Reader Settings

FOR YOU 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA KUMI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Kwa akili ya haraka, Omari akapinda mgongo, naye Hussein akarudi nyuma kisha kukimbia kwa kasi na kudunda kwenye mgongo wa Omari, akiruka sarakasi hewani na kujirusha mpaka upande wa ndani. Nathan Masunga bado alikuwa hapo na kushtuka baada ya kuona hilo, hivyo akaanza kukimbia kuelekea kwenye nyumba. Hussein akanyanyuka haraka na kufungua mlango wa geti, kisha kwa kasi akaanza kumkimbiza Nathan huku wenzake wakiwa wanakuja kwa nyuma pia. Alifanikiwa kumwahi kabla hajaufunga mlango wa ndani na kumsukuma kwa nguvu mpaka akaanguka chini. Ndani hapo palikuwa pazuri sana, pakipangiliwa vyema na vitu vingi vikiwa vya gharama.

Nathan alikuwa mwanaume mwenye miaka 50, naye alikuwa mfupi na mwenye kitambi kiasi. Akawa anajisogeza nyuma akiwa anamwangalia Hussein kwa hofu, na ndipo Luteni Michael na wengine wakaingia pia. Vedastus na Omari wakaelekea sehemu za jikoni na vyumbani ili kuona ikiwa kulikuwa na mtu yeyote, huku Luteni Michael na Hussein wakimzingira mzee huyo.

"Una mbio kwa mtu aliyevunjika mguu na mwenye kitambi!" Luteni Michael akamwambia.

Hussein akacheka kidogo.

"Tafadhali msiniumize... mimi... mimi..."

"Wewe nini?" Luteni Michael akamuuliza.

Nathan akawa anapumua tu kwa kutetemeka. Vedastus akarejea kutokea chumbani akiwa amemshikilia mwanadada wa miaka kama 20 hivi, akiwa amevalia khanga moja kutokea kifuani, kisha akamwachia alipomfikia Nathan na yeye kukaa karibu na mzee huyo huku akiogopa. Ni bunduki zao hasa ndiyo zilizowaogopesha sana.

"We' pimbi... kwa nini umekimbia? Unatujua sisi?" Luteni Michael akamuuliza.

"Ha..hapana..." Nathan akajibu.

"Huyu ni nani? Mke wako?" Luteni Michael akauliza tena.

Nathan akatikisa kichwa kukataa.

"Ni nani sasa kama siyo mke wako?" Omari akauliza.

"Ni... dada wa kazi," Nathan akajibu.

Omari na Hussein wakacheka.

"Mzee mzima unakosa busara kula vischana vidogo? Halafu eti hawa ndiyo wenye pochi kubwa nchini... ona wanayoyafanya!" Vedastus akasema kwa kukerwa.

"Ninakupa sekunde 15 unieleze ni kwa nini umetukimbia, kwa nini hujavunjika mguu, na kwa nini mliiba zile pesa na wapumbavu wenzako," Luteni Michael akasema.

"Nini?" Nathan akauliza.

"Omari..." Luteni Michael akaita na kuitoa bastola yake.

"Moja... mbili..." Omari akaanza kuhesabu.

"Subiri, subiri, subiri, nita..nitakwambia kila kitu. Ona... mimi jamaa alinipa tu hela ili nisiende kazini siku hiyo lakini sijaiba pesa mimi... nakuapia kijana wangu!" Nathan akasema kwa hofu.

"Unamaanisha nini?" Luteni Michael akauliza.

"Yaani... mimi... nililipwa tu nisiende work... ndiyo nikaja kusikia kuhusu hiyo kitu... basi. Ni hivyo tu..."

"Ongea kama mtu mwenye akili anayejua akisema utumbo, ubongo wake utapasuliwa," Luteni Michael akamtisha kwa kumnyooshea bastola kichwani.

"No, no, no... ona... naapa kabisa kwa jina la Mungu sijaiba pesa. Haki ya Mungu. Mimi mwenyewe nilishangaa sana alipofanya hivyo hata sikuelewa..." Nathan akasema kiuoga.

"Ni nani huyo?" Hussein akauliza.

"Ni kijana fulani hivi. Nilikuwa naenda kwenye club moja hivi... nilikutana naye huko. Baadaye tukajenga urafiki maana alionekana kuwa na pesa na alinisaidia kwa mambo ya hapa na pale... akawa kama rafiki yangu. Ndiyo baadaye tulikuja kucheza mchezo fulani wa ku-bet mimi na yeye. Akaniambia nikipoteza basi siku fulani niache kwenda kazini na yeye akipoteza angenipa pesa nyingi. Alipopoteza... akanipa pesa... akasema angenipa double kabisa kama ningethubutu kuacha kwenda kazini siku hiyo ambayo ndiyo wale jamaa walikuja kuiba... lakini mimi sikuelewa kabisa maana yake wala nini... kwa hiyo nikakubali tu na yeye akanipa..." Nathan akaeleza.

"Alikupa shilingi ngapi?" Luteni Michael akauliza.

"Mwanzoni alinipa milioni 2, halafu akaniongezea milioni 3 zingine. Ana pesa sana huyo kijana inavyoonekana maana nilikuwa namwona hata kwenye kamari..."

"Tulia. Yaani wewe mtu mzima unakubali kupokea pesa yote hiyo ili tu uache kwenda kazini? Unatuona sisi mafala eti?" Luteni Michael akasema kiukali.

"Hapana, hapana, siwadanganyi jamani! Ni kweli! Mimi... nilipokea kwa kuwa sikuona noma, na nilikuwa namwamini maana alikuwa tight sana nami mpaka kufikia wakati huo na...."

"Anaitwa nani?"

"Aaa... Erick... anaitwa Erick..."

"Una picha yake?"

"Hapana. Hatukuwahi kupiga picha..."

"Marafiki hao!" Hussein akasema.

"Unajua kwamba unahusishwa na wizi wa matrilioni ya pesa kwa sababu hiyo? Nieleze ni kwa nini inasemwa ulijeruhiwa na kuvunjika mguu wakati hapa umetoka kukimbia kama swala anayewindwa. Au labda ni mguu mwingine ndiyo umevunjika?" Luteni Michael akauliza.

"Sidhani, maana ndiyo alikuwa ametoka kuuingiza kwenye shimo la huyu binti," Vedastus akasema.

"Hivi kwanza umemkuta kavaa khanga au suti yake ya kike tu?" Hussein akauliza kiutani.

"Vyote!" Vedastus akajibu, naye Hussein akacheka.

"Nijibu," Luteni Michael akamwambia Nathan.

"Mimi ndugu nilikaa tu nyumbani siku hiyo kumridhisha jamaa. Tena kiukweli nilimwona kama mtu aliyelewa kwa sababu hicho kitu alichoniomba nifanye hakikuwa kizito kwangu. Ningeenda tu kazini siku iliyofuata na kusema nilipatwa na tatizo fulani, basi. Sasa... nilipokuja kusikia wizi umetokea nilishangaa sana, nikajiuliza kama huyo jamaa aliniseti au aliniokoa, yaani sikuelewa. Nikaamua tu kukaa kwanza nyumbani nisikilizie nini kingefuata, ndiyo baadaye wakaja watu hapa kwangu wakaniambia nilipaswa kukaa hapa hapa nisitoke kabisa..."

"Wakina nani?" Luteni akauliza.

"Ni... watu fulani kutoka serikalini sijui... walionekana kuagizwa na mtu wa majuu. Wakaniambia nikae na nikitafutwa nisiseme lolote kwa yeyote yule mpaka wao wanitafute..."

"Lengo lao lilikuwa ni nini?"

"Sijui kijana wangu. Mimi hata hawakuniuliza nilikuwa wapi siku ile, wakaniambia tu nifanye hayo la sivyo... la sivyo ningeumia. Kwa hiyo nikakubali tu..."

Wanajeshi wakaangaliana kwa ufupi.

"Na huyo Erick?" Luteni Michael akauliza.

"Erick sikumwona tena tokea hapo. Yaani hata tu ile kunipigia simu hakunipigia ijapokuwa mimi mara nyingi nilijaribu kumtafuta lakini... sikumpata tena..."

Luteni Michael akarudisha bastola yake kiunoni.

"Familia yako iko wapi Nathan?" Vedastus akamuuliza.

"Nilitalikiana na mke wangu mwaka jana. Wanangu wako shule Tanga na Mwanza, kwa hiyo hapa niko peke yangu..."

"Siyo peke yako fala wewe, huyo ni paka au?" Omari akamwambia Nathan, akimaanishia dada wa kazi.

"Unaikumbuka sura ya huyo Erick vizuri?" Luteni Michael akamuuliza.

"N..ndiyo... namkumbuka," Nathan akajibu.

"Sasa nisikilize. Unakuja pamoja nasi kusolve hii ishu. Nenda kavae," Luteni Michael akamwambia.

"Lakini, lakini... sitakiwi kutoka! Nikitoka wanaweza wakani...."

"Hawatakufanya chochote. Sisi tutakulinda. Na ninataka nijue ni nani anayekuandama namna hiyo, kwa hiyo wewe utakuwa mwaliko mzuri ili waje kwangu. Kavae," Luteni Michael akasema.

Nathan Masunga akanyanyuka huku akionyesha unyonge, kisha akaanza kuelekea chumbani akifuatwa na Omari. Mwanadada yule akawa amebaki hapo na khanga yake akiangalia chini tu.

"Na huyu tunamfanyaje?" Vedastus akauliza.

"Tunamfanya," Hussein akajibu kimasihara, na mdada huyo akamwangalia.

"Unaitwa nani?" Luteni Michael akamuuliza dada huyo.

"Saida..." akajibu.

"Karoli?" Hussein akauliza kiutani.

"Umeanza kutoka na huyo mzee tokea kipindi gani?" Luteni Michael akamuuliza.

"Kabla... kabla hata hajatalikiana na mke wake," Saida akajibu kwa hofu.

Wanajeshi wakatikisa vichwa kwa kusikitika.

"Simama..."

Luteni Michael akamwambia hivyo, na binti huyo akasimama.

"Tunaondoka na huyo mtu wako. Wewe utakaa hapa mpaka atakaporudi. Fanya mambo yako hapa, fanya usafi, pika, angalia TV, masturbate kidogo, lakini usiondoke hapa, na usiongee na yeyote kuhusu yaliyotokea humu, la sivyo tutajua na tutakufunga. Umeelewa?" Luteni Michael akamwambia kwa kumtisha.

Saida akatikisa kichwa chake kukubali. Kisha Luteni Michael akamwambia aende chumbani kwake kuvaa pia. Saida akaondoka haraka haraka huku wanaume wakiangalia jinsi kalio lake lilivyotikisika kwenye khanga kwa nyuma.

Hussein akawa anachekea kwa chini, kisha akamwambia Luteni Michael, "Eti masturbate kidogo..."

Vedastus akacheka kidogo pia.

Nathan Masunga akarejea akiwa amevaa shati jeupe na suruali nyeusi ya kitambaa, pamoja na viatu vyeusi akionekana kama anakwenda ofisini. Ni hapa ndipo Luteni Michael akatafutwa na Mario, ambaye alimwambia kwamba hawakupata jambo lolote lenye nuksi upande wao walikoenda kwa Eunice Shirima. Luteni Michael akamwambia kwamba wao walipata, hivyo walikuwa wakijiandaa kurudi kule kwa Bobby. Mario akasema kwamba walikuwa wamepita hotelini na ACP Nora na Mishashi kupata kiamsha kinywa kwanza, hivyo wangewakuta huko baada ya muda fulani.

Luteni Michael akakata simu na kumpigia Bobby, kisha akamwambia atafute msanii mzuri wa uchoraji (sketch artist) kutoka katika vitengo vyao, ampeleke hapo ili wakutane na Nathan Masunga. Mpango wake ulikuwa kwamba Nathan aseme jinsi alivyoikumbuka sura ya huyo Erick, waichore kwa kutumia vifaa maalumu vya mchoraji huyo, kisha waweze kujua huyo Erick ni nani hasa.

Baada ya hayo, Luteni Michael akawaambia wenzake kwamba angewapeleka pamoja na Nathan mpaka kule, kisha yeye angekwenda kusuluhisha tatizo lolote ambalo lingejitokeza kutokana na Bobby kuingia kimarufuku kwenye mifumo ya kiteknolojia ya Ikulu. Alipanga kuongea na Kanali Oswald uso kwa uso ili amweleweshe ni kwa nini aliruhusu mmoja wa watu wa timu yake wafanye hivyo, na ili Kanali Oswald asaidie kumsafishia njia endapo watu wa Ikulu wangemzingua. Kwa hiyo wote wakaondoka hapo baada ya kuelewana.


★★


Walifika kule jengoni kwa Bobby na kumpeleka Nathan ndani, kisha Luteni Michael akaondoka kama alivyodhamiria. Bobby tayari alikuwa amefanya mpango wa kumleta mchoraji hapo, hivyo bwana Nathan akakaa kusubiri. Baada ya dakika kadhaa, ACP Nora, Mario, na Mishashi wakawa wamefika pia, wakiwa wamewaletea na wengine vyakula vyepesi. Nora akaketi na Nathan ili kuzungumza naye kiufupi, akimuuliza mambo mengi kuhusiana na utata huu, naye Nathan akatoa kila kitu alichofahamu. Nora alimwona kuwa aina ya mtu anayejitanguliza yeye kwanza na pesa tu maishani badala ya masilahi ya wengine, na baada ya kumhoji moja mbili tatu, akaketi na Bobby kuendelea na tafiti zingine.

Mchoraji waliyekaa kumsubiri alichukua muda mrefu sana bila kufika hapo, mpaka inafika saa 10 jioni bado hakuwa amefika. Luteni Michael akawa amerejea jengoni hapo muda huo, naye akawaambia kwamba suala la ku-hack Ikulu alikuwa amelisafisha tayari hivyo hawakupaswa kuwaza tena. Alipouliza kwa nini mchoraji hakuwa amefika, Bobby akamjulisha kuwa alisema yuko njiani lakini kwa sababu zisizojulikana bado hakuwa amefika. Kwa hiyo Luteni Michael akawaambia watu wake wakapate chakula kwanza, na waende pamoja na Nathan ili kumpa chakula pia. Yeye tayari alikuwa amekula, hivyo angekaa kusubiri mchoraji afike. ACP Nora, Mishashi, pamoja na Alex wakabaki pia kwa kusema hawahisi njaa, hivyo wakawa hapo kubadilishana mawazo ya hapa na pale.

Muda mfupi kutokea hapo, mchoraji huyo akawa amefika. Alikuwa mwanaume wa makamo, mrefu, na alionekana kuwa mstaarabu sana. Akaeleza kwamba gari lake lilipatwa na shida njiani na hiyo ndiyo sababu iliyomchelewesha sana. Moja kwa moja akaelezewa kwamba alihitajika kumchora mtu ambaye alikuwa akifuatiliwa na jeshi, lakini mwenye kumpa vielelezo alikuwa ametoka kidogo kwenda kula hivyo angepaswa kumsubiri arejee. Mchoraji huyo aliitwa Samuel, naye akakubali na kusubiri hapo huku akiongea mawili matatu na wenyeji aliowakuta.

Nora aliangalia simu yake na kukuta ujumbe mfupi kutoka kwa Lexi, ambaye aliuliza ikiwa yuko huru ili wakutane kule kupiga glasi mbili tatu za wine. Nora alikuwa ameshaanza kutabasamu tu baada ya kuona ujumbe huo, naye akamwambia kuwa angefika huko bila shaka, akijua uchoraji huu ungechukua muda. Hivyo akamwambia Luteni Michael kwamba alitaka kwenda sehemu fulani, na kama angekuwa hajarudi kufikia muda ambao wangekuwa wamekamilisha uchoraji basi angemjulisha ili afike haraka. Luteni hakuwa na kipingamizi, naye Nora akaondoka hapo upesi.

Ilikuwa imeshatimia mida ya saa 11 kabisa, naye Nora akaamua kwenda hotelini alikokaa ili kujimwagia tena na kubadili nguo. Yaani hakujua ni kwa nini lakini alianza kuchukulia kukutana kwake na Lexi kama "date" kabisa. Alipomaliza kujisafisha, akavaa nguo nzuri na kuanza kuelekea kule Sea House.


★★★


Upande wa ile sehemu ya maficho ya Mess Makers, ambayo waliita "chini." Wakati huu waliokuwepo huko ilikuwa ni LaKeisha, Kevin, pamoja na Torres tu, wengine wakiwa sehemu zingine nchini. Kevin alikuwa kwenye chumba chake akijilalia mwenyewe, akiwa bado ameboeshwa sana na uamuzi wa yeye kutakiwa kuwa huko "chini" muda wote. LaKeisha bado alikuwa anamchokoza Torres tokea wakati ule alipomtekenya pajani. Alikuwa anaendelea kumwonyesha kwamba anamtaka kimapenzi, lakini jamaa alimwambia kuwa hahitaji jambo hilo. 

Kwa sababu LaKeisha alikuwa amekaa na Torres kipindi kirefu tokea wapo kule Ghana, alijua kwamba Torres alikuwa na muda mrefu hajafanya mapenzi na mtu, hata alipofika Tanzania, hivyo alikuwa akimtania sana kwamba aidha yeye ni shoga au hajui tu jinsi ya kumridhisha mwanamke. Mara kwa mara tokea walipobaki wenyewe hapo, LaKeisha angejaribu kumzuzua kwa kumshika sehemu zenye kuamsha hisia za kimahaba, au kupita mbele yake akiwa nusu uchi kabisa makusudi, lakini bado Torres alikuwa amekaza tu.

Kihalisi LaKeisha alikuwa ameanza kuvutiwa sana na Torres. Alimwona kama mtu fulani mwenye uvutio wa hali ya juu ambao alikuwa anajaribu kuuficha, na kwa kumchokoza hivi, alikuwa anajaribu kuufichua. Aliipenda akili yake sana pia, naye alitaka kuona kama anaweza kufanya mambo mengi zaidi ya yale aliyomzoea kufanya, yaani kumshughulikia mwanamke ipasavyo. Huyo ndiyo alikuwa Lakeisha, mwanamke aliyependa sana "challenge." Sasa hata wakati huu akawa bado anamchokonoa jamaa ili apate chochote kutoka kwake, lakini bado Torres akawa anamzimisha tu.

Torres akiwa ameketi kwenye kiti kidogo huku anasoma mambo fulani kwenye kitabu, LaKeisha akaja usawa huo na kusimama mbele yake. Torres akaanza kuiangalia miguu yake kutokea chini, akimpandisha taratibu mpaka usoni. LaKeisha alikuwa amevalia kiblauzi chepesi kilichokatwa sehemu ya ubavu na kufanya tumbo lake liwe wazi, huku chini akivalia chupi laini ya rangi ya pink. Mkononi alishika kikombe cha udongo chenye chai, huku akimwangalia jamaa kwa nyodo.

"What do you want? (unataka nini?)" Torres akamuuliza.

"You (wewe)," LaKeisha akajibu.

"I'm not here (siko hapa)," Torres akajibu na kuendelea kusoma.

"Can you never be less boring? (hivi hauwezi kuacha kamwe kuboa?)"

"Ever... (kamwe)"

"Yaani you're home alone with a hot bitch, and all you do is read? We in the fucking stone age or what? (yaani uko nyumbani na malaya mkali halafu unachokifanya ni kusoma tu? Hivi tuko kwenye zama za mawe au?)"

Torres akabaki kimya tu.

"Tell me honestly. What is your problem? (Hebu niambie.. tatizo lako ni nini?)"

Kimya.

"It may be that you don't like me, or you just have a bad taste with women, but you gotta show some respect when a gal offers you some knock up... (inawezekana havutiwi nami, au una ladha mbaya tu kwa wanawake, lakini unapaswa kuonyesha heshima msichana akikupa ofa ya kumgonga..)" LaKeisha akasema.

Torres akachekea kwa chini bila kutoa sauti. LaKeisha alimfurahisha sana ijapokuwa hakujua hilo.

"So you wanna play it this way, huh? Fine (kwa hiyo unataka tucheze namna hii, siyo? Sawa)," LaKeisha akasema.

Torres akiwa anaendelea tu kusoma, akashtuka baada ya LaKeisha kuanza kukimwagia kitabu chake chai ya moto iliyofanya sehemu za vidole vyake ziungue kidogo. Akakiachia na kusimama akiwa ameshangaa sana.

"What do you... what do you think you're doing?! (unafikiri unafanya nini?)" Torres akamuuliza.

"Helping you read (nakusaidia kusoma)," LaKeisha akajibu kwa nyodo.

"Unajua... that book is sole... sitapata kingine, umeniharibia, kichwa wewe!" Torres akasema kiukali.

"Oops! My bad. So, what are you gonna do about it? (oops... ni mbaya.. kwa hiyo utafanya nini kuhusu hilo?)" LaKeisha akamuuliza kikejeli.

Torres akamwangalia tu na kutikisa kichwa, kisha akakiokota kitabu chake kilicholowana sasa.

"Damn! Man, una swagger kama za kuku! Una undugu na Elton John?" LaKeisha akamuuliza.

Torres akakiweka kitabu pembeni na ghafla kuishika shingo ya LaKeisha kama anamkaba. Akaanza kumsukuma mpaka sehemu ya ukutani kwa nguvu sana, naye LaKeisha akataka kumpiga na kikombe kile cha udongo lakini Torres akakiwahi na kuukaza mkono wake kwa chini. Alikuwa amemkaribia sana usoni huku akimkaba kwa nguvu kiasi, naye LaKeisha akawa anatabasamu kibabe.

"There it is..." LaKeisha akasema.

"What I am, what I do, what I don't, is none of your fucking business! Next time you play bitchy on me, I'll squash you like an insect. Do we understand each other? (kile nilicho, kile nachofanya, kile nisichofanya, ni mambo ambayo hayakuhusu hata kidogo.. ukija kunichezea kimalaya tena nitakusaga kama mdudu.. tunaelewana?)" Torres akasema kwa sauti thabiti.

"Please... do. I want you to squash me right now! (tafadhali.. fanya hivyo.. nataka unisagesage sasa hivi!)" LaKeisha akasema kibabe.

Torres akalegeza mkono aliotumia kuikaba shingo ya mwanamke huyu, naye LaKeisha akanza kushusha pumzi kwa nguvu huku anamwangalia kibabe bado. Torres alipotaka kumwacha, LaKeisha akaung'ang'ania mkono huo jamaa aliotumia kumkaba na kuuweka tena kwenye shingo yake kama vile anataka amkabe tena. Torres akabaki kumtazama tu, na bado alikuwa ameudhika, lakini LaKeisha akapeleka mchezo huu hatua nyingine baada ya kuishika sehemu ya siri ya Torres iliyofichwa ndani ya kaptura nyepesi aliyokuwa amevaa.

Kwa sababu fulani wakati huu Torres akamwachia tu, kutokana na ukweli kwamba alikuwa amepandisha hisia kali alipokuwa karibu na mwili wa LaKeisha. Wakaendelea kutazamana tu, huku mkono wa Torres ukiwa kwenye shingo ya LaKeisha bila kuikaza kwa nguvu kama awali, na mkono wa LaKeisha ukiwa unaivuta-vuta mashine ya jamaa taratibu.

LaKeisha akaachia tabasamu la kiburi baada ya kuona kwamba wakati huu alimweza jamaa, kisha akamsogeza nyuma kidogo huku akiwa bado kaishika sehemu ile ya kati ya Torres, bila kuacha kumwangalia machoni. Torres alimtazama mwanamke kama vile mtu mwenye chuki naye, huku kwenye akili yake akijua wazi ndiyo itikio ambalo LaKeisha alikuwa analitafuta.

Kisha mwanamke akashuka taratibu mpaka chini na kupiga magoti, naye akaishika kaptura ya Torres na kuishusha chini. Torres sasa alikuwa ameamua kumwachia mwanamke huyu ajithibitishie alichotaka kujua, na kwa kweli LaKeisha alivutiwa sana baada ya kuona kwamba Torres alificha jambo zuri sana.

"Kai masoyi ne na gaske, ba ku ba? (You are a real sweetheart, aren't you?/Wewe ni mtu mwenye mambo mazuri sana au siyo?)" LaKeisha akaongea kihausa.

"Karya... (bitch/malaya)" Torres akajibu kwa kihausa pia, naye LaKeisha akatabasamu.

Mwanamke akaanza kumpatia penzi la mdomo kwa upendo mwingi. Torres akawa akiutazama mwili maridadi wa mwanamke huyu jasiri. Hapa hangeweza kukataa kwamba kiukweli LaKeisha alivutia, na alikuwa na hamu ya kumwonyesha upendo pia. 

Wawili hawa wakaendelea kupeana mapenzi ndani hapo kwa dakika nyingi zaidi. Torres alitaka kumfurahisha mwanamke huyu pia. Hakujua ikiwa hili lingekuwa ni jambo la kudumu baina yao, hivyo aliona ni vyema ampatie msichana kumbukumbu nzuri kila mara ambayo angekumbuka penzi hili alilomshurutisha wafanye. Alijikaza kidogo asicheke kutokana na ukweli kwamba hakuwahi kumsikia mwanamke huyu akisema maneno kama 'Mungu wangu' au 'Jesus' kwa muda wote aliomfahamu.

LaKeisha alikuja kupiga kelele nyingi mwishoni baada ya kuridhishwa kwa mara ya kwanza na mwanaume huyo. Akajigeuza na kumtazama akiwa ameketi kilegevu.

"Nafikiri Kev amekusikia," Torres akasema.

"He can go to hell. I didn't think you had it in you (aende kuzimu.. sikufikiri ungekuwa na huu uwezo)," LaKeisha akasema.

"Well, now you know (basi sasa umejua)," Torres akajibu.

"Bado nakuhitaji Torre, kama utaweza lakini. Mara mbili usiku na mara moja tena asubuhi, sawa?" LaKeisha akamwambia.

"Is that a challenge?" Torres akauliza.

"You bet it is," LaKeisha akajibu.

"Mmmm... poa. Kama vipi tuanze kabisa..."

Torres akasema hivyo huku akimnyanyua kumbeba na kufanya LaKeisha acheke. Akatembea pamoja naye akimpiga denda kuelekea sehemu iliyokuwa ni chumba chake na kumrusha kitandani. Wawili hawa wakaendelea na mchezo wao mpya na mtamu sana kadiri dakika zilivyozidi kusonga....


★★★


Ni ndani ya wakati huo huo ambao Torres na Lakeisha walikuwa wamepatana mpaka kuanza kupeana mapenzi huko mafichoni kwao ndiyo Nora alikuwa amefika kule Sea House kukutana na Lexi. Mwanamke huyu alivalia kwa njia ya kawaida tu, siyo kwa mwonekano wake wa kiofisi wa suti za kike au koti gumu (leather jacket) na T-shirt kama kawaida yake. Wakati huu alivaa nguo nyepesi tu; T-shirt nyekundu yenye mikono mifupi iliyobana kiasi, na suruali nyeupe ngumu yenye kubana kiasi pia, huku miguuni akivaa viatu vya kawaida aina ya simple zenye rangi nyeusi. Nywele zake alizokuwa akizibana muda wote tokea Asteria kumsuka, wakati huu aliziachia na kuzisokota kwa pande mbili, yaani upande mmoja wa bega likalalia fundo moja na upande mwingine hivyo hivyo pia.

Ilikuwa imeshafika saa 12 jioni sasa, na baada ya kumkuta Lexi akiwa ameketi pale, akamwita huku akimkaribia taratibu. Lexi alikuwa amevalia T-shirt ya mikono mirefu yenye rangi ya zambarau, iliyoficha vyema ngozi yake mpaka kufikia shingoni na suruali ya mazoezi yenye rangi ya kijivu, huku miguuni akivaa viatu kama mabuti ya rangi ya kaki. Akawa anamwangalia Nora huku akitabasamu mpaka alipofika hapo, kisha akaketi kwenye kiti cha pembeni yake. Kulikuwa na chupa mbili za wine aina ya Imagi, ambazo zilikuwa ni ndogo sana, naye Lexi alikuwa ameshikilia moja.

"Karibu mheshimiwa," Lexi akasema.

"Asante. Hako kambilikimo umekaibia wapi?" Nora akauliza kiutani.

"Haka ka-Imagi? Leo sijaiba, nimenunua, lakini bado sijalipa. Tukimaliza tu tukimbie kabla Elias hajanitafuta," Lexi akatania.

Nora akacheka kidogo, kisha Lexi akampatia ile Imagi nyingine.

"Dodoma? We' si ulisema haunywi wine za Tanzania asilia?" Nora akauliza.

"Ndiyo. Lakini nimeona nianze tu kujaribu."

"Kwa nini?"

"We' ndiyo sababu. Nataka kujaribu vitu ambavyo rafiki yangu anatumia ili nione kama nitaipata furaha anayoipata..."

"Ahahah... sawa. Ila haka me sijawahi kunywa. Ni kazuri?"

"Sana. Nimekapenda. Onja..."

Nora akaifungua na kunywa wine kiasi, kisha akasema ni nzuri pia.

"Umependeza leo. Kama msichana wa high school," Lexi akamwambia.

"Ahahahah... acha basi..."

"Kweli kabisa. Nilivyokuona hapo nikadhani umetoka kutolewa out. Au ndiyo unaenda out?"

"Hapana. Nimevaa kawaida tu mbona? Na... nilikuwa nimetoka kwenye kazi kwa hiyo nikaenda kubadili mavazi kidogo..."

"Aaaa... sawa. Vipi kazi lakini? Umemtia bwege gani mbaroni leo?" Lexi akauliza.

"Emm... naweza kusema mambo yako jinsi yalivyo tu. Kuna kazi moja mimi na wenzangu tunaifatilia, angalau kuna mambo yameanza kujiweka vizuri," Nora akasema.

Kauli hiyo ikavuta umakini wa Lexi.

"Okay. Halafu inaonekana unapiga kazi wewe! Hivi huwa hata unapumzika?" Lexi akauliza.

"Ndiyo. Mimi kiukweli napenda sana kufanya kazi, hasa zikiwa ngumu. Ninapenda kutatua mambo mazito, na sikuzote mtu ukifanya kazi ngumu na matokeo yakaja vizuri unajua unapata furaha, si ndiyo..."

"Yeah..."

"Yeah, kwa hiyo, iko hivyo."

"Unamaanisha kwamba kuna kazi ngumu sana mnafanya sasa hivi eeh?"

"Ndiyo. Ni moja kati ya challenge kali sana ambazo nimewahi kuzipitia, lakini ninajua muda siyo mrefu tutatatua tu..."

"Challenge... kama Mess Makers vile?"

"Ndiyo."

"Iih! Subiri... unataka kuniambia kwamba wewe unafanya kazi ya kuwatafuta hao jamaa?" Lexi akaanza kumchimba kijanja.

"Yeah."

"Wow! Ah, saluti mheshimiwa rafiki..."

Nora akacheka kidogo.

"Ijapokuwa nawaona jamaa kuwa hatari lakini kiukweli wanawazungusha sana. Mpaka sasa mmewapata wangapi?"

"Hatujapata yeyote. Lakini kuna kitu tunafanyia kazi sasa hivi haitachukua muda mrefu tutawashika," Nora akasema na kunywa wine kidogo.

Uso wa Lexi ukawa makini kidogo. Alihitaji kujua ni kitu gani ambacho walikuwa wanafanyia kazi, lakini alijua pia kumuuliza moja kwa moja ni kitu gani hicho ingemfanya Nora amshtukie.

"Wakati wa kulala ukiutoa, ni muda mchache sana naotumia kupumzisha akili. Lakini muda wa kupumzika angalau kwa wakati huu nakuwa naufurahia... pamoja nawe. Company yako imeni...wear sana ndani ya hizi siku chache tulizojuana," Nora akasema.

Lexi akatabasamu na kusema, "Mimi pia nafurahia company yako mheshimiwa. Unapaswa kujitahidi kupumzika sana lakini hata kama mpango ni kustaafu ukiwa kijana bado."

"Ahahahah... ni kweli. Sema tu mimi siyo mtu wa kuacha mambo yakiwa hayajakamilika. Ni mpaka utata uishe ndiyo natafuta muda mrefu wa kupumzika," Nora akasema.

"Angalia lakini usije'anguka siku moja kwa sababu ya pressure kubwa unayojipa," Lexi akamwambia.

Nora akatabasamu huku akiyaangalia macho ya Lexi. Ilikuwa ni macho tu hayo ndiyo yaliyomfanya aufurahie zaidi uso wa "mwanamke" huyu.

Lexi akawa ametafakari jambo fulani, kisha akauliza, "Kwa hiyo hata na hapa ukitoka tena unaenda kuendelea na kazi?"

"Yeah, nadhani. Lakini tuachane na kazi. Nataka uniambie huko kwenu Pemba huwa mnafanya mambo gani mengi kujifurahisha," Nora akasema.

"Oh, Pemba ni pazuri. Kuanzia tamaduni mpaka mipasho ya kina Kopa, ni full raha tu..."

Nora akacheka na kuendelea kumsikiliza.

Lexi akajitahidi kumwambia mambo aliyojua kuhusu mkoa wa Pemba, kisha akamwambia anataka kwenda pale Sea House mara moja ili kufata kinywaji kingine haraka na kurejea. Nora akakubali, naye Lexi akaondoka. Lakini aliigiza tu kuondoka kwa kuwa alipofika usawa wa vichaka vya kukaribia sehemu hiyo, akajibanza, na kama matarajio yake, akamwona Nora anatoa simu na kupiga kwa mtu fulani. Alitumia umakini wa hali ya juu sana kuweza kusikiliza maneno ya Nora ijapokuwa alikuwa kwenye umbali fulani, naye akaweza kusikia Nora akisema mambo kama hayuko mbali sana, na wakikaribia tu kumaliza ajulishwe ili awahi huko upesi. Lexi akaondoka baada ya kuona Nora ameshusha simu yake.

Baada ya dakika tano hivi, Lexi akarejea hapo akiwa na Imagi zingine mbili na kuketi.

"Mm... umeleta zote hizo kwa ajili yako?" Nora akauliza.

"No, moja kwa ajili yako," Lexi akajibu.

"Ooh... nahofia nitaanza kusinzia ikiwa nitakunywa nyingine..."

"Siyo kali sana hizi..."

"Eti eeh? Basi zinywe wote wewe..."

Lexi akacheka.

Nora akawa anamwangalia sana mpaka Lexi akajishtukia.

"Vipi mheshimiwa, mbona unaniangalia hivyo?" Lexi akamuuliza.

"Macho yako mazuri sana Lexi," Nora akafunguka.

Lexi akabaki kumtazama tu. Nora akajishtukia kuwa alisema jambo ambalo huenda halikuwa sawa kwa njia fulani.

"Oh, samahani... nime... namaanisha wewe ni.... ila... katika njia ya kawaida. Nafikiri wine imenikolea," Nora akasema kiajabu-ajabu na kunywa tena wine.

"Sijui labda unataka kwenda kuogelea, au kuna kitu unataka kuniambia?" Lexi akauliza baada ya kuwa amemsoma.

"Kuogelea?"

"Yeah..."

"Kwa sasa hivi? Sijavaa nguo ya kuogelea kama unavyoona..."

"Ahahahah... ndiyo najua. Namaanisha, nahisi kama vile kuna kitu unataka kusema lakini unajizuia," Lexi akaongea ukweli bila kupindisha.

Nora akamwangalia tu.

"Siyo lazima ukae nayo kama siri, niambie tu. Kwa mfano, mimi siri yangu ni kwamba napendaga kukaa ndani uchi nikiwa nimeboeka..."

Nora akacheka na kusema, "Siyo siri tena..."

"Siyo siri tena," Lexi akamalizia.

"Ahahah... hamna kitu wala. Nisamehe kama nimekufanya unione wa ajabu," Nora akamwambia.

"Hamna kitu kama hicho. Besides... ninajua unachofikiria," Lexi akamwambia.

"Kweli?" Nora akamuuliza kiudadisi.

"Ndiyo."

"Nawaza nini?"

"Unawaza... kwamba kwa mwanamke wa aina yangu, kuna vitu vingi sana ambavyo nimewahi kufanya lakini wewe hukuwahi kufikiria kufanya. Kuwa hapa pamoja nami inakufanya ujihisi utofauti fulani, na unataka sana kujua ni mambo yapi mtu kama mimi napitia kwa sababu ninaonekana kuwa na siri nyingi... na kwa kuwa wewe ni mtu ambaye unapenda kufichua siri, unataka kuzijua na zangu... unitalii mimi... ujue inakuwa vipi kuwa mimi.... hata unawaza ingekuwa poa zaidi kuniona nikiwa bila nguo...." Lexi akamwambia.

Nora akatabasamu kwa hisia huku akimwangalia sana.

"Unawaza pia kwamba mimi ni mzuri. Unafikiri mimi ni.... mrembo..." Lexi akasema.

Nora akaangalia chini kidogo, kisha akatikisa kichwa kukubali na kumtazama tena.

"Halafu sasa unawaza... nini kitafata baada ya mimi kusema hivi vitu. Unataka kuona kwa mtu wa aina yangu... nitafanya nini nikiwa nimeshajua kwamba unawaza vitu hivyo juu yangu..."

Nora alipendezwa sana na maneno ya Lexi. Kiukweli alianza kuhisi ni kama alikuwa anaongea na mtu tofauti na yule aliyemwona mbele yake, bila kujua kihalisi kuwa ndani ya mwili wa mwanamke huyo ilikuwa ni mwanaume. Wakaendelea kutazamana kwa sekunde chache, kisha Lexi akamsogelea karibu kabisa na uso wake. Nora alikuwa ameshikwa na msisimko fulani hivi wa ajabu, akitarajia mengi sana hapo, naye Lexi akaisogeza midomo yake mpaka kwenye midomo ya Nora na kumpiga busu laini.

Lexi akaanza kuinyonya midomo ya Nora taratibu, naye Nora ni kama akawa anamfungulia njia tu Lexi ili atalii mdomo wake. Lexi alimpa denda nzuri sana karibia sekunde 30, kisha akajitoa mdomoni mwake na kujirudisha nyuma huku akimwangalia kwa makini. Nora yeye akawa anamwangalia kama mtu asiyeelewa hisia zake vizuri, kwa sababu Lexi ndiye aliyekuwa "mwanamke" wa kwanza kuwahi kumpiga busu katika maisha yake, hivyo hisia alizomjengea hapa zilikuwa na utofauti fulani mkubwa.

"Unaonaje?" Lexi akamuuliza.

Nora akabaki tu kumtazama na kuishia kusema, "Aam...."

Simu ya Nora ikaanza kuita. Akaichukua kutoka mfukoni mwake na kukuta ni Mario, naye akapokea. Mario alikuwa anamjulisha kwamba mchoro wa sura ya huyo "Erick" ulikuwa umekamilika, nao walikuwa wameshaanza kutafuta ufanani wa picha hiyo na mtu halisi, hivyo Nora akasema angefika upesi. Lexi, akiwa anajifanya hasikilizi maongezi hayo, akatambua kuwa kulikuwa na jambo fulani kuu linaendelea.

"Lexi... nahitaji kwenda. Tuta... tutakutana tena... nafikiri," Nora akamwambia na kusimama.

"Okay, you know what? Mimi pia nitaondoka maana itaboa kukaa hapa peke yangu. Twende," Lexi akasema na kunyanyuka pia.

Wakaviacha viti vile pale, huku Lexi akizibeba zile Imagi mbili na kuondoka pamoja na Nora.

Walipofika sehemu ambayo Nora aliegesha gari lake, Lexi akamuaga na kuelekea upande mwingine, kisha Nora akaingia upesi ndani ya gari na kuliwasha. Lakini alipolirudisha nyuma kidogo, akatambua kulikuwa na tatizo kwenye tairi, naye akashuka na kukuta pancha kwenye matairi mawili. Akakasirika na kujiuliza zilitokea wapi wakati aliliacha gari bila pacha hapo. Lakini msababishi wa pancha hizi alikuwa ni Lexi. Alipomwacha Nora wakati ule kwa kigezo cha kufata vinywaji, alikuja na kulitia pancha gari la Nora kwa makusudi, akiwa na lengo fulani akilini.

"Vipi Nora?"

Nora akageuka na kukuta ni Lexi ndiyo amemuuliza hivyo. "Lexi... bado hujaondoka?" akamuuliza.

"Yeah... nilikuwa nataka kuondoka nikaona umeshuka tena kutoka kwenye gari. Kuna tatizo?" Lexi akauliza kama vile haelewi somo.

"Puncture. Mbili kabisa. Na ninahitaji kuwahi sijui kama kwa... nitachukua taxi tu," Nora akasema.

"Oh no, ikiwa unahitaji, twende kwa gari langu. Kuna nafasi ya kutosha," Lexi akasema.

"Okay, asante sana Lexi..."

"Bila shaka... let's go."

Wawili hawa wakaelekea kwenye gari la Lexi. Ilikuwa ni gari aina ya Audi SR7 Sportback nyeusi, na baada ya Nora kuiona akamwambia Lexi kweli sasa amethibitisha zaidi kwamba mwanamke huyo alikuwa wa kishua. Lexi akampatia funguo Nora ili yeye mwenyewe aendeshe mpaka kufikia alipohitaji, naye Nora akakubali na kuwaondoa hapo. Nia ya Lexi ilikuwa ni kutaka kujua Nora na wenzake walipoweka makao na kufanya uchunguzi wao, ili ikiwezekana apange na timu yake kuja kupavamia wakati ambao hawangekuwepo na kuiba au kuharibu kila kitu walichofanyia utafiti.


★★


Nora aliendesha mpaka huko na kuegesha gari umbali mfupi kutokea jengo lile. Akamshukuru Lexi na kushuka, kisha akawahi kuelekea ndani kule. Sasa Lexi akawa amepaona, lakini tena bado alitaka kujua ni nini kiliendelea kwa wakati huu, na baada ya kufikiria njia kadhaa, ni kama muujiza ukawa umetokea. Nora alikuwa ameisahau simu yake ndani ya gari, hivyo Lexi akaichukua na upesi kuelekea huko kwa kigezo cha kutaka kumpelekea simu Nora ili aweze kuchungulia baadhi ya vitu humo ndani.

Jengo hili lilikuwa limejitenga sana na majengo mengine kwenye eneo lililo na uoto wa asili, kukiwa na vyuma vyuma vingi nje na makontena mawili ya magari makubwa kwa nje yaliyoachwa kwa muda mrefu. Alipofika langoni, Lexi alisukuma tu na kuingia kwa kujiamini kabisa, na hapo akaweza kuwaona wanaume kadhaa pamoja na Nora kwa mbele, kutia ndani Nathan. Aliyeanza kumwona Lexi alikuwa ni Vedastus, naye akamwangalia kiukali na kuanza kumfata.

"Wewe! Unafanya nini humu?"

Swali la Vedastus likawafanya wengine waangalie upande wa mlango wa kuingilia, naye Nora akamwona Lexi.

Lexi akasema, "Aa... samahani... nilikuwa...."

"Njoo hapa. Nani amekuruhusu kuingia humu?" Vedastus akamuuliza kiukali huku akimfata.

"Veda, Veda, subiri... namfahamu..." Nora akamwambia kwa tahadhari.

"Nani huyo?" Luteni Michael akamuuliza.

"Ni rafiki yangu. Lexi... njoo," Nora akasema.

Lexi akampita Vedastus akijifanya anaogopa fulani hivi, naye akafika usawa wa Nora, aliyesogea kukutana naye.

"Vipi?" Nora akauliza.

"Ulisahau simu yako," Lexi akasema na kumpatia.

"Oh, asante," Nora akaipokea.

Kwa jicho la kuibia, Lexi alitazama screen ya kompyuta alipokaa Bobby, na hapo akaona picha iliyofanya mapigo ya moyo wake yaanze kukimbia kwa kasi.

Ilikuwa ni picha ya Oscar!


★★★★★★★★★

 ITAENDELEA 

★★★★★★★★★

Previoua Next