ENDELEA.................
"Jina langu naitwa Aami Amadou Mbaye..."
"Hapana hapana hapana huo ni uongo" mtaalamu Qader aliipinga kauli ya mwanaume ambaye alidai kwamba siku ya leo alihitaji yeye amjue ni nani, kwake mara ya kwanza alikuwa anamjua kama Jiti Maalimu afisa usalama wa taifa lakini baadae alikuta mambo ni tofauti na wala hakuwahi kumjua mtu huyo ni nani, kwa mara ya mwisho mwanaume huyu alimsaidia ndani ya kijiji cha KIBETA wilaya ya BUKOBA baada ya mwanaume mmoja ambaye alitambulika kama Joash kuwaua vijana wake watatu hata yeye kupigwa sana wakati ameivamia nyumba ya mzee Philebert alifanikiwa kutoka pekeyake lakini hakuwa na nguvu za kufika mbali baada ya kufika barabarani alidondoka wakati huo alimuona mwanaume mmoja akishuka kwenye gari hakuelewa kilicho endelea mpaka alipokuja kujikuta ndani ya nyumba ya Jiti Maalimu kama alivyo mjua yeye na leo ndiyo ilikuwa siku ambayo aliahidiwa kupewa ukweli wa mambo na kumjua mtu ambaye alidai kwamba yeye pekee ndiye ambaye anaweza kumdondosha chini Zakaria Mansour.
Qader aligoma kwa nguvu sana baada ya mtu huyo kusema kwamba anaitwa Aami Amadou Mbaye, kwake isingekuwa kweli hiyo sentensi ilikuwa ya uongo na alikuwa na uhakika wa kubisha kabisa.
"Wewe hapo mimi unanijua?" Jiti Maalimu aliuliza bila hofu
"Hapana"
"Sasa hizo nguvu za kuanza kunibishia ninacho kwambia unazitolea wapi?"
"Huyo Mzee ambaye umemtaja hapo naijua familia yake na mzee huyo watoto wote na familia nzima iliweza kufa isipokuwa mtu mmoja tu ndiye ambaye alipona sasa haiwezekani nawewe uwe mmoja wao wakati haukuwa mwana familia huo ni uongo tena ni uongo mkubwa" Qader alijiamini sana.
"Hahahahahha hahahahahha sasa kama mtu hata hunijui na bado unabisha ninacho kwambia hii dunia utaweza kuiishi kweli wewe? Una umri mkubwa sana kunizidi ila kiakili wewe ni mdogo sana unaelewa maana ya jina Aami na unajua kwanini naitwa hivyo?"
"Hapana"
"Aami ni jina ambalo asili yake ni ndani ya nchi ya India huko ambalo limetoka kwenye lugha ya Malayalam ambayo ni lugha inayo zungumzwa kwenye eneo ambalo linaitwa Kerala, lina maana ya mpendwa mmoja anaye pendwa" alitulia baada ya kumjibu livyo.
"Sasa hiyo inamaana gani na inahusiana vipi na kile ambacho unakisema wewe?"
"Unahisi kwanini mpaka sasa sijakuua?"
"Hapana"
"Kwa sababu aliye kutuma wewe ni kaka yangu mimi"
"Hey whaaaat?"
"Sudi au Deruwash Amadou Mbaye ni kaka yangu wa damu tumeshea baba"
"Kivipi?"
"Jina langu naitwa Aami Amadou Mbaye mimi ndiye mtoto wa mwisho kabisa wa ile familia, mimi sijazaliwa ndani ya ile familia nimezaiwa nje ya familia. Baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana sio tu ndani ya Senegal na Libya bali karibia Afrika nzima walikuwa wanamtegemea sana kwa usambazaji wa mafuta, kwenye tembea tembea zake za biashara alibahatika kukutana na mwanamke mmoja ambaye asili yake ni mhindi hakuwaza kama ana ndoa alikotoka hisia za upendo wa kweli zilizama kwenye nafsi yake akaangukia kwenye mahaba mazito sana na huyo mwanamke ambaye ndiye mama yangu mzazi mimi hapa. Mimi ndiye mtoto ambaye nilikuwa kipenzi cha baba kwa sababu nimezaliwa pekeyangu yaani mimi ndiye wa kwanza na ndiye wa mwisho kwa mama angu ndiyo maana nilipewa jina la Aami japo ukilifuatilia asili yake ni jina la kike ila mzee wangu alifanya hivyo ili kumfurahisha mkewe na kweli alifanikiwa kwa hilo"
"Mhh mbona dunia ina siri sana, sasa kwanini hakuweza kukukutanisha na ndugu zako wengine ili baadae hata kukitokea tatizo nawewe uweze kujumuishwa kwenye mali ambazo alikuwa anazimiliki yeye?"
"Ungekuwa umezaliwa kwenye familia ambazo mwanaume anakuwa na wake wengi ungenielewa kirahisi Sana, hakuweza kunitambulisha kwa sababu mama yangu hakuwa mkewe kiuhalali wala hakuwahi kumtambulisha sehemu yoyote ile inadaiwa tu kwamba mamlaka za kiusalama zilijua kwamba ana mkewe mdogo wa siri kule Libya ila hilo lipo kwenye vifua vya watu wachache sana. Kuhusu mgao wa mali nadhani mimi ndiye mtoto wake mwenye pesa na mali za kutosha zaidi, hizi familia mara nyingi sana mtoto ambaye huwa ananufaika ni yule ambaye kwao anakuwa pekeyake kwahiyo vitu vingi anapewa yeye tofauti na wale ambao kwao wanakuwa wengi, hivyo mapenzi makubwa yote yalikuwa kwangu ndio maana hata uwekezaji karibia robo tatu ya mali zake zote aliwekeza kwa jina langu maana alijua akipotea hakuna mtu ambaye angeweza kunijali hivyo mimi sio mtu mwenye njaa kabisa"
"Hicho ndicho kitu ambacho kimekupa uhakika wa kupambana na mtu ambaye wewe mwenyewe umesema ni hatari sana kwa sababu ya pesa? Maana umri wako unaonekana bado mdogo sana sasa hayo mambo ya kuwa hatari sana umeyajulia wapi?"
"Unataka kunijua na upande wangu wa pili?"
"Ndiyo"
"Itakuwa ni hatari sana kwa ajili ya maisha yako kama utaufungua mdomo wako mahali popote pale basi huo ndio utakuwa mwisho wako wa kuishi siku hiyo hiyo"
"Najua kuhusu hilo na nina familia ya kuilinda ndio maana nimekuuliza siwezi kufanya kosa kama hilo"
"Ndani ya nchi za umoja wa kisovieti mnamo miaka ya 1954 walianzisha shirika kuu la kijasusi kwa ajili ya usalama wa nchi hizo mpaka lilipokuja kutenguliwa mnamo miaka ya 1991 wakati umoja huo ulipo vunjika. Ukiacha mashirika hatari ya kijasusi kama ISI la nchi ya Pakstan ambalo inadaiwa hata wakati ule CIA wanamtafuta sana Osama Bin La den wao walikuwa wanajua mtu huyo makazi yake yakipokuwa kwa wakati ule, lakini pia shirika kama M16 la Uingereza, pamoja na Mossad, KGB ndilo shirika la hatari na la kutisha zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu, huko kuna watu ambao hawana ubinadamu kabisa na walishajivua hii mioyo ambayo wanakuwa nayo wanadamu wa kawaida tu kutokana na aina ya matukio yao ya kutisha ambayo huwa wanayafanya.
Katika miaka ya 1980's kuna gazeti moja lipatwalo kuitwa TIME MAGAZINE ARTICLE liliwahi kuchapisha na kueleza kwamba KGB ndilo shirika maarufu zaidi kwa ukusanyaji wa taarifa za siri za kiserikali wakiwatumia sana watu ambao wanaitwa double agents,hawa huwa ni kama ndumila kuwili anakuwa huku na huku na ndio hao ambao nchi nyingi kwa sasa ambazo zimejiimarisha sana kiusalama zinawatumia sana kuweza kupata taarifa za mhimu za wapinzani wao kwa kuwalipa kiasi kikubwa sana cha fedha. Miongoni mwa opareshini zilizo ifanya KGB kuanza kuogopwa sana na kuheshimika ni ile ya kuweza kumpindua jasusi mmoja wa kimarekani ambaye aliitwa ROBERT HANSEEN, haikuwa rahisi kuyabadilisha mawazo ya mtu ambaye ameapa kuitumikia nchi yake halafu ni jasusi wa kutupwa mpaka akaja upande wako na kuisaliti nchi yake inahitajika akili kubwa sana kudili na watu wa aina hiyo kwa sababu unaweza ukakuta anakugeuka wewe mwenyewe baadae lakini KGB walilifanikisha hilo kwa kumshawishi huyo mwanaume wakimlipa pesa za kimarekani dola milioni moja na robo pamoja na madini ya shaba ili tu awauzie taarifa za siri "classified information".
Baada ya mwaka 1991 ndipo likaundwa shirika jingine ikiwa ni kama mwendelezo wa KGB ambalo linaitwa Federal Security Service (FSB) japo KGB bado nayo ipo kwa sababu nchi kama Belarus zilianzisha KGB yao pamoja na jamhuri ya kusini mwa Ossetia, haya yote niliyo kueleza nilitaka nikwambie kwamba mimi ni jasusi kutoka ndani ya shirika la KGB ama waweza kuliita FSB kwa sasa" Qader alisikiliza kwa umakini sana maelezo ya mwanaume ambaye alijitambulisha kama Aami Amadou Mbaye ila hii sentensi ya mwisho ilimtisha sana, alijifuta jasho tangu siku nyingi sana amewahi kusikia habari za kutisha sana kutoka kwenye hilo shirika ambalo linapatikana ndani ya nchi ya Urusi (Russia) na makao yake makuu yanapatikana katika jiji la Moscow, alishtuka mno.
"Wewe ni miongoni mwa memba wa KGB?"
"Ndiyo"
"Ni ngumu sana mtu kupewa nafasi ya kuingia kwenye shirika la hatari kama hilo iliwezekanaje mtu wa kawaida ukapata nafasi ya kufika huko?"
"Wewe hapo ndo unaniita mimi wa kawaida?"
"Sijamaanisha hivyo unavyo fikiria lakini sehemu kama hiyo sio rahisi mtu kama wewe kupewa nafasi kama hiyo"
"Unajua ni kwanini nimekwambia mimi pekee ndiye mtu ambaye ninaweza kumdondosha Zakaria Mansour?"
"Hapana"
"Mimi ni binadamu wa kutisha kuliko unavyo niona hapa naongea nawewe, kwenye huu ulimwengu wa watu wenye mabavu sana kuna watu wa aina tatu
1. Wakwanza ni wapiganaji, hawa ni watu ambao wanaipenda michezo ya ngumi, kwao kupigana ni sanaa na huwa hawakubali kushindwa hata kukitokea leo ukampiga basi mpaka azimie au afe ndo utakuwa mwisho wenu wa kupigana na hata akizinduka atakutafuta muweze kupigana tena. Watu wa namna hii wengi wanapatikana sana jeshini wao huwa wanayapenda mapigano kuliko hata wanavyo jipenda wenyewe kwahiyo usishangae siku unapo muona mwanajeshi analilia kwenda vitani.
2. Watu wa pili ni wauaji, hawa huwa hawana muda wa kwenda kupigana nawewe hawa ukiwaona sehemu basi ujue wamekuja kuyachukua maisha ya mtu, baadhi ya majasusi na makomando ndo wanaingia kwenye hili eneo pamoja na watu ambao wanayalinda masilahi yao au wanahitaji maslahi kwa nguvu yoyote ile huwa wanatumika sana hapa. Siku ukimuona komando akiwa kwenye vazi lake mbele yako na amekufuata wewe basi una nafasi ndogo sana ya kuwa hai kwenye maisha yako, ukipata nafasi kimbia na uende mbali sana asije akakufikia pale ulipo ni hatari mno.
3. Viumbe vya ajabu, hili ndilo kundi la hatari zaidi kwenye maisha ya mwanadamu wa kawaida, hapa unampata mtu kama Zakaria na mimi hapa mwenyewe. Hili kundi ni la watu ambao hawafanyi tu mauaji bali wanafanya mauaji ya kutisha na kwa kasi ya ajabu mno. Siku ukija kufanikiwa kuona mtu ambaye ameuawa kwenye mkono wa Zakaria hautakuja kutamani maisha yako yote uje ukutane na huyo kiumbe. Anaua vibaya sana kiasi kwamba hata kama wewe ni mtu wa kazi sana ila kama hauna roho ya paka basi hauwezi kutazama mwili ulioguswa na hilo dubwana au kuuangalia mara mbili unaweza ukawa unaota kila unapo inamisha kichwa chako au mgongo wako kuutafuta usingizi.
Daah nimeishiwa maneno, nadhani unamsikia mwenyewe kijana ambaye Qader alimchukulia mlaini sana kama afisa usalama wa kawaida tu kumbe ni memba wa kundi la kutisha la kijasusi duniani la KGB kwa mzee Putin huko. Sasa unataka kujua aliingiaje huko na amefanikiwaje kuondoka Russia( Urusi) kuja Tanzania na kwanini alijiunga na hilo shirika?.......50 natia nanga tukutane tena wakati ujao.
Wako
Bux the story teller
Chao.
Comments