Alitabasamu mara baada ya kuona kitu kama ngao flani hivi ya chuma umbo la mstatili, na palepale alivua Slides zake nakubaki peku.
"unataka kufanya nini?" Cid aliuliza
"Unataka kufa?" naye badala ya kujibu alimtupia swali
"Hapana" Cid alijibu
"Tulia sasa, kama sikosei wanatumia silaha ya M16 na kila magazini inabeba risasi thelathini nadhani mda si mrefu zinakwenda kuisha lakini hatupaswi kusubiri nani anajua labda wamebeba magazini zingine?" Jimmy alifafanua ilionekana alikuwa amepiga mahesabu ya kimya kimya
"Halafu inaonekana wanalenga kumuua mtu" aliendelea na Cid aliishia kutoa ishara ya "Sio mimi"
"Kama sio nyinyi ni nani si umesema familia yako ina maadui wengi au unaniona fala sio?" jimmy aliwaza kichwani mwake
Mara mlio wa risasi ukakoma na jimmy haraka alitambaa kwa kulala kutumia vifuti na magoti kama mwanajeshi akihama upande mwingine aliokusudia na mara baada ya kujiegamiza kwenye piano nyingine risasi zilianza kurindima tena safari hii zikielekea upande wa jimmy peke yake
"Rafiki yako ni kichaa" Bianca kwa mara ya kwanza aliongea tangu wafike hapo maana hata walinzi wenyewe licha ya kuwa na siraha hakuna aliethubutu kutoka pale alipo, vipi kuhusu jimmy? hakuwa na siraha yoyote ni ujasiri ulioje!
"Nadhani ana mpango"
Upande wa jimmy alishika ipasavyo ngao ya chuma iliyokuwa pembeni yake na kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha, ghafla kwa spidi alichomoka pale alipo akielekea upande wa majambazi wale akijinga na ngao ya chuma
"Bang! Bang! Bang! Bang!" mlio wa risasi na ngao ya chuma ulisikika na mlio wa sirasi ukakoma magazini zimeisha risasi na Jimmy hakutaka kuwapa nafasi pengine labda wana magazini nyingine, na kwa nguvu aliirusha ngao kumlenga mmoja wa wale majambazi kwenye shingo na alikuwa na shabahi, ngao ililenga kichwa kisawasawa na jitu kuanguka chini kama furushi akipoteza fahamu
"Shit! Huyu mshenzi inaonekana ana mafunzo" Kiongozi wao alimaka kwa hasira baada ya kushuhudia tukio hilo na idadi yao kupungua wakibaki watatu kwani jumla walikuwa wanne na mmoja ndio alikuwa amezimia
"Tumeishiwa risasi" mwingine aliongea
"Damn!"
Kwakuwa waliishiwa na risasi Kwenye M16 zao ni Kiongozi wao pekee alikuwa na "back-up plan" nayo ni bastola na wakati anachomoa na kuikoki Jimmy huyu hapa mbele yake
Anakuja kushtuka bastola haipo mikononi mwake ni kitendo cha haraka sana
"Paah! Paah! Paah! Paah! Paah! " Zilipigwa risasi tano Tatu kila moja ilitua kwenye kila goti la majambazi hao wakipiga kelele za maumivu na mbili zilitua kwenye matairi ya gari walilokuja nalo
"Si unaona ninsi inavyouma lakini hayo maumivu hayatoshi kufidia vifo mlivyovisabisha" Jimmy aliongea akimlenga kiongozi wao kwenye paji la uso
"Niue tu hata hivyo maisha hayana umuhimu sana" alifumba macho akiwa tayari kufa
"kwako wewe na hawa wapuuzi wenzako labda vipi kuhusu wale waliokufa kwa mikono yenu? Mliwauliza kama kuishi kwao ni muhimu ama lah? Hivi unajua maisha yana thamani gani? Baba anahangaika kila siku kwaajili ya familia yake, mama anapambana na ku'save kila senti kwaajili ya maisha bora ya baadae kwa bintiye, hao wadada mliowaua ni binti za watu pia pengine hata wao wana familia zao ambazo zinawategemea na wanawasubiri halafu unaniambia kuishi hakuna umuhimu? Wewe ni mpumbavu haswaa na katika wapumbavu niliobahatika kukutana nao nakupa namba tatu" Jimmy aliongea maneno hayo
"lakini mwisho wa siku kifo ni sehemu ya maisha yao kitawakuta tu"
"Hayo maneno nenda kamwambie mama ambaye ametoka kujifungua kwa uchungu na kumshika mtoto wake mchanga kwa mara ya kwanza, kwa mwanajeshi aliyetoka vitani salama kurudi nyumbani, kwa mtu ambaye amepoteza kila kitu lakini akapata sababu ya kusimama tena uone jinsi ulivyo mpumbavu" jimmy aliongea na kumsogelea karibu akichuchumaa na kuendelea
"Maisha hayana thamani kwasababu tunakufa ni kwa....... Kwanza sitaki kupoteza muda kumuelewesha mpimbavu ambaye mwisho wa siku bado anang'ang'ania upumbavu wake na juhudi zangu kwenda bure" kisha alisimama
"Mwisho wa siku na ngojera zako zote lumeshika bastola kutekeleza mauaji" alicheka yule kiongozi
"Unakosea we mpumbavu na siku ukijua ya kuwa wewe ni mpumbavu na kwanini unaitwa mpumbavi basi kumbuka kati ya wale waliokuita mpumbavu mimi ni mmoja kati yao niliyekuita mpumbavu kwa hekima sana ili upate kujitambua kwamba wewe ni mpumbavu" aliongea na kumuongozea risasi ya goti jingine
"Aaarggghh" alipiga kelele kiasi kwamba sauti ilianza kufifia
"Shh shh sshhh!" jimmy alimpa ishara ya kunyamanza
"Mimi sio muuaji" alivyomaliza kutoa kauli hiyo Cid alitoka mafichoni pamoja na Bianca na walinzi wake
"Nyie washenzi mmenisababishia hasara" Cid aliwasogelea na kuwatandika mateke kwa hasira kila neno moja alilisindikiza na teke
Hasara anayozungumzia ni kuhusu piano yake mpya ambayo hata hakuigusa iliharibiwa kisawasawa na matobo ya risasi, karibia vinanda(piano) vyote viliharibiwa na risasi
"Bro wewe ni jasusi?" Cid aliuliza kwa wasiwasi
"Hapana ondoa shaka nilibahatika tu kupitia mafunzo mbalimbali" aliongea ukweli
"Kumbe ulipita jeshini!"
"Sio jeshini ni mzee mmoja myahudi alinifunza mbinu mbalimbali za kujilinda kama shukrani" hakuona haja ya kuficha
"Usiniambie bongo kuna myahudi"
"Kwanini isiwezekane bro mbona kuna wachina wazungu, waarabu halafu akosekane myahudi?"
Kwa jinsi wanavyoongea ni kama vile hakuna kitu kilichotokea Isipokuwa kwa mrembo Bianca ambaye bado alikuwa na hofu licha ya yote kuisha pengine ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia uhai wa watu ukimtoka mbele ya macho yake
Jimmy alimfata Bianca na kumsogelea karibu kabisa akimshika mabega yote mawili "Usiogope kila kitu kimepita sawa? na ni jambo la kushukuru upo salama pamoja na kaka yako kuhusu wengine ni ajali imetokea hivyo tunapaswa kusahau" aliongea kwa sauti ya upole akimtuliza
Mara Bianca alianza kulia tena safari hii akitoa sauti, ni kwasababu ya hatia aliyoihisi moyoni, dada za watu wamekufa kwasababu yao, haikuwa mara ya kwanza kutaka kuuwawa maana alishatekwa sana ila siku hiyo ya watu kuuliwa mbele yake wasiokuwa na hatia na maadui katika familia yake, alijiambia pengine wasingekuja hapo wangekuwa salama na kuendelea kuishi
Ilimbidi kaka mtu aende mwenyewe na kwenda pembeni kumtuliza, Bianca alikuwa ni kama mtoto mdogo tu licha ya umri wake. Madhara ya kudekezwa kupindukia hayo.
Walinzi wale sita mmoja akisaidiwa kusimama kwa kushikwa bega kutokana na mguu wake mmoja kujeruhiwa na risasi
"Wewe ni nani?" kiongozi wa walinzi aitwaye Abdul alimuuliza jimmy
"Nani mimi? Naitwa jimmy wakuu ni rafiki mpya wa....." akimnyooshea kidole Cid aliyekuwa pembeni akidili na Bianca
"Haiwezekani sisi wenye siraha na mafunzo tushindwe kudili ni hawa panya lakini wewe umeweza kuzizima hizi panya nne zenye siraha...... wewe ni nani?"
"Kama nilivyosema mimi ni Jimmy hamjaelewa wapi wakuu"
"Kuna kitu anatuficha huyu isije kuwa ana mpango wake wa siri kwa bwana mdogo" aliongea Shaw akimwita Cid kama "Bwana mdogo"
"Nafsi yangu inaniambia huyu ni jasusi" alidakia mwingine
"Mnawaza mbali wakuu mimi ni raia mwema nilichofanya ni kuokoa maisha yangu na yenu pia je hampaswi kushukuru?"
"Haha ndio ndio tunapaswa kutoa shukrani, mimi Derick natoa shukrani zangu za dhati kabisa" aliongea mlinzi mwingine aliyekuwa akiwatusi wale majambazi walipovamia
Mara mlio wa gari za polisi ulisikika na sekunde si nyingi waliweza kufika eneo hilo
Ifahamike kwamba alichoongea Jimmy kuhusu myahudi kumfunza mbinu mbalimbali ni kweli. Kipindi jimmy anampoteza baba yake alilia sana na kuwa mpweke kwani baba yake ndiye aliyekuwa rafiki yake mkubwa hakuwa na marafiki wengi.
Na kila siku alikuwa akienda mahali ambapo yeye na baba yake hupenda kufika na kuongea mawili matatu wakipunga upepo, alilikuwa akienda mahali pale kila anapomkumbuka baba yake, sasa siku ya siku akiwa shuleni ulitokea ugomvi ambao ulipelekea Jimmy kumuumiza mwanafunzi mwenzake na kutoroka shule kuepuka adhabu na sehemu aliyofikia ni mahali pale
Wakati amekaa katika hali ya mawazo akimkumbuka baba yake aliweza kugundua kuna uwepo wa mtu mwingine mahali hapo. Alikuwa ni mwanaume mzee hivi wa kiyahudi amekonda sana, nguo alizovaa zilikuwa zimechakaa sana na alikuwa amelala chini akipumua kwa chini sana
Jimmy alijiongeza maana kwa kumuangalia alijua atakuwa ni ombaomba alivua begi lake na kutoa bakula kubwa ls kuhifadhia chakula ambacho mama yake kila siku humuandalia kabla ya kwenda shule, kulikuwa na viazi vitamu, chapati za mayai na mayai manne ya kuchemsha bado vikiwa na umotomoto kwa mbali.
Alimkaribia mtu yule mzee akibeba chakula chake ambacho hata yeye hakula ni kuguswa kwake na hali ya mzee huyo ndiyo kulikomsukuma kufanya hivyo, alichuchumaa na kukiweka karibu ya yule mzee harufu ikisambaa puani mwake
"Ukarimu siku hizi ni adimu sana" aliongea mzee kwa kiswahili akifumbua macho taratibu akitazama chakula kile
"Babu amka ule" aliongea jimmy
"Nilikuwa nimeamka muda tu kabla ya wewe kunigundua" aliongea babu yule na taratibu aliamkaa akiketi kitako
"Una miaka mingapi kijana" mzee aliuliza
"Saba"
"Niambie ni nini kilichokufanya udhani labda nina njaa unisaidie?" mzee aliuliza huku akichukua kiazi kimoja na kutafuna
"Ni moyo wa huruma babu"
(mzee alicheka kidogo na kuendelea) "Unaitwa nani kijana?"
"Jimmy"
"Jimmy unaweza niambia kwanni upo hapa peke yako ukiwa na hali ya mawazo?"
"Nimemmisi baba yangu"
"Yuko wapi" aliuliza tena na Jimmy alinyoosha mkono kuelekea juu na mzee alimuelewa
"Koh...Koh...Koh.." mzee huyo alikohoa na jimmy alitoa chupa ya maji na kumpa
Mzee yule alipokea maji yale na kunywa na kuendelea kula huku akiongea
"Umetoroka?"
"Hapana"
"Uongo kwa wakubwa si jambo zuri" alimwambia lakini jimmy alikuwa kimya na hakumuuliza zaidi alikula na kumaliza na alimshukuru sana Jimmy kwa msaada huo mdogo
Basi ikawa kila Jimmy akienda mahali pale alikutana na Mzee huyo na kuwa marafiki wazuri tu bila kujali umri na alikuja kugundua mzee huyo ana siri nyingi sana. Siku aliulizwa swali na mzee huyo "Kijana unataka kukua kijana?" na alipojibu "ndio" mzee huyo alimfunza mambo mengi sana mengine ni siri yake mwenyewe
°°°°°°°°°°
Ndani ya jumba kubwa la kifahari ndani kwenye sebule pana walionekana watu wakiwa wameketi kwenye masofa wengine wakisimama
Mara ilisikika sauti ya hatua za miguu ikikaribia sebuleni humo kwa kasi na alikuwa ni mwanamama mnene kiasi mwenye umbo kama la Hamisa mobeto akiwa na sura yenye wasiwasi
"Bianca uko salama mwanangu?" aliongea kwa kuhema na Bianca aliyekuwa ameketi kwenye sofa alitingisha kichwa kuwa yupo sawa na kwa kiasi mama huyo alipatwa na ahueni
"Huyu ni nani?" aliuliza baada ya kumuona mtu asiyemfahamu ndani kwake
"Mama huyo ni rafiki yangu unapaswa kumshukuru bila yeye tusingekuwa hapa" Cid alimueleza
"Oh kijana asante sana kwa mchango wako mimi kama mzazi nashukuru sana naahidi nitakulipa"
"Shukrani inatosha huna haja ya kunilipa isitoshe nilikuwa nafanya kile nilichoona sahihi kufanywa" Jimmy aliongea kwa tabasamu
"Hicho sahihi ulichofanya kimeokoa maisha ya wanangu ni kitu ambacho siwezi kupotezea"
"Lakini sikufanya nikitegemea kulipwa"
"Ninaelewa lakini vipi unajua ni nini ninachokwenda ku-offer?"
"Pesa labda au kazi au chochote kile cha kubadilisha maisha yangu?"
"Na unaona ni kitu kibaya?"
"Hapana ni vile sio vya lazima"
"Ooh inaonekana una uchumi mzuri sio?"
"Hata robo sifikii"
"Sasa kwanini ukatae? Wanangu wapo hai sababu yako na nina kila sababu ya kukulipa"
"Vipi kama nisingekuwepo unadhani tungekuwa hapa tunaongea bimkubwa?"
"Lakini ulikuwepo" alitulia kidogo kisha akaendelea "aya chukulia sikulipi kwasababu ya wema wako bali ni kwasababu nataka kukusaidia kwasababu moyo wangu umetaka"
"Wapo wanaohitaji huo msaada kuliko hata mimi"
"Haha wewe ni msumbufu sana ila nimekupenda bure, unaitwa nani?"
"Jimmy" Cid aliropoka kana kwamba aliulizwa yeye
"Sasa Jimmy ukiwa unahitaji msaada wowote usisite kuniambia unakaribishwa hapa muda wowote" aliongea na jimmy alitingisha kichwa kukubaliana nae
Mwanamama huyo aliitwa Velora Mwakalebra na ndiye mama mzazi wa Cid na Bianca na ni mfanyabiashiara mwenye mafanikio makubwa nchini Tanzania naweza kusema ndiye mfanya biashara tajiri namba moja nchini akimiliki kampuni ya VELORA GROUP iliyowekeza kwenye sekta mbalimbali kampuni yenye thamani ya dollar billioni mia tano huku yeye akiwa na utajiri wenye thamani ya dollar billioni kumi na tano
Mwanamama Velora aliwageukia walinzi akiwa na sura ya ukauzu na hakuna hata mlinzi mmoja aliyethubutu kumuangalia machoni. Alikuwa amepata taarifa ya kile kilichotokea
"Nyie nitadili nanyi muda ukifika" aliwaambia
Wakiwa sebuleni aliingia mwanamke mwingine na kuongeza idadi alikuwa akitembea kwa maringo sana mkononi ameshikilia mkoba wenye thamani.
"Wewe mpuuzi unafanya nini humu ndani? Nani amekukaribisha" Mwanamke huyo aliongea alipomuona Jimmy
Alikuwa ni yule mwanamke waliyekutana bar siku ile na leo hio wanakutana tena kwa mara nyingine tena
TO BE CONTINUED..........
Comments