti ya utulivu.

“Kila kitu kimewekwa kama ulivyo hitaji vitu vyote sasa viko sawa.” Alijibu mlinzi huyo.

Liam aliingia ndani akipitia njia ya mawe iliyoelekea kwenye mlango wa mbele. Nyumba hiyo ya ghorofa moja ilikuwa ya kuvutia – vyumba vitano vya kulala, sebule kubwa yenye dari la vioo, jiko la kisasa, ofisi ya ndani, bustani ya mbele na bwawa la kuogelea nyuma. Samani zote ziliwekwa tayari na zilionekana kutokea duka la kifahari.

Alipofungua mlango na kuingia ndani, akavuta pumzi ndefu ya hewa ya baridi ya kiyoyozi, halafu akalisogeza begi lake hadi kona ya sebule na kulitua. Akazunguka taratibu ndani ya nyumba, akitembea kwa utulivu kana kwamba alikuwa akisoma historia iliyojificha kwenye kuta.

Baada ya muda mfupi, alikwenda jikoni, akafungua jokofu, na kuchukua juisi baridi ya tikiti maji. Alikunywa glasi moja taratibu huku macho yake yakiwa yameelekezwa dirishani, akiangalia bustani iliyopambwa kwa taa ndogo ndogo za usiku.

“Hatimaye,” alisema Liam kwa sauti ya chini, “Sasa nimepata sehemu ninayoweza kuita nyumbani.”

Jioni hiyo, Liam akiwa kwenye nyumba yake mpya, alijilaza kwenye kochi kubwa la sebuleni, huku televisheni ikiwa imefunguliwa lakini macho na akili yake vikiwa mbali kabisa. Hakujua kama alikuwa anafikiria kuhusu kazi, maisha, au zile siri nzito alizozibeba moyoni. Lakini kabla hata hajazama vizuri kwenye mawazo yake, simu yake iliita.

Aliinua taratibu, akaangalia namba isiyojulikana, halafu akapokea.

"Hallo?" Alisema kwa sauti ya kawaida.

"Habari za jioni. Bwana liam napiga simu hii kutoka ofisi za Royal Shield Security

Tunapenda kukuarifu kuwa maombi yako ya kazi yamepitishwa kwa hatua ya awali. Tafadhali fika kesho saa mbili asubuhi kwa ajili ya usaili." Alisema sauti ya kike kwa sauti ya kirafiki lakini ya kiofisi.

Sawa, nashukuru kwa taarifa." Alijibu Liam kwa utulivu.

"Karibu sana. Ofisi zetu zipo maeneo ya Mikocheni, nyuma ya hospitali ya TMJ. Tafadhali hakikisha umevaa rasmi." Aliongeza sauti hiyo kabla ya kukata simu.

Liam alitabasamu kidogo. "Mwanzo mzuri." Alijinong'oneza

Alipomaliza, alipanda ghorofani kwenye chumba chake kikuu, akajilaza juu ya kitanda kikubwa chenye mashuka meupe ya pamba laini. Usingizi ulimchukua bila kupambana.

*****

Asubuhi ya jua tulivu iliangaza kwa upole kupitia madirisha ya gorofa aliyohamia Liam. Alikuwa ameamka mapema, kama kawaida yake. Alikua amevalia suti ya bluu, alisimama mbele ya kioo na kujitazama suti ile ilimpendeza sana mtu yoyote a gemuona na kusikia alikua akienda kwenye interview tena kazi ya ulizi asinge amini kabisa kwani Liam alionekana kama mwanamitindo ukizingatia na sura nzuri alio kua nayo hakuendana kabisa na kazi ya urinzi, kwa dakika kadhaa. Alijitazamu na kujikubali Uso wake ulikuwa mtulivu,

Alijichukulia pochi, simu, na bahasha ndogo iliyokuwa na nakala ya fomu ya kazi aliyotuma mtandaoni – ile aliyodanganya kuwa aliwahi kuwa mwanajeshi. Alitoka nje na kupanda taksi aliyoiita kupitia programu ya simu.

Njia yote ya kuelekea kwenye kampuni ya ulinzi, hakusema chochote. Macho yake yalitazama madirisha ya jiji kwa mbali, lakini akili yake ilikuwa mbali zaidi. Alikuwa anajiandaa kwa siku muhimu – siku ya interview yake ya kwanza nchini tangu kurejea Tanzania. Ata yeye alijishangaa imekuaje ameamua kutafuta kazi tena ya urinzi

Baada ya dakika 25, taksi ilifika mbele ya jengo la kisasa lenye maandishi makubwa: Royal Shield Security

Ni kampuni maarufu ya ulinzi binafsi jijini Dar es Salaam kampun hiyo ilijipatia umalifu kutokana na kusifika kua na walizi wenye mafunzo ya hali ya juu hivyo kupelekea watu mashuhuli, wafanya biashara wakubw, pamoja na baadi ya vigogo kuchukua walinzi kutoka katika kampuni hiyo, ukiachana na hivyo kampuni hiyo ilichukua watu wenye sifa maalum hivyo ili wakuajili ni lazima uwe na ujuzi wa mapigano ndio sifa ya kwanza walio zingatia. Liam baada ya kushuka kwenye taksi alikwenda adi getini na kugonga, Baada ya mlinzi wa lango kufungua alimkagua kwa macho makali na kumuuliza:

"Nikusaidie nini

"Niko apa kwa ajili ya interview?”alijibu Liam kwa sauti ya utulivu. “Naitwa Liam

Mlinzi yule alimluusu kuingia na Alipelekwa hadi kwenye sehemu ya mapokezi. Msichana wa mapokezi, aliyevalia sare za kampuni, alimkaribisha kwa tabasamu dogo na kumpatia kitambulisho cha muda. Kisha alimuonyesha sehemu ya kusubiri.

Liam alikaa kwenye sofa la rangi ya samawati lililowekwa pembeni mwa chumba, akisubiri. Muda mfupi baadaye, alisikia jina lake likiitwa:

“Liam Carter, tafadhali fuata mimi,” alisema kijana mmoja mwenye mwonekano mkali.

Akaongozwa hadi kwenye chumba cha mahojiano kilichopambwa na picha za mafanikio ya kampuni hiyo – picha za walinzi wao wakiwa kwenye kazi pamoja na viongozi wakubwa wa serikali na wageni mashuhuri.

Mezani waliketi watu wawili – mwanaume wa makamo aliyevaa suti ya kijivu, na mwanamke kijana aliyeonekana kuwa afisa wa rasilimali watu.

Watu hao baada ya kumuona liam waliingiwa na dharau na kua katika nyuso za kukatishwa tama

Kwani Liam hakua vile wao walivyo talajia. Ukweli ni kwamba takribani wiki mbili nyuma kampani hiyo iliweza kupokea tenda au odaa kutoka katika familia yenye nguvu na ushawishi mkubwa sana nchini familia hiyo ilihitaji bodyguard na vigezo ilivyo taka iliitaji bodyguard mwenye uwezo mkubwa wa dalaja la juu na aliitajika kwa ajili ya kumlinda memba mmoja wa wamilia hiyo sasa kwa kipindi hichi kampini hiyo haikua na bodyguard mwenye sifa ambazo familia hiyo iliitaji walio kuepo walikua ni wa kawaida sasa kampuni hiyo hawakutaka kuipoteza tenda kama hiyo ambayo ingewapa pesa nyingi na kuifanya kampuni yao kuzidi kupata jina kwani kufanya kazi na familia hiyo ilikua ni baati moja kubwa sana kwao hivyo hawakutaka kuiachia na kuona ikiangukia kwenye kampuni nyingine sas takribani wiki mbili walikua wakiangaika kutafuta mtu ambae atakae endana na sifa hizo wangeweza hata kutafuta mtu kutoka nje ya nchi lakini walipewa angalizo mtu anaeitajika awe mtanzania halisi muda walio pewa ulikua ni mchache sana sasa baada ya kupokea maombi na kuona sifa ambazo liam aliziweka matumaini yao yote waliyaelekeza kwa liam sas kitendo cha kumuona na muonekano wake waliingiwa na nyuso za kukata tamaa

Licha ya hayo yote waliamua tu kumkalibisha hivyo hivyo Liam Karibu sana, Mr Liam,” alisema mwanaume huyo kwa sauti ya mamlaka . “Tueleze kwa kifupi uzoefu wako katika masuala ya ulinzi au kazi za kijeshi.”

Liam alijibu kwa kujiamini. Alizungumza kwa utulivu mkubwa, akielezea jinsi alivyojihusisha na kazi za usalama kwa miaka kadhaa, akionyesha kana kwamba ni mtaalamu wa mapigano na silaha. Aliwasilisha kila kitu kwa ustadi, bila kuruhusu hata chembe ya shaka kuonekana.

Kwa jinsi alivyokua akiwajibu iliwafanya kuingiwa na imani nae ila hawakuamini moja kwa moja hivyo waliitaji kujilizisha kwa vitendo zaidi hivyo walimtaka kuona uwezo wake wa mapigano Liam hakua na shida hiyo walielekea katika chumba maalumu kwa ajili ya majalibia na uko Liam aliweza kuonyesha uwezo wa hali ya juu wa mapigano na kuweza kumlinda mtu qkiwa katika hatali yalikua ni mapigano ya kawaida tu. Waliweza kumfulahia sana Liam na kumkubali kutokanq na uwezo alio uonyesha

Masaa 4 mbele ndio Muda ambao intreview iliisha kwa heshima kubwa kabisa

“Tutawasiliana nawe ndani ya siku mbili,” alisema yule afisa wa HR kwa sauti ya uchangamfu na furaha kubwa sana

Liam alitoka nje ya jengo hilo akiwa mtulivu. Macho yake yalikuwa yamelegea kidogo, lakini ndani yake alijua alikuwa amecheza karata kwa usahihi. Alijua pia kazi hiyo ingeweza kumweka karibu na watu wa aina tofauti

Baada ya kutoka kwenye interview katika kampuni ya Royal Shield Security, Liam alirudi nyumbani kwake kule Masaki. Hali ya hewa ilikuwa ya utulivu, upepo mdogo ukivuma kwa upole kutoka baharini. Alifungua mlango wa sebuleni, akapita hadi jikoni kunywa maji baridi kabla ya kujilaza kwenye sofa. Alionekana kuchoka lakini bado mwenye akili iliyobeba tafakari nyingi.

Simu yake iliita. Alipotazama, aliona jina la Edina. Alishangaa kidogo, lakini akapokea kwa sauti ya utulivu.

“Haloo,” Alisema Liam.

“Liam, unamaanisha kabisa uliamua kuondoka bila hata kuniaga sasa kuna haja gani ya kua marafiki?” Alisema Edina kwa sauti yenye hisia zilizochanganyika na maumivu.

“Liamu kusikia lawama hizo alishidwa

Acheke ama alie. Nisamehe… sikupanga iwe hivyo.” Alijibu Liam kwa sauti ya pole.

“Kila siku ulikuwa ukishuka pale mapokezi, hata kama ulikuwa mtu wa kimya, nilikuzoea. Halafu ukaondoka tu ghafla kama mtu anayekimbia kitu.” Alisema Edina kwa sauti ya chini lakini yenye uzito.

Liam alikaa kimya kwa sekunde chache kabla hajajibu. “Nimekuwa nikijaribu kutuliza maisha yangu, Edina. Kulikuwa na mambo ambayo nilihitaji kuyakamilisha. Sikukusudia kukuacha bila taarifa.”

“Ulikuwa mtu wa tofauti, Liam. Ulikuwa mtu wa heshima, si wa kubadili mawazo ghafla… nilitegemea angalau ungeniambia.” Aliongeza Edina kwa sauti ya kukata tamaa.

“Nimekosea, na nakubali. Sikupaswa kuondoka hivyo.” Alisema Liam kwa ukweli.

Edina alikaa kimya kwa sekunde chache, halafu akasema kwa upole: “Sawa. Nimekuelewa. Lakini usirudie tena. Si watu wote wanaweza kustahimili ukimya wako.”

“Nitalikumbuka hilo,” Alisema Liam.

Simu ikakatwa kwa utulivu, lakini kimya kilichofuata kilibeba hisia nzito kwa pande zote mbili. Liam alibaki akitazama dari kwa mawazo mengi kichwani—akijua fika kuwa kila uhusiano anaojenga sasa, una msingi wa uongo aliolazimika kuishi nao.

*****

Upande mwingine jengo refu lenye vioo vinavyomeremeta lilisimama kwa fahari katikati ya eneo la kifahari la jiji, likionekana kutawala mandhari kwa sura yake ya kisasa na nembo iliyokuwa imechorwa kwa herufi za dhahabu: VELORA COMPANY . Ndani ya jengo hilo, froo ya 18, kulikuwa na ofisi ya kifahari iliyopambwa kwa mapambo ya bei ghali, maua safi yaliyowekwa kwenye vase ya kioo, na harufu ya marashi ya kifaransa iliyotamalaki angani.

Katika ofisi hiyo, kulikuwepo na msichana mwenye mvuto wa kipekee, umbo la kuvutia, ngozi laini yenye rangi ya kahawia iliyonyooka kama ya malkia wa kale. Alikuwa na macho ya kutazama kwa ukali lakini yakibeba busara ya ndani, mdomo uliochorwa kwa uangalifu na rangi ya waridi iliyowekwa kwa ustadi. Nywele zake ndefu zilikuwa zimefungwa kwa ustadi nyuma ya kichwa, na alivalia suti ya kifahari ya rangi ya navy blue iliyomkaa kama iliyoshonwa kwa ajili yake tu.

Ingawa umri wake haukuwa mkubwa—miaka isiyozidi 25—sauti yake ya kutembea, namna alivyotazama watu, na jinsi alivyotoa maagizo, vyote vilidhihirisha mamlaka, msimamo na nguvu alizokuwa nazo. Alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa VELORA, kampuni kubwa ya biashara za kimataifa, teknolojia na mali zisizohamishika.

Msaidizi wake binafsi, mwanamke mwenye miwani na mkononi alishikilia baadhi ya mafaili, aliingia taratibu akigonga mlango kwa heshima.

“Samahani mkulugenzi ninajambo la kuwakilisha,” Alisema msaidizi huyo kwa sauti ya upole. “Kampuni ya ulinzi Royal Shield Security imetuma ujumbe asubuhi ya leo. Wanasema mlinzi binafsi anayekidhi mahitaji yako amepatikana, na wako tayari kupanga muda wa kukabidhiana kwa makubaliano ya awali.”

Msichana huyo mrembo alinyanyua kichwa chake taratibu, akimtazama msaidizi wake kwa macho makali lakini ya kutulia. “Kwa hiyo hatimaye wamepata mtu?” Alisema kwa sauti yenye mamlaka, bila kuinua sauti. “Nataka majina, rekodi zake, na siku ya kumpokea. Sitaki kupoteza muda wangu na mtu wa kawaida.”

“Ndiyo mkulugenzi. Nimeagiza faili lake lifikishwe mapema leo kutoka kwao.” Alijibu msaidizi wake kwa heshima.

“Vizuri. Nipe kila taarifa punde ifikapo mezani kwangu. Na usimwambie mtu yeyote kuhusu hili mpaka niamue mwenyewe.” Alisema huku akiangalia nje ya dirisha, ambapo jiji lilikuwa likisonga kwa mwendo wa kasi. Macho yake yakionekana kutazama mbali zaidi ya vioo vya jumba hilo—kana kwamba yalikuwa yakitafuta kitu ambacho bado hakijafika.

WILL CONTINUE

Previoua Next