SEHEMU YA 204.
Ngumi kwa Ngumi
Ilikuwa ngumu kutafsiri hali ambayo ilitanda ghafla ndani ya eneo hilo kutokana na mabadiliko ya Hamza, ilikuwa ni kama alikuwa ametawaliwa na kivuli ambacho hakikuwa cha kawaida na kusababisha hali ya msisimko ambayo ilikuwa haielezeki.
Ingawa macho yake yalikuwa katika hali ya ukawaida lakini ki-uhalisia hayakuwa kawaida kabisa kwa namna yalivyokuwa yakimwangalia Gonzalez.
Zaidi ya watu elfu therathini ambao walikuwa wameshitushwa na ngumi nzito ya Gonzalez kwenda kwa Asmuntis, walijikuta wakinyamaza haraka mara baada ya kukumbwa na msisimko ambao Hamza alikuwa akisambaza.
Karibia watu wote waligeuza macho yao na kumwangalia Hamza , huku wale waliokuwa waoga wakianza kutetemeka.
Kila mmoja alikuwa na wazo moja tu , kwamba Kundi la Metal Tide limefikia mwisho wake.
Mabadiliko ya Hamza yalivutia pia watu waliokuwa kando yake. Magwiji hao tisa waliokuwa katika jukwaa walionekana kuwa katika hali za kutotaka kuingilia kabisa suala hilo , wengine walionekana kuwa katika mkao wa hamu ya kuona kile kinachokwenda kutokea.
Meza za chini karibu na jukwaa lao , viongozi wa Baraza la Maksi na wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali , walikuwa pia wamekaa wakiangalia kwa shauku kubwa.
Kanuni ya ulimwengu wa giza mara nyingi ni kwamba dhaifu anapaswa kumheshimu mwenye nguvu. Hata kama kuwe na sheria ili mradi una nguvu za kutosha sheria inaweza kukusamehe baadhi ya makosa. Hivyo kwasababu Gonzalez ndio alietaka kujihima na Hamza hakuna ambae alipanga kuzuia . Lakini sasa mara baada ya Hamza kutoa msisimko wake , watu wengi walimwangalia Gonzalez kwa macho ya huzuni.
Gonzalez alijikuta mwili wake ukikakamaa. Alikuwa katika hali ya mshituko na viashiria vya woga vilevile vilimuonekana , hata hivyo mara baada ya kukumbuka Hamza hakuwa na nishati zozote za mbingu na ardhi, ujasiri wake uliongezeka kwa mara nyingine.
“Hatimae hasira zimekupanda! Nilishachoka kusubiria mimi , nilidhani utaendelea kujificha”Aliongea Gonzalez huku akitoa tabasamu la kumkejeli Hamza.
Hamza aliishia kutoa pumzi nyingi kama vile amepatwa na ahueni lakini macho yake yaliokuwa na ukali kama kisu hayakupoa.
“Unaweza kusema kweli sina vigezo vya kukaa hapa kwasababu haujawahi kupambana na mimi na haunijui vizuri. Lakini umekosea kuwajeruhi ndugu zangu”Aliongea Hamza.
Sura ya Azzle ilibadilika palepale katika hali ya hofu na alijikuta akiharakisha kutaka kumzuia Hamza.
“Bosi usiwe na haraka. Huyu hana hadhi ya kupigana na wewe”Aliongea kwa nguvu Azzle na kumfanya Mameni aliekuwa amekaa pembeni kukunja sura.
“Unaongea ujinga gani wewe Mhunzi. Yaani mtu kamuumiza Mchafu halafu unataka aendelee kumwangalia tu? Sio hivyo tu hata wewe jana uliumizwa pia”
“Ni kweli. Mhunzi na Mchafu mbona siwaelewi, kwanini mnamzuia bosi kumshikisha adabu huyu mshenzi?”Aliongea Berly.
“Nadhani wanahisi wanadeni kubwa kwa bosi ndio maana, lakini hata hivyo deni letu kwa bosi ni la maisha. Haitokuwa mbaya akiendelea kutudai”Aliongea Leviathani akiunga mkono.
Azzle , Asmuntis na Black Fog wote waliishia kuangaliana kwa hali ya wasiwasi. Walikuwa na wasiwasi wa kuongea ukweli kama bosi wao hakuwa na nguvu yoyote ya kupambana na Gonzalez.
Hamza alimalizia kuvuta moshi wa mwisho kutoka kwenye sigara na kisha palepale alitupia kipisi chini na kukikanyaga na kisha akatoka jukwaani kumsogelea Gonzalez.
Kila hatua aliokuwa akipiga ni kama vile mguu wake ni wa chuma kutokana na presha aliokuwa akizalisha na kuzidi kuugusa moyo wa Gonzalez.
Licha ya hatua za Hamza kutotoa sauti lakini kila akipiga hatua moja hatua zake zilisikika kuwa nzito katika vichwa vya watu kama vile walikuwa wakichanganyikiwa.
Watu wote waliokuwa katika Arena , walijikuta wakishindwa kujizuia na kumeza mate mengi huku wakijikaza kisabuni.
Gonzalez kwa sababu ambazo hazikuwa zikielezeka alijikuta akianza kupaniki huku jasho la baridi likichuruzika katika paji la uso wake.Alijiuliza nini kinaendelea? Kwanini huyu mtu ana mkandamizo mkubwa bila ya kuwa na nishati za mbingu na ardhi?.
Gonzalez hakutaka kukubali. Aliamini yeye ndio aliekuwa akitisha zaidi lakini kwanini Hamza aliekuwa mfupi alikuwa akimtisha bila hata ya kuwa na nishati ya mbingu na ardhi?.
“Mwili wa chuma!”
Gonzalez mara baada ya kuona mambo sio mazuri hakutaka kuchelewa na palepale aliongea kwa nguvu kuita mwili wake wa chuma na palepale mwili wake ni kama unaota magamba ya chuma na ndani ya sekunde tu ulibadilika.
Misuli katika mwili wake ilikua , umbo la mwili wake liliongezeka katika kimo kingine kabisa. Alikuwa ni kama kifusi cha mtu, kama mnyama mkali ambae hajawahi kuonekana katika uso wa dunia.
Gonzalez mikono yake ilitingishika mara baada ya kupiga hatua na kukanyaga ardhi huku akisababisha eneo hilo kutetemeka.
“Aaaahhhh!!”
Gonzalez alijikuta akibweka kuelekea angani. Ukubwa wake wa kimwili ulionekana kumziba Hamza aliekuwa mdogo. Kwa kuangalia tu umbo lake ilikuwa ikiogopesha sana kwa mtu wa kawaida kusogea karibu.
“Jamani eh , ndio lenyewe hili. Its fu*king giant, chuma chuma kweli!!”
“Kuamua kutumia uwezo wake wote katika hatua ya mwanzo ya pambano. Inaonyesha ni kiasi gani Gonzalez amedhamiria kupigana na mfalme wa kuzimu”
“Nimesikia umbo lake la chuma linaweza kuhimili kombora. Hata kama aumie anao uwezo wa kujiponyesha kwa kunyonya elementi za chuma tu”
“Sidhani hili pambano litaisha vizuri. Mkumbuke pia Lucifer uwezo wake ulithibitishwa na vita takatifu kati ya The Odd ones na watu wa Jumba takatifu na amepigana nao kwa zaidi ya miaka miwili. Hata kama Gonzalez alitamani kuwa katika nafasi ya ugwiji naona angechagua mtu mwingine wa kupambana nae”
“Wewe nae umekuwa mjinga? Unadhani ni rahisi kudili na wale wataalamu wengine. Tumchukulie tu Phoenix girl ambae ndio mdogo pale , lakini ana miliki moto , unadhani Gonzalez atamfanya nini? Njia rahisi alioona ni kumchagua Lucifer basi”
“Huna haja ya kuongea sana. Kati ya Adept’s, ni Gonzalez ambae ameweza kufikisha uwezo wake katika hatua ya juu zaidi huku ikichangizwa na mafanikio yake ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi na kufikia daraja la ukamilifu wa mwili. Mimi naamini anatosha kushindana na gwiji yoyote pale”
“Naunga mkono hoja , hata kama asishinde Lucifer atapata shida sana kupambana nae na kumdhibiti”
Hadhira ilikuwa katika majabizano ya kina kuhusu pambano linalokwendqa kutokea. Wengi waliomfahamu Gonzalez walijuwa uwezo wake sio wa majisifu tu , alikuwa na uwezo haswa.
Wakati huo Gonzalez alikunja ngumi yake huku akiwa ameng’ata meno kana kwamba kukunja ngumi huko kulikuwa kukimsababishia maumivu.
“Lucifer kwanini unaficha uwezo wako wa nishati za mbingu na ardhi kufikia hatua hii?”
Hamza alitembea mpaka kufikia mita kama kumi hivi mbele ya Gonzalez na aliachana na dharau zake na kuelekeza macho kwa washikaji zake.
“Msaidieni mchafu apumzike. Siku nyingine usiwe una kurupuka”Aliongea Hamza.
“Bosi ..”Azzle alitaka kuongea baada ya kukumbuka kitu lakini aliishia kutoa macho tu asijue namna ya kuendelea.
Asmuntis aliishia kutingisha kichwa chake pekee , kama vile alikuwa akimuomba Hamza asije kufanya jambo la kijinga. Black Fog na yeye alikuwa na wasiwasi mno kiasi kwamba alitamani kulia. Huku akimwangalia Hamza kwa macho ya kubembeleza.
Walijua fika kama Hamza atapigika siku hio mioyo yao itavunjika vipande vipande na ndoto zao pia zingesambaratika pamoja na imani waliokuwa nayo kwa muda mrefu kuvurugika.
Hata hivyo Hamza, licha ya kuona namna walivyokuwa na wasiwasi , aliishia kutoa tabasamu hafifu na kisha alimgeukia Gonzalez palepale.
“Kudili na mtu kama wewe sihitaji nishati za mbingu na ardhi kabisa”Aliongea Hamza lakini maneno yake yaliamsha zogo kutokana na kutokuamini kama Hamza anaweza kupambana na Gonzalez bila ya kutumia nishati.
“Ni kweli hataki kutumia nishati za mbingu na ardhi hata kidogo au anatania?”
“Labda anapanga kutumia nguvu za mwili wake pekee kupambana na jitu la chuma. Huku si kuji..”
“Sidhani, anajigamba tu , hakuna mtu ambae anaweza kufanya hivyo , hata magwiji wenzake hawawezi kuwa na ujasiri wa aina hio”
“Tangu lini Lucifer akamdharau adui yake. Akiongea kitu maana yake amekwisha mpima adui”
Makelele ya watu kujadili kauli ya Hamza yalikuwa mengi sana. Kuna waliohisi Hamza ana majigambo sana , wengine kauli y ake iliwapelekea kuhisi damu zao kuchemka kutaka kuona kile kinachokwenda kutokea.
Regina aliekuwa katika viti , alikuwa na wasiwasi mno kiasi cha kufanya mikono yake kumtoka jasho wakati huo Helena alionekana kuwa na furaha kubwa. Alijua kwa kauli ya Hamza kutotaka kutumia uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi basi kile walichootea ni sahihi. Hamza hakuwa na uwezo wowote.
Upande wa Gonzalez kusikia maneno hayo ya dharau kutoka kwa Hamza hasira yake ilimpanda maradufu. Alijihisi ni kama anachukuliwa poa.
“Haha.. kwa mtazamo wangu sio kama hutaki kutumia uwezo wako wa nishati , bali uwezo huo huna. Vigezo vya kuendelea kuwa Gwiji huna kabisa na leo hii nipo hapa kwa ajili ya kuwaonyesha watu wote namna ulivyo dhaifu”Aliongea Gonzalez.
Magwiji tisa waliokuwa wakisikiliza maneno hayo ukiachana na Mathias Huge wa Binamu na Nyakasura , wote walimwangalia Hamza kwa shauku, wakijiuliza ni jambo gani Hamza alipanga kufanya.
Kuhusu Hamza kuwa ama kutokuwa na nishati za mbingu na ardhi hilo halikuwaumiza sana vichwa. Kwa levo zao walikuwa wakielewa katika mapigano sio tu nishati za mbingu na ardhi zinazoweza kumfanya mtu kuwa na nguvu.
Hamza upande wake hakuonekana kuathirika kabisa na maneno ya Gonzalez na alikuwa amesimama tu katika eneo moja.
“Nitakupa nafasi ya kushambulai wa kwanza”Aliongea Hamza.
“Mh! Bado unajifanya mjuaji?”
Gonzalez alijihisi hasira huku akijiambia huyu bwana kwanini anamdharau hivi , ni muda wa kumshikisha adabu na kupanda daraja na kuwa gwiji wa dunia. Kufikiria vile palepale nishati za mbingu na ardhi katika mwili wake zilianza kujikusanya kufikia katika hatua ya juu kabisa.
Mara baada ya kusambaza wimbi la nishati zile , wawakilishi ambao hawakuwa na mafunzo kabisa ya nishati za mbingu na ardhi walijikuta wakihisi mioyo yao ni kama inataka kuwatoka.
Baadhi ya magwiji pia walimwangalia Gonzalez kwa namna ya kumkumbali.
“Yeah! Naona Gonzalez sio wa mchezo mchezo” Aliongea Phantom Oleg.
“Kwa mtazamo wangu uwezo wake wa kinishati bado ni dhaifu”Aliongea Holy Knight, Auland, ambae muda wote alikuwa kimya.
“Auland kwa kujilinganisha na wewe unadhani ni watu wangapi watakuwa na uwezo wa kinishati dhaifu? Gonzalez anaonekana kuwa dhaifu kwasababu ya umri wake pekee , kama angekuwa kijana angekuwa zaidi ya pale”Aliongea Mikaeli.
“Kuna mtu kaniambia kuwa jana Gonzalez alihimana kwa muda mfupi na Miss Nyakasura. Vipi unaonaje kuhusu uwezo wake?”Aliuliza Huge akimwangalia Nyakasura.
“Unajiita msomi lakini vilevile ni bosi wa Binam. Inamaana hujui uwezo halisi wa Gonzalez au unanijaribu?”Aliongea Nyakasura akiamini kupitia teknolojia ya jicho la Umbea ya watu wa binamu lazima wanataarifa zote juu ya uwezo wa Hamza na Gonzalez na swali lake limekaa kisanifu tu.
“Tukiachana na uwezo wake wa nishati , tuzungumzie kwanza uwezo aliozaliwa nao kama ni dhaifu au ni mkubwa. Swali hili nadhani mtu ambae anaweza kutujibu ni Raisi wake. Mr Air unazungumzia vipi kuhusu uwezo wa Gonzalez?” Aliongea mrembo Silvia.
Mr Air ambae kilichokuwa kikionekana ni koti pekee lililojishikiza hewani sauti yake ilisikika.
“I don’t judge others” Alijibu akimaanisha kwamba yeye sio hakimu wa wengine.
“Haha.. Hakika wewe ni rais wa wasio wa kawaida. Tabia yako ni ya tofauti sana kuliko wengine wote hapa”Aliongea Oleg huku akicheka.
Kundi hilo la Magwiji hakuna ambae alikuwa na wasiwasi , waliongea kwa kucheka tofauti na watu wengine, lakini kwa wakati mmoja walichokuwa wakitaka kuona ni uwezo aliokuwa nao Gonzalez. Ni kama vile hawakuwa na wasiwasi wa Hamza kushinda ila walitaka kujua kama Gonzalez anazo nguvu za kuweza kuhimana vyema na Hamza au ni mdebwedo.
Muda huo, Gonzalez alikuwa amekamilika katika kukusanya kila nguvu iliokuwa katika mwili wake na uwezo wake wa kimapigano ulikuwa katika kilele.
Aliishia kukunja ngumi na kisha palepale alipiga hatua moja kwenda mbele huku akikusanya upepo.
Alikuwa ni kama roboti ambalo lilimsogelea Hamza kwa kasi kutaka kumpiga. Spidi yake na msukumo wa mwili ilikuwa ni kama vile ni mti unaodondoka kutokana na mmomonyoko wa udongo.
Ki-ufupi ni kwamba licha ya Gonzalez kuwa na mwili mkubwa ila hakuwa slow kabisa , kila hatua aliokuwa akipiga ilileta mtetemeko.
“Ngumi ya chuma kizito!”
Gonzalez aliongea kwa nguvu huku ngumi yake ikiwa ni kama jiwe FATUMA wakati alipokuwa akimlenga Hamza.
“Bosi!”
Chini ya steji Asmuntis na Azzle alijikuta wakishindwa kujizuia na kupiga makelele wakiomba Hamza kufanikiwa kuzuia ngumi ile. Hata hivyo mwanzo mwisho Hamza mwonekano wake ulikuwa katika hali ya utulivu kabisa na mara baada ya kuona shambulizi lile aliishia kuinua mkuno wake
Muda ule ilikuwa ngumu kwa watu kuona nini kimetokea na hio ni kwasababu spidi ya Gonzalez ilikuwa kubwa sana. Karibia watu wote walijikuta wakibana pumzi huku wengine wakifumba macho wakiamini Hamza anakwenda kugeuzwa nyama. Lakini sasa ndani ya sekunde, kile kilichotokea kiliwafanya watu kuwa katika hali ya butwaa .
“BOOM!”
Katika hali ya kushangaza Hamza alikuwa amenyanyua mkono wake wa kushoto na kuizuia ile ngumi ya Gonzalez na kiganja cha mkono kama vile ni golikipa anaejaribu kubetua mpira.
Muda ule ngumi ile ya Gonzalez ilipogusana na kiganja cha Hamza sakafu iliokuwa chini ya miguu ya Hamza ilititia na kusababisha mtikisiko mkubwa na haikuchukuwa muda steji ilianza kuyumba kudondoka kwenda chini.
Hamza alikuwa amesimama vilevile , licha ya kwamba miguu yake ilikuwa imedidimia ndani, hakuonyesha ishara za kusogea kabisa.
Mawe mazito yaliokuwa yameshikilia nguzo za jukwaa lile yalikosa mhimili na kuachia na muda ule chuma kilifyatuka kumsogelea Hamza kutaka kumtoboa lakini Hamza alikuwa mwepesi kwani kabla hakijamdhuru aliweza kukidaka na mkono wa kulia.
Mwanzo mwisho Hamza hakuonyesha ishara yoyote ya kutumia nishati za mbingu na ardhi , lakini amefanikiwa kuzuia shambulizi zito la Gonzalez.
Mara baada ya vumbi kutulia , Gonzalez alijikuta akimwangalia Hamza kwa macho ya hisia mchanganyiko. Alianza kuhisi ubaridi wa aina yake ukisambaa mgongoni.
“Hili.. inawezakana vipi?”
Gonzalez macho yalimtoka , akishindwa kuamini kile anachoona, alihisi ukatili wa uhalisia na hisia za kushindwa zilimvaa palepale na kumfanya fuvu la kichwa chake kuanza kumuwasha.
Baadhi ya malijendi waliokuwa katika jukwaa waliishia kusinyaza macho wakiangalia tukio hilo kwa kutokuamini , huku wengine wakiwa katika hali ya kutafakari.
Upande wa Azzle , Asmuntis na Black Fog wote walikuwa katika hali ya bumbuwazi huku wakiwa wameachama kwa kushindwa kuamini.
Walikuwa washaamuini balaa linakwenda kutokea katika steji ile , lakini uhalisia uliwafanya kuwa katika hali ya kutamani kulia kwa furaha kubwa.
Mameni , Berly , Leviathani na wengine ambao walikuwa wakijua Hamza hakuwa na tatizo walijikuta wakishangaa pia maana hawakuamini kama Hamza atakuwa na uwezo zaidi ya vile walivyokuwa wakimkadiria. Walijikuta wakishikwa na msisimko wa hali ya juu na kupiga makelele ya furaha.
Hata Asmuntis ambae alikuwa ameumizwa alijikuta nguvu zikimrejea na kuanza kupiga makelele ya kuita jina la Hamza.
Mashabiki wote wa Hamza walisimama na kuanza kushangilia kwa kumuita majina tofauti tofaati , wengine walitaja kwa nguvu jina la Divini-rth , wengine Lucifer , wengine Prince of hell.
Washikaji zake Hamza damu ziliwachemka huku wakipata msisimko wa furaha kwa namna Hamza anavyowaheshimisha. Yale makisio watu waliokuwa nayo yalipotea mara moja na sasa ni kama walitegemea kuona mapigano ambayo yamebalansi.
“Oh my god! Ule sio ubinadamu , kawezaje kuzuia lile shambulizi?”
“Unadhani kwanini anaitwa Gwiji. Maana yake uwezo wake sio kitu cha kuotea”
“Najihisi vigoti kunilegea .. ni hatari sana”
“Gwiji ni Gwiji siku zote. Gonzalez alichokosa ni uzoefu na ninavyoona hapa Lucifer alikuwa akimpotezea kwasababu alijua ni mdogo sana kwake la sivyo angemmaliza muda mrefu tu”
“Upo sahihi, utofauti wao wa nguvu ni mkubwa mno , pale tu hajatumia kabisa nishati za mbingu na ardhi na ameweza kuhimili”
Mabishano hayo yaliwafikia watu wa Metal tide na yalikuwa ni kama visu vilivyochoma mioyo yao.
Helena na kundi lake walikuwa na sura mbaya sana huku wakishindwa kuzuia hisia za kuangaliwa na macho ya dharau kutoka kwa watu.
Regina mara baada ya kuona jambo lile nafsi yake ilitetemeka kwa sekunde. Hakuamini mwanaume aliekuwa juu ya steji ambae watu wanamshangilia kwa mayowe mengi ni mume wake. Kulikuwa na hisia zisizoelezeka katika moyo wake. Baadhi zilikuwa za furaha , baadhi zilikuwa za kujivunia na zingine zilikuwa ni za kuridhika. Lakini hata hivyo hisia nyingine zilikuwa ni za kupoteza , wasiwasi na kujutia.
Muda ule alijihisi kitu cha baridi kikugusa kiuno chake na kumfanya Regina kugeuka na aliweza kumuona Helena ambe ameshatoa kisu chake na alikuwa amemuwekea kiunoni.
“Miss Regina acha kujiona ni mwenye bahati..”Aliongea Helena akiwa na uso uliojaa usiriasi.
“Huwezi shinda”Aliongea Regina kwa kujikaza.
“Hata kama ila wewe si upo , mwanamke aliekuchagua na kukuoa”
“Na yeye yupo, mwanaume niliemchagua”Aliongea Regina akimwangalia Helena kwa macho makali.
Helena kutokana na kauli ile alijikuta akishikwa na mshangao. Alikuwa na mwonekano usioelezeka na aliishia tu kukaa kimya.
Katikati ya ukumbi huo , hali ilikuwa patashika . Gonzalez alionekana kutojidhibiti huku mkono wake ulionekana kutetemeka. Kama sio mwili wake wa chuma pengine damu ingeshamkauka.
“Wewe.. Ni shetani wa aina gani wewe?” Aliongea Gonzalez huku akimwangalia Hamza.
“Shambulizi lako limekwisha , sasa ni zamu yangu”Aliongea Hamza.
Kabla Gonzalez hajashituka Hamza alikuwa ashachukua hatua , mkono wake wa kulia alikunja ngumi , huku mwili wake ukiegamia mbele na mkoo wake ulirudi nyuma mara moja na kisha ukaelekea mbele.
Misuli katika mwili wake ilitanuka , ikifuatishana na mnyongeo wa mwili na kufanya nguvu ya mikono yake kuzidi kuongezeka.
Hamza mwili wake ulikuwa na muunganiko wa kimisuli wa kutosha mno, ilikuwa ni kama alikuwa akielekeza misuli yake namna ya kujipanga ili kutoa nguvu ya kutosha katika ngumi yake.
Juu ya jukwaa , Auland , Sebastian na Mikaeli walijikuta wakiwa katika mshituko mkubwa.
Kupitia macho yao waliweza kuona namna misuli ya mwili wa Hamza ilivyokuwa ikimwitikia.Ilikuwa ni tofauti na kwa watu wa kawaida ambao waliona shambulizi la Hamza ni la kawaida sana.
Kabla ya Gonzalez kushituka ngumi ya Hamza ilitua katika eneo la tumbo lake na ile inagusana na mwili , Gonzalez hakujisikia vizuri hata kidogo , lakini sasa mara baada ya nguvu zote za mwili za Hamza kukusanyika katika ile ngumi , Gonzalez alihisi ni kama vile ni volkano inakaribia kulipuka na kujikuta akishangaa mno.
“Bam!!”
Na sauti kubwa ya kishindo, mwili wa Gonzalez uliokuwa mkubwa ulipanda hewani kwa namna ya kufyatuka kama mpira.
Ilikuwa ikishangaza kwasababu mwili wa Hamza ulikuwa ni zaidi ya mara tatu ya mwili wa Gonzalez , lakini kupitia ngumi yake tu alifanikisha kumfyatua Gonzalez.
Watu elfu therathini waliishia kumwangalia Gonzalez akipokea shambulizi lile na kupaa hewani na kisha kurudi chini kama furushi na kutengeneza shindo nzito.
“Mmeona sasa , ngumi moja tu jitu lipo hoi”
“Haha.. hii inathibitisha kabisa utofauti uliopo ni sawa na mbingu na ardhi. Hatari sana hii”
Azzle na wenzake kuona jambo lile walijikuta wakiruka tuka kwa kushangilia
“Bosi mtu hatari sana. Hii nguvu alioonyesha ni zaidi ya kipindi kile”Aliongea Mameni huku akicheka kwa furaha.
Azzle , Asmuntis na Rhoda walikuwa katika hali ya butwaa.
“Bosi … Inamaana bosi hakupoteza uwezo wake?”Aliongea Asmuntis kwa kiwewe.
“Mchafu usiniambie ulikuwa hujui lolote? Ni kweli bosi hana nishati za mbingu na ardhi na anatumia mbinu tofauti ya nishati?”
“Nini!”
“Kuna mbinu nyingine ya kumfanya binadamu kuwa na nguvu isio ya kawaida tofauti na nishati ya mbingu na ardhi!?”
“Bro.. inamaana ulikuwa ukinidanganya!” Black Fog alikuwa hasira na furaha kwa wakati mmoja.
Azzle na Asmuntis walikosa usemi na waliishia kuangalia majeraha yao pekee na kuishia kutingisha vichwa vyao kwa masikitiko wakiona kweli Bosi wao alijua kucheza na akili zao.
Muda huo Gonzalez ambae alikuwa amedondoka chini alikuwa ametoboa kwa mara nyingine eneo la steji huku eneo la tumbo lake kukiwa kumebonyea.
Gonzalez alijikuta akitetemeka kuanzia kichwani mpaka miguuni kama ana kifafa, wakati huo akijitahidi kujinyanyua. Hakuweza kujizuia na aliishia kutema damu nyingi chini.
Uwezo wake wa kichuma haukumzuia kutokuumia kwa viungo vya ndani, alichojua ni kugeuza ngozi yake pekee kuwa chuma na sio viungo vya ndani.
Muda huo Hamza alikuwa ameshasogelea mahali ambapo Gonzalez amedondokea na kumwangalia.
“Ngumi niliokupiga ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa ajili ya Asmuntis , inayofuatia ni kwa ajili ya Azzle ..”
Comments