Reader Settings

FOR YOU 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA TISA

★★★★★★★★★★★★


Luteni Michael na wenzake walirejea jijini Dar es Salaam mida ya usiku kwa kutumia helicopter, kama tu walivyokwenda kwa usafiri huo kule Geita. Waliwakuta wengine tayari wakiwa jengoni, nao wakawafahamisha kwamba baada ya kufanya upekuzi huko hawakupata jambo lenye kutia mashaka, kwa sababu nguo zile zilitumiwa tu na walinzi wa kampuni ile. Vilevile, ACP Nora na wengine walimfahamisha Luteni kuwa hata wao walikuta hali iko hivyo hivyo, kwa hiyo kwa suala hilo ilionekana kuwa kikomo kimefika.

Wakati wakiwa wanaendelea kujadiliana kuhusu njia mpya ya kutumia ili kuwapata Mess Makers, Luteni Michael akapigiwa simu na Kanali Oswald Deule. Akapokea na kuzungumza naye, na ingawa wote hapo walisikia upande wa Luteni Michael wa mazungumzo, walielewa kuwa Kanali Oswald alikuwa akimwambia Luteni afanye upesi sana kuwakamata watu wale kwa sababu kuna mambo mengi yalikuwa yameharibika. Baada ya kukata simu, Luteni Michael akaona jinsi wengine walivyokuwa wanamtazama kama wanasubiri awaambie jambo fulani.

"Nini?" Luteni Michael akauliza.

"Sauti iliyokuwa inatoka ndani ya hiyo simu ni kali sana mpaka nimejiuliza imekuwaje sikio lako halijaziba," akasema Mishashi.

"Alikuwa anafoka nini huyo?" Vedastus akamuuliza.

"Kwamba tunachelewa kuwakamata jamaa. Anasema Raisi amekasirika sana na anataka tuwakamate haraka isivyo kawaida," akasema Luteni Michael.

"Ni nini kimemkasirisha?" ACP Nora akauliza.

"Nafikiri ni kitu inahusiana na treni ya leo," akasema Bobby.

"Treni gani?" akauliza Luteni Michael na wengine pia.

"Hamjasikia kumbe? Kuna treni ilikuwa inatoka Kigoma, imefika wapi sijui Igandu, sijui Morogoro, ikakatwa mabehewa sita ya nyuma. Ilikuwa na kokoto nafikiri za masuala ya ujenzi labda... or not," akasema Bobby.

"Imekatwa mabehewa... yaani ni ajali au?" akauliza Hussein.

"No. Imekatwa makusudi mabehewa huku bado inatembea. Waliokuwa wanaiendesha wamekuja kuona hilo tayari ishafika Ruvu. Wamekuta behewa moja limepasuliwa, sijui hata jinsi gani, na kokoto zimemwagwa chini. Halafu unajua nini?" Bobby akasema.

"Nini?" akauliza Luteni Michael.

"Kwenye hilo behewa ilibandikwa ile chata ya simba mweupe," akasema Bobby.

"Eh! Mess Makers?" akauliza Mario kimshangao.

"Ndiyo maana yake," akasema Bobby.

Wote wakaanza kuangaliana kimaswali.

"Kwa hiyo Mess Makers walikuwa wemeenda kuiba kokoto?" akauliza Omari.

"Hapana. Kulikuwa na kitu fulani ndani ya hilo behewa," akasema Nora akiwa makini.

"Kuna treni zingine zozote leo zimepita reli hiyo, hata kwenda njia za mkato?" akauliza Alex.

"Hapana. Tena, nimefatilia nikajua ni kwa agizo la Raisi hiyo treni ilipaswa kupeleka hizo kokoto Dar bila bughudhi. Leo hakuna mtu amesafiri kwa treni. Lakini... ilikuwa kitu fulani low sana... kama vile..."

"Kulikuwa na jambo limefichwa," akamalizia Alex.

"Ndiyo maana Mdeme amekasirika eeh? Kumbe kulikuwa na midoli yake humo," akasema Hussein.

"Angekuwa ameficha nini sasa?" akauliza Mishashi.

"Kiukweli, hiyo haituhusu. Kinachotuhusu ni kwamba hao jamaa leo wametoka hadharani lakini hatujawa na muda wa kutambua hilo na tumewakosa tena. Yaani... hawatabiriki. Tukisema twende huku, wenyewe tayari wako kule. Tunawapataje?" akasema Luteni Michael kwa mkazo.

Nora akaanza kusema, "Lakini Luteni... naanza kuona kama vile hawa watu hawaibi tu ili kujinufaisha. Wanaitarget serikali... kama vile wanaichallenge... na ninadhani hiyo inamaanisha kuna kitu personal kati yao na Raisi. Labda..."

"No, ACP. Nilikwambia sisi hatupaswi ku-delve kwenye mambo yao ya siasa... sisi tunatakiwa tu kufanya kazi tuliyopewa," akasema Luteni Michael.

"Luteni, nafikiri ACP anachojaribu kukwambia ni kwamba huenda kuna njia ya kufanikiwa kuwapata hao jamaa kama tutajua ni nini kinachoendelea baina yao na Raisi. Hivi vitu vilivyofichika ndiyo vinaweza kuwa ufunguo," akasema Vedastus.

"Ndiyo naelewa. Lakini hiyo haiko ndani ya description yetu. Hatutajiingiza huko," akasema Luteni Michael.

Wenzake wakawa wanaangaliana kwa kukerwa, hata Mario akazungusha macho yake.

Nora akashusha pumzi, kisha akasema, "Okay. Kuna jambo nitakwenda kufatilia kesho hospitali kuu. Labda litasaidia kwenye hii mission."

"Hospitali? Kwa nini?" akauliza Mario.

"Wacha afanye utafiti wake kwanza, ndiyo atakwambia. ACP, unastahili kupumzika. Nenda kapige juice na usingizi ili kesho ukiwashe," Alex akasema.

Nora akatabasamu, kisha akakubali na kuwaaga huku akiondoka. Luteni Michael akamwambia kama angependa basi amsindikize, lakini ACP Nora akasema haikuwa na shida kwa kuwa alikuwa na gari, kiutani tu, kisha akaondoka hapo. Luteni Michael alipowageukia wenzake, akakuta wanamcheka kichinichini.

"Mnacheka nini?" akawauliza.

"Unajua nini Luteni, ukitaka kumfanya mwanamke aone kwamba unavutiwa naye, jitahidi kuondoa hiyo superiority... yaani... onyesha wakati mwingine kwamba nawe una udhaifu ili ukianguka tu, akuokote, halafu umng'ang'anie forever," Bobby akamwambia, nao wengine wakacheka.

"Aliyekwambia nani ananivutia nani?" Luteni Michael akamuuliza.

"Siyo siri ACP ni mkali. We mwenyewe unamtamani basi tu unajishaua," Mishashi akamwambia.

"Ukija kusema hivyo tena, nakutoa meno yote," Luteni Michael akamwambia.

Mishahi akacheka.

"Hivi huwa anatoka na nani? Najua hajaolewa," akauliza Alex.

"Ana maisha ya kivyake tu. Ana hela sana lakini ni mtu mmoja asiyependa kujionyesha. Umeshawahi kufika kwake? Tena siyo kufika, umeshawahi hata kupaona?" Bobby akauliza.

"Pakoje?" akauliza Mario.

"Pazuri sana. Ana mjengo mkali Dodoma, ngoja niwatafutie hapa muuone. Lakini anaishi kivyakeee," Bobby akawaambia huku akianza kubofya 'keyboard' ya kompyuta yake.

"Siyo ajabu kuna mbunge huwa anaenda huko kum-do," akatania Hussein, nao wote wakacheka.

Luteni Michael akabaki kutafakari maneno ya Bobby. Aliona kuna ukweli mwingi ndani yake kwa sababu kiukweli Nora alimvutia. Lakini kutokana na mambo yaliyokuwa yanawazunguka ilionekana kama huu haukuwa muda mzuri kuanzisha masuala ya mapenzi, ndiyo maana alikuwa kama anampotezea tu. Baada ya wanaume hao kukaa hapo kwa dakika nyingi, nao pia wakaondoka kwenda kujipumzisha.


★★★


Siku iliyofuata, kundi la Mess Makers tayari lilikuwa kule "chini" kwenye jengo la maficho yao. Ilikuwa ni 'full shangwe' kwa sababu kwa mara nyingine tena walikuwa wamefanikiwa kumtia hasara Raisi Paul Mdeme na serikali yake iliyoficha maovu na ufisadi mwingi. Ikiwa ni asubuhi sasa, wote walikuwa wakifurahia mlo kwa pamoja, kukiwa na vyakula mbalimbali hapo kama vile siyo asubuhi. Wapishi wa vyakula walikuwa ni Torres na Kevin, wakisaidiwa na Lexi pamoja na Lakeisha baada ya kurudi kutoka kwenye mishe yao jana.

Huu ndiyo mlo wa pamoja kama familia ambao Kendrick alimwambia Lexi wangeupata baada ya kukamilisha zoezi la kuziiba dhahabu zile. Bado Oscar alikuwa akiisifia sana timu yao hii, akisema hakutawahi kutokea watu wengine kama wao kwa sababu wamefanya vitu ambavyo hakuna mtu aliyewahi kuthubutu kufanya, huku huo ukiwa ni mwanzo tu.

"Sisi ndiyo Mess Makers!" Oscar akawa anasema huku anatafuna nyama.

"Halafu Oscar, hilo jina siye hatulitaki. Umelazimisha kutuita Mess Makers mpaka vyombo vya habari vimetukariri hivyo," Victor akasema.

"Mission ya kwanza si aliacha ile sticker yenye hayo maneno, na jana tena kayaacha kwenye treni... ndo' tushakuwa Mess Makers, sijui hata alikuwa anafikiria nini..." akasema LaKeisha.

"Nyie... Mess Makers jina kali kama sura ya Zelda. Tunawaambia hao maboya kwamba sisi ndiyo wachafuzi wa hali ya hewa. Mlishaiona ile movie ya The A Team?" Oscar akauliza.

"Ile ya wale wajinga wanaofeli kama The Losers?" akauliza Torres.

"Hawafeli bwana. Ni vizuri kuwa na jina namaanisha, siyo kuitwa wezi tu wakati kazi yetu inastahili jina kubwa," akasema Oscar.

"Mh! Unajifanya mpenda kazi sana, wakati jana ulikuwa unawaza tungemaliza saa ngapi ili uwahi kwenda kutia tu hako kamguu kako kwenye tundu lolote la wale... wale wanini wa Dar?" LaKeisha akasema.

Lexi akacheka kidogo na kusema, "Wazaramo."

"Yeah... hao hao," LaKeisha akakubali.

Wengine wakacheka.

"Hivi wewe... unajua kwamba huu mkokoliko ni hatari kuliko wa yeyote nchi hii?" Oscar akasema.

"Aah wapi!" akasema Victor.

"Mkokoliko wenyewe umelala yooh," LaKeisha akasema, nao wote wakacheka.

"Ahahah... maneno ya nani hayo?" akauliza Kendrick.

"Jamaa fulani hivi Facebook. Ndiyo mkokoliko wa Oscar ulivyo," akasema LaKeisha.

"Nikuonyeshe? Ah-aaah, nikuonyeshe?" Oscar akawa anamuuliza LaKeisha.

"Mpaka nisikie umebebesha mtu mimba, ndiyo utanionyesha," akasema LaKeisha.

"Mimba wapi wewe, unagwaya tu. Au hujui mimba huwa tunazo sisi muda wote? Nyie dada zetu huwa mnatusaidia kuzibeba tu," Oscar akasema.

"A-aaah bro, kama unayo wewe ni wewe mwenyewe," akasema Victor.

"Kwenda huko na mashavu yako kama Bambo," Oscar akamwambia Victor hivyo na kufanya wengine wacheke.

"Bwana, jana Liutenant Michael na ACP Nora wameenda kwenye kampuni za boss Geita na huko huko Dar," Torres akasema.

"Walikuwa wameenda kufanya nini?" akauliza Mensah.

"Kufatilia fabric zenye bulletproof. Nadhani wanafikiri wanaweza kutufikia sisi kwa njia hiyo kwa sababu Nora alipompiga Lexi risasi siku ile Mwanza, zilidunda," akasema Torres.

"Boss, hakutakuwa na tatizo lolote hapo? Vipi kama wakipeleleza na kujua mwenye hizo kampuni ni wewe... na wakafanya uchunguzi kujua wewe ni nani..." Victor akauliza.

"Hawawezi. Boss anaziendesha kwa umakini, na hata kama angekuwa anatumia jina lake halisi hawangedhani ni yeye," akasema Torres.

"Eee kweli... bado jina lako litaendelea kuwa 'boss'," akatania Victor.

Kendrick akatabasamu.

"Ukirudi Dar baadaye, mchimbe huyo malaya ujue wamepata nini kingine," LaKeisha akamwambia Lexi.

"Siyo kichwa kichwa tu. Nora ni..."

"Yeees, tunajua. Nora ni mwerevu, ana elimu kali, blah, blah, blaah... Lakini bado Lexi atajua tu," Oscar akamwambia Torres.

"Well boss, hapa tuna zigo nene. Hebu fikiria. Nimepima ounce zote za gold nimepata kilo 4000 kamili... pure kabisa. Kwa mahesabu ya haraka hizo ni 200 something million dollars, na kwa Tanzania ni kama billioni 500 huko!" Torres akasema.

LaKeisha akamwangalia na kutabasamu, kwa sababu alipendezwa na jinsi Torres alivyoongea na kasi yake nzuri ya kupiga mahesabu.

Victor akacheka na kusema, "Kwa hiyo... Mdeme alikuwa anataka kufidishia tulichochukua benki kwa hiyo shilingi mia?"

Wengine wakacheka pia.

"Bila shaka alikuwa anataka adanganye kwamba wametukamata baadhi yetu na kuzirudisha hizo, ili support kwake kutoka ndani na nje iwe kubwa," akasema Lexi.

"Lakini Mess Makers tumempika kwenye mwiko wake mwenyewe!" Oscar akasema ki-swagger.

"Lexi... Oscar akituita hilo jina tena, mwambie Zelda aitafune midomo yake," Kevin akasema.

"Zelda halagi nyama mbichi, Masai wewe," Oscar akamtania Kevin.

Wote wakaendelea kula huku wakifurahia mazungumzo yao. LaKeisha alikuwa amekaa kiti kilicho pembani ya kiti alichokalia Torres. Kiutundu, akapitisha mkono wake kwa chini na kuanza kutembeza kiganja chake juu ya paja la mwanaume huyu, naye Torres akamwangalia kiufupi, kisha akajikausha na kuutoa mkono wake kwa chini bila kumtazama. LaKeisha akacheka kidogo, kwa kuwa alikuwa anaanza kumchokoza mwanaume huyu mwenye akili nyingi sana lakini yeye akampiga chini.

Kendrick alifurahia sana muungano wao huu uliokuwa kama wa familia. Akamwangalia Lexi, ambaye alimwangalia pia, naye akamnyooshea glasi yenye juice kama kumwonyesha 'cheers,' naye Lexi akafanya vivyo hivyo pia.


★★★


Kule Dar es Salaam, Nora aliamkia kujisafisha na kwenda kupata kiamsha kinywa peke yake ndani ya hoteli ile ile aliyokuwa amechukua chumba kwa muda ambao angekuwa jijini, kwa kuwa sasa angetumia muda mwingi pamoja na wanajeshi wale mkoani huku. Alipomaliza, alichukua gari lake na kuanza kuelekea hospitalini akiwa na lengo la kufanya utafiti fulani aliousema jana.

Wakati akiwa mwendoni, Raisi Paul Mdeme alimpigia simu yeye mwenyewe kumuuliza kama kuna maendeleo yoyote aliyofanikisha kuyafikia mpaka wakati huu, naye Nora akasema alikuwa akifuatilia suala fulani ambalo alitumaini lingeleta matokeo mazuri. Mdeme alimsihi sana atie nguvu zaidi kwa sababu Mess Makers walikuwa wanamuumiza sana kichwa chake. Ijapokuwa Nora alitaka kumuuliza kuhusiana na treni ile, akaamua kughairi tu kwa kuwa kwa kadiri fulani aliyaona maneno ya Luteni Michael kuwa kweli, ingawa alihisi kuna vitu Raisi huyu anaficha.

Basi, baada ya kuagana naye, Nora akafika hospitalini kule na kwenda moja kwa moja mpaka idara iliyotunza kumbukumbu mbalimbali za wagonjwa. Alijitambulisha kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), na hapo alikwenda kufatilia taarifa kuhusiana na wafanyakazi wa benki kuu ambao walijeruhiwa siku ile kwenye bomu lililolipuka kwenye ule wizi wa wahalifu waliojiita Mess Makers. Wale waliotunza makablasha hayo walisema isingewezekana kumpatia, lakini Nora akasisitiza kwamba ilikuwa muhimu sana kuyapata kwa sababu alikuwa akifuatilia kesi hii, na kuchunguza taarifa hizo ilikuwa ni muhimu.

Watunza mafaili hao wakamjulisha kuwa mafaili hayo hayakutunzwa hapo, bali yalitunzwa na daktari fulani ambaye kwa wakati huo hakuwepo hospitali. Nora alipouliza ni kwa nini hawakuwa wameyatunza hapo, watu hao wakamwambia kwamba hawakujua sababu, ila tu yaliwekwa huko kama kufichwa. Nora akashangaa kiasi, naye akauliza daktari huyo alikuwa nani. Wakamwambia aliitwa daktari Shani Immanuel, naye Nora akaachia tabasamu dogo. Alifahamiana naye, na alikuwa na namba zake. Hivyo akawashukuru na kuwaaga akisema angemtafuta ili wazungumzie suala hilo.

Simu yake ikaanza kuita alipokuwa ameanza kuondoka sehemu hiyo. Alipoangalia mpigaji, akakata upesi na kuirudisha mfukoni. Ilikuwa ni baba yake, Jenerali Jacob mwenyewe. Akaendelea kumpigia binti yake huyu, lakini hakupokea hata moja. Nora akarudi mpaka kwenye gari lake, kisha akamtafuta daktari Shani.

Mwanamke huyo alisalimiana naye vizuri kwa kuwa ulipita muda mrefu bila ya marafiki hawa kuongea, naye Nora akamjulisha kwamba alihitaji msaada wake katika uchunguzi mpya aliokuwa anaufanya. Shani akampa pole kwa kumkosa leo hospitalini, na kumwambia kwamba kesho angemkuta, hivyo wangeonana wakati huo. Nora hakuwa na kipingamizi, na baada ya hayo akaagana naye na kuwasha gari sasa ili aelekee jengoni kule kujiunga na timu ya Luteni Michael.

Lakini alipoiangalia simu yake tena, akakuta ujumbe kutoka kwa baba yake. Alimwambia anajua yuko Dar, na kwamba mdogo wake Nora amejiingiza kwenye shida fulani ambayo imesababisha akamatwe. Kwa kuwa Nora alikuwa huku huku Dar es Salaam, akamwomba aende kumtoa kwa sababu yeye (Jenerali Jacob) alikuwa mbali. Akamwandikia pia kwamba anapaswa kuacha utoto, awe anapokea simu zake.

Nora aliudhika sana. Alitamani hata kumjibu kumwambia aagize mtu mwingine, lakini alijua angepaswa tu kwenda kumsaidia mdogo wake. Mdogo wake huyo alikuwa wa kike, naye alikuwa mtukutu vibaya mno, aliyependa kuishi kwa kujiachia kutokana na miendekezo ya baba yake. Lakini walipendana na Nora, na ijapokuwa yeye Nora hakuwa na ukaribu na baba yao kama mdogo wake, bado alimwongoza mara kwa mara, ingawa kwa sababu ya umri mdogo wa ujana, mdogo wake huyo alikuwa na kichwa kigumu na ndiyo sababu mara kwa mara angejiingiza kwenye shida.

Nora akampigia Luteni Michael kumjulisha kwamba kuna suala fulani lilizuka alilohitaji kwenda kusuluhisha hivyo huenda angechelewa au asingefika leo, lakini kama wangepata jambo jipya ambalo wangehitaji ahusike basi angemtaarifu. Luteni Michael akamwambia hakukuwa na shida, naye Nora akaondoka hapo na kwenda mpaka kule mdogo wake alipowekwa ndani. Alikuwa ameshikiliwa na mapolisi kwa sababu usiku wa jana alikuwa kwenye club moja, ambapo fujo zilitokea, na yeye alihusika. Kwa hiyo maaskari walimkamata yeye pamoja na vijana wengine kutokana na fujo hizo walizofanya kwa sababu ya kulewa sana.

Baada ya Nora kumtoa, alikwenda naye mpaka hotelini kwake ili kumpa somo kuhusu mwenendo wake usiofaa. Alimkanya kutenda kama mtu mpumbavu, na kumwambia asingemsaidia tena wala kuongea naye endapo hali hiyo ingejitokeza. Binti akamwomba dada yake samahani, kwa kusema jana alikuwa tu na misongo kwa kuwa alimwomba mpenzi wake watoke, lakini mpenzi wake huyo akamkwepa na kusema hangeweza kutoka naye kwa jana kwa kuwa angeenda sehemu nyingine, hivyo aliudhika tu na kwenda na vijana wengine ambao wangekuwa ndiyo njia rahisi ya kumsaidia kuchangamsha akili.

Binti huyu alikuwa ndiyo wa mwisho kuzaliwa, na ijapokuwa alikuwa na miaka 23, bado mambo mengi aliyafanya kama mtoto kwa sababu ya kuwa kitindamimba. Alikuwa mrembo kama dada yake tu, "black beauty," naye aliitwa Asteria. Nora akaongea naye na kumpa ushauri mzuri kuhusu kujidhibiti, kisha baada ya maongezi yao, wakatumia muda pamoja kufurahia undugu wao kama dada. Asteria hata akamsuka Nora kwa mtindo mzuri wa rasta, kisha baadaye Nora akampeleka mpaka kule Asteria alikoishi, yaani kwenye nyumba waliyokuwa wamejengewa na baba yao. Nora hakuwahi kabisa kukanyaga ndani huko, na hii ikiwa ni kwa sababu ya chuki yake kumwelekea Jenerali Jacob. Hivyo akampeleka tu na kumshusha njiani, kisha akajiondokea zake.


★★


Kufikia wakati aliporudi upande wake wa jiji hili, giza tayari lilikuwa limeshaingia kutokana na yeye kutumia muda mwingi na mdogo wake. Akaamua tu kuelekea kule kwenye bar/mgahawa ule, yaani Sea House, ili kuichangamsha akili kidogo kwa kuwa hakutafutwa na Luteni Michael. Hakutaka pia kusumbuliwa na yeyote, bali kuwa peke yake tu na kupiga kilevi kwa kadiri ambayo ingemfanya atulize akili kutokana na mambo mengi yaliyokuwa yanamzunguka. Alifika tu kwenye meza ya bartender na kumwambia Elias amwekee kama kawaida yake, naye jamaa akamsogezea kinywaji.

Akiwa bado amekaa huku akinywa taratibu, akasemeshwa na sauti aliyoikumbuka haraka.

"Habari mheshimiwa?"

Nora akageuka na kukuta ni Lexi. Alikuwa tayari amerudi jijini na kuja kujifanya raia mwema mbele ya Nora. Alivalia suruali ya kardet, sweta la rangi ya blue lenye sehemu ya kufunika mpaka kichwa (hood), lakini alikuwa hajakifunika. Uso wake mzuri mweupe usio na make up ya aina yoyote ulimwambia Nora kwamba kiukweli "mwanamke" huyu hakuwa na uhitaji wa kujionyesha sana kwa kuwa alijikubali.

"Safi, vipi?" Nora akajibu, lakini bila kuonyesha hisia yoyote.

"Fresh. Naona umekuja kujichimbia tena huku," Lexi akasema huku akichukua glasi ya wine.

"Yeah... unaweza kusema hivyo," Nora akasema na kukirudia kinywaji chake.

"Umependezea hivyo ulivyosuka," Lexi akamwambia.

"Nashukuru," Nora akajibu bila kumtazama.

"Naona unapendelea ladha asili za nchi... Dane red wine. Dodoma wamepiga hatua," Lexi akasema.

"Yeah ni nzuri. Ulishawahi kuonja?"

"Naaah... me za nchi hii sigusagi."

"Unaonekana kama vile haupendi mambo mengi ya Tanzania. We' ni mhamiaji au?"

Lexi akacheka kidogo. "Hata wewe unaonekana kama vile umetoka kulazimishwa kumeza tango huko ulikotoka," akatania.

"Leo umetoa wapi ujasiri wa kuongea nami namna hiyo?" Nora akauliza huku amekaza macho.

"Oh, shit, sorry... nilikuwa tu natani..."

"Mimi siyo rafiki yako, kwa hiyo usinitanie. Hatujuani," Nora akasema kiukali kidogo.

Lexi akatazama tu pembeni na kuangaliana na Elias, ambaye alikuwa amemsikia Nora akisema hivyo. Baada ya kutambua kwamba alimfokea Lexi pasipo sababu yoyote, Nora akajihisi vibaya kwa kadiri fulani. Akatazama tu chini na kujituliza, akifikiria kumwomba samahani kwa kumsemesha kwa njia hiyo. Lakini akaanza kusikia wanaume fulani waliokuwa wamekaa meza za pembeni nyuma yao wakiongea mambo yaliyomhusu Lexi.

Walikuwa wakisema mara eti demu ni mkali sana, anaonekana ana kalio jeupe sana kama uso wake, anaonekana ndiyo ametoka tu kuvunja ungo, na kwamba hapo hakuwa akitafuta chochote zaidi ya mtu wa kumhonga, hivyo yeyote kati yao angekubali tu kutoka naye. Walikuwa wakiutania mwonekano wake kwa kusema amejiweka kama mwanaume fulani hivi ili asifuatwe, lakini kihalisi anataka kufuatwa. Nora alipomwangalia Lexi, alitambua yeye pia alikuwa akiwasikia lakini akawapuuzia tu. Alipowaangalia wanaume hao, walikuwa ni watano, watu wazima kabisa kwenye miaka ya 40 mpaka 50 huko, wakiwa wameweka vilevi vingi mezani kuonyesha wazi pombe pia ilikuwa ikiwasumbua.

Nora akawa anatafuta njia ya kumsemesha Lexi ili amwombe samahani, lakini mmoja wa wanaume wale akanyanyuka na kwenda mpaka nyuma yake Lexi. Akamshika kiunoni kiutongozi na kuegamia kaunta ya bartender huku anamwangalia kwa tabasamu la uchokozi, lakini Lexi akaendelea tu kunywa wine yake bila kufanya lolote. Nora akawa ameingiwa na hasira kiasi bila hata kujua sababu ni nini kwa kuwa kama alivyosema, yeye na Lexi hawakuwa marafiki. Lakini ni hali hiyo tu ndiyo iliyomkera sana na kumfanya atamani ingekuwa ni yeye wamemfanyia hivyo ili awanyooshe, ila akataka kuona Lexi alikuwa mwanamke wa aina gani; kama ni kweli walichosema wanaume hao kumhusu, au la.

"Mambo vipi joto?" mwanaume huyo akamwambia Lexi huku anatabasamu.

"Oy Elias, niongezee kinywaji," Lexi akasema kwa kumpuuzia mwanaume huyo.

"Usijali dear, naweza kukuagizia kreti zima ukitaka. Sema chochote unachotaka," mwanaume huyo akamwambia.

"Nataka uutoe mkono wako kiunoni kwangu," Lexi akamwambia bila kumwangalia.

Nora akamtazama mwanaume huyo. Alikuwa amelewa kiasi lakini siyo ya kuyumba.

"Aaaa... lakini si unapenda nikikubinya-binya kama hivi..." mwanaume huyo akasema huku akiwaonyeshea wenzake sasa ili wampe sifa.

"Luka, em' mwache dada wa watu. Mkeo atamuua," Elias akamwambia mwanaume huyo.

"Hahahaaa... Elias, we' kaa kutumiminia tungi, njugu tuachie sisi," Luka akasema.

Nora mpaka hapo alikuwa tu akisubiria zari lianze ili atembeze maumivu haswa. Lexi yeye alikuwa ametulia tu kama haelewi somo vile. Mwanaume huyo, Luka, akamsogelea Lexi karibu zaidi na sikio akitaka kumsemesha kiutongozi, naye Lexi hakutikisika.

"Niambie mrembo... unanionaje? Kama John Cena mweusi, au siyo? Nakwambia huko chini nina mdudu muhogo uhogo yaani... utafurahia sana leo," Luka akasema.

Wenzake wakacheka kwa sifa.

"Aliyekwambia me nataka muhogo nani?" Lexi akamuuliza.

"Najua umenipenda tayari, na sikulaumu maana ndiyo sipeshilialiti yangu. Dada mzuri kama wewe unahitaji mwanaume ngangali kama mimi.... eeh..."

"Mm-hmm..." Lexi akasindikiza.

"Yeah. You know... kuna watu huwa wananichanganya na mwanaume fulani hivi lakini siyo mimi. Kwanza me sina mke. Mke wangu alikufa mwaka kesho siku kama ya leo, kwa sababu ndiyo siku niliyokutana na wewe...."

Nora akatikisa kichwa akimwonea huruma Luka kwa kuwa alianza kuona mwanaume hakuwa kitisho kikubwa sana kama alivyodhani, na kufikiri huenda hata Lexi alikuwa akifurahishwa naye.

"Hebu niambie... unaponiona mimi hivi... hivi unavyoniona... nakupa hisia gani nzuri? Mmm? Sema tu nijue..." Luka akasema.

"Hapana hautaki kujua," Lexi akamwambia.

"Come oooon... niambie bwana... tell me...." Luka akawa anabembeleza kilevi-levi.

"Mmm... okay. Kiukweli hisia nayopata ni kama kupigia punyeto kichwani, lakini ubongo haufiki kileleni kwa sababu uso unaouona ni wako," Lexi akamwambia hivyo.

Luka akabaki kutumbua macho.

Elias pamoja na watu wengine waliomsikia Lexi wakacheka kwa sauti sana na kuendelea kumcheka Luka. Jamaa akaanza kuangalia huku na huko kama kujiona amekuwa kituko kikubwa. Nora alikuwa akitabasamu kwa kufurahishwa na maneno ya Lexi, naye Lexi akampa Luka tabasamu la kumwambia kwa heri. Luka akasonya na kusema 'Malaya wewe' na kuanza kuondoka, kitu kilichofanya watu waendelee kumcheka. Nora naye akachekea kwa chini huku akimwangalia sana Lexi, naye Elias na wengine wakawa wanamtania jamaa aliporudi kuketi na wenzake.

Lexi akamwangalia Nora na kutabasamu kirafiki, naye Nora akatabasamu pia.

"Ona... samahani kwa kuwa sikukusemesha vizuri sana muda ule..." Nora akasema.

"Siku ngumu kazini eh?" Lexi akauliza.

"Yeah..."

"Twende, nifate..." Lexi akasema huku akinyanyuka.

"Kwenda wapi?" Nora akauliza.

"Kuna sehemu hapo nje imetulia zaidi. Twende tukakae maana hapa naona kuna kelele tu za hawa mbwa," Lexi akasema huku anamwangalia Luka na wenzake.

Nora akatabasamu kwa kuona jinsi Lexi alivyokuwa mwenye kujiamini. Akamalizia wine yake yote kwenye glasi na kunyanyuka pia, kisha akatoka pamoja na Lexi kuelekea nje. Walikuwa wakielekea taratibu upande wa fukwe za bahari.

"Umeoga?" Lexi akauliza wakati wakiendelea kwenda.

"Hapan... yaani, kuoga asubuhi au?"

"Namaanisha ulipotoka kazini..."

"Ahah... hapana. Nimekuja moja kwa moja hapa..."

"Okay, basi ndiyo maana moody ilikuwa high..."

"Kwa hiyo kuoga ndiyo ingeituliza eeh?"

"Nothing a good shower won't solve."

Nora akatabasamu.

"Nina mambo mengi wakati mwingine inaweza kupita hata siku nzima sijaoga," akasema Nora.

"Mwenzako ziliwahi kupita wiki 3 sijaoga, nilipokuja kuoga nilimaliza tank zima la maji..."

"Ahahah... aa wapi. Haiwezekani..."

"Kwamba nilikaa wiki zaidi ya tatu bila kuoga au kumaliza maji tank zima?"

"Vyote."

"Well, angalau nimekufanya utabasamu. Nilifikiri wewe huwa ni makwenzi na pingu tu..."

"Ahahah... no, huwa siko hivyo. Siku hazifanani kwa hiyo wakati mwingine inaweza kunikuta vibaya... hata wewe una siku za namna hiyo bila shaka..."

"Yeah, najua unachomaanisha. Its okay. Mimi napenda sana utani... na ijapokuwa sisi siyo marafiki nilitaka tu kuchangamsha mazungumzo. Ila ushauri kidogo; kama unataka kutuliza akili basi tafuta sehemu iliyotulia maana hapo ndani ni kwa machizi kama sisi..."

"Ahahah... basi na me ni mmojawapo kwa kuwa nilikuwa humo pia..."

"Yeah, sema we ukiingia tu inabidi mbwa mwitu wengi humo wavae ngozi ya mbuzi... angalau Luka kajitahidi leo," akasema Lexi, naye Nora akacheka kidogo.

"Nilidhani angekusumbua. Nilikuwa nimeshajiandaa kumfumua," Nora akasema.

"Ahah... ningekuwa shabiki wako mkubwa kama ningeona hilo," Lexi akamwambia.

Simu ya Nora ikaita, lakini baada ya kuangalia aliyepiga, Nora akakata tu na kuirudisha kwenye mfuko wake.

"Boyfriend?" Lexi akauliza.

Nora akatabasamu na kusema, "Sina huo muda."

"Kwa nini?" Lexi akauliza.

"Kama nilivyokwambia... mambo mengi."

"Mmmm... okay.

"Nini... mbona unaguna?"

"Hamna kitu. Ni kwamba tu nimeenda moja kwa moja kwenye 'boyfriend' bila kufikiri uwezekano kuwa ni 'husband'..."

"No, mimi sijaolewa. Au naonekana kama nina miaka 70?"

"Aam... kiukweli nilikuwa nafikiri 90 umeshafikisha..."

Nora akacheka. "Asante. Huku tunakoenda ni ili ukaogelee au?" akauliza.

"Na hii baridi? La. Nilikuwa tu nataka kukuonyesha sehemu fulani nzuri sana hapa..."

"Hapa pote napajua vizuri sana. Nimetembelea sehemu hii mara nyingi na kuzunguka mno..."

Wawili hawa walifika sehemu yenye miti na giza kiasi nyuma ya jengo fulani dogo la mbao. Kulikuwa na mti katikati ya bonde dogo, sehemu ambayo mtu angeshuka kama ngazi, na mwanga wa mwezi ulimulika vizuri sehemu ya mbeleni. Wakapapita, naye Nora akaona sehemu nzuri yenye vichaka, miti na beach kwa mbele. Kulikuwa na viti viwili vya beach vilivyowekwa kutazama upande waliotokea, na moto wa kuni uliwaka chini baina yavyo.

Nora alipofika hapo, Lexi alimtazama na kuona jinsi mwanamke alivyopendezwa sana na mandhari hiyo.

"Karibu kwenye sehemu yangu ya siri," Lexi akamkaribisha.

"Ahahah... eti sehemu ya siri. Hivi vitu umeviweka hapa wewe mwenyewe, au?" Nora akauliza.

"Ndiyo. Ona nimeficha na chupa za wine hapa," Lexi akachuchumaa kumwonyesha chupa zenye wine zilizokuwa zimefukiwa chini.

"Ahahah... unazitoleaga wapi? Sikujua kama una kiwanda," Nora akauliza.

"Huwa naziiba hapo House. Siku ukikuta sina sikio moja ujue tu ni Elias!" Lexi akatania.

Nora akacheka kisha akaketi kwenye kiti cha pembeni. Aliiona bahari mpaka mbali, na sauti ya mawimbi ikamfanya atulie. Lexi naye akaketi na kumpa chupa moja ya Dompo.

"Asante. Kwa hiyo... hii ndiyo... sehemu ya... kuwa kivyako?" Nora akamsemesha.

Lexi akajibu, "Ndo' nayopenda zaidi, na ndo' rahisi kuifikia. Zipo nyingine kibao kuzunguka fukwe. Unajua wakati mwingine huwa nawaza naweza kukaa tu siku moja nikashtukia nafumuliwa na mtu kwa sababu ya kuingia kwenye sehemu yake."

Nora akacheka kidogo na kusema, "Nafikiri hii beach iko free kwa kila mtu, kwa hiyo usiwaze kuhusu hilo."

"Yeah, ni moja kati ya sehemu tulivu. Nzuri kwa ajili ya romance," Lexi akasema.

"Kweli. Ni vizuri ukimleta boyfriend wako hapa..."

"Ahah... sina boyfriend mie."

"Kwa nini?"

"Basi tu. Sijawahi kuwa na boyfriend maisha yangu yote."

"Mmm..."

"Nini sasa?"

"Hamna kitu."

"Ni ngumu kuamini?"

"Sidhani kama kuna mtu atakayeweza kuamini hilo. Unaplay hivyo kwa kuwa me ni askari au?"

"La. Nachokwambia ni kweli. Kuwa na boyfriend siyo kitu yangu kabisa..."

"Sawa."

"Ahahahah... hutaki kuamini. Hutaki sina boyfriend, unataka nina boyfriend..."

Nora akacheka kidogo.

"Sitakulazimisha. We' inaonekana ushaweka hadi na mpango wa ndoa kabisa..." Lexi akamwambia.

Nora akacheka tena na kunywa wine kidogo.

"Kuwa care usiitamani sana, nasikia hizo zinawahi kuwazeesha wanawake hatari..." Lexi akatania.

"Ikifika itafika tu, lakini siyo sasa. Baada ya muda. Bila shaka hata wewe unatamani siku moja kuolewa, kuzaa watoto, kuwa na mume wako, si ndiyo?"

Lexi akamtazama kwa sekunde mbili tatu, kisha akasema, "Hapana. Hiyo siyo kitu yangu kabisa mheshimiwa."

"Mh? Ina maana hautaki kuolewa? Kila mwanamke anataka kuolewa, kuwa na familia," akasema Nora.

"Ndiyo najua, hata ma-sister pia... lakini siyo mimi..."

"Ahahahah... ila wewe! Kwa nini sasa?"

"Wanaume siyo type yangu."

"Kwa hiyo type yako ni nani... wanawake?"

Lexi akamtazama kwa umakini kiasi, kisha akasema, "Ndiyo."

Nora akapandisha nyusi juu kidogo kwa kuwa hakuwa ametarajia jibu hilo. "Okay. Kumbe wewe ni Bi?" akauliza.

"Hapana. Yaani... inachanganya kidogo, lakini..."

"Usijali. Nimekutana na watu wengi kama wewe, na ni kawaida tu," Nora akasema.

Lexi alijua kwamba kwa yeye ilikuwa tofauti si kwa sababu alizofikiri Nora, lakini akamwacha afikiri hivyo hivyo. "Kwa hiyo na wewe unayesema unataka kuolewa lakini kwa sasa mambo mengi... utafika huko lini? Miaka 40?" akauliza.

"Ahahah... sijui. Nachojua tu ni kwamba kwa sasa hapana," akajibu Nora.

"Wanaume wengi wanaumiza vichwa eeh?"

"Yeah. Nafurahia zaidi kuwa mwenyewe kwa sasa..."

"Umekuwa mwenyewe kwa muda gani?"

"Ni muda mrefu..."

"Alright. Una uhakika hautaumwa? Mwanamke anahitaji show za hapa na pale mara kwa mara..."

"Ahahahah... basi nitakuwa naukaribia ubikra tena maana ni miaka imepita..."

"Damn! Uko vizuri. Unakumbuka hata mara ya mwisho show ilikuwa vipi?"

"Agh... yaani mimi kwenye uchaguzi sikufichi, nilikuwa ovyo sana. Punda wote niliopanda walikuwa na miguu kama ya panzi..."

Lexi akacheka.

"Angalau wa mwisho alikuwa na jiti kali, lakini kulitumia hakujua..."

"Ilikwendaje?"

Nora akasema, "Yaani tulimaliza muda siyo mrefu hata wa mimi kufika kileleni. Hilo linakuambia nini?"

"Oooh shit, dakika nne! Ahahahah... alijitahidi," Lexi akasema.

"Huyo jamaa hapana. Like, alikuwa na dude zuri tu ila muda kwake ndo' ilikuwa shida. Halafu eti likajitoa akili kabisa. Eti linafikiri nimeenjoooy, linasema tupige nyingine kesho, ya dakika mbili?" Nora akasema na kumfanya Lexi acheke.

"Akakuacha unajisikia kama shimo tu eeh," akasema Lexi akamwambia.

"Wee! Acha yaani..."

"Ahahah... pole. Mapenzi ni mapenzi tu lakini. Huwezi jua lipi litakuwa zuri au baya mpaka uingie... au niseme... ufanye..."

Maneno ya Lexi yakamfanya Nora awaze kuwa huenda "mwanamke" huyu alikuwa ni mmoja wa wale wanaojua kutoa raha haswa. Nora akashindwa kujizuia kuzama sana kwenye kuyaangalia macho mazuri ya Lexi. Alipatwa na hisia fulani hivi kama vile yuko na mtu anayemfahamu vizuri sana, na kufikia hapa alitambua kuwa Lexi alimfanya ajiachie kwa kadiri fulani na kupunguza mikazo yake kiasi.

Wakaendelea na maongezi ya kirafiki kwa dakika kadhaa, kisha Nora akamuaga akisema alihitaji kupumzika kwa ajili ya kazi muhimu kesho. Akamwacha Lexi akiwa amemwambia wangeonana tena endapo angerudi hapo Sea House au sehemu nyingine.

Lexi sasa akawa ameshaanza kufanikiwa kumwingia Nora. Alianza kuona aina ya utu aliokuwa nao mwanamke huyu, naye akawa anatafakari atumie njia zipi ili kuweza kupata taarifa mpya kutoka kwake kuhusu tafiti zao kuwaelekea Mess Makers.


★★★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

Previoua Next