Masaki, Dar es Salaam
Alhamisi, Februari 20 — Saa 5:00 Usiku
Alijivua nguo zake taratibu, akiwa amezubaa kama mtu alietoka kuamka ndotoni. Na alipobaki uchi, alichagua kuvaa night dress nyekundu iliokolea ili damu isionekane kwa haraka.
Beatrice Nyaki alikikagua kile chumba cha kulala kwa mara ya mwisho na kutambua kilikuwa ni chumba kizuri mnoo ambacho kiliweza kumlea kwa zaidi ya miaka thelathini sasa, na kilikuwa kiko safi na nadhifu.
Alifungua droo ya meza ya pembeni ya kitanda, akachukua bastola yake. Bastola hiyo ilikuwa nyeusi inayong’aa, na chuma chake kilikuwa na ubaridi wenye kutisha. Aliiweka kando ya simu mezani, kisha akapiga namba ya binti yake, Brenda, aliyekuwa akiishi Nairobi.
Akasikiliza mlio wa simu ukilia kutoka mbali. Kisha sauti ya upole ikasikika.
"Halo?"
"Brenda… nimejisikia kuisikia sauti yako, mpenzi wangu."
"Wooow!! What a nice surprise, Mom."
"Natumai sijakuamsha binti angu?"
"Hapana. Nilikuwa nasoma kitabu changu nikitafuta usingizi mama. Mimi na Brian tulitoka kwa ajili ya chakula cha jioni, lakini hali ya hewa ilikuwa mbaya. Mvua imenyesha kweli huku kwetu. Huko vipi?"
Ee Mungu wangu, Beatrice alifikiria, tunazungumza kuhusu hali ya hewa, wakati kuna mengi natBrenda kumwambia… lakini siwezi.
"Mama? Bado upo?"
Beatrice akatazama dirishani. "Huku mvua inanyesha pia."
Na akawaza, Inaendana sana na hisia zangu. Kama kwenye movie ya Her Side of Silence.
"Huo ni sauti kubwa ni kitu gani mama?" Brenda akauliza.
Ngurumo. Beatrice alikuwa amezama sana katika mawazo yake kiasi cha kutoisikia. Dar es Salaam ilikuwa katika dhoruba. Mvua ya siku nzima, matabiri wa hali ya hewa kutoka kituo kikubwa cha habari hapa Dar, alikuwa amesema hali ya hewa ya siku hio ni yuzi joto sitini na sita. Na Usiku, mvua ingezidi zaidi na kuambatana na radi.
"Msisahau miamvuli yenu," walikuwa wameonya. Lakini Beatrice alikuwa haitaji mwavuli.
"Ni ngurumo ya radi hiyo, Brenda." Akajitahidi kuweka furaha kwenye sauti yake.
"Niambie yanayojiri huko Nairobi."
"Najihisi kama malkia kwenye hadithi za kale, Mama." Brenda alisema kwa shauku.
"Sikuamini kabisa kuwa mtu anaweza kuwa na furaha kiasi hiki. Kesho usiku nakutana na wazazi wa Brian."
Akabadilisha sauti madoido kama vile mtu anaesoma tangazo kwa sauti ya heshima: "The Okello, of Muthaiga," Akimanisha familia ya Okello kutoka Muthaiga.
"Ni watu maarufu sana huku. Nina wasiwasi sana mama."
"Usihofu. They will love you, darling."
"Brian anasema haitajalisha hata kama watanikataa. Ananipenda. Na mimi nampenda mno. I cant wait for you to meet him. He is so special mom."
"I'm sure he is special, darling."
Lakini Beatrice alijua fika hawezi kukutana na Brian, wala asingekuwepo kumpokea na kumbeba mjukuu wake katika mapaja yake. Hapana, sipaswi kufikiria hivyo.
"Does he know how lucky he is to have you, baby?
"Hivi anaelewa ana bahati sana kuwa na wewe?
"Kila siku namwambia." Brenda akacheka.
"Vipi kuhusu wewe mama? Kuna yanayojiri huko? Unajisikiaje?"
Beatrice alisema anajisikia vizuri. Kwa kweli, alikuwa na afya njema. Daktari wake, Dkt. Rushi, alikuwa amesema: "Upo kwenye afya bora kabisa. Utaishi mpaka miaka mia." Moja ya kejeli zake za maisha.
"Najisikia poa kabisa."
"Na vipi kuhusu mpenzi? Tayari ushapata?" Brenda akamdokeza kwa utani.
Tangu mume wa Beatrice alipofariki miaka mitano iliyopita, hakuwahi kufikiria kuwa na uhusiano tena, licha ya msukumo kutoka kwa Brenda.
"Hakuna mpenzi."
Kisha akaamua kubadili mada:
"Kazi yako je? Unaendelea kuifurahia?"
"Nai-enjoy sana. Brian hana tatizo nikibaki kazini hata baada ya ndoa yetu."
"Hilo ni jambo zuri, mpenzi wangu. Anaonekana ni mtu muelewa sana."
"Ni kweli. Utajionea mwenyewe."
Kulisikika kishindo kikubwa cha radi - kama ishara ya mwisho mfano wa igizo stejini huku mapazia yakijifunga ikimanisha igizo lilikuwa limefikia tamati. Ilikuwa ndio wakati. Hakukuwa na maneno mengine zaidi ya kusema, isipokuwa kwaheri ya mwisho.
"Kwaheri, mpenzi wangu," Beatrice alitamka kwa sauti ya utulivu wa makusudi.
"Tutaonana kwenye harusi, mama. Nitakupigia simu mara tu mimi na Brian tutakapopanga tarehe rasmi."
"Sawa kipenzi changu." Lakini kulikuwa na jambo moja la mwisho kusema.
"Nakupenda mno, mno, Brenda." Na Beatrice Nyaki akaweka mkononi simu taratibu.
Akaichukua bastola mkononi mwake.
Kulikuwa na njia moja tu, ya kulitimiza jambo hili kwa wepesi…. Njia yenyewe ni kulifanya kwa haraka.
Akaielekeza bastola upande wa kichwa chake na kubonyeza trigger ya kutoa risasi.
Comments