Reader Settings

SEHEMU YA 208.

Because I love you.

Watu  walijikuta wakishangazwa na  jambo  lile , kila mmoja alishangaa kuona  Mr Air alikuwa akipaa.

“Anapaaa jamani!!”

Ingawa ilikuwa ni rahisi kuweza kushindana na kani mvutano kwa wale wenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi , lakini ni mbinu ambazo zilikuwa zikienda kinyume na kanuni za anga.

Mr Air aliifanya hewa iliokuwa chini  alivyotaka  na mara baada ya kujiimarisha hewani  alianza kuinua matofali na vyuma na kuvifanya vielee pia angani. Kwa namna ilivyokuwa ikionekana ni kama vile kulikuwa na kamba ambazo zilikuwa zikivuta vitu  hivyo.

Tukio la kushangaza liliendelea kuonekana katikati ya uwanja ule , ilikuwa ni kama vile  eneo la katikati lilikuwa haliathiriwi na  kani mvutano ya dunia  na kufanya vitu viwe kama vile  vipo ndani ya eneo lenye zero gravity na kuelea angani.

Mara baada  ya Air  kutingisha mkono wake hewani ,  alisababisha mawe na vyuma  kuanza kugawanyika na kugeuka chembembe. Ilikuwa ni kama mawe yale  na vile vyuma viligeuka  na kuwa vumbi ambalo lilielea hewani kwa kusambaa pande zote.

“Hii ndio mbinu yake ya elemental Decomposition?”

“Itakuwa , nimesikia anao uwezo wa kutawala elementi  zote za maada . ili mradi awe na muda wa kutosha anao uwezo wa kutenganisha kila kitu.Hivi vyuma na  mawe vina elementi za kawaida sana kwake kutenganisha”

“Mbona hio sasa ni hatari . Kama akitumia uwezo huo kupambana si anaweza kumyeyusha adui tu?”

“Umefikiria mbali sana , ijapokuwa ni kweli  uwezo wake ni wa juu  na anao uwezo wa kugawanyisha vitu  lakini  ili kufanikisha mchakato mzima anahitaji nguvu nyingi sana za kiroho  na kadri  muunganiko wa vitu unavyokuwa mgumu  maana yake  atahitaji nguvu nyingi zaidi  kufanikisha. Kwa lugha nyepesi ni kwamba  ana  mwisho pia wa  kiasi anachoweza kutenganisha , ikiwa atakutana na  mwanajeshi ambae  ana nishati kubwa za  mbinu na ardhi anaweza asifanikiwe”

Hayo yalikuwa maneno ya  watu kadhaa waliokuwa wakielewa kuhusu uwezo wa Mr Air.

Ndani ya dakika  tatu kila kitu kilikuwa kimesagwa na kuwa unga unga unaoelea hewani  katikati ya uwanja.

Mara  Mr Air alishuka  ardhini na kukandamiza mkono  wake mmoja kwenye ardhi  kama vile alikuwa akiipasha ardhi  moto  na ghafla tu  sauti kama ya tetemeko ilianza kusikika.

Wakati watu wakimaka kile kinachotokea  ghafla tu  zile chembechembe  zilianza kujikusanya  sehemu moja kwa kasi na  kitu mfano   wa umbo mraba lilianza kujitengeneza kwa kupanda juu hewani.

“Duuh! Uwezo   wa ajabu sana huu , sidhani kama kuna mtu  anaweza kuvuna nishati za mbingu na ardhi na kuja kupata ufunuo wa kutawala elementi za maada kama hivi?”Aliongea Silvia.

“Air uwezo wake  ni wa asili , hata kama atokee  mtu aweze kupata ufunuo hawezi mfikia”Aliongea Mikaeli.

“Kuzaliwa na Karama  ni habari nyingine. Hebu fikiria tokea saa unayozaliwa unakuwa  mtawala  wa vitu . Hata ujitahidi vipi kuwaonea wivu na kutamani kuwa wao  , hutofanikiwa”Aliongea Hamza.

“Lucifer  huna haja ya kumuonea wivu  Mr Air , kwa ninavyokuona umezaliwa pia na Karama  ya kuzifahamu siri za mwili , hivyo uwezo wako sio  mdogo pia”Aliongea Auland na kumfanya Hamza amwangalie Auland.

“Mr Auland  naona muda wote umelivaa hilo helmeti la chuma , hujisikii vibaya?”

“Sijisikii vibaya”Aliongea Auland kwa sauti kavu.

Wakati wakiongea hatimae steji  ya umbo la mraba  yenye upana wa  mita za mraba zaidi ya mia na kimo cha  mita mbili iliweza kusimama katikati ya  uwanja , ila bado haikuwa imekamilika kwani kulikuwa na chembe  zingine nyingi tu zilizokuwa zikielewa hewani.

Mr Air  alisimama na kuanza kuzungusha mkono wake  juu angani kwa kuchezesha kama anakoroga hivi na zile  chembechembe zilianza kujitenga kimakundi  na kisha alianza kushusha kundi baada ya kundi na kwenda kuivaa kile kifusi cha  umbo la mraba  kwa staili  ya kufunika kama shuka. Mpaka anakuja kumaliza kundi la mwisho kufunika steji ile  hatimae ilikaza na alifanikisha kumaliza kazi  na upepo kutulia na sasa watu waliweza kuona eneo la  steji  ile  likiwa imefunikwa na  madini ya rangi ya silver ya kung’aa sana na kufanya ivutie  kwa macho.

Watu walijikuta wakishindwa kuzuia hisia zao na kusimama na kupiga makofi mengi. Hakika walionekana kupendezwa na kile ambacho  Gwiji huyo alikamilisha ndani ya muda mfupi.

“Tutumie nafasi hii kumshukuru Mr Air kwa  msaada wake wa kimiujiza”Aliongea Maxim na kufanya watu wazidishe makofi  na muda ule  wafanyakazi maalumu wa Baraza la Maksi waliingia  na  viti na baadhi ya vitu vingine na kuviweka katika mpangilio uliokuwa mwanzo kabla ya jukwaa kuharibika.

Muda huo ilikuwa ni usiku sana , lakini  hata hivyo Baraza hilo halikuwa la kawaida, na  ni sawa tu kwa watu kutotamani kula  au kulala hivyo  mkutano uliendelea kama kawaida.

Siku ya kwanza ya Baraza la maksi ilikuwa ni kwa ajili ya  kutoa mjumuisho wa maendeleo  ya jumla ya  ulimwengu wa siri au giza kwa kipindi cha miaka mitano  na hio ilihusisha  suala zima la kutambua  wachangiaji wakubwa wa maendeleo hayo.

Na kupitia hivyo baadhi ya  taasisi , makundi na watu binafsi na hata vitengo maalumu vya siri vilipandishwa vyeo na vile vilivyolega vilishushwa  madaraja. Kulikuwa na hisia za  furaha kwa waliopandishwa  na  za huzuni kwa walioshuka.

Hamza na magwiji wengine hawakuhudhuria kwa ajili ya kukaa jukwaani tu , hata wao pia walihusika katika  majadiliano. Ukweli ni kwamba magwiji walikuwa ni kama viongozi  na wawakilishi wa  jumuiya kubwa za siri. Hamza  katika muda huo  aliwakilisha kitengo cha Malibu ambacho kilikuwa ni daraja A  huku wengine kama Oleg waliwakilisha makundi yao ya kiharamia. Watu wa Madhabahu takatifu na ya giza ijapokuwa  hawakutambuliwa  kimadaraja  lakini  kama  wangepewa  wasingekuwa chini ya  daraja  S kama ilivyokuwa kwa  jamii kama Freemason na kuendelea.

Adept Association  au jamii ya watu waliozaliwa na Karama zisizo zakawaida  walikuwa wakipewa heshima ya pekee pia katika  Baraza hilo. Ingawa  ushawishi wao ulikuwa ukiyumba na kukua  vizazi na vizazi lakini  uwepo wa Mr Air  ambae haijulikani asili yake  ilifanya jumuia hio kupewa hadhi ya juu.

Ukiachana na Hamza kubeba kitengo cha Malibu , lakini kwa wakati mmoja pia aliwakilisha  jamii yake ya siri ya  Inferno. Ingawa ilionekana ni kama jamii ambayo haifanyi kazi  lakini  wengi hawakuona hivyo  na Hamza pia hakuichukulia jamii yake  kama  imekufa.

Sababu ya  kwanini Magwiji kumi waliketi katika jukwaa la juu kabisa  chini ya  viongozi wa  mashirika mengine  sio kwa ajili ya kuwapa watu wa kawaida changamoto za  kimotisha , lakini vilevile  ilikuwa ni kuonyesha heshima juu ya mafanikio yao. Kama ilivyo kanuni ya watu wa ulimwengu wa siri kwamba mwenye nguvu anapaswa kukaa juu ya wengine.

Usiku huo  Hamza aliwapatia  washikaji zake  watatu tuzo , yaani Asmuntis , Azzle na Leviathani  kwa  mchango wao mkubwa katika ulimwengu wa siri.

Katika kipindi cha miaka mitano  ni  makundi matatu pekee yalioweza kukwea madaraja  na kuingia daraja A  na makundi hayo yote yalikuwa  yakiongozwa na   jamaa zake Hamza. Wakati wa kupokea tuzo juu ya jukwaa wote walionekana kujivunia kwa mafanikio yao.

Regina pia alishiriki  katika kikao hicho na  kwa bahati nzuri aliwasiliana na  wafanyakazi wa kampuni yake tanzu na kuwaambia hatokuwepo mjini. Kutokana na mazingira mapya ya ulimwengu wa siri alijikuta  akiwa  na msisimko  mwingi na hakupata   hali ya usingizi hata kidogo.

Black Fog ndio aliechukuwa jukumu la kumuelezea Regina kila kitu ambacho hakuwa akielewa  na kwa jinsi Regina alivyosikiliza kwa umakini  ni kama  vile angefanyishwa mtihani baada ya hapo.

Regina alishikwa sana na hali ya kujivunia na furaha  wakati ambao alimuona Hamza akikabidhi tuzo  huku watu wengi wakimshangilia.

Hatimae usiku wa saa tano  Baraza lilihitimishwa kwa siku ya kwanza na kutarajiwa kuendelea siku inayofuata. Magwiji ndio waliokuwa wa kwanza  kutoka ukumbini na kisha ndio wengine wangefuatia.

Hamza ile anakaribia  njia ya VIP  ya kutokea Khalid alikuwa tayari yupo  anasubiri na alimkabidhi  ufunguo wa  gari yake ya Leykan.

Ile Hamza anasogelea uelekeo wa parking ya magari  aliweza kukutana na mtu ambae alimfahamu , alikuwa ni  Mr Air ambae alionekana kuwa hapo  kwa ajili ya kuchukua ufunguo wa gari yake pia.

Hamza mara baada ya kumuona alishindwa kuzuia shauku yake na kujiuliza  huyu mtu ambae anaweza  kupotea  na asionekane ina maana na yeye anaendesha gari na kama anaendesha gari ni ya aina gani?.

Kilichomfurahisha Hamza ni kwamba Mr Air hakuficha  sura yake , ungekuwa mtu  wa kawaida usingemfahamu. Ila magwiji  wanatambuana.

Unachopaswa kujua Hamza alishawahi kukutana na  Mr Air miaka mitano iliopita katika baraza la maksi , lakini sura ambayo alikutana nayo kipindi hicho ilikuwa tofauti kabisa na  ya muda huo anayiona , ya kipindi kilichopita ilionekana  ya kijana zaidi kama alikuwa na miaka ishirini na nane , lakini ya muda huo  alionekana kuwa mzee  hivi na  mwonekano wake kwa ujumla ulikuwa tofauti.

Kulingana na taarifa zilizopo , Mr Air  mara zote anapoonekana sura yake ni tofauti, akificha muonekano wake wa kawaida. Sasa muda huo Hamza ni kama alihisi amemuona Mr Air katika muonekano wake halisi.

Ingawa hawajawahi kuwa na ukaribu  wa sana , ila Hamza aliona sio mbaya kama  atamchangamkia , isitoshe wote walikuwa daraja sawa la ugwiji.

“Hey Mr Air , na wewe upo hapa kuchukua gari yako?”Aliongea Hamza na kumfanya Khalidi mara baada ya kusikia  Hamza anaongea haraka sana alimsogelea yule mzee baada ya kumtambua na  kumkabidhi ufunguo  wa gari aina ya Volkswagen.

Hamza aliishia kukunja macho yake huku akihisi labda ameona tofauti, kwa haraka haraka aliweza  kugundua ufunguo huo ni wa gari aina ya Beetle(Mende) , vigari flani hivi vya kizamani sana.

Hamza alijiuliza yaani huyo bwana ni  kiongozi mkubwa wa  watu wasiokuwa wakawaida na   ana hadhi ya ugwiji lakini anaendesha kigari kadogo kanakofanana na mende?.

Ukiachana na swala la  kuwa gari hilo lilikuwa zuri au lah    suala zima lilionekana kutokuwa la kawaida.

Mara baada ya kumuona Hamza , Mr Air alionekana kushangaa pia. Hakuwa  mpiganaji hivyo  hisia zake hazikuwa  kali  sana  na hio ni moja ya udhaifu wake.

Mr Air aliishia kutingisha kichwa  kumuitikia Hamza na kisha  alichukua ufunguo wake na kugeuka kuondoka.

Hamza alijisikia vibaya  na kujiuliza  anaondokaje  sasa  wakati anataka kumuongelesha . Lakini  Hamza  kuona hivyo hakutaka kulazimisha pia , kwasababu hakutaka kuongea nae hakuona haja ya kumlazimisha pia.

Wawili hao walisogea mpaka upande wa gereji na muda huo Hamza alianza kuhisi harufu hafifu ya marashi  ikimtoka Mr Air  na kumfanya amwangalie kwa umakini , kwa hali isio ya kawaida  Hamza alihisi  harufu inayomtoka ni kama alishawahi kuinusa mahali lakini hakukumbuka.

Ile Mr Air alipofikia kigari chake cha Mende  cha rangi ya njano na kufungua mlango kuingia ndani, Hamza aliongea;

“Mr Air tushawahi kukutana?”Aliuliza na kumfanya Mr Air kupozi kidogo.

“Miaka mitano iliopita”Alijibu.

“Hapana , namaanisha  ukiachana na baraza la maksi , tulishawahi kukutana  hapo kabla?”

“Hapana”

“Oh ! Basi sawa , tutaonana kesho”

Mr Air hakujali kingine zaidi na aliingia kwenye gari yake  na kuliwasha  na kuliondosha ndani ya eneo hilo.

Hamza alijihisi labda  ni hisia zake tu  hivyo  alipotezea  na yeye kuingia kwenye gari yake na kuondoka ndani ya eneo hilo.

Kwasababu ilikuwa usiku tayari , Hamza aliendesha moja kwa moja kurudi Shamba. Wengine pia  walikuwa wamesharudi wakiambatana na Regina.

Regina mara baada ya kufika  huko  alijikuta akishangaa na kujua kumbe kundi la Hamza linaisha sehemu nzuri hivyo  na sio hotelini. Alishindwa kujizuia  kumlalamikia Hamza kutokuja nae.

Upande wa Hamza hakujua kama mwanamke wake alikuwa akipenda  mazingira ya aina hio  na alimuahidi baada ya Baraza wataendesha farasi pamoja.

Saa saba za usiku meza kubwa iliandaliwa vinono na wapishi wabobevu kabisa. Hamza alimchukua Regina na kuungana na washikaji zake  na kufurahia chakula cha usiku wa manane.

Kila mmoja alikuwa  vizuri kwenye kudhibiti usingizi  hivyo matokeo yake hawakujali muda ilikuwa ni saa ngapi na walikunywa  kujigalagaza.

“Mhunzi na Mchafu  mniwie radhi kwa kutowasaidia mpaka mkaumia, nilitaka kuwaambia tokea mwanzo , lakini yule hayati mara baada ya kuona hila zake nikaona ngoja nicheze nae  kwanza”Aliongea Hamza huku akiwa ameinua glasi kwa ajili ya  kugongesheana na  washikaji zake.

“Bosi huna haja  hata ya kuelezea. Tunaelewa kabisa mbona”Aliongea Azzle.

“Ni kweli! Nadhani pia hatukupaswa kuwa na wasiwasi juu ya uwezo wako”Aliongea Asmuntis.

Hamza hata yeye  alijua  washikaji zake wasingemchukia kwa suala dogo kama hilo , hivyo alibadilisha  mada.

“Mchafu nichagulie vijana wa moto sana kwenye kundi lako, angalau wakiwa na rangi rangi hivi  za kujificha  itakuwa  vizuri. Nataka kuondoka nao kurudi Tanzania”

“Bosi unataka  kumuwekea ulinzi shemeji yetu?”

“Ndio, na itakuwa vizuri kama watakuwa  weusi  na wanaojua  tamaduni za  waswahili  ili kupunguza  kushitukiwa , tunaweza pia kuwaandalia  utambulisho feki”

“Bosi hilo limeisha , nitakuchagulia  vijana mahili sana”

“Unataka kunilinda?” Regina aliongea  kwa kumnong’oneza  Hamza.

“Mke wangu kwa akili zako , siwezi kukuficha kitu”

Regina aliishia kuvimbisha mashavu bila ya kuongea kingine , alijua fika  kama asingeweka watu wa kumlinda angetekwa tena na ingempa wakati mgumu. Lakini kwa namna Hamza alivyohitaji kundi la watu alijua  lazima sio yeye tu  ni pamoja na wengine, haikumfurahisha lakini asingeweza kumzuia.

Baada ya chakula  Regina ndio aliekuwa wa kwanza kutaka chumba cha kulala , hakuwa na mafunzo ya kijeshi kama wenzake hivyo  kuhimili purukushani  za siku nzima bila ya kupumzika asingeweza.

Hamza upande wake alimuita Black Fog na kwenda nae  kwenye majani nyuma y a banda.

“Bro  umeniita , kuna tatizo?” Black Fog alijua kwasababu ya ujio  wa Regina Hamza angekuwa bize  na mke wake , lakini alishangaa Hamza kumuita , licha ya hivyo alishikwa na furaha.

Hamza alieshikilia sigara  na mkono wa kushoto alinyoosha  wa kulia na kumshika Black Fog kichwani na Black Fog kuona hivyo  moyo wake ulitingishika mara baada ya kupatwa na wazo, au Hamza anataka wafanye.

Wakati  Black Fog akiwa  katika ulimwengu wake wa kujitakia , upande wa Hamza alikuwa akimrekebisha  mkao wake   kuanzia mikono  , kisha na shingo, kwa namna ya kuminya , yaani alikuwa akimrekebisha na kumpima kwa   wakati mmoja  kwa kulenga lymph node(tezi).

Ndio muda ule Black Fog alishituka  na kugundua kwamba sio kama alivyofikiria , kutokana na kuhisi hali mpya  katika mwili wake.

“Naona  majeraha yaliosababishwa na  mbinu ya Hundred Shadows yamekwisha kupona”

“Ni kwasababu nilipata muda wa kumpumzika ndio maana”Aliongea huku akitabasamu.

“Roda kuna mafunzo  nataka kukuelekeza ndio maana nimekuita , nilipanga nikuelekeze mapema lakini kwa ajili ya kuendeleza maigizo yangu   kwa Metal Tide ndio maana  ninakuelekeza sasa hivi”

“Bro , unataka kunifundisha mbinu ya  mafunzo ya nishati ya  Mbinu na Maji?”

Hamza mafunzo yake ya nishati  aliyapatia kutoka kwa Mr Black  na watu wengi walijua mbinu ya Mr Black ilikuwa ni  ya  nishati  za mbingu  na Maji , yaani tofauti na  mbingu na ardhi. Hivyo  Black Fog alijua labda Hamza anataka kumuelekeza mbinu hizo.

“Hapana ,  tayari  una nishati za mbingu  na ardhi za kutosha kwenye  mwili wako  na vilevile  umejifunza mbingu ya Hundred shadows  , hivyo haina haja ya kuongezea na mbinu  nyingine ya nishati. Ninachotaka kukufundisha  ni mbinu nyingine   kabisa ambayo nimeigundua mwenyewe. Sijaipa jina bado , lakini nadhani unaona uwezo wangu hautegemei nishati   tofauti na nguvu pekee za  kimwili.  Kuna utofauti  kati yetu hivyo  sitakuelekeza mambo magumu  sana , ila   njia nyepesi ambayo itaimarisha  mwili wako kwa ujumla  na kama utakadhania nina uhakika ndani ya miaka mitatu ijayo utaweza kuihimili nguvu ya  hundred shadows na kupanda  levo  zaidi”

Black  Fog hakupenda mwanzo lakini mara baada ya kusikia mbinu hio ingemwezesha kuhimili nguvu ya  hundred shadows  alifurahi.

“Bro kweli unataka kunifundisha mbinu yako , sio kwamba ni siri na muhimu kwako?”

“Mbinu ninayokufundisha haina siri kubwa sana , siri ipo kwa anaejifunza mwenyewe  kwa namna atakavyofungua  vifungo vya siri ya mwili wake . Hivyo ninachokufundisha ni maelekezo ya kawaida sana , lakini namna utakavyoyachukulia na kukufaidisha ni wewe mwenyewe”

“Sawa , lakini vipi naruhusiwa kumwambia Master?”

“Inaonekana  bado una heshima kubwa sana kwa Master wako. Usiwe na wasiwasi maana kabla sijafanya haya maamuzi nishaongea nae na anajua kinachoendelea”

“Basi itakuwa vizuri! Kama nitaweza kuihimili nguvu ya Hundred shadows, nina uhakika uwezo wangu utakuwa kwa viwango vingine”.

“Usiwe na wasiwasi kabisa , nitakuelekeza  hatua za mwanzo na ukishazimaliza nitakuelekeza hatua inayofuata”Aliongea Hamza.

Alichopanga kumfundisha  ni kile kile ambacho alimuelekeza  Yonesi na Dina.

Mara baada ya kumuelekeza  kutokana na uwezo wa Rhoda , ilikuwa rahisi kwake kuhimili  na  kuelewa kwa uharaka na kadri alivyojaribu  alijikuta akianza kuhisi kitu ambacho hakuwahi kukifikiria mwanzo na macho kumtoka.

Baada  ya kama  masaa manne hivi ,  wote walikubaliana kurudi kupumzika licha ya kwamba  kushapambazuka.  Kwasababu  watu walijua Hamza na  Regina ni mume na mke waliwaandalia  chumba kimoja.

Hamza  mara baada ya kuingia chumbani alihakikisha hapigi kelele kwa hofu za kumuamsha Regina lakini ile anaingia alishangaa kuona Regina alikuwa macho na alikuwa akimalizia kuongea na simu.

“Wife kumbe umeamka?” Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu.

“Nimeamka muda mrefu tu. Nilikuwa nikiongea na watu wa kampuni”

“Basi twende  tukapate kifungua kinywa”Aliongea Hamza na  Regina alitingisha kichwa na kushuka kitandani na kuvaa sendo.

“ Vipi na leo tunaenda kwenye mkutano?”

“Yeah, nina makubaliano ya watu wa kitengo cha Malibu. Leo nitaenda kukamilisha suala lao . Ila kwa wewe mke wangu kama umechoka huna haja ya kwenda , nitamuagiza mtu kwa ajili ya kukutembeza tembeza”Aliongea  Hamza

“Hata mimi nataka kwenda   kuangalia . Nataka kujua kwa undani kuhusu ulimwengu wa siri ulivyo , vinginevyo nitaendelea kujiona mjinga tu  wa kutoelewa vitu”

Hamza aliishia kumwangalia  mwanamke huyo na  tabasamu la ridhiko,  Regina alionekana kuwa  tofauti sana na siku zote hakuwa  kam bosi na hakuwa  na ukauzu wowote , alionekana kuwa mwanamke wa kawaida mrembo.

Mwanzoni  Hamza alikuwa  akijitahidi sana kumuelewa Regina , lakini mpaka kufikia hatua hio  walikuwa wakijuana. Pengine  ni kwasababu ya jana hatimae  Regina  ameanza kumchukulia Hamza kwa uhalisia wake na sio ule wa maigizo. Alionekana kuwa na amani zaidi  mbele ya Hamza kuliko siku zote.

“Wewe mbona unaniangalia tu” Aliuliza  Regina ambae alikuwa akipiga nswaki na mara baada ya kuona Hamza muda wote anamwangalia alihisi aibu.

“Ni kwasababu mke wangu , nimegundua kadri ninavyokuangalia ni kama unazidi kuwa mrembo na kufanya moyo wangu kushindwa kufanya kazi yake ya kusukuma damu kwa usahihi”

“Eeh Baba! Utakuwa kipofu wa macho wewe sio bure. Uso mkavu hivi!”

“Uzuri wa mwanamke  huonekana wakati wa asubuhi na kwako wewe mke wangu  licha ya uso wako kuwa mkavu , lakini unavutia”Aliongea Hamza huku akicheka.

“Laiti wale mashabiki zako wanaona ulivyo hivi , nina uhakikwa kichaa kinaweza kuwashika”Aliongea Regina akitingisha kichwa.

“Mimi  nina nini kwani, kwanza lazima wakubaliane na mimi kwamba mke wangu ni mzuri”

“Toka huko. Nwnda nje kwanza ataka kukojoa”Aliongea Regna huku akielekea bafuni.

Chumba hiko licha ya kuwa na choo cha ndani lakini hakikuwa na mlango ndio maana.

“Wewe kojoa tu , sitokuchungulia”

“Wewe toka bwana , la sivyo nitakasirika”

Hamza alijikuta akiwa hana jinsi na kuishia  kutoka na kufunga mlango. Lakini wakati akiwa mlangoni na kuvuta picha namna Regina alivyo uchi, alijikuta akishindwa kujizuia na mwili wake kuwa wa moto.

Mara baada ya Regina kumaliza mambo yake , wawili hao walichukuana na kwenda  dining kwa ajili ya kifungua kinywa , wengine  pia waliweza kufika na kuungana nao.

Katikati ya kifungua kinywa , Regina  alipokea simu  na alionekana kusikiliza na kisha kuitikia na kukata.

“Helena ameamka. Watu wa hospitali wanasema kama unataka kwenda na kumuona unaweza kwenda”Aliongea akionekana kufurahishwa na  taarifa hio.

“Shem, Licha ya Helena kutaka kukuua ila  uliamua kumuokoa. Nadhani umekwisha kufanya  yalio ndani ya uwezo  wako. Bado tu unataka kuonana nae?”Aliuliza Azazel.

“Lakini  hana ndugu yoyote , nimesikia kutoka kwa baadhi ya  wanajeshi, hana ndugu wala mume , ameamka mwenyewe akiwa hospitalini   nahisi kumuonea huruma”Aliongea Regina  kwa  kusita kidogo na kufanya watu wote kuangaliana.

“Shemeji hakika una roho nzuri sana”Aliongea  Berly.

Regina aligeuza macho yake na kumwangalia Hamza aliekuwa bize  na Sandwich.

“Unaonaje nikienda hospitalini kwanza na kisha  nitakuja kwenye mkutanano baadae?”

“Wife unadhani upo  Dar  hapa kwamba unaweza kupanda taksi  na kwenda unapotaka?  Inabidi nikupeleke mwenyewe , hata hivyo mkutano unaanza mchana, nadhani pia itakuwa vizuri  ukanunue na baadhi ya nguo na kusafisha nywele, unaonaje?”

“Sawa”

Previoua Next