Reader Settings

SEHEMU YA 209.

Kila mtu alimwangalia Hamza kwa namna ya mshangao , hakuna aliedhania Hamza angemsindikiza mke wake kwa ajili ya kufanya kitu kama hicho.

Walijikuta akishindwa kujizuia na kumwangalia  shemeji yao Regina na  mwonekano  usioelezeka.

Mara baada ya kifungua kinywa , Hamza alimchukua  Regina katika gari yake ile ya kifahari na kuelekea mjini.

Regina mara baada ya kukaa kwenye gari aliishia kumwangalia   Hamza aliekuwa siriasi na usukani.

“Marafiki zako nadhani wananiona  mimi ni mjinga kwakufanya  haya yote kwa mtu alietaka kuniua”Aliongea.

“Ni kweli wewe ni mjinga, lakini  ndio ninachokupendea mke wangu , nitafanyaje sasa?”

“Na umeongea  hapo. Pengine siku moja utanichoka nikiwa katili na hata  kuniita  kama watu wanavyonisema huko mtandaoni kwa kusema mimi ni  mfanyabiashara mkatili. Hata marafiki zako watakuunga mkono baada ya kuanza kunifuatilia mtandaoni na kuona watu wanavyoniita majina ya ajabu”

“Haha! Wife unachekesha , kumbe unafuatilia watu wanasema nini kuhusu wewe?”

“Unacheka nini ! Unadhani  kama sina akaunti  Instagram siingii  kuperuzi”

“Wife  huna haja  ya kujali watu wanavyokufikiria na kukuongelea”

“Inamaana wewe hujali wanavyoniongelea?”

“Sijali , Nakupenda na hio  inatosha”

“Lakini marafiki zako wanaweza kuniona mimi ni mtu mbaya na najaribu kuigiza tu kuwa mkarimu”

“Haha.. Wife unajua unavyoongea hivyo  ni  kwamba unaogopa  wakiona kwamba hufai  kuwa mke wangu ndio maana wasiwasi umekujaa.Naona hatimae umekubali kuwa mke  wangu  kabisa sasa?”

“Mimi nimeonyesha wasiwawasi wangu tu , linahusiana vipi na kuwa mke. Kwanza  hata   sijajua nikukubalie au nikukatalie wakati wa kunichumbia, acha  kujisifia. Mimi naongea  jambo la usiriasi wewe unaingiza habari nyingine”Aliongea huku akimpiga  na mkono begani.

Hamza alimshika mkono  Regina na kisha alimwangalia usoni  kwa usirasi

“Usiwe na wasiwasi mke wangu , hawawezi kukuchukia  na  badala yake nina uhakika lazima sasa hivi watakuwa wanajua kwanini nimeamua kukuoa”

“Kweli?”

“Kweli kabisa”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kufurahi.

“Ila hujaniambia kwanini umenioa. Au ni kwasababu bibi alikulazimisha?”

“Hapana bwana! Babe Regina  kwanini bado unaniuliza hili swali? Nishasema nakupenda na napenda kila kitu kuhusu wewe”

Regina mara baada ya kusikia kuhusu hivyo alijikuta  akiganda  na kuishia tu kutoa sauti ya ‘oh’ na kuacha kuongea.

Hamza mara baada ya kumwangalia mke wake namna alivyo aliona anazidi kuwa  Cute asipokuwa siriasi.

Hamza alishindwa kujizuia na alinyoosha mkono na kushika nywele za  Regina  kwa kuzipapasa tartibu.

Regina upande wake alihisi aibu kiasi cha kumpelekea kumzuia Hamza na mkono.

“Acha kunishika , nywele zangu zina mafuta sijaziosha”

“Wife mwili wako muda wo te unanukia , ni kama  una  mfumo maalumu wa kutengeneza marashi”

“Unaongea nini wewe , nimegeuka na kuwa mmea?”

“Hahaha…Wife unaonaje nikiosha nywele zako leo?”Aliuliza.

“Wewe! Sitaki , mimi mwenyewe sipendelei kuosha nywele zangu mwenyewe maana hazitoki kama ninavyotaka”Aliongea na Hamza hakubisha.

Mara baada ya kufika hospitalini  , walielekea moja kwa moja katika wodi Helena aliokuwepo.

Mara baada ya kuingia alikuwa ameamka  licha ya kwamba  alikuwa amekwekewa mabomba ya oksijeni puani.

Mara baada ya kumuona Regina na Hamza macho yake yalionekana  kucheza kwa   hisia.

“Helena unaendeleaje , Dokta kasema umevuka hali hatarishi”Aliongea Regina huku akiwa na tabasamu.

Helena aliishia kumwangalia Regina kwa sekunde na kisha akamwangalia Hamza.

“Sir Lucifer , kwanini uliniokoa?”Aliuliza na Hamza alimnyooshea  Regina kidole.

“Usiniangalie mimi , ni mke wangu  alietaka nikuokoe. Hivyo nilikufanyia upasuaji kwasababu aliomba  na kama unataka kumshukuru basi  fanya hivyo  kwake”

Helena mara baada ya kusikia maelezo hayo alionekana kushangaa  huku akionyesha mwonekno usio wa kawaida.

“Miss Regina kwanin.. nilitaka kukuua.. na ..”

“Ulitaka kuniua kwasababu ilikuwa ni  jukumu lako  kwasababu ulikubali kutii maagizo ya  kiongozi wako, sijawahi kuwa na uadui wowote  na wewe na siamini pia  wewe ni mtu mbaya. Vinginevyo usingetumia muda wako kunielezea  vitu vingi ambavyo sikuwa nikivijua  wakati wa mkutano, hivyo ndio maana sikujali kukusaidua . Huna haja ya kuongea chochote na  siwezi kukuomba shukrani. Maana licha ya kukusaidia najua bado  ni mtiifu kwa  kongozi wako”Aliongea Regina na kupozi kidogo.

“Ukweli  tu ni kwamba niliguswa na uaminifu wako , hata kama ulitaka kuniua  sina  nia  yoyote ndani yangu ya kutaka kukuchukia. Wewe ni mtu mzuri  ambae  ulijiunga na kumwamini mtu ambae si sahihi. Kama  nafasi ipo, nipo tayari kuwa rafiki yako muda wowote”Aliendelea kuongea Regina.

Helena mara baada ya kusikia hivyo macho yake yaligeuka na kuwa mekundu , ndani ya koo alijihisi ni kama kuna kitu kilichoanza kumkaba wakati  na kushindwa  kulia. Aliishia kufumba macho yake na kuruhusu machozi kumtoka na kuloanisha mashavu yake.

Hamza upande wake alimwangalia Regina kwa sekunde na kisha aligeuza macho yake na kumwangalia   Helena na alionekana kufikiria kitu.

“Helena utabakia hapa mpaka utakapo pona kabisa , sisi tunaondoka”

Wakati Hamza anataka kuondoka na Regina, Helena alionekana kuongea;

“Subirini kidogo ..”

Wawili hao walijikuta wakigeuka na kumwangalia .

“Unataka kuongea nini tena?” Ile wanauliza kilichotokea baada ya hapo kiliwashangaza , kwani Helena alichomoa mrija wa oksijeni  na drip  na kwa kuvumilia maumivu  alishuka chini ya kitanda.

“Helena unafanya nini!!?” Regina alishituka.

Helena aliishia kupiga  magoti chini kwenye sakafu  huku akiendelea kutoa kilio cha kwikwi.

“Miss Regina . I am already someone who  has died once. My life  was given to me by you .. If you don’t mind , please take me away”Aliongea Helena akimaanisha kwamba   yeye ni mtu ambae amekwisha  kufa mara  moja na  uhai wake  umerudishwa kwake na Regina na kama hatojali amchukue aondoke nae.

“Uhai wangu  haupo tena chini ya Metal Tide , wala haupo chini ya  taasisi yoyote ile . Kwanzia leo na kuendelea kama  nitapata nafasi nataka  kutumia  sehemu ya maisha yangu yote yaliobaki kukutumikia!”Aliendelea kuongea.

Regina kusikia vile , alijikuta akiwa katika hali ya kupaniki  na haraka sana alimsogelea Helena na kumsaidia ili asimame.

“Helena ,  usiwe hivi ,utasababisha  kidonda kufunguka”Aliongea

Ukweli ni kwamba kama isingekuwa  mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi aliokuwa nayo ,  kidonda chake kingekuwa kishaachia muda mrefu.

“Madam! Upo tayari kunichukua  niwe chini yako?”Aliongea Helena huku akiwa amemshikilia Regina mkono.

Regina aliishia kugeuza kichwa chake na kumwangalia Hamza  na kisha akamgeukia  Helena  aliekuwa akimwangalia na macho yake ya kizungu  ya kung’aa. Regina alionekana kama vile alikuwa akishindana  na nafsi yake  na baada ya sekunde kadhaa aliishia kutingisha kichwa.

“Sawa! Tutaondoka wote kwenda Tanzania  na  nitakuruhusu ujiunge na kampuni yangu , Sawa?”Aliongea Regina na Helena alitingisha kichwa mara kibao kwa furaha.

“Vizuri! Asante sana”

“Kwanzia sasa ndio unisikilize , hakikisha unapona kwanza vizuri mwili na roho. Vinginevyo siwezi kuwa na mfanyakazi mwenye mwili uliojaa majeraha”

“Usiwe na wasiwasi . Nitakuwa sawa , nitahakikisha napona haraka. Asante sana  Ms Regina , Asante sana..”

Mara baada ya kupata  malengo mapya ya kimaisha , Helena ambae alikuwa katika majonzi furaha ilimrejea.

Regina alimwachia Helena namna ya kuwasiliana nae na kuahidiana wangekutana  nchini Tanzania baada ya kupona kwake , kwani yeye anatangulia kuondoka  mapema.

Hamza alimchukua Regina na kumpeleka hadi kwenye gari na  mara baada ya kuingia , hakuwasha kwanza na kuishia kutulia.

Regina mara baada ya kuona Hamza yupo kimya na haendeshi gari aliishia kuuliza.

“Unafanya nini? Nipeleke saluni basi nikaoshe nywele”

Hamza aliishia kumwangalia  tu  akiwa na mwonekano usioelezeka  bila ya kuongea neno . Regina kuona hivyo alianza kujisikia vibaya.

“Una matatizo gani wewe? Kwanini unaniagalia tu bila ya kuongea..”

Hamza aliishia kuvuta pumzi nyingi , huku akionekana kufikiria kwa sekunde kadha.

“Wewe.. nahisi   ulitegemea  Helena angefanya vile?”

“Ulitegemea nini? Kwani  Helena nini amefanya?”

“Mwanzoni nilifikiri ulimuokoa kwasababu  ya  kuwa na  roho nzuri  na ulimuonea huruma kwa uaminifu wake . Lakini sasa hivi nimegundua kupitia yale maneno yako , ulivyosema amesalitiwa na watu wengi  ulimaanisha wewe pekee ndio tumaini lake …”

Regina mara baada ya kusikia maneno hayo mwonekano wake ulibadilika. Ghafla tu  ule pole  aliokuwa nao  tokea asubuhi ulipotea na alirudi katika hali yake ya kawaida ya ukauzu.

Hamza hakujali na aliishia kugeuza macho yake na kumwangalia Regina usoni  kwa umakini mkubwa.

“Niambie mke wangu. Ulipanga  kumuajiri  Helena tokea  mwanzo ndio maana ulitaka nimuokoe?”

Mara baada ya swali hio , hali ya hewa ndani ya gari  ilibadilika na kuwa ya ubaridiii huku anga likiwa zito.

“Kuna utofauti kwani?” Aliongea Regina  kikauzu.

“Unamaanisha nini?”

“Haijalishi nimefanya kwa roho nzuri au vipi. Ndio nilitaka awe chini yangu tokea mwanzo  lakini  kuhitaji kwangu  angalau kumemfanya kuwa hai. Isitoshe anakwenda kuanza maisha mapya , hilo si ndio jambo zuri kwake?”Aliongea Regina.

“Ndio , kila kitu kimekuwa sawa …. Lakini  kama ulifikiria tokea mwanzo kwamba kumuokoa  Helena itatosha kumfanya akufuate wewe  na kukutumikia kwa moyo wake wote , basi niseme tu  mke wangu  kweli wewe ni mke mjinga”

“Kwahio kama nimegeuka mjinga kweli ndio hunitaki tena au?  Do you  dislike me?, Do you think  I am a b*tch? Na mtu mnafiki?”Aliongea kiswanglish.

“Sijamaanisha hivyo ..”Hamza  hisia zake zilikuwa zikicheza  cheza kwa kubadilika mno  na alijitahidi kufosi tabasamu.

“Ila nahisi tu … ninachomaanisha ni kwamba  ni kama sikujui vizuri bado.”Aliendelea

Hamza aliishia kukumbuka mwanamke aliekuwa akipiga mswaki mbele yake  na kuosha uso wake  alivyokuwa  mrembo asubuhi na huyo wa sasa, mwanamke kauzu  ambae anamfanya kuwa ngumu kwake kujua anawaza nini , moyo wake ulikuwa katika mgogoro wa  kujua ni yupi  moyo wake  unapaswa kumpokea au apokee wote wawili.

“Kama unahisi mimi sio mwanamke  unaehitaji , muda wa kufanya maamuzi unao . Hutujatangazia watu uhusiano wetu  na hatujafanya  harusi , hivyo una  nafasi ya kuchagua..”Aliongea Regina.

“Tuyaache hayo mke wangu , kwa vyovyote vile siwezi kukuchukia kwasababu hii , ni kwamba tu..”

“Ni kwamba nini?”

Hamza alijikuta akibakia kuwa kimya  akishindwa kujua namna ya kuelezea.

“Ngoija nikupeleke saluni kwanza ukaoshe nywele”

“Haina haja”Bila ya kusubiria Hamza kuongea, aliendelea ; “Nilishaiona saluni ilipo muda mrefu  pale karibu tu” Mara baada ya  kuongea hivyo , palepale alifungua mlango wa gari na kutoka nje.

Hamza alijikuta akifungua mlango na kutoka nje na kweli aliweza kuona saluni iliokuwa  upande wa kulia  mkabala na hospitali. Muda huo Hamza  alijiuliza inamaana Regina alikuwa akimwigizia kuwa mjinga  hajui saluni ilipo ili ampeleke?.

Muda ule ni kama Regina alikuwa akijua Hamza alikuwa akifikiria nini   nyuma yake , hivyo aligeuka na kumwangalia.

“Mimi sio wewe , sina nguvu  za kutosha wala sina spidi  kama yako , sina  kundi la marafiki  wanaoweza kunisaidia muda wowote  kama wewe. Ninachotaka ni kulinda  biashara zangu. Na ili kulinda  kampuni yang kitu pekee ninachoweza kufanya ni kusimama mwenyewe . Kama unadhani mimi  ni tofauti na mwanamke  mjinga na mshamba  ambae ulikuwa ukimuota na kama unaona nilikuwa nikikudanganya  kwanzia mwanzo mpaka sasa endelea kufikiria hivyo hivyo. Sitaki kuelezea  kile ninachofanya  kwasababu mimi ni mimi  na  namna utakavyonifikiria hio ni juu yako. Unaweza kuondoka nikimaliza kuosha nywele zangu nitaondoka mwenyewe” Mara baada ya kuongea hivyo , Regina alivuka barabara  na kusogelea Saluni iliokuwa wazi  na bila kuangalia nyuma aliingia ndani.

Hamza aliishia kusimama  eneo moja  akiwa amekodoa macho , mara baada ya dakika kumi kupita aliishia kutoa sigara na kuiwasha  na kuegamia boneti ya gari huku akivuta moshi taratibu  na kuendelea kutafakari kuanzia siku aliokutana na Regina mpaka muda huo. Katika mawazo yake aliweza kugundua kulikuwa na vicheko , huzuni ,  utamu  na migogoro . Bila kujua dakika  arobaini zilipita  na hatimae macho yake yalionekana kupata mwanga.

“Bado tu hujaondoka?”

Hamza mara baada ya kusikia sauti hio aliishia kugeuza kichwa chake  na kumwangalia Regina ambae alishamaliza kuosha nywele.

Moja ya kitu kingine ambacho Regina  alibarikiwa  ni nywele , ni nywele ambazo alirithi kutoka kwa bibi yake. Zilikuwa nyeusi tii  na zilizopigwa pasi  na kunyooka haswa. Ilionekana hio saluni ilijua  nini inafanya.

Hamza mara baada ya kuangaliwa na macho ya kirembo , alihisi moyo wake ni kama unachomwa na visindano.

“Hio staili ya nywele imekukaa vyema sana , aliekutengeneza amekuwezea, unafanana  kabisa na mwanamke alieolewa”Aliongea lakini Regina mwonekano wake ulikuwa uleule.

“Kwanini tu hujaondoka?”

“Sijaondoka kwasababu nilikuwa nikikusubiri. Mke wangu kipenzi ingia kwenye gari tuondoke”

“Kwanini umenisubiri, si  unanichukia?”

“Mke wangu ni saa ngapi nimesema nakuchukia?”

“Kwahio  hunichukii kwa namna nilivyokufanyia , nimekuigizia  mbele yako kwa kujifanyisha kuwa m’cute, nimejifanya kuwa mkarimu  na mengineyo. Yote hayo nimefanya kwa ajili ya faida  yangu  na bado  unataka kuendelea kuniamini ?”

Hamza aliishia kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha alimwangalia mwanamke huyo usoni kwa sekunde kadhaa  na kisha alitingisha kichwa.

“Nakuamini”

“Nini.. Kwanini?”

“Its very simple. Because I love you”.

Previoua Next