Nairobi
Brenda alikutana na Brian Okello kwenye kongamano la kifedha ambapo Brian alikuwa mzungumzaji na mgeni rasmi. Alikuwa anaongoza taasisi ya uwekezaji iliyoanzishwa na babu yake mkubwa, na kampuni yao ilikuwa na biashara nyingi na benki ambayo Brenda alikuwa anafanyia kazi.
Baada ya hotuba ya Brian, Brenda alimsogelea ili kubishana na maoni yake kuhusu uwezo wa nchi za dunia ya tatu kulipa riba kubwa za mikopo waliyokopa kutoka kwa mabenki ya kibiashara ya kimataifa na serikali za magharibi. Mwanzoni, Brian alicheka kwa mchanganyiko wa mshangao na kuvutiwa - hakutarajia kupewa changamoto hadharani na mwanamke mrembo mwenye hoja kali.
Majadiliano yao yaliendelea hadi wakati wa chakula cha jioni katika Mgahawa wa Nyumbani wa Luthuli, mgahawa wa kihistoria uliojaa hadithi nyingi.
Mwanzoni, Brenda hakuwa na mvuto wowote kwa Brian Okello, licha ya kutambua kwamba alihesabiwa kama "mwanaume wa ndoto" wa Nairobi." Brian alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano, tajiri, mwenye mafanikio, na anatoka kwenye moja ya familia mashuhuri Afrika mashariki.
Alikuwa na urefu wa futi tano na inchi kumi, nywele zake rangi ya mchanga zikiwa zimeanza kupungua, macho ya kahawia, na tabia iliyochanganya na uelewa mkubwa wa mambo mengi na hulka ya kihistoria. Brenda alidhani,
"Huyu ni mmoja wa wale matajiri wanaoboa."
Ni kama Brian alisoma mawazo yake, akainama juu ya meza na kusema:
"Baba yangu anaamini alipewa mtoto wa mtu mwingine hospitalini."
"Whaat?" Brenda akastaajabu.
"I'm a throwback. I don't happen to think money is the end-all and be-all of life. But please don't ever tell my father I said so."
"Sina imani kwamba pesa ndiyo mwisho wa kila kitu maishani... lakini tafadhali usimwambie baba yangu nimesema hivyo."
Kuna kitu cha kuvutia na cha unyenyekevu wa kweli ndani ya Brian kilichomvutia Brenda polepole.
Nashangaa sana, sijui itakuwaje kuolewa na mtu kama huyu - mtu mwenye ubwanyenye wa jadi?
Ilimchukua baba yake Brenda karibu maisha yake yote kujenga biashara ndogo ambayo familia ya Okello wangeibeza kama kitu cha kawaida kisicho na thBrenda.
“Wazazi wa Brenda na wazazi wa Brian hawawezi kuchanganyika.” Alijiambia. “Mafuta na maji. Na familia ya Brian ndio mafuta.”
“Na mimi naongea nini sasa kama mpumbavu? Huyu mtu amenialika chakula cha jioni halafu mimi tayari nawaza kuhusu ndoa? Labda hata hatutawasiliana tena.”
Kisha Brian akamuuliza:
"I hope you're free for dinner tomorrow...?"
"Natumani kesho usiku utakuwa free kwa... chakula cha jioni?"
********
Nairobi ilikuwa jiji lililojawa na vivutio na shughuli mbalimbali. Jumamosi jioni, Brenda na Brian walihudhuria shoo za ngoma za taifa au wakamwona Maalim Rashid akiiongoza Orchestra ya Taifa ya Kenya katika ukumbi wa Goethe Institute.
Wiki nzima, walizunguka maeneo ya Village Market na maduka ya kipekee ya brands kubwa duniani kama LVMH, Chanel, Hermès, Gucci, Dior, Prada, na Versace.
Walikula mishkaki na chipsi za barabarani katika Luthuli Avenue, na walipokuwa wanataka hali ya kifahari walikula chakula cha usiku katika The Lord Erroll - moja wa migahawa ya kifahari jijini Nairobi.
Walitembea kupitia Makumbusho ya Taifa na Nairobi Gallery, na wakati mmoja Brenda alisimama mbele ya sanamu ya Mfikiriaji.
Alimtazama Brian na kucheka:
"Huyu ni wewe kabisa!"
Brian hakuwa mtu wa mazoezi, lakini Brenda alipenda sana kufanya mazoezi ya mwili. Kila Jumapili asubuhi alikimbia pembezoni mwa barabara ya Waiyaki Way au Uhuru Park. Pia alikuwa ni member wa darasa la yoga na T’ai Chi yanayofanyika kila Jumamosi mchana, na baada ya mazoezi yake- akiwa amechoka lakini mwenye furaha – ratiba yake ilimuelekeza kukutana na Brian kwenye ghorofa yake.
Brian alikuwa mpishi hodari mwenye kupenda kujaribu vyakula vya kimataifa. Alipika mlo wa bistilla ya Morocco, guo bu li (vitumbua vya China Kaskazini), na kuku wa Kiasili waliopikwa kwa limao na karafuu kwa ajili yao wawili.
Brian alikuwa ni mtu mwenye kujali mda kuliko mtu yeyote ambaye Brenda alikuwa amewahi kukutana naye. Siku moja, Brenda aliwahi kuchelewa kwa dakika kumi na tano kwenye mlo wa jioni waliopanga pamoja - na uso wa Brian uliojaa kutoridhika ulimuharibia Brenda usiku wake wote.
Tangu siku hiyo, Brenda alijiapiza kamwe hatochelewa tena pindi watakapo kuwa na mtoko au ratiba yeyote.
Likija swala la mapenzi, Brenda hakuwa na uzoefu mkubwa sana. Lakini hilo halikumzuia kutambua kwamba Brian alifanya mapenzi kwa staili moja kama ambavyo anaishi maisha yake: kwa ustaarabu mwingi, hatua zilizopimwa, na nidhamu kali. Siku moja, Brenda aliamua kujitoa akili na kuwa wa tofauti - akaamua kuwa jasiri na asiye na mipaka kitandani. Lakini hilo lilimshangaza sana Brian na kumfanya amtazame kwa namna flani mpaka ikambidi Brenda ajiulize kwa siri: Je, mimi naonekana napenda sana kunjunjana? Au nina hamu sana ya kufanya?
Mimba hiyo haikutarajiwa, na ilipomtokea, Brenda alijawa na wasiwasi. Brian hakuwa amewahi kuzungumzia ndoa, na Brenda hakutaka kumlazimisha kwa sababu ya ujauzito huo.
Hakujua kama angeweza kufanya uamuzi wa kutoa mimba, lakini chaguo jingine lilikuwa na uzito ule ule wa kiakili: Je, nitaweza kumlea mtoto huyu peke yangu? Na je, hilo litakuwa la haki kwa mtoto?
Alifanya uamuzi wa kumwambia Brian habari hiyo baada ya chakula cha jioni, usiku mmoja. Alikuwa ameandaa cassoulet, chakula cha nyama na maharagwe, kwa ajili yake kwenye apartment yake. Lakini kutokana na hofu iliyojaa ndani yake, aliunguza chakula.
Alipoweka mbele ya Brian huo mlo ulioungua, alisahau kabisa hotuba aliyokuwa amejiandaa nayo - na kwa ghafla, kama mtu aliyeteleza, akatamka:
“Brian I'm--- pregnant."
"Brian... mimi... mimi ni mjamzito."
Ukafuata ukimya mzito wa kuumiza moyo. Brenda alipokuwa karibu kuvunja kimya hicho, Brian akasema:
"We'll get married, of course."
"Tutaoana. Bila shaka."
Brenda alijawa na hisia ya utulivu na ahueni isiyoelezeka.
"I don't want you to think I--- You don't have to marry me, you know.”
"Sikutaka ufikiri kwamba... kwamba lazima niolewe kwa sababu ya hii hali. Usiwe na shinikizo, Brian."
Lakini Brian alinyanyua mkono wake, akamkatisha.
"Ninataka kukuoa, Brenda. Utakuwa mke mzuri sana."
Kisha akaongeza kwa polepole:
"Kwa hakika, mama yangu na baba wataona mshangao kidogo."
Akampigia busu la upole.
Brenda akauliza kwa sauti ya upole:
"Kwa nini watashangaa?"
Brian aliguna.
"Darling, I'm afraid you don't quite realize what you're letting yourself in for. The Okellos always marry--- mind you, I'm using quotation marks-- 'their own kind.' Mainline Kikuyu."
"Mpenzi... nahisi bado hujagundua kabisa unakoenda kuingia. Familia ya Okello huwa wanaoa - nasisitiza kwa alama za nukuu - 'aina yao wenyewe'. Wakikuyu. Wanajiona wao ni 'wasomi wa miji mikuu ya Kenya'."
"Na tayari walikuwa wamekuchagulia mchumba, sio?" Brenda akatabiri kwa sauti ya utani.
Brian akamvuta Brenda kwenye mikono yake:
"Hilo halina maana yoyote kwangu. Kinachojali ni nani nimechagua mimi. Jiandae Ijumaa ijayo nitakutambulisha kwa wazazi wangu kwa ajili ya dinner. Wakati umefika sasa wa wao kukujua mpenzi wangu."
Note: Brian alitoka katika familia ya Kikuyu wa tabaka la juu-jamii yenye ushawishi mkubwa nchini Kenya, haswa katika siasa, biashara, na elimu. Wakiwa na asili ya Mlima Kenya, Wakikuyu hawa wa "mainline" mara nyingi huishi mijini kama Nairobi na Kiambu, na hujiona kuwa waliosoma, waliostaarabika, na waliorithishwa majina yenye heshima. Kwao, ndoa ni muunganiko wa koo, hadhi, na mirathi ya kifamilia-si tu suala la mapenzi. Hivyo basi, kwa Brenda, msichana kutoka Tanzania, ambaye hana mizizi ya ukoo Kenya, kuingia kwenye familia kama hiyo ni kuingia kwenye ulimwengu unaoendeshwa na mila zisizoandikwa, matarajio ya vizazi, na macho ya ukoo mzima.
Comments