Reader Settings

Jengo refu la Velora Company lilisimama mithili ya mnara wa mamlaka katikati ya jiji. Sakafu ya mwisho, iliyozungukwa na kuta za kioo kilichochongwa kwa ustadi, ilihifadhi utulivu uliokuwa wa kipekee. Hapo ndipo alipokuwapo. Mwanamke ambaye hakuhitaji sauti ya juu kuamrisha, wala sura kali kuogopwa—macho yake yalitosha

Wengi walimtazama kama binti wa kizazi kipya—lakini ofisini, hakuna aliyeweza kumsogelea bila heshima ya hali ya juu. Alizoea kufanya maamuzi mazito akiwa ameketi mkao wa kawaida kabisa, kama mtu aliyekulia kwenye meza za wakuu wa dunia.

Wengine waliwahi kusema, “Mwanamke huyo si tajiri tu, labda ni kiumbe kutoka sayal nyingine.”

Wengine walimuita kivuli cha familia ya kifalme ya biashara.

Lakini kwa watu waliomjua kwa jina, waliita kwa sauti ya mchanganyiko wa hofu na heshima:

Diana.

Mlango wa ofisi yake ulifunguliwa kwa heshima. Msaidizi wake wa karibu, msichana mwenye umbo dogo na uso uliojaa nidhamu—Naila—aliingia kwa mala nyingine taratibu. Mikononi mwake alishikilia faili la samawati.

“Mkulugenzi,” alisema kwa sauti tulivu lakini thabiti, “hili ni faili kutoka kwa Royal Shield Security. lina taarifa zote.”

Diana aliinua macho kwa taratibu. Akamwangalia Naila bila tabasamu, lakini macho yale yalikuwa na maana elfu moja. Bila kusema neno, alinyosha mkono wake, na kulipokea faili kwa umakini.

“Walileta saa ngapi?” aliuliza, sauti yake ikiwa kama mvua ya usiku—tulivu lakini yenye uzito.

“.Ni Dakika chache tu zilizo pita. Wamesema kila kitu kiko ndani. Uhakiki, wasifu, rekodi na picha. Kama ukikubaliana, wanaweza kupanga utambulisho rasmi,” Naila alijibu kwa staha.

Diana alinyamaza. Alishika faili hilo kwa mikono miwili, akalisogeza mezani, lakini hakulifungua. Badala yake, aliangalia juu kidogo kama aliyekuwa akisoma maandiko yasiyoonekana kwenye dari la kioo.

“Naila,” alitamka kwa sauti ya chini lakini yenye mamlaka, “niachie hili hapa. Nitalipitia baadaye.”

“Una uhakika Mkulugenzi? Maofisa wa kampuni walionekana—”

“Nimekwambia nitalipitia baadaye,” alirudia kwa utulivu wa mtu mwenye utaratibu usiopingika.

Nila akainama kidogo, akatoka, akifunga mlango kwa uangalifu.

Diana alibaki peke yake. Ukimya ulitanda kana kwamba chumba kizima kilikuwa kikisubiri yeye afungue faili hilo. Lakini hakulifungua. Alilikazia macho tu, kana kwamba alikuwa akisubiri faili hilo lijifungue lenyewe.

Kwa sababu moyoni mwake… kulikuwa na hisia kuwa ndani ya faili hilo, hakukuwa na mtu tu—kulikuwa na tukio, sura, au kivuli ambacho kingebadilisha kila kitu.

Na kwa mara ya kwanza, jina lisilosikika likaanza kuchora mstari wa hatima kati ya nguvu, siri, na moyo wake wenye barafu.

*****

Siku hiyo liam mala baada ya kutoka kwenye ile interview alikua yuko tu nyumbani kutokana na kua mgeni hakua na malafiki wala mtu yoyote anae mfahamu zaidi ya Edina.Kwa siku nyingi sasa tangu arejee nchini, maisha ya Liam yamekuwa ya kimya. Alikuwa kama kivuli kinachopita mitaani bila kugusa ardhi. Aliishi kama mtu wa kawaida, kwa bidii akiepuka kujadili maisha yake ya zamani, hata na watu wachache waliomfahamu juu juu.

Lakini jioni hiyo, kuna kitu kilimsukuma. Labda ilikuwa hewa ya joto-joto yenye unyevunyevu, au ile kelele ya mbali kutoka kwenye bar ya jirani, au labda ni mwangwi wa ndani uliomwambia:

Akasimama taratibu, akakunjua mikono kama mtu aliyekuwa amepotea katika usingizi mrefu. Akaelekea bafuni, akaoga kwa maji ya uvuguvugu, akavaa suruali ya jeans nyeusi na fulana ya buluu yenye maandishi madogo ya kifaransa. Kiatu cha kisasa cha Nike alichokivaa kilikamilisha muonekano wake wa mtu ambaye hakuwa na haraka na dunia.

Alifungua simu yake, akaingia kwenye Bolt, na kuweka oda:

Wakati akisubiri, alisimama kwenye varanda yake ndogo, akinywa maji ya chupa, macho yake yakitazama magari yakipita taratibu barabarani.

Baada ya dakika saba, gari lilifika. Toyota Axio nyeusi iliyo safi. Dereva alimpigia honi fupi.

Liam taratibu, akafunga mlango wa nyumba yake, akapanda kwenye gari bila kusema mengi.

“Karibu boss,” dereva alimsalimu kwa heshima.

“Asante kaka nipeleke club yoyote ilio changamka ,” Liam alijibu kwa sauti ya kawaida.

Sawa hakuan shida boss," alijibu deleva huyo hakuonekana kua na maneno mengi kama ilivyo kwa madereva wengine

Njia nzima liam, alikaa kimya, macho yake yakizunguka kutazama jiji lilivyo. Aliona vijana waliovaa vizuri wakitoka maeneo ya Mikocheni, wanaume waliokaa pembeni mwa bar wakijadili siasa, akina dada waliokuwa kwenye bodaboda wakicheka kwa sauti kubwa, na taa za jiji zikiwa zinachomoza kwa rangi zenye ahadi ya usiku mrefu.

Alipofika, taa za club ziliangaza kwa rangi ya zambarau na samawati clubhiyo iliitwa Mzuka Empire. Muziki wa Afrobeat ulikuwa unavuma kwa nguvu ndani ya kuta. Watu walikuwa wanapiga picha nje, wengine wakifuta jasho kabla ya kuingia tena kucheza.

Mala baada ya kumalizana na taks au bolt,Uber Mlinzi alimwangalia kwa makini. Liam hakuwa mtu wa kupita bila kutazamwa mara mbili. Ukarimu wake wa kimya na sura iliyokuwa na mchanganyiko wa huzuni na mvuto, vilimfanya aonekane tofauti.

“Karibu ndani ndugu yangu,” mlinzi alisema kwa heshima.

Liam alitabasamu kidogo na kuingia.

Ndani, club ilikuwa hai kama moto. Taa zilizocheza sakafuni, muziki uliotia moyo, na harufu ya pombe mchanganyiko na marashi ya bei ghali vilimkaribisha kama mkono wa dunia ukimwambia: “Karibu tena.”

Alichukua kiti pembeni ya meza ya kona, karibu na dancefloor lakini si katikati. Alimwamuru mhudumu:

“Niwekee whisky kavu. Bila barafu. Shot mbili tu mwanzo.”

“Unaonja au unaanza?” mhudumu alitania kwa kicheko.

Liam akasema bila kutabasamu, “Naweka utulivu kwenye damu.”

Mhudumu alicheka.”

Alipotazama wachezaji wa dancefloor, watu waliocheka, waliokumbatiana, waliopoteza muda katika raha, Liam alijihisi mtu wa dunia kwa mara ya kwanza. Alijihisi tangu alipo ingia Tanzania ni kama maisha yake yamebadilika. Hakuhisi kuwa tofauti.

Kwa siku hiyo Liam alikuwa tu kijana wa kawaida, aliyeamua kunywa usiku mmoja, katika mji ambao bado unajaribu kumkumbatia.

Usiku uliendelea kupamba moto ndani ya Aurum Lounge. Muziki ulishika kasi, taa ziliendelea kucheza na kuangaza kwa rangi zilizokata giza, na sauti za vicheko, vilio vya furaha na kelele za music kuchezwa mezani vilichanganyika

Liam alikuwa ameegemea nyuma kwenye kiti chake, kinywaji mkononi, macho yakiwa yanacheza juu ya sakafu ya club lakini akili yake ikiwa kimya kabisa. Alikuwa na utulivu wa mtu asiye na haraka, mtu ambaye dunia haimpigi kelele. Lakini ndani ya macho yake kulikuwa na mwangaza wa mtu ambaye hawezi kupuuzwa.

Katika kona moja ya club, kwenye meza iliyojitenga na msongamano, mwanaume mmoja mrefu, aliyevalia suti nyeusi ya kuvutia na shati jeupe lililotulia kifuani, alikuwa akimwangalia Liam. Tangu Liam alipoketi, mwanaume huyo hakuacha kumfuatilia kwa macho. Ilikuwa si macho ya uhasama, bali ya kuchunguza, kuchambua—kama mtu anayemwangalia mgeni aliyeingia kwenye himaya yake.

Liam alihisi. Hakuwa mtu wa kawaida; hisia zake zilikuwa makini. Aligeuza shingo kidogo, akapeleka macho kwa haraka kwenye kona ile. Walipokutana macho na yule mwanaume, mwanaume huyo alicheka kidogo tu na kunywa kinywaji chake kana kwamba hakukuwa na chochote cha ajabu. Liam alimpuuza. Akaendelea na kinywaji chake.

Dakika chache baadaye, kama upepo wa manukato mazito ya Chanel, mwanamke mmoja mrembo sana alijitokeza karibu na meza ya Liam. Alikuwa mrefu kiasi, amevaa nguo ya kijivu iliyomkaa mwilini kama ngozi ya pili, na viatu virefu vilivyofanya miguu yake ionekane kama ya malkia. Alikuwa amekunja nywele kwa ustadi wa kisasa, na midomo yake mekundu ilisonga kwa tabasamu la kujiamini.

"Hi... Samahani, naweza kukaa hapa?" aliuliza bila hofu wala aibu, huku akiweka mkono wake mmoja mezani kama mtu aliyeshafika.

Liam alimtazama kwa sekunde chache, kisha akasema kwa sauti ya utulivu, "Ni meza ya wazi. Karibu."

Akatabasamu kwa upana, akaketi.

"Naitwa Sasha," alisema moja kwa moja, akimpelekea Liam mkono wa salamu. "Wewe ni nani? Au nikuite Mr. Hendsom?"

Liam alicheka kidogo kwa puani, akachukua mkono wake na kusema, "Liam."

"Liam," alirudia kwa sauti tamu kama melody. "Jina lako linaendana na sura yako. Mtu asiye na kelele, lakini hatakiwi kupuuzwa."

Aliongea naye kwa muda, akicheka, akimuuliza maswali, akimsifia fulana yake, macho yake, hata jinsi alivyoegemea kwenye kiti. Liam alijibu kwa staha, lakini bila kumpa nafasi ya kuingia ndani zaidi. Alijua aina hiyo ya wanawake—wanaokuja kama moto wa karatasi, unaowaka haraka lakini haudumu.

Lakini kadri walivyoendelea kuzungumza, Liam alihisi macho mengine yakiwa juu yao. Kisha kelele ya kistaarabu ya club ikakatizwa ghafla na sauti ya mwanaume iliyopasua utulivu wake:

"Sasha!"

Sauti hiyo ilijaa mshangao, hasira na uchungu. Watu waliogeuka, baadhi wakikodolea macho. Sasha alishika kichwa, kana kwamba alisahau kitu muhimu sana. Liam aligeuza uso wake, akamwona mwanaume mmoja aliyekuwa na mwili wa mazoezi, macho mekundu kwa hasira, akiwa amesimama mbele ya meza yao.

"We unafanya nini hapa? Huyu ni nani sasa?" mwanaume alifoka.

Sasha alijaribu kuongea, "Baby siyo kama unavyofikiria—"

"Usiniite baby hapa mbele ya mtu mwingine! Umenifanya mjinga sasa, eeh?"

Aligeuka kwa hasira kumkazia Liam macho.

"Wewe ni nani? Mwanaume wa watu unaingilia mahusiano ya watu wengine?"

Liam aliinua mikono, akasema kwa sauti ya kawaida kabisa, "Sikufanya chochote. Alikuja mwenyewe na akaketi."

"Usinijibu! We si mwanaume? Unamkubali mwanamke wa mtu? Au unajifanya huelewi?"

Bila onyo, mwanaume huyo alirusha ngumi ya kwanza. Haraka. Ghafla. Lakini Liam alijisogeza upande wa kushoto kwa ustadi wa ajabu—ngumi ikapita hewani. Kabla hajapumua, ngumi ya pili ikafuata kwa hasira zaidi—lakini Liam aliinama na kuepuka tena, bila hata kuonekana kuwa na hofu.

Watu waliokuwa karibu wakashtuka. Sasha akapiga kelele, "Stop it, Jamal! Unafanya nini?"

Liam akasema kwa sauti ya kutulia, "Sijasema tusi. Sijarudisha shambulizi. Nimekueleza ukweli. Shobo ni za mwanamke wako."

Maneno hayo yaliongeza hasira kwa Jamal. Akavuta pumzi kwa nguvu, akajiandaa kurusha ngumi ya tatu—

Lakini kabla hajakamilisha hatua hiyo, mkono mmoja mzito ulianza kushikilia bega lake kwa nguvu. Jamal aligeuka—na uso wake ukakutana na uso wa mwanaume alikua ni yule mwanaumealie kua akimuangalia sana liam.

"Acha. Hii si seemu ya kuanzisha vulugu. Wala si uwanja sahihi," mwanaume huyo alisema kwa sauti ya kuamuru, isiyohitaji kupigiwa kura.

Jamal alitaka kujibu, lakini alipoangalia macho ya mwanaume huyo, akaona jambo aliloshindwa kulitafsiri. Labda ni onyo. Labda ni mamlaka. Labda ni kitu kingine kisichoelezeka.

Akasukuma mkono wake, akageuka kwa hasira na kuondoka huku akitukana kwa chini.

Sasha alifuatilia nyuma yake akipiga kelele, "Baby! Subiri tafadhali! Si kama unavyofikiria!"

Club ikarudia hali ya kawaida taratibu.

Liam aligeuka kumtazama mwanaume aliyemwokoa. Waliangaliana kimya kwa muda mfupi. Halafu, mwanaume huyo akamwambia:

"Sikujua kama ni leo nitakuona uso kwa uso, Liam. Karibu tena nyumbani."

Halafu, bila kusema neno zaidi, aliondoka kuelekea upande mwingine wa club, akapotea kwenye mwanga wa taa za samawati.

Liam alibaki pale mezani, akikodolea macho seemu ambaye mwanaume huyo alisimama kabla ya kuondoka Akili yake ilikuwa bado haijakaa sawa tangu tukio ndani ya club lilipotokea. Mwanamke aliyemshobokea ghafla, mpenzi wake aliyewaka hasira kama moto wa petroli, na yule mwanaume wa ajabu aliyemwokoa. Kila kitu kilihisi kama tukio lililopangwa, lakini hakukuwa na ushahidi

"Liam alikua akiwaza Yule jamaa... alimaanisha nini kusema 'karibu tena nyumbani'?" Ananijua? Aliwai kuonana nae wapi? Au ni bahati mbaya?" Liam alijiwazia

Lakini majibu hayakupatikana. Akili yake haikutoa sauti. Na wakati mwingine, kimya kina maana zaidi ya maneno.

Alihisi kama maneno yale yalibeba kumbukumbu aliyosahau, au njia ya kuelekea kwenye ukweli alioutafuta kwa muda mrefu. Lakini kama kawaida yake, Liam alijua namna ya kuyasukuma mbali maswali ya aina hiyo.

"Acha muda uongee," alijisemea kimoyomoyo.

Kutokana na jambo lililo tokea Liam hakuitaji kuendelea kubaki teka kwenye club hiyo hivyo alichukua maamuzi ya kuondoka

Baada ya kutoka nje ya club Alichukua simu yake ili aliquest Bolt, lakini kabla hajakamilisha, hatua tatu mbele yake alizuiliwa njia. mbele walisimama watu watatu. Mmoja alikuani yule Jamaa aliyemshambulia club aliekua akiitwa jamal na wanaume wengine wawili kuusu yule mwanamke sasha yeye hakuwepo—Jamal—mwenye mwili wa misuli na sura ya dharau. Kulia na kushoto kwake walikuwa vijana wawili waliovaa mashati meusi na suruali za jeans zilizokunjwa

Jamal alitabasamu kwa dharau.

"Ndani ya clubu ulikuwa na bahati, umepata mtetezi. Hebu sasa tuone hapa nje ni nani atakaye kusaidia..."

Liam kusikia hivyo alipigwa na butwaa kwani alizmdhani mambo yote yalikua yamekwisha sasa nan angejua mbumbe ndia kwanza shuhuli imeanza

Jamal aliwaamuru vijana wake kwa ishara ya kichwa. Wakamkaribia Liam kwa kasi, macho yao yakiwa na uchu wa kumshugulikia vyema liam. Mmoja alirusha ngumi ya kulia—Liam aligeuka kwa ustadi, akaisogeza bega kwa kasi, na mkono ule ukapita. Mwingine alijaribu kumpiga teke—Liam alikanyaga mbele ghafla na teke likamkosa mwelekeo.

Kwajinsi walivyo kua wakishambulia ilionekana dhaili hawakua na mafunzo yoyote kwani walishambulia bila mpangilio lakini kadri walivyo jalibu kumshambulia Liam yeye aliwakwepa tu bila kuludisha shambulizi

Kilichowashangaza si kwamba Liam aliwakwepa, bali namna alivyokwepa bila juhudi yoyote. Kama anacheza mchezo anaoujua kwa mazoea

Jamal alisononeka kuona wenzake wakishindwa. Kwa hasira, aliamua kuingia yeye mwenyewe. Lakini licha yavyo haikusaidia chochote kwani kila walipo jalibu ilikua ni kama mtoto anaejalibu kupigana na baba yake

"Bado tu mnataka kuendelea licha ya kunishambulia na mmeshindwa kunigusa hata mara moja?" Liam aliuliza kwa sauti ya kutulia, lakini iliyojaa onyo.

Lakini Jamal hakuacha. Alirusha ngumi ya haraka upande wa kushoto wa uso wa Liam. Liam aliinama kidogo, akaikwepa, na kabla hajainuka vizuri, ngumi ya pili ikaja upande wa kulia. Hata hiyo aliikwepa, akirudi nyuma kwa ustadi wa ajabu.

"Hamwelewi, siyo? Bado tu basi ngoja niwape kile mnacho staili?" aliongeza Liam kwa sauti ya chini ilio jaaa msisitizo.

WILL CONTINUE

Previoua Next