Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

 

Zaidi ya kilomita 910 ambayo ni msaa 15 kutoka ndani ya wilaya ya Kyela mpaka kufika ndani ya jiji la Dar es salaam, saa mbili za usiku ndio muda ambao watu hawa wawili walikuwa wanaingia ndani ya jiji hili kubwa. Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa kijana Jamal kufika ndani ya mji ambao alikuwa akizisikia sifa zake kutoka kwa baba yake kwa uzuri pamoja na kuwa na mambo mengi sana ya hovyo ikiwa ni pamoja na magenge ya wahuni wengi kupitiliza. Walikuwa ndani ya bajaji Jamal hakuwa na muda wa kuongea na mtu zaidi ya kushangaa shangaa mataa yalivyokuwa yamelipendezesha jiji hili kubwa, alijihisi furaha kubwa mno kwa sababu alikuwa amechoka sana kuishi maisha ya milimani akiishia kuvua tu samaki pamoja na kulima mpunga kila siku yeye na mvua mvua nayeye. Mzee wake alimwangalia kijana wake aliyekuwa bize muda wote kuchungulia nje na kufurahia namna watu walivyokuwa wanapishana kwa wingi usiku huo kila mtu akiwa yupo bize na mambo yake.

 

Buguruni sheli ndipo safari yao ilipoweza kuishia, walishuka ndani ya hiyo bajaji na mzee wake akalipa nauli wakaaanza kuondoka, Baba yake alionekana kuwa mwenyeji sana wa haya maeneo walizunguka nyuma ya hiyo mitaa Jamal alishangaa sana kuona wanawake wengi sana waliokuwa wanavutia mno machoni pake alikiri wazi kuna watu wanapendelewa sana na MUNGU kwenye maisha yake hakubahatika kuwaona warembo wa aina hiyo alitabasamu na kujihisi amani sana kwenye moyo wake ila cha ajabu wanawake hao wote walikuwa wamevaa vinguo vifupi kupitiliza kiasi kwamba hawawezi hata kuinama kuokota kitu chini miili yao ingekuwa mitupu kabisa na maungo yao yote yangekuwa nje kama wangefanya hivyo, hakuwa mwenyeji wala hakuwa na uelewa juu ya biashara ya wanawake kuiuza miili yao kwa vijana wenye tamaa za kimwili kwa kipato kidogo na hicho ndicho kilicho wafanya wanawake hao wawe na uwezo wa kuendelea kuishi kwenye jiji hili ambalo mwenye pesa ndiye mwenye kauli ya mwisho. Alisikitika sana kwa hilo hakuwahi kabisa kujuana na mwanamke kwenye maisha yake yote wala kupenda mtu , aliahidi lazima ataitafuta mitaa hiyo aje apate mke mzuri wa kumuoa bila hata kuwajua kiundani uhalisia wa hao wanawake. Ilikuwa ni tofauti kwa baba yake hakuwa hata na muda wa kugeuka kuwaangalia hao wanawake alikuwa ameyakaza macho yake mbele akionekana kuyazoea hayo mazingira.

 

Safari yao ilienda kuishia kwenye nyumba moja ya wageni kwenye mitaa hiyo ya uswahilini, walilipia chumba wakatoka kidogo kwenda kupata kitu chochote kwani tangu watoke Kyela walikuwa hawajagusa kitu chochote kile kwenye vinywa vyao na hilo halikuwa tatizo kabisa kwao walikuwa wameshazoea. Walipata chakula na hatimae waliweza kurudi ndani ya chumba chao na kuiweka mizigo yao vizuri kabisa wakalala. Mida ya usiku wa manane baba yake Jamal aliamka kimya kimya na kwa usiri mkubwa sana akionekana wazi hakuhitaji kabisa mtoto wake alitambue hilo, alivaa koti kubwa jeusi na buti kubwa akaufunga mlango kwa nje baada ya hapo akapotelea kwenye vichochoro vya hiyo mitaa akiwa hana wasi wasi kabisa. Saa nane kamili usiku kwenye kambi kubwa zaidi ya jeshi la nchi LUGALO ipatikanayo ndani ya Mwenge jijini Dar es salaam kwenye jengo kubwa la mkuu wa majeshi ambapo alikuwa anaishi, nje ya geti alionekana mtu mmoja mwenye koti kubwa jeusi akiwa amesimama hapo, aligonga geti hilo akiwa hana hata tone la wasi wasi kabisa, ndani ya hilo geti kulikuwa na walinzi wawili ambao wote walikuwa ni wanajeshi walishangazwa na ugeni wa usiku wa manane huo haikuwa kawaida mtu kufika na kugonga kirahisi kiasi hicho nyumbani kabisa kwa mkuu wa majeshi, walikaa kimya hata hivyo geti liliendelea kugongwa kwa nguvu sana. Walichomoa silaha zao na mmoja akafungua akiwa na jaziba kubwa alikutana na mtu aliyekuwa amempa mgongo ameangalia upande mwingine kabisa.

"Kijana vipi hauijui vizuri kazi yako au nagongaje geti zaidi ya mara tano na upo umekaa tu humo ndani na mwenzako, unavyo jiona unahisi unafaa kumlinda mkuu wa majeshi kweli wewe kwa uzembe ulio nao huo" huyu mtu alimuuliza mlinzi aliye baki anamshangaa kwa sababu mwenye makosa ni huyu aliyekuwa amegonga na sio mlinzi.

"Nani wewe mpaka uniuliza maswali yote hayo" aliuliza mlinzi kwa sauti yake kavu akiwa anaangaza huku na huko kama labda walikuwa wapo wengi hapo nje lakini hakuona mtu mwingine yeyote yule.

"Sio kazi yako kunijua mpelekee taatifa bosi wako mwambie nahitaji kuonana naye saivi" alikuwa anamgeukia huyo mlinzi akiwa hana hata presha.

"Hahahaha utakuwa kichaa wewe sio bure ebu toka hapa nisije nikakupiga bure nikaonekana nawanyanyasa raia kwa kumpiga mtu kichaa kama wewe, unajua ni kwa nani hapa mpaka uulize kirahisi namna hiyo kukutana na huyo mtu? Pumbavu sana" mlinzi hasira zilikuwa zimemuisha baada ya kugundua kwamba mtu aliyepo hapo huenda ni kichaa ndio maana amegonga geti hilo usiku akaamua kufunga geti hilo ila kabla ya kufanya hicho kitu hilo geti lilidakwa kwa mkono ulio shiba alijitahidi kulivuta hakufanikiwa kulifunga aliichomoa bastola yake ili ampige nayo huyo mwanaume ambae ni wazi alionekana sio mtu mwema, ngumi tatu za mbavu zilimfanya asiweze hata kutoa sauti mlinzi huyo, mwenzake alikuwa kwenye tahaturi wakati anasogea ili amshambulie huyo mgeni alihisi kitu cha baridi kimegusa sehemu ya kichwa chake, alikuwa amewekewa bastola kichwani kumaanisha kwamba kama angefanya chochote ilikuwa inapita na ubongo wake.

"unataka nini?" aliuliza mlinzi huku mwenzake akiwa chini anagala gala baada ya kuona wamezidiwa.

"Nahitaji kuongea na bosi wenu muda huu" sauti ya kiume iliyo jaa utulivu ilijibu.

"Hiki unacho kifanya ni hatari sana kwa sababu hapa huwezi kwenda popote pale na hizi vurugu ulizo zianzisha ni hatari sana muda wowote kuanzia sasa unakamatwa huyo mtu kumfikia alipo ni kazi ngumu na sio kirahisi kama unavyo fikiria wewe" baada ya kumaliza maelezo yake yule mwanaume alichomoa magazine kwenye silaha aliyokuwa amemuweka nayo chini ya ulinzi akaitupa ile bastola, ilimshangaza mlinzi kuona huyo mtu anajiamini nini hasa mpaka afanye yote hayo.

"Sijaja hapa kwa ugomvi ndio maana hata geti nimegonga kistaarabu tu ningeamua kupita kwa njia zangu nisingepitia mlangoni, ni jambo la mhimu sana nahitaji kuongea naye nakuomba mpigie simu niongee naye mwenyewe saivi" kidogo maneno yake ya busara yalimshawishi yule mwanajeshi akaitoa simu yake na kupiga namba ya dharura, iliita kwa dakika moja ikapokelewa aliambiwa asuburi kwa sekunde thelathini baada ya hapo simu ilionekana kuita baada ya mwanajeshi huyo kupokea alishangaa anaambiwa ampeleke huyo mtu sehemu yenye bustani nzuri sana kisha yeye arudi getini, kilicho mshangaza hakuulizwa kwamba ni nani alikuwa amefika hapo lakini aliruhusiwa basi akafanya hivyo na kurudi zake getini kuendelea kudumisha ulinzi na kumpatia mwenzake huduma ya kwanza.

 

"Kaka" ni sauti ya mshangao ilitoka kwa mkuu wa majeshi akionekana kumuita mtu aliyekuwa amefika kuongea nae majira hayo ya usiku. Alionekana kumjua vizuri mno huyo mwanaume kuliko binadamu yeyote yule.

"Uache huo ujinga wa kuruhusu kila mtu akija majira ya usiku kukuona kirahisi sana namna hii kama baadhi ya watu wakija kulijua hili kwamba kuonekana kwako ni rahisi hivi basi itakuwa ni hatari sana" mwanaume aliyekuwa amefika hapo alijibu kwa sauti yake nzito akiwa anageuka upande alipikuwa amesimama mkuu wa majeshi kwani muda wote alikuwa ameangalia upande wa swimming pool zuri lililokuwa likionekana vyema kwa taa Safi zilizo kuwa zimezungushiwa hapo.

" Sikuwa nina imani kama ni wewe ila hisia zilinituma hivyo kwani hakuna binadamu mwingine anayeweza kuja kugonga nyumbani kwangu usiku kirahisi hivi, namshukuru MUNGU umerudi niliogopa sana nikajua umekufa" mkuu wa majeshi aliongea kwa sauti ya masononeko akimkumbatia huyo mtu aliyekuwa akimuita kaka.

"Siwezi kufa kirahisi sana namna hii mdogo wangu bado nina kazi ngumu sana ya kukulinda" alitabasamu wakiwa wanatafuta sehemu ya kwenda kukaa wakipigwa na upepo majira hayo ya usiku. Mwanaume huyu alitoa sura yake ya bandia ambayo alikuwa ameiweka usoni mwake kwa miaka mingi sana, sura yake na ya mkuu wa majeshi ilikuwa ni moja, hawa walikuwa ni mapacha wa tumbo moja na walizaliwa siku moja ila walipishana masaa kadhaa tu na mkuu wa majeshi ndiye aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa ndio maana alikuwa akimuita huyo mwanaume mbele yake kaka.

"Daud Hauston au Mmarekani mweusi jina lako la zamani sana ulikuwa ukipenda kujiita tukiwa wadogo, ni miaka zaidi ya mitano imepita sasa sijakutia machoni kwa yale niliyo yasikiaga mwanza niliogopaga kwamba huenda utakuwa umekutwa na jambo baya ulikuwa wapi kaka?" Walionekana kuwa ni watu waliopendana sana mapacha hawa mkuu wa majeshi alikuwa haamini kabisa kama mwenzake huyo alikuwa yupo hai mpaka leo.

"Nina mengi sana ya kuzungumza nawewe lakini muda nilio nao ni mchache sana kukaa hapa saivi, nimekuja hapa kwako kuna bwana mdogo ambaye ndiye pekee aliyepona kwenye ile familia nahitaji awe chini yako akachukue mafunzo ya ukomando nje ya nchi kwa sababu kuna kazi nzito sana ambayo anatakiwa kuifanya ipo mbele yake sina imani sana na uwezo wake na huko kuna mambo mengi ambayo nataka akajifunze ili akirudi nimrejeshee kumbukumbu zake ajitambue yeye ni nani na kazi itaanzia hapo kwa sasa anaweza akaishi kwa mawazo sana inatakiwa abaki vile vile" Kwa maelezo yake alikuwa ni baba yake Jamal huyu akidai mtoto aliye naye ndiye pekee aliyefanikiwa kupona kwenye familia moja huko mwanza akiwa anafahamika kama Daud Hauston au Mmarekani mweusi kama alivyo onekana kupenda kujiita tangu akiwa mdogo.

 

"Mhhhhhhh kumbe kuna mtoto mwingine alipona katika lile tukio?" Mkuu wa majeshi aliongea kwa mshituko akiwa bado haamini.

"Unamaanisha nini kusema mtoto mwingine alipona kwenye lile tukio wakati alipona mmoja pekee" Daud Hauston waweza kumuita baba Jamal aliuliza kwa mshangao.

"Siku ile hawakufa wote kuna mtoto wa kike tulifanikiwa kumuokoa akiwa yupo kwenye hali mbaya ila mpaka saivi yupo mzima wa afya kabisa ila tatizo moja tu alishapoteza kumbu kumbu zote alipata mshtuko mkali sana hivyo hapa duniani ananijua mimi pekee kama baba yake na hamwamini mtu yeyote mwingine zaidi yangu" mkuu wa majeshi aliongea maneno yaliyo mfanya huyo mwanaume atoe macho kwa mshangao mkubwa alijua ni utani 

"Bwana mdogo tangu lini ukaanza masihara tukiwa kwenye mambo yenye usiriasi mkubwa sana namna hii?" Kauli yake wala haikujibiwa kwa maneno zaidi mkuu wa majeshi aliingiza mkono wake kwenye mfuko wa koti lake akaitoa picha na kumpatia mwanaume huyo. Kwenye hiyo picha kulikuwa na sura nzuri sana ya mtoto wa kike aliyekuwa akifanana kila kitu na Jamal sema utofauti wao ni kwamba huyu binti alilelewa kwenye maisha mazuri na Jamal alikulia kwenye maisha ya taabu hivyo yeye alikuwa amekomaa japo sura yake ilikuwa yenye mvuto bado. Alikuwa ni pacha wake wa kuzaliwa kabisa ajulikanaye kama Octavian Jonson.

"Hili jambo kuna nani mwingine analijua?" Kaka mtu aliangaza akiwa anaangalia huku na huku kuona kama kuna mtu anasikiliza hayo mazungumzo yao hakuona yeyote hiyo sehemu.

"Ni mimi pekee kaka haya siyo mambo ya kuufahamisha uma litakuwa ni tatizo lingine hili"

"Hakikisha hii inabaki siri yetu mimi na wewe na huyo mtoto mhifadhi sehemu salama sana mdogo wake kesho inabidi uje umchukue majira ya saa mbili za jioni buguruni sheli kwa nyuma atakuwa pale, hakikisha anachukuliwa baada ya hapo utanirudishia huyo bwana mdogo baada ya miaka mitatu na hili jambo lisiende mahala popote pale" mwanaume huyo baada ya kumaliza maneno yake akiondoka hapo kwa kasi kubwa kiasi kwamba alimuacha mdogo wake ambaye ni mkuu wa majeshi kwenye tafakuri kubwa akiwa ana maswali mengi sana kuhitaji kujua alikuwa wapi miaka yote hiyo.

Kulikuwa kumekucha vyema yeye na Jamal walikuwa wapo kwenye mgahawa wakipata supu baada ya kutoka hapo walienda kukaa kwenye daraja lipatikanalo Mandela road, barabara ya kuelekea mbagala.

"Leo jioni inawezekana ikawa siku yako ya mwisho kuniona, kuna mahali unaenda hakikisha unaenda kufanya unacho ambiwa hata kiwe nini chukulia kwamba hicho kitu nakwambia mimi, utarudi baada ya miaka mitatu na kama utafanikiwa kurudi salama nitakuwa na mazungumzo marefu nawewe na nitayajibu maswali yako yote" Jamal alikuwa anayasikiliza maneno kutoka kwa baba yake ambayo yalizungumzwa kama utani ila ndo alikuwa amemaliza hivyo na huwa harudii mara mbili.

"Baba!!" Aliita kwa mshangao Jamal ila alikatishwa njiani.

"Zingatia sana kuhusu hicho kidani kilinde kuliko hata unavyo weza ukanilinda mimi, haya nyanyuka twende nikalale nimechoka mimi sitaki maswali saivi" Jamal hakuwa na namna zaidi ya kunyanyuka na kuanza kuelekea kwenye chumba walicho lipia kwenye nyumba ya wageni, tangu wapo Kyela mpaka leo alikuwa na maswali mengi sana ambayo yote yalikuwa yanakatishwa njiani bila kupewa majibu basi alisubiri muda uamue zaidi.

Majira ya jioni saa mbili kasoro za usiku ndio muda ambao baba yake Jamal alikuwa anaamka kutoka usingizini wakati huo bwana mdogo alikuwa ametoka kuzunguka zunguka maeneo ya karibu kuijua mitaa kidogo.

"Shika pesa hiyo kaniletee maji haraka kichwa kinaniuma sana" sauti ya baba yake ilimshtua kwenye mawazo akiwa amejiegesha kitandani akiwaza mambo mengi sana. Alikuwa anampenda sana baba yake alivyo sikia anaumwa alitoka haraka humo ndani wakati huo ilikuwa ni majira ya saa mbili. Hatua kumi na tano kutoka kwenye hiyo nyumba ya wageni akitafuta duka la karibu na hayo maeneo mbele yake walikuwa wamesimama wanaume wanne, alitaka kubadili njia wakati anaangalia njia nyingine alimuona baba yake akimpungia mkono wa kwaheri akiwa hata haangalii nyuma alipokuwa mwanae aliishia vichochoroni ambako Jamal hakuelewa mzee wake anaelekea wapi, Jamal alicheka kwa hilo tukio lakini moyoni mwake aliumia sana kwa sababu hakujua sababu za msingi za baba yake kufanya yote hayo. Hakuhitaji hicho kitu kifanyike kijana huyu alikuwa ameivishwa sana alichukua kitambaa kidogo akaufunga mkono wake wa kulia alitabasamu kidogo, akianza kukimbia kuelekea upande walipokuwa wamesimama wanaume hao wanne.

 

Sehemu ya tatu sina la ziada naishia hapa mpaka wakati mwingine tena.

 

Bux the story teller.

Previoua Next