"Usiishie kuchungulia tu shuka umsalimie bimkubwa"
Mlango wa gari ulifunguliwa na alishuka Binti aliyevalia gauni jeupe fupi lililofinka magoti na kuchora umbo lake namba nane sijui sita vuta picha inavyokupendeza ndugu msomaji,, rangi yake ya ngozi ambayo ni nyeupe ilimfanya kuvutia zaaidi, alikuwa ni mrefu wa wastani na nywele zake zilikuwa fupi lainiii, kifupi ni kwamba mwanamke huyo alikuwa ni zaidi ya urembo wenyewe achilia mbali dada zetu wenye nyashi kama viroba vya mpunga
Majirani hasa wanaume walikuwa wakimuangalia kwa macho yaliyojaa uchu Kulikuwa na mbaba mmoja mwenye kitambi akitoka ndani ya chumba chake almanusura ajikwae ni kama vile amemuona malaika
"Huyu ni Bianca mdogo wangu alikuwa akinisindikiza, Salimia" alimtambulisha na kumtaka asalimie
"Shikamoo" Bianca alisalimia, alikuwa ni wale mabinti wenye aibu mbele za watu na idadi ya majirani walioko nje wakimtazama ilichangia.
"Marahaba mwanangu karibu ndani" mama yake Jimmy na monica alimkaribisha na alikubali na kuingia ndani akifuatwa na Cid
Upande wa Jimmy alikuwa akimalizia kupulizia unyunyu na alikuwa amevaa kikawaida sana, T-sheti oversize rangi ya damu ya mzee na suruali nyeusi aina ya Cargo pants.
Alibeba slides zake nyeusi akipanga kuzivalia nje na kutoka zake chumbani kuelekea sebuleni.
Ile anafika sebleni tu macho yake yalitua kwenye kochi lililokaribu na dirisha, aliketi binti asiyemfahamu lakini alivutia macho kwa kumtazama, alikuwa akigeuzageuza shingo akitalii baadhi ya vitu vilivyopo sebuleni kwa utulivu, mwanga hafifu wa jua ulimmulika ngozi yake na kufanya ing'ae kama dhahabu, Jimmy ni kama vile alikuwa kwenye ndoto ambayo hakutaka iishe
Binti yule mara alihisi kuna mtu akimwangalia na alikuwa sahihi kwani alipogeuza shingo hisia zake zilikomuelekeza alikutanisha macho na Jimmy
Jimmy alitoa tabasamu hafifu na kupotezea na kusogea zaidi sebuleni na kumkuta Cid pia akiwa ameketi kwenye kochi
Cid baada ya kumuona jimmy alianza kuongea
"Ndo ushajiandaa? tuondoke sasa na huyu ni mdogo wangu anaitwa Bianca anatusindikiza, Bianca huyu ni rafiki yangu mpya anaitwa Jimmy" alichukua nafasi hiyo kufanya utambulisho
"Ni jambo zuri kukufahamu" Jimmy aliongea pasipo kujibiwa
"Nimesahau kukwambia anashida ya usikivu hivyo ongea naye ukiwa karibu na taratibu" Cid alimueleza
"oh sawa" Jimmy alitingisha kichwa na kumsogelea karibu
"Nimefurahi kukufahamu" alimpa mkono Bianca, na binti huyo hakuongea na badala yalitingisha kichwa kirafiki na kutabasamu kisha aliupokea mkono wa jimmy
"Tuondoke" aliongea Cid
"Subirini kwanza mpate kifungua kinywa kabla hamjaondoka" Aliongea bi mkubwa akiwa ameshika sahani iliyojaa chapati za mayai zikiwa zimetoka jikoni muda si mrefu
"Kwaleo utatusamehe tu mama tumeshiba, tulikula kabla ya kufika hapa ila usiwaze sana siku nyingine tutakuja pia" Cid alijieleza
"Sawa basi vipi na wewe Jimmy utakula kabla ya kuondoka?" alimuuliza Jimmy
"Niwekee kwenye bakuli nitakula njiani" Jimmy aliongea hakutaka kuondoka bila kula kitu na mama yake alichukua kibakuli vile vya mviringo vya kuhifadhia chakula na kuweka chapati za kutosha kisha kufunika na kumpatia
Baada ya hapo waliaga na kuondoka, kwenye gari Jimmy aliketi siti ya nyuma na mbele walikaa Cid na Bianca dereva akiwa Cid
Njiani gari likiwa kwenye mwendo wa wastani huku ngoma ya "Shake it off" ya mwanamziki wa kimarekani Taylor Swift ikidunda na upande wa Jimmy alikuwa bize na chapati zake akitingishwa kichwa kuendana beats
Wakiwa njiani jimmy aligundua kuwa kuna gari mbili aina za land rover defender zilikuwa zikiwaunga mkia tangu watoke kwao
"Hey Cid"
"Naam bro"
"Tunafuatiliwa" Jimmy alimwambia na kumfanya Cid aachie tabasamu
"ondoa wasiwasi hao ni walinzi wetu sikutaka waingie kule kwenu ili kutoleta attention na minong'ono isiyo na maana"
"Walinzi? unataka kusema?"
"Nadhani ni wakati sahihi wa kujitambulisha vizuri kifupi ni kwamba familia yetu ni familia yenye maadui wengi na ndio maana tunalindwa"
"ooh kumbe mbona jana sikuona ukiongozana na hao walinzi?"
"Sikutaka waongozane nami bro ni vile tu nipo na Bianca hapa ndio maana wapo nasi isitoshe ni mtoto wa kike na anahitaji ulinzi zaidi, ila inashangaza umeweza kugundua kama tunafuatiliwa, bro inaonekana upo makini sana"
"Umakini ni jambo muhimu sana mwanaume hupaswi kukaa kiholela holela hata hivyo mtu yeyote angeweza kugundua maana kila kona tunayokata wapo nyuma yetu"
"Hahaha ni kweli bro nilipanga kuja mwenyewe ila kwasababu ya Bianca kuambatana nami wamekataa kutuacha hata hivyo sio mimi ninayewalipa" alimwelezea na Jimmy hakujali sana kuhusu hilo na alibadilisha mada
" Unakwenda kununua piano kweli bro? Mi nilijua unatania"
"Nitanie wapi bro nilikuwa namaanisha"
Muda mchache mbele waliweza kufika kwenye shopping mall kubwa ya kisasa ipatikanayo mjini na gari lilikwenda kupark kwenye sehemu maalumu ya kuegeshea magari.
Ila wanashuka tu walikutana na walinzi sita waliojazia miili yao wakivaa suti wamejipanga ipasavyo kutoa ulinzi na kwa mara ya kwanza Jimmy alijiona kama Don flani hivi mwenye heshima kwa kuzungukwa na walinzi pembe zote nne za dunia
Shopping mall waliyofikia ilikuwa ni ile yenye hadhi ya juu mno, ilikuwa ni shopping mall yenye ghorofa tano kwenda hewani ghorofa la vioo. Na, floor ya chini kabisa ilikuwa ni ya vyombo vya muziki vya kila aina, kuhusu floor zinazofuata hio ni habari nyingine
Waliongozana mpaka ndani kisha Bianca na walinzi wote sita walipandisha juu wakiwaacha Jimmy na Cid chini kwanza Cid hakutaka habari za kufuatana na walinzi kama kumbikumbi kingine wlinzi wataonekana wambea alitaka 'privacy' kidogo
Jimmy na Cid walienda mpaka sehemu ambayo piano hupatikana, kulikuwa na mbalimbali za piano, kulikuwa na piano kubwa(Grand piano) zile ambazo hutumika kwenye maonyesho makubwa na zinatoa sauti ya juu na ni bora zaidi ni kama ile Bosendorfer aliyokuwa akiitumia jimmy kule hotelini, pia kulikuwa na piano za kidijitali ambazo hazikutumia nyaya na hutumiwa kuonganisha vifaa vya muziki vya kielektroniki na mara nyingi hutumiwa studio kutengeneza album, na aina nyingine nyingi
"Karibuni wateja wa nguvu" muhudumu wa kike wa eneo lile aliwachangamkia kwa bashasha na kuwatembeza akiwaonyesha na kutoa maelezo kuhusu piano mbalimbali
"Bro ipi inafaa kwa kutumia nikiwa nyumbani na i bora zaidi?" Cid aliuliza kama vile hakukuwa muhudumu
"Hio si kazi yangu unapaswa kumuuliza muuzaji"
"Miimi nataka maelezo kutoka kwako mtaalamu unadhani nimekuleta uje ushangae? "
"Kwa wewe unayeanza kabisa nadhani hii itakufa" aliongea Jimmy akinyooshea mkono moja ya piano zile za mbao zinazotumia kamba kutoa sauti
"Kwanini hiyo na si zingine? " Ciid aliuliza akitaka maelezo zaidi
"Kwasababu hii ni Bösendorfer 155, sababu ya kiuitwa 155 ni kwa sababu ina urefu wa sentimita 155 sawa na futi tano, Imetengenezwa kwa mbao imara ya spruce, ambayo huongeza usambazaji wa sauti na kutoa sauti ya kipekee kingine ni Inatumia mfumo wa single-stringing, ambapo kila nyuzi ina pini yake ya kushikilia, jambo linalosaidia katika kudumu kwa mlio wa sauti na mwisho kabisa ni "made in Austria" Alimuelezea kwa kifupi na muhudumu alikubaliana kwani alichosema ni sahihi kabisa
"Nadhani kwa maelezo yako inanifaa kabisa haha inaonekana unajua vizurii kuhusu piano vipi kuhusu bei?"
"Bei hubadilika kila nyakati hivyo ni vyema kumuuuliza muuzaji" aliongea akimgeukia muhudumu
"Hili ni toleo la mwaka huu kabisa na kama alivyosema huyu kaka imetengenezwa kwa mbao imara ya spruce hivyo kufanya iwe ghali kidogo" aliongea muhudumu yule
"Wewe taja bei usiwe na shaka hii lazima niinunue" Cid alimtoa wasiwasi
"Ni dollar elfu themanini na tano thamani sawa na shillingi millioni mia mbili ishirini na nne"
"Nitanunua" Cid alijibu bila wasiwasi na kumfanya Jimmy ameze mate kama vile hayataki kupita kooni na aliishia kujiambia ingakuwa yeye hata awe tajiri kiasi gani haweza nunua piano kwa bei kichaa namna hio labda gari
Palepale muhudumu alitoa kifaa cha kielektroniki cha kulipia kwa kadi ya benki akisubiri malipo na Cid alitoa kadi nyeusi ya benki na kuipitisha kufanya malipo
Kwa wale msiojua kadi nyeusi ni kadi za benki ambazo hutolewa na taaisi za kifedha kwa watu matajiri zaidi UHNWIs(Ultra High Net Worth Indibiduals), Ni kadi ambayo huwezi pata hivihivi tu hutolewa kwa mwaliko tu kwa wale waliokishk vigezo vya kifedha vya juu mabillionea, wafanya biashara wakubwa, viongozi wenye maokoto ya uhakika n.k
Vigezo hivyo ni kuwa na kiasi kingi cha pesa na kutokuwa na kikomo cha matumizi unatakiwa kutumia zaidi ya billioni moja kila mwaka. Jimmy hakuwa mshamba kivile na aliweza kuigundua na kujiuliza huyu rafiki yake itakuwa anatoka kwenye familia kubwa inayotambulika nchini na palepale mawazo ya kumchuna pesa mbili tatu yalianza kumjia
"Asante sana unakaribishwa tena muda wowote kununua nidhaa pia tunasafirisha bidhaa mpaka mahali unapohitaji bure kabisa unachopaswa ni kutupa anwani ya unapotaka ifikishwe" aliongea muhudumu na Cid alimpatia address ya anapoishi na mara moja muhudumu yule alianza mchakato wa kusafirisha bidhaa hiyo
"Vipi naruhusiwaku cheza piano kidogo? " Jimmy aliuliza
"Ndio unaweza isitoshe hakuna wateja eneo hili" alimruhusu
Jimmy alinyoosha vidole vyake vizuri kiasi cha kutoa mlio na kuketi kwenye kistuli maalumu cha wacheza piano na kuanza kubonyeza taratibu kwa ustadi
Awamu hii ulikuwa ni mtindo tofauti na aliocheza mara ya kwanza, ulikuwa ni wa tofauti ni mtindo maarufu ufahamikao kama Moonlight sonata ambao mwanzilishi wake alikuwa ni Ludwig van beethoven mcheza piano maarufu wa miaka ya 1800s
Ni mtindo ambao huwakilisha hali ya huzuni na inasemekana beethoven alitunga mtindo huu wakati akiwa anaanza kupoteza uwezo wake wa kusikia na kujikatia yamaa, ni mtindo unaoelezea hisia za huzuni, ina sehemu tatu sehemu ya kwanza ni ile ya taratibu ya pili ni ile ya kawaida na ya mwisho ni ya haraka na kipekee sana
Sasa Jimmy alikuwa akicheza sehemu ya kwanza ya taratibu huku akiimba kufuatana na mziki huo
🎶In the silence I walk alone🎶
🎶Under the skies that are yet unknown🎶
🎶A story untold, a heart unknown🎶
🎶I search the truth in the shadows I have grown🎶.....
Alinyamanza baada ya kuhisi ongezeko la watu eneo hilo maana aliweka umakini kwenye piano
"Mbona umeacha sasa unapaswa kuendelea mpaka mwisho huku ni kukatana stimu bhana" Cid alitoa lawama
Japokuwa urafiki wao ni.wa siku mbili ila walionekana ni kama marafiki wa siku nyingi sana
Jimmy aliishia kutoa tabasamu tu na kumwambia hakuwa akitumbuiza bali alikuwa akijaribu kuona ubora wa sauti.
Kwa watu walioongezeka walikuwa ni wahudumu wa floor hiyo jumla wakiwa sita, Bianca pamoja na msafara wa walinzi, haikueleweka walifika hapo muda gani, na aliweza kumsikia Jimmy mwanzo mpaka alipoishia, unapaswa kuelewa kwamba licha ya Bianca kuwa na shida ya usikuvu haikumaanisha ni kiziwi, hapana, ni kama mfano wa bendera ipeperukayo kutokana na upepo kuwa mkali lakini inaacha kupeperuka upepo ukiwa mdogo ndivyo ilivyo kwa Bianca kuna muda masikio yanakuwa yanasikia vizuri na mda mwingine yanagoma katakata
Kwahiyo hapo alisikia vyema na kuvutiwa na mtindo huo licha ya kutokuonyesha waziwazi.
Kwa nje ya mall hiyo kupitia vioo Jimmy aliweza kuona gari la Toyota Alpha jeusi likipiga breki ya nguvu na walishuka watu kadhaa wamefunika nyuso zao kwa kuvaa vinjago mikononi wakishika siraha za moto aina ya M16 na palepale akili yake ilimuambia kuna ujambazi unaenda kufanyika
"Laleni chini!" Jimmy alipiga kelele na kuwarukia Cid na Bianca wakilala chini na kwenda kujificha chini nyuma ya Piano
Walinzi now walikuwa 'alert' muda wote na kujikinga lakini haikueleweka kwanini hawakuweza kugundua hatari hiyo mapema, upande wa wahudumu walikuwa wamechelewa sana kwani risasi zilianza kumwagwa kwa fujo bila huruma na kuondoka na maisho yao(wapumzike kwa amani)
Basi yalikuwa ni majibizano ya risasi kutoka pande mbili upande wa walinzi na upande wa majambazi hao
"Hawa wapumbavu wanapata wapi ujasiri wa kufanya ukatili namna hii mchana kweupe, Shenzi!" mlinzi mmoja alimaka
"Kuwatusi haitasaidia kitu fanya kuwasiliana na polisi hatuwezi kumalizana nao wote hawa pasipo kuhatarisha maisha ya raia wengine" mwingine aliongea
"Shaw fanya mawasiliano sasahivi" Kiongozi wa walinzi alitoa amri
"Sawa mkuu.... Aarggh" alipiga ukelele wa maumivu baada ya risasi kupenya kwenye mbao kuutoboa mguu
Upande wa Jimmy, Cid na Bianca walikuwa wamejificha nyuma ya piano kubwa yenye mbao nene isiyoruhusu risasi kupenya kirahisi, Bianca alikuwa amepaniki na kutetemeka kwa woga mara baada ya kushuhudia maisha ya binadamu wenzake yakiondoshwa mbele ya macho yake, hakika hambo hilo lilimuogopesha sana na machozi yalianza kumtoka kama mfereji kibaya zaidi harufu ya damu ilimtia kichefuchefu, alikuwa akiogopa kupoteza maisha yake angali akiwa mdogo ndio kwanza alioka kutimiza miaka ishirini wiki chache zilizopita na anatarajia Kuanza Chuo mwezi ujao
Upande wa Jimmy aliishia kusikitika na kufanya ishara ya msalaba kama mapope wafanyabyo wakiaga maiti, ilionekana haikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia binadamu akikata roho mbele ya macho yake. Cid naye hakuwa ametulia alikuwa akiwatukana matusi ya kila aina majambazi hao alienda mbali kwa kuwaita majina ya ajabu ajabu ambayo hayakuwa kusikika ulimwenguni, lakini sasa wangemsikia?
"Tukiendelea kuzubaa hapa tunakwenda kuitwa marehemu" aliongea Jimmy kwani risasi zilizidi kutoboa mbao mdogomdogo na suala la muda tu kuweza kupenya
"Tunafanyaje bro una mpango wowote?" Cid aliuliza akiwa hayupo tayari kufa na kumfanya jimmy aangalie huku na huko kutafuta kitu na palepale alitoa tabasamu
TO BE CONTINUED..........
Comments