Lilikuwa ni tabasamu lenyeafsiri ya ukiburi ndani yake
"Sikia bidada, usinione mnyonge hivi ukadhani labda unaweza nipelekesha utakavyo kwanza sikujui hunijui halafu kama unaona radhi yangu haitoshi hilo si tatizo langu ni lako" Jimmy aliongea na kumpa ishara monica waondoke lakini sasa wale mabaunsa walikataa kupisha mlangoni
"Waache waende" ilisikika sauti ya kiume ikikaribia mahali hapo
Alikuwa ni mwanaume mweusi japo sioo sana ni ule weusi tunaoita maji ya kunde, alivalia suti nyeusi iliyomkaa vyema mwilini, alikuwa ni mrefu wa wastani na rika kama la Jimmy
"Naitwa Cid, samahani kwa usumbufu uliosababishwa na dada yangu mnaweza kwenda" Cid aliongea akiomba radhi kwa niaba ya dada yake
"Lakini....." hakumaliza sentensi kwa jicho alilopigwa na Cid na kuishia kufunga mdomo
Cid aliwapa ishara wale mabaunsa wawapishe Jimmy na monica na walitii bila shuruti
"Hey, mind if we become friends?" Cid aliuliza akimwambia Jimmy kama hatojali wakiwa marafiki na jimmy alitingisha mabega kama ishara kwamba hajali
Cid alitabasamu na kutoa simu mfukoni kisha kumpa jimmy aandike namba ya sjimu na hakukataa aliandika na kumrudishia simu yake kisha akaondoka akitanguliwa na monica
Muda mchache mbele Jimmy na monica waliweza kufika nyumbani na walimkuta mama yao amesinzia sebuleni, ilionekana alikuwa akiwasubiri mpaka kupitiwa na usingizi.
Baada ya kumuamsha na kula hawakuongea sana, kila mmoja alikwenda zake kulala na siku ikaishia hivyo
°°°°°°°°°°
Hatimae kukapambazuka na kuwa siku nyingine tena ya jumapili, siku hiyo Jimmy aliamka asubuhi na mapema, akifanya mazoezi ya mwili kuondoa uchovu wa asubuhi akiwa kifua wazi
Alifanya mazoezi mpaka alichoka na kukaa chini kupumzika mara alisikia mlango getini ukigongwa, of course kulikuwa na fensi.
Kwenda kufungua alikuwa ni Sara rafiki yake Monica, alikuwa amevaa akapendeza kisawasawa, gauni fupi la njano lililofunika magoti ni kama alitengenezewa yeye
"Karibu ndani" Jimmy alimkaribisha na tabasamu
"Asante" aliitikia
Licha ya Sara kuwa na urafiki na Monica kwa jimmy haikuwa hivyo, ukaribu wao ulikuwa ni ule wa salamu basi
"Ingia tu ndani utawakuta mwenzako wakimalizia"
"vipi wewe huendi kanisani?" aliulizwa
"kufanya nini?"
"kufanya Ibada na kumtukuza Mungu"
"Nitafanya nikiwa hapahapa nyumbani" Jimmy alijibu
"Sawa" aliitikia huku bado akiwa amesimama mahali pale
Ni wazi alikuwa akiutazama mwili wa jimmy na kuvutiwa na mpangilio wa six pac na kifua bila kusahau jasho ambalo liliongeza mvuto sasa sijui kama alikuwa akiisikia harufu ya jasho ama alikuwa akijisahaulisha.
Hazikupita hata dakika mbili Monica na mama yake walitoka nje wakiwa tayari wamejiandaa vya kutosha kwenda kanisani
"Msisahau kuniombea baraka na mimi"
"kama unataka baraka nenda ukaombe mwenyewe" monica kama kawaida alijibu
"Siongei na wewe kwanza naongea na hawa" aliongea huku akiwanyooshea mama yake pamoja na Sara
"Una pepo wewe sio bure"
"Mama uniombee Mwanao nipate kwenda chuo kizuri si unajua maombi ya baraka ya mzazi kwenda kwa mwanae yana nguvu" jimmy alimpuuza monica
"Nitakuombea mwanangu lakini na wewe siku moja moja uwe unaenda kanisani sawa J?"
"Oh sawa"
"mmmh!" monica aliishia kuguna tu
Tangu Jimmy ampoteze baba yake ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kukanyaga ardbi ya kanisa lake akiwa na sababu zake binafsi.
Basi jimmy aliwaaga wanawake hao na kwenda zake ndani kujisafisha mwili na baada ya kumaliza kwa mtoko
Alivaa T-shirt ya mikono mirefu rangi ya kijivu, suruali ya kitambaa iliyofunika vifundo vya mguu ilikuwa rangi ya kijivu iliyokolea kuzidi T-shirt yake, miguuni alivaa sendo nyeusi zifahamikazo kama slides. Alipendeza kwelikweli kifupi alikuwa tafsiri halisi ya neno bishoo!
°°°°°°°°°°
Upande wa Masaki uliyopo wilaya ya kinondoni, mtaa wenye sifa ya kuwa na upepo mzuri kutokana na kwamba sehemu hiyo hupatikana karibu na bahari. Mazingira safi na makazi yake yaliyo katika mpangilio ulionyooka ulizidi kuupendesha mtaa huo
Watu wengi waishio masaki ni wale wenye uchumi mzuri yaani kipato cha kueleweka kuweza kukidhi mahitaji yao
Katika mtaa huo kulikuwa na nyumba kubwa ya kifahari yenye ghorofa mbili, ndani kulikuwa na bustani nzuri yenye kuvutia macho, mazingira safi kila kona.
Pia yalionekana magari mawili yakiwa yamepark nje moja likiwa Range roverEvoque jekundu na Mercedes A-Class jeusi, yote yakiwa ni ya kifahari
"Mkufu wangu uko wapi, we Sam mkufu wangu uko wapi?" ilikuwa ni sauti ya kike yenye lawama na hasira ndani yake
"Mi sijui bhana tangu lini ukanikuta nashobokea vitu vyako? " Cid alijibu na kutupia swali huku akitabasamu na kuzidi kumchochea hasira dada yake
Mwanamke huyo alionekana akipekua kila sehemu akiutafuta mkufu wake bila mafanikio na alienda mpaka kwenye sofa alilokaa nduguye na kumtaka ampishe kufanya upekuzi
" Ebu tulia basi unanikata ujue" aliongea Cid huku macho yake yakiwa yame'focus kwenye runinga ambayo muda huo kulikuwa na tamthilia ya kifilipino ikionyeshwa
"Utanunua mkufu mwingine bhana acha usumbu....." kabla hata Sam hajamaliza sentensi yake TV ilizimwa
"Move your ass bro! Imenigharimu kiasi cha shilling millioni thelathini kuumiliki move!" alifoka kwa hasira lakini Samson wala hakukasirika na badala yake alitabasamu tu na kuyanyuka.
"Eniwei nikatembee tembee kidogo" alijiongelesha mwenyewe na kuchukua hunguo ya Mercedes iliyokuwa kwenye meza ya kioo na kutoka zake nje
°°°°°°°°°°
Muda mchache mbele gari aina ya Mercedes ilionekana ikiegeshwa kwenye maegesho ya magari ndani ya hoteli ya nyota tano iitwayo Golden Tulip Hotel.
Ndani kabisa ya Hotel hiyo kulikuwa na sehemu maalumu ya kupumzika ni kama bar flani hivi lakini haikuwa bar licha ya kupatikana vinywaji mbalimbali
Waweza kusema ni kama sehemu ya watu mbalimbali waliofika hotelini na kukutania hapo na kuzungumza mawili matatu na kujenga urafiki au tuseme ulikuwa mfano restaurant lakini si restaurant anyway sio lazima kuelewa sana maana ata mimi nashindwa kuwaeleza wewe vuta picha tu sehemu yenye mkusanyiko wa watu.
Wengi wa watu hupendelea kuja hapo kwaajili ya kutuliza kichwa kwa kusikiliza nyimbo mbalimbali ambazo huimbwa na band tofauti tofauti kila jumapili na wenhi wao walikuwa ni wazungu na waarabu, ngozi nyeusi zilikuwa ni za kuhesabu na mmoja wao alikuwa ni Cid ambaye aliingia humo muda huo.
Na muda huo mbele ya ukumbi kwenye stage(jukwaa) ndogo kulikuwa na piano kubwa nyeusi pamoja kiti kidogo kwaajili ya mpigaji kikiwa wazi. Sekunda chache alionekana mwanaume akitembea kuelekea kwenye jukwaa dogo na kuketi kwenye kiti akiwa tayari kuwaburudisha wahusika.
Mwaanaume yule alisafisha koo na kutulia kidogo kisha taratibu kwa ustadi wa hali ya juu alianza kucheza piano.
Ulikuwa ni mtindo maarufu wa piano ufahamikao kama clair de lune
Clair de lune ni neno la kifaransa lenye maana ya moonligh kwa kingereza au mwangaza wa mwezi kwa kiswahili. Mtunzi wa mtindo huo alifahamika kwa jina la Claude debussy na aliitunga mtindo huo mnamo mwaka 1890
Ni sehemu ya mkusanyiko wa piano unaoitwa Suite Bergamasque, ambao una vipande vinne, lakini Clair de Lune ndiyo uliokuwa maarufu zaidi, Ni moja ya kazi bora za Impressionism, mtindo wa muziki ambao hujaribu kuonyesha hisia na taswira, Inaanzia na noti za taratibu, mithili ya mwanga wa mwezi unaong’aa juu ya maji, na kisha huingia kwenye sehemu yenye hisia nzito
Clair de Lune imekuwa moja ya nyimbo za piano zinazotambulika zaidi duniani, Imetumika kwenye filamu nyingi kama "Ocean’s Eleven," "Twilight," na "Atonement," mara nyingi ikiwakilisha hali ya utulivu, huzuni,, tafakari n.k
Inapendwa sana na wanamuziki wa piano kwa sababu ni ya kihisia na ya kuvutia, na ugumu wake kwenye kuicheza ambapo ni wataalamu pekee ndio huweza
Mwanaume yule alikuwa akipiga piano kwa utulivu na ustadi wa hali ya juu kiasi cha kuwashangaza watu wengi waliokuwa wakisikiliza kwani iliwavutia sana
"paah paah paah paaah" yalikuwa ni makofi kutoka kwa watu kama pongezi baada ya mziki huo kumalizika, wazungu baadhi hawakutaka unafiki na kwenda jukwaani kumpongeza mwanaume yule kwa dollars kadhaa.
Upande wa Cid alikuwa katika hali ya kumkubali mcheza piano yule na mara akakumbuka kitu na kutabasamu na palepale aliingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake ya Iphone na kupiga
Upande wa mwanaume aliyekuwa jukwaani akijiandaa kushuka mara simu yake iliita na kama kawaida sauti ilikuwa ni ya juu.
Ile kuangalia namba ya mpigaji alikuta ni namba ngeni na kuona si mbaya akipokea, alibonyeza kitufe cha kupokelea na kuiweka sikioni
"Hello"
"unaamini kwenye bahati? nani angedhania kama tungekutana kwa mara nyingine tena" upande wa pili ulisikika na kumfanya mwanaume yule kugeuza shingo kuangalia upande wa kulia mwisho kabisa kwenye kona ndani ya ukumbu huo na aliweza muona Cid akimpungia mkono
Of course mwanaume huyo mcheza piano alikuwa ni Jimmy. Alienda moja kwa moja mpaka kwa Cid
"Bro kumbe na wewe ni mtu wa mahoteli ya maanahahaha" aliongea Cid
"Aah wapi nimepewa mualiko tu bro"
"kumbe ila umetisha sana bro yaani unacharanga piano kama Beethoven vile" (Beethoven ni mchezo piano maarufu wa miaka ya 1800s)
"Haha kawaida tu bro ni kuweka juhudi kwenye kujifunza hata wewe unaweza"
"unaonaje ukawa mwalimu wangu nimekuwa nikipenda sana kujifunza kucheza piano kwa mda mrefu"
"sidhani kama nitakuwa na mda huo"
"Usiwe na wasiwasi nitakulipa pesa nzuri tu kuhusu piano nitanunua tu" aliongea kisha kunyamanza kidogo na kuendelea "vipi si kama ile" alinyooshea piano iliyokuwa jukwaani
"Nadhani hiyo ni brand ya Bosendorfer imperial yenye keys 97 gharama yake itakuwa ni kuanzia dollar laki mbili na nusu($230,000) mpaka laki tano($500,000)"
"Duuh mpaka kujua brand na gharama yake kweli utakuwa ni mtaalamu haswa"
"vipi bro uko free?" Cid aliuliza
"Niko free nikishatoka saloon" jimmy alimwambia
"Sio mbaya nitakusindikiza, by the way bro jina lako bado silifahamu"
"Jimmy" alijitambulisha na kumpa mkono Cid (hand shake)
Baadae kidogo Jimmy na Cid waliweza kuingia saloon ambayo ilikuws ikipatikana humohumo hotelini
"Unataka kunyoa mtindo gani?" Jimmy aliulizwa na kinyozi
"Low fade" alijibu kisha kinyozi alianza kumnyoa taratibu na ndani ya dakika ishirini alimaliza na Jimmy alitokelezea haswaa na kuzidi kuwa mtanashati
"Asee bro hapo lazima mademu wakugombanie oya barber fanya na mimi uninyoe kama hivo" Cid hakuwa na mpango wa kunyoa ila ilimbidi tu anyoe isitoshe alikuwa na nywele nyingi
Dakika ishirini nyingine zilipita na Sam alomaliza kunyolewa
"Bei gani?" Cid aliuliza
"Elfu thelathini na tano (35,000) kila mmoja hivyo jumla ni elfu sabini(70,000)"
"What the f*** Yaani kinyozi cha buku unataja bei ya Almasi?" aliwaza jimmy
"Haina shida nitalipa" aliongea Cid na kufanya malipo palepale
°°°°°°°°°°
Muda mchache mbele lilionekana gari jeusi la kifahari lime-park karibu na ufukwe wa bahari na wanaume wawili wakiwa wamesimama mbele ya gari kwa kuagamia boneti la gari hilo mikononi wakishika Ice cream
"Tamu sana hizi Ice cream" Jimmy aliongea huku amefumba macho akisikilizia utamu wa Ice cream
Upande wa Cid yeye alikuwa amekaa kimya tu akilamba Ice cream yake
"Jimmy" Sam aliita
"Naam bro" aliitika
"Tembea nami kama hjtojali"
"Sure" jimmy aliungana nae kutembea pembeni ya ufukwe wa bahari
"Unajua, nimekuwa nikifikiria jambo fulani tangu tulipokutana kwenye baa. Usiku wa jana, nilikuomba tuwe marafiki, na ulikubali bila kusita. Hakukuwa na maswali, hukusita hata kidogo. kwa nini?" Cid alimuuliza
"Kwa nini isiwe hivyo?"
"Hilo siyo jibu bro. Watu wengi husita, hata kama ni kwa sekunde moja. Wanafikiria kwanza. Wewe hukufanya hivyo"
"Nadhani sioni haja ya kusita linapokuja suala rahisi kama kukubali uwepo wa mtu maishani mwangu"
"Vipi kama ningekuwa na nia mbaya? Kama nisingekuwa mtu anayestahili kuwa rafiki?"
"Kama ingekuwa hivyo, ningekuja kugundua baadae. Urafiki siyo kuhusu uhakika, ni kuhusu utayari wa kuungana," Friendship isn't about guarantee it's about willingness to connect" Kama ungenijia na nia mbaya, hilo ni juu yako, . Lakini usiku ule, sikuhisi chochote kibaya kutoka kwako. Ulikuwa tu mtu anayetafuta koneksheni"
"unaamini watu kirahisi sana basi?"
"Hapana. Nachagua tu kutoishi kwa hofu ya kile kinachoweza kwenda vibaya."
"una mtazamo wa tofauti sana"
"yeah it's the only way I know" Jimmy aliongea akimaanisha ndio njia pekee anayoijua, na wakati anaongea alichuchumaa kwani kulikuwa na kitoto cha mbwa kilichokuwa kimetelekezwa
Wakati anamshika manyoya mara Cid alimshiika bega akimshtua
"oya jimmy ona mbele hapo kuna mbwa"
"Amesimama tu, Tulia"
"Sawa lakini.... Mbona anatuangalia sana halafu kama ananguruma hivi?"
"potezea tu hawezi fanya chochote" mara ghafla mbwa huyo mweusi aina ya Doberman alianza kubweka kwa hasira na kuanza kuwafata kwa kasi kama vile ameona mwizi
"oh shit! Kimbia" jimmy alipayuka akimwambia Cid na kukiacha kitoto cha mbwa na kuchomoka nduki pasipo kujua Sam alikuwa ameshamuacha mita kumi mbele ilionekana walikuwa ni waoga wa mbwa
Uzuri gari halikuwa mbali sana hivyo walichomoka na kwenda kujifungia ndani ya Mercedes waliyokuja nayo
Hahaha Siku sio vichaa tu wanaokukimbiza bila sababu ya msingi yaani mimi ndio wa kukimbizwa na mbwa" Cid aliongea kwa masikitiko na kitendo kile huku Jimmy akibaki kucheka tu
"Haha bro kumbe we ni muoga mbwa sikutegemea ungeniacha bila ya kukushtukia"
"Kama unajiona jasiri shuka nje" Cid aliongea na kumfanya Jimmy kuchungulia dirishani na kukutana na sura ya mbwa isiyotaka masihara kabisa
TO BE CONTINUED.........
Comments