SEHEMU YA 206.
Devil and Angel.
Watu hawakuamini Hamza angeweza kumpiga Gonzalez na ngumi moja tu na kumdondosha chini, hata wale ambao hawakushangilia mwanzo walijikuta wakishindwa kuficha hisia zao na kuanza kupiga makelele.
“Ngumi nyingine moja tu hadi chini!?”
“Nguvu aliokuwa nayo sio ya kawaida”
“Inatisha , anatisha sana Lucifer! Yaani nashindwa kuamini kafanikisha vipi kuhimili uzito wa Gonzalez ambao ni zaidi ya tani kadhaa”
“Huyu ndio mfalme wa kuzimu sasa,ana stahili kuitwa hivyo”
“Magwiji ni magwiji tu siku zote , ingawa Gonzalez yupo nafasi moja nyuma kufikia daraja la Ugwiji lakini utofauti wake na magwiji ni mkubwa sana”
Watu walikuwa katika butwaa kubwa , hata wale wa kundi la Metal tide walijihisi mioyo yao inawadondoka.
Kiongozi ambae walikuwa wakimsujudia kutokana na uwezo wake na kuamini ni mwenye nguvu nyingi ndio huyo ambae amedondoshwa na ngumi moja tu, ilikuwa ngumu kumeza kwao.
Muda huo wanachama hao wa metal Tide walikuwa katika hali ambazo hazielezeki , wengine walifikia hatua ya kuweka mikono yao kwenye kichwa.
Helena macho yalimtoka , kisu alichokishikilia kilianza kumtetemeka , haikujulikana ni kwasababu ya woga ama hasira.
Regina alikuwa katika msisimko wa hali ya juu sana lakini hakuonyesha, alitamani na yeye kuamka na kumshangilia Hamza kwa nguvu lakini alijitahidi kujizuia kutokana na kuwa mateka.
Hajawahi kujivunia kuwa mke wa Hamza tokea wafunge ndoa , lakini siku hio namna Hamza alivyosimama huku akishangiliwa na jitu zito kama Gonzalez likiwa chini alimuona ni shujaa mkubwa.
Gonzalez aliishia kuangalia mkono wake ambao umeharibika sana katika hali ya kutokuamini. Hakuweza hata kufikiria jambo kama hilo lingemtokea tena kupitia kwa ngumi ya kibinadamu ya mkono wa Hamza.
Aliishia kujiuliza ni nguvu ya namna gani ambayo Hamza ana miliki. Haikuwa kwake tu hata kwa Magwiji waliosimama mbali walijikuta wakiguswa na jambo hilo.
“Nguvu alizokuwa nazo zinashangaza mno!” Aliongea Huge.
Ukweli ni kwamba bwana huyo alikuwa akijua Hamza alikuwa na uwezo wa juu sana wa mbinu hio inayofahamika kwa jina la Mgawanyiko, kama angemchukulia Hamza mtu dhaifu kama alivyofanya Gonzalez , basi angempokonya pete muda mrefu sana.
“Huyu mtoto anazidi kunishangaza”aliongea Silvia huku akivuta pumzi nyingi na kuzitoa.
“Hii sio mbinu ambayo alijifunza kutoka kwa Mr Black kwa miaka yote. Mr Black licha ya uwezo wake, ilikuwa ngumu kushambulia na ngumi yenye nguvu namna hio hata kama aunganishe na nishati zake zote za mbingu na ardhi”Aliongea Sebastiani.
Ikumbukwe kwamba Hamza master wake ni Mr Black , ki ufupi ni kwamba Hamza aliachana na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ambayo alijifunza kutoka kwa Mr Black mara baada ya kumuua.
“Hata mimi naona , inaonekana Lucifer ameamua kuachana na mafunzo ya nishati aliojifunza kutoka kwa Master wake baada ya kumuua. Hakika ni kijana mwenye akili nyingi sana”Aliongea Oleg.
Mikaeli na Auland wenyewe waliishia kutingisha vichwa vyao pekee , ukweli ni kwamba tokea mwanzo mpaka mwisho hawakuwa na wasiwasi kabisa juu ya uwezo wa Hamza
Mara baada ya kumdondosha adui yake chini, Hamza hakuchukulia kama fursa ya kumshambulia tena na badala yake aliishia kumwangalia tu kikauzu . Ijapokuwa mkono mmoja wa Gonzalez uliharibika lakini bado aliweza kusimama vyema huku akivuta pumzi nyingi . Macho yake yalijaa hisia za kukosa hiari na woga, lakini vilevile alionyesha ishara ya uovu na kukata tamaa.
Alikuwa amesubiria kwa miaka mingi sana kuja kutimiza ndoto zake za kuwa sehemu ya magwiji , lakini mwisho wa siku juhudi zake zote zimeharibika , ilikuwa ni kawaida kukumbwa na hali ya kujisikitikia.
Chini ya kundi lote hilo la watu alikuwa amepigwa mara mbili na Hamza. Alijihisi kudharalishwa kusikokuwa kwa kawaida.
“Lucifer unaonekana kuwa na mbinu , lakini unadhani ndio nimefikia mwisho?”
Gonzalez bado alikuwa na kadi yake ya hakiba ambayo hakuicheza bado na alipanga kuitumia katika muda kama huo.
“Kabla ya kuzuia shambulizi langu fikiria mara mbilimbili ..”aliongea Gonzalez huku akigeuza macho yake kuelekezea upande ambao Regina yupo. Alichokuwa akimwambia Hamza ni kwamba kama atazuia shambulizi lake tena basi Regina atakufa. Yaani kwa lugha nyepesi anataka Hamza asizuie na akubali kushambuliwa.
Lakini licha ya hivyo , Hamza hakuonyesha mabadiliko yoyote kama vile kuwa na hofu.
“Nitakupa nafasi ya mwisho. Unataka kufa au kuishi?”
Swali lile lilimfanya Gonzalez kushituka na kuishia kukunja sura.
“Lucifer una tania? Umefikiria mara mbilimbili kama nilivyokushauri, unadhani unaweza kuniua kirahisi?” Aliongea huku akianza kucheka kwa kuonyesha kiburi na kufanya watu kushangazwa na tabia yake.
“Mshenzi wewe Gonzalez , unathubutu vipi kumteka shemeji yetu? Wewe ni muoga”Aliongea Mameni kwa kufoka.
“Hustahili kuwa Gwiji , kama unataka siku nyingine kushindana na bosi rudi kwenye machimbo ya chuma ukajiimarishe upya”Aliongea Berly.
“Kaeni kimya! Najua mnabweka kwa kujua bosi wenu anakwenda kupoteza pambano. Endeleeni tu kuongea ujinga ila mimi Gonzalez sio mshenzi kama mnavyofikiria”
“Hata kama uwe mshenzi vipi unapaswa kujiwekea mipaka. Gonzalez nilikuheshimu sana zamani lakini sikutegemea utaenda mbali na kumteka shemeji yetu kwa ajili tu ya kutaka kujipandisha hadhi . Umedhalilisha hadhi ya kundi lako la Metal Tide”Aliongea Asmuntis.
Mara baada ya watu wachache kusikia maneno ya watu wa Hamza , minong’ono ya chini chini ilianza kusikika na ni kama sasa wanaanza kupata ufahamu kitu ambacho Gonzalez amefanya.
“Hivi ni kweli! Kamteka mke wa Lucifer? Lakini ni lini Lucifer akawa na mke?”
“Sidhani kama ni kweli , Metal Tide hawawezi kufanya jambo la namna hio maana hakutakuwa na maana ya kushinda sasa”
Watu walianza kuongea , wengi wakijizuia kuamini kama kweli Gonzalez na watu wake wameamua kutumia mbinu ya ajabu ya utekaji. Watu wa Metal Tide kusikia maneno mengi ya namna hio ya walianza kukosa utulivu.
Ingawa ulimwengu wa Giza haukuzingatia sana sheria , lakini hadhi na heshima ni sifa kubwa zaidi.
“Jamani msisikilize ujinga wanao ongea. Wasiwasi wao ni kuogopa bosi wao anakwenda kushindwa pambano”Aliongea Gonzalez akijaribu kutuliza minong’ono kwa kujitetea.
“Haha .. siku zote umekuwa ukisema mimi ni mtu mweusi mfanyabiashara ambae ni fuata upepo niliekosa maadili. Lakini katika kundi letu Mhunzi ni mtu wa heshima kubwa na vilevile Mchafu pia anaheshimika kwa uongozi wake . Kwanini waongee mambo ambayo hayapo?”Aliongea Mameni.
“Sina muda wa kupoteza kuongea na nyie. Lucifer tumia uwezo wako wote uliokuwa nao na mimi Gonzalez nitakuonyesha nini maana ya nguvu ya kweli niliokuwa nayo”
Mara baada ya kuongea hivyo Gonzalez kwa mara nyingine alichanua mikono yake kwa kuisambaza huku akipanga kunyonya elementi za chuma za uwanja huo ili kuponyesha mkono wake. Mara baada ya ishara za elementi za chuma kuonekana kuuvaa mkono wake , macho ya Hamza ya Hamza yalionyesha nia isio nzuri na ghafla tu alipotea alipokuwa amesimama katika macho ya kawaida.
“What a speed!!” Auland alijikuta akitoa mshangao wa sauti. Ukweli kwa macho ya kawaida watu wanaona Hamza amepotea ila kwa magwiji walikuwa wakimuona Hamza, ni kwamba tu alikuwa katika spidi kubwa.
Kufumba na kufumbua Hamza alikuwa mbele ya Gonzalez. Alikuwa na kimo kirefu sana mpaka kufikia kichwa chake na mara baada ya kumuona Hamza akijitokeza mbele ya macho yake alihisi kitu hakipo sawa.
Hamza mwili wake ni kama ulikuwa katika slow motion kwa namna ambavyo alikuwa amegota hewani huku akitoa ngurumo ya hasira nyingi, wakati huo akirusha ngumi kumlenga Gonzalez.
“Boom!”
Ilikuwa ni kama ngurumo namna ngumi yake ilivyotua katika kichwa cha Gonzalez , chuma kilichokuwa kikilinda kichwa chake kilishindwa kuhimili uzito wa ngumi ile na kuifanya itoboe katika paji la uso na ile Hamza anavta mkono nje ulitoka na vipande vya chuma pamoja na uji uji mweupe na damu.
Kichwa kikubwa cha Gonzalez kilitengenezwa shimo huku wakati huo Hamza akitua chini ardhini na jitu chuma mdogo mdogo likianza kuporomoka kwenda chini.
Ghafla tu eneo lote la uwanja lilitulia tuli , huku watu wakiwa katika hali ya mshituko usiokuwa wa kawaida, wakishuhudia mwili wa Gonzalez ukidondoka na kutua chini.
Hakuna ambae aliamini Gonzalez ambae alikuwa akiongea sana kwa kujisifia na kuonekana kama mtu amabe angepigana na Hamza kwa raundi kadhaa angeweza kuuliwa na ngumi moja tu.
Mwanzo mwisho Hamza alikuwa amefanya mashambulizi matatu pekee na kisha shambulizi alilofanya lilikuwa na madhara makubwa , lakini la mwisho ndio lilimaliza kabisa kazi kwa kumuua palepale.
Ghafla tu watu wengi walijihisi miili yao kutetemeka huku vigoti vya miguu vikikosa nguvu , hisia waliozokuwa nazo zilikuwa za hofu.
“Divin-rth!”
Ilikuwa ni sauti moja tu kutoka kwa mwanachama wa Inferno na sauti hio ilikuwa kama kitufe kilichofungulia makelele mengi ya kushangilia.
Azzle , Asmuntis na wengine walijikuta wakiwa katika hali ya msisimko kiasi kwamba walitamani kupiga magoti na kuanza kusujudu.
Ilikuwa ni kama vile muda umerudi nyuma na kuwa siku ile ya kiumbe aliebatizwa jina la Ghadhabu Takatifu akiwa amesimama katika uwanja wa vita huku chini kukiwa na miili ya watu iliosambaa wa vita akiwa amemaliza kazi kwa kujipatia ushindi.
“Bosi , Bosi.. Aah bosi…” Leviathani uchizi ulimvaa palepale akishindwa kuelezea hisia zake.
Mapigo ya moyo ya Black Fog yalizidi kwenda mbio , mkono mmoja aliuweka kifuani mwake kama kwamba alikuwa akizuia moyo wake usije kuchoropoka. Macho yake yalijaa matamanio na penzi zito.
Lakini hata hivyo licha ya watu wengi kumshangilia kama wameshikwa na ukichaa haikumfanya Hamza kujisikia furaha hata kidogo wala kujivunia. Macho yake muda wote yalikuwa upande wa watu wa Metal Tide na palepale aliongea kwa nguvu.
“Jamazeni wote!”
Kauli yake ilikuwa ni kama batani ya umeme imebonyezwa kwani mara baada ya sauti yake kusikika watu walinyamaza na kumwangalia wakitaka kujua anakwenda kuongea nini.
“Watu wa Wimbi la Chuma naomba mnisikilize , Kapteni wenu amekufa …”
Wanajeshi wa Metal Tide siti zilikuwa za moto , huku wakati mmoja wakihisi ubaridi usio wa kawaida ukisambaa katika kila kiungo cha miili yao.
Kifo cha Gonzalez , kilikuwa cha haraka sana , alikuwa ndio mwasisi mkuu wa kundi hilo la kimasenari na kutokana na kifo chake kila mtu alikuwa katika hali ya kupaniki kushindwa kujua nini hatima yao.
Ni kama uti wao wa mgogo umeshindwa kufanya kazi ghafla na sasa wapo katika hali ya kupalalaizi na kufanya wawe katika hali ya kutojiweza.
Mshituko ambao Hamza aliwasababishia ulikuwa mkubwa mno. Picha walioweza kushuhudia ilikuwa na athari kubwa mno kisaikolojia ambayo ilienda kushitua kila neva ya moyo na kulipua homoni za uoga katika hifadhi zake na kufanya zisambae katika damu na kusafirishwa mwili mzima.
“Nitawapa machaguo mawili , mosi mwachieni mke wangu akiwa hai na kisha poteeni na nitasahau kilichotokea leo , pili mnaweza kumuua mke wangu lakini nyie na kizazi chenu chote kwanzia wake zenu , wanaume wenu , watoto wenu mpaka ndugu zenu wa mbali , nitawaua wote”
Hayakuwa maneno tu , sauti yake pia ilisafirisha maneno hayo na msisimko ambao ulisambaa katika moyo wa kila mmoja wa kundi hilo la Metal Tide.
Ilikuwa ni sawa na kusema uhai wa Regina ulitaka kubadilishwa na maisha ya familia zote za watu wa Metal Tide. Hakuna ambae angekubali kuona famili yake inakufa kwa ajili ya uhai wa mtu mmoja , isitoshe kama ni kapteni wao amekwisha kufa , kuna haja gani ya kwenda mbali kumchokoza mfalme wa kuzimu kwa ajili ya tamaa za Gonzalez?.
“Msidhani natania , nawahakikishia kila ninachoongea hapa nitakikamilisha ipasavyo, Nadhani wote mnajua hakuna binadamu ambae alishawahi kutafutwa na mimi dunia hii na akakosekana”
Mara baada ya kuongea hivyo watu wake wote wa Infenro , wanajeshi wa Barhams na Maninja a Baffodil wote walipiga saluti kuuunga mkono amri yake kuonyesha kwamba wapo tayari kwa maelekezo kutoka kwa bosi wao.
“Helena, unadhani ni kipi kinapaswa kufanyika?”Aliuliza Gray.
Wasingekubali tu kukubali kumwachia Regina kwasababu , alikuwa pia ndio tiketi ya uhai wao. Yalikuwa maamuzi magumu kumteka mwanzo lakini vile ni maamuzi magumu kumwachia.
Uhalisia ulikuwa na ukatili sana kwao, ilikuwa ni wazi kwamba hata kama wakiamua kuchagua chaguo la mwisho ingekuwa ngumu sana kushindana na makundi matatu ya Daraja A bila ya uwepo wa Gonzalez.
Hivyo kauli ya Hamza kusema ataua kila mwanafamilia , haikuwa ya mkwala tu , alikuwa na uwezo huo kwa asilimia mia moja.
Regina mara baada ya kusikia maneno ya Hamza moyo wake ulidunda kwa nguvu. Alikuwa katika hali ya woga lakini alijua fika Hamza alikuwa akitumia kila njia kuhakikisha anakuwa salama. Alihisi pia Hamza kauli yake ni ya kikatili sana kwa kuona hata kama akifa kuua familia za watu wote hao isingekuwa vizuri , kwani ni watu ambao walikuwa wakitii tu maagizo na familia zao hazikuwa na kosa.
“Kushindwa ni kushindwa tu, ila hata kama tumeshindwa bado tunapaswa kusimamia ahadi tuliowekeana na kapteni wetu, Uhai ni mwanzo wa wimbi na kifo ni mwisho wa wimbi na hatimae mwanzo wa wimbi lingine la maisha ya kipepo”Aliongea Helena akimalizia na kauli mbiu ya kundi lao.
“Helena unamaanisha nini , kwahio unataka kweli kwenda kinyume na na maneno ya Lucifer na kumuua Regina?”Aliuliza Gray kwa mshangao.
“Bila kufanya hivyo tutakuwa tumemsaliti Kapteni , tumeisaliti taasisi yetu, ni nani atakubali kufanya kazi na mwanajeshi wa kulipwa anaevunja kiapo? Tutaondoka kwanza na Regina hapa na kumtumia kama mateka . ili mradi tutachelewesha kifo chake na wao pia hawatokurupuka kutushambulia”Aliongea.
“Helena wewe uko peke yako , lakini sisi wote hapa tuna wake zetu , tuna watoto na familia .. hebu acha kujaribu kuwa jasiri , Kiongozi wetu amekwisha kufa” Moja ya masenari aliongea.
“Kweli kabisa , Helena kiongozi wetu hajawahi kuwa na njia za kunyooka katika kufanya mambo yake. Tunapaswa kumuomba msamaha mtawala wa kuzimu. Amekwisha kusema tukimwachia mke wake hai atasahau kuhusu hili , ameongea kauli hii mbele ya watu wengi hivi hawezi kwenda kinyume” Jamaa aliefahamika kwa jina la Sean aliongea.
“Kaeni kimya , upo wapi ujasiri wenu? Kwanini ghafla tu mnakiogopa kifo?”Aliongea Helena.
Sean , Comb na wengine walikuwa na sura zilizokuwa na hali ya uchungu.
“Helena kubali kushindwa , tunashindana na Lucifer , nguvu zake ni kitu ambacho hatuwezi kushindana nacho , mbele yake sisi hatuna tofauti na sisimizi tu”Karibia watu wote wa Metal Tide walimwangalia Helena kwa macho ya kubembeleza.
Regina mara baada ya kuona tukio hilo , hatimae alijua kwanini Hamza aliamuakutumia maneno ya kikatili.
Hamza alitumia ngumi tatu tu kumuua Gonzalez na kwa wakati mmoja alikuwa pia ameiharibu kinga ya kundi lote la Metal Tide na kufanya wanajeshi wote waliobakia kukosa kujiamini kabisa na kuwafanya wote kutaka kujisalimisha.
Lakini licha ya yote , Regina alijikuta aishangazwa mno na mwanamke Helena, yanaweza kuwa maamuzi mabovu kwa upande wa Helena kutokana na uaminifu wake lakini kwa wakati mmoja ilikuwa ni sifa ya fahari kama mfuasi kwa kiongozi wake.
“Kaeni kimya nyie wasaliti? Mnadhani kapteni alikuwa akijipambania mwenyewe? Ameamua kujitoa kwa ajili yetu wote. Sio yeye aliewaajiri na kuwafanya kupata hela nyingi? Kwanini mnataka kumsaliti kikatili?”Aliongea Helena kwa hasira na uchungu mwingi.
“Tuliweka rehani uhai wetu kwa ajili ya hela tulizopata! Ndio tunamshukru kapteni kwa yale aliotufanyia lakini hatuwezi kuweka rehani uhai wa familia zetu kwa ajili ya kapteni aliekufa”
“Kweli kabisa! Helena hebu acha kuwa mbinafsi, unapaswa kuzingatia maisha ya kila mtu”Aliongea Sean.
Helena alikuwa na hasira mno kiasi kwamba mwili wake ulianza kumtetemeka. Palepale alizungusha mkono wake katika shingo ya Regina na kusimama na kisha alitumia kisu kukandamiza katika shingo yake.
Regina na sura yake ya kirembo alijikuta akifubaa huku akili yake ikiwa tupu. Hakudhania Helena angekuwa mgumu namna hio.
“Wote kaeni kimya! Mimi Helena sipo tayari kuwa msaliti. Natii maelekezo ya kapteni na utii wangu kwa Metal Tide , hivyo siwezi kwenda kinyume na kiapo changu. Nitaua kwa ajili yake sasa hivi….. Arghhh..”
Kabla Helena hajamalizia sentesi yake alijikuta akitoa mguno wa maumivu.Macho yake yalikodoa na kwa uchungu mwingi aligeuza kichwa chake na kugeuka nyuma na kumwangalia Gray.
Mkono mmoja wa Gray ulikuwa umeumia lakini mwingine ulikuwa ukifanya kazi vizuri tu na bila ya kueleweka amefikia kisu muda gani Gray alimchoma Helena kupitia mgongoni kwa kulenga moyo wake.
“Gray!”Katika macho ya Helena kulikuwa na viashiria vya huzuni kubwa, kutokuamini na masikitiko.
“Nisamehe Helena , siwezi kukuruhusu kwa ajili ya mtu aliekufa kutuua kila mmoja”Aliongea Gray akiwa siriasi.
Mara baada ya kuona hivyo , Comb palepale alichukua hatua na kumsogelea Helena na kumpokonya kisu kilichokuwa katika mikono yake na kumuokoa Regina.
Regina aliishia kushikwa na mshituko huku akiangalia kisu kilichotoboa kutoka nyuma na kutokea mbele katika eneo la moyo wa Helena.Hakutarajia hali ingegeuka na kuwa hivyo.
“Tuli.. tulifanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi na mbili pamoja , ila umeamua kunisaliti mwishoni” Aliongea Helena akiwa na machozi katika macho yake huku akimwangalia Gray.
Gray upande wake alikuwa na mwonekano usioelezeka , hakujali tena na palelae alichomoa kisu kutoka katika mwili wa Helena na kuusukumia kutoka kwenye ngazi za viti.
“Nooo!”
Regina mara baada ya kuona Helena akisukumwa chini na kuanza kuporomoka katika ngazi alijikuta akipiga yowe.
“Kwanini mmemsukuma , mmeshamjeruhi tayari asingeweza kuniua?”Aliongea Regina kwa kufoka na kuwafanya Gray na wenzake kupiga magoti mbele ya Regina.
“Samahani sana Ms Regina , tumelazimishwa na Gonzalez kukukamata, tunaomba msamaha wako tafadhari”
Regina alihisi kuchanganyikiwa , hakujua kwanini mambo yamefikia hatua hio , ni kweli alistahili kuokolewa lakini katika moyo wake alihisi hali ya chuki isioelezeka juu ya watu waliomuokoa . Muda huo watu wote walipiga makelele kwa tukio lile.
Hamza palepale aliruka kutoka alipokuwa amesimama kwa mita kadhaa na kwenda kutua katika viti vya ngazi mbele ya Regina.
“Wife , uko sawa?”
Hamza alikuwa amezima ile mbinu mgawanyiko na kufanya kile kivuri kumpotea na kurudi katika hali ya kawaida , ile ile anayomwonyeshea Regina siku zote.
Ukweli Hamza hakuwa na mpango wa kumuua Gonzalez tokea mwanzo, alipanga kumshikisha tu adabu mbele ya watu , lakini mara baada ya kumteka mke wake aliona atumie uwezo wake wa juu kumuua Gonzalez ili kuvunja safu ya ulinzi ya kundi hilo na kuwatengenezea machafuko baina yao ili iwe rahisi kumuokoa Regina.
Ijapokuwa ilikuwa njia hatari tokea mwanzo , lakini ndio alioona ipo salama zaidi na pili hakutaka kuhatarisha usalama wa Rhoda na kutumia uwezo wake wa spidi usiokuwa wa kawaida kujaribu kumuokoa Regina.
Hivyo ni sahihi kusema kwa asilimia mia moja kile alichopanga Hamza kilifanikiwa lakini kwa wakati mmoja alijifunza kutoka kwenye kosa alililolifanya na alipanga baada ya hapo anapaswa kumtafutia Regina mlinzi wa kumlinda masaa ishirini na nne na sio yeye tu kwa kila mtu wake wa karibu.
Regina mara baada ya kusikia neno ‘wife’ kutoka katika sauti alioizoea alihisi ni kama amesubiria neno hilo kwa karne nzima. Lakini kwa wakati mmoja alipoinua macho yake na kumwangalia aliemuita alihisi ni kama mtu mgeni kwake. Mrembo Regina alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa.
Comments