Reader Settings

DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★


Dylan akamwachia na kumshika usoni kwa viganja vyake, akiwa amesahau kabisa uwepo wa wazazi wake hapo. Camila akaanza kuhofia huenda kijana huyu angesema jambo fulani ambalo lingeleta shida. 

"Aunt Cami.... ni wewe kweli?" Dylan akauliza kwa shauku kubwa.

Gilbert na Jaquelin wenyewe walikuwa wanachukulia hiyo kuwa ni furaha tu ya mpwa kumwona shangazi yake. Camila akaishika mikono ya Dylan taratibu na kuishusha, kisha akatabasamu kwa mbali.

"Ndiyo. Cómo están Dylan? (Uhali gani Dylan?)" Camila akamuuliza.

"I've missed you..." Dylan akasema kwa hisia sana. 

Ijapokuwa lilikuwa jambo la kawaida kwa familia yao kuonyeshana shauku za namna hiyo, wonyesho huu wa hisia wa Dylan uliitia udadasi akili ya Gilbert. Aliona badiliko kwenye uso na sauti ya mwanaye, kwa kuwa yeye pia alikuwa mwanaume alijua vizuri sana jinsi mwanaume anavyokuwa akionyesha hisia zake za moyoni, hata kwa kumwangalia tu usoni. Lakini akahisi labda alimjaji kupita kiasi, kwa kuwa walikuwa ndugu hata hivyo, isingewezekana fikira hizo kuwa sahihi. 

Camila akajitahidi kuzuia hisia zake na kutabasamu kirafiki, huku Dylan akimtazama kwa upendo.

"Ahahah... leo utadeka sana," akasema Jaquelin.

Ni hapa ndipo Dylan akatambua kuwa bado alikuwa amemshika karibu sana shangazi yake, hivyo akamwachia na kurudi nyuma kidogo. 

"Umekuja na mgeni?" Gilbert akamuuliza Dylan.

Dylan akageuka nyuma na kukuta bado Fetty amesimama mlangoni. Alikuwa ameshasahau kabisa kwamba alikuja na rafiki yake hapo! Akamfata na kumwomba samahani kwa kumwacha hapo mwenyewe, kisha akaanza kuelekea waliposimama wengine pamoja naye.

"Shikamooni..." Fetty akawasalimia wakubwa.

Wote wakamwitikia kwa kusema 'marahaba.'

"Mom, dad, aunt, huyu ni rafiki yangu... Fetty," Dylan akamtambulisha.

Watatu hao waliitikia kwa njia tofauti lakini wakaonyesha kwa nyuso zao kuwa wamefurahi kumfahamu. Gilbert kihalisi alifurahi kutambulishwa kwa rafiki ya mwanaye, hivyo tabasamu lake lilikuwa la kutoka moyoni. Jaquelin alitabasamu lakini moyoni mwake hakupendezwa kabisa na Fetty. Camila ndiyo alikuwa amefika tu, na kwa kutegemea historia yake pamoja na Dylan, fikira ya kwanza iliyokuja akilini mwake ni kwamba bila shaka Dylan angekuwa na mahusiano na binti huyo. Alionyesha tabasamu, lakini kwa kiasi fulani moyoni akawa anaumia, bila kujua kwamba kihalisi Fetty alikuwa ni rafiki tu kwa Dylan. 

"Fetty... huyu ni baba yangu, anaitwa Gilbert. Huyu ni mama yangu, anaitwa Jaquelin, na huyu... ni aunt yangu... anaitwa Camila," Dylan akamwambia.

Wote wakamkaribisha vizuri sana Fetty, kisha wakaketi kwenye masofa. Dylan hakuweza kujizuia kumtazama sana Camila. Alihisi kama vile ni ndoto kwamba shangazi yake yuko hapo. Wakawa wanapiga story, hasa kuhusiana na Camila na kisha Fetty.

"Oooh... unamaanisha wewe ni waitress?" Jaquelin akamuuliza Fetty, baada ya kuwa amemwambia kuwa anafanya kazi kwenye mgahawa.

"Ndiyo," Fetty akajibu.

Jaquelin akatoa tabasamu la bandia.

"Umefika saa ngapi aunt?" Dylan akamuuliza Camila.

"Tanzania nimefika juzi," akajibu.

"Yaani wewe... ulikuwa huku siku mbili nzima halafu hata hatukujua!" Gilbert akamwambia.

"Ahah... nilikuwa nataka kuwa-surprise," akasema Camila.

"Na kweli ilikuwa bonge moja la surprise. Yaani kidogo nipae kwa furaha!" akasema Jaquelin, na wote wakacheka.

"Naona pamebadilika sana huku," akasema Camila.

"Hamna hata hapajabadilika, sema ni kwa sababu ulitukimbia kwa muda mrefu sana," akasema Jaquelin.

"Aa... Fetty, unakumbuka nilikwambia nimeishi na aunt Camila Brazil kwa miaka mingi? Ni moja kati ya watu ninaowapenda mno," Dylan akasema.

Camila akamwangalia Dylan kwa makini.

"Aaaa... uliposema aunt Camila mara ya kwanza sikuwa nimetambua ndiyo yule wa Brazil uliyeniambia. Kumbe ndiyo huyu?" Fetty akasema.

"Ndiyo, ameniogesha huyu. Lakini hebu mcheki, kama ndiyo ametoka sekondari tu yaani," Dylan akatania, na wote wakacheka.

Camila alijihisi vizuri kujua kwamba Dylan bado alimwona kuwa wa maana sana kwake mpaka kusimulia kumhusu kwa rafiki zake. 

"Kwa hiyo Fetty, uli... mlikutana vipi na Dylan?" Jaquelin akauliza.

"Alinikuta napigwa na vibaka, akawapiga wote wakakimbia. Ndiyo kuanzia hapo tukawa ma-best," Dylan akatania.

"We' naye, nilikuwa naongea na wewe?" Jaquelin akamwambia.

Wote wakacheka, kisha Fetty akasema, "Tulikutana mgahawani."

"Kwa hiyo kumbe hamjuani muda mrefu sana?" Jaquelin akauliza tena.

"Siyo muda mrefu sana," Fetty akajibu.

"Okay. Mgahawa unaofanyia kazi... ni restaurant au kwenye hotel?" Jaquelin akauliza.

"Mama... mbona hupumziki?" Dylan akamwambia Jaquelin.

"Si ndiyo tunajuana au?" Jaquelin akasema.

"Ni mgahawa wa kawaida tu. Uko maeneo ya hapo mjini," akajibu Fetty.

"Mmmm... sawa. Nimeshangaa kidogo Dylan kusema kwamba ana rafiki. Yeye siyo mtu wa marafiki kabisa. Najiuliza ulifanya vipi mpaka akakuona kama 'rafiki,'" akasema Jaquelin.

Fetty alianza kuingiwa na wasiwasi sasa, huku Gilbert na Camila wakiona wazi kwamba Jaquelin alikuwa anataka kumchanganya binti wa watu. Dylan alikerwa kiasi na njia ya mama yake ya kumchokonoa rafiki yake.

"Mom... mbona hivyo? Kwani kuna ubaya nikiwa na rafiki?" Dylan akauliza kwa hisia.

"Sijasema hivyo. Pole Fetty kama nimekufanya uhisi vibaya. Nachomaanisha ni kwamba, najua Dylan hanaga time na mtu, anapenda sana kuwa kivyake. Watu wachache anaofahamiana nao ni watu wa kuwa nao tu, huwa hawaoni kama marafiki. Urafiki mlio nao ni urafiki wa kirafiki au wa kimapenzi?" akauliza Jaquelin kwa udadisi.

"Ni marafiki tu wa kawaida," akajibu Fetty.

"Nafurahi kwamba unatengeneza marafiki sasa. Itapendeza ukiwa unawaleta muwe mnajifurahisha," Gilbert akamwambia Dylan.

"Halafu wakiichoma nyumba moto?" Jaquelin akauliza.

Swali lake lilimfanya Fetty ahisi alikuwa anamsema vibaya, kana kwamba kwa kuwa yeye hana pesa sana basi hajui mambo mengi hapo, hivyo angekuwa mharibifu tu. Gilbert na Camila wakatabasamu ili kufanya ionekane kwamba Jaquelin alikuwa anatania tu.

"Usijali mama. Hekalu lako litasimama daima," Dylan akamtania Jaquelin.

"Mhm... una miaka mingapi?" Jaquelin akamuuliza Fetty.

"25," Fetty akajibu.

"Unaonekana mkubwa, ila kumbe mdogo," akasema Camila.

"Ana mwili mnono," Dylan akasema.

Gilbert na Fetty wakacheka kidogo, lakini Camila akamtazama tu Dylan, naye Jaquelin akazungusha macho yake kwa kutopendezwa, lakini hawakumwona. Ni wakati huu ndipo wasaidizi wa kazi wakawa wanaitayarisha meza ya chakula upande mwingine wa sebule, wakiiwekea vyakula mbalimbali vilivyotoa harufu nzuri.

"Ninataka kumweka Fetty awe assistant manager kwenye Dy-Foods Restaurant," akasema Dylan.

Jaquelin akakunja uso kimaswali.

"Die what?" akauliza Camila.

"Ahahah... Dylan amefungua restaurant nzuri sana. Anaiita Dy-Foods, yaani Dylan's Foods," Gilbert akamwambia Camila.

"Wewe! Kweli?" Camila akauliza huku anatabasamu.

Dylan akatabasamu pia na kutikisa kichwa kukubali.

"Wow... hongera sana," Camila akampongeza.

"Ataweza assistancy, au unataka tu kumsumbua mtoto wa watu? Ili akiboronga, uwe na mtu wa kulalamikia," akasema Jaquelin.

"Hamna. Ni ili tumbo lako likikoroga, ukimbilie Dy-Foods kula bamia," Dylan akamtania Jaquelin.

Wote wakacheka, na Jaquelin akachukua mto na kumponda Dylan.

"Ahahah... kutakuwa na bamia kweli?" akauliza Gilbert.

"Ndiyo. Kwa ajili ya mama," Dylan akaendelea kutania.

"Mwone kwanza... halafu unaiita restaurant ya kisasa," akasema Jaquelin.

Baada ya hapo, iliwekwa wazi na Jaquelin kuwa wote waende mezani kupata chakula, nao wakasimama na kwenda mezani pamoja. Dylan akawahi kiti fulani ambacho Camila alidhamiria kuketi, kisha akakivuta kwa ajili yake ili akae hapo bila shida. Wazazi wake walifurahia kuona anamtendea kwa staha sana shangazi yake mdogo, bila kujua kihalisi kuwa kwa Dylan ilikuwa ni wonyesho wa upendo wa dhati kumwelekea Camila.

Wakala chakula pamoja, nao walikifurahia sana kwa kuwa kilikuwa kizuri mno; nyama za kukaangwa za kuku, wali, tambi, mboga za majani, nyama za kukaangwa na kupikwa, juisi, matunda, na vyakula vingine vya ajabu-ajabu tu wanavyokulaga watu wa kishua. Dylan alijitahidi kumfanya Fetty ajihisi huru, huku moyoni akisubiri kwa hamu kubwa sana kuja kuweza kuwa peke yake na Camila ili waongee.

Mara ya mwisho Dylan kumwona shangazi yake ilikuwa ni 2018, kipindi kile alipotoka Brazil na kwenda Ulaya pamoja naye baada ya mama yake kupelekwa huko kwa ajili ya kupandikiziwa ini lingine. Walionana kifupi tu, kwa kuwa Dylan alirudi Brazil tena kuendelea na chuo, na hawakushiriki mambo mengi sana, kwa kuwa ilikuwa kipindi kilichomvunja Dylan moyo. Baada ya hapo, hakuonana naye tena, kwa kuwa Camila alibadili makazi na hata mawasiliano kati yao yakawa yamekata. 

Ijapokuwa umri wake uliongezeka kufikia wakati huu, bado Camila alionekana kama mwanamke mdogo kutokana na urembo wake na kujitunza vizuri. Dylan alitaka sana kujua maisha yake yalikuwaje, ikiwa alipata mtu mwingine labda, na kama alimkumbuka pia. 

Baada ya kuwa wamemaliza kupata chakula, waliendeleza maongezi kidogo, kisha Fetty akasema alihitaji kwenda kwake sasa. Walimuaga vizuri, huku Jaquelin bado akiwa na roho ya kwa nini, kisha Dylan akaongozana naye mpaka kwenye gari lake na kuanza kumpeleka kwake sasa.


★★


"Yaani nilete chakula mpaka kwenye kampuni yenu?" akauliza Fetty, wakiwa mwendoni bado.

"Yeah. Ole wako uache," Dylan akamwambia.

"Ina maana... ahah... nichukue chakula, nikilete huko... kweli unashindwa kuagiza huko huko? Mwanzoni ulikuwa unakula wapi?" 

"Haijalishi. Nataka kula chakula chako asubuhi kabla sijaenda kule. Kwa hiyo lazima uniletee."

"Utanilipa milioni, si eti tajiri?"

"Ahahah... usiwaze. We' panda tu bajaji kesho ulete."

Walikuwa wakiongelea kuhusu safari yake Dylan ya kesho. Alikuwa amemwambia Fetty ampelekee supu ya nyama na chapati zao ofisini kwake kabla hajaondoka, kwa hiyo Fetty alishangazwa kidogo maana ilikuwa mbali. Lakini Dylan alimwahidi kumlipa mara mbili, na hiyo ilikuwa biashara nzuri kutoka kwa mteja, kwa hiyo Fetty akakubali.

"Umepaonaje kwetu?" Dylan akauliza.

"Ni pazuri. Wazazi wako wana hela sana," Fetty akasema.

"Yeah. Baba ndiyo King, mama ndiyo Queen, mimi ndiyo Prince," akasema Dylan.

"Yaani unavyopenda kujisifu wewe!" 

"Ahahahah... facts. Ndiyo ukweli."

"Lakini nyumba yenu kubwa sana. Hamna ndugu zenu wengine wanaishi hapo?"

"Hapana. Sisi... masuala ya ndugu huwa hatuyaleti hapo home."

"Kwa nini?"

"Stress. Kama wanakuwa wanahitaji msaada, tunawasaidia wakiwa huko huko, masuala ya kuanza kubanana siyo poa."

"Asa' hapo mnabananaje?"

"Ahahahah... aaah... me naona wazazi wangu wako sahihi. Hawapendi kero, kama mimi tu. Na ndugu wengi wanakera. Au nadanganya?"

"Mhm... siyo kwa wote lakini."

"Wee! Wanakera acha. We' mwenyewe hapo unajinyima unapiga kazi unatunza pesa kwa ajili ya malengo yako, halafu kidogo tu unapigiwa simu eti oooh mjomba wako huku amemeza shoka, tuma hela atibiwe..."

Fetty akacheka sana.

"Ahahahah... Sa' unakuwa unajiuliza kwani we' ndo' ulimwambia alimeze ama?" Dylan akasema.

"Ahahahah... ila wewe," Fetty akasema kwa furaha.

"Ndiyo hivyo. Hata mimi stress za hivyo ah aah," akasema Dylan.

"Ahah... mbona wewe unaishi kwenu wakati umri wako mkubwa hata kuweza kuoa?" akauliza Fetty.

"Nimuoe nani? Kila mtu ana mtu... yaani dah! Siyo poa."

"Mhm... wapo walio free."

"Yeah... kuna wakati unapata mtu unafikiri yuko free, kumbe yuko free-mason... yaani kwenye chama... kila kona ana watu," Dylan akatania.

"Ahahahah... hivi wewe unaishiwaga maneno kweli?" 

"Mpaka nipigwe busu ya mdomo."

"Mh... hmm... haya bwana."

"Ahahah... aam... niko nyumbani hapo kwa sababu ya mama. Kuna wakati aliumwa sana, na mimi nilikuwa mbali muda mrefu mno. Kwa hiyo niliporudi hii miezi michache iliyopita niliona ni vyema nikiwa karibu naye zaidi. Lakini ningeamua kukaa kivyangu ningefanya hivyo. Nina nyumba yangu mwenyewe," akaeleza Dylan.

"Kweli?"

"Yeah."

"Umeijenga lini wakati haukuwa huku?"

"Ilikuwa yetu zamani. Tuliishi kwenye hiyo mpaka baadaye nilipoondoka na wazazi wangu kujenga hii nyingine. Kwa hiyo baba akaiandika ile nyingine chini ya jina langu. Naifanyia ukarabati wakati huu."

"Iwe ya kisasa zaidi."

"Ndiyo maana yake."

"Ahahah... Na yenyewe ni kubwa eeh?"

"Nitakupeleka siku moja uione."

"Mhm... nitafurahi."

Dylan akatambua kuwa sauti ya Fetty ilikuwa na aina fulani ya deko aliposema hivyo.

"Vipi msosi uliuonaje?" Dylan akamuuliza.

"Ulikuwa mzuri sana jamani. Yaani natamani ningekuwa nakula kama hivyo kila siku," akasema Fetty kwa shauku.

"Ahahah..."

"Mama yako anaonekana mkali," Fetty akasema.

"Oh... siyo mkali yaani... ni kwamba tu yuko... persistent sana... sijui nitumie neno gani la kiswahili..."

"Usijali, nimeelewa."

"Yeah. Yaani... pole kwa kuwa alifanya uogope. Ndiyo yuko hivyo... mbabe sana," Dylan akamwambia.

"Okay. Nilihisi wasiwasi kidogo. Eti 'au urafiki wa kimapenzi?'"

"Ahahah... alikuwa anafikiri labda unanichuna."

"Ahahahah..."

Fetty alipendezwa sana na Dylan. Alianza kuvutiwa naye hata zaidi wakati huu, kwa kuwa kiukweli alijithibitisha kuwa mwanaume wa aina tofauti sana na wengi aliowajua. Akimtazama mara kwa mara kwa hisia, Fetty aliwaza ni kwa nini ijapokuwa Dylan alimwonyesha upendezi, bado hakumwambia au kufanya jambo ambalo lingemwonyesha anavutiwa naye kimapenzi. Fetty alikuwa na vigezo vyote vya kusemwa kuwa ameumbika, lakini Dylan alimwonyesha staha na heshima sana kama rafiki afanyavyo, na hilo likamhakikishia kwamba hangecheza na hisia zake.

Dylan alimfikisha Fetty mpaka maeneo ya ghetto lake mtoto, kisha wote wakashuka na kutembea mpaka karibu na nyumba ile. Dylan akamtakia usiku mwema, naye Fetty akafanya hivyo hivyo. Dylan akarejea kwenye gari lake na kugeuza ili arudi nyumbani, akimwacha Fetty anatabasamu kwa furaha huku anamtafakari sana mwanaume.


★★


Dylan alifika kwao yapata saa sita usiku, naye akaingia ndani na kukuta ni baba yake tu ndiyo yuko sebuleni; akiwa anajiandaa kupanda juu kwenda kulala. Akamwambia kuwa wanawake walikuwa wamekwishatangulia, hivyo na yeye aende kupumzika pia kwa ajili ya safari yake kesho. Dylan akasema ameelewa, kisha baba yake akaanza kupanda ngazi kuelekea juu chumbani kwake.

Dylan akabaki sebuleni hapo anamtafakari sana Camila. Akahuzunika kwamba hakuweza kuwahi na kuongea naye kidogo, ukitegemea kesho alihitajika kuondoka mapema kuelekea mkoa mwingine wa mbali kikazi, akahofia huenda hata Camila angeondoka na hakupata hata nafasi ya kuyajenga naye. Moyo wake bado ulikuwa na hisia nzito sana kwa shangazi yake, zilizoamshwa kwa mara nyingine tena baada ya kumwona.

Akatoka hapo baada ya dakika kadhaa na kuzima taa zote, kisha akapanda juu na kuelekea chumbani kwake. Alivua nguo zake na kuvaa nguo nyepesi tu, kisha akajitupia kitandani, akiwa bado anatafakari mambo. Camila alikuwa hapo, nyumbani kwao, naye hakuweza hata kuongea naye! Hapana, aliona haiwezekani nafasi hii impite kirahisi-rahisi namna hii. Alihitaji sana kumwona, na sasa kitu kilichokuwepo ni kumfata chumbani kwake alikokuwa. 

Kwa king'ang'anizi alichokuwa nacho Dylan, alipuuzia uwezekano wa kusababisha tatizo kubwa endapo angekamatwa na wazazi wake akiwa chumbani kwa shangazi yake usiku. Aliazimia moyoni mwake kuwa kwa vyovyote vile, iwe isiwe, lazima amwone tu. Akatazama saa kwenye simu yake, na sasa ilikuwa ni saa saba na nusu usiku, na kwake muda huo ulitosha kumwambia kuwa wote wangekuwa wamelala, hivyo angeenda chumbani kwa Camila kimya kimya na kumwamsha waongee.

Akanyanyuka na kuelekea mlangoni, kisha akaufungua na kutoka polepole. Uzuri ni kwamba milango yao haikutoa sauti za kukwaruza, hivyo akanyata taratibu kuelekea upande wa vyumba vya wageni na kufungua mlango wa cha kwanza. Alipoingiza shingo ndani kuchungulia humo, palikuwa na giza, lakini aliweza kuona kwa mwanga hafifu kuwa hakikuwa na mtu kitandani. Hivyo akaufunga na kuelekea kingine.

Alipofungua mlango kidogo, akaona mwanga hafifu wa taa, naye akatambua kuwa bila shaka ulikuwa ni mwanga wa taa ya mezani karibu na kitanda, hivyo akapenya na kuingia ndani, na hapo akamwona Camila akiwa ameketi kitandani. Dylan alisisimka baada ya kumwona akiwa amekaa kwa kuegamia mto huku miguu ameinyooshea kitandani, na night dress alivyovaa ikiishia mapajani. Alikuwa ameshika kitabu, na hilo likamwambia Dylan kuwa bila shaka shangazi yake alikuwa anasoma. 

Camila alikuwa amekunja uso kimaswali, akishangaa baada ya kumwona mpwa wake ndani humo. Mapigo ya moyo yalianza kumkimbia kwa kasi, naye akashuka kitandani na kusimama chini akimwangalia kwa wasiwasi. Dylan akaufunga mlango na kisha akaanza kumfata Camila upesi.

"Dylan... what are you doing in here? (unafanya nini ndani humu?)" Camila akamuuliza kwa mnong'ono. 

Dylan akapotezea swali lake na kumkumbatia kwa wororo. Alikuwa amemkosa sana! Camila hakujua afanye nini, kwa sababu kiukweli mwili na moyo wake vilifurahia sana uwepo wa Dylan hapo, lakini akili yake ikawa inapinga jambo hili. Dylan akamwachia na kumshika usoni kwa wororo huku anamwangalia kwa hisia sana.

"Dylan... you should leave... please (Dylan... unapaswa kuondoka.. tafadhali)," Camila akamsihi kwa kunong'oneza.

Dylan akatikisa kichwa taratibu kukataa.

"Please go. You might get into trouble (Tafadhali nenda. Unaweza kuingia matatizoni)," Camila akasihi tena.

"I don't want to. Me solo te quiero (Sitaki kufanya hivyo. Nakutaka wewe tu)," Dylan akasema kwa hisia.

"Dylan..." Camila akasema huku akihisi udhaifu sana.

Dylan akaifata midomo yake papo hapo na kuanza kuipiga denda laini. Kisha akaingiza ulimi wake ndani na kuanza kuinyonya midomo yake kimahaba zaidi. Camila aliipokea denda hii vyema, akionyesha dhahiri pia kwamba alimkumbuka sana Dylan. Mkono mmoja wa Dylan ukausogeza mwili wa Camila karibu naye zaidi na kuubana, huku mwingine ukiishika shingo yake kwa nyuma alipoendelea kumpa penzi la mdomo shangazi yake. Camila alilegea na kumwachia mpwa wake amdendeshe jinsi alivyotaka, huku hamu ya kimahaba ikiwavaa wote wawili kwa kasi sana. 

Taratibu, Dylan akaiachia midomo yake na kuweka paji lake la uso kwenye paji la Camila, huku wote wakiwa wamefumba macho na kupumua kwa uzito.

"After seeing you earlier... solo me quedo el requerdo de la felicidad intensa que me hiciste sentir (Baada ya kukuona tena muda ule... nilirejewa na kumbukumbu ya furaha kubwa sana uliyonipa kipindi kile)," akafunguka Dylan kwa hisia nyingi.

"Oh Dylan..." Camila akasema kwa sauti yenye huzuni kiasi.

Dylan akaibusu tena midomo yake laini mara tatu, kisha akajitoa usoni kwake na kumtazama machoni. Camila naye akamwangalia, kilegevu sana, akiwa amelikosa sana penzi la kijana huyu; mpwa wake! Lakini kufikia wakati huu mambo mengi yalikuwa yamebadilika sana.

"De que servirán requerdos cuando ya no estés conmigo? (Kumbukumbu zitasaidia nini wakati hauko nami tena?)" Camila akamuuliza.

Dylan akatambua kuwa ni kama shangazi yake alikuwa anataka kumwambia jambo fulani.

"What do you mean?" Dylan akamuuliza.

Camila akashusha pumzi na kumshika usoni kwa wororo. "I'm engaged, Dylan (nina mchumba, Dylan)," akasema.

Dylan akabaki kumwangalia tu machoni shangazi yake. Kwa mambo mengi, alikuwa anafikiria kuwa huenda sababu iliyomfanya Camila aje kwao ilikuwa yeye. Lakini sasa akawa ametambua kuwa mambo mengi mno yalikuwa tofauti. 

Wakati huu Camila alikuwa na mchumba, na kilichomleta nchini huku ilikuwa ni matembezi, lakini pia alikuwa amekuja na mchumba wake kumtambulisha kwa ndugu zake na watu wa jamii yake. Walikuwa wamefikia hotelini juzi, na leo Camila alipokuja kwa kaka yake, alimwambia kuhusu mchumba wake huyo ili kumwandaa kwa ajili ya kuja naye kesho hapo nyumbani. Ni wakati ule Dylan alipompeleka Fetty kwake ndipo Camila aliwaambia Gilbert na Jaquelin kuhusu jambo hilo. Dylan akaishiwa pozi kabisa. Akaitoa mikono ya Camila usoni mwake na kuvishika viganja vyake huku anamwangalia machoni.

"Umepata mchumba?" Dylan akauliza kwa sauti ya chini.

"Ndiyo," Camila akajibu.

"Wow..." akasema Dylan kwa njia ya kuvunjika moyo.

Camila akawa anamtazama kwa huruma.

"Okay... aam... sijui.... nisemeje.... Hongera," Dylan akasema.

Camila akafumba macho na kugeuzia uso wake pembeni, akijikaza asilie.

"Anaitwaje?" Dylan akamuuliza.

"Felipe Matsunaga," Camila akajibu bila kumtazama.

"Ana sura nzuri kama mimi?" Dylan akauliza kiutani.

Camila akacheka kidogo tu kwa chini.

"Unampenda?" Dylan akauliza.

Camila akatikisa kichwa taratibu kukubali bila kumwangalia. 

Yaani ilikuwa ni kama Dylan ni mkubwa kwake, maana Camila alionyesha woga fulani kumwelekea kwa sababu alimjali sana. 

"Sawa," Dylan akasema na kushusha pumzi ndefu.

Ni wazi alikuwa amevunjika sana moyo. Alifikiri mchezo wake wa kimapenzi pamoja na Camila ungeendelea baada ya kumwona tena, lakini bila shaka hii ndiyo ilikuwa tamati ambayo sikuzote alijua ingefika tu. 

Kihalisi, ikiwa Camila angeamua kuendelea kufurahia penzi kutoka kwa mpwa wake hata kama ana mchumba, basi Dylan angekuwa tayari kwa hilo. Lakini kitendo tu cha Camila kumwambia vile, ilimdhihirishia kijana huyu kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwamba Camila aliyachukulia mahusiano yake pamoja na mchumba wake kwa uzito, na hakutaka kum-cheat. Ni kama Camila alimwambia Dylan hivi: Dylan, siwezi kuwa nawe hata kidogo kwa kuwa nina mchumba tayari.

Dylan akaiachia mikono ya Camila na kurudi nyuma kidogo. Camila akamwangalia kwa hisia za huruma, na uso wa Dylan kweli ulionyesha huzuni. Kijana akageuka na kupiga hatua kuurudia mlango, lakini akasita na kusimama. Kisha akamgeukia tena shangazi yake.

"Kwa nini umeniruhusu nikubusu?" Dylan akauliza.

Camila hakutoa jibu, bali macho yake yakaanza kujawa na machozi. 

Dylan akatikisa kichwa taratibu kwa huzuni, kisha akaona ni bora ajiondokee tu. Lakini wakati ameugeukia mlango, akapatwa na machale kuwa kulikuwa na mtu nje ya mlango. Ilikuwa ni kama hatua zinakaribia mlangoni hapo, na kwa kasi sana Dylan akaelekea mlangoni upesi na kuipandisha miguu yake kwa kukanyaga kuta za pembeni, akipanda juu kama vile spiderman!

Camila alishtushwa kiasi na jambo hilo, kwa kuwa hakuelewa Dylan alikuwa na maana gani kufanya hivyo. Akawa anamwangalia jinsi alivyojikaza juu hapo, na hapo hapo mlango ukafunguliwa taratibu. Mapigo ya moyo ya Camila yakaanza kupiga kwa kasi pale alipomwona Jaquelin akiwa amesimama mlangoni hapo, lakini hakuingia mpaka ndani baada ya kumwona Camila amesimama usawa wa kitanda.


★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Previoua Next