Reader Settings

DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!


★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA TANO

★★★★★★★★★★★


"Boss, amefika," sauti ya mwanaume ikasema.

"Mwache aingie ndani," akajibu mwanamke.

Mwanaume huyo akatoka, kisha akaingia mwanaume mwingine ndani ya chumba hiki akiwa amevaa mask usoni. Huyu alikuwa ni Killmonger. 

Mwanamke huyu alikuwa ni Queen, yule yule mwanamke mzungu aliyetaka sana kumfanya Killmonger awe mpiganaji wake ambaye alitaka kumtumia mpaka nje ya nchi. Sasa akawa hapo kwenye chumba cha Queen, kama ofisi yake ya sehemu hii, akimtazama kwa mkazo sana. Queen akaachia tabasamu huku akiwa ameketi kwenye kiti chake, na pembeni yake walisimama mabaunsa wawili, huku nyuma ya Killmonger akisimama mwanaume yule aliyemruhusu kuingia.

"Welcome... my favourite Tanzanian fighter (karibu.. mpiganaji wa kitanzania nayempenda sana)," Queen akamkaribisha Killmonger.

Jamaa akawa anamtazama tu kwa hisia kali sana.

"Ulikuwa kwenye hiatus... watu wameku-miss. Nafurahi umeamua kurudi," Queen akasema.

"Bosco yuko wapi?" Killmonger akauliza kwa mkazo.

"Oh... kwani ninaishi naye?" Queen akauliza kikejeli.

"Sina muda na michezo yako Queen. Naomba uniambie Bosco yuko wapi," Killmonger akasema kwa ujasiri.

Queen akanyanyuka polepole na kuanza kumfata Killmonger taratibu. Alikuwa amevaa nguo ndefu na nyepesi sana yenye kuubana mwili wake, huku nywele zake akiwa ameziachia kwa nyuma na usoni akipendeza kwa kupaka lipstick nyekundu mdomoni. Akamsogelea Killmonger mpaka usoni na kuanza kumwangalia kama anamtathmini.

"Dy..lan. Una jina zuri," Queen akamwambia kwa madaha.

Killmonger akatambua kwamba alikuwa amepatikana haswa. Queen alitambua jina lake sasa, na bila shaka alijua hilo kupitia Bosco. Ujumbe aliotumiwa wakati yuko na Harleen kwenye gari ulikuwa kutoka kwenye simu ya Bosco, lakini aliyeutuma alikuwa Queen. Alikuwa amemwambia ikiwa anamjali rafiki yake, basi angekutana na Queen ili wayajenge, la sivyo Bosco angeumizwa.

"What do you want?" Killmonger/Dylan akauliza.

"Acha kujifanya kama hujui ninachotaka already. You make me lose a lot of patience man. Why are you so stubborn? Ninakupa offer nzuri, unakataa. Nahitaji kujua wewe unachotaka ni nini hasa hapa kwenye hii Fight Club. Ikiwa hupigani kwa ajili ya pesa tu, what is it that you are really after, huh?" Queen akamuuliza.

"Queen, jambo hili halipaswi ku-escalate namna hii. Mimi... ndiyo sipigani kwa ajili tu ya pesa, niko kwenye haya mashindano kama kujifurahisha tu," Killmonger akasema.

"Kujifurahisha? Are you kidding me?" Queen akamshangaa.

"Ni ngumu kuamini ndiyo, lakini ni kweli. Najua wengi lengo lao ni kupata pesa, lakini kwangu huwa ni njia nzuri tu ya kushusha misongo. Sina tatizo na yeyote ninayepigana naye. Simjui, hanijui. Tunaingia arena tunapigana punch mbili tatu, basi... hivyo tu," Killmonger akaeleza.

Queen akacheka sana. "Mbona umekuwa mpole ghafla? Kiburi chote kimeenda wapi?" akamuuliza.

"Bosco yuko wapi Queen? Tafadhali ninakuom..."

"Don't tafadhali me!" Queen akamkatisha kwa ukali.

Killmonger, yaani Dylan, akawa kwenye hisia za kuudhika sana. Alimwangalia Queen kwa mkazo mno, akijitahidi kuzuia hasira yake ili acheze sambamba na mchezo wa mwanamke huyu mpaka ahakikishe Bosco yuko salama.

"I'm not the type of a person who takes no for an answer (Mimi siyo aina ya mtu ninayepokea hapana kama jibu)," akasema Queen.

"Queen please jaribu kuelewa. Iko nje ya... yaani..."

"Acha kujing'ata, kuwa kama mwanaume basi!" Queen akasema.

Killmonger/Dylan akatulia kidogo, kisha akamshika kiunoni na kumvutia kwake kwa nguvu, akiubana mwili wake na wa mzungu huyo. Wale mabaunsa wakajaribu kumfata Killmonger ili wamdhibiti, lakini Queen akanyanyua mkono wake kuwazuia, naye akaachia tabasamu la hila kumwelekea Killmonger. Kisha, akatumia mkono wake kuibandua mask ya jamaa kutoka usoni pake, na kwa mara ya kwanza akauona uso wa Dylan kikamili. 

Queen alipendezwa na sura ya kijana huyu, na alishangazwa kiasi kwa kuwa baada ya kuweza kumwona vizuri alitambua alikuwa kijana mdogo tu, lakini alikuwa amekwishawaaibisha wababa watu wazima kwenye mapigano yote aliyofanya. Dylan alijua kwamba Queen alipenda masuala ya kibabe-babe, ndiyo maana akachukua hatua hii ya kumbana kwake.

"Let's make a deal (tufanye makubaliano)," Dylan akasema.

Queen akaachia tabasamu huku anamwangalia mdomoni, kisha akasema, "Break it."

"Wherever you are holding Bosco, let him go, on one basis. I fight someone of your choice, and if he wins... I go with you. But if I win... you forget this bullshit once and for all (Popote ulipomweka Bosco, mwachie, chini ya jambo moja. Nipigane na mtu yeyote unayetaka, na ikiwa atanishinda, basi nitakwenda nawe. Lakini nikishinda.. usahau kabisa huu upuuzi wote," Killmonger akasema.

"Ahahah... wazo hilo ni rahisi sana, just poppin' in your head right? Well no, sikubali," Queen akasema.

Kisha akajitoa kwenye mwili wa Killmonger/Dylan kwa nguvu na kumwangalia kwa hisia kali.

"Kama kweli unataka kumwokoa rafiki yako, utapaswa upigane na watu watatu leo... na ukiwashinda, ndiyo nitakupa mtu wako. Fair enough right?" Queen akasema.

"Lakini Queen... hakukuwa na haja ya kufanya haya... hauoni ni kama unapoteza muda? Wako wengi wanaojua zaidi yangu... watafute... mimi nina maisha ya..."

"Blah, blah, blah, blah, blaaah... I don't care. Get your ass in that pit... then we'll see (...sijali. Nenda kwenye ulingo huko ndiyo tutaona)," Queen akamwambia kwa njia iliyoonyesha hakujali.

Dylan alikuwa na wakati mgumu hapa. Hakujua Bosco yuko wapi, na alijua mwanamke huyu kwa kiasi kikubwa alikuwa mwenye kiburi sana asiyetaka kushindwa, hivyo angefanya lolote ili kutimiza lengo lake. Kupigana na wanaume watatu ambao hakujua wangekuwa nani kuliifanya akili yake itambue kuwa bila shaka Queen alipanga mambo kwa njia fulani ili kuhakikisha anashindwa, lakini akajiweka sawa kifikira na kumkubalia Queen jambo hilo. 

Queen akaondoka, naye Dylan/Killmonger akaongozwa na mabaunsa wale mpaka kwenye chumba cha kupasha mwili kabla ya pambano. Kwenye mtandao huo ambao pambano lilirushwa, iliwekwa wazi kuwa usiku huo Killmonger angepigana na watu watatu, siyo wote kwa wakati mmoja, ila mmoja baada ya mwingine. Mashabiki wengi wa mchezo huu walifurahi sana na kuanza kumwaga pesa nyingi za kubashiri pambano hilo; Killmonger akipewa kipaumbele kuwa angewashinda wote. 

Dylan alijiandaa vyema na kwa nia moja tu akilini mwake; kushinda. Alihitaji kupambana kwa ustadi wa hali ya juu ili kuwachengua wote ambao angepigana nao, na ili kumtoa rafiki yake kutoka mikononi mwa mwanamke huyo.


★★


Ilipofika saa 6 kamili usiku, pambano la kwanza likaanzishwa. Killmonger, yaani Dylan, alikuwa anapambana na mtu aliyejiita Kumalija. Ijapokuwa jina hili lilikuwa la mtu (😁), yeye tokea mwanzoni alilitumia kama la sifa, siyo la kwake kihalisi. Alikuwa mwanaume mwenye mwili mdogo kiasi cha kumfikia Dylan, naye alivaa mask nyeupe yenye sura ya katuni anayecheka. Alifahamika kupigana kwa staili ya 'boxing' mara nyingi, na aliwahi kushinda mapambano kadhaa kipindi cha nyuma. Hii ilikuwa ni mara yake ya pili kupigana na Killmonger; mara ya kwanza walipopigana Killmonger alimshinda.

Kengele ikagongwa, na pambano likaanza. Mwanzoni wote walikuwa makini sana kukwepa mapigo ya mmoja na mwenzake lakini baada ya muda Killmonger aliweza kupata njia za kumwingizia Kumalija maumivu sehemu za mwili zenye udhaifu. Wakati huu kiukweli Dylan alipigana kwa umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha anashinda, na ikawa hivyo. Alimshinda baada ya kama dakika 20 hivi, naye akamnyanyua na kumpa mkono wa amani, Kumalija akimpa pia kuonyesha 'peace.' Wakati huu Dylan hakupigana kwa njia ya masihara hata kidogo, kwa kuwa alijua usalama na uhuru wa rafiki yake ulitegemea ushindi wake hapo.

Baada ya hapo akafata mpiganaji mwingine aliyefahamika kama Jiwe. Alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya Killmonger, naye alivalia mask nyeusi yenye sura ya kondoo. Ilikuwa ngumu kumtia maumivu usoni kwa kuwa kiziba uso chake hicho kilikuwa kigumu, lakini Killmonger alikuwa amewahi kumshinda kipindi cha nyuma, kwa hiyo hii ilikuwa mara yao ya pili kupambana pia. Killmonger akampa mkono wa amani kabla hawajaanza kupigana, naye Jiwe akaupokea kukubali. Kisha pambano likaanza. 

Pigana, pigana, pigana. Jiwe angalau aliweza kumtia maumivu sehemu kadhaa Killmonger, lakini bado ustadi mwingi wa Killmonger ulimshinda jamaa. Pambano lilichukua dakika 30 hivi, kwa kuwa kila mmoja wao hakutaka kukubali kushindwa, lakini mwishowe Killmonger akashinda. Fujo zilijaa kwenye mtandao huo baada ya Killmonger kufanikisha matarajio ya wengi. Alikuwa anahisi uchovu na maumivu sehemu za mwili wake, lakini akajikaza kiume kwa ajili ya pambano lililofuata.

Hazikupita dakika nyingi na mpambanaji mwingine akaingia. Huyu alijiita "The Crusher," naye alijulikana sana kwa kupigana kwa mtindo wa kutia maumivu makali kwenye miili ya wale aliopigana nao. Yaani kila mara alipopambana ilibidi mpambanaji mwenzake awe amekuja na daktari pembeni! Hakuwa amewahi kupigana na Killmonger, kwa hiyo hii ndiyo ilikuwa mara yao ya kwanza na watu walikuwa na hamu kubwa ya kuona nani angeibuka mbabe kati yao. 

Killmonger akampa mkono wa amani The Crusher, lakini jamaa akaupiga pembeni kwa dharau. Hivyo Dylan alijua angepaswa kupigana kwa uhodari wote maana huyu mtu bila shaka hakuelewa neno amani. Queen, alikuwa ni mdhamini wa The Crusher pia. Kabla ya pambano hilo kuanza, alikuwa amemwita pembeni mpiganaji huyo na kumwambia ahakikishe kwa hali na mali anashinda, naye jamaa akamwambia asihofu hata kidogo. The Crusher alivaa kiziba uso chenye rangi nyekundu kilichoyaacha macho na mdomo wake wazi. Alikuwa na mwili uliolingana na wa Killmonger, ila alimzidi urefu kiasi.

Baada tu ya kengele kugongwa, papo hapo The Crusher akamfata Killmonger kwa kasi sana na kumrukia kwa nguvu kisha kumtandika kwa ngumi usoni. Killmonger hakuwa ametarajia kasi hiyo, na kutokana na uchovu aliohisi alianguka chini. The Crusher alionyesha hataki mchezo hata kidogo kwa kuwa alimfata na kuanza kumpiga ngumi nyingi hapo chini kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake bila kupumzisha. Kwa ustadi, Killmonger akaigeuza nguvu ya The Crusher na kumsukumia upande aliokuwa ameegamiza mwili wake, kisha akajinyanyua huku akihisi maumivu. The Crusher hakuwa aina ya mpambanaji aliyetaka kumpumzisha adui, alipenda kupigana kwa kasi na kutumia nguvu nyingi aliporusha mapigo yake.

Killmonger alikuwa anahitaji utulivu wa kiakili ili apigane vizuri, lakini The Crusher hakumpa hiyo nafasi. Kila sehemu Killmonger aliyoenda tayari angekuwa hapo, na hili likafanya aanze kupoteza mwelekeo. Kama ni sehemu ambayo Dylan aliumia sana, basi ilikuwa ni kwenye ubavu wake wa kushoto. Alijitahidi kutoonyesha kwamba ameumia hapo ili adui yake asipakazie fikira, na kila mara alipoangushwa chini na kuulizwa na mwamuzi pembeni ikiwa alitaka kuacha, angekataa, na The Crusher angeanza kumshushia kipondo tena.

Ilifikia hatua Killmonger alihisi hasira sana kwa kuwa alitambua kwamba huyu jamaa alipigana namna hiyo kwa maagizo ya Queen. Aliwaza atumie njia ipi ili amzingue huyu bwege, na njia moja aliyofikiria ambayo hakuwa ameitumia bado ni ile ile aliyotumia sikuzote, yaani, capoeira. Alikuwa amelala chini, hivyo akajinyanyua kwa mtindo wa kulewa-lewa na kuanza kuupeleka mwili wake huku na huku kama anacheza muziki. 

The Crusher alicheka kwa dharau kwa kuwa alijua mtindo huu wa Killmonger ndiyo uliopendwa na wengi, lakini kwa wakati huu aliona usingemsaidia chochote. Akamfata na kumrukia, lakini Killmonger akajiviringisha chini na kunyanyukia upande mwingine. Kila mara The Crusher alipojitahidi kumvaa jamaa, Killmonger alitumia ufundi mwingi sana wa sarakasi ili kumkwepa na mara nyingine hata kumpiga kidogo hapa na pale.

Queen alikasirika sana baada ya kuona Killmonger ameanza kuugeuza mchezo kwa faida yake, naye akasimama alipokuwa ameketi na kupaza sauti kumwelekea The Crusher akisema, "Finish him!"

Kwa kutiwa hamasa hiyo na boss wake, The Crusher alianza kumfata Killmonger kwa kasi zile zile kama mwanzoni, lakini Killmonger akawa ameshazizoea; yaani alijua jamaa angekuja vipi, hivyo akawa anamchenga na kumpiga kwa ufundi sana, hasa kwenye miguu. Kihalisi Dylan alikuwa anajitahidi sana kusitiri maumivu yake aliyoyahisi, na sasa akaanza kuona The Crusher amechanganywa na mitindo yake ya kupigana. 

Hivyo, kwa werevu Killmonger akamsubirishia wakati ambao The Crusher alianza kumfata tena, kwa kuwa jamaa alikuwa amezoea tu kwamba Killmonger angemkwepa, wakati huu Killmonger akafanya kama anapiga shuti la mpira kwa nguvu huku mwili wake ukizunguka hewani mara mbili akiwa amejikunja, na alipojikunjua akamfumua The Crusher teke la usoni lililofanya jamaa ashtue mshipa wa shingo yake kwa nguvu baada ya kukigeuza kichwa kwa kasi kutokana na pigo hilo!

The Crusher alidondoka chini na kutulia hivyo hivyo tu, na baada ya mwamuzi kumwangalia, akathibitisha kuwa jamaa alikuwa ameumia sana, hivyo wakaita daktari hapo amhudumie. Killmonger alikuwa amekaa chini, akipumua kwa uchovu mwingi huku akikaza meno yake kusitiri maumivu ya kichwa na ya mwili. Baadhi ya wadhamini waliokuwepo hapo walianza kumpigia makofi, huku kelele za mashabiki mitandaoni zikisikika wakimshangilia mwanaume. 

Dylan akanyanyua uso wake kumwelekea Queen, nao wakatazamana kwa sekunde kadhaa, huku baadhi ya watu wakija kumsaidia jamaa anyanyuke. Yeye kutokuwa na mtu wa kumdhamini hapo ilimaanisha kwamba hakuwa na daktari endapo angehitaji kupoza maumivu, na kiukweli hakuhitaji daktari kwa kuwa sikuzote alijiamini vya kutosha kujua kwamba angeshinda tu. Na sasa hata baada ya pigano na watu watatu akawa ameshinda. Watu hao wakampeleka mpaka kwenye chumba kimoja na kumketisha, kisha wakaanza kuhudumia sehemu walizojua aliumia sana. Alishangazwa na jambo hili kwa kuwa hakutambua ni nani aliyewaagiza wafanye haya. 

Ndipo baada ya dakika kadhaa mlango wa chumba hicho ukafunguliwa na Queen kuingia akiwa na mabaunsa wake nyuma. Akawaambia wote waliomsaidia watoke na kuwaacha humo, nao wakatii, kisha akamsogelea Dylan na kumtolea mask yake usoni. Akamwangalia jinsi alivyokuwa ameweka sura iliyoonyesha uchovu, huku damu ikionekana kuvuja puani na ikitoka mdomoni pia. Akachukua kikaushio na kuanza kumfuta taratibu huku Dylan akimwangalia tu.

"Once again... you've proven that I was right about you. You are very talented (Kwa mara nyingine tena umethibitisha nilikuwa sahihi kukuhusu. Una kipaji sana)," akasema Queen kwa sauti ya chini.

"Bosco.... yuko wa..?" Dylan akauliza kivivu.

"Dont worry. He is fine," Queen akasema.

Kisha akatoa ishara ya vidole kwa mabaunsa wake, na mmoja akatoka nje ya chumba hicho.

"Nilifanya kila jambo kuhakikisha unashindwa... but you're just so stubborn, ain't ya? (...lakini wewe ni mgumu sana eti?)" Queen akauliza.

"Queen.... I know you're powerful. But I have the right to choose what I wanna do with my gifts. I... I DON'T do this for money. I... (Queen..najua una nguvu sana. Lakini nina haki ya kuchagua ninachotaka kufanya na zawadi nilizonazo. Sifanyi hii kitu kwa sababu ya pesa. Nina...)"

"I understand," Queen akamkatisha.

Dylan akabaki kumtazama kivivu tu. 

Ni hapa ndipo Bosco akaingia pamoja na yule baunsa, akionekana kuwa nzima kabisa. Akaanza kumwangalia Dylan hapa na pale na kumpa pole.

"I'm so sorry bro... nimekusababishia haya yote," Bosco akamwambia.

"Niko sawa. Vipi wewe? Hawajakuumiza hawa?" Dylan akamuuliza.

Queen akacheka na kutikisa kichwa chake.

"Hamna. Walinifungia tu... kwenye chumba, na kuniacha humo masaa machache," Bosco akasema huku anamwangalia Queen kwa hofu kiasi.

"Una moto mwingi sana ndani yako Dylan ambao niliona ni kama unapotea tu bure huku. Wenzako wanapata pay nzuri, lakini najua kama ungekubaliana na wazo langu ungepata nyingi zaidi. Najua pia kwamba pesa zote ambazo umepata toka umefika huwa unampa Bosco ili azigawe orphanages... ahahah... who does that I mean?" Queen akasema.

Dylan akaendelea kumwangalia kwa hisia makini.

"You are special. I just... wanted to help make it so your talent doesn't go to waste (Wewe ni wa kipekee. Nilitaka kusaidia tu ili kipaji chako kisiwe cha kazi bure)," Queen akaeleza.

"Na ili upate pesa nyingi kupitia kwangu," Dylan akasema.

"Ahahah... yeah," Queen akajibu.

Dylan akasimama huku amejishika ubavuni. "So what happens now? (Kwa hiyo nini kinafuata sasa?)" akauliza.

Queen akatabasamu, akamsogelea Dylan usoni na kulamba shavu lake kidogo, kisha akamwambia, "Nenda ukaoge... Killmonger."

Dylan akaachia tabasamu hafifu akikumbukia siku ile alipomfanyia Queen hivyo, na hapo hapo Queen akaondoka pamoja na mabaunsa wake.

"Oy Dylan... nisamehe sana mwanangu. Queen kanichukua tu leo na kuanza kuniuliza vitu kuhusu wewe... nilipokuwa nakataa kusema wakaanza kunipiga mangumi mwanangu halafu wakanifungia kwenye...."

"Bosco usijali, hao ni washamba tu. Mechi zote tatu nimeshinda, kwa hiyo hakikisha hiyo hela... nusu uniletee... sss aagh..."

"Dylan, hauko sawa. Twende hospitali," Bosco akasema kwa kujali.

"Agh... hamna. Me na... kuna sehemu naenda kwanza," Dylan akasema.

"Sa'hivi saa tisa kasoro Dylan... unaenda wapi?"

"Siwezi kurudi home nikiwa hivi. Nitaenda sehemu nyingine kwanza."

"Lakini..."

"Usijali kuhusu mimi Bosco. Wewe fanya kama nilivyokwambia," Dylan akasema.

Baada ya hapo, akaelekea pamoja na Bosco mpaka kwenye gari lake kule nje. 

Sehemu hii, kama mtu angefika kwa mara ya kwanza na kuingia, angedhani ni jengo dogo la michezo ya kamari (casino), lakini kwa ndani zaidi ndiyo kulikokuwa na sehemu ile ya mapambano, iliyofichwa vyema. Sikuzote wamiliki (kutia ndani Queen) walihakikisha hakuna mtu yeyote ambaye hakuwa na kibali cha kwenda hapo aweze kupita. Dylan, akisaidiwa na Bosco, akaingia ndani ya gari lake na kuketi kimaumivu, lakini akajikaza tu na kuliwasha ili aondoke. Wote hawangeweza kutambua kwamba Queen alikuwa ndani ya gari lake pembeni akimwangalia sana Killmonger wake huyo.

Dylan akaliondoa gari hapo na kurudi mpaka kwenye ile nyumba yake tena, alikotoka na Harleen muda fulani uliopita usiku huo. Alifika hadi ndani na kwenda chumbani, ikiwa ni usiku wa saa kumj sasa, naye akajivuta polepole mpaka bafuni na kujimwagia maji. Akarejea chumbani na kujilaza kitandani kiuchovu sana. Shughuli kali ya mara mbili pamoja Harleen, pambano dhidi ya watu watatu wenye nguvu, jumuisha na njaa vilikuwa vimemfanya ahisi kutojiweza sana kwa wakati huu. Akalala tu hapo huku akiyazoea taratibu maumivu aliyohisi, kisha usingizi ukamjia.


★★★


Alikuja kuamka saa mbili asubuhi, lakini kutokana na kuhisi usingizi mwingi bado, aliendelea kulala mpaka saa sita mchana. Akaamka na kujivuta taratibu, akihisi maumivu sana sehemu ya ubavu wake, miguuni, mikononi, na kichwani pia. Akajikongoja hivyo hivyo mpaka bafuni/chooni na kukojoa. Kisha akajimwagia maji kwa zaidi ya dakika 15. Alitoka na kujikausha, na kwa kujikaza akavaa nguo zake na kuichukua simu. Alikuta 'missed call' nyingi kutoka kwa watu kadhaa, hasa mama yake. Harleen alikuwa amemtumia jumbe nyingi pia za upendo bila kujibiwa. Dylan akaona ampigie mama yake kwanza.

"Dylan! Uko wapi? Tokea jana... kwa nini haupokei simu?" Jaquelin akalalamika upande wa pili.

"Nilipatwa na dharura..."

"Dharura gani?"

"Aam... ni mambo fulani tu nafatilia. Niko nje ya mkoa," Dylan akasema.

"What?! Yaani unaondoka bila taarifa Dylan... una matatizo gani? Unajua kuna mambo huku yanakuhitaji halafu unafanya hivyo kweli?"

"Najua mama... samahani..."

Jaquelin alishangaa kiasi. Hakutarajia Dylan angemwomba samahani kwa kuwa alimzoea kuwa mtu asiyekosa sababu ya kujitetea.

"Dylan... uko sawa?" Jaquelin akauliza kwa kujali.

"Yeah... nipo sawa, nitarudi ndani ya siku chache. Nipe tu update za mambo yatakayotokea... we'll be in touch," Dylan akamwambia.

Jaquelin akabaki kimya tu, kama kuhisi kulikuwa na tatizo upande wa Dylan maana hata sauti yake haikuwa kwa jinsi alivyoizoea. Akaona amkubalie tu bila kumuuliza sababu ya kuwa huko, kisha akakata simu. Dylan akamtafuta na Harleen, akimwambia pia kwamba dharura yake ilimpeleka nje ya mkoa na angerudi siku chache baadaye, na mrembo akimjibu kwa kumwambia kwamba angem-miss sana hivyo angepaswa kujitahidi kuwahi kurudi. 

Baada ya hapo, Dylan alijitahidi kutoka na kwenda kutafuta dawa za kuituliza misuli yake, naye akajinunulia na chakula pia ili ale kuongeza nguvu. Akaendelea kujiuguza mwenyewe kwenye nyumba yake hiyo kwa siku chache, bila yeyote kujua yuko hapo na mambo aliyoyapitia.


★★★


Hii ikawa ni wiki ya pili kupita tokea mara ya kwanza Dylan alipojiunga kwenye kampuni ya baba yake, na mambo yalikuwa yameanza kwenda vizuri sana. Washiriki wengi wa bodi ya kampuni na wafanyakazi kwa ujumla waliona jinsi mawazo mengi ya Dylan yalivyowaletea faida. 

Uingizaji wa teknolojia za hali ya juu hapo ulisaidia sana kurahisisha kazi nyingi, na pia Dylan alikuwa ameagiza vifaa vingi vya ulinzi zaidi viwekwe maeneo yaliyozunguka kiwanda cha kampuni kama camera, kengele za hatari (alarms), kuweka taa kubwa eneo la nje zenye kuzunguka kwa ajili ya usiku, na makontena magumu ya kutunzia vifaa; kwa kuwa kulikuwa na wizi uliofanywa wa vifaa uliosababisha kushuka kwa viwango bora kwenye masuala yao ya ujenzi. Wengi walimpongeza sana Gilbert kwa mambo haya mazuri, lakini yeye alizielekeza sifa zote kwa mwana wake tu.

"I can't believe this!" akasema Mr. Bernard kwa sauti ya juu, huku akiwa ametupa rundo la vitabu chini.

Alikuwa kwenye chumba fulani, sehemu fulani, wakati fulani, pamoja na MTU fulani. Kulikuwa na hali yenye mkazo sana ndani ya chumba hiki.

"... halafu mimi kipanyabuku kile kinakuja kunifanyia zengwe hili? Hapana... haiwezekani. Yaani siamini hata inawezekanaje hako katoto kameweza kuleta haya mambo haraka hivyo... katakuwa kametumwa, siyo siri!" Mr. Bernard akaendelea kulalamika, akimwambia huyo mtu.

Mtu huyu alikuwa ameketi kwenye sofa moja huku ameshikilia glasi yenye wine mkononi, naye akanywa kidogo na kuendelea kuwa kimya tu.

"Sa' hivi wameleta hadi surveillance equipment za hali ya juu... haitakuwa rahisi kuiba vifaa pale. Board members wameanza kufurahishwa na Gilbert tena, sasa hivi mambo yanaenda kuharibika," Mr. Bernard akalalamika.

Mtu huyu akawa anamwangalia tu bila kusema lolote. 

Mr. Bernard akamsogelea karibu. "Mbona husemi lolote? Kumbuka kwamba letu ni moja, na matatizo haya lazima tuyasuluhishe sote. Ukikaa kimya haisaidii kitu," akamwambia.

"Kwa hiyo kichwa chako bado kina tope sana kiasi kwamba hujui la kufanya?" mtu huyu akamuuliza Mr. Bernard kwa kejeli.

"Tunafanyaje? Ili kisasi chako kitimie, na ili mimi hatimaye niichukue kampuni, ni lazima tumwangushe Gilbert now. Mambo yalikuwa yameanza kuwa advantageous kwetu, lakini sasa..."

Mtu huyu akanyanyua kiganja chake kumkatisha Mr. Bernard.

"Nikumbushe maneno ambayo huyo kijana alisema mara ya kwanza kufika kwenye kampuni," mtu huyu akamwambia.

"Hivi kweli unaniambia ma..."

"Yaseme!" mtu huyu akamkatisha kwa ukali kiasi.

Mr. Bernard akashusha pumzi na kumwambia, "Alisema kwamba tunaangalia sana tatizo badala ya njia za kulitatua."

"Huoni kwamba ndiyo unachokifanya sasa hivi?" mtu huyu akamuuliza.

"Lakini tutafanya nini sasa? Methali hazisaidii," Mr. Bernard akasema kwa mkazo.

Mtu huyu akatoa picha fulani na kuiweka mezani. Ilikuwa ni picha ya Dylan. Mr. Bernard akamwangalia kwa makini.

"Hiki... ndiyo kitu kinachompa Gilbert nguvu. Na ili ashuke, ni lazima nguvu hiyo itoweke," mtu huyu akasema.

Mr. Bernard akatafakari kidogo, kisha akauliza, " Unamaanisha... tum...?"

Mtu huyo akaachia tabasamu la hila na kuichukua glasi yake yenye wine, kisha akaanza kuimiminia picha hiyo. Kwa kuwa wine ilikuwa na rangi nyekundu kiasi, ilionekana kama damu imeifunika picha hiyo, na hapo Mr. Bernard akawa ameelewa mtu huyu alichomaanisha. 


Dylan angepaswa kufa!


★★★★★★★★★

 ITAENDELEA 

★★★★★★★★★

Previoua Next