Reader Settings

Lakini hasira iliwapanda zaidi. Wale vijana waliendelea kushambulia, lakini sasa kwa pupa zaidi. Liam alichukua hatua moja tu nyuma na kuwatazama

Kisha akachukua hatua ya kwanza ya kujibu.

Kwa mkono wa kushoto alikamata mguu wa mmoja wao, akavuta kwa nguvu chini na kuliweka goti lake juu ya bega. "Krraack!" Ilisikika sauti ya mfupa wa mguu kuvunjika. Jamaa akapiga yowe, akaanguka.

Mwingine alirudi nyuma kidogo kwa hofu, lakini Liam alishamfikia. Alishika mkono wa kulia wa yule jamaa kwa mzunguko wa ustadi—hakukuwa na fujo, ila uhodari wa kupindua bega na kuuvunja kiwiko. "Krrk!"

Wote wawili walianguka chini wakilalama. Jamal alipigwa na butwaa, lakini kabla hajarudi nyuma, alijikuta Liam amesimama hatua tatu tu mbele yake.

"Bado unataka kuendelea?" Liam aliuliza kwa sauti ya upole, lakini yenye kutetemesha.

"Unajifanya nani wewe?" Jamal alijaribu kurusha ngumi kwa hasira.

Liam aliinamisha kichwa, akakwepa kwa ustadi, akazunguka nyuma ya Jamal kwa wepesi, akamvuta mkono kwa nguvu na kuupinda kwa namna ya ajabu—"Krraack!"

Sauti ya kuvunjika kwa mfupa ikazama katikati ya ukimya wa usiku. Jamal alianguka magotini, akishikilia mkono wake uliokuwa umelegea.

Liam alisimama juu yao watatu waliokuwa chini, wakivuja jasho na maumivu. Akavuta pumzi ndefu, akavua koti lake begani, akalivaa tena taratibu.

Alisema kwa sauti ya chini, bila hasira, lakini ya mwisho"Msinifuate tena. Usiku mwema."

Kisha aligeuka, akatembea kama vile hakukuwa na chochote kilichotokea. Barabara ilinyamazishwa na heshima isiyo ya kawaida—kimya cha wanaume watatu waliovunjwa kwa ustadi, si kwa nguvu, bali kwa ukimya wa mtu asiye na haja ya kujionesha.

****

Pembeni kidogo ya Club Breeze, kulikuwa na jengo lefu la ghorofa. Juu ya ghorofa, alisimama mwanaume mmoja akitazama chini kana kwamba jiji lote liko kwenye kiganja cha mkono wake.

Alikuwa mrefu, mwenye mwili uliojengwa kwa ukimya na mazoezi. Mavazi yake hayakuwa ya kawaida. Alikuwa amevaa joho jeusi lililokuwa linapepea polepole, limeshonwa kwa uangalifu wa hali ya juu, mikunjo yake ikidokeza asili ya kifalme na kumfanya aonekane kupendeza macho.

Uso wake ulikuwa thabiti, bila tabasamu. Alikuwa na ndevu ndogo zilizonyolewa kwa ustadi, na nywele zake nyeusi zilizosukwa kwa njia ya kipekee zilimpa sura ya mtu asiye wa kawaida. Lakini kilichoogopesha zaidi... macho yake. Yalikuwa meusi kupindukia, na ndani yake kulionekana moto hafifu wa bluu uliokuwa ukicheza-cheza kwa mbali.

Alikua ni yule… mwanaume aliyekuwa akimuangalia sana Liam wakati akiwa club muonekano ambao alikua nao muda huwo ni tofauti kabisa na jinsi alivyo kua mwanzo wakati akiwa ndani ya club haikueleweka imekuaje mpaka akawa hivyo.Mda huo hakua na ule uso wa kirafiki, wala tabasamu.

Alisimama huku mikono yake ikiwa imefungwa kifuani, na macho yake yakikazia eneo la club chini. Alishuhudia kila kitu kilicho tokea —tangu Jamal na vijana wake walipomsogelea Liam, hadi jinsi alivyojiepusha kwa ustadi na kuwavunja mikono kiwepesi, kana kwamba alikuwa anacheza chess. Hakuonekana kushangaa wala Hakushtuka. Aliishia kutikisa kichwa kwa dharau.

Kisha akajisemea kwa sauti ya chini na nzito

“We mpuuzi umekuwa dhaifu kiasi hiki? Hahaha… mpaka umeamua kukimbilia Tanzania?”Akatikisa kichwa chake kwa huzuni ya dhihaka. Maadui zako wakijua hili… watakuponda kama funza. Hili ni. Kosa kubwa sana.” nilivyo sikia kua uwezo wako umeshuka sikutaka kuamini ila sikutalajie ingekua ni kwa kiasi hiki

Alinyamaza kwa sekunde chache, macho yake yakiwa bado yamemkodolea seemu ambayeo Liam aliyekuwa tayari ameondoka mbele ya club.

Kisha akakunja midomo yake kwa kejeli, na kusema tena kwa sauti yenye mchanganyiko wa chuki na furaha “Lakini usijali... nitakupa muda kidogo ujifurahishe na jua la Afrika. Lakini nikirudi kwa mara nyingine… itakuwa ni siku ya mwisho ya jina lako kutajwa duniani.”

Palepale alitoa, kifaa ambacho mala tu baada ya kukitoa kilitoa mwanga wa mduara na mwanga ule ulianza kuzunguka miguu yake na kupanda adi kuanza kumzunguka mwili mzima, na sekunde iliyofuata, Alichukua hatua moja kwenda mbele kisha Akajirusha kutoka kwenye ukingo wa jengo.

Mwili wake ulishuka kwa kasi kama kivuli kinachoanguka kwenye mwanga. Lakini — baada yakufika chini hakuonekana tena haikueleweka apipotelea wap. Kama mtu yoyote angeshuhudia tukio hilo lingemshangaza sana na kumstaajabisha kwa wakati mmoja

****

Ilikua ni siku ya juma tatu jua la asubuhi lilijitahidi kuvuka mapazia mepesi ya rangi ya krimu yaliyokuwa yakining’inia kwenye dirisha la chumba cha Liam. Saa ya ukutani iligonga saa kumi na mbili asubuhi.

Liam Alikuwa ameshaamka tangu muda. Lakini hakuwa na haraka ya kweli. Badala yake, alisimama mbele ya kioo cha chumbani kwake, akiangalia uso wake mwenyewe kama mtu anayejitafuta kwenye fremu ya maisha mapya.

Alivuta pumzi ndefu kisha akaachia taratibu.

Alitazama koti jeusi la kawaida alilokuwa amelitundika kwenye mpini wa mlango.

“Ni kweli naenda kuwa mlinzi,” alijisemea kwa sauti ya chini, huku akiwa kama anajicheka yeye mwenyewe. “Hiyo ni kazi sasa?”

Alikumbuka siku ya jana aliweza kupokea simu tutoka kwenye kampuni ya ulinzi na ilimtaka kwesho ambayo ni siku ya juma 3 afike kwaajili ya kuanza kazi yake lasmi

Alitikisa kichwa polepole, macho yakiwa yamejaa hisia isiyoeleweka — mchanganyiko wa fedheha ya ndani na kejeli isiyo na mwelekeo.

Lakini hakudumu kwenye hilo wazo. Aliyapotezea.

Alijua hakuwa mtu wa kulalamika kuhusu nafasi. Hakuzaliwa na hadhi ya kuchagua kazi. Alikuwa hapa Tanzania na alihitaji Maisha mapya.

Na hiyo ndiyo ilibaki kuwa silaha yake pekee — kuendelea mbele, bila kuuliza maswali yasiyo na majibu.

Alivaa fulana ya ndani ya rangi ya kijivu, suruali nyeusi yenye mifuko mingi pembeni, na juu akajitwisha koti jeusi alilolitazama kwa sekunde tano kabla ya kulivaa. Kisha akachukua pochi yake, simu, na vitambulisho alivyotayarishiwa siku mbili zilizopita.

Macho yake yaliangalia saa kwa mara ya mwisho: 1:27 asubuhi. Alikuwa na dakika chache kabla ya dereva wa Bolt aliyemwita kumfikia.

Alifunga mlango kwa ufunguo, akateremka ngazi taratibu kutoka kwenye ghorofa ya pili ya nyumba yake aliyokuwa akiishi kule Masaki.

Barabara ilikuwa tulivu. Harufu ya chumvi kutoka bahari ya karibu na upepo wa asubuhi vilimkumbusha kwamba alikuwa bado yuko hapa — kwenye ardhi isiyoandikwa.

Mara gari aina ya Toyota Axio nyeupe likasimama taratibu mbele yake. Mwanaume mwenye tabasamu la kawaida aliteremsha kioo.

“Liam?” aliuliza kwa sauti ya kirafiki.

Liam alitikisa kichwa. “Ndiyo, ni mimi.”

Akaingia ndani ya gari, akavuta mlango taratibu.

Safari ya kuelekea makao makuu ya Loyal Shield Security ikaanza kwa ukimya.

Njiani, Liam aliangalia mandhari ya jiji kupitia kioo cha dirisha la nyuma. Picha za maisha, watu waliokuwa wakikimbizana na wakati, wapita njia waliovaa sare za kazi zao... vyote vilikuwa kama filamu ya maisha yasiyomhusu.

Alijaribu kupoteza mawazo yake kwenye vichwa vya watu waliokuwa wakitembea barabarani, usumbufu wa magari mengine, na spika za redio za madereva waliopishana nazo kila baada ya sekunde kumi.

Kulikua na ukimya ndani ya gali ila muda ule ule ukimya ulikatishwa na simu ya liam ilio anza kuita

“BRRRRRRR… BRRRRRRR…”

Aliitoa haraka kwenye mfuko wa koti. Namba haikua imehifadhiwa. Kioo cha simu kilionyesha tu: "No Caller ID."

Alibofya kitufe cha kupokelea na kuiweka sikioni.

“Sema,” alisema kwa sauti ya kawaida.

Lakini sauti iliyomjibu haikuwa ya kawaida hata kidogo.

> “Mr. Liam,” ilisema sauti ya kiume — nzito, ya kutetema kidogo, kama ya mtu aliyebeba uzito wa hofu iliyojificha kwenye kila silabi.

Liam alisita kwa sekunde moja.

> “Naitwa Director Warren Kaze — kutoka Loyal Shield Security.”

Moyo wa Liam ulipiga hatua mbili mbele.

Director? Liam alionekana kushangaa kwani akutalajia Angepigiwa na mkurugenzi wa kampuni mwenyewe wala si afisa rasilimali watu jambo hilo lilimshangaza

Aliinyanyua macho juu kidogo kama mtu anayetafuta majibu ya ghafla juu ya paa la gari.

Lakini kama kawaida yake, alitulia, akaufunga mshangao wake ndani ya kifua kama sanduku la siri.

“Ah, salama Director. Nashukuru kwa simu. Upo fresh?” alisema kwa sauti ya utulivu.

> “Salama. Nimefurahi umepokea haraka. Samahani kwa kukupigia bila taarifa.”

“Hamna shida kabisa. Ila... kuna tatizo?” aliuliza Liam, akiangalia saa ya simu. “Maana niko njiani kuja ofisini sasa hivi.”

Director Warren alikaa kimya kwa sekunde mbili kabla ya kujibu kwa sauti ile ile ya tahadhari.

> “Tafadhali aghalishe kwenda kwenye makao makuu. Hatutakutana huko. Badala yake... nitatuma anwani nyingine, ndipo utakabidhiwa rasmi sehemu yako ya kazi. Huko ndipo unapopaswa kuwa kuanzia sasa.”

Kauli hiyo ilimshtua Liam kidogo.

Alitabasamu tu kama mtu aliyesikia ndoto ya mtu mwingine usiku wa manane.

“ooh ok Sawa Nitafika. Alijibu kwa sauti ya mchanganyiko wa mshangao na ucheshi wa ndani. “

> “Tayari natuma anwani hiyo kwenye simu yako sasa hivi.” Sauti ya Director ilikatika baada ya hayo.

Simu ilikakatwa. Liam aliikunja paji lake la uso sekunde moja, kisha akayapotezea tena mawazo kama kawaida yake.

Sekunde tano tu baada ya kukata simu, ujumbe ukaingia.Liam alikunja midomo na kutikisa kichwa taratibu

Alimgeukia dereva aliyekuwa akiendesha kwa umakini

“Hey bro um badilisha uelekeo na ufuate Adress hii. Alisema liam uku akimuonesha dereva huyo address alio kua ametumiwa

Posta. Velora Company.”Dereva alinyanyua nyusi kwa mshangao mdogo mala baada ya kuona address hiyo

“Velora? Ah, kule naifahamu. Pale karibu na jengo la zamani la TRA, sio?”

Liam alitikisa kichwa kukubali utadhani alikua akipajua sehemu hiyo

Dereva hakuwa na maneno mengine. Aliangalia nyuma kisha akaongeza mwendo kuelekea Posta.

Ndani ya gari, Liam alibaki na kimya chake. Kichwa chake kikiwa kwenye mizunguko ya maswali:

Kwa nini kazi ya ulinzi inaenda kumpeleka Posta? Kwa nini Director mwenyewe amempigia? Na kwa nini kampuni aliyopaswa kuingia haimsubiri tena?

Lakini kama kawaida yake... hakuzama kwenye tafakuri. Aliamini kila kitu kitajieleza wakati wake ukifika.

Baada ya muda kidogo Gari ilisimama taratibu mbele ya jengo refu lililojivuta hewani kwa umbo la kisasa. Jengo lililokuwa na vioo vya glasi nyeusi zilizoreflect mandhari ya mji wa Dar es Salaam, kama macho ya chuma yanayotazama chini kwa ukimya.

Liam alishuka taratibu, mikono yake ikiwa mifukoni,Lakini kabla hata hajalifikia lango, macho yake yakakutana na sura mbili alizoziona kwenye siku ya usaili

Alikuwa ni mwanaume mrefu, mweupe kiasi, mwenye umbo jembamba lililojikunja ndani ya koti la bei ghali lenye mistari mifupi myeupe juu ya rangi ya navy blue. Suti yake ilionekana kutengenezwa kwa mikono — na harufu ya mafuta yake ya nywele yenye harufu ya oud ilifika mbali kidogo. Alikua ni Director Warren Kaze

Warren alikuwa amevaa miwani ya rangi nyeusi iliyoifanya sura yake kuonekana kama mtu asiye na roho ya kuaminika. Macho yake yalikuwa yakitazama kila upande, huku akijaribu kupandisha tabasamu bandia kwa Liam.

Kuna kitu kuhusu macho ya Warren kilionekana kama mtu anayejua jambo kubwa kuliko anavyoonyesha.

“Karibu sana Mr. Liam.”

Alisema kwa sauti ya kubanwa — sauti ambayo haikueleweka kama ilikuwa na furaha, huzuni, au hofu ya ndani.

Kando yake alisimama yule mwanamke mrembo wa umri wa makamo alie julikana kama Afisa Rasilimali Watu – Lorretta J. Munishi

Ambae pia alijumuika siku ile kumfanyia Liam interview. Lorretta alikuwa amevalia gauni refu la rangi ya burgundy lililokuwa limebanwa kiunoni kwa mkanda mwembamba wa ngozi halisi. Alikuwa na nywele zilizosukwa kwa ustadi

Mikononi mwake Alishikilia faili. Sura yake ilikuwa tulivu, lakini macho yake yalisaliti utulivu huo.

Alimtazama Liam kwa juu hadi chini, akatoa tabasamu dogo la maana nyingi.

“Karibu tena, Mr Liam.”

Liam alitikisa kichwa tu na kuwapungia. Hakusema neno zaidi, ila alihisi kama yupo mahali ambapo mambo makubwa yanachemka chini kwa chini.

Warren alimtazama Liam na kusema, “Tafadhali, tufuate ndani.”

Waliongozana wakapita lango la mbele la kioo kilichofunguliwa kwa utaratibu na mlinzi aliyevaa sare safi za bluu iliyokolea. Korido ilikuwa tulivu, yenye sakafu ya marumaru nyeupe iliyong’aa kana kwamba watu hawatembei humo. Kuta zilikuwa na vioo vikubwa na picha zisizoeleweka – za majengo, anga, na sanamu zisizojulikana.

Walifika kwenye mapokezi ya juu ambapo alipokuwepo msichana aliyekuwa amekaa nyuma ya meza kubwa ya mbao nyeusi iliyoandikwa:

> Executive Access – Reception

Warren Kaze, aliyekuwa ameambatana na Liam pamoja na Bi Lorretta, akamsogelea msichana huyo na kujieleza kwa sauti tulivu:

“Tuna miadi na Bosi. Tumemleta huyu kijana. Jina lake ni Liam.”

Msichana wa mapokezi alinyanyua simu yake ya mezani, akabonyeza kitufe cha mawasiliano aliongea dk1 alishusha simu hiyo

Baada ya dakika kadhaa akifika msichana mmoja Alikuwa msichana wa miaka isiyozidi ishirini na saba. Mrefu kiasi, mrembo wa sura ya Kiasia, mwenye ngozi laini ya kahawia ya dhahabu. Nywele zake zilikuwa zimerudi nyuma kwa mtindo wa sleek ponytail na alikuwa amevaa suti ya kijivu yenye mikunjo ya kisasa. Alikuwa na hereni ndogo za dhahabu na miwani nyembamba ya macho ya kisasa. Alikua ni Naila – Executive Assistant

Karibu sana Mr Warren Kaze. Naila aliwakalibisha na baada ya macho yake kutua kwa liam alionekana kushangaa na muonekano wake na kujisemea kimoyo moyo isije ikawa huyu ndie. Aliishia apo apo na na kuyapotezea mawazo yake

> “Samahani kwa usumbufu kidogo,Mr Warren,bosi yuko na wageni. Tafadhali nitawapeleka kwenye chumba cha kusubiria. Naitwa Naila, nitawaalika punde kila kitu kitakapotengemaa.”

Warren alitabasamu kwa nidhamu. Lorretta alitikisa kichwa kwa shukrani. Liam hakuwa na neno, zaidi ya kushangaa

Baada ya apo naila aliwachukua na kuingia kwenye lift na kupandisha juu baada ya dakika kadhaa walitoka nje ya lift, Wakaelekezwa upande wa kushoto, kwenye mlango mweupe ulioandikwa Waiting Room A

Ndani kulikuwa na viti vya ngozi maroon, meza ya glasi, sanamu ndogo ya askari aliyesimama na mikono nyuma, na picha ya kijana wa sura ya huzuni aliyekuwa amevaa koti la vita

Chumba kile kilikua kizuri sana

Liam hakuonekana kua na wasiwasi wa aina yoyote ile zaidi kuonekana mtulivu na mwenye kujiamini ila kichwani alibaki na swali moja tu kichwani “Kwani kazi yenyewe ni nini hasa? Ni nani huyo ambae ndio anaetakiwa kumlinda

Chumba kilitawaliwa na ukimya. Mr Warren Kaze, alionekana kukosa utulivu kabisa, Wasiwasi ndio ulimtawala.

Zilipita kama dakika 30 hivi hatimae Naila aliweza kuludi tena kwa mala nyingine

Mr Warren Kaze, samahani kwa usumbufu ulio jitokeza unaweza bosi amemaliza mazungumzo na wageni wake hivyo uko huru kuonana nae tafadhali ongozana na mimi

WILL CONTINUE

UNADHANI NI NINI KITATOKEA USIKOSE

Previoua Next