SEHEMU YA 211.
Mwanamke aliekuwa mbele yake , hakuwa mwingine bali ni Rehema Mndeme , katibu muhtasi wa balozi Rajabu.
Rehema mara baada ya kumuona Hamza mbele yake , sura yake ilijawa na wasiwasi mwingi kiasi cha kufubaa.
“Mr Hamza , kwa kwanini..”
“Kwanini nimejua upo hapa , si ndio unataka kuuliza hivyo? kukujibu swali lako ni kwasababu kuna mtu alikuwa akikufuatilia”
“Kunifuatilia! Nimefanya nini mpaka kuwe na mtu wa kunifuatilia?”
“Sister Ray , kwasababu mambo yamefikia hatua hii , kuna haja ya wewe kukimbia. Ukweli tokea siku niliokutana na wewe kwa mara ya kwanza nilihisi una tatizo , hivyo huna haja ya kuendelea kujificha”Aliongea Hamza na kumfanya Rehema kuwa katika hali ya mshangao.
“Wewe..! Kwani uliona nini?”Aliuliza kwa shauku.
“Wewe sio sekretari wa idara ya kawaida . Bali ni katibu muhtasi wa kitengo cha Malibu idara ya mambo ya nje ya nchi. Hata kama unafahamika kuwa Katibu wa balozi lazima utakuwa unajua sheria zote zinazoangazia idara nyeti kama ya Malibu. Itifaki ya kwanza katika idara zote za usalama wa taifa kwa wafanyakazi wake ni kutokuongea sana. Lakini mara baada ya kukutana na wewe pale hotelini , uliongea mambo mengi sana kuhusu Mboma. Ingawa ni kwasababu ya Mboma kutokuniheshimu na ulitaka kunifariji lakini tukirudi katika misingi ya kitaaluma kama katibu wa usalama wa taifa ulichokifanya kilikuwa nje ya miiko ya kisheria kama mwanausalama. Kuongea kwako sana ilikuwa ni kwa ajili ya kupoza hatia yako na lazima utakuwa pia unafahamu ujio wangu hapa kama moja ya wawakilishi wa Malibu ni kwasabbu ya Himidu kanipa kazi ya kutafuta msaliti , ndio maana ulivyokuwa ukiongea ulikuwa ukitaka niwe na aina flani ya mawazo ambayo yanakuweka mbali na hatia . Lakini kwa bahati mbaya umekutana na Hamza na ulichokifanya kimekufichua”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
Rehema mara baada ya kusikia maelezo ya Hamza alijikuta akishangaa sana , hakutarajia werevu wake ndio umemfanya kuumbuka.
“Kama ukitoka kwenda kumnunulia bosi wako Rajabu chakula , watu wengi wataona ni sehemu ya kazi yako ya kuagizwa , na sio tu kununua chakula lakini pia muda mwingine unaagizwa na kutoa kopi baadhi ya mafaili na hata kuyapangilia , hivyo hata kama utoe kopi zaidi ya mbili hakuna atakaekushitukia , hususani na mwonekano wako wa kipole”Aliongea Hamza huku akicheka.
Muda ule Rehema alibadilika kabisa , alijawa na ukauzu na kuwa tofauti na mwanamke alieonekana mara ya kwanza alipokutana na Hamza.
“Hamza sina uadui wowote na wewe , ninachotaka ni kutumia hela na kuishi maisha ya furaha yasio na upweke na kuachana na kazi ya kutumwa tumwa. Nimeteketeza ujana wangu wote kwa ajili ya usalama wa taifa , sina mume, sina mtoto , sina kitu. Sidaiwi na nchi bali mimi ndio naidai nchi . Watu wa aina yangu huoni kama tunasikitisha sana?. Kwanini usijifanye hujaniona na kuniacha nikaishi kwa uhuru kwa sehemu ya maisha yangu yaliobakia?”
Rehema alionekana akiwa na mwonekano wa majonzi makubwa, ikionesha anaongea kutoka moyoni.
“Kama ulichofanya ni kuvujisha baadhi ya nyaraka pengine ningekuacha , lakini Dada Rehema , ulichokifanya kimesababisha watu kupoteza maisha katika shambulizi lile la kigaidi”
Rehema mara baada ya kusikia hivyo , uso wake ulijikunja , huku akiwa amegandishwa katika eneo moja.
“Kama ni hivyo .. kwahio huna mpango wa kuniachia ?”Aliuliza na Hamza alitngisha kichwa.
“Sister Rehema , weka vitu vyako chini na nifuate”
“Haha..” Rehema alicheka kikauzu ,” Nikirudi na wewe naenda kufa, siwezi kuondoka hapa na isitoshe sipo mwenyewe. Unachopaswa kufanya ni kunikamata na kunichukua kwa nguvu”
“Unajigamba tu. Haina haja hata ya Bro kukumamata”Aliongea Rhoda na palepale alifyatuka aliposimama kumsogelea Rehema kwa nia ya kumzimisha lakini sasa sekunde ileile mikondo miwili ya nishati ya rangi ya kijivu ilichomoza kama radi kumsogelea Black Fog.
“Rhoda!!”
Hamza pia aliweza kuhisi msisimko wa nguvu hio isio ya kawaida na palepale kumpigia makelele Rhoda.
Black Fog alikuwa mwepesi mno , kwani haraka sana alitumia nishati ya mbingu za ardhi na kujifyatua pembeni na kukwepa mishale ile ya mwanga.
Ule mwanga wa kinishati ulienda moja kwa moja kutua katika benchi la mbao na mara baada ya kugusana , benchi lile liligeuka unga unga kama vile limeliwa na mchwa na kusambaratika.
“Uchawi wa kifo!!”
Hamza alimaka baada ya fahamu zake kufanya kazi mara baada ya kugundua nishati hio, haraka sana alisogea mbele na kumkinga Rhoda kwa mbele huku akiangalia nyuma ya kanisa.
“Hii ni ajabu , kuna mtu ndani ya hili kanisa mwenye uwezo wa kutumia aina hii ya uchawi! Au tumeingia ndani ya kanisa feki?” Hamza aliwaza.
Tokea dakika ambayo Hamza aliingia katika kanisa hilo hakuweza kuhisi nguvu yoyote isiokuwa ya kawaida ambae amejificha , kutoweza kuhisi uwepo wake ilimtisha.
Uchawi wa kifo ni aina pia ya mafunzo ya nishati ambayo mtu hategemei nishati ya kawaida kupandisha uwezo wake , bali mchawi anavuna nishati kwa kukinga mvuke unaotolewa na maiti. Mvuke huo humtoka mtu pale tu anapokata roho na kuiachia huru nafsi yake kutengana na mwili. Sasa kadri mtu anavyovuna nishati ya wafu kwa mtindo huo, hufikia katika daraja la kuwa na uwezo hata wa kuongea na wafu, na watu hao ndio sasa huitwa Necromancer.
Yote hayo Hamza aliyajua , hivyo kitenod cha kutokuhisi uwepo wake huyo necromancer, maana yake alikuwa na uwezo mkubwa kulingana na wa kwake na kuna uwezekano pengine mtu huyo alikuwa na uwezo wa juu zaidi kumzidi.
“Father!!” Aliita Rehema kwa furaha.
Hamza aliweza kumuona mwanaume ambae alikuwa amevalia joho la rangi nyeusi akitokea nyuma. Alikuwa ni mzungu mwenye nywele zilizobadilika rangi kutokana na umri. Alikuwa amevalia miwani yenye fremu za chuma na uso wake ulikuwa mwembamba.
Hamza alizidi kuhisi hatari mara baada ya kumwangalia Padri huyo na kugundua hakuwa akitisha kabisa na kulingana na uzoefu wake wa kivita alijua kadri mtu anavyozidi kuwa wa kawaida ndio hatari zaidi.
“Ikitokea mapigano na huyu mzee , usije kukurupuka , sio mtu wa kawaida kabisa”Aliongea Hamza kwa kumuonya Black Fog.
Black Fog mara baada ya kusikia kauli hio , hisia zake zilikakamaa.Alijiuliza ni mtu gani wa kumfanya mtu kama Hamza kuwa katika hali ya tahadhari namna hio.
“I didn't expect you to be here, Lucifer,” Aliongea akimaanisha hakutegemea kumuona hapo Hamza.
“Unanijua?”
“Ndio nakujua , ijapokuwa hunifahamu , lakini nimekujua kwa muda mrefu mno”Aliongea padri yule kwa sauti ya kujiamini.
“Wewe ni nani? Maana kwa kile ninachofahamu katika ulimwengu huu hakuna mtu mwenye mwenye mafunzo ya nishati za wafu na kuongea nao zaidi ya Mr Skeleton”
“Oh! Ndio unavyojua?” Aliongea yule father na kisha alimpotezea Hamza na kwenda moja kwa moja mpaka aliposimama Rehema
“Rehema haupo makini , sababu ya mambo kufikia hatua hii ni kwasababu ya uzembe wako”
“Father tafadhari naomba uniondoe hapa , nipo tayari kukupatia nusu ya hela zangu”Aliongea Rehema.
“Lady , money means nothing to me..” Wakati akiongea hivyo palepale Rehema alionekana kuingiwa na mvuke mweusi kupitia pua , masikio na mdomo.
“Arghhhhh!!”
Rehema aliishia kutoa ukulele mkubwa , huku akidondoka chini na kuanza kutetemeka kwa nguvu. Ndani ya sekunde chache tu mwili wake wote ulitoa mvuke na kukauka..
Hamza alikwisha kutarajia suala kama hilo lingetokea na aliishia kuhema kwa nguvu kwa masikitiko ndani ya moyo wake. Hata hivyo hakuwa na muda wa kujali kuhusu kifo cha Rehema.
“Lucifer , sikutarajia kama utakuja na kuharibu mpango wangu, unachukiza mno ..”Aliongea huku akimwangalia Hamza kwa namna ya kumchunguza na kisha akaendelea.
“Ila kwasababu ya kuhakikisha mpango unaendelea kukamilika kama ilivyopangwa . kwa leo nitaondoka”
Hamza akili yake palepale iliingiwa na hisia zisizo za kawaida mara baada ya kusikia mtu huyo bado ana mpango sehemu nyingina katika muda tofauti , alijiuliza au anamaanisha muda wa kufungua kiboksi.
Kwa mchawi mwenye nguvu namna hio kujitokeza ndani ya mji wa Limour bila ya kushitukiwa . Ilikuwa ni adimu na isio kawaida.
Hamza palepale hisia zake zilimwambia bwana huyo mpango wake haikuwa kwa Rehema kabisa bali ni kupitia Baraza la maksi.
“Rhoda rudi haraka ukumbini na umwambie Rais Maxim kuna Necromancer anaepanga kushambulia Baraza”
Black Fog palepale alijua hali ilivyo hatari na haraka sana aliitikia na kugeuka kuondoka.
Mara baada ya kuona hivyo , yule padri haraka sana aligeuzia mkono kuelekea upande wa kutokea na ghafla tu mlango ulijaa kiwingu kilichokuwa kikitoa msisimko uliokuwa ukipambana na nafsi.
Black Fog uwezo wake wa nishati bado ulikuwa mdogo , hivyo palepale aligeukia madirisha , lakini ile anakaribia dirisha ili kuruka , ghafla tu aliona kisu kilichotengekezwa kwa mfupa kikisogea kutoka nje kwa kurushwa.
“Clang!!”
Kioo cha dirisha kilipasuliwa na kisu kilichoonekana kurushwa na mtu kutoka nje. Black Fog mara baada ya kuangaza macho yake nje alijikuta mwili ukimsisimka mara baada ya kuona maskeleton ya watu yakitembea kusogelea kanisa hilo , huku kila moja likiwa limeshikilia siraha, mbaya zaidi yalikuwa zaidi ya ishirini hivi huku yakiwa yamezungukwa na kiwingu cha ajabu kama mvuke.
Hamza mara baada ya kuona vile mara moja alianza kumshambulia yule padri.
Eneo hilo lilikuwa na makaburi na kwa jinsi lilivyozingirwa na nguvu ya ajabu , ilionyesha kabisa bwana huyo kuna uwezekano alikuwa ameficha maskeletoni hayo kwa ajili ya kuyatumia kama wanajeshi.
Na kwa mantiki hio Hamza aliona haitokuwa busara kupigana na maskeleton na badala yake ni vizuri kupambana na mwenye maskeletoni.
Hamza alikuwa na spidi mno na ile anamkaribia yule Padri alirusha ngumi nzito kumlenga kichwani na ilifanikiwa kumpata.
“Bang!”
Hamza alijikuta akishangaa na hio ni mara baada ya mwanzo kufikiria Padri huyo angekuwa na uwezo wa kukwepa na kujilinda lakini matokeo yake ngumi yake ilitua vizuri tu katika paji la uso wake na kumchangua.
Hamza kuona vile alihisi kuchanganyikiwa mara baada ya kugundua hali haikuwa shwari.
Ilikuwa ni tofauti na alivyotegemea , kwani mara baada ya kushambulia kichwa kile na kupasuka , tofauti na damu kumtoka , kulitokea moshi mweusi wenye msisimko wa ajabu mno.
Hamza palepale alijihisi kuwa mjinga , alipaswa kujua tokea mwanzo sababu ya kutokujua kwanini hakuweza kuhisi uwepo wa huyo Padri tokea mwanzo , sio kwasabbau ya uwezo wake bali alikuwa ni skeletoni pia akiongea kwa niaba ya mtu mwingine na kwa mantiki hio aliamini lazima Padri huyo alikuwa ni wa hilo kanisa na alizikwa hapo.
Moja ya uwezo wa wachawi wa aina hio ni kwamba wanaweza kukutengenezea uhalisia wa mtu , kwa kumvalisha ngozi bandia , ila ki uhalisia sio ngozi ni macho yako mwenyewe ndio yanayokudanganya na ndio kilichomtokea Hamza, Rhoda na Rehema.
Hamza alijikuta akiwaza palepale na kuona kumbe hata Rehema mtu ambae alikuwa akiongea nae alikuwa amekwisha kufa kitambo.
Hamza alijikuta akijiuliza kama ni hivyo huyo mchawi halisi yupo wapi, hakutaka kujiuliza mara mbilimbili na haraka sana alitoka nje ya kanisa kumsaidia Rhoda kushambulia maskeletoni mawili kwa mpigo.
Black Fog alikuwa ni mwanamke na pia alikuwa akipambana vita vya aina mbili kwa wakati mmoja vya kimwili na nafsi , hivyo ilizidi kuwa ngumu kwake kupambana na hayo maskeletoni.
“Bro tunafanyaje sasa?” Aliuliza Black Fog kwa wasiwasi
“Nitaharibu kwanza haya majitu wewe umpigie simu Asmuntis, mwambie Maxim kusitisha mara moja kikao”
Wakati Hamza akiongea alikuwa akishambuliana na maskeletoni kwa kasi ya ajabn ila licha ya hivyo wanajeshi hao wa vifo hawakuwa wakichoka hata kidogo. Maana kila wakipigwa chini kudondoka walikuwa wakisimama tena na kuendelea kushambulia.
Kilichomsumbua zaidi Hamza ni kwamba yalionekana yakiongezeka kadri muda unavyosogea.
“Bro hili eneo halina mtandano , nina uhakika wameukata”Aliongea Black Fog alieshikilia simu akijaribu kupiga.
“Damn it .. hawa watu wanajaribu kufanya nini?”
Hamza palepale alijikuta akiwaza kwa sekunde na kisha aling’ata meno yake na kuongea.
“Haina haja ya kuendelea kushambuliana nayo , tutaruka kwenda kutoa taarifa”Aliongea Hamza.
“Tutaruka!?”
Black Fog alionekana kutokuelewa lakini muda ule Hamza alishambeba juu juu na mara baada ya kushambulia maskeletoni mawili alipiga hatua mbili kwenda mbele na ile anapiga ya tatu kama mwanariadha aliruka hewani.
Hamza alikwenda kutua mita kumi mbele mbali na yale Maskeletoni na kumuweka chini BlackFog . Lakini sasa ile wanataka kuanza kukimbia waliweza kuona kivuli cha mtu alievalia joho la rangi nyeusi akiwa amesimama katikati ya barabara kwa namna ya kuwazibia njia.
Ilikuwa ngumu kumuona , kwasababu alikuwa amezingirwa na kiwingu cheusi usoni huku mkononi akiwa ameshikilia kitu cha maajabu kama fimbo ilioning’iniza mifupa mingi ya kila aina kwanzia ya ndege, binadamu na wanyama.
Hamza mara baada ya kuangalia ile fimbo ilivyokuwa ikitoa msisimko wa nguvu ya uchawi ya kutosha alijikuta akikaza macho yake na kumwangalia kwa umakini na palepale moyo wake ulipiga kite. Haikuwa kwake tu hata kwa Black Fog hivyo hivyo.
“Mr Skeleton!!!”
Hawakuamini , mtu ambae alikuwa akiwashambulia alikuwa ni mchawi wa misitu ya Amazoni , Mr Skeleton moja ya magwiji kumi wa Baraza la maksi.
Comments