Licha ya Jasmine kukataa wanaume wengi na kutotaka kujihusisha na mapenzi chuoni, lakini alikuwa ametokea kumpenda Rafaeli tokea siku ya kwanza anamuona akiwasili chuoni hapo.
Siku ambayo Rafaeli alifika chuoni ni siku ambayo Jasmine alikuwa ofisini kwa wadeni kujiandikisha na huduma ya afya ya bima. Licha ya kwamba siku hiyo Rafaeli hakumwona, lakini Jasmine alimuona na kumsikia wakati akiongea na wadeni, na hakupenda kumshirikisha yoyote yule. Zaidi ya kukaa kimya, hata marafiki zake walivyokuwa wanamjadili, yeye alijua tu ni yule aliyekutana naye ofisini — japo hakutaka kuliweka sana akilini na kulipa kipaumbele, lakini alitamani sana kumwona.
Siku ambayo Rafaeli anaingia darasani, alijikuta akitaka kuwa karibu na Rafaeli, japo awe hata rafiki yake. Ndo maana wanachumba wenzake walivyokuwa wanajipanga kwenda kumwambia kuhusu Neema, alijihisi wivu wa ghafla — kitu ambacho hakijawahi kumtokea kwenye maisha yake.
"Inabidi kesho nihakikishe hawamwambii… sitotoka darasani mapema," Jasmine alikuwa akijiwazia mwenyewe.
****
Kiufupi, tokea Rafaeli awasili chuoni, alikuwa maarufu kwa muda mfupi sana. Katika vyumba vya wasichana wengi walikuwa wakimzungumzia:
"Shosti, hivi unamwonaje yule mkaka tuliekutana naye akitoka kwenye mazoezi na wakina Elisha jana?"
"Mbona sikumuona ile jana. Na wewe, si yule mwenye weusi wa chocolate alinunua maji pale dukani wakati unaongea na yule John wa Tigopesa? Hebu nieleze yukoje huyo."
"Yukoje? Yukoje huyo?"
"Na wewe, mkaka flani mrefu, saizi ya kati, mweusi rangi ya chocolate, ana nywele kama za singasinga hivi… kimwona kama mtoto hasa ukiangalia lips zake."
"Utanionesha bwana, hata simkumbuki. Poa," walisema Judith na rafiki yake Lea, wanafunzi waliokuwa wanachukua kozi ya nursing mwaka wa kwanza sawa na wakina Rafaeli.
Lea alikuwa moja ya wasichana warembo sana pale chuoni. Alikuwa mmoja wa wasichana wanaojipenda sana na anayejua kupangilia mavazi. Tokea aingie pale chuoni hajawahi kuvaa nguo moja siku mbili.
Ukiachilia mbali kuwa mrembo, alikuwa akionekana nadhifu muda wote. Lea alikuwa mweusi maji ya kunde, mfupi wa saizi ya kati, na macho flani hivi makubwa ya kurembua. Pia naye alikuwa amejaaliwa shepu nzuri, na kilichokuwa kinamfanya awe mzuri zaidi ni wakati akicheka akiionesha mwanya na meno yake meupe.
Wengi walipenda kumwita mrembo wa Kimasai, kwani kabila lake alikuwa Mmasai japo hakukulia umasaini. Baba yake alikuwa Mmasai na mama yake alikuwa Msambaa.
Licha ya wanaume wengi kujigonga kwake wakitaka kung’oa kigori, hakuna aliyewahi kumpata. Hii ni kutokana na kwamba tayari alikuwa na mpenzi wake aliyemtokea kumpenda sana. Yaani kwa kifupi, kafa kaoza kwa huyo jamaa yake.
Japo hakupenda sana kupiga soga na wenzake, kila siku alikuwa akiwaskiliza marafiki zake wakimzungumzia Rafaeli. Hakuwa hata na time nao, lakini kila alipozisikia taarifa zake, alikuwa akitamani sana kumwona huyo mtu.
"Mbona amekuwa gumzo sana? Natamani na mimi nimwone… ila naamini hawezi kumzidi Fredi wangu kwa u-handsome," alijiwazia Lea wakati akiwa anaoga bafuni.
****
Ilikuwa ni siku nyingine asubuhi akijiandaa kwenda class. Alijiandaa, na baada ya kumaliza akaona leo achukue iPad aitumie kusomea maana hakuwa na laptop. Akamalizia kujipuliza marashi yake kisha akatoka kuelekea class.
Akaingia na kwenda sehemu yake. Alimkuta Jasmine anajisomea. Alimsalimia kisha akaendelea kujisomea. Hawajakaa sawa akaingia mwalimu wa kipindi cha asubuhi kufundisha. Akamaliza, akatoka.
Wakatoka wakaenda break fupi, wakaendelea na kipindi kingine. Baada ya mwalimu kutoka, Jasmine akamwambia Rafaeli:
"Yeye anaenda hosteli."
Rafaeli akamwambia:
"Poa."
Lakini hajakaa sana, akamwona anarudi na kuja kukaa nafasi yake.
"Naomba unielekeze ule mfumo wa damu mwalimu aliokuwa anaufundisha."
"Anhaa, poa," akamjibu wakati wakimwelekeza.
Mara wakaja Catherine na Sadiki wakiwa wanamvuta Neema.
"Rafa, kuna mtu hapa kuna kitu anataka kukuambia," alisema Sadiki.
"Kitu gani hicho, mzee?"
"Wee, atakuambia mwenyewe," Sadiki akajibu.
"Lakini hapa tunasoma… kwa nini asimwambie baadaye?" akasema Jasmine.
"Na wewe Jasmine unatugeuka eeh? Au hutaki akimwambia?" alizungumza Catherine.
"Rafa, tufanye baadaye. Ngoja nikuache kwanza. Naona Neema kuna kitu anataka kukuambia," akasema Jasmine huku akiinuka kinyonge kwenye kiti alichokaa na kuanza kuondoka.
"Poa, baadaye utanistua tukamalizie," Rafaeli alimwambia.
"Enhe, haya Neema, nasikia unataka kuniambia… niambie sasa," alisema Rafaeli.
Neema akaanza kunying’ata-nying’ata mara akamwambia:
"Mimi nilitaka nikuambie kwamba iPad yako ni nzuri."
Kisha akakimbia. Rafaeli alijikuta tu akitabasamu.
"Huyu naye ana lake jambo… au kapenda mchuma nini? Ngoja niende zangu gheto kwanza mpaka baadaye," alijiwazia.
Ile anatoka, akakutana na Sadiki na Abdi.
"Enhee, yule dogo alikuwa anataka aniambie nini? Maana mmemuacha kaishia kuniambia iPad yangu nzuri. Hahaha!"
"Yule dogo jana wakati upo kwenye boda wakati tupo discussion akaanza kukusifia. Mara una macho mazuri sijui sura nzuri… sasa tukaona asitusumbue lazima tumlazimishe akwambie. Hahaha!"
"Sasa itabidi nianze kuyalegeza vizuri… kumbe mimi ni mtoto jicho-jicho. Hahaha!"
"Freshiii. We lilegeze hilo mpaka lidondoke."
******
"Oya we TMJ, vipi? Kesho ligi inaanza, so leo tuwahini uwanjani tukajiandae na mechi ya kesho. Sisi tunaanza na Nursing mwaka wa pili," alisema Elisha.
"Poa, Elisha. Tena mimi kipindi cha Dokta Shayo sitokuwepo. Naenda town kuchukua viatu kabisa na soksi. So usisahau kuniwekea nipo maana we si ndio CR."
"Poa, we usiwaze. Usichelewe. Nitamwachia Madam CR majina yetu maana hata mimi sitokuwepo. Namfata Juma gheto kwake kule kuna mishe tunaenda kufanya, so by saa tisa na nusu tuwe tushafika."
"Basi poa. Sichukui muda mrefu. Nachukua boda chap tu narudi," alisema Rafaeli.
Akaingia roomu, akachange nguo chapu. Ile anataka kutoka mara simu ikaita.
"Hellow Miri, vipi huko? Biashara zinaendaje?"
"Biashara zinaenda vizuri, lakini Ema kanipigia simu kasema zile mashine za ice cream na koni hazifanyi kazi vizuri. Amemuita fundi kasema matengenezo ni shilingi laki moja na nusu. So vipi, tunafanyaje sasa?"
"Mwambie atoe hiyo hela ampe huyo fundi atengeneze. Nitai-replace wiki ijayo, sawa?"
Huyo alikuwa moja ya wafanyakazi wa Rafaeli waliokuwa wanamsaidia kuendesha biashara zake ndogo ndogo zinazomuingizia hela.
Rafaeli, baada tu ya kumaliza kidato cha nne, alikuwa na hamu sana ya kufanya biashara licha ya kwamba ndoto yake ilikuwa ni kuwa daktari. Lakini hakupenda sana suala la kuajiriwa na mtu. Ndio maana baada ya kumaliza kidato cha nne alimuomba mama yake akaishi na baba yake mkubwa aliyekuwa anaishi mkoani Pwani, wilaya ya Bagamoyo.
Baba mkubwa wake huyo alikuwa ni mkufunzi na mkuu wa chuo cha marine kinachohusika na masuala ya uinjiania. Licha ya kazi yake kubwa hiyo, hakubahatika kupata mtoto kutokana na ajali aliyoipata nchini Uingereza — ajali iliyompelekea kuto kuwa na uwezo wa kupata mtoto tena. Ilikuwa ni pigo kubwa kwake, lakini ilibidi akubaliane na hali. Kitu kilichomfanya kumpenda sana Rafaeli, mtoto wa mdogo wake, kama mtoto wake mwenyewe. Akaamua kuongea na mama yake Rafaeli ili kumsomesha.
Rafaeli, baada tu ya kumaliza kidato cha nne, akaenda kuishi na baba mkubwa wake huyo akiwa na wazo la kutafuta chochote cha kufanya. Ndipo alipomuomba mtaji aanzishe biashara yake. Biashara aliyoiona inafaa na ingemuingizia pesa ilikuwa ni biashara ya ice cream na koni za maziwa, ambazo alipanga kumtafuta mtu wa kumsaidia kuzipitisha mashuleni huku yeye akifungua duka la koni na ice cream karibu na chuo kikuu cha St. Mary’s Bagamoyo.
Biashara ilimuendea vizuri sana na koni zikapata umaarufu. Hii pia ilichangiwa na wanawake wengi wa chuo hicho kumpenda kwa sura yake ya kipole na jinsi alivyoongea na wateja huku akionekana kama mtoto. Baada ya muda akaongeza mashine nyingine ya kutengenezea na kuwapa watu waendelee kuuza katika mashule mpaka alipojiunga na shule ya Makongo, akaanza kulima tikiti maji na kuziuza kwenye mashule kama Makongo na Baobab. Licha ya hivyo, hakuna aliyejua anamiliki biashara kwani alikuwa akiishi maisha ya kawaida kama wenzake.
Rafaeli alifika mjini, akachagua viatu vya mpira vya elfu sabini na soksi. Akakodi tena boda boda akiianza safari ya kurudi chuoni awahi mazoezini.
****
Basi, mrembo wa Kimasai, baada ya kurudi kwenye chumba chake wakipiga stori:
"Jamani, kesho kuna mpira kati ya CO mwaka wa kwanza na Nursing mwaka wa pili. Mnaonaje tukienda? Halafu tena nasikia yule Rafa naye anacheza!"
"Wee kweli? Lazima niende huko nikaangalie mpira. Vipi Lea, we si upendagi kuangalia mpira, kesho utaenda?"
"Mhmh, kesho nataka niende mjini kununua baadhi ya mahitaji yangu. Mimi, nyie mtaenda tu," alijibu Lea.
"Poa ahosti, ningekupeleka lakini mwenzio najikuta kwenda uwanjani ile balaa," wakacheka huku Lea akiingia bafuni.
"Nimemmisi Fredy jamani. Halafu siku hizi hata hanipigii simu sijui ana nini. Halafu sijui niende nikaone huyo wanaomsifia kila siku nikamuone. Si wamesema anacheza hiyo kesho? Ila kweli mahitaji nitanunua Ijumaa bhana, kwanza hayana umuhimu sana," akajiwazia Lea, au mrembo wa Kimasai.
Akaoga harakaharaka, akatoka bafuni, akamkuta rafiki yake anasoma kitabu.
"Shosti, kesho usiniache. Nimeghairi, nataka nikapoteze poteze mawazo uwanjani huko. Japo sipendi mpira, ila nitaenda tu," alisema Lea.
"Kweli, rafiki yangu. Twende, mimi nitakupeleka kununua hayo mahitaji keshokutwa bhana."
"Haya, poa."
*******
"Daah, mzee, hiko kiatu sio poa. Yaani ulipotoka kama Ronaldo vile. Yaaah, mbona kawaida tu? Sema kiatu nimekipenda, ila asante kwa kuniazima viatu vyako mzee Lewisi."
"Poa, usiwaze. Twende zetu sasa uwanjani, nadhani wenzetu washafika," aliitika Drogba.
Ilikuwa ni saa sita baada ya vipindi.
"Vipi Rafa, leo utaenda kucheza mpira?" akauliza Jasmine wakati wanatoka.
"Ndio, nitaenda. Wee si utakuja kutushangilia?"
"Mhmh, nitaangalia. Maana sipendi kutoka toka. Pia nataka nikafue."
"Anhaa, basi poa. Baadaye."
Basi watu walifika uwanjani — wengi wadada na wakaka, wengine na wapenzi wao kushuhudia mechi ikichezwa. Wakiwemo wakina Lea. Siku hiyo alipendeza balaa japo ni kawaida yake, lakini siku hiyo alipitiliza.
Alikuwa amevaa blauzi flani ya pink, jeans ya blue, na raba zake nyeupe. Alionekana mrembo kweli kweli. Kila alipopita watu walimkodolea macho.
"Duuh, huyu jamaa anayeendesha huu mchuma jamaa anabahati sana," mmoja akasema.
"Haha, ndo hivo mzee. Usione anapendeza hivo, jamaa anahudumia. Ila yote na yote haingii kwa yule Jasmine wa mwaka wa kwanza. Yule mtoto ni hatari. Akivaa suruali yule na ile shepu… tutapanga foleni maana sio poa," aliongeza mwenzake.
"Halafu yule dogo katulia ile mbaya yani."
"Kweli mzee, yule dogo mkali. Tena nasikia Mrangi yule," waliendelea kuzungumza wanafunzi wa Nursing mwaka wa pili.
Muda huo wachezaji walikuwa ndio wanaanza kuingia uwanjani, akiwemo Rafaeli, huku akirukaruka akiwa amempa mgongo Lea.
Lea sasa akamwuliza rafiki yake:
"Yule mkaka niliyekuambia yule… anaekuja upande wetu?"
Lea akaangalia alikoelekezwa… akakutana macho kwa macho na Rafaeli.
Lama umeipenda weka maoni hapo chini, niweke mwendelezo
Comments