Reader Settings

DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!


★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA SABA

★★★★★★★★★★★


"Ulijuaje hilo?" Dylan akauliza kwa utulivu.

"Me ni daktari Dylan. Walijitahidi kuficha origin ya tatizo kwa sababu nisizozijua, lakini kwa kuangalia tu jinsi thrombocytopenia ilivyokuwa severe mwilini mwake, nilitambua haraka," Harleen akasema.

"Dah, madaktari nyie na hayo madude yenu sijui thomborositepainia, huwa mnayawekaje vichwani?" Dylan akauliza kiutani.

Harleen akacheka kidogo kisha akasema, "Samahani, its a force of habit."

Dylan akatulia kidogo, kisha akasema, "Ndiyo, uko sahihi. Mama alikunywa sumu... lakini mpaka leo sijajua ilikuwa ni kwa nini."

"Pole Dylan..."

"Ahah... asante. Unajua... ukweli ni kwamba bado niko nyumbani kwa sababu nahofia huenda hata akaingiwa na mood swing inayoweza kusababisha atende kwa njia mbaya kama kipindi hicho... ijapokuwa siwezi kumwangalia muda wote lakini angalau kuwepo pale kunanipa ahueni. Mara nyingi nilipokuwa Brazil, niliwaza sana ingekuwa vipi kama... ingetokea mama angekufa kipindi hicho halafu sikuwa nimekaa naye kwa muda mrefu vile. Kwa hiyo sasa hivi najitahidi kufidishia muda huo," Dylan akaeleza kwa hisia.

Harleen akasogeza mdomo wake kwenye mdomo wa Dylan na kuanza kumpiga busu ya faraja.

Wakaendelea kudendeshana kwa sekunde chache, nao wote wakasikia simu ya Harleen ikiita kutokea sehemu ya sebule. Dylan akaivunja busu taratibu na kumwambia Harleen angemfatia simu yake pamoja na zile juice ili wanywe, lakini Harleen akawa anakataa na kumng'ang'ania ili waendelee na mapenzi yao. Dylan akasisitiza kuifata simu kwa kuwa iliendelea kuita karibia mara saba, hivyo alijua huenda ingekuwa muhimu. Hatimaye akafanikiwa kumkimbia mrembo huyo na kwenda kuifata akiwa bila nguo, na alipoichukua ilikuwa ikiita huku jina la aliyepiga likisomeka "Ray."

Akarejea kwa Harleen na kumpa huku anamwambia ni Ray ndiyo anapiga. Harleen alikuwa amejilaza kwa pozi lenye kuamsha hisia za mwanaume endapo angemtazama kwa uvutio lakini baada tu ya Dylan kusema jina "Ray," akaketi vizuri na kwa umakini akaichukua simu yake. Dylan yeye akawa anatabasamu tu kwa furaha, naye Harleen akatoa tabasamu la kujilazimisha, kisha Dylan akaelekea sebuleni tena. 

Harleen akapokea simu yake lakini alizungumza kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba hata Dylan hangeweza kujua ikiwa alipokea simu. Mwanaume akarudi akiwa na zile juice mikononi na kupanda nazo kitandani, na hapo Harleen akaagana na aliyekuwa akiongea naye kisha kuiweka simu pembeni.

Dylan akampa juice moja, naye akabaki na moja, kisha wakagongeana glasi na kuanza kunywa taratibu huku wanatazamana kwa hisia. Kisha kwa utundu, Dylan akaisogeza glasi yake yenye juice karibu na kifua cha Harleen ambacho kilikuwa wazi, kisha akakimiminia juice kidogo iliyolowanisha kifua chake kwa michirizi. 

Harleen alishtuka kiasi na kuachama mdomo wake, naye Dylan akacheka tu. Kisha mrembo akaiweka juice yake pembeni na kuichukua ya Dylan pia na kuiweka pembeni. Dylan bila kuchelewa akakisogelea kifua cha bibie na kuanza kukilamba kwa hamu, akizipa umakini sehemu ambazo michirizi ya juice ilipita. Kisha akaanza kuyanyonya matiti yake na kuzing'atang'ata chuchu za Harleen kwa njia iliyompagawisha sana daktari huyu ambaye alikuwa amepandwa upya na mizuka ya kimahaba.

Wawili hawa wakaurudia mchezo wao mtamu; Dylan akimsugua vyema mwanamke huyu kwa zaidi ya dakika arobaini zingine mpaka alipofikia mshindo wake wa tatu wenye nguvu sana, kutokana na usuguaji wa haraka-haraka alioufanya mwanaume huyo mwenye stamina kali. Wote wakawa wameridhishwa na mmoja na mwenzake, na hapo wakalala pamoja na usingizi kuwapitia.


★★


Dylan akawa wa kwanza kuamka baadaye, huku Harleen akiwa amelala pembeni yake kwa kuonekana amechoka. Mwanaume akatabasamu na kumbusu kwenye shavu, kisha akaivuta simu yake Harleen aliyokuwa ameiweka pembezoni mwa kitanda na kuiwasha ili aangalie muda. Ilikuwa ni saa mbili usiku sasa, na wakati anataka kuirudisha alipoitoa, akaona ujumbe fulani kwenye kioo hicho cha simu uliovuta umakini wake. 

Ujumbe huu ulisomeka 'excited for tomorrow my dearest,' yaani 'nina hamu kubwa kwa ajili ya kesho mpendwa wangu wa pekee.' Mtumaji wa ujumbe huo alikuwa ni Ray, naye Dylan akajua bila shaka ni yule yule jamaa aliyepiga muda ule. Hakujua ni nani, lakini akapotezea tu na kuiona kuwa jumbe ya kirafiki kutoka kwa mtu aliyefahamiana na mwanamke huyu. Akanyanyuka na kwenda kujimwagia maji, kisha akarudi chumbani na kuvaa nguo zake. 

Akamwangalia Harleen kwa upendezi sana, ambaye bado alikuwa amelala huku mwili wake ukiwa bila nguo, naye akamsogelea kitandani hapo na kumfunika vizuri kwa shuka. Akarudi sehemu ya sebule na kuchukua peni na karatasi kutoka kwenye daftari dogo, kisha akaandika ujumbe mfupi wa kumuaga mrembo huyo na kuuweka mezani. Aliona ni bora amwache apumzike, kwa sababu yeye alihitaji kwenda sehemu fulani haraka.


★★


"Okay sawa. Hapana, iko ofisini... nikifika kesho nitaituma mapema wala usijali. Yeah... kila jambo liko safi kabisa. Okay, asante sana. Kwa heri..."

Huyu alikuwa ni Dylan akiongea na mtu fulani kutokea upande mwingine wa jiji kwenye simu kuhusu masuala ya kazi. Alikuwa akiendesha gari bado baada ya kuondoka kwa Harleen, na sehemu aliyokuwa akielekea wakati huu ilikuwa ni kule mgahawa wake ulipokuwa. Alihitaji kwenda kuangalia mambo yako vipi kwa kuwa ulikuwa karibu sana kukamilika kwa kila jambo alilohitaji pale. Hakuwa ameweka simu sikioni wakati anaongea na mtu huyo, bali kifaa cha sikioni kilichounganishwa na simu yake (Bluetooth).

Akiwa anaendelea na safari yake hiyo, alipata kumwona mwanamke fulani pembezoni mwa barabara akitembea kuelekea upande alikoelekea yeye. Mwonekano wa mwanamke huyo haukuwa mgeni sana kwa Dylan, kwa kuwa nguo aliyovaa ilifanana pia na nguo ya yule dada mhudumu wa ule mgahawa walikoenda na Harleen mchana kwa ajili ya chakula. Kwa hiyo alivuta umakini wake kwa sababu moja kwa moja alimfikiria dada yule. 

Dylan akampita na kumwangalia kupitia kioo cha pembeni (side mirror) ya gari, na sasa akawa amehakiki kuwa ilikuwa ni huyo huyo dada baada ya kuuona uso wake kupitia kioo hicho. Akaegesha gari upande huo wa barabara na kusubiri afike usawa wake. Akashusha na kioo cha mlango wa gari, na mwanamke huyu akawa amefika usawa huo.

"Hey..." Dylan akaita.

Mwanamke huyo akasimama na kumwangalia kupitia uwazi wa mlango wa gari. Alikuwa ameweka uso wa kawaida tu, huku Dylan akitabasamu.

"Mambo?" Dylan akamsalimu.

"Poa tu," akajibu huku naye akitabasamu.

"Unanikumbuka?" Dylan akauliza.

Huyo dada akatikisa kichwa kukubali.

"Unaelekea wapi... nyumbani?" Dylan akauliza.

"Ndiyo."

"Aaaa... unaishi maeneo ya huko mbele?"

"Eee."

"Kama vipi panda nikupe lifti maana naelekea upande huo pia."

"A... ahah... hapana... asante. Ninaenda tu hapo mbele kuchukua bajaji..."

"Bajaji ya nini sasa wakati ndinga kali hii hapa?"

"Mhm... kwani nani amekwambia me nina uhitaji wa kupanda ndinga?"

"Oh... samahani... sikumaanisha vibaya. Yaani... nimeona tu nikusaidie kidogo..." Dylan akasema kwa upole.

"Wala usijali. Mimi nitapanda tu bajaji... na... wewe si kuna sehemu unaenda, au?"

"Ndiyo, lakini kama unaelekea upande huo haina shida... nitakupeleka, halafu kwanza... itaku-save hela..."

"Haina shida. Me..."

"Come on, usiwe hivyo. Me sitafuni watu bwana."

Mwanamke huyo akacheka kidogo.

"Ingia twende. Halafu pia... gari langu linanukia vizuri kuliko bajaji... kwa hiyo humu ni bora," Dylan akatania.

Mwanamke huyu akamwangalia kwa sekunde chache, kisha akafungua mlango wa mbele na kuingia ndani ya gari. Dylan alifurahi, naye akaliingiza gari barabarani tena na kuendelea na mwendo.

"Utakuwa unanielekeza eti?" Dylan akamwambia.

"Kwani unanipeleka hadi nyumbani?"

"Sawa tu, kwa kuwa umeniomba."

"Ahahah... wewe ni mtu wa wapi?" dada huyo akauliza.

"Kwa nini?"

"Unavyoongea... hiyo lafudhi siyo ya kitanzania."

"Ahahah... Me mbona mtanzania? Mzawa kabisa."

"Kabila gani?"

"Hayo masuala huwa sina habari nayo kabisa," Dylan akasema.

"Mhm..." dada huyo akaguna na kutazama mbele.

"Jina lako ni nani?" Dylan akauliza.

"Niambie la kwako kwanza."

"Ninaitwa Dylan."

"Aaaa... sawa."

"Na wewe unaitwaje?"

“Naitwa Fetty," akajibu.

"Oooh... msukuma eeh?" Dylan akatania.

"Hapana. Kwa nini umefikiri me msukuma?"

"Well... jina lako hilo bila shaka limetolewa kwenye Fatuma kama sikosei," Dylan akatania tena.

"Ahaaah... Kwa hiyo wooote wanaoitwa Fatuma ni wasukuma?"

"Ndiyo navyojua. Labda kama mambo yamebadilika sasa hivi lakini..."

"Ingia hapo hivi," Fetty akamkatisha ili kumwelekeza pa kuelekea.

"Kwa hiyo umefanya kazi pale kwa muda mrefu?" Dylan akauliza.

"Siyo sana," Fetty akajibu kifupi.

"Sawa."

Dylan alikuwa ametambua mwanamke huyu alikuwa mwenye utu fulani wa kivyake sana. Alitaka kujua mengi kumhusu, na hili lilichochewa na jinsi walivyoangaliana leo wakati wapo kwenye ule mgahawa.

"Unakaa na wazazi nyumbani?" Dylan akauliza.

"Hapana, nimepanga," Fetty akajibu.

"Aaa... okay. Nilipenda jinsi ulivyokuwa unaniangalia leo pale unapofanyia kazi, na sijui ni kwa nini..." Dylan akasema.

Fetty akamwangalia na kuachia tabasamu. Dylan pia akatabasamu baada ya kuona amemfurahisha binti.

"Nilifikiri ni kama vile hukutosheka na maji yaliyonimwagikia kwa hiyo nikahisi labda unataka kuniongezea," Dylan akatania.

"Ahahahah... hamna hata. We' umeona vibaya," Fetty akakanusha.

"Mmmm hamna bwana, nilikuona vizuri kabisa..."

"Kwani hupendi kuangaliwa?"

"Nisingetabasamu ikiwa ningekuwa sipendi."

Fetty akatabasamu na kuangalia mbele.

"Kwa hiyo... ndo' sipati jibu au?" Dylan akauliza kichokozi.

"Mwenzangu nayefanya naye kazi pale alikuwa anakusifia sana... anasema wewe mzuri," Fetty akajibu.

"Hahah... kwa hiyo ukawa unaniangalia sana kwa ajili yake au?"

"Hamna. Alikuwa anataka nimsaidie ili mwongee maana alikuwa anaona aibu... na pia alikuwa anamwogopa yule dada uliyekuja naye."

"Hivi kweli... yaani kashaniona niko na mtu mwingine halafu anakushurutisha uongee nami... kwa nini asingefanya hivyo yeye mwenyewe? Anaogopa nini wakati hii nchi huru bwana?"

"Kata kona hapo hivi... Me mwenyewe nilimwambia anajisumbua tu maana mnaonekana ni watu wenye hela na... yule ni mke wako sijui?" Fetty akasema.

"Hapana... siyo mke wangu."

"Ni girlfriend?"

"Mmmm... hatujafikiria kuweka mambo kati yetu kwa njia hiyo rasmi zaidi lakini ni mtu wangu wa karibu sana."

"Sa' si ndiyo girlfriend au?"

"Ahahah... ndiyo. Ukisema kwa njia hiyo ni kweli."

Fetty akaangalia chini na kusema, "Ni mzuri."

Dylan alihisi kitu fulani. Yaani ni kama Fetty alikuwa anaficha jambo lililohusiana na yeye baada ya kumwambia ana girlfriend, hivyo akaona amchokoze kwa utundu.

"Ndiyo ni mzuri... lakini siyo kama wewe."

Fetty akageuka na kumtazama Dylan kwa makini, huku jamaa akiangalia mbele tu kwa utambuzi wa kwamba binti alikuwa anamwangalia. Akajua bila shaka maneno hayo yalimwingia mtoto kwa njia yenye kusisimua. Akamgeukia pia, na wote wakaangaliana machoni kwa sekunde chache.

"Fetty..." Dylan akaita.

Fetty akaendelea tu kumwangalia.

"...tumekaribia kufika au bado?"

Baada ya Dylan kuuliza hivyo, Fetty akawa kama ameshtuka kutokana na kuzubaa.

"Ai... simama, tumepapita," akasema kwa uharaka.

Dylan akasimamisha gari huku akitabasamu. Fetty akashuka ili arudi kwa miguu, naye Dylan akashuka pia na kumwahi.

"Wewe vipi... mbona faster hivyo?" akamuuliza.

"Aa... asante sana. Nimefika tayari ni hapo tu hivi naingia," Fetty akajibu.

"Sa ndo' unaondoka hata kuaga hamna jamani?"

Fetty akabaki kumwangalia tu usoni.

"Ahahah... usiniogope Fetty. Mimi nataka tu tuwe marafiki. Sijui ni kwa nini, lakini napendezwa nawe sana."

"Aliyekwambia nakuogopa nani?" Fetty akauliza.

"Sasa kinachokufanya ukimbie ni nini?"

"Nilikuwa nawahi..."

"Siyo tabia nzuri," Dylan akajifanya kaudhika.

"Sawa. Nisamehe," Fetty akasema.

"Nipe namba yako ndiyo nitakusamehe," Dylan akamwambia huku anatabasamu kwa utundu.

Fetty akatabasamu pia na kuanza kumtajia namba zake. Dylan akaziandika, kisha akamshukuru na kumwacha aelekee kwake. Akarejea kwenye gari na kuanza kuelekea kwenye mgahawa wake akijihisi furaha fulani ambayo ilichochewa sana na mwanamke huyo mwenye kuvutia.


★★★


Siku iliyofuata, Dylan alikwenda kwenye kampuni kama kawaida kwa ajili ya kazi. Sasa alikuwa anafurahia zaidi kuwa ofisini kuliko mwanzo, kwa kuwa mambo mengi aliyofanya yalikuwa yanaleta matokeo mazuri aliyotarajia, na hata ingawa wengi walimsifia, hakujigamba kwa kiburi. Ilipofika mida ya mchana, alimpigia simu Harleen mara kadhaa lakini hakupokea. Akamtumia ujumbe kuwa alitaka kwenda kupata chakula kwenye ule mgahawa wa jana pamoja naye ikiwa alikuwa na nafasi, au kama alikuwa amebanwa sana basi haingekuwa na shida.

Baadaye, Harleen alimjibu kwa ujumbe kuwa hangeweza kwa kuwa alibanwa sana leo, hivyo wangeenda siku nyingine pamoja. Dylan alipomuuliza ikiwa angepata nafasi ya kukutana baadaye zaidi, Harleen alikanusha na kusema haingewezekana kwa leo, na angemjulisha endapo angepata nafasi. Dylan kama Dylan hakuhisi chochote kwa njia mbaya, akamuaga tu na kuendelea na mambo yake, kisha akaondoka kuelekea kwenye ule mgahawa.

Kichwani kwake aliwaza kwenda pale hasa ili kumwona rafiki yake mpya, Fetty. Hakuwa amemtafuta kwa simu tokea usiku wa jana alipoipata namba yake, kwa hiyo aliwaza pia kwamba angetafuta nafasi ya kuongea naye kidogo. Alifika pale na kwenda moja kwa moja mpaka mezani, kisha mwanamke fulani akaja alipo, naye akiwa ni muhudumu wa hapo.

"Ungependa kupata chakula gani kaka?" akamuuliza.

"Ningependa uniitie Fetty tafadhali. Asante," Dylan akajibu.

Mwanamke huyo akashangaa kidogo, lakini akaona tu atii ijapokuwa halikuwa jibu alilotegemea. 

Sekunde kadhaa zikapita, naye Fetty akaonekana akija upande wa Dylan. Dylan alitabasamu kwa furaha, naye Fetty akashindwa kujizuia kutabasamu. Kijana alimwangalia jinsi alivyokuwa na mwili mzuri sana, na wakati huu Fetty alikuwa amevaa T-shirt ya kijani na suruali ya jeans ya samawati (blue) yenye kubana ambayo ilichoresha hips zake vyema. Akafika hapo karibu na kumsalimu.

"Mbona kimya?" Dylan akamuuliza.

"Unamaanisha nini?" Fetty akauliza pia.

"Hujanitafuta kwa simu!"

"Aliyechukua namba si wewe? Ningekutafuta vipi wakati hukunipa yako?"

"Shida ndiyo hiyo... kwa nini hukuniomba?" Dylan akauliza kimasihara.

Fetty akacheka kwa chini na kutikisa kichwa. Dylan akatabasamu pia.

"Unahitaji chakula gani?" Fetty akamuuliza.

"Ish... yaani chakula kinauliza nahitaji chakula gani? Mhudumu katoka hapa sasa hivi nimemwambia aniletee chakula, kimefika tena kinaniuliza nataka chakula gani!" Dylan akatania.

"Hivi wewe..." Fetty akashangaa huku anatabasamu.

"Ahahahah... au hujui kwamba wewe ni chakula?"

"Acha mambo yako. Nina... kazi za kufanya, niambie basi..." Fetty akaomba.

Dylan alipendezwa sana na ustaarabu wa Fetty. Akamwambia chakula cha kawaida tu, kisha Fetty akamfatia. Wakati Fetty anarejea nacho, Dylan alipigiwa simu na Bosco, ambaye alimjulisha kwamba kuna mpiganaji ametoa 'challenge' ya kupigana na Killmonger kwa kuweka dau kubwa sana kutoka kwa wadhamini wake. Fetty akamwekea Dylan chakula mezani, naye Dylan akamwonyeshea kwa midomo ishara ya 'asante,' naye Fetty akarudia kazi zake zingine akimwacha Dylan anaongea na simu.

Bosco alimshawishi sana Dylan akubali maana alikuwa na uhakika angeshinda tu, lakini Dylan akakataa na kusema awapige chini. Bosco akamwambia nafasi hiyo iko wazi mpaka kufikia saa nne usiku, hivyo ikiwa angebadili mtazamo wake amshtue tu; na alimsihi afanye hivyo. Dylan alijua jamaa yake huyo alipenda na kujali tu pesa ambazo angepata, hivyo akampotezea na kuendelea na msosi.

Mpaka anamaliza kula, Fetty hakuwa ameonekana sehemu hiyo tena, ikionekana alikuwa anafanya kazi fulani huko nyuma. Hivyo akanyanyuka na kumfata mhudumu mwingine, kisha akampa noti ya elfu kumi na kumwambia ampatie Fetty. Akaondoka na kuingia kwenye gari lake, naye akamtumia Fetty ujumbe huu: Asante kwa chakula, chakula wewe 😉. 

Kisha akaondoka hapo na kuelekea kwenye jengo la mgahawa wake mpya ili kuuangalia.


★★★


Baadaye mwamba alirudi nyumbani, akiwa hana jambo lingine la kufanya kule kwenye kampuni, naye akaanza kufanya mazoezi yake ya viungo mpaka alipotosheka. Akausafisha mwili wake vizuri na kuketi tu chumbani kwake, akipitia jambo fulani kwenye simu. Ilikuwa ni mida ya saa kumi na mbili na nusu jioni sasa, naye akafikiria kumshtua Harleen. 

Lakini wazo bora hata zaidi likamwingia. Kwa nini asiende hotelini kule kabisa ili akamfanyie 'surprise?' Alijua huenda asingemkuta, lakini kama ingekuwa hivyo basi angeenda hospitalini kabisa ili kumwona. Harleen alikuwa ameanza kumwingia vyema Dylan, kwa hiyo akaona hii ingekuwa njia nzuri ya kunogesha mambo kati yao; ijapokuwa mrembo alisema mambo yalikuwa mengi kwa leo, lakini hata kumwona tu ingetosha. Akavaa viatu haraka na kwenda kwenye gari lake. 

Dakika hazikupita nyingi sana naye tayari akawa amefika nje ya Queen Hotel. Akashuka na kuelekea kule juu, akiwa na hamu kubwa sana ya kuona itikio la mrembo wake wakati angemwona ghafla yuko hapo. Kabla hajafika mlangoni kwa Harleen, alipata ujumbe kutoka kwa Fetty, aliyesema asante pia kwa shukrani ya Dylan ya chakula. Dylan akamtumia ujumbe wa utani kuwa hapa alipo anaenda kukamua chakula kingine, hivyo angemshtua baadaye tena. Fetty akakubali, kisha Dylan akaendelea kwenda mpaka kwenye mlango wa mrembo wake. Akaugonga na kusubiri ufunguliwe, akitumaini Harleen yuko ndani, na baada ya sekunde chache, ukafunguliwa.

Ilikuwa ni Harleen, akiwa amevaa kigauni kirefu na chepesi sana kilichoonyesha viungo vyake vya mwili kwa mbali. Alishangaa kumwona Dylan hapo, naye Dylan akawa anatabasamu tu kwa kuwa alitegemea itikio hilo la mshangao.

"D... Dylan..."

Harleen akaita kwa sauti ya chini huku akiwa bado ametoa macho. Dylan akaingia ndani na kumfata moja kwa moja mdomoni mwake, akimpiga denda ya furaha. Harleen alikuwa anaipokea busu ya Dylan, lakini kwa njia fulani kama vile alikuwa anataka kuiepuka. Kisha akajitoa mdomoni kwa Dylan na kurudi nyuma kidogo. Dylan akawa anamwangalia kwa matamanio.

"Dylan... mbona uko hapa?" Harleen akauliza.

"Surprise!" Dylan akajibu kwa shauku.

Harleen akageukia upande wa mlango wa kuingilia kwenye chumba chenye kitanda, kisha akamtazama tena Dylan kwa uso wenye kuonyesha wasiwasi.

"Dylan... now's not a good time... tutaonana kesho..." Harleen akasema kwa sauti ya chini.

"Unamaanisha nini?" Dylan akauliza kwa kutoelewa.

Harleen akageukia tena upande ule na kumwangalia tena Dylan kwa uso wenye hofu. Dylan akaangalia huko pia na kumtazama tena.

"Is there a problem?" Dylan akauliza.

"Aam..." Harleen akashindwa kuongea.

"Oh! Aunty Beatrice yuko hapa?" Dylan akauliza kwa kunong'oneza.

Harleen akawa kama anatikisa kichwa kukubali, na hapo hapo sauti ikasikika ikiuliza, "Harleen, vipi ni nani?"

Dylan alishtushwa na sauti hiyo. Alishtuka kwa sababu ilikuwa ni ya mwanaume ambaye hakutambua ni nani. Akabaki kumwangalia Harleen kwa njia ya kawaida lakini kimshangao, huku Harleen akimtazama kwa wasiwasi mwingi mno.


★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Previoua Next