Reader Settings

SEHEMU YA 207.

Hamza aliweza kuona hali ya hofu  katika macho ya  Regina  na kumfanya ahisi moyo wake kuuma na  palepale hakujiuliza mara mbili  na kumkumbatia kwa nguvu kumhakikishia usalama.

Aliishia kumpiga  piga mgongoni  kumtuliza huku akipapasa nywele zake  kumfariji.

“Usiwe na wasiwasi mke wangu. Nitakununulia Donati  zenye strawberry tukirudi nyumbani  na utasahau kila kilichotokea hapa..”

Regina mara baada ya kusikia kauli hio ni kama  ameshituka kutoka ndotoni na kugundua mwanaume aliemkumbatia hakuwa amebadilika. Ni yule yule mwanaume aliemzoea.

Ilikuwa ni kwasababu ya  uhalisia wa maisha yake yaliopita ndio ulimduwaza mpaka kushikwa na hofu kwa muda.

Watu wengi mara baada ya kuona tukio hilo walijikuta wakipiga makelele mengi  na makofi ya kumpongeza Hamza.

“Kumbe ndio  ilikuwa  plan yake , nilishangaa kwanini bosi ametumia nguvu nyingi kumaliza pambano kikatili kumbe…”Aliongea Mameni.

“Bosi amepitia mengi sana  na ndio maana siku zote  anafikiria  hatua  mbili mbele kuliko  sisi”Aliongea Asmuntis.

Black Fog kuona namna Hamza alivyomkumbatia Regina kimahaba  macho yake yalijawa na wivu  mwingi.

Upande wa Regina aliweza kuhisi joto la kumbatio la Hamza  na alijihisi utamu moyoni  lakini kwa wakati mmoja aibu  ya kike ilimvaa kutokana na macho ya watu wengi yalivyokuwa yakimwangalia.

“Wewe unanichukuliaje  , nawezaje kusahau kila kitu kwa kula tu Donati?” Aliongea Regina huku akimsukuma  Hamza. “Halafu hata  hujajisafisha lakini unanikumbatia kwa  kunibana  hivi?”

Hamza muda ule ndio sasa anashituka na kugundua mikono yake ilikuwa na damu  na  kumfanya atoe tabasamu la kizembe.

“Samahani mke wangu , kwa jinsi ulivyopendeza  na  vazi la kijeshi nilishindwa kujizuia  na kutamani sana kukumbatia”

Regina mara baada ya kusikia hivyo alishindwa kujizuia   na kutabasamu. Kwa namna alivyopendeza ni kama  ua linalochanua nyakati  za kiangazi kirefu.

Mara baada ya kumuona Regina ametabasamu , hatimae moyo wake ulijawa  na ahueni  lakini bado hatia haikumtoka.

“Nilifanya makosa , sikudhania watakuteka , siku nyingine nitahakikisha..”

“Shhii… wewe sio malaika , huwezi kunilinda kwa asilimia mia moja. Siwezi kukulaumu bila sababu”Aliongea Regina , alijua  kama sio Hamza angekuwa ameshakufa muda mrefu tu  na hata kama angekufa awamu hio lisingekuwa kosa  lake.

Pembeni, Gray na wenzake waliendelea kuomba  kwa kubembeleza wakitaka Hamza aache hilo lipite  na Hamza mara baada ya kuwageukia aliishia kuwaangalia kwa shauku.

“Kwanini bado tu hamjaondoka?”

Gray na wenzake mara baada ya kusikia kauli hio ,  wangewezaje kutokujua kauli hio inamaanisha nini . Haraka sana  walisimama na kukimbia kutoka ndani ya eneo hilo.

Upande wa Regina muda ule aliweza kukumbuka  jambo na kuanza kupiga makelele .

“Helena  jamani! Hamza  naomba usaidie kumuokoa Helena”Aliongea Regina kwa kubembeleza na kauli hio ilimshangaza Hamza. Alijikuta akiangalia upande wa chini Helena alipodondokea  namna alivyolala akiwa katika dimbwi la damu.

“Unataka kumsaidia! Kwanini?”Aliuliza.

“Anatia huruma sana kwa namna alivyosalitiwa na  wenzake , ukweli alichokuwa akifanya ni kutimiza kiapo chake , sidhani kama ni kosa”Aliongea Regina.

“Wife , huyo ndio mtu alietaka kukuua kumbuka”

“Mtu alietaka kuniua sio  Helena ni kiongozi wake! Kwanini unakuwa hivyo, wewe si daktari? Haraka basi msaidie kumuokoa”Aliongea Regina akiwa na wasiwasi mkubwa.

Hamza aliishia kumwangalia mwanamke huyo na nia yake ya dhati ya   kutaka kumsaidia Helena na alishindwa  kujizuia na kuhisi kitu kisichokuwa cha kawaida katika moyo  wake.

Pengine katika macho ya mwanamke huyo   kila kitu kwake alichukulia kama vitu vyepesi mno. Alimuona kama mwanamke mfanyabiashara ambae siku zote alizingatia mahesabu lakini  alishangaa kuona upande wake mwingine  wa kitoto.

“Basi sawa ,  nitajitahidi kumsaidia kama ulivyosema” Hamza alijua hata kama atamsaidia Helena kupona hatokuwa na  hatari yoyote  kwake.

Hivyo licha ya watu  kumshangaa aliishia kukimbia chini  na  kumbemba  Helena juu na mkono mmoja.

“Nini kinaendelea! Wanataka kumuokoa?”

“Lakini  si Helena alitaka kumuua mke wake?”

“Inaonekana mke wa Lucifer anataka kumuokoa  Helena”

“Devil  and Angels! What a couple” Aliongea mwingine akimaanisha  Hamza ni shetani  na Regina ni malaika  na kushangazwa na mahusiano yao.

Upande wa Regina hakujali watu watafikiria nini , alichotaka kujua kwanza ni kama Helena alikuwa hai na anaweza kupona.

“Vipi , bado yupo hai , anaweza kupona?”

“Kama angekuwa hospitalini chumba cha upasuaji , pengine angeweza kupona ila  kwa hapa  naweza sema  tumechelewa..”

“Kwahio unamaanisha amekufa?”Aliuliza Regina kwa masikitiko na Hamza alionekana kupata wazo.

“Kuna njia tunaweza kujaribu”

Mara baada ya kuongea hivyo bila ya kusubiri Regina kumuuliza ni njia gani , Hamza aliubeba mwili  wa Helena ambao umekwisha kuwa wa baridi  na kukimbia nao mpaka katikati ya uwanja na kumsogelea Silvia.

“Madam, hili ni ombi kutoka kwa mke wangu,  naomba unisaidie”

Muda ule  ndio sasa watu walikumbuka kulikuwa na  Gwiji mwenye miujiza ya uponyaji kutoka  kwa wavuna nishati wa ufunuo wa nuru.

“Pale sawa! White Queen anaweza kumponyesha”

“Lakini  mume wake ameuliwa na Lucifer. Atakuwa tayari kumsaidia?”

Hadhira ilijawa na shauku  nini kingetokea. Je White Queen angekataa kumsaidia Hamza kutokana na  mume wake kuuliwa?.

Silvia alionekana kushituka  kwa dakika kadhaa  na kisha palepale alitoa tabasamu.

“Sijategemea  Hamza umekwisha kuoa na unataka nimpatie  mke wako zawadi , kama ni hivyo basi na mkono huu  wa baraka ya miujiza na uwe zawadi  kwake”

Mara baada ya kuongea vile  alichaneli nguvu kumtoka kupitia mkono wake na ukaonekana mwanga  mwepesi  mweupe kama wingu ambao ulianza kuzingira mwili wa  Helena kimaajabu.

Dakika ile damu iliokuwa ikimtoka Helena iliacha mara moja  moja  na hali ya joto  ilianza kuurejea mwili wake

“Jeraha la moyo haliwezi kuponyeshwa na  ufunuo wa nuru , lakini kupitia mkono wangu wa baraka  ya muujiza , nimezuia hali yake kutokuwa mbaya zaidi na  pengine utakuwa na muda wa kutosha kumfikisha hospitalini  na kumfanyia upasuaji”Aliongea Silvia akiwa na tabaasmu.

“Mpaka hapa inatosha ,  na nitaondoka nae kwanza.  Kwa hali ilivyo sidhani pia kama  mkutano utaendelea”

Hali ya Arena ilikuwa mbaya sana , jukwaa maalumu limekwisha kuharibika na hata  eneo la juu  liliharibika pia , hivyo  kwa  Baraza hilo la maksi kuendelea ni mpaka maboresho yafanyike kwanza.

Hivyo Hamza palepale aliomba kuandaliwa gari na   alimchukua Helena na mke wake na kwenda hospitali ya karibu ndani ya  mji huo wa  Limour.

Ndani ya hospitali Hamza alifanya upasuaji kwa zaidi ya masaa mawili na nusu  na hatimae alifanikiwa kuokoa uhai wa Helena.  Ilikuwa rahisi pia  kumuokoa kwasababu  kwa uzoefu wa Hamza aligundua  Gray  hakudhamiria kumuua moja kwa moja  Helena  na badala yake namna alivyokizamisha kisu alitengeneza  asilimia kadhaa za  Helena kupona , lakini hata hivyo kama isingekuwa msaada wa Silvia ingekuwa ngumu.

Helena mara baada ya kutolewa chumba cha upasuaji , hatimae presha ilimshuka  na kujihisi ahueni kubwa.

“Wife umeridhika sasa? Ila kama akiamka na kutaka kukuua tena sitokuwa  na muda wa kumuokoa tena”Aliongea Hamza huku akicheka.

“Sidhani kama itatokea , ameshakufa tayari na ukamfufua, Sidhani  atakuwa tena chini ya  kifungo cha  kutimiza  kiapo chake kwa Gonzalez”

“Wife  nimekuja kugundua muda mwingine una roho nzuri kiasi kwamba inakufanya uwe  kama mgonjwa ,  nikifikiria swala la Lamla na  la Helena, nakuona kama mama Teresa wa wakati wetu” Aliongea Hamza huku akitingisha kichwa kumuonea huruma mke wake kwa kuwa na roho nzuri kupitiliza.

Regina kusikia kauli  hio alishikwa na haya kidogo  na kuishia kumwemwesa lipsi zake.

“Nimemchukulia kama mwanamke mwenzangu aliesalitiwa na watu wengi  na alieshindwa kujizuia , ndio maana..”

“Kwenye ulimwengu wa giza tendo la huruma moja tu linaweza kukufanya upoteze uhai. Naweza kuonekana mkatili lakini  ukweli  si kuzaliwa mkatili  ni  uzoefu ndio maana”

“Basi sawa, najua mimi ni  mjinga lakini  nilishindwa kujizuia. Isitoshe  Helena si mtu wa kawaida tu  mbele  yako? Kama atageuka na kuwa mbaya kwangu  unaweza kunilinda tena. Hata hivyo mimi sio mtoto mdogo , nimetekwa leo  na kidogo tu niuliwe na nimechoka sana ..  acha kuongea kama unanifokea basi”Aliongea Regina  huku akionyesha hali ya machungu kwenye macho yake.

“Haya basi yameisha mke wangu,  kwasasa hakuna namna, nitakuwa na wasiwasi ukirudi Paris peke yako. Kwanini usikae na sisi hapa , haitokuwa mbaya kama utashiriki  katika mikutano iliobakia ..”Alishauri  Hamza.

“Naweza kushiriki? Watu wa Baraza la maksi si watanizuia”

“Mpaka sasa ushajulikana ni nani  kwangu , nani anaweza kuthubutu kukuzuia”

“Najua una nguvu na wanakuita mtawala wa kuzimu na Gwiji  lakini sina vigezo  vyovyote vingine mimi kama mimi”

“Wewe tayari ni mke wangu , vingezo vingine vya kwako vya nini?”

“Lakini hujanichumimbia na kunioa  vizuri”Aliongea Regina kama mtoto huku akipepesa macho yake haraka haraka.

Hamza alijikuta akikosa usemi , mara baada ya kufikiria swala la kuchumbia tena  na harusi  kichwa kilianza kuuma. Sio kama hakutaka lakini  bado hakupata  wazo sahihi la namna ya kuchumbia.

“Wife nipe muda , nikishapata wazo zuri  haraka  sana nitakuchumbia na  tufunge harusi”

“Usijali , unaweza kufanya taratribu taratibu , isitoshe sio kama nina haraka na harusi wala nini.”

“Hapana , hili swala linatakiwa kuharakishwa”Aliongea Hamza  huku akijiambia namna ya kupunguza ukauzu  wa Regina kwake  ni kumpa kile  kitakachomridhisha ili  amuweka kifuani na kwa namna hio  kidogo atarahisisha  baadhi ya matatizo mengi yatakayojitokeza.

Wawili hao mara baada ya kutoka nje ya hospitali , watu wa Inferno walikuwa wakiwasubiria  na kila mmoja alisogea  na kumsalmia Regina kwa kumuita Shemeji.

Jina hilo lilimfanya Regina kuhisi aibu  na kufanya sura yake kuwa ya moto  na hio yote ni kutokana na kwamba watu hao wengi walikuwa ni wazee  kuliko Hamza, lakini waliokuwa wakifanya ni kama Hamza ndio aliekuwa mzee.

“Wife ngoja nikutambulishe , huyu ni  Azzle,   unaweza kumuita tu Aziza  kurahisisha,  ni mhunzi anapenda sana kugongelea vyuma, Huyu  hapa  ni  Asmuntis au mtu mchafu,  pepo lake linamruhusu kuoga mara moja tu kwa mwaka. Huyu Bonge  hapa  tunamuita Mameni , anajishughulisha na biashara za siraha , anapenda sana kamari  na  wanawake . Huyu hapa  Braza tunamuita  Leviathani  a.k,a Ngisi  mkubwa kwasababu  bendera  ya meli zake  zina chata la Ngisi , ana mtoto mdogo wa kike  na sio mtu wa kunyoa kipara , alikuwa na rasta ndevu na ngumu kama maganda ya  mua.  Kuhusu huyu mrembo wa sura hapa   ni mshikaji wangu Berly  ,  ni mvivu kupindukia , ukiachana na kupenda kwake kula vinono lakini vilevile ana swaga hatari mbele ya wanawake. Ujuzi wake mwingine ni  kujua kukopa  mpaka wanaomdai, hana sifa nyingine kubwa..”

Regina  mara baada ya kusikia utambulisho huo  alijikuta akichanganyikiwa , alijiuliza kwanini kila alietambulisha  katika kundi hilo hakuna  anaeonekana kuwa wa kawaida. Lakini hata hivyo alijua watu hao  walikuwa maarufu zaidi katika ulimwengu wa giza  na walikuwa marafiki  wa Hamza wa kufa na kuzikana . Hivyo hakuwadharau na  alijitahidi kufahamiana nao vizuri.

Mara baada yakufikia zamu ya Rhoda , Regina alionekana  kushangaa.

“Dada  na wewe ..”

“Samahani sana Dada Regina kwa kukudanganya ile siku,  Master wangu ni Asmuntis na mimi kazi yangu ni  kuua”

“Wewe ni muuaji!?” Regina  alishangaa maana hakutegemea msichana mzuri na  mwenye sura ya kipole kama huyo  angekuwa muuaji.

“Ndio” Alijibu  Black Fog bila  ya kuwa na aibu kuhusu kazi yake.

Ijapokuwa Regina alijikuta akijisikia furaha  hatimae kumjua mume wake , lakini  mara baada ya kukutana na watu hao  wasiokuwa wa kawaida  alishikwa na wasiwasi.

“Bosi , watu wa Baraza wanasema  kazi  ya kuweka mambo sawa imekaribia kumalizika , unaweza kujunga kwa ajili ya kumalizia kikao cha leo”Aliongea  Asmuntis.

“Okey! Napaswa kuwakabidhi tuzo leo , hivyo  twendeni maana sitaki hili swala lipite”

Mara baada ya kurudi  ukumbuni   watu wengi waliwaangalia , asilimia kubwa walimwangalia Hamza , tofauti na mwanzo sasa walionekana kumheshimu zaidi.

“Hehe.. bosi  ndondi ulioonyesha leo imekuongezea mashabiki wengi sana. Unaonaje tukirudisha  umoja wetu wa Inferno. Nitatamba sana mjini”Aliongea Bellie.

“Hebu acha zako Belli , hii ndio mara yangu ya mwisho kuhudhuria Baraza la  maksi , kama isingekuwa   kitengo cha Malibu kunishinikiza nisingeshiriki”Aliongea Hamza kwa kingereza  na kufanya wenzake kukubaliana kinyonge , lakini upande wa Regina alionekana kunyaka baadhi ya maneno.

“Una uhusiano  gani na  kitengo cha Malibu?”

“Mke wangu ni stori ndefu, nitakuambia tukifika nyumbani”Aliongea Hamza.

Kila mmoja alirudi  katika siti  yake  huku Regina akizungukwa   na watu na kuwa kama  malkia.

Mara baada ya kila mtu kupata muda wa kupumzisha akili kidogo ndio sasa waligundua  takataka na mchanga vilivyokuwa vimechafua eneo hilo vimesafishwa . Lakini hata hivyo jukwaa  ambalo liliharibiwa  halikutengenezwa upya.

Vyuma vyuma na viti  na matofali yalikusanywa na kuweka  katika eneo moja na kutengeneza kifusi.

Ukiachana na  Hamza , magwiji wengine ambao walienda kupumzika  walilerejea pia.

Mzee Maxim , ambae  ni raisi wa Baraza  la maksi   alimsogelea  Raisi wa Adept Association  na kisha waliongea kidogo kwa sauti ya chini. Kwa namna  alivyokuwa akiongea  mtu wa kawaida angesema Maxim ni kichaa kwa kuongea na koti  na suruali hewani.

“Jamani naombeni utulivu wenu , kutokana na  jukwaa letu  kuharibika  tutajenga la dharula sasa hivi  na nimemuomba Mr Air  kutusaidia  katika  jambo hili, naombeni tumshukuru  kwa kumpigia makofi mengi”

Mara baada ya  Maxim kuongea hivyo ,   watu walianza kupiga makofi mengi  ya kumshangilia  na hio yote ni kwamba  Mr Air alikuwa ni mtu wa  mambo ya chini chini sana , ni adimu sana kuonyesha uwezo wake , hivyo  ni kama  kujenga jukwaa la dharula  ni nafasi ya kuona uwezo wake.

Hata Hamza mwenyewe na magwiji wengine , walijawa na shauku ya kutaka kuona ni kwa namna gani Mr Air anakwenda kujenga jukwaa ndani ya muda mchache.

Mr Air  alisogea mpaka katikati ya eneo la wazi  na bila  ya kutoa sauti , chini ya macho zaidi ya  watu elfu therathini  , ghafla  tu hali ya mkondo wa upepo ndani ya eneo hilo  ilibadilika na  kufumba na kufumbua   ule upepo   uligeuka  kimbunga na kuanza kumuinua kutoka chini na kumpandisha juu hewani.

Previoua Next