Reader Settings

Mheshimiwa jaji mkuu hakuwa na amani kabisa mpaka wakati huo hivyo alimsisitiza sana dereva wake kuweza kuongeza sana mwendo wa gari, alikuwa na imani kwamba familia yake haikuwa kwenye eneo salama sana hivyo ni yeye pekee ndiye ambaye alikuwa anatakiwa Kwenda kuikomboa familia hiyo huku machozi yakiwa yanauzonga zonga uso wake mpaka makamasi kwenye pua yake ilikuwa sehemu ya kumfanya kuwa na wasi wasi zaidi.

“Nisamehe sana mke wangu nisamehe sana mama” alikuwa anaongea mwenyewe akiwa ndani ya gari hiyo, alikuwa akimhusudu sana mwanamke huyo kwenye maisha yake na alizoea kumuita mama ni kwa sababu mwanamke huyo aliichukua nafasi ya mama yake mzazi, alimdekeza mwanaume huyo, alimpa mapenzi mazito ambayo alikuwa ana imani kabisa kwamba kwa kizazi hiki kulikuwa na watu wachache sana ambao walikuwa wana uwezo wa kuyapata mapenzi ya kweli kama hayo. Huyo mwanamke kwake alikuwa zaidi ya mke alifikia kiwango cha kumfanya kuwa kama mama yake alimjali yeye pamoja na mdogo wake Jason ambaye mpaka kwa wakati huo hakuwepo ndani ya nchi ya Tanzania na ukizingatia asubuhi yake walikuwa wamekwaruzana na mkewe hivyo alitamani sana awahi akamuokoe kwenye hilo janga ambalo aliambiwa lazima litamkuta mkewe pamoja na Kwenda kumuomba msamaha.

DREAM LOVERS LOUNGE

Mwanaume kumbu kumbu zake zilirudi ndani ya hilo eneo, siku ile baada ya kufanikiwa kuisikia moja ya sauti ambayo alimsifia sana MUNGU kuiumba duniani na yeye akapata bahati ya kuweza kuisikia ilikuwa ni siku ya furaha sana kwenye maisha yake, alikuwa mwenye furaha sana siku ile hata aliporudi nyumbani kwenye sehemu ambayo alikuwa akiishi na mdogo wake, bwana mdogo alimshangaa sana kaka yake kwani siku zote huwa ni mtu ambaye anakuwa na mawazo sana lakini siku hiyo alikuwa mwenye furaha kupita kiasi alifanya kazi zake zote akiwa anacheka cheka mwenyewe ilimlazimu mdogo wake amuulize siri ya mafanikio hayo lakini hakujibiwa zaidi ya kuishia kuchekeana tu.

Alitamani sana kesho yake ifike haraka ili awahi lile eneo majira ya jioni aweze kubahatika kuiona sura ya mwanamke huyo ambaye aliishia kuisikia sauti yake tu, muda huwa ni daktari mzuri sana siku hiyo alikuwa amewahi kwenye mizunguko yake ambayo aliimaliza mapema sana na Kwenda kukaa eneo la nje kabisa na ile lounge sehemu ambapo kulikuwa na tax nyingi alijipenyeza hapo mapema sana akiwa anasubiria mwanamke huyo aweze kupanda jukwaani kama alivyokuwa amesikia tangu jana yake kwamba princess Prisca angekuwa hapo kwa muda wa wiki nzima akiwa anatoa burudani kwa wateja wa eneo hilo hali iliyo pelekea eneo hilo kufurika sana. Majira ya saa nne za usiku ndio muda ambao malkia huyo alikuwa anapanda jukwaani, hali hiyo ilimfanya kijana huyo ambaye kwa wakati huo damu yake ilikuwa ikimchemka sana kuongeza umakini ili aweze kumuona mwanamke huyo, bahati mbaya sana kwake ambayo ilimpelekea kusonya kwa nguvu eneo la jukwaa kulikuwa na taa za pink na blue zilizo mfanya ashindwe kuing’amua sura nzuri ambayo aliitarajia yeye kwenye nafsi yake. Zilipita dakika kama tano bendi ikiwa inasikika kwa mbali ndipo ile sauti ya kumtoa nyoka pangoni, sauti safi ambayo ilipangiliwa kama zile nyaya za gitaa ambavyo huwa zinatengenezwa kwa ufasaha ili pale mtaalamu wa gitaa anapo lishika liweze kuziteka hisia za wasikilizaji ilisikika kwenye maiki ya mkononi ambayo ilishikwa na mwanamke huyo, ukumbu mzima ulitulia kila mtu alitamani sana kuweza kuisikia sauti hiyo kwa usahihi zaidi hata na wale ambao walikuwa wanakula walisimamisha zoezi lao kwa muda kwanza malkia aifanye kazi yake.

Hicho ndicho kilichompa umakini mkubwa kijana Mark kuweza kuisikiliza sauti hiyo akiwa amekodoa macho pima kwenye jukwaa ambalo alikuwa amesimama mlimbwende huyo, ghafla sana uliwaka mwanga mweupe na hapo ndipo ambapo aliona sura ambayo ilimfanya mdomo ubakie wazi, alijikagua kwanza yeye juu mpaka chini alitingisha kichwa chake kujikataa yeye mwenyewe.

  When your day is long

 And the night, the night is yours alone

 When you’re sure you’ve had enough

 Of this life, well hang on

 Don’t let yourself go

 ‘Cause everybody cries

 Everybody hurts sometimes

 Sometimes everything is wrong

 Now it’s time to sing alone

 When your day is night alone (hold on, hold on)

 If you feel like letting, go (hold on)

  If you think you’ve had too much

 Of this life, well hang on

 ‘Cause everybody hurts

 Take comfort in your friends

 Everybody hurts

Kwa yeye suala la kujisikitikia lilikuwa ni kujipimanisha au kujilinganisha kama anaweza kuendana kwa namna yoyote na yule mwanamke lakini jibu lilikuwa ni Hapana, ile shingo ndefu kiasi ambayo ilikuwa ni laini sana kwa sababu ya mafuta safi na maisha safi ambayo yaliizunguka, ule mwonekano wa kutamanisha wa Rihanna kwenye umbo la kifuani, sura ya malkia wa mziki duniani Beyonce, bila kusahau ule mgawanyiko wa kile kiuno na umbo la nyuma mithili ya Kim Kardashian yule wa Kanye West na ile miguu iliyo elekeana na Zarina Hassan mama yake na Princess Tiffa bila kusahau gauni la pink lililo ishia magotini na vile viatu mchuchumio vya bei ndefu ndicho kilicho mfanya ajikatae kabisa kwamba kwa yeye hakuwa mwanaume wa kukatiza mbele ya mwanamke huyo na akaweza kumuelewa kwa chochote kile. Tafsiri halisi ya mapenzi imeuliwa na neno pesa na yeye hakuwa kijana ambaye maisha yake yalikuwa safi ndio kwanza kula kwenyewe ilikuwa milo miwili wala sio mitatu kama wengi waishivyo angeanzia wapi kuyavaa kwa mwanamke mwenye ngozi nyororo na uzuri wa kumfanya ndege wa mwituni kumsifu kwa sauti nzuri kila apitapo kama huyo? Maisha yake yalikuwa ni ya maumivu makali sana asingeweza kufanya kitu chochote kile mbele ya mwanamke huyo au ambacho kingemsaidia yeye kuweza kumpata huyo mwanamke.

Akiwa kwenye hayo mawazo mazito ya kujikatia tamaa ya maisha yake ndipo ilipo sikika sauti nzuuri sana tena zaidi ya sana na hiyo ndiyo ambayo ilimfanya yeye kuja hapo majira ya usiku huo, nyimbo moja safi sana ambayo ilitoka mnamo mwaka wa 1992 kutoka kwa R.E.M.’S ijulikanao kama EVERYBODY HURTS ni wimbo ambao uliyarudisha matumaini makubwa sana kwenye moyo wake na kuna mstari ambao aliupenda sana kwenye wimbo huo ambao unasema 

Usijiache wewe mwenyewe uende

Kwa sababu kila mtu hulia

Kila mtu huumia muda mwingine 

Kuna muda kila kitu hakiwi sawa

Sasa ni muda wa kuimba mwenyewe

Kutoka kukata tamaa mwili wake ulipata sana nguvu kwa sababu yeye alijihisi kwamba ndiye mtu mwenye matatizo sana kwenye maisha yake ila aligundua kwamba kila mtu kuna muda huwa anapitia wakati mgumu sana kwenye maisha ila kikubwa ni kuendelea kuwa mstahimilivu pale unapo kutana na nyakati ngumu sana kwenye maisha yako, alivutiwa sana na kila kitu kutoka kwa huyo mwanamke alitabasamu na kuanza kucheka mwenyewe alicheka sana huku akiwa anaufuatisha wimbo huo ambao hata hakujua anaimba nini, moyo wake ni kama ulikuwa umepata ahueni kubwa sana tangu aweze kuujua na kuutambua uwepo wa mwanamke huyo kwenye maisha yake, kuna madereva tax ambao walikuwa wapo pembeni wakiwa wanasubiria wateja ambao wangetoka humo ndani walibaki wanamshangaa kijana huyo na kuhisi huenda hakuwa na akili timamu huenda alikuwa na matatizo ya akili.

Muda ulivyo zidi kwenye ndivyo watu wengi walikuwa wakinogewa na mwanamke huyo ambapo huo wimbo ulirudiwa kwa mara tano huku watu wakiwa wanatikisa vichwa na wengine wakiwa wanatoa vitambaa vyao na kuyafuta machozi ambayo yalikuwa yanashuka kwenye mashavu yao, ni wimbo ambao ulikuwa unahuzunisha mno tena sana ndiyo sababu watu walikuwa wakilia kimya kimya huku wakiwa wanaufuatisha wimbo huo ambao ulitendewa haki bara bara na mrembo ambaye alikuwa ameishika maiki yake yeye mwenyewe machozi yakiendelea kumshuka taratibu huku akiuimba wimbo huo kwa hisia kali sana.

Kijana Mark alijikuta anashawishika taratibu na kuanza kusogea eneo ambalo alikuwepo mwanamke huyo aliyekuwa akiuimba wimbo huo maeneo hayo, aliingia mpaka mlangoni ambapo hapakuwa na mlango bali ni mbao tu za kisasa ambazo zilizungushiwa kote na kumfanya hata mtu wa nje kuona vizuri ndani, kutokana na watu hao kutekwa na utamu wa mziki hata walinzi hawakuwa na muda na mlango tena macho yao yalikuwa jukwaani na hiyo ndiyo nafasi ambayo Mark aliitumia kuingia humo ndani, alivyokuwa akisogea ndivyo alivyokuwa akizidi kunogewa na sauti ya mwanamke huyo na kujikuta anashawishika kutamani kumgusa hata ngozi yake mrembo Prisca, wakati anakaribia kupanda kwenye hilo jukwaa kuna mlinzi mmoja alimrukia baada ya kumuona anaelekea sehemu ya jukwaa bila ruhusa alimbeba kwa nguvu na kumbamiza kwenye meza iliyokuwa pembeni kwa kasi akihisi huenda alihitaji kumvamia mwanamke huyo, kichwa chake kilianza kutoa damu alipiga sana kelele kwa maumivu makali ambayo aliyapata usiku ule.

“Bosi bosi bosi”

“Eeeh mama uko salama?” alishtuka kwenye hayo mawazo mazito baada ya kuitwa, alihisi ni mkewe anamuita ndipo aliposhtuka kwamba alikuwa ni dereva wake, aliogopa sana mwili wake ukiwa na jasho sana hata suti ilikuwa imeloa japokuwa ndani ya gari hiyo kulikuwa na kiyoyozi cha kutosha.

“Bosi tumefika nyumbani ila nimesimamisha mbali kidogo maana nimeona kama kuna mwili wa mtu getini pale umelala na geti lipo wazi” dereva wake alimpa maelekezo bosi wake huku akiwa ana msikitikia sana, alijua wazi mheshimiwa alikuwa anapitia kipindi kigumu sana.

“A a a a saaante sana nitakupigia simu nikikuhitaji hiyo gari nenda nayo” Aliongea kwa kitete midomo yake ikiwa mizito sana inatetemeka huku akiwa anashuka ndani ya gari hiyo, hakusubiri hata jibu la mtu huyo tena alikuwa tayari ameshafika mlangoni, aliogopa sana baada ya kuona miili ya watu watatu ipo chini ikiwa inamwaga damu. Damu ilionekana kuwa bado mbichi sana na wote walipigwa risasi za kichwa alikimbia mpaka kwenye mlango wa nyumba kubwa hapo alisita kidogo baada ya kukuta walinzi wake wengine wote watano wamepigwa risasi za kichwa, mwili ulimsaliti kabisa alianza kuogopa kuingia kwenye nyumba yake yeye mwenyewe hakutamani kile ambacho alikifikira akutane nacho humo ndani.

Alianza kusogea taratibu kwa uoga ni michirizi ya damu tu ndiyo ambayo ilikuwa inaonekana mpaka kwenye kochi hapo alicho kiona alipiga magoti machozi yakiwa yanashuka yenyewe hakuelewa alie kwa sauti au aendelee kuangalia alichokuwa anakiona mbele, binti yake wa pekee ambaye aliikamilisha furaha ya maisha yake kwa kuwa baba kwa mara ya kwanza hapa duniani, walimwengu walikuwa wameondoka na nafsi yake hakuwa hai wala kuwa na matumaini ya kuwa hai tena kwenye ulimwengu wa wanadamu hawa wanao jivunia pumzi kama walijipa wao.

Sijui ilikuwaje na nini kinaenda kufanyika ila niseme tu kufikia hapa sehemu ya 4 sina la ziada tena na sijui kinaenda kutokea nini………..bye-bye.

Wasalaam

Bux the storyteller.

Previoua Next