Reader Settings

SEHEMU YA 212.

On Fire.

Hamza alishangaa mno kuona mchawi ambae alikuwa  akishambuliana nae kupitia maskeletoni ni  Skelidon Magus ambae alikaa nae jukwaa moja la magwiji wakati wa vikao.

“Imekuwaje..! Bro si tulimuacha ukumbini?”Aliuliza Roda kwa mshangao.

Hamza pia alikuwa katika mshangao mkubwa na hakuacha kuhisia , suala hilo linazidi kuchukua sura  mpya.

“Haha.. haha..khoo..” Mr Skeleton alitoa kicheko kilichoambatana na  kikohozi, “Lucifer mwili wako una  nguvu mno , yaani unao uwezo wa  kuruka umbali mrefu hivi bila ya kutumia  nishati yoyote. Ni kwa bahati mbaya tu  siwezi  kuwaruhusu muondoke sasa hivi  na kuvujisha taarifa”

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa  Hamza kusikia  Skelidoni au Skeletpni  akifungua mdomo na kuongea. Tokea aingie  kwenye ukumbi ile jana hakuongea neno hata moja.

Hamza pale mara baada ya kuwaza ni kama akili yake iliingiwa na wazo lingine na kumfanya kukunja sura.

“Wewe..!  Sio wewe uliekuwepo ukumbini  bali ni..”

”Naona umegundua!”Aliongea huku akiendelea kucheka, “Yule sio mimi  tokea mwanzo , ni lijimfupa linaloitikia wito wangu”

“Mr Skeletoni wewe ni moja ya  Magwiji  kumi wa dunia, kwanini unashirikiana na Sinagogu! Au wewe  ndio  wanaekuita Devasi , mfalme na kuhani wa Sinagogu, una uhusiano na makanisa  ya Wabrazili?”Aliongea Hamza.

“Una maswali mengi sana  na hakuna haja ya mimi kuyajibu. Wewe na huyo mwanamke  mnapaswa kukaa  na mimi hapa kwa muda”

Mara baada ya kuongea hivyo aliinua kile kitu alichoshikilia mkononi  na mfoko  wa nguvu ya kifo  uliongezeka na kuwavaa Hamza na Black Fog.

“Msisimko wa kifo!”Aliongea

Hamza mara baada ya kuona vile , haraka sana alimkumbatia Black Fog na kukwepa shambulizi lile kwa kusogea pembeni.

Spidi ya Black Fog ilikuwa ndogo kuweza kuhimili nguvu ya  Msisimko wa kifo.

“Bro usiwe na wasiwasi  juu yangu , ukiendelea hivi utamshindwa, nitajilinda mwenyewe”Aliongea Black Fog.

Lakini Hamza hakutaka  kuchukulia suala hilo kiwepesi. Na palepale aliruka  mara mbili na kwenda kutua juu ya paa la kanisa  na kumtua chini Rhoda.

“Wewe  kaa hapa  kwanza, ndio namna pekee ya kuwaeupuka  wale maskeletoni  na pia kuepuka uchawi wake”Aliongea Hamza.

Muda ule ndio sasa alijua Hamza amemleta hapo kwa ajili ya kuwa salama, hivyo haraka sana alitingisha kichwa.

Hamza mara baada ya kuachana na msichana huyo . aliruka  kurudi chini. Alijua  kama  hatoweza kumshinda Skelleton , hata kama anao uwezo wa kukimbia , Black Fog anaweza asifanikiwe kuondoka akiwa hai . Hivyo njia pekee  ilikuwa ni kupambana.

Hamza alijiambia ni  kheri  bwana huyo angekuwa mchawi wa kawaida kama wa Wican , lakini alikuwa  katika  daraja la kuongea na wafu hivyo  ni hatari  sana kushindana na msisimko wa kifo anao  toa.

Hamza alitumia spidi kubwa kukimbia na kukusanya hewa nyingi kumzunguka  na  staili ile ilimsaidia kusukumia mbali  ile nishati ya  kifo  na kumsogelea Skeletoni kwa spidi na  kulenga kichwa chake na ngumi.

“Mfupa ngao!!”

Skelitoni  palepale aliita  mfupa  uliobeba nguvu nyingi ya kichawi na  kujikinga  na Hamza.

“Bam!”

Hamza alijikuta akipambana na  wimbi  kubwa  la nguvu ya kichawi lililokuwa  kama ngao  na ile analisambaratisha kwa ngumi yake aligundua Skelitoni alishaondoka aliposimama na kuelea angani  kama  pepo kwa kurudi nyuma nyuma. Muda ule  yale maskeletoni walioyaacha mwanzo nyuma yalimsogelea Hamza kwa spidi huku yakionekana kuungua kwa moto usiokuwa wa kawaida.

“Miale  ya kuzimu!”Aliongea Skelidoni

Hamza mara baada ya kusikia vile na kuona , aliishia kukunja ngumi huku akisaga meno yake  na kwa spidi kubwa alianza kuyasambaratishya  yale maskeletoni  na ngumi na mateke.

Mara baada ya kushambulia kama mara nane hivi  aliyamaliza. Lakini kitu  kingine  alichogundua ule moto  uliokuwa ukiwaka katika miili yao haukuwa na joto na badala yake ulikuwa na hali flani ya ubaridi isiokuwa ya kawaida ambayo  ni kama ilikuwa ikizuia mzunguko wa damu.

Hamza mara baada ya kuguswa na moto ule mikono yake  ilijihisi ni kama imekufa ganzi , lakini hata hivyo hakukuwa na madhara makubwa.

“Unao uwezo wa  kuhimili miale yangu!?”

Hamza hakuwa na muda wa kuongea nae. Aliamua kutumia faida ya spidi yake  na kumsogelea  Mr Skelletoni kwa spidi  na kisha  alirusha ngumi kulenga kichwa chake . Hata hivyo  ghafla tu  nyoka  alichomoza katika kofia(hood)  na kutaka kumng’ata Hamza.

“Hiss .. Hiss!!”

Kwa kuangalia tu nyoka hio na rangi yake , ilikuwa ni rahisi kujua ni kwa namna gani ilikuwa na sumu kali.Ilikuwa ni nyoka jamii ya Viper.

Ilikuwa ni kwa  bahati nzuri , Hamza spidi yake  ni  kubwa  kuliko mtu wa kawaida , hivyo aliweza kukwepa shambulizi  lile la nyoka kwa kuondoa mkono wake.

Nyoka yule mara baada ya kufeli , alijificha  ndani ya ukaya(hood)  na kupotea.

Hamza kuangalia  ukubwa wa  koti hilo kama joho alilovalia alijiuliza   kutakuwa kweli na nyoka  mmoja au kuna wengi zaidi. Hamza aliona anapaswa kuwa makini   maana  kuna uwezekano kuna siraha  nyingine alizoficha.

“Hehehehe… . hatari sana , hatari sana  ila kwa bahati nzuri  kipenzi changu aliwahi  kushituka . Lucifer  spidi  na nguvu zako ni kubwa mno. Ndio maana umeweza kumuuwa Gonzalez kikatili”

“Acha maneno yako ya kimitego , najua uwezo wako  sio huu unaonyesha”Aliuongea Hamza mara baada ya kuona ni kama bwana huyo hakuwa akitaka kutumia mbinu zake zote.

“Wewe na  mimi  tunapaswa kutumia uwezo wetu wote ili mshindi kupatikana  lakini tutahitaji muda mwingi sana na kwa  bahati mbaya sina muda wa kupambana  na wewe mpaka mshindi apatikane”

Muda ule ghafla Black Fog aliekuwa amesimama juu ya paa la kanisa alianza kupiga makelele.

“Bro hatari ! Angalia upande wa makaburini”

Hamza alijikuta akigeuka haraka sana na kuangalia upande wa makaburini  na eneo la katikati katika   moja ya kaburi kubwa  palionekana kuzingirwa na kiwingu kikubwa cha moshi kilichoambatana na msisimko wa kifo.

Aura iliokuwa ikitokea   katika eneo lile na   hisia  zake , ilikuwa ni dhahiri  kuna roho  nyingi za wafu zimeitwa.

Palepale  ghafla tu  maskeletoni na  watu wenye miili iliooza walianza kuibukia kutoka chini. Walikuwa wamebeba kiwango kikubwa cha roho ya umauti na kufanya kuogopesha mno.

Kwa namna maskeletoni yale yalivyoibukia katika eneo moja  , Hamza alijua fika lazima yatakuwa yamefikishwa hapo  na watu kwa ajili ya Skellidon kuyaamsha kwa kuyafukia na mchanga mwepesi.

Kwa haraka haraka   maskeletoni hayo pamoja na maiti, idadi yao ilifikia  angalau miatatu au mianne hivi.

Ile kauli ya mtu mmoja  jeshi , hatimae uwezo wa Mr Skelliton wote ulianza kuonekana.

“Haha.. hahaha..” Skelidoni alitoa kicheko cha nguvu cha uovu huku  akiinua kile kifaa  chake alichoshikilia mkononi na  kuanza kuelea kama vile anapeperushwa na upepo kurudi nyuma.

Muda ule  wingu la  rangi  ya kijivu lilianza kusambaa  na kuyafunika yale maskeletoni na miili ya wafu.

“Fanaka isiokoma!!”

Mara baada ya Skelliton kuongea vile , ghafla tu kile kiwingu kilianza kuvamia  yale maskeletoni na kuyafanya yaanze kuchangamka kama vile yameguswa na nyaya za umeme.

Mara baada ya kutulia  na kupata nguvu za kusimama  vizuri  ghafla yale matundu  ya macho katika eneo la fuvu yalijaa  miale  ya  kimizimu na kugeuka na kumwangalia Hamza.

Maskeletoni yale ya mwanzo hayakuwa na nguvu  kama hio ,  hayo ya muda huo  yalikuwa sio   ya kawaida kabisa  na  mpaka mtu kuweza kuyatawala  yakiwa mengi hivyo  maana yake  uwezo wake  ni mkubwa mno.

“Go! My undead army!”

Skellidon mara baada ya kuinua kile kifaa mkononi  mwake juu angani,  palepale yale maskeletoni  yalianza kutimua  kuelekea  upande mmoja, huku ikisikika sauti  ya ajabu  ya  kibundi bundi , ilikuwa ni ngurumo ya ajabu mno.

Muda ule Hamza alijua Maskeletoni hayo  yalilengwa  kumshambulia yeye  , lakini kilichotokea   ilikuwa ni tofauti  kabisa , kwani  yalichukua uelekeo mwingine, na Hamza mara baada ya kupima uelekeo wake, aliweza kugundua ni upande wa  Baraza la maksi linakofanyikia.

Hamza alijikuta  kichwa chake kikimuwasha na kujiuliza isije ikawa huyo  mshenzi anapanga kwenda kuua kila mtu   ndani ya  ukumbi.

Ijapokuwa kwa Magwiji isingekuwa hatari na kwa baadhi ya wanajeshi wenyewe uwezo , lakini kwa baadhi ya  wanachama ambao hawakuwa na mafunzo  ingekuwa hatari sana.

Hamza alijiambia kama Nyakasura angekuwepo hapo, pengine ingekuwa rahisi kuweza kuzuia  maiti hizo  zisiondoke katika hilo eneo kwa moto wake  lakini  Hamza   uwezo wake   haukumruhusu kushambulia   maskeletoni mengi namna hio .

Kitu pekee ambacho aliona anaweza kufanya ni kurudi haraka  na kwenda kuwataarifu wengine juu ya balaa linalokuja . lakini   Skelidoni ndio huyo hakutaka kumpatia nafasi ya kuondoka.

“Lucifer  nimekuchanganya!”

Skellitoni aliongea huku akicheka vibaya  na  palepale  alituma tena wimbi  la kifo kuelekea kwa Hamza.

Hamza kukwepa shambulizi lile ilibidi aruke juu na kwenda kutua kwenye ukuta wa kanisa na kisha akapiga sarakasi na kupiga mbizi kurudi chini kumsogelea Skelitoni.

Hata hivyo Mr Skelitoni hakuwa mzembe pia juu ya  spidi yake . Mara baada ya kuona Hamza anamsogelea kumshambulia  kwa mara nyingine  alipeperuka na kurudi nyuma.

Hamza aliishia kutua  chini huku akijizuia na mkono mmoja kwa kushika chini  na kisha  aliruka tena  na kumsogelea Skelleton kwa spidi.

Ingawa Skelitoni hakuwa na spidi kama Hamza , lakini alikuwa na mbinu nyingi za kujilinda.

Mara baada ya kumuona Hamza anamsogelea aliita  mkuki kama reki na kumrushia Hamza  kwa  spidi kubwa.

Hamza aliishia kusambaratisha mfupa ule hewani kabla ya kumfikia  na kushidwa kumshambulia kwa mara nyingine.

“Kubali kushindwa Lucifer , huwezi kushindana na mimi , hata kama uwezo wako umeongezeka kuliko ulivyokuwa  miaka  mitano iliopita. Mbinu  unayojifunza ni kwa ajili ya kufufua asili ya mwili pekee. Watu wa nyama kama wewe mbele yangu hamfurukuti .. hahaha.. hahaha”Skeletoni alicheka kwa nguvu.

Hamza alijawa na ukauzu mwingi usoni , ijapokuwa hakutaka kukubali lakini bwana huyo aligusa penyewe.

Kama ingekuwa ni miaka iliopita  , akiwa na  nishati ya   mbingu na maji ya  uhai pamoja na mbinu nyingine za mapigano , ingekuwa rahisi  kushindana nae. Kwasababu muda huo ni sawa na  kuingia katika vita ya  kiroho na mwili wa kawaida, jambo ambalo  ni ngumu mno kushinda.

Mfano Hamza angekuywa na nishati  ya  mbingu na ardhi ya ufunuo wa maji ,  ambacho angefanya ni  kuzingira eneo hilo na   nguvu ya  nishati yake  na kutengeneza uzio ambao usingeruhusu  maskeletoni kupita.

Sasa muda huo mafunzo ya Hamza yalikuwa ni ya nyama kwa nyama na alitegemea zaidi kufanya mafunzo makali , uvumilivu wa juu , spidi na  sifa nyingine ili kuboresheka. Lakini hata hivyo mbinu yake ilihitaji  mshindani ambae ni kama Gonzalez na sio yule anaetumia nguvu za kiroho.

Skellitoni   hakupambana nae ana kwa ana na badala yake alitupia tu uchawi  kufanya mashambulizi  hivyo na kufanya mbinu za Hamza  katika kushambulia kukosa nguvu.

Ilikuwa  ni rahisi kupambana na Nyakasura , kwasababu  Nyakasura mapigo yake ni  yale yanayoonekana  ambayo yalihitaji ukaribu zaidi wa kimwili ili kufanikiwa. Lakini  sasa muda huo amekutana na  Skellitoni ambae  ni mchawi mkubwa , asingepigana kwa kusogeleana nae zaidi ya kushambulia kichawi kwa mbali na kumfanya kutokuwa na  uwezo wa kumfikia.

“Kama nikiendelea hivi , hata kama sitokufa lakini  nitachoka mno kiasi cha kufa”Aliongea Hamza  katika moyo wake.

Eneo hilo lilikuwa la makaburi na kwa mtu kama Skeletoni ambae  nguvu zake  zilitegemea zaidi  nguvu ya roho za umauti , angeweza kuhimili kupambana hata kwa siku kumi mfululizo lakini sio kwa Hamza. Japo ni kweli Hamza hakuathiriwa na uchawi huo wa kifo lakini  hakuwa na uhakika kama anaweza kuhimili kwa muda mrefu.

Shida haikuwa kuvumilia na kupambana kwa muda mrefu , jambo lingine abalo lilikuwa likimpa wasiwasi ni juu ya mke wake Regina. Alikuwa akitaka pia kumlinda na yupo mbali,uwezo wa kukimbia kumfuata  Regina  alikuwa nao lakini asingeweza kumuacha Black Fog peke yake.

Muda ule  Skelleton alitoa shambulizi  lingine la nguvu za kichawi kumlenga Hamza.

“Shimo la Umauti!”

Kiasi kikubwa cha  msisimko wa nishati ya kifo  kilimzunguka Hamza. Wakati huo huo  mifupa  ya  yale maskeletoni yaliokwisha kuharibika ardhini yaliinuka kama vile yanapeperushwa na upepo na kumvaa.

Hamza  aliishia kukwepa  kwa kwenda mbele na kurudi nyuma kwa ustadi wa hali  ya juu lakini kwa wakati mmoja nafsi yake ikizidi  kuathiriwa na  roho ya umauti .

“Miale ya kuzimu!”

Skeletoni kwa mara nyingine aliona achukulie  nafasi  kuhangaika kwa Hamza  na kuamsha maskeletoni yaliobakia yakiwa na  moto ule wa baridi kumsogelea Hamza na kumgonga.

Hamza bila ya kupenda alijikuta akivuta hewa nyingi ya  umauti  na kwa wakati mmoja akiathiriwa na  ubaridi wa miale ile ya kuzimu. Alianza kuhisi nafsi yake ikianza kujitawala nje ya hiari na kufanya mwili wake kumshinda.

Black Fog aliekuwa amesimama juu ya kanisa , ingawa aliweza kuona wapo wanajeshi  wengi wa  umauti  ambao angeshindana nao , kumuona Hamza akiwa amezingirwa pande zote na maskeletoni yale . Alishindwa kujizuia na kujawa na wasiwasi mkubwa.

“Bro kimbia! Kimbia tu na usijali  kuhusu mimi”

Makelele hayo ni kama yalimkumbusha Skeletoni kuna mtu mwingine ndani ya eneo hilo.

“Lucifer, nitamuua yule msichana kwanza  na kisha nitapigana na wewe kisawa sawa”Aliongea  na kisha palepale alitoa sonyo lililoambatana na  tabasamu la ukatili.

Mara baada ya kugeuka alirusha,  mfupa  ulionekana kama wa paja la mtu  kuelekea kwa  Rhoda.

Black Fog alikuwa mwepesi mno  na sarakasi moja tu aliweza kukwepa  mfupa ule  kwa namna ya kipekee , lakini hata hivyo  Skelletoni alikuwa ametarajia jambo hilo  , hivyo alisukumizia  wimbi la upepo wa nishati ya  kifo.

Kuhusu wimbi hilo lilikuwa  ni kama upepo wa kawaida tu , hivyo ilikuwa ngumu kwa Black Fog kukwepa.

Mara baada ya kuona  Black Fog anakwenda kumezwa na upepo ule wa kisulisuli  wenye nguvu ya umauti . Hamza aliruka  haraka sana  na  kumpiga  Black Fog kikumbo  na kumrushia mbali.

Black Fog aliishia kudondoka  kutoka juu ya kanisa , lakini haikiwa  tatizo  kwake , ila sasa ile anageuka na kumuangalia Hamza . Aliweza kumuona akikakamaza misuli akishindana na nguvu ile ya uchawi wa kifo .

Hamza alivuta pumzi kwa shida , alihisi mapafu yake ni kama  yanashindwa kupanuka   na kuingiza hewa , huku ule uchawi wa kifo ukipelekea hali ya kulegea kwa viungo vyake  vya ndani.

“Bto kwanini umeniokoa na kujiingiza kwenye matatizo”

Black Fog alishindwa  kuvumilia na kupiga sarakasi mbili na kumsogelea Hamza  huku machozi yakiwa yamemvaa.

“Usinisogelee! Kaa nyuma yangu” Hamza licha ya kuwa katika hali mbaya alijikamamaza na kumkemea Black Fog.

“Ni makosa yangu , kama sio mimi   usingeumia.”

Kinadharia ,  ingawa Hamza  alikuwa na wakati mgumu kushindana na Skeletoni , kama angeamua kuondoka , Skeletoni   hata kwa uwezo wake asingeweza kumzuia. Lakini kwasababu yake Hamza  alikosa jinsi na  kupambana nae ili kumlinda  na  kuzidi kumpelekea  kuwa na wakati mgumu kuweka umakini kwenye  kupigana.

“Lucifer , hakika umenishangaza! Ni  mbinu gani unajifunza mpaka kuweza kuhimili   nguvu yangu kubwa ya wimbi la umauti  na kuendelea kuishi?.. haha unanipa  hamasa ya kutaka kukuua na kukugeuza  mwanajeshi wangu , nina uhakika utanifanyia kazi kubwa kuongoza waumini wangu duniani kote”

“Bado hatujafikia mwisho wa pambano  ushaanza kufikiria mbali?”

“Oh! Kwahio  bado unafikiria kupambana na mimi?”

Hamza hakujisumbua kujibishana nae , aliona kama  hali itaendelea kama hivyo atachoka mpaka kufa.

“Mgawanyiko!!

Hamza ghafla tu alisimama  wima na kutoa  sauti  kwa nguvu na kwa mara nyingine  aliamua kutumia mbinu ya  mgawanyiko.

Ingawa Hamza alitumia mbinu  hio ya mgawanyiko  jana yake tu , ila hakuhisi  shida yoyote, ukiachana na kwamba nguvu zake  za mwili zilipungua , lakini hakuhisi tofauti   yoyote  mbaya.

Hivyo  Hamza hakujali sana kuitumia tena, ukweli ni kwamba hakujua  kuhusu madhara ya mbinu hio ni nini kwasababu ilikuwa ni nusu  tu, lakini alitaka kuitumia kumdhibiti Mchawi wa misitu ya Amazoni.

Seli zote za mwili  zilijikusanya  na kukaa pande  kwa ajili ya kupambana  na sumu ya kifo iliokuwa ndani ya mwili wake.

Hamza mara baada ya kutumia mbinu hio , alihisi mwili wake ni kama unajitengeneza upya. Na kwa mara nyingine alijihisi  kuwa ni mwenye bahati kuja kukutana na Yonesi na kumpatia mbinu hio.

“Asante sana Yonesi!”

Hamza aliongea katika moyo wake , hakutaka kusahau kwamba  yote hayo ni Yonesi  alieyawezesha na kuna muda alihisi pengine kukutana kwao si kwa bahati mbaya.

Kwa namna yoyote  Hamza hakutaka kufia hapo , alipanga kumrudia mke wake na kumalizana na masuala ya Ufaransa na kurudi nyumbani.

Black Fog alijua ni muda wa Hamza kuanzisha  mapigano  kisawa sawa , hivyo hakutaka kuwa mzigo tena na kujificha nyuma yake.

Mr Maskeletoni   alionekana kuwa makini  kuliko mwanzo , aliita  wimbi kubwa la upepo wa kifo wa kisulisuli na kumzingira  huku kwa wakati mmoja akitumia  mifupa mingi  kama ngao  yake.

“Njoo , Lucifer  ni muda wa kuona  una nguvu kiasi gani mpaka ukaweza kumuua Goliati wa Chuma , Gonzalez”Aliongea

Hamza hakuongea neno . Aliruka  na kwenda kukaa   usawa wa  Mr Maskeletoni  na muda ule wakati anasogea  ni kama alianza taratibu na ghafla tu alipotea

“Bang! , Bang! , Bang!”

Mifupa mitatu ya ulinzi iliokuwa ikizunguka hewani  kama kinga, ilisambaratishwa na  nguvu za kinyama za Hamza .

Mr Maskeletoni , alionekana kuogopa.Hakutegemea  baada ya Hamza kuchukua sura mpya  angeweza kuwa na uwezo mara mbili yake.Ile anataka kujipeperusha kurudi nyuma , Hamza huyu hapa mbele yake.

Hamza  macho yake yalionekana  kama vile yanaungua na moto,  na  mwili wake uliokuwa na nguvu zaidi ya mara mbili  ulifyatua ngumi  nzito katika ukaribu  mkubwa zaidi.

“Kufa!”

Hamza ngumi yake ilichomoza , ile nyoka  ndani ya ukaya , haikuwa hata na muda wa kujichomoza tena  kumng’ata Hamza , kwani ngumi ilikuwa ishawasili tayari.

“Bam!’

Hakukuwa na damu yoyote , Hamza alijihisi ni kama mkono wake umepigana na fuvu tu.

Muda ule akishangaa , ghafla tu  mwili wa  Mr Maskeletoni  ulitoa mvuke na kujaribu kumvaa  Hamza. Sio mvuke  tu , nyoka wa rangi tofauti tofauti pia walichomoza  kutaka kumng’ata.

Hamza mkono wake ni  kama radi kwani kupitisha tu aliua  nusu ya wale nyoka,  huku kwa wakati mmoja akirudi nyuma  na kukwepa  minyororo ile ya roho ya kimauti.

Kilichomshangaza Hamza ni kwamba   Mr maskeletoni mwenyewe alionekana kuwa limfupa  tupu lisilo na nyama ambalo amelifunika na koti . Skeletoni lenyewe liliharibika na ni nusu yake tu ndio lilibakia baada ya kulitia ngumi.

Lakini sasa ile nguvu ya kifo iliokuwa imemzingira  ilikusanya ile mifupa na kujirudisha   tena na  fuvu lake  lilijirudisha katika hali ya kawaida.

“Shenzii! , wewe ni kitu gani?”

Hamza alishindwa kujizuia na kuishia kulaani , katika maisha yake alipigana na  maadui wengi sana na washindani wa kila  aina , pamoja na vita  vingi.  Lakini hakuwahi kushuhudia  fuvu likijirudisha upya baada ya kuchanguliwa.

“Unafikiri wanaosema  mimi ni wa milele  na Mchawi  wa Maskeletoni wanadanganya?. Mimi Skeletoni  ni nafsi  ya umilele , hata kama uharibu skeletoni  langu naweza kuvaa lingine tu  na kuzaliwa upya”

“Bullshit , wewe sio Mungu  ila ni mchawi tu . Ijapokuwa najua mwili wako ni wa skeletoni lakini kama siwezi kukuua kwa shambulizi moja , kama ni unakufa  kwa mashambulizi mawili  au hata mia moja nitafanya hivyo”

Hamza aliishia kung’ata meno yake kwa hasira , mwili wake uligeuka na kuwa kama mshale  na kwa mara ya pili alimsogelea Mr Maskeletoni. Lakini awamu hio Mr Maskeletoni , alikuwa amejiandaa . Ingawa ilikuwa ngumu kukwepa shambulizi la Hamza kwa asilimia mia  lakini aliweza kuita dhoruba ya umauti ndani ya wakati kujikinga.

“Tufani ya umauti!”

Mr Maskeletoni  mwili wake ulizingirwa na kimbunga  cha msisimko wa kifo , kwa umbali wa mita mia moja za mraba , mchanga na vitu vyote vilivyokuwa ardhini vilianza kupanda hewani  kwa namna ya kuzunguka na kumzuia Hamza.Haikuwa hivyo tu , mifupa mingi ilimsogelea Hamza  kwa kasi na kuanza kumshambulia.

Ingawa Hamza alikuwa na uwezo wa kuzuia  mifupa hio , ilikuwa ngumu kumsogelea Mr Skeletoni  pale alipo  na kumshambulia tena kama mwanzo.

Mr Maskeletoni  alijitengenezea kimbunga na kujjiweka kati na Hamza alipambana na kimbunga ili kumfikia katikati na kumshambulia na ngumi.Ilikuwa patashika ya kuvutana.

 

Previoua Next