SEHEMU YA 202.
Karibu kuzimu.
Katika zile Skrini kubwa zilizokuwa zimezungushwa kwenye jukwaa kulionekana kitabu kikubwa kilichokuwa kina maandishi kikifunguliwa kurasa zake huku yakionekana maandishi yalioambatana na picha. Katika kitabu hicho ulionekana wasifu wa Gwiji namba moja na yule mshereheshaji palepale alianza kusoma maandishi yale kwa namna ya kuvutia;
“Amebeba wasifu wa jina sawa na la mfalme mkuu wa mithiolojia za Kiarmenia, ambae alifunga elementi nne za mhimili wa dunia. Uwezo wake uliibua wivu mkubwa kwa watu wote wanaotumia nguvu za ziada kwa kuwa na uwezo uliomruhusu kuzitumia elementi kwa faida yake pekee. Hakuna anaejua jina lake halisi ni nani , mwonekano wake ni wenye kubadilika badilika milele. Ana uwezo wa kubadilika na kuwa hewa na ndio maana watu wa ulimwengu wa siri wakaamua kumbatiza jina la Air . Makofi mengi kwa ajili ya kumkaribisha Raisi wa Adept Association, Mr Air”
Mara baada ya mshereheshaji kuongea watu wote walipiga makofi na kisha walitulia kwa ajili ya kumuona gwiji namba moja akiingia. Lakini sasa, hakuna mtu yoyote alieweza kumuona akiingia katika njia maalumu iliotandazwa zuria na badala yake watu walishangaa tu mtu kuwa tayari amekwisha kukaa katika siti iliokuwa na jina la Air ndani ya jukwaa la Magwiji.
Alikuwa amevaa vazi la kikale mfano wa joho lililofungwa na kamba kiunoni. Licha ya mwili wake kuonekana lakini sura yake haikuweza kuonekana moja kwa moja na kujua alikuwa ni mtu wa rangi gani. Kwa namna ambavyo alifika katika jukwaa hilo ni kama vile aliteleport na kuibukia moja kwa moja kwenye siti yake.
Kitendo kile cha ajabu kilifanya watu ndani ya uwanja huo kupiga makofi mengi sana na kupiga makelele ya kumshangilia, hususani kwa binadamu ambao ni wanachama wa umoja huo wa watu wenye vipawa maalumu.
Mr Air alisimama na mkono wake ulionekana kupungia watu na kisha alirudi na kukaa kwenye kiti chake.
Regina ambae alikuwa akiangalia mlolongo wa matukio hayo alijikuta akifikicha macho yake kwa nguvu akiwa haamini kile ambacho anaona.
“Inawezekanaje , amewezaje kufika pale bila ya kuonekana au ni kwa mazingaombwe?”
“Hapana ule ni uwezo wake, anaitwa hewa kwasababu anaweza kujifananisha na hewa na asiweze kuonekana kwa macho. Hajawahi kujulikana kwa sura moja kwasababu kila anapotokea ana sura tofauti na sauti tofauti , hivyo hakuna anaemfahamu ni sura ipi ni ya kwake halisi au kama alishawahi kuonyesha sura yake kabisa. Kwa lugha nyepesi ni mtu ambae haonekani , na kwasababu hajawahi kuwa na ugomvi na mtu yoyote haijawahi kufahamika uwezo wake halisi ni upi .”
Regina kama binadamu wa kawaida ilikuwa ngumu kwake kuamini mtu anaweza kuwa translucent na asionekane hewani , kitu ambacho kilikuwa nje ya mantiki za kisayansi.
Maajabu ya ulimwengu wa siri yalikuwa ni zaidi ya kile alichowahi kufikiria. Regina alijikuta akisahau kabisa kama ametekwa na kumuona Helena ni kama mtu ambae amemleta hapo kwa ajili ya matembezi.
“Kwahio unasema kuna watu aina ya Mr Air kwenye Chama cha Adept?”Aliuliza Regina.
“Usifikirie sana, umoja wa Adept una watu wasiopungua mia moja , licha ya kuwa na uwezo wa ajabu ila hawana uwezo mkubwa wa mapigano. Mr Air anaaminika sio kiumbe wa sayari ya dunia, Asilimia kubwa ya watu wa jumuia ya Adept wana vina saba vya damu ya wanyama”
“Damu ya Wanyama !” Regina aliishia kutingisha kichwa kwa mshangao, “Ila inawezekana kwa namna alivyo haonekani kuwa binadamu wa kawaida”Aliongea Regina na kumfanya Helena kucheka.
“Miss Regina hata wewe pia unaonekana kushangaza? Yaani nimekuteka kukuleta hapa lakini naona umeshanigeuza kuwa Tour Guide wako. Huogopi nitakuuwa na kisu changu?”
“Nitafanyaje sasa? Kwamba nikuogope mpaka kufa. Nimeona kwasababu siwezi kujiokoa ni bora nikachukulia kama fursa ya kujifunza zaidi”Aliongea Regina na Helena alitaka kuongea neno lakini aliacha baada ya kusikia mshereheshaji akimtangaza Gwiji mwingine.
“Kutokana na uadilifu wake wa kiimani , aliogelea katika utukufu mkuu wa Bwana mtakatifu na kuishi katika baraka za mbingu na ardhi. Alipofikisha miaka ishirini na moja alielekeza mikono yake juu na kupokea upanga wa kiapo, alipofikisha miaka ishirini na tanu akaelekeza mikono yake juu na kupokea mkuki wa kulinda mbingu na ardhi. Hata baada ya miongo kadhaa kupita bado alisimama kileleni kama shujaa juu ya Jumba takatifu. Tunamkaribisha kwenu Malaika Mkuu Mika kutoka Madhabahu takatifu ya kifalme”
Akiwa amevalia joho refu lililonakishiwa na nyuzi za dhahabu alionekana. Alikuwa amevaa mkanda kiunoni wa rangi ya dhahabu kama shujaa. Huku akiwa ameshikilia mkuki mrefu kwenda hewani kuzidi kimo chake uliokuwa umenakishiwa na vito vingi vya thamani
Alikuwa na nywele za kahawia , na masharubu mengi katika uso wake. Alikuwa akitembea huku kichwa chake akiwa amekiinua juu bila ya kukipindisha kama mwanajeshi. Mwanaume huyo aliaminika kuwa na umri zaidi ya karne moja. Hakuwa mwingine bali ni Malaika ama kiongozi mkuu wa Mahakama takatifu Mikaeli.
Mika mara baada ya kwenda kusimama juu ya jukwaa wafuasi wake kutoka Falme ya Mahakama takatifu walisimama na tofauti na kushangilia walianza kusali huku macho yao yakiwa yameng’azwa na nuru ya imani.
Lakini hata hivyo kulikuwa na kundi la watu ambao walikuwa wamekunja sura kama wamebanwa na mlango huku sura zao zikiwa zimejaa dharau , walikuwa ni wafuasi wa shetani wakiwakejeli wafuasi hao kwa sala zao.
Mikaeli aliinua mkuki wake juu angani na kufanya utoe mwanga wa kuumiza macho na kisha ukazima na haukuonekana kwenye mikono yake bali ulionekana kusimikwa katika mkono wa kulia wa kiti chake.Akiwa na mwonekano wa kujiamini alikaa chini.
Mapema tu kabla ya mshereheshaji kutangaza Gwiji mwingine kujitokeza mwanaume mwenye mwili mkubwa sana kama kiboko alitokea katika njia ya kutokea uwanjani.
Mtu huyo alikuwa na kimo zaidi ya mita mbili kwenda hewani na alikuwa amevalia Vest ya ngozi ya mamba bila shati na kufanya mikono minene sana kuonekana , nywele zake zilikiwa ni nyeupe kama mvi na masharubu yake pia.
Alikuwa amevalia kofia ya kijeshi kichwani ilionekana kuwa ya zamani mno na mkononi alikuwa ameshikilia kiko na alitembea huku akivuta sigara kutoka katika kiko kile.
Kiunoni mwake kulikuwa na Kitara au sime ndefu na pana, mpini wa Sime ile ulitengenezwa kwa madini ya Silver na dhahabu na vito vingine vya kuvutia. Ilionekana haikuwa Sime ambayo unaweza kuikadiria bei yake.
Bwana huyo alionekana kujikaribisha mwenyewe huku akipunga mkono hewani kwa kucheka.
“Nadhani sina haja ya kumtambulisha tena , kila mmoja wenu amemuona na kumfahamu”
Alikuwa ndio mkuu wa kundi la kiharamia namba moja duniani. Inasemekana ushujaa na ujasiri wake alirithi kutoka kwa watangulizi wak, yaani mababu zake maarufu kama The Vikings !. Kundi lake la kharamia lilikuwa la Daraja A lililofahamika kama Nyangumi wa Barafu(Ice Whaler).
“Ni kapteni Phantom Oleg” Sauti za maharamia wa Ice Whaler zilisikika zikishangilia.
Leviathani aliekuwa amekaa, alimpigia makofi Oleg . Ingawa walikuwa washindani lakini Oleg alikuwa mkubwa kwake katika kazi ya uharamia, kwa Lugha nyepesi ni kwamba Leviathani alimkuta Oleg kazini.
“Maharamia pia wanaruhusiwa kushiriki katika huu mkutano , si wanawinda na serikali nyingi duniani?”Aliuliza Regina .
“Haha.. kwa nguvu waliokuwa nao hao maharamia inaweza kutishia usalama wa nchi yoyote ile wakijaribu kumkamata , kingine katika Mkutano mkuu wa Baraza la Maksi hakuna mtu mzuri wala mbaya , au mhalifu na asie mhalifu. Ukisikia sehemu ambayo wafuasi wa mungu na shetani hupeana mkono wa amani, basi ni hapa”
“Hili jitu Midevu linaonekana kuwa na msisimko mkubwa kuliko Mr Air na Mika licha ya kuonekana uwezo wake ni mdogo”Aliongea Regina.
“Regina usimchukulie poa Phantom. Ingawa anaonekana wa kawaida lakini ni maarufu mno katika mbinu za kivita baharini. Ana miliki meli ya kivita yenye upanga maarufu kama Sea God Blade, unaovumishwa kuwa na uwezo wa kukata meli yoyote mara mbili.
“Sea God Blade!” Regina licha ya kutokujua tamathali za kijeshi hakutaka kuamini kama kuna meli ya kivita ambayo ina uwezo wa kutenganisha meli nyingine mara mbili kupitia upanga.
“Ndio. Meli yake ya kivita imefungwa upanga mkubwa mbele wenye nguvu kubwa. Phantom anajitambulisha kutokea katika kizazi cha Vikings, yaani waliobarikiwa juu ya bahari. Anaweza asiwe na uwezo wa kupigana mkubwa akiwa nchi kavu lakini katika bahari ni mtu mwinginge kabisa.Anao uwezo wa kuponya majeraha yake yote kwa kugusana na maji ya bahari”
“Kweli!?”Regina aliuliza kwa kushangaa.
“Hakuna uthibitisho , ila inasemekana anao uwezo wa kuwasiliana na viumbe wanaoishi chini ya bahari, ikiwemo Majini bahari na Nguva na ndio wanaomsaidia kuzamisha meli na kuiba mali. Inasemekana uwezo wake aliupata baada kufariki akiwa baharini na nafsi ya kiumbe wa ajabu ilimvaa na akafufuka. Kama isingekuwa uwezo wake mkubwa wa kupambana akiwa majini unadhani angeweza kulipa umaarufu kundi lake la kiharamia la Ice Whalrer? Yote ni kwasababu sio mtu wa kawaida”
Regina mara baada ya kusikia maelezo hayo aliihsi ubaridi wa mgongoni ukimpitia, kwasababu alichosikia ni kama Oleg hakuwa binadamu. Alijikuta akitoka mawazoni mara baada ya kumsikia mshereshaji akiongea tena;
“It is said that the real Dragon Knights will not be harmed by the dragon flames. They can bathe in the dragon flames and dance with the dragon …”
Mara baada ya kuongea hivyo sauti zilianza kupiga mayowe ya shangwe huku wakiimba kwa shangwe kwa kutamna neno; we’re burning.
“Nichukue nafasi hii kumkaribisha kwenu Aulando- Saint Rodriguez, kiongozi mkuu wa Holy Knight na mlinzi mkuu wa DSS(Dragon Slaying Sword)”
Mara baada ya kuongea hivyo palepale alitokeza mwanajeshi alievalia vazi la kijeshi la chuma kuanzia miguuni mpaka kichwani huku akiwa na upanga mrefu kiunoni.
Vazi lake lote la chuma cha silver lilikuwa na nakshi za ajabu zilizochongwa na kubandikiwa madini ya dhahabu ya michoro ya nyoka. Eneo la kifa chake kulikuwa na picha kubwa ya Dragoni akitema moto.
Kilichovutia zaidi ni helmeti la kiroma alilovalia katika kichwa chake katika eneo la macho. Kulikuwa kumetengeneza kama vile ni miwani kubwa ya madini ya kung’aa na kumfanya aonekane kutisha mno.
Ala ya upanga wake ilikuwa imenakshiwa na chata la Wyvern na kuangalia tu mpini wa upanga huo unaweza kugundua haikuwa siraha yenye uzito wa kawaida.
“Wanaongea nini?”Aliuuliza Regina.
“Ni Creed. Tafsiri yake ni ‘We’re Burning’ maana yake ni kuwaamrisha waendesha madragoni kuwabatiza kwa moto wa Dragoni bila woga. Kwa lugha nyepesi ni kama kauli ambazo dini huwaamrisha wafuasi kuongea kama njia ya kukubali kuwa muumini kwa kubatizwa. Holy Dragon Knight ni umoja wa kiimani wa wanajeshi katika majeshi ambao wanaamini wana nguvu kubwa sana , si tu kiroho lakini kimwili pia . Ingawa Auland ndio mwanajeshi pekee alieweza kuingia katika hadhi ya Ugwiji lakini inaamnika kuna zaidi ya wanajeshi wenye uwezo kupita hata wa Auland , lakini yeye ametangulizwa machoni mwa watu kama mwakilishi pekee..”
Regina muda huo aliweza kukumbuka kauli ya Hamza kuhusu madaraja ya jamii za siri na daraja la juu zaidi ni S Class.
Ikumbukwe hata watu wa dini kubwa duniani pia wanachukuliwa kama jamii au jumuia na huingia katika Daraja S , hivyo wote hao walikuwa na misemo yao maalumu ya kutamka ukitaka kujiunga nao.
Auland hakuvua helmeti lake hata baada ya kukaa , ilionyesha ni dhahiri hakutaka kuonyesha sura yake.
“Najua wote mmekuwa na hamu ya kumuona Auland ambae ni mara chache sana kuonyesha sura yake. Lakini mtu anaefuatia ndio mzito zaidi” Mshereheshaji alitulia kidogo na kisha palepale akaongea.
“Kila kiza kinapoingia yeye ndio huamka na hakuna la kumshinda kufanya . Namkaribisha kwenu mwanachama wa kudumu wa Madhabahu ya Giza , Mwanachama pekee wa damu ya kifalme ya Strigoi . Prince Sebastianii!!”
Mara baada ya kuongea watu hawakushangilia kama ilivyokuwa kawaida, japo kwa mbali yalisikika makofi , ilionyesha watu wengi walikuwa na shauku ya kumuona pekee na hawakuwa na ushabiki nae.
Muda ule aliweza kuonekana mwanaume mzungu mwenye ngozi iliopauka , na nywele za kiblonde, aliekuwa katika makadirio ya umri wa miaka arobaini hivi akitembea kwa kujiamini kusogelea jukwaa, alikuwa amevaa Tuxedo na viatu vyeusi vya ngozi.
Sebastiani mara baada ya kupungia mkono watu kidogo , alisogea kwenye jukwaa na kuketi kwenye nafasi yake. Lakini sasa bwana huyo aligeuza uso na kumwangalia Mikaeli na wawakilishi hao wa Madhabahu ya Nuru na Madhabahu ya Giza walionekana kukasirikiana kiasi cha kufanya macho yao kuwaka.
“Regina je unaweza kuamini Prince Sebastiani umri wake ni miaka elfu tatu?”Aliongea Helena akimwongelesha Regina.
‘Nini! Miaka elfu tatu?”
“Ndio , ijapokuwa Strigoi wanakufa kama binadamu tu , lakini wanaishi muda mrefu sana, lakini hata hivyo ni wachache sana wa kufikisha zaidi ya miaka elfu moja , kutokana na kwamba wengi wao hutegemea zaidi vipawa vyao vya kulala muda mrefu ili kurefusha maisha. Mfano Prince Sebastiani mpaka kufikisha umri aliokuwa nao ni kutokana na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kulala muda mrefu na kupigana pale anapoamka ili kujilinda , la sivyo isingekuwa rahisi kuwa hai mpaka leo hii”
Regina aliishia kumeza mate mengi na kujihisi mambo ambayo alikuwa akisikia muda huo yalikuwa ni ngumu sana kuamini. Hakuamini Vampire kama huyo ameweza kuishi miaka yote hio kwa kutegemea usingizi tu.
Ikumbukwe Strigoi wanachukuliwa kama wafu , lakini uhalisia sio wafu bali wanakuwa katika hali ya usingizi tu kwa muda mrefu. Mfano Prince Sebastiani anaweza kweli kuwa na umri wa miaka zaidi ya elfu moja lakini asilimia themanini ya umri wake ameutumia kulala usingizi mzito.
“Hakuna asie na mwisho , nadhani nikiongea kauli hii wengi wataelewa ninachomaanisha. Hatua inayofuata nakwenda kumkaribisha mwanamke ambae ameachiwa majukumu makubwa na mume wake na kujisimika katika hadhira ya watu wengi kupitia uwezo wake. Kiongozi mkuu wa The Odd ones na mwakilishi mkuu wa mamajusi wa nuru. The White Queen, Madam Silvia Somerset”
Hatimae muda huo alionekana mwanamke mrembo sana alievalia mavazi ya rangi nyeupe akipandisha kwenye jukwaa. Umbo lake na uzuri wake ulivutia wengi mno.
“Yule mwanamke ni mrembo mno. Mume wake amefariki?”Aliuliza Regina ambae alishindwa kujizuia kushangazwa na uzuri wake.
“Ms Regina huyu mwanamke kwa namna moja ama nyingine mna ukaribu..”Aliongea Helena akiwa na tabasamu la uchokozi.
“Unamaanisha nini?”
“Utakuja kujua baadae ukipata nafasi”Aliongea Helena akiacha kumuweka wazi Regina. Ukweli moja ya sababu ya kuitishwa kwa mkutano mkuu wa Magwiji ni huyo mwanamke pia.
Ijapokuwa Silvia alikuwa na uwezo mkubwa wa mapigano na kuwa maarufu lakini siku zote hakuwa akionyesha uwezo wake zaidi ya kujificha nyuma ya aliekuwa mume wake. Kwasababu ndio kwa mara ya kwanza anasimama kama kiongozi wa The Odd ones watu wengi walitaka kuona uwezo wake halisi.
Silvia mara baada ya kufika kwenye steji aliishia kuwatingishia vichwa wenzake waliotangulia na kisha alienda kukaa katika nafasi yake.
“Gwiji anaefuatia anatokea ndani kabisa ya Amerika ya Kusini , gwiji mwenye uwezo wa kuicha nafsi yake kuzurura kuzunguka msitu wote wa Amazon. Gwiji anaejitanabahisha kutokufa milele. Nawaletea kwenu Mr Skeleton kutoka Amazoni.Jeshi la mtu mmoja”Aliongea Mshereheshaji.
Palepale alionekana mtu alievalia mavazi ya kitamaduni ya asili ya Red Indiani huku kila kiungio cha mwili wake alikuwa amejifunga kwa kuning’iniza mifupa, ya aina mbalimabli kuanzia ya watoto mpaka wazee na pia ya wanyama na ndege mbalimbali. Mwonekano wake hakika ulitisha sana.
Haikuonekana sura yake kutokana na rangi alizopaka usoni na pia ngozi yake haikuwa ya kawaida , ilikuwa ni kama vile inaelekea kuoza. Regina mara baada ya kumuona mtu huyo sura yake ilikunjamana.
“Usiwe na wasiwasi, yule anafahamika kama Mchawi wa msitu wa Amazoni, ile mifupa haijatoka katika miili ya binadamu hai bali kutoka katika maiti zao”Aliongea Helena.
“Mshereheshaji kasema mtu huyu ni jeshi la mtu mmoja. Anamaanisha nini?”
“Ni rahisi sana , inamaanika kupitia uchawi wake kupitia ile mifupa anaweza kuamsha wafu na wanyama waliokufa na kupigana kwa ajili yake. Akiwa eneo la vita kadri watu wanavyokufa ndio namna anavyozidi kuwa na nguvu”.
“Unamaanisha kama White Walker wa GOT?” GOT ni filamu ya Game of throne.
“Haha.. kumbe unaangalia filamu! Ndio ni kama ulivyokisia”
“Kwanini hawa Magwiji kila mtu ana stori ya kuogopesha?”Aliuliza Regina.
“Anaefuatia sio wa kuogopesha na kubwa zaidi anatokea ukanda wa Afrika ya mashariki mathalani nchi unayotokea”Aliongea Helena na kumfanya Regina kushikwa na shauku akitaka kujua ni nani
“Mabibi na mabwana. Kabla ya White Queen kuingia katika orodha ya magwiji kumi , anaefuatia alikuwa ni mwanamke pekee kushikilia hadhi ya ugwiji. Anamiliki damu ya kifalme yenye maajabu ya moto. Anaweza kuunguza chochote. Moto ni wa kuogopwa na binadamuy wa kawaida lakini kwake ndio chanzo cha uhai. Namkaribisha kwenu binti mdogo kutoka Afrika mashariki . Nyakasura ,Miss Phoenix Girll”
Mara baada ya kuongea , palepale alionekana Nyakasura aliekuwa katika mavazi yake ya aina moja ya rangi nyekundu, hadhira haikuwa nyuma kumpokea kwa makofi mengi na vifijo.
Nyakasura siku hio licha ya kwamba hakubadilisha rangi , lakini alikuwa amevalia gauni refu lenye chata la ndege wa maajabu. Huku akiwa ameachia nywele zake ndefu.
Regina alishangazwa na mwonekano wa Nyakasura kwa kiasi kikubwa.
“Huyu msichana ni mdogo mno na yeye pia ni Gwiji?”
“Kwani humjui! Huyu ndio mlinzi mkubwa wa nchi yenu chini ya kitengo cha Malibu. Regina unaonekana kuna mambo mengi sana ya siri ambayo huyafahamu”
Regina alijihisi kuwa mjinga , aliishia kuzungusha macho yake kuangalia watu namna walivyokuwa katika majadiliano makali.
Ukweli kama sio uwepo wa Helena karibu yake asingewewza kufahamu lolote.
Walikaribisha jumla ya Magwiji nane na ni wawili tu ambao walikuwa wamebakia kutambulishwa.
Mshereshaji, ilikuwa ni kama makusudi kwani aliacha kuongea kwa nusu dakika hivi huku akiiangalia hadhira kabla ya kumtaja mtu wa tisa. Na muda uleule aliweka maiki na kuongea.
“Mtu anaefuatia kutambulishwa , jina lake halisi watu wengi hamlifahamu , lakini kulingana na mtiririko wa Alfabeti anashika nafasi ya tisa. Ni mtu wa pekee sana kulingana na sifa zake , kwasababu kwa kipindi cha miaka mitano ameacha doa kubwa la wino mzito ndani ya ulimwengu wa giza.
Kuonekana kwake kumebadili muundo wa zaidi ya miaka mia moja ya ulimwengu wa siri. Kutokana na kughairishwa kwa Mkutano mkuu wa Magwiji katika baraza la maksi lililopita chini ya maombi ya wanachama wa jumuia, nitachukua nafasi hii kuelezea kwa kina utambulisho wake kama njia ya kuonyesha heshima juu ya huyu Gwiji mwenye umri mdogo kabisa!”
Mara baada ya maneno hayo kusikika , asilimia kubwa ya wahudhuriaji wa mkutano huo walishamjua ni nani. Watu wengi hususani wale ambao ni binadamu wa kawaida katika ulimwengu wa giza walijawa na machozi katika macho yao na hamasa ya juu mno. Wote macho yao yalikuwa ni katika mlango wa kutokea kwenye juktwaa kwa hamu kubwa ya kumuona huku wakijiandaa kumshangilia.
“Alikuwa na miaka sita pekee alipoletwa na kuingizwa katika kundi la The Odd one. Alithaminiwa sana na mtawala mkuu Mr Black na hatimae kukidhi vigezo na kuwa mwanafunzi wa Black Emperor wa kwanza…Aliweza kupata hadhi ya Selafi akiwa na umri wa miaka kumi na tatu huku akiwa katika daraja la juu sana la mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi. Katika kipindi chake cha mafunzo ya nishati alifanikisha kuishambulia kambi ya kundi la kimauaji la Kichwa cha Faru na kumuua kiongozi wao. Alipofikisha umri wa miaka kumi na sita alivunja rekodi ya ufanisi mkubwa wa kuua na wingi wa watu aliowaua katika vita. Katika umri wa miaka kumi na saba alivunja rekodi ya kuwa Bounty Hunter aliefanikisha kuwinda watu wengi duniani na kuwapata. Watu wengi walimuona kama mwiba katika harakati zao na kumtegea kila aina ya njama lakini hawakuweza kumzuia. Baada ya kutimiza miaka kumi na nane aliachana na Uanajeshi pamoja na uninja na katika hali isiotegemewa akavunja tena rekodi ya kuokoa raia wengi katika maeneo ya vita . Mwaka huo huo kwa ajili ya kupata uhuru wake alimuua Gabriel, Mkuu wa Mahakama takatifu na kuamua kujitegemea kutoka kwa Mtawala wake.
Ndani ya mwaka mmoja na nusu wa kujitegemea aliweza kukusanya wafuasi na kuingia katika vita kali na mahakama takatifu. Mapigano yalikuwa makali na yaliosambaa dunia nzima ya ukubwa tofauti tofauti bila ya kushindwa. Mwaka mmoja baadae Mahakama ya Baraza la giza wakaamua kumuunga mkono na kulazimisha watu wa Holy Court kukimbia. Kwa nguvu zake aliweza kufufua makundi ya Baffodil na Barhams na kuzima makundi mengi ya daraja A na B ili kukuza hadhi ya makundi yake….”
Wakati wote mshereheshaji akiwa anaongea , Azzle , Asmuntis , Mameni, Berly, Leviathani na wengine waliokuwa wamekaa katika siti chini ya jukwaa pamoja na wanachama wa Barhams, Baffodil na Seas Demons, macho yao yaligeuka na kuwa mekundu kwa furaha kubwa.
Upande wa Regina ambae alikuwa akifuatilia tukio hilo kwa ukaribu kabisa alijikuta akitetemeka kwa sifa hizo. Ijapokuwa hakujua zaidi ya maneno yaliokuwa yakiongelezwa yalikuwa yakimaanisha nini . lakini maelezo hayo yalitosha kumuonyesha huyo Gwiji mwenye sifa hizo alikuwa ni hatari kiasi gani.
Alijikuta akiwa na shauku na kutaka kumjua ni Gwiji gani mwenye sifa nyingi namna hio.
Upande wa jukwaa, Mika, Silvia na wengine walikuwa na mwonekano usioelezeka katika nyuso zao. Wanachama wa mahakama takatifu na watawala wa zama zile walionekana kutofurahia . Lakini walijua hata kama MC asingetaja sifa hizo watu walikuwa wakizijua.
Mshindi ni mfalme na alieshindwa ni mhalifu, hio ndio ilikuwa sheria ya ulimwengu wa siri bila kujalisha ulikuwa ukipigania nini. Mwenye nguvu ndio mwenye haki ya kuongea. Hivyo kwa watu wenye madaraka makubwa kama hao waliishia kuinamisha vichwa vyao chini huku wakijiambia kushindwa kwao ni kwa muda mfupi tu, kisasi kinakuja.
“Katika miaka miwili yeye na wafuasi wake walitembea sehemu mbalimbali ulimwenguni na kuwakomboa watu walionyimwa haki na uhuru wao wa kuishi. Aliharibu mashirika mengi ya giza na kupandisha mengi, Ari yake ya kutokukubali kujisalimisha imewapa watu wengi motisha ya kupambania haki zao na kuathiri mpangilio mzima wa utendaji wa ulimwengu wa giza. Vita hii iliodumu kwa miaka miwili imebatizwa jina la Vita takatifu ya ukombozi na kufanya watu wengi kumkubali lakini yeye mwenyewe anajihisi ni mtu aliwaasi binadamu na anapostahili ni kuzimu pekee na kupitia msimamo huo,Nuru ilimpotea katika uso wake na Giza likamwangukia na kumfanya adondokee kuzimu na hatimae jamii ya watu kumi na mbili wenye dhambi zisizosameheka ikazaliwa. Jamii ya watu wa Karibu Kuzimu ya daraja S ikazaliwa na kubatizwa jina la INFERNO. Nichukue nafasi hii kumkaribisha kwenu. Lucifer, kiongozi wa Karibu Kuzimu(Inferno) ambae amerudi tena. Anaefahamika kwa jina lake maarufu na la siri,Devin-rth”
Comments