"Kweli kumpenda asiyekupenda ni kama kutikisa umande utiririke kutoka juu ya mti," Shata alimwambia Rehema akiegeza gari lake kando ya benki.
Pasipo na kusema lolote, Rehema alishuka akamuongoza mpaka afisini alipokusudia kuwa naye kwa maongezi.
"Kwa nini usimuache mume wa mwenzako," Rehema aligonga ndipo akijua anatia msumari moto kwenye kidonda, "mshale ambao hujaingia sana si mgumu kuchomoa. Kubali kwamba yalishatokea akampata aliyeumbiwa na Maulana."
Shata alipokuwa …
Tafadhari Ingia/Jisajili uweze kuendelea.
Comments