Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Kimya kifupi kilipita baada ya kicheko ndani ya gari hilo na Cid aliamua kuvunja ukimya

"unapaswa kujua sababu ya mimi kuomba urafiki halikuwa jambo la bahati" kauli hiyo ilimfanya jimmy amtazame Cid kwa makini

"una maana gani?"

"uliniokoa jimmy" aliongea kauli yenye utata na kumfanya jimmy amtazame kwa jicho la swali ni kama alikuwa akisema "nilikuokoa? Lini?"

"ilikuwa ni miaka miwili iliyopita, Nilipatwa na ajali mbaya niligongwa na gari kiasi cha kurushwa nisiweze hata kusimama, damu nyingi zilikuwa zikitiririka kutoka kwenye majeraha, watu walinipita tu, wengine wakiniangalia na kupiga simu bila ya kufanya chochote" Cid alinyamanza kidogo kisha aliendelea

"Lakini wewe hukupita ulinisaidia, kwa mazingira yale ambulance isingeweza kufika kwa wakati, ulinifunga majeraha kuzuia damu kisha kunibeba na kukodi bajaji kunipeleka mpaka hospitali"

"Mbona sikumbuki vizuri" 

"Nadhani kwako, ulikuwa unafanya tu kilicho sahihi. Lakini kwangu… ulikuwa mtu pekee aliyeniona kama binadamu mwenzie na sio majeruhi tu" aliongea na kumfanya jimmy aanze kuvuta kumbukumbu

"oh kumbe wewe ndio yule jamaa uliyekuwa ukiendesha Duccati kwa mbwembwe barabarani na kupata ajali?" maeneo ya mikocheni sio?" hatimae aliweza kukumbuka

"Ndio ndio ni mimi" 

"Sema uso wako ulikuwa unavuja damu ndio maana sikuweza kukumbuka kirahisi ila sikutegemea kama utanikumbuk9a" 

"Siwezi kusahau bro, kingine Sura yako haijabadilika ni umeongezeka urefu na mwili basi" 

"Oh sikutarajia mtu aliyekuwa akilala pale chini angenikumbuka" jimmy aliongea na kutabasamu kidogo

"Sitasahau siku ile, halafu nina swali..... Unajua kwa hali ile nisingeweza fika hospitali nikiwa bado hai hisia zangu zinaniambia kuna kitu ulifanya ambacho si cha kawadi" Cid aliongea

Jimmy aliishia kutingisha mabega kwamba hajui kabisa na hakufanya chochote

"Anyway sikutaka urafiki wako kwa sababu ya deni au shukrani. Nilihisi tu… mtu ambaye anaweza kufanya hivyo kwa mtu asiyemjua bila kufikiria mara mbili ni mtu wa kipekee. Na nilitaka kuwa na urafiki na mtu kama huyo, kuna ule msemo wa wazungu" a blessing in disguise" nadhani unakufaa"

"Okay bro tuachane na hii mada nina njaa fanya mpango tupate chakula kwanza  halafu ndio mambo mengine yafuate" jimmy aliongea huku akipiga miayo 

Cid aliwasha gari na kuliondoa mahali pale kwa mwendo wa taratibu akitafuta mgahawa wowote uliokaribu kwaajili ya ckula

°°°°°°°°°°

Mahali pasipojulikana ndani ya jiji, eneo lililokuwa limezingirwa na misitu na hakuku na dalili ya watu kuishi ama kupita maeneo hayo kulikuwa ni a fensi kubwa iliyozunguka mita za mraba elfu hamsini(50,000 meter squares) 

Kulikuwa na majengo mbalimbali ndani ya hiyo fensi sasa kwenye jengo moja ndani ya chumba kilichokuwa na mwanga hafifu, hewa ilikuwa nzito na sauti za milio ya kama mapigo na pumzi nyingi zikihemwa zilisikika

Kilikuwa ni chumba cha mazoezi na walionekana watu wapatao nane walikuwa wakifanya mazoezi mazito mazito kwa usahihi kabisa

Mara mlango ulifunguliwa na kufanya watu hao kusitisha kile walichokuwa wakifanya na kuweka umakini wao kwa yule aliyeingia, alikuwa ni mwanaume mweusi mwenye mwili uliotuna kama baunsa akiwa amevalia gwanda nyeusi isizokuwa na nembo uoyote

Bila kusema neno alienda moja kwa moja kuchukua rimoti na kuwasha runinga iliyokuwa ukutani na Taarifa ya habari ya kusikitisha ilionyeshwa kwenye skrini.

Breaking news: Miili ya watu wapatao ishirini na tano imepatikana ikiwa haina uhai kwa kosa damu, mamlaka hazielewi vifo hivyo vya ghafla vimetokana na nini, polisini wanaendelea kufanya uchunguzi kwenye maeneo hayo kubaini tatizo na kukusanya ushahidi hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa vifo vya ghafla ninavyotokea usiku na miili kubaki ikiwa imekauka"

"Vifo vingine tena" aliongea mwanaume yule mweusi tii na sauti nzito kama roboti

Kundi lile la watu walitazamana wao kwa wao kila mmoja na kushusha pumzi nyingi, lilionekana jambo lile halikuwa geni machoni pao

"wale wapuuzi wanywa damu sio?" Mmoja wao mwanamke mwenye asili ya wahabeshi aliongea

"Na leo ndio mwisho wao watake wasitake" aliongea aliyeingia na gwanda ambaye ndio kiongozi wao walimuita "kamanda"
 
"Nadhani nyote mnajua kwanini mpo mahali hapa kwanini kundi hili lilianzishwa" aliendelea

Kimya kilifuata kisha mwingine mwanamke mwenye nywele fupi rangi ya silver(rangi ya fedha) alidakia "Yeah, by a damn half-breed. An ex-military bastard with Mysterious blood running through his veins" (Ndio yule mwanaharamu, mwanajeshi wa zamani. Chotara mwenye damu isiyo ya kawaida ndani yake) aliongea kingereza kwani alikuwa ni mzungu

"Don't forget that" bastard"  saved your damn life from those blood thirsty asshol*s"(Usisahau huyo "mwanaharamu" aliyaokoa maisha yako kutoka kwa wale punda wenye kiu ya damu) alimkumbusha na kuendelea "He also saved yours too before he also saved yours too before he made you guys  what you are now(aliyaokoa na yenu pia kabla ya kuwajenga kama mlivyo sasa)

"Lugha tafadhari wengine wengine hatujjaenda shule ujue" aliongea mmoja afahamikaye kwa jina la Ben

"ondoa wengine sema wewe halafu sio kama huelewi hapo" aliongea Caren muhabeshi

"kwani hujui kiswahili ndio lugha yetu ya taifa?" Ben alikazia msimamo wake kwa swali

Mwanzilishi wa kundi hili aliona kile ambacho serikali ilikataa kuona. Alipigana na kile ambacho dunia ya sasa inapinga uwepo wake, aliokoa maisha ya wengi" alinyamanza kidogo na kuwatazama kila mmoja "lakini sasa hatunaye tena lakini haimaanishi tukae tu, hapana tunakwenda vitani kumaliza kila kitu"

Chumba kilijaa ukimya wa hali ya juu na hewa kuzidi kuwa nzito, nyuso za kila mmoja zikikunjamana.

"We are........" aliongea kamanda

"HIDDEN SUPREMACY" wote walijibu kwa pamoja wakiacha sajti ikijirudia mwangwk

°°°°°°°°°°

Upande wa Jimmy na Cid baada ya kumaliza kula walitoka nje mgahawani jua likipiga kwelikweli na joto la jiji kuongezeka. na jimmy wala hakujali na zaidi alitoa pendekezo la kutembea tembea kidogo kunyoosha miguu na kusafisha macho maana alishachoka kukaa sana kwenye gari

Wakiwa wanakatiza kwenye kona za hapa na pale za mitaa yenye pilikapilika alionekana mzee mmoja ambaye alikuwa akihitaji vijana wa kumsaidia kushusha kreti za soda zilizokuwa kwenye lorry na wengi wa ma'dayworker walikuwa bize na shughuli nyingine zakuwaingizia kipato

"Kijana unahitaji pesa za haraka? Nisaidie kushusha hizi kreti za soda" aliongea yule mzee akimlenga jimmy isitoshe alikuwa akijulikana kama dayworker kwenye mtaa huo

"Zote hizo?" aliuliza huku akiliangalia lorry kampuni ya pepsi lililobeba kreti za soda na kwa hesabu za haraka haraka zilikuwa kreti si chini ya 100, kikawaida lorry size ya kati hubeba kreti 500-800

"Ndio nahitaji zote ila wewe shusha kadri uwezo wako unavyoruhusu"

"Ni bei gani mzee"

"kwa kila kreti utakayoshusha na kuingiza mule ndani ni mia mbili" aliongea yule mzee huku akimnyooshea sehemu ya kuzipeleka

"Nisubiri hapa nitamaliza haraka" Jimmy alimwambia Cid

Cid alitingisha kichwa na kwenda kujiegamiza pembeni kwenye ukuta huku akikunja mikono yake kama boss flani hivi

Jimmy alikwenda mpaka kwenye lorry la kreti kisha alinyoosha shingo kwa kuikunja kulia na kushoto kisha alipandisha mikono ya shati kisawasawa na kuanza kazi mdogomdogo

Nusu saa mbele alikuwa amebeba kreti mia tatu na ushee na hakuonyesha dalili ya kuchoka ndio kwanza anachangamka

"Hujachoka tu?" Cid aliuliza

"Vp unataka kunisaidia? Karibu" Jimmy alimkaribisha kupiga mishe za ki'dayworker mtoto wa kishua

"Juhudi nyingi sana lakini maokoto ni kidogo kuliko ulivyojituma" 

"Watoto wa kishua hamuwezi elewa, hakuna anayependa kufanya kazi ngumu lakini ni bora kuliko kutofanya chochote Isitoshe nahitaji maokoto" 

"ungekuwa nazo za kutosha  vipi ungeendelea kufanya kazi ngumu?" Cid aliuliza

"Ndio, kama ni jambo la maana nitajiuma vya kutosha isitoshe hapa nilipo nafanya la maana, kuhangaika kwangu angalau napata pesa ya kukidhi mahitaji yangu na familia yangu" aliongea huku akitabasamu

Cid bila kuongeza neno naye alikunja mikono ya shati lake na kuungana na Jimmy kubeba kreti "Can't let you take all the glory"(Siwezi kukuacha ukibeba utukufu peke yakok alitabasamu

Lisaa likapita na hatimae waliweza kumaliza kushusha kreti zote zikiwa jumla mia saba hamsini(750), Cid akibeba kreti 80 tu lakini alikuwa hoi bin taaban kuliko hata Juimmy na jua lilivyokali waliloa jasho kana kwamba wametoka kubatizwa kwa mwamposa

"Asee vijana mna nguvu sana na ni wachapa kazi" mzee alisifia na mkononi alishika pesa noti nyekundu na kilikuwa ni kiasi cha shillingi lakini moja na nusu

"kama tulivyokubaliana kijana ila sikutegemea kijana kama mdogo kama wewe kuweza kubeba kreti nyingi kiasi hiko" aliongea akimpatia pesa zile jimmy na alizipokea kiroho safi

Alichomoa elfu hamsini na kumpatia Cid "Gawio lako" lakini Cid alitingisha kichwa kukataa na kumwambia abaki nazo tu isitoshe alifanya kusaidia sehemu ndogo tu

°°°°°°°°°°

Usiku wa saa moja Jimmy alionekana akifungua geti na kuingia ndani akitoka kuzurura siku nzima na rafiki yake mpya, alienda moja kwa moja mpaka kwenye apartment yao na kuingia ndani na mkononi alikuwa ameshika mfuko mweupe wanye chata la KFC

Aliwakuta mama yake na dada yake wakiwa bize kufuatilia tamthilia ya kihindi kwenye runinga na aliwapa salamu na kuweka mfuko kwenye meza ndogo iliyoko sebleni hapo

Ile Harufu tu ya kuku wa Kfc ilitosha kumvuruga monica ambaye alikuwa makini kufuatilia tamthilia ile. Macho yake yalitua kwenye mfuko ambao harufu yenye kuisumbua pua yake inatokea

"Nimewaletea zawadi warembo wangu" aliongea jimmy kwa bashasha

Monica kusikia vile ni kama amepewa kibali cha kuvamia mfuko ule kwani slienda moja kwa moja na kutoa viboxi vidogo vidogo jumla vikiwa sita, viwili vikiwa na chipsi, viwili kuku wa kukaanga na viwili vingine vikiwa na kuku wa kuchoma

"Kuleni mshibe tena mmalize kabisa msijali kuhusu mimi nimeshakula na nimeshiba" aliongea jimmy na kuwaaga zake anaenda kulala na waliishia kumshukuru na kumtakia usiku mwema na siku ikaishia hivyo

°°°°°°°°°°

Ikawa siku nyingine tena, siku ya jumatatu siku ambayo haipendwi na watu wengi miongoni mwao wakiwa ni vijana hasa wanafunzi, usiniulize kwanini maana hata mimi sijui licha ya kutoipenda hii siku ya juma

Siku hiyo kama kawaida Jimmy alikuwa amelala fofofo muda huo wa saa mbili asubuhi mara ghafla simu yake iliita na kumuharibia usingizi wake, alipoangalia namba ya mpigaji aliishia kutingisha kichwa kwa masikitiko

"Huyu jamaa anataka nini asubuhi-asubuhi" alijiongelesha huku akijpokea simu na kuiweka sikioni

"Toka nje bro" Ilisikikika sauti kutoka upande wa pili bila hata salamu

"Nitoke nje kufanya nini kaka saizi bado hakujakucha" 

"Oh habari za asubuhi aya toka nje bro" alimpa salamu ya asubuhi kama kielelezo cha kwamba kumekucha

Jimmy alijinyanyua kivivu kutoka kitandani na kwenda dirishani kuchungulia nje na alishuhudia gari la kifahari Aston martin DB12 jeupeee kama theluji likiwa limepark nje tena ndani ya apartment
Ni gari la kifahari linalogharimu $269,000 sawa na millioni mia saba za kitanzania

"Bro who did you rob?" akimaanisha hilo gari amemuibia nani

"Haha ebu toka nje bro ninaangaliwa sana kama jambazi" 

Ni kweli raia waliokuwa wakiishi kwenye apartment hiyo walikuwa wakikodolea macho gari hilo n zaidi ni mwenye gari na kujiuliza amekuja kufanya nini wengine walienda mbali kwa kuwaza labda anataka anunue eneo hilo

Jimmy alinawa uso haraka haraka alivaa vest nyeusi akibaki na kaptura ileile aliyolala nayo, alichukua mswaki na kuweka mdogo kisha mdogomdogo mpa nje

"Unalala sana bro nilitegemea kukukuta upo macho" aliongea Cid lakini Jimmy alimpuuza na kuelekea gari alilokuja nalo na kuanza kulitazama kutoa ushamba

"Unaendesha hili sio?" jimmy aliuliza

"Yeah" Cid alijibu

"Tunaenda wapi?" 

"Umesahau? Tunakwenda kununua Piano then uanze kunifundisha leoleo" aliongea na kufanya majirani kumshangaa

"Jimmy anacheza piano? Mbona ya leo kali" mmoja wa majirani alinong'ona maana Jimmy wanayemjua wao ni mpenda kulala sana na mvivu
Mara monica na mama yake walitoka nje pia

"Oh kumbe mnaishi pamoja" Cid alishangaa alipomuona monica

"Huyo ni dada yangu bro" 

"Kumbe mi nilidhani labda........." aliongea na kuacha sentensi iende hewani

"Uliwaza mbali sana bro kama nilivyosema huyo ni dada yangu" 

"Sio mbaya eneweii nichukue nafasi hii kujitambulisha tena, naitwa...." 

"Cid si ndio?" Monica alimalizia sentensi yake

"Ndio ndio ni furaha kwangu kukumbukwa jina na mtu ambaye tulikutana kwa bahati" alifurahi meno yote yakiwa nje

"Na huyu hapa ni mama yngu mzazi, mama huyu ni rafiki yangu" Jimmy alifanya utambulisho

"Oh shikamoo mama" Cid alimsalimia mama yake jimmy

"Marahaba mwanangu hujambo" 

"Sijambo kabisa mama, unajua mwanao ni mtaalamu sana likija suala la kucheza piano" aliongea na kumfanya Monica kuangua kicheko kile kicheko cha umbea na Jimmy kuona hivyo alitoka hapo na kuelekea ndani huku aki-brush meno yake kwa mwaki

"wapi bro? " 

"Naenda kujiandaa sikawii sana" 

"Unasema Jimmy anajua kucheza piano?" mama yake aliuliza
 
"Ndio mama au ulikuwa hujui?" Cid alishangazwa kidogo

"Pengine ni siri yake, vijana mna siri nyingi ambazo wakubwa zenu hatujui au nasema uongo?" mama yake jimmy alisema

"Hujakosea mama sisi vijana huwa tuna mambo mengi sana" 

"Ni kweli, aya karibu ndani usisimame tu hapo mgeni kuishia nje haipendezi au nasema uongo mwanangu?" 

"Haha wasema lakini sikai sana nimekuja kumpitia Jimmy kuna mahali tumepanga kwenda" 

"Sawa karibu ndani"

"We Bianca njoo usalimie wakubwa" jimmy aliita na kioo cha gari siti ya abiria kilishuka

 


TO BE CONTINUED.......... 

Previoua Next