Reader Settings

GENERAL KAGIMU

Generali mkuu wa jeshi la Uganda na mkuu wa majeshi wa Taifa hilo bwana jenerali Kagimu, alikuwa ni moja ya watu ambao walikuwa wanaheshimika na kuogopeka mno kwenye taifa la Uganda. Alikuwa ni moja ya sehemu za mhimu mno za raisi wa taifa hilo ambaye kwake taifa lilikuwa kama lake yeye na familia yake.

Generali huyo alikuwa ni mtu mjivuni na mpenda sifa mbele za watu, alikuwa anaogopwa sio kwa sababu ya kupendwa ama kuheshimika bali kwa sababu alikuwa anamuua kila ambaye alionekana kuwa kinyume na matakwa yake yeye. Alikuwa ni sehemu mhimu ya raisi wa taifa hilo kuhakikisha taifa linakuwa salama lakini kwa wakati huo hawakuwa na mazungumzo mazuri kwa sababu kulikuwa na tetesi kwamba bwana huyo alikuwa mbioni kuweza kumpindua raisi ambaye alikuwa madarakani kwa wakati huo.

NAKASONGOLA AIRFORCE BASE

Kwenye moja kati ya base kubwa zaidi za kijeshi ndani ya Uganda za jeshi la Anga ndiko ambako jenerali Kagimu alionekana, alikuwa ameenda huko kwa ajili ya kuwatunuku nishani majenerali wengine ambao walikuwa wamepanda vyeo pamoja na wanajeshi ambao nao walikuwa wamepandishwa vyeo kutokana na kazi zao tukuta ambazo walikuwa wamezifanya ndani ya taifa hilo kiasi kwamba walikuwa wakihitaji heshima ambayo walistahili.

Zoezi hilo lilifanyika kwa masaa matatu mfululizo ndipo alimaliza kazi hiyo na kisha akakagua gwaride la watu hao na vifaa vya anga na alipohakikisha kwamba kila kitu kipo sawa, alijiandaa kwa ajili ya kuondoka lakini kabla ya kuondoka alihitaji kwanza kukutana na kiongozi wa eneo hilo kwa sababu alikuwa na mambo kadhaa ya kuweza kuongea naye tena kwa usiri mkubwa bila mtu mwingine yeyote kuweza kuyasikiliza hayo mazungumzo yao.

Generali Kato, mwanaume ambaye alikuwa na historia ya kutisha huko nyuma akiwa kijana, historia ambayo ilimfanya kukaa kwenye nafasi yake ndiye ambaye alikuwa anaenda kufanya mazungumzo na mkuu wa majeshi wa taifa hilo. Wote wawili walikuwa ni watu wazito ndani ya taifa la Uganda ambapo mmoja alikuwa ni mkuu wa majeshi yote na mwingine alikuwa ni kiongozi wa jeshi la anga la taifa hilo.

“Mheshimiwa kuna uvumi unasambaa kwa sasa, kuna ukweli wowote kuhusu jambo hilo?”

“Kato unanijua vyema kwamba huwa sipendi kabisa kuongea kwa njia za mikato, unaweza ukaniambia kwamba ni jambo gani ambalo unalizungumzia hapa”

“Nasikia kwamba unataka kuwa raisi wa taifa hili!”

“Mhhhhhh Kato, wewe sio mtu wa kuanza kuamini kila habari ambayo unakuwa unaiokota kwenye mitandao”

“Ndiyo maana nipo hapa kukuuliza wewe mheshimiwa kwa sababu sitaki kabisa kuamini habari ambayo nitaipata kwa mtu mwingine yeyote zaidi yako”

“Wewe baada ya kuzisikia habari hizo ulizipokeaje?”

“Sikuzipokea kwa uzuri kwa sababu zinaenda kuleta mgawanyiko mkubwa kati yetu na unalitambua hilo general”

“Haujaibu swali langu”

“Mimi na wewe tumetoka mbali mno, unahisi kwamba naweza kwenda kinyume na wewe?”

“Kwa mtazamo wako unaona kwamba huyu raisi anafaa kuendelea kuwepo Ikulu baada ya kukaa kwa takribani zaidi ya miaka ishirini na mitano sasa?”

“Inawezekana sio sahihi lakini pia sioni kama ni ustaarabu mkuu wa majeshi kuingilia jambo hili kwa sababu linaweza kuja kuleta madhara makubwa na mpasuko kwa taifa jambo ambalo sina imani kama hata wewe unatamani kuweza kuona likiwa linatokea kwenye taifa letu’’

“Do you think i care that much about this country?”

“Why not sir?”

“Nobody cares anyway”

“Are you serious about this sir?”

“Nilikuwa nimepanga kuweza kumuua raisi lakini kwa sasa sioni kama jambo hilo lina umuhimu hivyo zoezi litasimama mpaka kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo”

“Ulipanga kumuua raisi wa Uganda”

“Wanauawa maraisi wa Marekani itakuwa Uganda Kato”

“So it’s true about the rumours”

“Yes”

“Hili jambo ambalo unaliwaza halina afya kwa usalama wa taifa hili mheshimiwa”

“Tusipoteze muda na jambo hilo, nilitaka kuzungumza na wewe kuhusu Tanzania”

“Imefanyaje?”

“Kuna taarifa ambazo nimezipata asubuhi ya leo kwamba kuna watu wamekutwa wamekufa tena kwa kuuawa kikatili’’

“Sasa hao watu wanatuhusu nini sisi?”

“Nadhani punguza kulala na wanawake kwa sababu wanakufanya unasahau baadhi ya mambo ya mhimu. Kwamba umesahau kila kitu?”

“Usiniambie kwamba jambo hili linahusiana na yale matukio ambayo yametokea miaka ya huko nyuma!”

“Hiyo ndiyo maana yake”

“Unajaribu kuniambia nini?”

“Kuna mtu mwingine ambaye ameonekana kuingia kwenye hili jambo hivyo kumeanza kuonyesha ishara mbaya”

“Sijakuelewa bado”

“Wewe ni mtu msomi jeneral hivyo kuna wakati unatakiwa kujitahidi kuweza kwenda na alama za nyakati kila unapokuwa unayafanya mambo yako”

“Ni stori ambayo unanielezea kana kwamba mimi ndiye nilikuwepo eneo la tukio vile”

“Kuna mtu mwingine ambaye ameingia kwenye jambo lile hivyo ni wazi kwamba kuna watu walikuwa na zile taarifa jambo ambalo linaweza kuwa na hatari kubwa kwetu”

“Kwahiyo ile kesi imefufuliwa?”

“Sio moja kwa moja ila inawezekana kwamba ikafufuliwa muda wowote ule kuanzia hivi sasa’’

“Lakini walituahidi kwamba jambo lile lingeshughulikiwa vyema”

“Hilo ni kweli lakini wote tunajua hapa duniani siri inapokuwa kwa watu kuanzia wawili basi kamwe haitaweza kuwa siri tena”

“Wamemjua huyo mtu?”

“Hapana, wanadai kwamba walikuwa na wasiwasi juu ya mambo kadhaa na kuhusu watu kadhaa ambao walihisi wanaweza kuwa na hiyo siri jambo ambalo lilipelekea watu hao kuanza kutafutwa na mmoja alikutwa usiku wa manane akionekana kwenye dalili za kuweza kukutana na mtu mmoja. Inadaiwa kwamba haieleweki kama alikutana naye au hawakukutana na baada ya hapo hao watu ambao walitumwa kufuatilia jambo hilo ndio ambao wamekutwa wakiwa wamauliwa”

Ukurasa wa tatu unafika mwisho.

Febiani Babuya.

Previoua Next