Reader Settings

DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!


★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA TATU

★★★★★★★★★★★


Walipomaliza kula, waliketi kwenye masofa tena na kuendeleza maongezi yenye kufurahisha. Angalau muda huu Jaquelin alijitahidi kuonyesha kachangamka. Beatrice alipendekeza kwamba Dylan awe anatoka kufanya mazoezi na Harleen, na kwa kuwa Dylan alisema asubuhi huwa ana kawaida ya kwenda kukimbia (jogging), basi Beatrice akasema ikibidi waanze kesho. 

Harleen yeye aliishi kwenye chumba cha hoteli kubwa ya kisasa (apartment) katikati ya jiji, kwa dhumuni la kuwa karibu na hospitali kwa kuwa nyumbani kwao palikuwa mbali. Kila mmoja wao alikuwa ameshaelewa kwamba Beatrice alitaka sana kuwafanya Harleen na Dylan watengeneze uhusiano wa karibu zaidi. Wazo hilo lilikuwa zuri kwa vijana, hivyo wakakubaliana kukutana kesho asubuhi na mapema maeneo fulani ili waanze zoezi.

Ilipofika saa 5 usiku, wageni hao wapendwa wakaagana na rafiki zao ili waelekee hotelini kupumzika.

Hakukuwa na jambo lolote lililowaunganisha wanafamilia hao watatu pindi wageni walipoondoka. Jaquelin alienda zake chumbani, Dylan pia, na Gilbert akabaki mwenyewe sebuleni akisoma vitu mitandaoni. Ilikuwa imebadilika kuwa familia yenye nafasi kubwa zilizoachwa wazi ilipokuja kwenye suala la mahusiano ya karibu baina yao, na kulikuwa na sababu iliyofanya hali iwe hivyo. Harleen aliposema kuhusu upasuaji wa Jaquelin, alikuwa amewakumbusha sababu hiyo. Hivyo kila mmoja wao akawa amejitenga tena kama ilivyokuwa kawaida yao.


★★★


Asubuhi ikafika. Dylan aliwahi sana kuondoka nyumbani, kukiwa bado na giza-giza la alfajiri na baridi kiasi. Alivalia nguo za mazoezi, kisha akabeba maji, taulo, na kuchukua gari lake kuelekea kule alikoahidiana na Harleen kukutana. Alipofika, akatoka ndani ya gari na kuelekea sehemu iliyokuwa na uwanja mpana uliofyekwa nyasi vizuri. Akaanza kupasha mwili wake kwa mazoezi rahisi mpaka pale Harleen alipofika.

Alikuwa amevalia nguo za mazoezi zilizoubana mwili wake vyema na kuchora umbo lake vizuri. Ijapokuwa alikuwa na mwili ulionawiri, hakuwa na manyama makubwa au likitambi. Nguo yake ya mazoezi ilikuwa ya aina hiyo hiyo na rangi ya kijivu, juu yenye mikono mirefu, na suruali yenye kubana iliyovutika na kufanya kalio lake lijikate vizuri kwa nyuma. Alivaa na raba nyeupe za mazoezi, huku nywele zake zilizosukwa akiwa amezibana kichwani kwa juu.

Walipoanza mazoezi ya kadiri, Dylan angemtazama mwilini mara kwa mara, akiangalia jinsi mikunjo iliyonona ya mwili wa mrembo ilivyokuwa yenye kutia hamasa kwa mwanaume yeyote yule kumtazama sana. Nyakati ambazo angemwelekeza jinsi ya kuweka mikono, miguu, mgongo, angehitaji kumshika kwa nyuma, na hilo lilifanya jamaa aweze kumwangalia kwa upendezi hata zaidi kutokana na ukaribu huo. Angetabasamu au kuchekea pembeni kila mara wazo la kiutundu lilipoingia kwenye akili yake kumwelekea daktari huyu, lakini baadaye angepotezea tu.

Walipomaliza ya kujinyoosha, wakaanza ya kukimbia, nao walitumia takribani dakika 40. Kwa Dylan, zilikuwa ndogo sana. Lakini aliona zimempasha mrembo vyema, hivyo akaona waache ili wapumzike kidogo. Harleen alikuwa anapumua kwa kasi kiasi, akijaribu kurudisha mfumo mzuri wa upumuaji. Dylan akamwongoza warudi kwenye uwanja ule na kuketi sehemu waliyokuwa wameweka vitu vyao vichache. Harleen akanywa maji kiasi na kuketi chini. Dylan akaketi karibu yake pia.

"That was... heatfull!" akasema Harleen kwa shauku.

"Ahahah... hauna kawaida ya mazoezi eti?" Dylan akamuuliza.

"Oh, huwa ninafanya mazoezi. Sema, sijakimbia kama wiki sasa. Na wewe yako ni magumu mno," akasema kiutani.

"Ahahah... you big baby," Dylan akatania.

"Ndiyo hivyo."

"Okay, I guess... kila kitu unaweza. Kunipasua unaweza, mazoezi unaweza, lugha unaweza, wewe... ni mweza," akasema Dylan.

"Ahahahah... acha mambo yako bwana. Kila mtu ana vipawa fulani. Unapoamua tu kuvi... extend... unaweza," akasema Harleen.

"Yeah ni kweli. Kwa nini ulijifunza Spanish? Ni wivu tu kwamba nilienda Brazil, au?" akauliza Dylan kiutani.

"Ahahahah... mwone kwanza, eti wivu!"

Dylan akatabasamu.

"Me gusta español mucho (napenda Spanish sana)," akasema Harleen kwa ufasaha sana.

"Wow!" Dylan akapendezwa na hilo.

"Nilitaka sana kujua lugha hiyo kwa kuwa nilianza kuiona kama kiswahili vile. Na pia niliwaza... huyu bichwa akirudi atakuwa ameshasahau kiswahili... kwa hiyo nikajiweka tayari," akaeleza binti.

"Kumbe? Inafurahisha sana kujua ulijifunza kwa ajili yangu," Dylan akasema kichokozi.

"Ahahah... kwa sehemu tu... wewe siyo sababu yote," akasema Harleen, na wote wakacheka.

"Ustedes como aprendieron? (ulijifunza vipi?)" Dylan akamuuliza.

"En linea (online/mtandaoni)," akajibu.

"Ooh..."

"Yeah. Las personas en este... grupo han ayudado me mucho (ndiyo. kuna watu kwenye.. grupu fulani mtandaoni ambao wamenisaidia sana)," akasema Harleen.

"Ahahah... Napenda unavyokiongea. Kama mzawa wa kule kabisa," Dylan akasema.

"Muchas gracias (asante sana)," akajibu Harleen.

"Aunty umemwacha anakoroma?"

"Ahahahah... hakoromagi bana."

"Wee! Nakumbuka vizuri wakati tunaishi kwenye ile nyumba bado. Alikuwaga akija kwa mama kufanya sleepover anakoroma huyo! Nilikuwa naweka mito kwenye masikio ili nilale kwa amani," Dylan akatania.

"Ahahahah... ameacha siku hizi. Halafu... hiyo nyumba yenu ya kule iliuzwa au?" Harleen akauliza.

"Hapana. Kuna kipindi mama alitaka waiuze lakini baba akakataa. Alisema anaitunza kwa ajili yangu."

"Wow! Ni nyumba kubwa nakumbuka. Walipojenga hii nyingine ndiyo wakaiacha tu eeh?"

"Yes. Huwa naenda pale mara kwa mara kui-check, nafikiria kuja kuipiga remake ya ukweli halafu nikakae kwenye mansion langu hilo."

"Ahahah... itapendeza. Unajua imekuwa kitambo sana. Natamani kupaona tena kule," akasema Harleen.

"Ukipenda twaweza kwenda... upaone. Kama utakuwa na nafasi lakini," Dylan akapendekeza.

"Ndiyo. Nina nafasi zaidi leo. Vipi tukienda mida ya saa 10? Au una mazoezi muda huo?" akasema Harleen.

"Hapana. Mazoezi hayafati ratiba hususa. Nitakupitia basi," akasema Dylan.

"Sawa."

Baada ya kuwa wamepata maongezi hayo, wote waliachana muda mfupi baadaye na kuelekea makwao. Kwa kuwa Dylan hakwenda kazini wala Harleen kwenda hospitali, ilikuwa ni siku huru kwao kutembelea mazingira yale ambayo kwa kipindi fulani waliyaishi pamoja wakiwa wadogo.

Harleen alijihisi uchangamfu wa hali ya juu sana; fikira ya kuwa na rafiki yake wa kitambo sehemu waliyokua na kucheza pamoja ilimsisimua sana. Kuna mambo mengi kuhusu Dylan ambayo yalimfanya ajihisi huru sana nyakati zote ambazo aliwahi kuwa pamoja naye, na sasa hisia hizo zilikuwa zimeamka tena.


★★


Ilipofika saa tisa na nusu alasiri, Dylan alitoka kwao na kuelekea hotelini kwa Harleen kumpitia. Alikuwa amewahi ili waweze kuondoka mapema kwa sababu mwendo wa gari kufika kule kwenye nyumba ya Dylan ilikuwa saa zima. Baada ya kufika na kumtaarifu kuwa amefika, Dylan alikaa ndani ya gari lake akisubiri binti amalize kujiandaa ili waianze safari.

Zikapita kama dakika 10 hivi, na mtoto mzuri akaonekana akilifata gari la jamaa taratibu. Dylan aliweza kumwona kwa mbele, naye alipendezwa na mwonekano wa rafiki yake huyo daktari. Alikuwa amevaa kigauni chepesi chekundu kilichoishia kwenye magoti yake. Mkononi alishika mkoba mwekundu, na miguuni alivaa viatu virefu vyekundu. Nywele zake aliziachia kwa nyuma na mdomoni alipaka 'lipstick' nyekundu iliyoupendezesha mwonekano wake mzuri sana.

Akiwa anakaribia kulifikia gari lilipoegeshwa, Dylan akamwashia taa za mbele mara mbili, kama kumkonyeza, naye Harleen akaonekana akitabasamu. Kisha akaingia siti ya mbele baada ya kufika na kuketi.

"Umependeza!" Dylan akamsifia.

"Asante."

"Road trip?"

"Twen'zetu," akasema Harleen.

Kisha safari ikaanza. 

Walipiga story za hapa na pale, huku Dylan akimsimulia jinsi mambo mengi ya huko kwenye nyumba ile yalivyobadilika. Baada ya nusu saa hivi, wakawa wamefika upande huo wa jiji na kuelekea kwenye nyumba hiyo. Ilikuwa na uzio wa ukuta mrefu kuizunguka, na geti jeusi lenye mwonekano mkuukuu. Dylan akashuka na kwenda kulifungua, kisha akarudi ndani ya gari na kuliingiza mpaka ndani. Akashuka na kurudi tena getini kupafunga, akimwacha Harleen ameshuka pia akiangalia-angalia eneo hilo.

Nje hapo palikuwa tu kama jinsi mrembo alivyopakumbuka. Akaiangalia nyumba ile, ambayo ilikuwa na ghorofa moja pana, naye akatabasamu baada ya kukumbuka michezo mingi waliyofanya pamoja na Dylan kwenye nyumba hii. Upepo ulikuwa unapuliza kwa nguvu wakati huu, hivyo kulikuwa na baridi kwa kadiri fulani.

"Mashavu, twende ndani. Tutaganda hapa," sauti ya Dylan ikasikika nyuma yake.

Wakauelekea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba, kisha Dylan akaufungua na kisha kuufunga baada ya wote kupita ndani. Macho ya Harleen yalizungukia nyumba hii, akitambua kuna vitu kadhaa vilikuwa vimebadilika sana.

"Pamebadilika eti?" Dylan akamuuliza.

Harleen akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Yeah, uko sahihi. Wazazi wetu walipenda sana jinsi mpangilio wa hapa ulivyokuwa. Vitu vingi vimeondolewa."

"Yeah ni kweli. Ila muda siyo mrefu ninataka kuja kupajaza hapa," Dylan akamwambia.

"Nyumba nzuri sana. Kwenye masuala ya ujenzi kweli uncle Gilbert yuko vizuri," Harleen akaisifia.

"Speaking of which, njoo huku uone. There's something you might be interested in seeing," Dylan akasema.

"Wapi?" akauliza Harleen.

"Sigueme (nifuate)," Dylan akamwambia kwa ki-spanish.

Harleen akamfuata jamaa mpaka usawa wa dirisha kubwa upande mwingine wa nyumba. Sehemu hiyo ya nje ilipendeza sana kutokea hapo waliposimama. Walitazama uwanja huo uliokuwa na swimming pool, miti kadhaa na sanamu ndogo ya simba iliyokuwa imejengwa chini kama pambo.

"Wow! Hiyo sanamu bado ipo!" Harleen akasema kwa shauku.

"Ahahah... yeah."

"Nakumbuka tulikuwaga tunaisemesha na kuigiza hapo kwamba simba anatung'ata..." akasema Harleen huku akicheka.

"Eee ndiyo. Ile michezo ilifurahisha sana," akasema Dylan.

"Sana. Nakumbuka karibia kila jambo tulilofanya hapa."

"Mimi pia."

"Hivi unaweza kuamini muda umepita haraka sana namna hii? Tulikuwa tukikaa muda mwingi mno kwenye hiyo pool pamoja. Yaani ni kama vile sa' hivi tuko kwenye maisha mengine," akasema Harleen kwa hisia.

"Yeah ni kweli. Los momentos... (nyakati hizo)," akasema Dylan.

"La alegria (zile shangwe)," akasema Harleen.

"La risas (vicheko)," akasema Dylan.

Harleen akatulia kidogo kisha akasema, "La espera (kusubiri sana)."

Dylan akamgeukia taratibu na kumtazama. Harleen pia akamwangalia kwa hisia. Maneno hayo ya mwisho ya bibie yalimfanya Dylan atambue kuwa kuna kitu fulani Harleen alitaka kusema, hivyo akampa umakini wake. Harleen akaonyesha wazi kuna jambo alitaka kumwambia jamaa kwa kumgeukia vizuri.

"Nakumbuka ulikuwaga unanichungulia nilipokuwa huko nyuma. Tena sanasana nilipoenda kuogelea. Ningejifanya kama vile sikukuona, ila nilijua ulikuwa unanitazama," akasema Harleen kwa hisia huku anatabasamu.

"Ahahah... asa' ulitegemea nini? Ulikuwa ndiyo msichana mzuri zaidi ya wote mtaani, nami nilikuwa ndo' nimeanza kupata mahisia," Dylan akajitetea.

"Hahah... eti mahisia."

"Ni kweli. Huo ulikuwa muda mrefu sana uliopita. Check sa' hivi tulivyo, yaani inaonekana ni kama jana tu."

"Do you still think about me? (bado huwa unanifikiria?)" Harleen akauliza kwa hisia sana.

"What do you mean? (unamaanisha nini?)" Dylan akauliza.

"Huwa... unanifikiria kama ulivyokuwa unanifikiria kipindi hicho? You know... me... coming out of the pool... wet... (yaani... kama jinsi nilivyokuwa natoka ndani ya bwawa.. nikiwa nimelowana)."

Dylan tayari aliweza kukisia mazungumzo haya yalikuwa yanaelekea wapi, lakini kwa sababu fulani alikuwa hataki yafike huko ijapokuwa kwa jinsi mambo yalivyojitengeneza hapa, ingekuwa ngumu sana kukwepa.

"Kwa nini unauliza?" mwanaume akauliza pia badala ya kutoa jibu.

"Curiosity. Me nikienda kuogelea mara kwa mara huwa nakumbukia hilo," akasema Harleen.

Kwa kuwa sasa Dylan alijihakikishia kwamba mtoto anataka kuingia ndani ya 18, akaona amfungulie milango. Akamsogelea usoni zaidi huku anamtazama kwa macho yenye hisia na utundu mwingi.

"Curiosity killed the cat (udadisi ulimuua paka)," Dylan akatania.

Harleen akacheka kidogo huku akiitazama sana midomo ya jamaa.

"I'll be honest. Nilipenda kukuangalia sana kwa kuwa vinguo vya kuogelea vilifanya sehemu kubwa ya mwili wako ionekane. Sikuwahi kuona msichana akiwa bila nguo, na wewe ulikuwa umekaribia jambo hilo. Uli... ulinisisimua," akasema Dylan kwa sauti yenye hisia, huku anausogelea mdomo wa Harleen kichokozi.

Harleen akabaki kumtazama tu kwa ukaribu huo, kama anasubiri kwa hamu jamaa afanye kitu fulani. Mara Dylan akarudi nyuma na kufanya matarajio ya rafiki yake huyo yakate.

"Anyway, jioni inaingia. Tumalizie tour yetu kwenye nyumba halafu tuondoke. Kuna jambo lingine unataka kuona?" Dylan akabadili mada ghafla.

Harleen akaangalia nje kupitia dirisha, kisha akasema, "Nimeshaona kila kitu nilichohitaji kuona. Imerudisha kumbukumbu nyingi nzuri sana. The best part about all this is that... nimeweza kukuona tena," Harleen akasema kwa hisia.

"Asante," akasema Dylan.

"I want to go swimming (nataka kwenda kuogelea)," akasema Harleen.

"Wewe! Hayo maji ni ya baridi sana," Dylan akamtaarifu.

"Najua. Lakini sitakaa ndani ya maji muda mrefu. Nataka twende wote. Itakuwa fun," Harleen akasema kwa shauku.

"Kuna mambo mengine fun zaidi ya kufanya hapa... ila hilo... mh..."

"Hayo mengine hayataburudisha sana kama kuogelea humo. Najua unataka kujaribu pia, wewe si ndiyo Dylan asiyeogopa chochote?"

"Ndiyo mimi. Ila wewe nakuonea huruma, sitaki ushikwe na baridi," Dylan akasema kwa kujali.

"Usiwaze. I want to do something crazy, kama wewe ulivyozoea."

Dylan alimwangalia Harleen na kuona kweli alikuwa na hamu ya kufanya jambo hilo. Kwa muda huu, hakuonekana kama mwanamke mwenye umakini wa kidaktari tena, bali kama yule Harleen aliyemzoea wakati wako wadogo. Hakukuwa na pointi ya kubishana naye tena, hivyo jamaa akalegeza.

"Haya... ngoja nikafate taulo," akasema Dylan.

"Thank you," akasema Harleen kwa furaha.

Upesi Dylan akapanda kuelekea chumbani ili kufata taulo. Akachukua mbili, moja kwa ajili yake na nyingine kwa ajili ya rafiki yake huyo. Jambo hilo walilopanga kufanya halikuwa sehemu ya mambo aliyofikiria yangefanyika hapa, na aliliona kuwa wazo baya kiasi. Lakini kwa kuwa lilingempa furaha mtoto, akaona ni vyema kuacha afanye kile kilichomfurahisha; na yeye ajaribu kufurahi pamoja naye pia.

Akarejea kwa Harleen na kukuta anavua nguo zake. Alisimama na kumtazama kwa makini. Juu alikuwa ameshatoa kigauni chake, hivyo akawa amebaki na sidiria ya kijani iliyong'aa na chupi nyepesi ya aina hiyo hiyo. Ngozi yake nyeupe ilimng'arisha vizuri sana, na umbo lake liliyavutia sana macho ya Dylan.

Wakati huu alikuwa anafungua mikanda midogo ya viatu vyake miguuni, hivyo alikuwa ameinama na kufanya kalio lake libinuke kwa nyuma. Dylan akawaza bila shaka Harleen pia alikuwa mwenye uzungu mwingi maana hakuwa na aibu kuhusu kuvua nguo akiwa na rafiki yake wa kiume peke yao kwenye nyumba moja. Alipomaliza, akasimama na kuzibana nywele zake vizuri kwa nyuma. Dylan akaanza kumwelekea polepole huku anatabasamu. Harleen akamgeukia na kuachia tabasamu huku anamwangalia jamaa kwa hisia.

"Damn," Dylan akamsifia kwa ufupi.

Harleen akacheka kidogo kisha akasema, "Es tu turno (zamu yako)."

Bila kuchelewa, Dylan akavua shati lake mbele ya Harleen na kuliweka pembeni. Kisha akaanza kufungua mkanda wa suruali yake kimadoido ili kucheza na akili ya Harleen, naye mrembo akatazama pembeni akizungusha macho kikejeli. Dylan akacheka, kisha akaishusha suruali yake na kuitoa yote, akiwa amebaki na boxer sasa. Harleen alitazama kwa matamanio sana mashine ya jamaa. Jinsi ilivyokuwa imejichora juu ya boxer yake ilimsisimua, lakini akajitahidi kukwepesha macho yake ili jamaa asimshtukie. 

Vitu hivi kwa Dylan pia vilikuwa vya kawaida kwa kuwa kule Brazil watu huishi kwa kujiachia sana. Alikuwa amekwishatembelea sehemu nyingi kama beach, ambazo zilijawa na wanawake wengi waliovalia chupi na sidiria tu, hivyo kumwona mwanamke akiwa namna hii hakukuwa jambo geni. Sema ilipokuja kwa Harleen, ni kwa kuwa hakuwa amemwona kwa muda mrefu sana, na sasa siku ya pili tu tayari rafiki yake huyu akawa ameanzisha michezo yenye kusisimua, hivyo Dylan alipenda sana hali hiyo.

"Okay. Nimemaliza," Dylan akasema.

Harleen akamshika mkono na kuanza kumwongoza kuelekea nje kwenye swimming pool. Dylan alikuwa anachekea kichini-chini jinsi kalio la mtoto lilivyonesa-nesa huku na huku kila alipopiga hatua. Akaanza kumtania kwa kuupigisha ulimi wake ndani ya mdomo kufatisha mwendo wa kalio la Harleen, naye Harleen akacheka kidogo kwa furaha.

Walikubaliana kwamba wakifika usawa wa swimming pool, wangekimbia kwa pamoja na kujirusha ndani ya maji. Baada ya kuhesabu 1, 2, 3, wote wakayakimbilia maji wakiwa wameshikana mikono bado, kisha wakajirusha na kudumbukia ndani kwa nguvu, maji yakiruka juu. Ilionekana kama muda unapita sana walipokuwa ndani ya maji baada ya kujitupia, kisha taratibu miili yao ikaanza kupanda juu tena. Walipofika juu, kila mmoja alikuwa akicheka kutokana na burudisho hilo walilopata pamoja, na kama Dylan alivyokuwa amesema, maji hayo yalikuwa baridi sana.

Hivyo Dylan akamshika Harleen na kuanza kuogelea naye kuelekea kwenye kingo ya swimming pool ili waweze kutoka. Akatoka kwanza, kisha akamvuta mtoto, ambaye alikuwa akitetemeka sana. Dylan akamwongoza kuelekea ndani mpaka sehemu ile waliyoacha taulo. Akaanza kumfuta maji Harleen kwa taulo moja, kisha akachukua nyingine na kumfunika nayo. Ijapokuwa Harleen alitetemeka kutokana na baridi, bado alijitahidi kutabasamu kwa kuwa jambo walilofanya lilimburudisha kwa kiwango kikubwa.

Dylan akamketisha Harleen kwenye sofa moja lililokuwa hapo, kisha yeye akaelekea sehemu ya jikoni kuangalia ikiwa angeweza kupata kiberiti ili atafute kuni na kuwasha moto wa kuipasha miili yao. Alitafuta lakini akakosa, huku naye mwili wake ukihisi baridi pia. Akarejea kwa rafiki yake na kukuta amejifunga taulo moja kuanzia kifuani mpaka ilipoishia mapajani, na alipotazama kwenye kiti cha pembeni akaona sidiria na chupi ya bibie zimewekwa hapo; kama kuanikwa.

Harleen alikuwa ameketi kwenye sofa, huku mdomo wake ukitetemeka kiasi, naye alikuwa anatumia taulo nyingine kujifutia nywele.

"Mashavu..." jamaa akamwita.

Mrembo akamtazama na kuacha kujifuta nywele.

"Samahani... nimekosa kitu cha kukupasha mwili joto... sijui kupasha joto mwili... mwili joto kuupasha..." Dylan akawa anababaika kuongea.

Harleen akatabasamu na kumrushia taulo jamaa, kisha akasema, "Usijali."

Dylan akaanza kujifuta-futa maji mwilini huku anamtazama rafiki yake. Nywele za Dylan zilikuwa zimemwagikia kuzunguka kichwa chote, hivyo akaanza kuzifuta pia kwa fujo. Harleen akawa anamwangalia kwa njia yenye uvutio mwingi sana, kama kutaka kumwambia vitu vingi ila akawa anashindwa. Dylan alipomaliza kujifuta, akamwambia anakwenda chumbani mara moja. Alikuwa anataka kuitoa boxer yake iliyolowana ili avae taulo kwa chini, kwa kuwa hakukuwa na nguo zingine hapo za ziada tokea walipoiacha nyumba hii.

Baada ya kumaliza kuvua boxer, kuvaa taulo kiunoni, na kurudi, alimkuta Harleen akiwa ameketi vile vile huku ameibana mikono yake kwa viganja ili asitiri baridi aliyohisi. Akaenda usawa wa sehemu aliyovulia nguo zake na kutoa simu kwenye suruali ili atazame muda. Akakuta ni saa 12 jioni na dakika kadhaa tayari.

Dylan alijua wazi kuna njia nyingine ya kumsaidia Harleen ili apate joto kiasi, lakini akawa anahofia labda rafiki yake angechukulia vibaya. Alitaka kupendekeza kwamba, aketi naye karibu, kisha amkumbatie ili miili yao itokeze joto ambalo lingesambaa kadiri ambavyo muda ungekwenda. Lakini kujua kwamba hawakuwa wamevaa nguo zozote isipokuwa taulo tu, kulimtia wasiwasi kiasi. Ila bado Dylan aliona haingefaa kumwangalia tu, kwa hiyo akaona ajaribu kutoa wazo hilo. Akamfata pale alipokuwa na kuweka simu yake pembeni, kisha akamwangalia.

"Aam... Harleen..." akaita.

Harleen akamtazama.

"Nina wazo. Unaonekana kuhisi sana baridi. Vipi tuki... cuddle? Najua inaweza kuwa inappropriate, but... nataka tu kusaidia," akamwambia.

Harleen akatabasamu na kusema, "Haina shida. Let's do it."

Dylan akafarijika na kumfata alipoketi kisha kukaa karibu yake. Akazungushia mikono yake kwenye mwili wa mtoto na kuubana vyema kwenye wake ili watengeneze joto. Dylan alihisi jinsi Harleen alivyokuwa wa baridi, hivyo akawa anasugua-sugua ngozi yake pia kwa kiganja ili kuleta joto haraka.

Baada ya dakika chache, Harleen akasema, "Umeniita kwa jina langu... nimependa."

Dylan akatabasamu na kusema, "Ila ujue ni gumu sana kutamka. Napendelea binti-mashavu."

"Ahah... Napenda ukiniita hivyo pia," akasema Harleen.

Zikapita dakika chache tena za ukimya, na sasa Harleen, ambaye alikuwa bado amelalia kifua cha Dylan, akajisawazisha kidogo na kukunja miguu kwa kupiga nne, kitu kilichofanya sehemu kubwa ya paja lake kuelekea kiunoni ionekane. Dylan akawa anayaangalia mapaja ya Harleen jinsi yalivyoonekana kuwa laini na manono, naye akaachia tabasamu kama kawaida. 

Harleen akanyanyua uso kidogo kumtazama machoni jamaa na kukuta analiangalia paja lake. "Enjoying the view? (unaufurahia huu mwonekano?)" akamuuliza huku akitabasamu kwa mbali.

"Ahahah... Nilikuwa nahakikisha uko sawa. Dakika chache nyuma ulionekana kama unataka kufa," Dylan akamwambia huku anamtazama usoni.

"Ndiyo, nilikuwa nakaribia."

"Yeah, ndiyo ujue sasa jinsi gani wazo lako halikuendana hata kidogo na hali ya hewa."

"Ahahah... sikusema ni wazo zuri. Nilisema tu itaburudisha. Na huwezi sema haijaburudisha."

"Hapo siwezi kubisha."

"Halafu pia umepata kuona sehemu kubwa ya mwili wangu. Si ndiyo ulichopendaga sana kufanya zamani?"

"Kumbe ndiyo lilikuwa lengo lako?"

"Ahahah... hapana. Sikufikiria kufanya hivi mpaka tulipofika hapa. Nilichotaka mwanzoni ilikuwa kupaona hapa, pamoja nawe. Nimepitia mambo fulani magumu huu mwaka mmoja uliopita, so nilihitaji kufanya jambo fulani wild for a change," akasema Harleen kwa hisia.

"Pole dear. Nimejionea pia baadhi ya wanawake ambao huwa wanapitia nyakati ngumu maishani, angalau wewe una pesa, wenyewe hata hawajui watalisha nini watoto wao. Maisha yako tofauti kwa watu mbalimbali, na najua haifai kulinganisha watu kwa kuwahukumu jinsi wanavyoonekana kwa nje tu. Unapopitia wakati mgumu kama hivyo, unapata kujua kuwa kuna wakati utahitaji kuituliza nafsi na kusonga mbele... ndivyo maisha yalivyo. Najua hata wewe mtoto wa Beatrice unaweza, tena sana. Na kitu kizuri hata zaidi ni kwamba unakuwa mrembo mara mia kila unapokuwa happy," Dylan akamwambia kwa hisia pia.

Harleen akanyanyua uso wake na kumwangalia tena jamaa. Alionekana kutaka sana kumwambia jambo zuri kwa kuwa uso wake ulionyesha furaha.

"Asante. Maneno yako mazuri sana," akasema Harleen.

"Siyo kama wewe," Dylan akamwambia kichokozi.

"Unajua ni kwa nini nilikuwa na hamu ya kutaka kuja huku?" Harleen akauliza.

"Ndiyo, niambie."

"Well, mbali na kutaka kuiona tu nyumba hii, ni kwa sababu nilitaka kuwa pamoja nawe sana. Sikuzote tokea tulipokuwa wadogo nilifurahia sana kuwa karibu yako. Na ijapokuwa tumeishi mbali kwa miaka mingi, bado ninaweza kuhisi upendezi wako uliokuwa nao kunielekea upo. Wewe ni mtu mmoja ambaye unapendezwa nami kwa jinsi nilivyo, kwa kuwa wanaume wengi wanachoangalia kwangu ni pesa, na sex," Harleen akafunguka.

Sehemu hii ilijawa na msukumo mkubwa wa kihisia (tension) baada ya Harleen kunena hayo. Dylan alikuwa amemwelewa vizuri sana, na asingekaa kuigiza kwamba hakujua kihalisi mtoto alimaanisha nini. Akamwangalia kwa hisia sana, huku wimbi kubwa la hisi za kimahaba kumwelekea Harleen likitembea mwilini mwake kwa kasi mno.

"Yaani Harleen... sijui hata nisemeje," akasema Dylan.

Harleen akajinyanyua taratibu kutoka kifuani kwa Dylan na kumwangalia usoni vizuri zaidi. Dylan aliweza kuona jinsi Harleen alivyoonyesha hamu kubwa ya kimapenzi kumwelekea, hivyo akaifata midomo yake polepole na kuibusu taratibu kwa juu. Midomo yao iligandiana kwa nguvu, kisha wakaifungua na kutoa ndimi zao kwa wakati mmoja na kunyonyana kimahaba sana. Ilikuwa denda laini, ya taratibu, iliyojawa na mahaba ya hali ya juu huku wakiwa wamefumba macho yao kusikiliziana.

Hisia walizojengeana hapa zilikuwa nzuri ajabu, nao wakaendelea kwa dakika chache zaidi.


★★★★★★★★★

 ITAENDELEA 

★★★★★★★★★

Previoua Next