Reader Settings

 

ENDELEA..............................

"Ndugu yangu umenifanya nianze kuogopa sana kuwa nawewe Karibu naona kabisa maisha yangu kama yapo ukingoni Sina imani Kama hata hapa nitatoka salama maana naona Kama nipo na kiumbe ambacho kimevaa ngozi ya mwanadamu ila hakina uwanadamu wowote ule ndani yake" Qader alinena maneno yake huku akiwa anajifuta jasho mbele ya Aami Amadou Mbaye, alitamani hata kukimbia lakini hakuwa na huo uwezo.

 

"Kwa sasa wewe hapo una vitu viwili vya kukufanya uendelee kuwa hai kwa sababu mimi Kama ningetaka kukuua tangu miaka minne iliyoweza kupita ningeshakuua muda sana. Kitu Cha kwanza hakikisha niliyokwambia na ninayo kwenda kukuongezea kuhusu mimi yanabaki kwenye kifua chako vinginevyo hautamaliza hata dakika tano huo moyo wako wako ukiwa unadunda na huo mdomo wako ukiwa unaweza kuufungua lakini cha pili unatakiwa utafute sehemu ya kujifichia na familia yako narudia tena kama hilo dubwana litarudi kutoka huko liliko na likajua wewe ndiye uliye iua familia yake hizo sekunde ambazo huwa zinaonekana ni chache sana kuifikia dakika moja zitatosha mtu huyo kukupata" Aami alikuwa amampta taalarifa za Zakaria Qader ambaye mpaka muda huo hakuelewa afanye nini.

 

"Unanitisha sana hivyo simuogopi labda serikali kama ikijua uwepo wangu ndo kutakuwa na shida kubwa sana" Qader aliongea akiwa anapiga funda la maji ya baridi.

 

"Kweli wewe akili huna kabisa"

"Kivipi tena"

"Yaani unaiogopa serikali kuliko hicho kiumbe?"

"Yes, siwezi kumuogopa mtu mmoja serikali ina mkono mrefu sana ikiamua kulivalia njuga suala lolote lile"

"Hivi unajua unacho kipngea bwana mdogo?" Aami alikuwa ni mdogo sana kwa Qader ila alimuita bwana mdogo kwa sababu alimzidi kwa kila kitu kuanzia akili na uwezo.

 

"Hilo nina uhakika nalo asilimia zaidi ya miamoja" Aami hakuongea kitu chochote kile aliingiza mkono wake mfukoni akatoa simu yake, aliigeuzia upande wa Qader na kumrushia, kwenye hiyo simu ilikuwa inaonekana video mwanaume mmoja alikuwa anaua watu kikatili mno kwa kutumia nyembe ambazo zilikuwa kwenye pete vidoleni Kisha mwanaume huyo aliutoa upanga wake na kukitenganisha kichwa cha mzee mmoja wa kiarabu kisha akakiokota kichwa hicho na kutoka nacho ndani ya hiyo nyumba video hiyo ikaishia hapo. Qader alifumba macho mwili ulimsisimka sana kwa alicho kishuhudia.

 

"Mhhhh hii dunia imefikia pabaya sana Kuna watu wana moyo wa kufanya hivi kwa wanadamu wenzao?"

 

"Huyo ndiye Zakaria Mansour mwenyewe ambaye ulimi wako unamtaka kiwepesi kama vile unautafuta mkate dukani, hiyo ni video ambayo huwa naishi nayo kwenye maisha yangu yote nitaifuta mpaka siku ambayo nitakutana naye na kuhakikisha nimemuua kwa mkono wangu, huyo aliyekatwa kichwa hapo ndiye baba yangu mzazi AMADOU MBAYE mwenyewe"

 

"Hata Kama alimkosea vipi hakutakiwa kumuua kwa namna kama hiyo sidhani kama hata MUNGU anaweza kumsamehe"

"Mhhhh nawewe leo unamtamka na MUNGU unakumbuka namna ulivyo muua mkewe na mwanae?" Qader alikaa kimya hakuweza kuchangia chochote kile kwa sababu alikuwa anaambiwa ukweli.

 

"Baba yangu ndiye mtu ambaye aliniingiza kwenye kundi hilo la KGB ama waweza kuliita FSB kwa sasa nikiwa bado mdogo sana. Mzee wangu alikuwa anajihusisha na biashara nyingi sana ambazo hazikuwa za halali hivyo alijua wazi kwamba muda wowote ule mamlaka za nchi mbali mbali zitaanza kumtupia jicho kuanza kumfuatilia kwa umakini kwahiyo ili kujilinda alitakiwa kuwa na mtu kwenye hayo mashirika ya kijasusi ambapo angekuwa na uwezo wa kuzipata taarifa mapema sana na akachukua tahadhari.

 

Mpaka leo sijawahi kujua alifanyaje mpaka nikapata nafasi kule maana nilikuwa bado mdogo sana lakini nakumbuka siku moja nikiwa nimekaa na mama yangu walikuja wanaume wawili mama akanipa ruhusa kwamba niondoke nao ni baba amewaagiza kufanya hivyo mimi nilijua naenda kukutana na baba yangu labda lakini haikuwa hivyo nilishangaa nachukuliwa mpaka airport na pale ndipo nilipo anza kuleta vurugu nikitaka kuongea na baba, kweli alipigiwa simu alinambia ni yeye ndiye aliyewapa maagizo huko ninako enda ndiko aliko anaanza kunitengenezea maisha yangu ya baadae, nikiri tu kwamba nilikuwa nilimsililiza sana yule mzee hivyo sikuwa na hofu tena huo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kuingia kwenye hizo kazi za kijeshi. Nilipelekwa kwenye kituo kimoja ambako nadhani mtoto nilikuwa mimi tu wengine umri wao ulikuwa mkubwa, tofauti na nilivyokuwa nimefikiria sikumuona baba wala ndugu yangu yeyote zaidi ya watu ambao walikuwa hata kucheka kwao Kuna hesabika aisee wale jamaa wana roho mbaya, nilizoeshwa maisha mazuri sana hivyo nilianza kulia Kama nipo nyumbani nilipigwa sana siku ile kama vile nimeiba.

 

Baada ya kukaa miaka mitatu ndipo nilikuja kugundua kwamba baba yangu ndiye ambaye alifanya huo mpango wa mimi kwenda huko ikanibidi niwe mpole na nilikuwa nimeshaanza kuzoea nikawa kama nipo nyumbani, tulipewa mafunzo makali sana ya mapigano kwa muda mrefu, kwa siku tulikuwa tunapata saa moja na nusu tu la kupumzika na kula ila muda wote uliobaki tulikuwa tunafanyishwa mazoezi kana kwamba kulikuwa na vita ambayo ilitakiwa kwenda kuipigania. Iliisha miaka saba ndipo rasmi tulipo tambulishwa kwenye hilo shirika la hatari la kijasusi la FSB huko ndiko niliko enda kutolewa roho ya kibinadamu unapewa mtihani wa kumtesa mtu mpaka aseme kwa kutoa kiungo chake kimoja kimoja ndani ya mwili, hilo ni jambo rahisi sana kulisimulia ila ni gumu mno kulifanyia utekelezaji.

 

Nilijikuta nakuwa kiumbe cha hovyo sana kuua ndo yakawa maisha yangu, kutesa watu ikawa sehemu ya maisha yangu, niliua watu wengi sana. Kuna siku tulipelekwa ndani ya maabara kubwa tuliingizwa watu hamsini ila tulifanikiwa kutoka ndani watu watano tu wenzetu wote 45 walifia mle ndani. Tulichomwa sindano za kutufanya mifupa yetu kuwa migumu mno ndio maana mpaka leo nikikupiga ngumi yangu kama wewe ulivyo mlaini hivyo huwezi kusimama tena, baada ya kuchomwa hizo sindano tulipambanishwa kupigana na maroboti na huo baadae ndio tuliambiwa kwamba ulikuwa mtihani wa mwisho kwenye mafunzo yetu yote. Unapigana na mashine na unatakiwa uishinde ikiwa ina kila silaha kwenye mwili wake ambazo zinajitoa zenyewe.

 

Ndiyo nilifanikiwa kutoka japo mwili wangu ulitobolewa sana kwa visu vingi ila ile ndiyo siku ambayo nilichukua muda mrefu zaidi kuisahau kwenye maisha yangu kila nikilala nilikuwa naiota na kuteseka sana, cha ajabu baada ya kutoka kwenye kile chumba kupambana na yale maroboti ndiyo siku ambayo nilikutana na baba yangu akiwa na mama yangu nililia sana siku ile na ndipo baba yangu alipo nisimulia chanzo cha yeye kunileta kule kwamba anawindwa sana hivyo mimi ndiye nitakayekuwa mlinzi wa maisha yake. Ile ndiyo siku ambayo nilithibitisha kwamba hata mzazi akukosee vipi bado atabaki kuwa mzazi tu nilijikuta ile hasira yote imetoka juu yao nikaapa kuwalinda kwenye maisha yangu yote.

 

Tangu pale baba yangu aliishi kwa amani sana kwa sababu yeyote ambae alikuwa anaingia kwenye njia zake nilihakikisha namtoa mapema sana, hakuna adui wa baba yangu ambaye alimaliza masaa 24 jina lake likifika kwenye mikono yangu, nilifanikiwa kuwateka mpaka viongozi wa serikali kwa wale ambao walikuwa wapo kinyume na mzee wangu na hapo akajikuta anaiweka hata serikali kwenye mkono wake, nilikuwa na taarifa za karibia kila shirika la kijasusi duniani hivyo nilihakikisha mzee wangu anakuwa salama pamoja na familia nzima. Mpaka muda huo nilikuwa naweza kufanya kitu chochote kile na kwa mtu yeyote yule hapa duniani, Mimi na wenzangu tulifanya oparesheni nyingi sana zenye mafanikio makubwa Kama vile kuiba mifumo ya ulinzi ya Korea kasikazini pamoja na Uingereza hicho ni kitu ambacho kilitufanya sisi team ya watu watano wote tukiwa majasusi wa kutisha kuheshimiwa na kuogopwa sana ndani ya shirika la FSB hakuna kazi ambayo ingefika kwenye mikono yetu ikashindikana hicho kilitufanya tuhisi dunia hii tumeiweka kwenye mikono yetu na hicho ndicho kilichonifanya nikashindwa mpaka kuilinda familia yangu, sifa ni mbaya sana duniani pale unapo wadharau wanadamu ambao kimsingi hata huwajui vizuri" Aami Amadou Mbaye waweza kumuita Jiti Maalimu alisimulia kisa chake cha kutisha na kusikitisha sana ikamlazimu kutulia kidogo sehemu ambayo ilionekana kumuumiza sana kwenye moyo wake, wakati huo Qader alikuwa amekaa pambeni anahema na jasho likiwa linamtoka kwa wingi wakati humo ndani kulikuwa na kiyoyozi cha kutosha tu kuna binadamu alikiri wazi hawatakiwi kabsa kuwazoea vibaya unaweza ukajikuta upo sehemu mbaya sana.

 

"I messed up" aliongea huku macho yake yakiwa mekundu lakini bado Qader hakuchangia chochote kile alibaki anamtazama tu kwa uoga alikuwa anaogopa kwamba kama angeutumia vibaya mdomo wake kwa namna mwanaume huyo alivyo onekana kuwa kwenye uchungu mkubwa huenda angajipotezeshea sifa ya kuendelea kuivuta pumzi ya bure.

 

"Kuna muda kwenye maisha ukurupukaji huwa unawapa faida sana watu watulivu ambao huwa wanakutazama kila hatua yako ambayo unaipiga, Sina uhakika ila watu ukitaja shirika la kijasusi hatari zaisi duniani huwa wanaitaja KGB huenda ni kwa sababu ya matukio yake ya kutisha sana ambayo huwa yanawekwa wazi ila hii dunia nadhani kiuhalisia hakuna shirika lenye nguvu kuwazidi CENTRAL INTELLIGENCE AGENCY (CIA) ya marekani hili ni shirika ambalo lina nguvu kubwa sana duniani, limebeba asilimia karibia 50+% ya uchumi wa marekani, hawa ndio huwa wanaamua nani atakuwa raisi na nani hawezi kuwa raisi wa nchi kiufupi ni kwamba hawa wakikukataa basi hauna chako tena na usiombe waanze kukufuatilia hata uishi ndani ya bahari wanakukamata.

 

Kuna siku niliwahi kupewa taarifa na mkurugenzi wangu wa FSB yeye alidai kwamba anawaheshimu zaidi ISI ya PAKSTAN kwa sababu ya uimara wao pamoja na Mossad ila nadhani hata yeye haujui mtego ambao upo CIA, CIA wamezoeleka sana duniani kwa sasa ndio maana wanaonekana wa kawaida hata taarifa zao zinaonekana kuwa zipo wazi sana ndio maana baadhi ya watu wanajidanganya kwamba hili shirika kwa sasa limepoteza nguvu ila huo ni uongo na hilo nililishuhudia kwa macho yangu na nafsi yangu mwenyewe. Hili ndilo shirika la kiusalama ambalo kwa macho yako lazima utaona taarifa zao zipo wazi sana ila tukikwambia kazichukue uzilete hapa hauna huo uwezo hata uwe nani hata uwatumie double agents wao huwezi kupata kitu kinachoitwa CLASSIFIED INFORMATIONS (taarifa za siri) kutoka kwao huwa wanaweka taarifa feki Kama mtego hizo ndizo watu wengi huwa wanajivunia kwamba ni rahisi sana kupata taarifa za hilo shirika bahati mbaya ukweli hawawaujui, hili ndilo shirika ambalo lina watu wenye akili zaidi ulimwenguni na ndilo shirika ambalo lina watu makatili wa hii dunia sijawahi kuona, hawa ndio chanzo cha mimi kushindwa kuilinda familia yangu kutoka kwenye mikono ya Zakria Mansour na ndio waliofanya mpaka FSB na KGB wanajua kwamba mimi nilishakufa" Aami alizidi kutoa historia ya kutisha sana mbele ya Qader.

 

"Whaaaaaat umekufa?" Qader alishtuka sana kusikia hayo maneno.

 

Je ni kweli Aami anachosema kwamba CIA ndio shirika linalotisha zaidi duniani kwenye ishu za kiusalama? Je CIA walimfanya nini mpaka anawaogopa sana namna hiyo na alikuwa anafanya nini kwako? Na kivipi CIA ndio wasababishe yeye ashindwe kuwasaidia wazazi wake na kuonekana yeye emekufa?....51 inafika tamati tukutane wakati ujao.

 

Bux the story teller.

 

Chao.

Previoua