Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Yalikuwa ni majira ya asubuhi jijini dar es salaam chini Tanzania jua likichomoza kutoka mashariki na mwanga hafifu wenye kupendeza macho, upepo wa asubuhi ukivuma taratibu na kufanya hali ya hewa kuwa yenye utulivu. Watu walikwishaamka kuendelea na majukumu yao ya kila siku ya kutafuta ridhiki za kila siku.

Apartment ya hali ya kati yenye ghorofa tatu kwenda juu ipatikanayo maeneo ya Mbezi majirani walikuwa wakiendelea na shughuli zao za hapa na pale. Ndani ya apartment hiyo ghorofa la kati kwenye chumba kidogo cha wastani alionekana mwanaume kijana akiwa amelala fofofo mpaka wakati huo na hakuonyesha dalili yoyote ya kuamka muda huo, ni wazi kwamba usingizi ulikuwa ni mtamu mno.

 

Wakati bado amelala mlango wake wa chumba uligongwa kuashiria kuna mtu yupo nje ya mlango wa chumba hiko

 

"ngo! ngo! ngo!' uligongwa tena safari hii kwa sauti kuzidi mwanzo

 

"We monica acha kunikata stimu basi" aliongea mwanaume huyo kwa sauti ya lawama

 

"Amka kumekucha" 

 

"Sawa naamka subiri kidogo" alijibu akiwa bado amelala

 

Mara mlango ukafunguliwa na kuingia mwanamke mrefu wa wastani, mweupe wa ngozi na kwenda kufungua dirisha lililokaribu na kitanda kisha kulivuta shuka alilojifunika mwanaume huyo kwa fujo

 

"Asee we monica kuna kitu unakitafuta sio?" Hatimae aliweza kuamka akiwa hana furaha kabisa 

 

"amka wewe kumekucha unalala-lala hovyo acha uvivu dogo"

 

"Si uniache sasa kwani kulala kwangu hovyo unapungukiwa na nini?" Aliuliza na bila kusubiri jibu alirudi zake kulala lakini alikuja kushtuka kwa kifinyo mguuni na kwa hasira alinyanyuka akitaka kumkamata lakini ilionekana monica alikuwa ashajipanga kwani alikimbia nduki kutoka chumbani humo kabla hata hajadakwa

 

Hehehe na ubabe wote lakini mwisho wa siku unakimbia tu" alijiongelesha na kuamka maana usingizi ulikuwa umekata kabisa

 

Hao walikuwa ni dada na kaka wa damu walikuwa wakilumbana asubuhi hio monica akiwa ndie mkubwa na mwanaume huyo aitwae jimmy akiwa mdogo

 

Ndugu hao walikuwa ni kama paka na panya waishio pamoja kwani kila siku ni malumbano tu na ugomvi usioisha muda yaani kifupi ni kwamba upendo wao kama ndugu ulikuwa ukidhihirishwa kwa ugomvi tu, ni bahati sana kuwakuta wakiwa pamoja bila kuzozana.

 

Mwanaume huyo ambaye kwasasa anatambulika kama jimmy alikuwa kijana ambaye umri wake ulikuwa miaka ishirini ya mwanzoni(early 20s).

Alikuwa ni mwanaume mtanashati na mweupe wa ngozi kama dada yake, alikuwa mrefu wa wastani na asubuhi hio alikuwa amevalia suruali nyepesi ya kulalia rangi nyeusi juu akiwa kifua wazi kuonyesha mwili wake machachari uliojengeka vizuri kuanzia mabegani mpaka kiunoni kama mwanariadha na urefu wake wa wastani

 

Basi Jimmy kama ilivyo kawaida ya wanaume wengi baada ya kuamka aliupasha mwili joto kwa push-ups na sit-ups kadhaa kabla ya kwenda kuusafisha mwili na baada ya kumaliza shughuli ya usafi wa mwili alivaa nguo za kawaida na kuzichana nywele zake fupi zilizonyolewa mtindo wa low fade na kumfanya azidi kuwa mtanashati haswaa. baada ya kumaliza mdogomdogo alielekea sebuleni

 

Kufika sebuleni aliwakuta wanawake wawili ambao ni muhimu kwake na kukamilisha familia yenye idadi ya watu watatu ambao ni yeye, dada yake na mama yake mzazi. Baba yao yeye dada yake alikwishatangulia mbele za haki miaka mingi nyuma wakiwa na umri mdogo

 

"Shikamoo mama" jimmy alimsalimia mama yake kipenzi

 

"Marahaba, umeamkaje mwanangu"

 

"Sio salama mama kuna kunguni alikuwa akinipigia kelele"

 

"Kuwa na heshima dogo nani unamuita kunguni?"

 

"Wewe unaniheshimu?"

 

"Dogo......."

 

"Hey hey mtapasua ngoma za masikio ysngu jamani nimeshachoka makelele yenu ebo! "mama yao alilalama ilioonekana kweli alikuwa na kazi ngumu sana kuwalea hao watoto mpaka kufikia wakati huo

 

"Angalau kuwe na amani basi tukipata kifungua kinywa ndio muendelee na hizo ngojera zenu" aliendelea na ndugu hao waliamua kutii mara moja

 

"Enhee asubuhi hii tunakula nini mama nimemisi sana chapati zako tamu kama asili" jimmy aliuliza

 

"Tena zipo za kutosha tu ni wewe na tumbo lako" monica alidakia

 

"Haya ndio mambo sasa ndio maana mama yangu nakupenda huwaga huniangushi kwenye misosi hahaha" jimmy alianza kumsifia mama yake

 

Basi familia hiyo walikula na kifungua kinywa kwa amani mpaka kumaliza na kila mmoja aliendelea na mambo yake jimmy aliondoka kwenda kwenye kibarua chake, dada yake akielekea chuo akibaki jimmy ambaye muda huo alikuwa amemaliza elimu yake ya advance akisubiri kuanza chuo hivyo alibaki peke yake

 

Licha ya kusubiria "selection" za chuo haikumaanisha akae tu kizembe,hapana kijana huyu alikuwa akifanya kazi ndogo ndogo za u'dayworker angalau apate pesa za kujikimu hapo baadae isitoshe familia yake ilikuwa ni ya hali ya kawaida hivyo kuna mda pesa inakosekana

Hakukaa sana humo ndani aliondoka baada ya kufungo mlango wa apartment yao.

 

<<<<>>>

 

Muda ulienda na hatimae kufika saa kumi jioni. upande wa mbezi beach beach ufukweni mwa bahari ya hindi kulikuwa kumechangamka sana mida hio kutokana na watu kuwa wengi wakipunga upepo wa jioni hio ulioambatana na baridi kwa mbali wengine wakiogelea majini wengine wakiwa na wenzi wao wakifurahia mandhari nzuri ya bahari na kadhalika

 

ilikuwa ni kawaida kwa jimmy baada ya kumaliza mishemishe zake kuja hapo kutulia kabla ya kurudi nyumbani na siku hiyo alionekana kumaliza mapema sana. alienda kwenye chimbo lake pendwa la kila siku na kujilaza kwenye mchanga bila kujali kama atachafua nguo au lah

 

kabla ya kulala alijifunga kitambaa kichwani ili nywele zake zisiingie mchanga na kuuchapa usingizi.

Moja ya sifa ya jimmy ni kupenda sana kulala na hachagui sehemu yeye popote kambi tu ilimradi ni salama na ana usingizi wa kutosha

 

ameshalalamikiwa sana kulala mchana lakini yeye wala hajali anadai kwamba usingizi wa mchana na jioni ni mzuri sana kwa afya ya akili huongeza nishati mwilini na kuondoa uchovu na kupunguza msongo wa mawazo n.k

 

Muda ulizidi kusonga taratibu, jua nalo lilianza kuzama hatimae giza kuingia Jimmy akiwa bado amelala mahali alipokuwa. Muda ulikuwa ukisoma saa moja na dakika arobaini na hakuonyesha dalili ya kuamka muda huo

 

°°°°°°°°°°

 

Katika sehemu tulivu yenye bustani nzuri iliyopendeza kulikuwa na watu wawili wamekaa kwenye benchi mmoja akiwa ni mwanaume wa makamo na mwingine akiwa ni mvulana mdogo ambaye kwa kumuangalia tu alikuwa kati ya miaka sita au saba. Muda huo ulikuwa ni jioni, mwangaza wa jua uking'aa kwa rangi yake ya dhahabu na kufanya mandhari waliyokuwa wakiangalia kuzidi kupendeza. 

 

"Jimmy"

 

"Naam*

 

" kwenye maisha hutakiwi kukata tamaa ata kama unapitia changamoto pambana mpaka mwisho usikate tamaa sawa? "

 

" sawa baba nimekuelewa lakini kwanini unaniambia saaahivi" aliuliza

 

"kwasababu nataka uwe mwenye nguvu, siku zote wenye nguvu huwa hawakati tamaa kirahisi"

 

"kwahiyo wale wanaokata tamaa ni dhaifu?"

 

"Ndio, vipi unataka kuwa dhaifu?"

 

"Hapana"

 

"vizuri kuanzia sasa nataka uwe 'strong' mwanangu ili ikifika wakati ambao mimi sioo uweze kuwalinda dada na mama yako na wale wote uwapendao*

 

"Nakuwaje sasa mwenye nguvu?"

 

"kuhusu hilo usijali mimi nipo nitakufundisha"

 

Hayo yalikuwa ni maongezi kati ya jimmy na Baba yake kipindi cha nyuma wakati marehemu baba yake alipokuwa hai

 

°°°°°°°°°°

 

Mara taratibu jimmy alifumbua macho yake ikionyesha ni wazi alikuwa kwenye kumbukumbu akiikumbuka siku aliyokuwa akiongea na marehemu baba yake na hakutegemea kama siku ile ingekuwa ndio siku yake ya mwisho kumuona baba yake kwenye uso wa dunia kwani siku iliyofuata baba yake alifariki kwa kupatwa na ajali mbaya. 

 

Alinyanyuka mahali pale na kuikung'uta michanga iliyonasa kwenye nguo zake kisha alijinyoosha vizuri na kupiga miayo

 

"Nina njaa sasa ngoja ninunue chochote kitu angalau nipooze kidogo kabla ya kurudi nyumbani kula" alijiongelesha na kuingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha pesa shillingi elfu tano kisha kuangaza huku na huko na kugundua kulikuwa hakuna wate wengi na mda ulikuwa umeenda

 

"ina maana nimelala mda mrefu kiasi hiki" aliongea baada ya kuangalia muda kwenye saa yake ya mkononi na kukuta ni saa mbili na nusu

 

"Nitasema kulikuwa na foleni kubwa" alijiambia na kuanza kuzipiga hatua kuondoka maeneo hayo. 

 

°°°°°°°°°°

 

Upande wa mbezi kwenye apartment ya waishio jimmy na familia yake sebuleni alionekana mama yao akiwa peke ameketi kwenye meza ya chakula na chakula kilikuwa tayari kimeandaliwa mezani na alikuwa akiwasubiri wanae warudi waweze kula. 

 

"Hivi hawa watoto mpaka muda huu bado hawajarudi tu" alilalama mwanamama huyo

 

Alichukua simu yake aina ya Samsung S22 na kufungua kisha kuingia kwenye apo ya 'contact' na kuanza kuisaka namba ya bintiye monica na alipoipata alipiga lakini aliishia kusikia sauti nyororo ikimwambia "namba unayopiga haipatikani kwa sasa* na kuishia kukunja sura

 

Alipoona hivyo alimpigia mwanae Jimmy na uzuri ni kwamba alikuwa hewani kwani simu ilikuwa ikiita

 

°°°°°°°°°°

 

" Twiiii twiiii twiii twi twiiii!!" simu ilikuwa ikiita kwa nguvu kama 'mic' mbovu, Ilikuwa ni kiswaswadu aina ya Tecno zile za zamani

 

Jimmy alipokea simu baada ya kuona ni mama yake ndiye anapiga

 

"Hallo ma...."

 

"Uko wapi?" alimkatisha na swali

 

"Ndo niko njiani naelekea huko nyumbani" alijibu huku mkononi alikuwa ameshika Ice cream aliyokuwa anailamba huku akiongea na simu

 

"Mpigie rafiki yake na dada yako umuulize monica alipo maana kwenye simu hapatikani"

 

"Usiniambie bado hajarudi mpaka muda huu"

 

"wewe umerudi?"

 

"lakini si ndo niko njiani"

 

"utajua mwenyewe fanya ujue dada yako yuko wapi mana kila siku kunitia presha tu"

 

"usijali nafika naye hapo nyumbani"

 

"eeh ndio mmefike mapema chakula kinapoa"

 

"sawa mama" kisha akakata simu na kumpigia simu mtu mwingine

 

°°°°°°°°°

 

Ndani ya Bar moja maarufu ya kisasa iliyoko maeneo hayohayo ya mbezi beach watu walionekana wakipata huduma yao ya ulevi, kila mmoja akiwa bize na chupa yake.

 

Sasa kulikuwa na mwanamke aliyeketi sehemu yake akinywa bia kwa fujo sana huku machozi yakimtoka na pembeni yake kukiwa na mwenzake ambaye alikuwa akimuangalia kwa kumuonea huruma

 

Wakati akiendelea kunywa kulikuwa na mziki ukilia taratibu kusindikiza huzuni yake

 

🎶Ila siri ya penzi, siri ya moyo

Siri ya nani?🎶

🎶Siri ya chozi ni maumivu ndani kwa ndani🎶

 

Alinyanyuka mwanamke huyo na chupa yake ya bia lakini kwa bahati mbaya alikosa balance kutokana na kulewa hivyo kudondoka lakini hakuweza kufika chini kwani alitokea mwanaume na kumdaka

 

Na mwanaume huyo hakuwa mwingine bali ni jimmy

 

"Sara, asante kwa kunipa taarifa" jimmy alishukuru kwa moyo wa dhati kabisa akimlenga yule mwanamke aliyekuwa amekaa na alikuwa ni rafiki yake na monica

 

"anytime" akimaanisha muda wowote

 

Monica baada ya kuona aliyemzuia asidondoke ni kaka yake ndio alizidisha kulia ni kama vile jimmy amefungua maji ya bomba kwani alilia sana kiasi cha jimmy kupatwa na wasiwasi na kumgeukia Sara akitaka maelezo

 

Sara alimpa ishara ya kwamba amevunjwa moyo yaani mapenzi ndiyo yanayomliza

 

"Unajua mapenzi ni ya ajabu sana, na sijawahi kuyaelewa. Unatoa moyo wako, uaminifu wako, yaani kila kitu ili mwisho wa siku uje kulipwa na maumivu? Mapenzi ni kama mchezo flani hivi ambao sheria zake hazijawahi kueleweka

 

Love's a bullsh*t you know?" aliongea monica huku machozi yakimtoka

 

"I hear you, kila neno, maumivu yatokayo kwenye moyo wako, nayaelewa na siwezi kukaa hapa nikikuangalia tu ni lazima nimshikishe adabu huyo mpuuzi ila unapaswa kujua mapenzi ndivo yalivyo, kuna muda yankuacha na maumivu, maswali na majeraha ya moyo ambayo huchukua muda kupona

 

Lakini sikia.... Hutakiwi kuwa mnyonge hivi na kulialia unapaswa kujikaza. Sio mapenzi yanayokuumiza bali ni mpuuzi mmoja anacheza na hisia zako. Cha kufanya ni kusahau tu na kuanza upya you're still of worth something true" alimfariji dada yake na kumpa moyo na kwa kiasi flani alifarijika

 

"Nilidhani labda utaanza kunifokea na kunisema" monica aliongea

 

*na kweli ningekufokea sema tu muda haukuwa sahii" alijiwazia na kuishia kumpa tabasamu tu

 

"ata kama ningekufokea kesho ungesahau tu" aliongea na kumfanya monica atabasamu

 

"Twende nyumbani mama anatusubiri kwaajili ya kula" aliongea jimmy akiwa ameshaanza kupiga hatua na monica alianza kumfata kwa nyuma kama kifaranga, ungedhani labda jimmy ndio kaka mkubwa kutokana na mwili wake pamoja na urefu.

 

Wakati anakaribia mlango wa kutokea aligongana na mwanamke aliyekuwa akiingia kwenye bar hiyo, haikueleweka ni makusudi ama kutokuwa makini kwa mwanamke yule mpaka kugongana mabega

 

"Samahani dada" licha ya kosa kutokuwa lake jimmy aliomba radhi na kuuelekea mlango

 

"Subiri kwanza kijana unaenda wapi?" aliongea yule mwanamke

 

"Naondoka" jimmy alijibu lakini alipofika mlangoni aliweza kuzuiwa na mabaunsa wawili wakisimama mbele yake

 

Alikuwa ni aina ya wale wanawake wenye mashauzi sana, maringo meengii na kujiona wa matawi ya juu sana kiasi kwamba aliwadharau binadamu wenzake aliowaacha mbali kimaendeleo

 

"Si umeombwa radhi na wewe" Monica aliingilia kati ni kama vile sio yeye aliyekuwa akilia dakika chache nyuma

 

"Haitoshi" 

 

"hehehe eti haitoshi, unajiona nani kwani?" 

 

"Na wewe ni nani wa kuingilia yasiyokuhusu" aliongea mwanamke yule akisindikiza na sonyo kama la jini kabula

 

"kwa taarifa yako huyo ni kaka yangu hivyo yananihusu bibiye halafu inaonekana wewe ndio mwenye kosa ni wewe ndiye uliyemgonga mwenzio halafu na bado ukaombwa msamaha ety" haitoshi" screw you! 

 

"Inatosha Monica, unatakaje ili tumalizane haraka?" jimmy alimtuliza dada yake kisha kuuliza

 

"piga magoti" 

 

"Unasema?" 

 

"Nimesema piga magoti kwani we kiziwi?" aliongea na kumfanya jimmy aachie tabasamu ambalo ni monica pekee alilielewa

 

 

TO BE CONTINUED..........

Next