Reader Settings

Ni kipindi cha mwezi wa nane kuelekea wa tisa, kipindi ambacho wanafunzi wengi wanafanya maombi mbalimbali ya kujiunga na vyuo vikuu, na wengine wale waliokosa alama za ufaulu wakijaribu kufanya maombi kwenye vyuo vya kati katika ngazi ya diploma kwenye vyuo vya ufundi, afya, na kilimo.

Moja ya wanafunzi hao ni kijana Rafaeli kutoka Tanga, wilaya ya Lushoto. Akiwa ni mmoja wa vijana waliokuwa wakifanya maombi kwenye vyuo vingi vya afya, licha ya kwamba Rafaeli alikuwa amepata ufaulu mzuri wa kidato cha sita kwa alama ambazo zingemwezesha kuomba course chuo kikuu, yeye anaamua moja kwa moja kujiunga na chuo cha afya katika ngazi ya utabibu, kwani alitaka kutimiza ndoto zake za kuwa daktari mkubwa hapa nchini.

Rafaeli alifanikiwa kupata ufaulu wa daraja la pili pointi kumi na mbili, pointi ambazo kwa mwaka huo hazikumwezesha kujiunga na chuo kikuu kama alivokuwa anatamani katika ngazi ya udaktari. Ndipo alipamua kuomba udahili kwenye vyuo vya ngazi ya diploma.

Chuo alichofanikiwa kupata nafasi kwenye udahili huo ni katika Chuo cha Bombo Tanga mjini, kwenye hospitali ya rufaa, ambapo alikuwa amebakiza mambo machache ili kujiunga na chuo hicho, ambapo masomo yanaanza mwezi wa kumi.

Ni tarehe 11 mwezi wa kumi na moja, Rafaeli ndiyo siku aliyoripoti chuoni hapo. Alifika moja kwa moja katika ofisi ya utawala na kupokelewa na kukamilisha taratibu zote za usaili, hatimaye kupelekwa katika hosteli ya Mwongozo. Wale waliokabidhiwa kumpokea ni Elisha, ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa first year kwa upande wa darasani.

Rafaeli ni kijana mwenye umri wa miaka 20, anayetokea katika familia ya Mzee Mswaki huko wilayani Lushoto. Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya International School Braeburn huko Arusha, kisha akahamia katika shule ya St. Eugene’s iliyopo wilayani Lushoto. Licha ya familia ya Mzee Mswaki kuwa na uwezo wa kati kiuchumi, alimpenda sana Rafaeli kati ya watoto wake wanne, ndiyo maana alijitahidi kuhakikisha mtoto wake anasoma katika shule nzuri hapa nchini.

Mwezi wa kumi na mbili mwaka 2005, Mzee Mswaki alifariki kwa ugonjwa wa kisukari, ndipo mama yake alipomhamishia katika shule ya St. Eugene’s, sehemu alikomalia elimu yake ya msingi. Baadaye alijiunga na kidato cha kwanza Shambalai Secondary, na kisha akajiunga na kidato cha sita katika shule ya Makongo Secondary iliyopo katika jiji la Dar es Salaam.

Licha ya yote hayo, Rafaeli alikuwa anapendwa sana na watu kwa mwonekano wake wa upole na sura yake nzuri inayomvutia kila mtu tokea akiwa mtoto, kitu kilichompelekea kupendwa na watu wengi.

“Karibu, man. Hapa ndo umefika mzee, karibu! Halafu daaah mzee, unajua wewe ni bonge la handsome, utatuchukulia watoto haha…”

Huyu ni Elisha alivyoanza kumkaribisha Rafaeli.

“Hamna mzee, mimi wala hayo mambo sina mpango nayo kabisa. Yaani hapa kitabu tu na kulala.”

“Daa kweli mzee, hii kozi sio poa. Mzee, ukileta michezo unafeli. Yaani nasikia mwaka wa tatu walianza mia na wamemaliza mwaka huu watu nane tu.”

“Duuh! Mzee noma. Ila mimi naamini kama tutakomaa tutapasua, au wewe unaonaje?”

“Kweli, ukikomaa unatusua… Chumba chako kitakuwa hiki namba tano. Hapa anaishi jamaa mmoja wa mwaka wa tatu na jamaa wa mwaka wa pili. Jumla mtakuwa watatu, so chumba kishakuwa full. Nadhani mtafahamiana na wenzako.”

“Poa, man. Ahsante.”

“Niambie kijana, mimi naitwa Rafaeli Mswaki. Ndo nimepangwa room hii, mimi ni first year.”

“Anhaa, poa. Mimi ninaitwa Abasi, nalala hapa juu. Na kuna mshikaji katoka, yeye analala hapo chini, anaitwa Mkwizu. Ila karibu sana.”

“Asante sana. Vipi chuo hapa?”

“Hapa kama kawa, kama unavyoona hapa msuli tu. Maana mambo sio michezo. Ukizingua, kozi inakuzingua.”

“Enhe, nasikia hii kozi si michezo?”

“Ndo hivo. Ila ukikaza, mbona unafaulu tu kama wengine.”

“Poa mzee. Sema nimechelewa kuripoti hapa, naamini nina mzigo wa kusoma mpaka niwafikie wenzangu. Ngoja nianze kukomaa mpaka niwafikie.”

“Poa, wewe kaza. Wala usiwaze. Mambo marahisi tu. Kama ukiyachukulia magumu yanakuwa magumu, ila ukiyachukulia mepesi yatakuwa simple tu.”

“Fresbi kaka, umenipa nguvu. Yaani mimi hapa ni wendo wa msuli tu, sitaki mbwembwe.”

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa kijana Rafaeli siku ya kwanza kufika chuoni.

Ni asubuhi ya siku nyingine ya Alhamisi. Wanafunzi wote walikuwa wameenda darasani, isipokuwa kwa Rafaeli. Yeye aliamua kwenda vipindi vya mchana maana hakuwa ameweka sawa uniform zake.

Ilipofika vipindi vya mchana, alikuwa amekamilisha uniform, sema alikuwa amechelewa dakika chache kuingia darasani kwani wenzake wengi walikuwa washaingia. Sasa, wakati anatoka, aliulizia darasa la wanafunzi wa first year, akaoneshwa na moja kwa moja akaelekea kwenye darasa hilo na kuingia, kisha kwenda kukaa nyuma kabisa.

Siku hiyo ilikuwa kipindi cha Communication, na ilikuwa siku ya kurepresent kazi waliopewa. Mara hajakaa sana akaingia mwalimu wa somo hilo.

“Enhe, wale wanaotakiwa kurepresent wasogee wakaanze.”

Wanafunzi walianza kurepresent huku kichwa kikiwa Challenges that face communicating with deaf people (yaani changamoto tunazokumbana nazo tukiwasiliana na watoto wenye ulemavu wa kusikia — yaani viziwi).

Mwalimu alikaribisha maswali na mmoja wa wanafunzi waliotaka kuuliza alikuwa Rafaeli.

“Madam, I have a question about the topic according to what has been presented.”

(Madam, nina swali kutokana na jinsi walivyowakilisha na kuinyumbulisha topic hii.)

Wanafunzi wote wakamgeukia Rafaeli wakitaka kumsikia…

Next