SEHEMU YA KWANZA.
Saa mbili za usiku ndani ya jiji la mwanza katika barabara kubwa ambayo pia ni nzuri kimwonekano ikiwa inaelekea ndani ya Capri point linaonekana gari moja zuri sana aina ya Land cruiser Prado likiwa kwenye spidi sana wakati huo kulikuwa na manyunyu manyunyu ya Mvua zilizofanya usiku kuwa mtulivu ndani ya jiji lenye utajiri wa mawe ya kutosha.
Ndani ya hili gari anaonekana mzee mmoja wa makamo ya kawaida akionekana kuwa na miaka isiyopungua 50 hivi ila kwa sababu ya ukwasi aliokuwa nao bado alionekana kama ni kijana na ana safari ndefu ya kuufikia uzee. Alikuwa anarejea nyumbani kwake baada ya kutoka kwenye mihangaiko yake ya kila siku ili kuhakikisha familia yake inakuwa na furaha muda wote. Alikuwa anatamani sana afike nyumbani haraka baada ya kununua zawadi nyingi za kutosha alijua watazifurahia hao wana familia wake ambao aliwapenda kuliko kitu chochote kile. Akiwa kwenye hiyo furaha kubwa ndani ya gari gari yake alihisi kama kuna kitu amekikanyaga baada ya gari hiyo aliyokuwa nayo kuyumba nusu ipoteze uelekeo ikamlazimu kuisimamisha ghafla tu huku akiwa anahema kwa nguvu hakutarajia hilo tukio.
Aligeuka kuangalia nyuma alikokuwa ametoka ni kweli alikuwa amemkanyaga paka ambaye alikuwa anakatiza kwenye barabara hiyo majira ya usiku, yule paka baada ya kugongwa hakuwa na maisha marefu hata kidogo alipoteza maisha pale pale, hiyo ilikuwa ni ishara mbaya sana majira hayo ya usiku, alikuwa mtu wa dini sana huyu mzee hivyo hiyo ishara alijua wazi ni ishara mbaya na huenda kuna mambo hayako Sawa, kama imani yake inavyo mruhusu alifanya maombi kwa dakika tatu baada ya hapo aliliondoa gari kwa mwendo wa taratibu kuelekea nyumbani kwake, ile hamu na furaha kubwa aliyokuwa nayo tangu mwanzo ilimpotea kabisa usoni pake, akawa anawaza kuhusu tukio ambalo halikuwa zuri kwa dakika kadhaa zilizoweza kupita nyuma.
Alifika nje ya nyumba yake alisimamisha gari kama dakika tano akiwa ameulalia usukani akiwaza, alionekana anawaza mbali sana, aliichukua simu yake akaandika meseji ambayo haikuwa na maneno mengi sana akaituma mahali kisha akaizima hiyo simu. Alipiga honi kwenye hilo geti la nyumba yake, dakika moja mbele geti lilifunguliwa na mlinzi wale ambaye walikuwa wanataniana sana lakini siku hii ilikuwa ni tofauti kidogo kwa huyu mlinzi alijaribu kumtania bosi wake alinyamaza baada ya kumuona mzee huyo hakuwa sawa.
Jina lake halisi alikuwa anaitwa Jonson Malisaba, alikuwa amebahatika kupata familia kubwa na nzuri yenye furaha muda wote, alikuwa na mke wake aliyefahamika kama Anastazia Lewin pamoja na watoto watatu mmoja ambaye ndiye mkubwa zaidi alikuwa anaitwa Cleopatra Jonson na wawili ambao walikuwa ni wadogo kwa Cleopatra walikuwa ni mapacha wawili wakiume alikuwa anaitwa Lenovatus Jonson na wakike alifahamika kama Octavian Jonson pia humo ndani walikuwa wakiishi na mfanya kazi wakike pamoja na wa kiume bila kumsahau mlinzi wa getini, hawakuwa na utofauti kati ya wafanyakazi na wana familia wote waliishi kwa usawa na furaha kiasi kwamba kwa mgeni ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuwatambua kama wengine ni wafanyakazi tu wa ndani.
Kabla ya kurudi kwa mzee huyu familia ilikuwa ipo mezani wakati huo wakiwa wanaandaa chakula kwa sababu walijua baba mwenye nyumba muda wowote ule alikuwa anafika na ndiyo ilikuwa mida yake ya kurudi kila siku, hakuwa mtu wa kuchelewa kwa vile alikuwa anayajua vizuri majukumu yake kama baba bora wa familia.
"Octavian nenda ukamuamshe mwenzako maana naye kwa kulala lala huyo kisa anajua ndo wamwisho basi ndo anajidekesha wewe subiri nife atakoma mbona na itokee ndo aletewe mama wa kambo ataelewa" ni mama wa familia Anastazia Lewin mke wa Mr Jonson alikuwa akimtania binti yake mdogo Octavian ambaye alimtuma akamuamshe pacha wake wa kiume Lenovatus aliyekuwa amelala mpaka muda huo wanakaribia kupata chakula cha usiku huku akiwa anacheka.
"Mama kwa sababu yeye ni doto basi unaona kama mimi sio wa mwisho sitakiwi kudeka sawa tu" binti huyu mdogo aliye barikiwa kuwa na uzuri wa mama yake alimjibu mama yake meno yake yote yakiwa nje kwa kicheko kwa sababu alipenda sana kumtania sana pacha wake huyo huku mara kadhaa akiwa anamwambia kwamba hata afanyaje yeye ni dada yake kwani alimzidi dakika thelathini za kuzaliwa. Mapacha hawa walikuwa na miaka 14 kwa muda huo na dada yao Cleopatra alikuwa ana miaka 20.
"Heee heee nitokee hapa nawewe unamuonea wivu mwenzako sasa wewe nayeye si ni mtu mmoja" mama huyu aliongea tena na familia nzima ilikuwa kwenye kicheko kikubwa wakiwa na furaha sana.
"Hahahahahaaa mama na hao watoto wako mtanivunja mbavu zangu mie mwisho wa siku nishindwe kupata watoto mimi" dada mtu Cleopatra alimtania mama yake ambaye aliishia kutabasamu humu akiwa anapakua chakula kwenye hiyo meza.
"Anakuja lastborn wako huyo" Octavian baada ya kutoka chumbani alimtania tena mama yake huku akienda kukaa kwenye sehemu yake, mama yao alitabasamu sana alikuwa mtu mwenye furaha kubwa kubahatika kupata familia bora iliyojaaliwa amani na furaha ya kutosha.
Mr Jonson baada ya kuingiza gari ndani ya geti la nyumba yake alienda sehemu alipokuwa anatumia kupaki magari yake akalipaki vyema hilo ambalo alikuwa amelitumia hii siku, aligeuka ili aelekee ndani akawaite waje wamsaidie kushusha mizigo ndani ya hilo gari ila wakati anageuka alishangaa kuona bado geti liko wazi haikuwa kawaida kwani ilitakiwa akiingia tu humo ndani geti lifungwe ilikuwa ni usiku tayari na hilo geti halikutakiwa kuwa wazi.
Alitaka kuita jina la mlinzi wake huyo wa getini lakini alisita kidogo baada ya kuona mwili wa mtu umelala chini alihisi huenda mlinzi wake huyo amepatwa na tatizo hivyo anapaswa kumsaidia, alisogea hatua mbili akiwa anaelekea sehemu ulipokuwa huo mwili ila alisimama baada ya kuhisi kuna mtu hiyo sehemu ni kweli mbele yake walikuwa wamesimama wanaume wawili waliokuwa wamevaa suti safi na hawakuonekana kabisa kuhofia manyunyu ya Mvua mida hiyo ya jioni.
"Kwanini umeamua kutukimbia na kuja kuishi huku bila taarifa yoyote" ni swali la mmoja ya wale wanaume wawili waliokuwa na suti safi nyeusi na kofia kubwa vichwani.
"Mnataka nini mpaka mnifuate na huku? nilishaamua kutoka kwenye maisha yenu ndio maana sijawahi kuwatafuta tena ni miaka miwili sasa imepita hivyo sitarajii kunifuatilia tena ondokeni hapa" Mr Jonson alionekana kuwajua kwa undani hao watu walio onekana kumtafuta kwa muda mrefu sana.
"Leo umekuwa jasiri wa kutufukuza watu kama sisi kweli? mbona unajisahau sana namna hii mkuu, umemdanganya mpaka mke wako hakuwahi kuujua uhalisia wako kwamba wewe ni nani na tulikusaidia kulilinda hilo saivi unaanza kujibu jeuri.
Bosi ametuagiza vitu vitatu kwako cha kwanza ni kuchukua mzigo wetu tukuache hai, chapili uende wewe mwenyewe ukamkabidhi huo mzigo na umpe sababu za msingi kwanini umekuwa msaliti mkubwa sana namna hii kwa mtu ambaye uliaminiwa na kupewa nafasi kubwa mno, lakini cha tatu kama vyote hivyo viwili vikishindikana basi tuue familia yako yote" yalikuwa ni maelezo yaliyo jitosheleza vyema hayakuhitaji maswali mengi sana ili yaeleweke.
"Siendi mahali na hakuna kitu ambacho mtakifanya kwangu siwezi kurudi kwenye maisha yale ya utumwa mimi" Mr Jonson alitamka kijasiri wakati huo aliichomoa bastola yake kwa nguvu ila kabla hajafanya chochote alipigwa yeye risasi ya bega iliyo mtoa kilio kikubwa kilicho washtua mpaka ndani, familia karibia nzima ilitoka nje kasoro Lenovatus ambaye ndo alikuwa anaamka, ni baada ya kusikia kelele za Mr Jonson walihisi huenda anahitaji msaada wa ghafla hivyo wote walikuwa wametoka nje ila waliogopa baada ya kuona mzee huyo amewekewa bastola ya kichwa akiwa anaamriwa kuwakabidhi hazina yao kama walivyokuwa wanadai wao.
Watu hao walionekana kufurahia baada ya kuona familia ya mzee huyo yote ipo nje, mmoja wa wale wanaume aliwasogelea na kuwamiminia risasi wote bila hata kuuliza, Mr Jonson alinyanyuka akihitaji kwenda kumzuia mtu huyo alipigwa risasi mbili za miguu akawa hana hata uwezo wa kutembea tena, alitoa machozi kwa kushindwa kabisa kuisaidia familia yake ambayo alikuwa anaona kabisa inakufa Kwa sababu ya uzembe wake, hakuwa na cha kufanya mzee huyu hakupata hata nafasi ya kuwaaga wana familia hao ambao kwenye kuangaza kwake hakumuona mtoto wake wa mwisho ambaye alikuwa ni pacha wa Cleopatra kidogo alipata matumaini na aliomba MUNGU amlinde huko aliko hata amtumie malaika wake amlinde mtoto huyo asiweze kuonekana hiyo sehemu.
"Umeshindwa kuilinda familia yako kwa sababu ya ujinga wako mwenyewe ungetupatia tunacho kihitaji haya yasingetokea kabisa, sasa tunaua familia nzima hakuna shahidi atakaye baki wa kuendelea kuificha hiyo hazina ambayo haupo tayari kuitoa haya yanaishia hapa hapa mkuu naomba unisamehe sana japo umekuwa mkuu wangu kwa muda mrefu kidogo leo sina namna ya kufanya" mwanaume huyo aliyekuwa amesimama karibu yake alikuwa anampa wosia wa mwisho mwisho Mr Jonson.
"Ipo siku haya yote yataisha najua yupo mtu atayafanya haya tu na mtaisha wote" hakuongeza neno lingine alipigwa risasi nyingi sana za kichwa, milio mingi ya risasi nyingi nje ya nyumba hiyo ndiyo iliyokuwa imemshtua Lenovatus na kumaliza usingizi wake wote, alifika sebuleni lastborn huyu wa familia kwani ilikuwa lazima akadeke kwa mama yake kwanza ndo aendelee na mengine ila hakumkuta mtu yeyote sebuleni hapo chakula kikiwa kimeandaliwa tayari, alichukua zake paja la nyama ya kuku akaendelea kulitafuna taratibu ndipo alipokumbuka alisikia sauti kubwa nje na mlango ulikuwa upo wazi kabisa, alielekea kwenye huo mlango ili ajue nini kinaendelea huko nje ambako kulikuwa kuna mwanga wa kutosha wa umeme.
Baada ya kufika hapo mlangoni nyama ilimdondoka mkononi baada ya kuona damu imetapakaa alimuona mama yake amelala chini akiwa na damu nyingi sana inamtoka kichwani pembeni ya mama yake alikuwa amelala pacha wake ambaye walipendana kuliko kitu chochote kile kwenye huu ulimwengu, Lenovatus alikuwa bado ni mdogo ila uchungu ulio mpata ulikuwa ni mkubwa sana alikuwa anaelewa vyema kwa sababu alikuwa anaona kwenye movie nyingi namna watu wanavyokufa alitambua hao wote hapo chini walikuwa hawapo tena duniani, aliyainua macho yake mbele kidogo ambapo aliona kuna mwanaume mwenye suti yake nzuri sana akiwa anakata shingo ya baba yake kisu.
"Baba" aliita kwa nguvu mtoto huyu akitaka kukimbilia kule nje ili akamzuie mtu huyo kufanya hicho kitu kwa baba yake mzazi, sauti yake iliwashtua wale wanaume ambapo yule mmoja alikuwa amekamilisha kukikata hicho kichwa na alikuwa amekishika mkononi. Kabla huyo mtoto hajatoka kwenye huo mlango ikiwa ndo anaanza kukimbia kuelekea nje mlango ulipigwa na teke la ghafla ulijifunga pembeni mwa huyo mtoto alitokea mwanaume mmoja aliye onekana kuwa wa makamo kidogo akiwa na barakoa iliyo uziba uso wake kwa usahihi alimziba Lenovatus mdomo aliyekuwa anapiga makelele kwa mambo aliyo yaona hapo nje kwa familia yake, baada ya kuona mtoto huyu anahangaika ajinasue kwenye mikono yake ili atoke kwenda huko nje alipitisha kidole chake kwenye mshipa wa shingoni Lenovatus akatulia kimya.
Wanaume hao walikuwa wanakuja kwa tahadhali sana baada ya kugundua walikuwa hawajaimaliza familia nzima, mmoja aliupiga mlango kwa teke wakati huo wanafika kwenye huo mlango yule mtu aliyemziba Lenovatus mdomo alijirusha juu ya kabati kubwa la vyombo hapo sebuleni akatulia kimya akiwa amempakata mtoto huyo. Hao watu waliingia humo ndani na kukagua kila chumba lakini hawakuona chochote kile.
"Kwa nilivyo muona bado ni bwana mdogo sana hata kama ameona kilicho tokea hawezi kukumbuka atakapokuwa mkubwa, tukienda kwa bosi tutamwambia wote wamekufa kwani hata hatujui alikuwa na watoto wangapi kwa maisha ya siri aliyokuwa anaishi na familia yake" baada ya kuonekana kukubaliana na hilo walitoka humo ndani wakaondoka na kichwa cha Mr Jonson. Yule mtu aliyekuwa amemsaidia Lenovatus kutoka kwa hao watu baada ya kuhakikisha watu hao wameondoka alishuka kule juu ya kabati akaangaza huku na huku kisha akaelekea mlango wa nyuma wa nyumba na alionekana kuijua vyema sana hiyo nyumba akatokomea zake gizani akiwa amembeba kijana mdogo sana Lenovatus.
Mr Jonson Malisaba ni nani?, Siri gani ambayo aliificha familia yake?, Huyu aliye msaidia Lenovatus ni nani hasa mpaka afike muda kama huu?, kuna nini kinaendelea kati ya hawa watu waliompa Mr Jonson machaguo matatu ya kuchagua? Na hicho kitu kilikuwa na umuhimu gani mkubwa mpaka wafikie hatua kama wakikikosa waue familia nzima ili kusiwe na Shahidi yeyote??......
Ndio kwanza tunaianza hadithi mpya ndani ya sehemu ya kwanza kabisa , utakuwa nami mpaka mwisho wa kisa hiki kinacho mhusu bwana mdogo Jamal utajua kwa undani Jamal yeye ni nani hasa na alipitia nini kweye maisha yake kikubwa usibanduke ungana namimi mpaka mwisho kabisa wa hadithi hii.
Bux the story teller.
Comments