Reader Settings

Kulikucha asubuhi na mapema sana baada ya kunyanyuka kwenye kitanda chake aligeukia pembeni yake hakuweza kabisa kumuona mumewe kipenzi alishtuka sana mama kijacho wa jaji mkuu, aliamka haraka na kujisogeza kwenye chumba cha kujisomea ambako ndiko alijua mumewe mara nyingi sana mtu huyo alikuwa anapenda kuwa. Alimkuta kama alivyo muacha jana yake usiku hakupata hata tone la usingizi alikuwa amejiinamia mkononi ameishika kalamu yake ya wino akiwa anaiangalia kwa umakini sana mkewe alimsikitikia mno mumewe alikuwa anateseka sana.

“Umelala hata kidogo?” alimuuliza kwa upole japo alielewa kwamba mtu huyo tangu jana yake hakuweza kabisa kulala wala kuigiza kuupata usingizi.

“Najihisi kama nimelala mwaka mzima sina hata tone la kuigiza tu la usingizi mwili wangu umegoma kabisa kuleta hisia za kitu kinacho itwa usingizi tangu jana ulivyo niacha hapa”

“Unahisi utajitesa hivyo mpaka lini? Kwa sababu kuna muda kwa nafasi yako utakuwa ukikutana na kesi za ajabu za kutisha sana kama unajiona kwamba hauko sawa una nafasi ya kumteua jaji mwingine yeyote asimame kwa niaba yako leo mahakamani”

“Hakuna kesi ambayo itakuja kuwa mbaya na ya kutisha kuizidi kesi hii huyu aliye uawa ni mheshimiwa raisi wa nchi lakini ukiacha hilo aliyekufa ni rafiki yangu halafu unakuja kuniambia nimuachie mtu mwingine kesi hii unahisi kuna mtu gani ataweza kuzikataa pesa kwa majaji waliopo? Kuna muda uwe unawaza kama mtu mzima” aliongea kwa hasira sana akiwa anatokwa na machozi haikuwa kawaida kwake yeye kuongea kwa ukali sana namna hiyo mbele ya mkewe, mkewe alijua amemkosea mumewe alihitaji kumuomba msamaha lakini ni kama alichelewa mtu huyo alitoka humo ndani muda huo huo alienda kujifungia chumbani ambako baada ya dakika kumi tu alitoka akiwa amevaa zake suti na begi mkononi hakuweza hata kumuaga mkewe siku yake ilikuwa imeharibika asubuhi na mapema kabisa.

Alifika nje na kutoa maagizo kwa walinzi wake haikuwa taabu kwa sababu alikuwa mtu mkubwa hivyo hata ulinzi wake ulikuwa ni wa namna yake, aliondoka na gari yake pamoja na walinzi kadhaa na dereva wake kuelekea mahakamani. Akiwa njiani mawazo yalimpeleka mbali sana.

“Unajua kwanini sipendi siasa?”

“Haujawahi kabisa kunipa sababu”

“Siasa ina mambo ya kutisha sana ndani yake ndiyo maana naiogopa sana nilishawahi kusikia kesi kadhaa nikajikuta nawaogopa mno hawa wana siasa rafiki angu nakuona kabisa umenogewa sana huko jiangalie sana maisha yako ndugu yangu tunaishi mara moja tu”

“Mark shida yako wewe ni muoga sana unajua hii nchi inahitaji viongozi wenye maono makubwa ambao bado ni vijana na hao viongozi wenyewe ndio sisi, ebu acha kuogopa kiasi hicho rafikio angu kama kila mtu angekuwa muoga sana namna hiyo basi mpaka leo nchi hii isingekuwa imepata uhuru tungekuwa tupo bado chini ya watu”

“Huwa naipenda sana nukuu ya methali moja inasema KINGA NI BORA KULIKO TIBA ina maana kubwa sana ndani yake ukiielewa vizruri. Ni kweli nchi inahitaji viongozi wenye maono na vijana lakini hao wenzetu ambao unawaona wanafanya hivyo tayari wana watu, wana mifumo na wana njia mbalimbali za kukimbilia hasa pale yanapotokea matatizo, wanajua tunaingilia hapa na tunatokea hapa sasa wewe hapo likitokea tatizo utakimbilia wapi na anakulinda nani? kumbuka hapa nakushauri kama marafiki ambao tumetoka mbali sana pamoja mimi sihitaji kukupoteza kabisa kwenye maisha yangu” zilikuwa ni kumbukumbu za Markvelous Japhary akiwa ndani ya gari lake, alikumbuka siku moja akiwa anamshawishi rafiki yake ambaye alikuwa anaipenda na kuihusudu siasa kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yake lakini mwenzake huyo hakuweza kabisa kukubaliana na hilo jambo aliamua kuziishi ndoto zake ambazo kweli zilimpeleka mpaka Ikulu akasimama kama raisi wa nchi na ndiye ambaye aliweza kumteua Markvelous Japhary kuwa jaji mkuu kutokana na uwezo wake mkubwa lakini pia kama rafiki ambaye wametoka naye mbali sana.

Huyu ndiye aliyeweza kuyabadilisha maisha ya jaji mkuu wa Tanzania

“Kwa yeyote aliyehusika na hili hakika sitaweza kumuacha akiwa hai haitajalisha nitajiingiza kwenye matatizo gani ila lazima nihakikishe amekufa mbele kabisa ya mahakama kama malipo kwa walicho kifanya kwa rafiki yangu, najua watakuwa wameandaa watu wengi kwa ajili ya kumtetea mtu wao ili aachiwe huru ila mwamuzi wa mwisho ni mimi hapa lakini kuna maswali najiuliza huyo muuaji aliweza vipi kupatikana kirahisi sana namna ile? Mkuu wa majeshi hajanipa undani wa mambo ebu ngoja kwanza niweze kumalizana na hili kisha nikae nae vyema aweze kunisimulia kwa undani” alishtuka kutoka kwenye kuongea mwenyewe baada ya mlinzi wake kumfungulia mlango alijiweka saw ana kushuka tayari alikuwa kwenye eneo la mahakama.

“Afe huyo, afe huyo”

“Hakikisha unamuua hawezi kutuondolea kiongozi wetu”

“Afe afe ikiwezekana aletwe kwetu tuondoke naye afe huyo afe” zilikuwa ni kelele ambazo alizisikia kwa wananchi wenye hasira kali walichukizwa mno na raisi wao ambaye walimpenda sana kuuawa walihitaji mtuhumiwa aweze kuuawa. Hilo jambo lilimpa nguvu sana jaji baada ya kuona wananchi wote walikuwa wapo upande wake, akiwa anajiandaa kuanza kuelekea lilipo lango kuu la mahakama aliivua miwani yake baada ya kuona gari la magereza linaingia likiwa na ulinzi mkali mno dakika mbili zilipita alishushwa mwanaume mmoja mwenye upara na ndevu nyingi sana ambazo ni muda mrefu hazikuwahi kunyolewa, alikuwa kwenye minyororo mizito alivyo inua uso wake moja kwa moja alikuwa anaangaliana na jaji mkuu mwanaume huyo alimkonyeza jaji mkuu huku akitema mate chini, ni moja ya dharau kubwa sana ambayo aliifanya hapo. Markvelous aliitoa miwani yake na kumuangalia vizuri huyo mwanaume kwa hasira ambazo wazi wazi macho yalizungumza kwamba kama leo ukipona wewe shetani basi mimi naacha kazi ya kuwa jaji narudi kijijini kulima vitunguu na kuchambua dagaa.

Alianza kutoka pale na kuelekea kwenye ofisi yake humo mahakamani akavae nguo za kazi wakati huo maaskari wakiwa wanatangulia na mtuhumiwa kumpeleka kizimbani, akiwa anaingia kwenye lango kuu la mahakama alipokea meseji mbili kwenye simu yake ambazo zilipishana kwa dakika moja na nusu tu moja ilikuwa imetoka kwa CDF Jaiwelo Mkupi Makubilo na nyingine ilitoka kwenye namba ambayo bila shaka alikumbumbuka kwamba ilimtafuta jana yake usiku wa manane.

‘’USIFANYE MAAMUZI YA HASIRA MARK HILI NI JAMBO ZITO SANA LA NCHI NZIMA, HII NI KWA USALAMA WAKO NA FAMILIA YAKO LAKINI PIA KWA TAIFA ZIMA LINATEGEMEA MAAMUZI YAKO SAHIHI LEO” aliisoma meseji ya CDF ila hakujihangaisha hata kuijibu aliifungua hiyo ya pili.

“UNA DAKIKA CHACHE SANA ZA KUFANYA MAAMUZI YA BUSARA KWA AJILI YA KUIKOMBOA FAMILIA YAKO KISHA BAADA YA HAPO UTAINGIZIWA SHILINGI ZA KITANZANIA BILIONI KUMI KWENYE AKAUNTI YAKO YA BENKI UTAKAPO TOA TO MAAMUZI YA BUSARA NA YA KIUME ILA ZINGATIA SANA KAMA UKIENDA KINYUME KITABU CHAKO NA FAMILIA YAKO KINAENDA KUFUTWA KWENYE HUU ULIMWENGU” hii ni meseji ambayo ilimfanya atoe kitambaa kwenye mfuko wake na kujifuta jasho ambalo lilikuwa limeanza kumtoka kwenye uso wake alihisi joto kali mno, alihema kwa nguvu na kuizima simu hiyo hakuhitaji kujisumbua nayo tena.

Tukio la kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya mheshimiwa raisi lilikuwa linaonyeshwa moja kwa moja mubashara kabisa kwenye kituo kikubwa cha televisheni cha nchi kilicho julikana kama Tanzamax, kilikuwa ni kituo ambacho siku zote kilitoa habari za kuaminika na zenye uhakika zaidi na kilipendwa sana na wananchi hususani wale ambao huwa wanapenda sana kupata habari moto moto ambazo huwa zinajiri ndani ya nchi yao kutoka kwa watangazaji wao mahiri ambao walipendwa sana ndani ya nchi ya Tanzania.

“Tanzania oyeeeeeee”

“Nchi yetu oyeeeee”

“Idumu nchi yetu ya amani”

“ALale mahali pema peponi kipenzi chetu raisi wetu ambaye tutampenda siku zote za maisha yetu”

“Tanzania ya amani inawezekana”

“Uishi miaka mingi mheshimiwa jaji mkuu”

“Tanzania oyeee”

“Sisi ni watanzania”

“Tunaipenda Tanzania yetu” zilikuwa ni sauti kubwa za shangwe na vigelele vingi japo vilitoka kwenye vinywa vya watu kwa majonzi sana baada ya kusikia kauli ambayo iliwafariji sana na kuyafuta machozi yao kwa kumpoteza mpendwa wao ambaye ni wazi walimpenda sana

“WITH THE CLEAR EVIDENCE FOUND I SENTENCE YOU TO PUBLIC DEATH BEFORE THE COURT MR ABIR MUSHKANI (KWA USHAHIDI WA WAZI ULIO PATIKANA NAKUHUKUMU KIFO CHA HADHARANI MBELE YA MAHAKAMA MHESHIMIWA ABIR MUSHKANI)” Hii ndiyo kauli kutoka kwa jaji mkuu ambayo iliwapa matumaini wananchi ambao walikuwa nje ya mahakama na hata wale ambao walikuwa wanaona hilo tukio moja kwa moja kwenye runinga, hukumu hiyo ilifuata baada ya takribani masaa manne kupita wakiwa wanaiendesha kesi hiyo ambapo wanasheria wengi wakubwa na wabobevu walikuwa wakimtetea sana mtuhumiwa ila wote walikuja kunyong’onyea baada ya jaji mkuu mwenyewe kuonyesha ushahidi wa video moja kwa moja wa mtu huyo akiwa anafanya hilo tukio, ni jambo ambalo lilikuwa wazi hakukuwa na namna ya kulikataa tena.

Mtuhumiwa aliyejulikana kama Abir Mushkani alinyongwa hadharani mahakamani akiwa na minyororo yake mwilini kwa sababu alionekana kuwa mtu hatari sana kama angefunguliwa hapo, hilo tukio lilionyeshwa moja kwa moja ili kama kuna wengine wenye tabia kama zake waweze kukoma mara moja, ni tukio ambalo lilimpa heshima kubwa sana Markvelous Japhary ambaye aliona kama ametua mzigo mzito kwa kulipa kisasi kwa kifo cha rafiki yake japo kwa kutenda haki. Alitoka mahakamani na kuingia kwenye chumba chake aliichukua simu yake kwenye begi lake akaiwasha, alijaribu kumpigia mkewe kwa sababu asubuhi waligombana alihitaji kumuomba msamaha kwa kumkosea na kumtamkia maneno makali sana simu iliita kidogo na kukata akahisi huenda mkewe bado alimkasirikia, alijaribu kupiga kwa mara ya pili haikupatikana akajaribu tena na tena lakini haikupatikana kabisa.

Akiwa amekata tamaa alipokea ujumbe kwenye simu yake meseji zilikuwa mbili ilionekana zilitumwa muda kidogo sema kwa sababu aliizima simu ndiyo maana ziliingia kwa kuchelewa watumaji walikuwa ni wale wale.

“UMEFANYA MAKOSA MAKUBWA SANA MARK ILE VIDEO HAIKUTAKIWA KUONYESHWA HADHARANI NAMNA ILE UNAYAJUA MADHARA YAKE?” Ilitoka kwa CDF haikumshtua sana yapili ilitoka kwenye ile ile namba ambayo tangu jana ilimpa sana onyo.

“UNA DAKIKA KUMI NA TANO TU ZA KUWAHI NYUMBANI KWAKO KAMA UTAFIKA NDANI YA HUO MUDA UNAWEZA UKABAHATIKA KUIKUTA FAMILIA YAKO SALAMA ILA ZAIDI YA HAPO UTAUJUTIA SANA ULIMWENGU HUU NA NILIKWAMBIA MAPEMA” meseji iliishia hapo hakukumbuka hata kulivua vazi lake linalo mtambulisha kama jaji mkuu alitoka nje akiwa anakimbia sana.

Mchezo ndo kwanza unaanza chukua juisi safi na popcorn tuweze kusonga pamoja.

Bux the story teller.

Previoua Next