SEHEMU YA 198.
The White Queen.
Nyakasura mara baada ya kumuona Hamza amefika , alifuta midomo palepale na kumwangalia:
“Nimesikia hapa kuna farasi , nipeleke basi nikaendeshe?”Aliongea na Hamza kabla ya kumijibu aligida pafu la bia kwanza;
“Farasi wapo upande ule kwenye zizi. Unaweza kwenda na kuchagua mmoja na kumtoa nje , kwanini unataka nikupeleke?”
“Mimi ni mgeni hapa, si sahihi kwa mwenyeji kunipeleka?”Aliongea Nyakasura akiwa hajaridhika.
Hamza alijiambia ni mgeni gani anajikaribisha mwenyewe , lakini kutokana na kuhofia tabia yake aliamua tu kumkubalia.
“Sawa nitakupeleka ukaendeshe”
Nyakasura kusikia hivyo , furaha ilimvaa palepale na kuchukua mhindi wa kuchemsha na kumnyooshea achukue.
“Hivyo ndio inavyotakiwa , malizia na huu muhindi kwanza”
Hamza aliangalia mhindi huo , ingekuwa afadhali ulikuwa haujaguswa ila mwanamke huyo alikuwa amekula nusu na kuubakisha na kibaya zaidi ulikuwa na mate ya kutosha.
“Asante ila nimeshiba sana”
“Mh! Nilikuwa nakujaribu tu , siwezi kuruhusu mtu wa kawaida kama wewe kumalizia nilichoanza kula”Aliongea.
Pembeni Leviathani , Mameni na wengine mara baada ya kuona tukio hilo waliishia kutingisha vichwa vyao tu , waliona ni msichana huyo pekee ndio anaeweza kumuendesha Hamza atakavyo ila sio wao.
Ilibidi wawaache wengine kumalizia kutafuna nyama huku wao wakiongozana mpaka kwenye zizi la farasi
“Mbona wote ni weusi tu , hakuna mweupe?”Aliuliza Nyakasura huku akionekana kutoridhishwa na farasi hao.
“Hawa weusi ndio wazuri sasa, wana damu ya kifalme na ni ghali zaidi kuliko farasi wa kawaida. Wewe ni Nyakasura hivyo unapaswa kuendesha wa hivi , kwanini unataka kuendesha kulingana na rangi yake?”
Nyakasura mara baada ya kusikia hivyo , aliona ni kweli na aliridhika na maelezo ya Hamza.
“Upo sahihi , mimi pia nina damu ya kifalme hivyo napaswa kuendesha farasi yenye damu ya kifalme. Leo umejua kuniridhisha na maneno yako”
Hamza aliishia kufurahi kisirisiri , ni kama sasa alijua namna ya kudili na mrembo huyo , ili kumfanya akubali ni kuongea kile ambacho anataka kusikia.
Hamza alimtoa farasi mmoja mpaka nje ya zizi na kisha kumpa ishara ya kupanda.
Nyakasura mwili wake ulikuwa mwepesi mno kwani aliruka na kutua katika mgongo wa farasi juu ya tandiko lake na kisha alishikilia hatamu. Farasi ile ilionekana kutishika na kuanza kupandisha miguu yake ya mbele hewani ikitaka kumtupia Nyakasura chini.
“Ahh! Inafanya nini hii ?”
Nyakasura yalimshinda na alijikuta akiruka kutoka kwenye Farasi na Hamza haraka haraka alisogelea ile farasi na kuishikilia.
“Wewe umefanya kuirukia ulifikiria ni bindamu huyu , kwanini usingepanda kawaida tu?”
“Sasa si ungesema , au ulitaka kuona nikidondoka?”Aliongea huku akiwa ameweka mikono yake kiunonni.
“Sasa mimi ningejuaje kama inaogopa kurukiwa?”Aliongea Hamza akijitetea na kumfanya Nyakasura kumwangalia kwa macho ya mashaka na kisha alipanga kujaribu tena.
“Wewe Farasi ole wako utake kunidondosha tena , nitakugeuza nyama”Aliongea Nyakasura bila ya kujali farasi hio ilikuwa ikielewa maneno yake au lah.
Mara baada ya kupanda , hatimae alifanikiwa kukaa bila ya farasi ile kuleta ukinzani
“Haha.. Hamza umeona hii farasi inaniogopa?”
“Ni kweli kabisa. Inaonekana kuogopa nguvu zako za kifoeniksi”Aliongea Hamza kumridhisha.
“Tembea”
Nyakasura alitingisha ile hatamu ya farasi lakini farasi ile haikusogea hata kidogo zaidi ya kutingisha kichwa chake kulia na kushoto.
“Hii farasi mbona imekaa kivivu vivu , kwanini haitembei?”Nyakasura alijikuta akikasirika baada ya kuona farasi hio inakataa kumtii, “Wewe farasi kimbia”
Hamza alitamani kucheka kuona mwanamke huyo anataka kuendesha farasi kwa kuiamrisha na maneno.
“Hebu fanya kukandamiza miguu yako kwa pamoja kwenye tumbo lake uone”Aliongea Hamza.
Nyakasura alifanya kama Hamza alivyoongea na kweli farasi ile ilianza kutembea kwenda mbele.
“Wow! Inatembea. Vipi nikitaka itembee kwa kasi?”Aliuliza na Hamza alifikiria kidogo.
“Unaonaje tukiendesha pamoja , nitakufundisha kidogo , ijapokuwa hio kamba ni kwa ajili ya kuongoza lakini mwili wako ndio unaoweza kuiongoza farasi kwa haraka”
“Sasa unabwabwaja nini , panda haraka unifundishe”Aliongea Nyakasura, muda huo hakufikiria sana alichotaka ni kujua kuendesha basi.
Hamza palepale alipanda juu ya farasi na kwenda kukaa nyuma ya Nyakasura. Awamu hio wawili hao walikuwa wamekaribiana mno na Hamza aliweza kuhisi ulaini wa mwili wa mrembo huyo.
Upande wa Nyakasura pia aliweza kuhisi kitu cha tofauti na kufanya uso wake kukakamaa na mara baada ya kukandamiza lipsi zake aliishia kukaa kimya.
“Inama kidogo kwa usawa wa mwili , kisha shikilia hio hatamu vizuri. Hizi lijamu zote zinatumika kuongoza farasi na pia ni kama breki unapotaka kupunguza na kuongeza mwendo. Ukiona spidi yake ni ndogo tumia mjeledi kuichapa kwa upole kuihimiza iongeze mwendo”
Hamza alimwelekeza kwa vitendo Nyakasura huku akiwa ameshikilia mikono yake namna ya kushikilia hatamu na kisha alimshika kiuno na kuweka sawa mwili wake.
Ni muda huo sasa Hamza aligundua ndani ya koti jekundu alilovalia ndani alikuwa amevalia nguo nyeusi ambayo ilikuwa imebanana na mwili wake kutokana na wepesi wake , aliweza kuona kutokana na kikoti kile kupandisha juu na kuacha kiuno wazi.
Mara baada ya farasi kuanza kutembea , miili yao ilianza kucheza kwa kupanda na kushuka na kufanya Hamza mwili wake kuzidi kujisugua katika ngozi laini ya mrembo Nyakasura. Hisia alizokuwa akipata zilikuwa za ajabu kabisa.
Hamza mara baada ya kuona eneo lake la mbele limemkaribia sana Nyakasura ilibidi atumie magoti yake kukandamiza makalio ya Nyakasura ili kugosea nyuma , lakini sasa mkandamizo huo ulimwongezea msisimko na kumfanya ashindwe kujizuia na kukandamiza tena.
Upande wa Nyakasura hakuwa akijua kinachoendelea , alikuwa akifurahia hisia za kuendesha farasi kwa spidi. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuendesha farasi.
“Hamza angalia inavyoenda kwa spidi.. hahaha.. kumbe kuendesha ni raha mno , nikirudi nyumbani lazima ninue farasi”Aliongea Nyakasura kwa fuaha huku akiona ashagundua namna nyingine ya kupoteza muda.
Lakini Hamza aliekuwa nyuma alikuwa akifurahia hisia nyingine. Alichokuwa akifikiria muda huo ni kama mrembo anaemkandamiza makalio yake ni mrembo maarufu anaefahamika kama Phoenix Girl.
Nyakasura muda huo aliweza kugundua kuna kitu kigumu kama mti kinachomkandamiza eneo la karibu na kiuno chake na bila kuwaza sana alipeleka mkono kugusa ili kujua ni nin.
“Ah!”
Hamza aliekuwa kwenye fantasy zake alijikuta akishituka mara baada ya mwanamke huyo kushika naniliu yake.
“Ni nini hichi ndani ya suruali yako?”
“Nyakasura hakugundua mara moja na alikuja kujua mara baada ya kuminya na kuhisi joto lake.
Haraka sana alitoa mkono wake kama vile ameshika kitu cha moto huku sura yake ikipatwa na moto. Alishikwa na aibu kiasi kwamba hata pumzi ilimkata.
Kubwa zaidi ni kwamba baada ya kushika hicho kitu, kilibadilika na kuwa kikubwa zaidi na kwasababu farasi ilikuwa mbio kitu kile kilizidi kujisugua katika eneo la kiuno mpaka kwenye mgongo wake na kumfanya ajihisi hali ya ajabu mno.
Tokea awe mdogo , Nyakasura hakuwahi kukutana na tukio la namna hio kwenye maisha yake na ndio maana alishindwa kujua ajiweke vipi katika hali ya ajabu iliojitokeza kama hio.
Upande wa Hamza aliishia kutabasamu kifedhuli huku akizidi kusikia raha namna msuguano ulivyokuwa ukiendelea na alisogea karibu zaidi.
“Wewe.. mshenzi usinisogelee..”Nyakasura alijikuta akishindwa kujizuia na kuongea kwa nguvu.
“Sio kama nakusogelea , ni kwasababu Farasi inatembea kwa kasi na kunitingisha”
“Basi , iambie isimame”
“Sawa!” Hamza palepale alishikilia kamba ya Farasi na kisha akapunguza mwendo.
Nyakasura muda huo alijihisi ni kama amegeuka na kuwa mtiifu ghafla na kujikuta akipandwa na hasira.
“Wewe mwanaharamu , kwanini unanishika?”
“Sijakushika , mimi nilikuwa nikijaribu kuzuia farasi isije kutudondosha”Aliongea Hamza akiwa na mwonekano wa kizembe.
“Na vipi kuhusu hapo chini , ulikuwa unafanya nini?”
“Hii ni hali ya kawaida kwa mwanaume. Nisipokuwa hivi kwa mwanamke mrembo kama wewe inabidi niende hospitalini nikapimwe”
Nyakasura mara baada ya kusikia neno mwanamke mrembo hasira iliokuwa kwenye moyo wake ilipotea palepale na alijikuta akipepesa macho na kushikilia hatamu ya Farasi na kuifanya isimame moja kwa moja na kisha aligeuka na kumwangalia Hamza.
“Unahisi mimi ni mrembo?”
“Ndio”
Hamza hakuongea uongo , mwanamke huyo alikuwa mzuri mno ambae alikuwa na ile hadhi ya uanamke Clasic na ukisasa.
“Upo sahihi , kwa mwanamke mrembo kama mimi ni ngumu kujizuia.Lakini naomba uelewa kitu kimoja nilipohisi hicho kitu chako mgongoni nilikigusa bila kujua , huruhusiwi kunitania kwa kusema nimegusa makusudi la sivyo nitakachokufanya hutosahau”
Hamza aliona mwanamke huyo alikuwa mwepesi kutegeka kuliko hata Regina , hivyo haraka haraka alitingisha kichwa kukubali.
Hakuna shida kabisa, siwezi kuongea. Halafu kwa mwanamke mrembo na hatari kama wewe naanzaje kwa mfano?”Aliongea Hamza na Nyakasura aliruka kutoka kwenye farasi na kutua chini.
“Huna haja ya kujitetea , najua kabisa mwanaume kama wewe huna damu ya kifalme na hadhi ya familia yako ni ya kawaida , hivyo ni kawaida kujiona wa hadhi ya chini kuliko mimi. Lakini angalau unajitahidi , kuna vitu vichache tu unapaswa kuvifanyia kazi hasa kuboresha silika yako na kujiamini kidogo , ukifanikiwa unaweza kujaribu pengine naweza kukupa nafasi”
Hamza mara baada ya kusikia hivyo hakujua acheke ama alie na kujiuliza anaongea nini , mbona imegeuka ni kama anamfukuzia?.
“Madam Nyakasura kwa hadhi yako ilivyo kubwa natoa wapi ujasiri wa kujaribu kukukaribia? Isitoshe nimekwisha oa tayari , siwezi kuwa na wazo hilo zidi yako”Aliongea Hamza huku akicheka na muda huo Nyakasura alikumbuka Hamza alikuwa amekwisha kuoa.
“Oh tena nimekumbuka kumbe umeoa , kama ni hivyo basi kazi unayo. Lakini najua mke wako hawezi kunizidi uzuri hivyo huwezi kuacha kunifikiria. Nikushauri ukijihisi umeshaanza kunipenda ili kunipata unapaswa kwanza kumtaliki mkeo , vinginevyo siwezi kukubali”Hamza mara baada ya kusikia hivyo kidogo tu atapike.
“Nyakasura usinielewe vibaya ,ni kweli sina mawazo hayo kabisa na wewe. Tuwe tu marafiki na nipo hapa kukufndisha kuendesha farasi na kilichotokea ni bahati mbaya tu kama mwanaume”Hamza aliona ni vizuri kujielezea.
“Unakataa nini? Si wewe ulieniita mrembo sasa hivi na hata kupandisha midadi yako kwasababu yangu?”
“Hamna bwana ni..” Hamza alishindwa kujua namna ya kujielezea , aliona ni kama stori nyingine sana ambayo ingekuwa na mwisho mwingine.
“Nadhani nishaanza kukuelewa sasa , unaonekana kwenye moyo wako unanitamani , lakini unaogopa nitakukataa. Kama mwanaume sioni ni ajabu kuvutiwa na mwanamke mrembo kama mimi , hivyo usiwe na wasiwasi , siwezi kukucheka” Mara baada ya kuongea hivyo alijishika kiunoni kuonyesha umbo lake vizuri.
“Sittaki kuendesha tena , narudi zangu kwenye nyumba kule , Berlly amesema atanipa mvinyo mtamu , naenda kunywa”
Hamza hata yeye hakutaka kuendelea kujielezea mbele ya mwanamke huyo , maana aliona kabla atakavyoongea ndio namna atakavyoharibu.
Mara baada ya kurudi , Hamza alimpeleka farasi yule kwenye zizi na muda huo aliweza kuhisi kuna mtu aliekuwa akiingia katika zizi hilo. Hamza hakuwa hata na haja ya kugeuka kujua ni nani kwali alishamjua kupitia hisia zake ni Asmuntis.
“Boss!!”Aliita Asmuntis huku akiwa na uso uliosawijika.
“Nini tatizo mchafu? Mbona unaonekana kuwa na huzuni namna hio, unapaswa kuwa na furaha kwa kukutana kwetu mara nyingine”Aliongea Hamza na kumfanya Asmuntis kushusha pumzi.
“Nilikuwa na mazungumzo na Azzle na tumeona itakuwa vizuri kutowaambia wengine kuhusu hali yako ili tusije kuwapanikisha , nadhani unajua Berrly na Leviathani walivyo. Lakini kesho hata kama usipoenda kwenye Baraza , lazima Gonzalez atataka kukuchallenge. Amekuwa akiwazia nafasi yako kwa muda mrefu. Hivyo tumeona ni vizuri kukaa chini na kupata suluhisho”
“Suluhisho? Nyie mnadhani ni kipi kifanyike?”
“Tumeona kwasababu huwezi kupigana , basi itakuwa ni vizuri ukiwaruhusu wanachama wa INFERNO kupigana , hii ndio njia pekee ya kulinda heshima yetu. Hivyo itakuwa vizuri kama tukimruhusu Sally kufanya safari ya kuja hapa haraka. Kwa uwepo wake ndio njia rahisi ya kuweza kushinda”Aliongea Asmuntis na maneno yake yalimfanya Hamza uso wake kuongeza usiriasi.
“Roho Mchafu nadhani utakuwa umesahau? Nilishawahi kusema mwanzo ili mradi ninapumua nitamlinda Sally kwa uwezo wangu wote na kutoruhusu mikono yake kujichafua na damu. Ukimwambia Sally aje ni kweli atakuja lakini unajua nini kitatokea akiwa uwanja wa mapambano na kushindwa kujidhibiti, nini matokeo yake?”
Asmuntis aliishia kupanua mdomo wake tu akitaka kuongea kitu lakini alishindwa na kuishia kutingisha kichwa.
“Bosi , upo sahihi , kumuita Sally kuja ni hatari zaidi”
“Usiwe na waswasi Asmuntis , nakuahidi kesho hakuna kitakachotokea”Aliongea Hamza na kisha alitembea na kumshika bega kwa kuligonga gonga kumtuliza aondoe wasiwasi na kisha alitoka nje ya zizi.
Dakika ambayo alitembea mpaka nje ya nyumba aliweza kuona magari kadhaa ya Mercedenz Benz rangi nyeusi yakisogelea ueleko wa shamba yakiwa yamewasha taa za mbele kutokana na giza.
Kila mtu ndani ya nyumba hio aliweza kugundua kuna mgeni aliekuwa akifika hapo shambani na kufanya watoke , akiwemo Nyakasura aliekuwa ameshikilia glasi ya Blood Mary.
“Bosi ni nani? Au ni Metal Tide wameamua kuja mpaka huku?”Aliuliza Mameni.
“Hapana , kwa spidi ya gari zao, inaonyesha sio watu waliokuja kwa ajili ya kutafuta ugomvi”Aliongea Hamza.
Haikuchukua muda mrefu gari zile zilisimama katika eneo la kuingilia katika upande wa nyumba hio na kundi la watu lilishuka. Watu wote walikuwa wamevalia mavazi ya suti na mashati ya rangi nyeupe na tai. Kulikuwa na wazungu na watu weusi na wote walionekana kuwa walinzi wenye mafunzo.
Muda ule kundi lile lilitengeneza safu mbili na kumuongoza mwanaume wa makamo hivi, mzungu ambae nyewele zake alikuwa amezichana vizuri. Mkononi alikuwa ameshikilia Briefcase, na kabla ya kupiga hatua alionekana akitingisha kichwa uelekeo wa Hamza na kisha alianza kutembea kusogea na jumla ya walinzi nane.
Ijapokuwa ilikuwa ni usiku lakini kila mtu aliweza kuona bango lililokuwa katika eneo la kifua chake karibu na mfuko wa suti , ni bango ambalo lilikuwa na nembo ya siraha na ngao na chini yake kulikuwa na maandihi ya ‘SETH’.
“Ni mtu kutoka Set Association”Aliongea Asmuntis.
“Inaonekana wapo hapa kwa ajili ya bosi”Aliongea Azzle.
Sekunde chache tu watu wale waliweza kufika mbele ya Hamza na wale walinzi walimuonyeshea heshima Hamza na Nyakasura.
“Honorable Prince of Hell and Phoenix Lady, I am a member of the Sytry Council. My name is Hewitt. Please forgive us for intruding and disturbing you.”Aliongea akimpa heshima Hamza kwa kumuita mtukufu Prince wa kuzimu na Bi Phoenix na kujitambulisha kwamba ni mwanachama wa Baraza la maksi akifahamika kwa jina la Hewitt. Na anaomba radhi kwa kuwavamia usiku usiku.
Bwana huyo Hewitt alisaliamaiana na Hamza na Nyakasura tu , wakati akiwapa tabasamu wengine , ilikuwa ni ishara ya kutoa heshima kwa wataalamu wa mapigano wa hadhi ya Ugwiji.
“Kwanini mwanachama wa Baraza la maksi kufika usiku usiku hapa kunitafuta?”Aliuliza Hamza na bwana yule palepale alifungua ile Briefcase na kisha alitoa bahasha iliokuwa ikimeta meta kwa kumwagiwa madini ya almasi na madini ya dhahabu na kisha alifungua.
“Sir Lucifer , tuwie radhi sana , ukweli tulikuwa tukikutafuta sana kwa kipindi cha miaka miwili iliopita , lakini hatukuweza kukupata. Tumetunza hii barua yako ya mwaliko kwa ajili ya kilele cha magwiji mwaka huu , mpaka tuliposikia kuonekana kwako leo hii, ijapokuwa tumechelewa , ila ni matumaini yetu utaupokea mwaliko kwa ajili ya kuhudhuria katika Baraza la maksi mwaka huu”
Hamza aliishia kuangalia bahasha hio ambayo ilionekana kutumia hela nyingi kwa ajili ya kuiandaa na kisha alitoa tabasamu.
“Ni mwaliko tu kwani kuna haja ya kuyakuza namna hii?”
“Kumbe hukupata mwaliko , mimi nilipewa mwaliko mwaka jana”Aliongea Nyakasura.
“Haha.. bosi nilikuambia mimi , haiwezekani hawa watu wakakusahau? Kama usipoenda haiwezi kuwa kikao tena”Aliongea Berlly lakini mwonekano wa Azzle na Asmuntis ulizidi kuwa siriasi. Kwasababu waliona kukubali kwa Hamza kupokea mwaliko huo maana yake aangeenda kuhudhuria.
Hamza licha ya kuona mabwana hao walivyo na wasiwasi , lakini alipokea mwaliko ule.
“Hii bahasha mmeijua kupamba vizuri mno , nadhani itakuwa vizuri kumpatia mke wangu”
Mara baada ya kusikia hamza akuongea hivyo , wenzake walishangaa kiasi cha kuzimia.
Hewitt mara baada ya kuona mwaliko huo Hamza ameupokea , palepale alitingisha kichwa kwa ishara ya heshima.
“Wa kuheshimiwa , Prince of hell na Phoenix Girl , barua zetu zimepokelewa vyema na tunatarajia ujio wenu siku ya kesho. Tumewaandalia siti maalumu katika eneo la VIP kwa ajili ya Magwiji wakati wa Baraza likiendelea na pia kutakuwa na siti hizo hizo maalumu katika kikao kikuu . Kama mtakuwa na maswali yoyote mnaweza kuwasiliana na bodi ya wakurugenzi moja kwa moja. Nafasi zenu zitapatikana ndani ya masaa ishirini na nne”
“Naona watu wa Set siku hizi mnazidi kuwa profesheno na kufanya baraza la mwaka huu kuwa kama sherehe ya kifahari , sio mbaya”Aliongea Hamza huku akihisi kusanyiko la mwaka huu litakuwa la kiheshima zaidi kuliko la miaka mitano iliopita.
“Your encouragement is our motivation to move forward.”Aliongea Hewwit na kisha aliwapungia mkono kila mmoja na kisha aliongozana na kundi lake kuondoka ndani ya eneo hilo.
Mara baada ya watu wale kuondoka , Black Fog alimsogelea Hamza akiwa na wasiwasi.
“Bro , una uhakika unataka kwenda? Hata kama usiende hawawezi kusema chochote”Aliongea na muda ule Nyakasura aliingilia.
“Wewe mtoto unajua nini? Kushiriki katika Baraza kuu la maksi ni raha sana pia ni mahali ambapo utaweza kukutana na watu wengi wazito. Au unaogopa watakuchokoza kwasababu unaonekana mdhaifu . Usiwe na wasiwasi , kwanzia sasa hivi niite dada na nitahakikisha nakulinda”
“Miss Nyakasura , ijapokuwa una cheo cha Ugwiji , tafadhari naomba uniheshimu , mimi sio mtoto”
“Haijalishi unavyojiona , ila wewe ni mdogo sana kwangu .”Aliongea huku akimkagua na kisha akaendelea , “Naona una umbo matata sana , hakika umejua kujitunza”
“Wewe..” Black Fog hasira zilimjaa na palepale alipeleka mkoo wake kiunoni na kutoa visu.
“Ah!” Asmuntis alikuwa fasta sana kumzuia Roda kufanya alichokusidia.
“Black Fog , umekuwa kichaa! Hebu acha kuwa mkorofi mbele ya Miss Nyakasura, kwa uwezo wako mdogo hustahili hata kupigana nae”
Black Fog aliishia kupumua kwa nguvu kudhibiti hasira zake na aliishia kupiga piga miguu chini na kisha alikimbilia ueleko wa porini kwenye shamba la chakula cha farasi. Huku Nyakasura aliishia kumtolea ulimi kwa kumuweza.
“Kwanini unamchokoza , anaonyesha wasiwasi wake juu yangu,. Kama wewe ni mtu mzima kwanini usiwe kama mdogo wake kweli?”Aliongea Hamza.”
“Sio mdogo wangu, Kama ni kuwa na mdogo wangu yupo ila sio yeye”Aliongea Nyakasura.
“Oh! Niambie huyo mdogo wako ni nani?”
“Wewe jua tu hivyo na ni mtiifu kuliko yeye, ni ..”Nyakasura alitaka kuongea lakini aligundua ni kitu ambacho hapaswi kuongea hivyo aliishia kumwangalia tu Hamza.
“Kwani lazima nikwambie kuhusu mdogo wangu? Naenda zangu kunywa , kwaheri”
Hamza aliishia kufosi tabasamu , alitaka kumfanya aongee kidogo ili amjue zaidi lakini alionekana kuwa makini.
“Amekasirika kwa namna ulivyomfokea , itakuwa vizuri ukienda kumtafuta”Aliongea Hamza akimwambia Asmuntis.
“Usiwe na wasiwasi bosi , hawezi kufanya chochote , Amefunzwa kuwa ngangari tokea akiwa mdogo”Aliongea Asmuntis na palepale aliona aingize kitu kingine, ‘Lakini bosi tunapaswa kufikiria mara mbili kuhusu hili suala la kesho”
“Najua unachotaka kusema ni mimi kutokwenda , ila nishakuambia usiwe na wasiwasi. Ngoja nikamtafute mdogo wangu nimbembeleze”
Hamza mara baada ya kuongea alitembea kuingia katika shamba la majani kumtafuta Chimera na aliweza kumuona akiwa amekaa juu ya kifusi cha majani yaliokauka akiwa anaangalia juu angani.
Hamza aliishia kusimama kwa mbali akimwangalia huku akionekana kufikiria na ni muda huo Black Fog aliweza kugundua kuna mtu aliekuwa akimwangalia.
Comments