As you hosted about the challenges… no one of you concluded what are the ways to be taken to combat these challenges. Generally, we always get used to seeing these people living in our community, and even in rehabilitation centres they live well and communicate.
So far, my curiosity is to know how this can be facilitated.
(Kama ulivyowakilisha kuhusu hizo changamoto, lakini sijasikia sehemu yoyote mliozungumzia kuhusu jinsi gani mnaweza kuziondoa au kuzifanyia kazi hizi changamoto. Kama tunavyojua, mahususi kwenye vituo vya watu wasiosikia, nilichokuwa nataka ni hatua gani zinazoweza kuchukuliwa kutatua hizo changamoto.)
Wanafunzi wengi walimshangaa kwa sababu kwanza alikuwa mwanafunzi mpya na ni mara yake ya kwanza kuingia darasani, lakini aliweza kuuliza swali tena kwa kujiamini na kutumia Kiingereza kilichonyooka.
"Vipi, umemuona yule mkaka mgeni aliyeingia leo darasani kwa kuchelewa?" aliuliza msichana mmoja anayeitwa Anjel akimuuliza rafiki yake Lucy.
"Anhaa, unamzungumzia yule aliyeuliza swali?"
"Eee, huyo. Ila mzuri, ni handsome halafu ana sura ya kipole."
"Ebu nitokee uko… ushamtamani tayari maana wewe!"
"Yaishe bhana! Mimi wala sijamtamani, sema nimependa tu mwonekano wake."
"Haya bhana, tutakuona mwaka huu. Tuwahi tukanunue chipsi kwa yule mkaka maana tukichelewa watajaa watu, si unajua wanavyompenda maana anaweka nyingi."
Hawa ni Lucy na Anjel, ambao ni marafiki tokea walipofika chuoni, hawaachani. Kwa upande wa Anjel, alikuwa mwembamba, mrefu hivi na mweupe. Lucy naye alikuwa mwembamba, mwenye shape nzuri, maji ya kunde.
Tofauti kati ya Lucy na Anjel ni kwamba Anjel alikuwa anapenda sana kushobokea wanaume wenye hela, na Lucy yeye alikuwa mcheshi. Yeye kuna kijana alikuwa ametokea kumpenda sana, kwa hiyo mara nyingi alikuwa akimtumia Anjel kuzifikisha taarifa zake.
Tukirudi upande wa Rafaeli, yeye baada ya kurudi hosteli moja kwa moja alimfuata mmoja wa wanafunzi wenzake na kumwomba amrushie notes kwenye simu yake pamoja na kumwonyesha malecturer walipoishia kufundisha katika masomo yote. Alioneshwa na baada ya muda akarudi chumbani na kujilaza kitandani.
"Lazima kesho nikae mbele ili nipate kuelewa vizuri maana naona kama macho yananisumbua," Rafaeli aliwaza.
"Ngoja kwanza niende stationary nikanunue rim paper nimpelekee yule madam kabla sijala pesa yote akanidai."
******
Jasmine ni moja ya wasichana waliodahiliwa kwenye chuo cha Bombo akichukua kozi ya Clinical Medicine (utabibu). Yeye alitokea mkoa wa Dodoma, Kondoa Irangi, huko ambako ndiko asili yake. Lakini baba yake alimpeleka katika shule za mjini huko Dar es Salaam akiamini huko ndiyo kwenye elimu bora.
Licha ya hivyo, pia aliamini mkoa huo ni mzuri kwa sababu ya kaka yake ambaye makazi yake yapo mkoani humo, atamsaidia pindi apatwapo na tatizo.
Jasmine tokea aingie katika chuo cha Bombo alisifika sana kwa uzuri. Wengi walifahamu Warangi wa Kondoa ni moja ya makabila yanayoaminika kwa uzuri hapa chini. Jasmine alikuwa mrefu, saizi ya kati, mweupe, mwenye sura nzuri ya kitoto, na akicheka anaonekana vishimo kwenye mashavu yake, kitu kinachoupamba uzuri wake.
Licha ya hivyo, alikuwa msichana aliyejaliwa shepu nzuri kuliko msichana yoyote darasani, kitu kilichomfanya kuwa gumzo chuoni kwa wanachuo wengi wa kiume.
Lakini licha ya kuwa mzuri na wengi kumtamani, hakuna aliyewahi kumsogelea na kumtongoza. Hii ni kutokana na alivyoonekana serious na masomo, pia alipenda dini yake ya Kiislamu hasa uvaaji wake na kutopenda kuonekana vibaya.
*****
Ni asubuhi mida ya saa moja. Rafaeli akiwa usingizini mara akasikia watu wakipita-pita. Mara akakurupuka kutoka kitandani.
"Daah! Kumbe kumekucha, ngoja nikaoge niwahi viti vya mbele."
Akachukua ndoo chapchap akaenda kukinga maji, akaoga na kuvaa uniform kisha akaingia darasani akakaa zake viti vya mbele kabisa.
Hajakaa sana mara akaingia dada mmoja aliyevaa shungi na miwani, akampa hi na kukaa naye pale pale mbele huku kila mmoja akijisomea zake wakimsubiri lecturer.
Mara akasikia:
"Aisha, mambo?"
"Poa," akajibu yule mdada aliyekaa pale mbele.
"Anhaa! Kumbe huyu mdada anaitwa Aisha," akajiwazia mwenyewe huku wakiendelea kupiga story na yule jamaa aliyekaa naye.
Asubuhi hiyo hakuna walichofundishwa mpaka baada ya kutoka lunch, ndipo mwalimu akaingia akafundisha Anatomy kwa kudemonstrate mifupa. Baada ya hapo mwalimu akatoka.
Mida ya saa tisa wanafunzi wakaanza kutawanyika. Mara akasikia:
"Kaka, samahani."
Rafa akageuka, akakutana na yule Aisha aliyekuwa amekaa naye pale mbele.
"Bila samahani, kuna dada aliyekaa pale nyuma. Alikosa kuingia mapema, pale mbele ulipokaa leo ni sehemu yake. Kanituma nikuambie maana ana shida ya macho."
"Anhaa, sawa. Nilikaa pale nikijua vile viti ni kuwahi kama nilivyoona vyuo vingine, ila haina shida. Mwambie Jumatatu atakaa sehemu yake."
"Okey, poa."
Moja kwa moja akaelekea hosteli kupumzika kidogo.
"Oya vipi mzee? Mbona umelala mapema? Sisi tunaelekea uwanjani kwenye mazoezi bhana, amka twende. We si umetoka shule ya vipaji Makongo? Twende ukatupe nguvu, wiki ligi inaanza na tumewekewa mbuzi na milioni moja na chuo. Kama tutakuwa washindi, fainali itakuwa siku ya Welcome First Year Night Party."
Huyu alikuwa ni Elisha, akimwamsha Rafaeli.
"Daah, ila mzee sina viatu vya mpira. Labda uniazime kama unavyo vingine."
"Poa, ngoja nikamcheki Lewis ana pea nyingine. We jiandae twende bhana."
"Poa, we kamcheki mshikaji halafu utaniambia."
"Poa."
Alijiandaa haraka haraka, na alipomaliza akitoka akamtafuta Elisha.
"Ngoja nikapashe mwili joto maana nimemiss sana mpira, nahisi hata kiwango kimeshuka."
"Oya, tayari ee?"
"Ndiyo, twende zetu."
Walifika uwanjani na kuanza mazoezi, wakijigawa timu mbili.
Usichojua ni kwamba Rafaeli alikuwa yupo vizuri sana kwenye mpira. Hata alivyokuwa Makongo, alikuwa akionyesha uwezo mkubwa kwenye soka.
"Daah mzee, kumbe upo vizuri!"
"Ndiyo mzee. Ila Elisha, mimi napendelea namba tisa. Naiweza sana kuliko nilivyocheza leo."
"Poa basi, tutakuweka tisa halafu Baraka tutamuweka kumi."
"Fresh."
Baada ya mazoezi, Rafa akachukua ndoo akaenda kwa mchungaji kuchota maji. Alipofika, akamkuta mdada wa chuo naye anakinga maji.
"Mambo," Rafa akamsalimia.
"Poa."
Yule dada akainua ndoo zake na kuondoka. Rafa akachota maji haraka.
Njiani akarudi, mara akamkuta yule dada kasimama na ndoo zake.
"Vipi? Unaelekea chuo? Nikusaidie ndoo moja?"
"Nitashukuru kaka angu, yaani nimeshindwa kubeba kabisa."
Rafa akabeba zile ndoo hadi alivyofika mlango wa hosteli yao akampa yule dada.
"Ahsante sana kaka yangu kwa msaada wako."
"Poa, usiwaze. Sasa hapa ni mwendo wa kuoga, niende kantini nikale, niingie class nipige msuli."
Emmy:
"Umechotea wapi hayo maji na mimi nikachote?"
"Nilichotea kule chini kwa mchungaji, ila kuyapandisha mpaka huku ndo ikawa shida. Yaani kuna mkaka yule mgeni ndo kanisaidia."
"Wacha wee… yule handsome boy wa darasa ee?"
"Eee."
"Yule mkaka mzuri halafu mpole hadi raha. Na ana sauti nzuri. Juzi alivyokuwa anajibu swali, yaani we acha tu… lazima nimshobokee yani."
"Wee Lizzy, na Joel utamwacha?"
"Joel bhana naye ana mambo ya kitoto. Mapenzi hata hayajui. Mwenzi nina ukame namuonesha kwa vitendo ila hata haelewi."
"Mhmh, haya bhana… mtajuana wenyewe."
Lewis:
"Oya mzee, unajua kupendeza sio?"
"Hamna bhana, hii kawaida yangu. Yaani kwenye vitu ninavyopenda ni mavazi na kuwa smart muda wote, ndiyo maana na shine haha!"
"Ni vizuri mzee. Sema, una demu kweli?"
"Mimi sina na sina hata mpango wa kuwa naye saivi. Nawazia kitabu tu mzee."
"Acha ushamba mzee. Mimi mzee wa kupiga na kuchapa raba. Unakajua kale ka Anjel kule class, ana rafiki yake anaitwa Lucy?"
"Yule flat hivi?"
"Eee, yule. Nishapita naye. Saivi namuwinda rafiki yake."
"Duuh, we jamaa sio poa. Kazi kwako. Mimi ngoja niingie class maana mmeniacha pakubwa."
"Poa."
Siku ya Jumatatu wanafunzi walijiandaa kuwahi darasani. Mmoja wao alikuwa Rafaeli.
Rafa aliingia class, akakaa nyuma akisubiri wenzake wajae huku akiendelea kujisomea. Dakika hazikupita nyingi akaingia mwalimu na kuanza kufundisha.
Ila Rafa alikuwa haoni vizuri ubaoni. Akaangaza-angaza mara akaona nafasi ipo wazi mbele. Ikabidi asogee.
"Vipi, sista, hapa kuna mtu?"
"Hakuna."
"Basi kwanzia leo nitakaa hapa ee?"
"Poa, karibu."
Mwalimu akaendelea kufundisha kitu kilichoanza kuwachekesha. Rafa akacheka, mara akamgeukia yule dada wa pembeni yake… macho yakamtoka huku akiacha kucheka.
Comments