Reader Settings

SEHEMU YA 213.

Katika  eneo la  kikao , mathalani ndani ya ukumbi ambao  mkutano wa Baraza la maksi ulikuwa ukifanyika.

Ijapokuwa Hamza hakuwa amerudi bado  ukumbini kwa muda mrefu , lakini  vikao viliendelea kama kawaida.

Mambo mengi ya hapa na pale  yanayohusiana na ulimwengu wa  giza yalikuwa yakijadiliwa  mpaka  usiku wa kiza. Kwa washiriki wengine walijikuta wakiboreka , maana majadiliano hayo yalikuwa  ni juu ya sheria mpya.

Lakini licha ya hivvo , hakuna ambae aliondoka mapema m kwasababu  tukio la mwisho lilihusisha  ufunguzi wa sanduku  lililoachwa na  mwanasayansi nguli  Dokta Genesha kama alivyofahamika  kwa jina lake la kawaida na Tembo wa  Trishaza jina lake rasmi la ulimwengu wa Giza.

Magwiji wote  waliokuwepo ,  macho yao yote na hamu zao zote zilikuwa ni kutaka kufahamu nini kipo ndani ya kiboksi hicho.

Tembo  wa trishaza alipotea  miaka miwili au mitatu iliopita  na hivyo  kudhaniwa kwake kufa haikuwa siri tena. Na kuhusu  kilichopo  ndani ya kiboksi hicho  waliamini ndio urithi ambao ameuacha  na pengine ikawa ni   utafiti wake juu ya dawa ya kuzuia kifo.

Hatimae , baada ya  saa nne za usiku  kutimia , raisi wa Taasisi ya Maksi na  wadumisha amani ,  Rais  Paul Maxim alisimama juu ya jukwaa.

“Naamini kila mmoja wenu amekuwa akisubiri  taarifa hii kwa muda mrefu , bila ya kuwasahau magwiji wetu kumi wa ulimwengu wa giza  juu ya juktwaa. Asanteni sana kwa  uvumilivu wenu”

“Hatua inayokujia  tutafungua  sandulu la Dokta Genesha na kuona ni kitu gani ametuachia  kabla ya kupotea kwake”

Watu mara baada ya kusikia maelezo hayo ,shangwe nyingi zilisikika, ukiacha masuala ya kutangaza sheria mpya  na  mikakati ya kudumisha amani ,  suala  ambalo lilisubiriwa na watu wengi kwa hamu , lilikuwa ni hilo.

Wafanyakazi kadhaa wa  Set Society  waliweza kuleta  kiboksi cha chuma cha rangi nyeusi juu ya jukwaa.

Kisanduku hicho kilipaswa kufunguliwa kwa nywira , hakukuwa na  ugumu mkubwa wa kufungua kama kutumia jicho  ama kidole , bali ni herufi tu ndio zilipaswa kuingizwa

Mara baada ya  kiboksi kile kuweka juu ya  jukwaa katika meza maalumu , Rais Maxim , alisogea  na kama kawaida yake na sauti kama ngurumo aliongea;

“Dokta  Tembo  mara baada ya kufika ofisini kwangu  kunitembelea , alinikabidhi hiki kiboksi na kuniambia password zake . Kwa miaka yangu sitini ya uzoefu  na hulka yangu , alikuwa na uhakika sitokifungua  kabla ya muda. Na ni matumaini yangu kwenu wote mtaamini maneno yangu  na kuona  na mimi ni mara yangu ya kwanza kwenda kuona kilichopo ndani yake”

“Mzee Maxim , huna haja ya kujielezea , kila mtu anakuamini hapa”Aliongea Oleg Phantom.

“Ni kweli kabisa , kiongozi tabia yako ni kielelezo muhimu  kwa kila mmoja ndani ya ulimwengu wetu”aliongea Silvia.

Watu wengi pamoja na taasisi  mbalimbali hawakuwa na pingamizi  na  kuungana na wengine kumuamini  Raisi Maxim.

Hakuaminika kwasababu ya   cheo chake , bali ni kwasababu   kwa muda mrefu amekuwa mtu  mwenye  busara sana na  anaeongozwa na  sheria ya uaminifu. Vinginevyo asingechaguliwa na kuwa raisi wa Set  mbele ya  watu wakubwa wenye nguvu  kama hivyo.

“Asanteni sana kwa kuniamini , nitafungua  kiboksi hiki sasa”

Aliongea na palepale chini ya macho ya maelfu ya watu aliingiza nywira zenye mkanganyiko mkubwa.

“Zii..! Ziiii!”

Hatimae kiboksi kilikubali  zile nywira na Maxim alifungua mlango taratibu wa kiboksi kile.

Ndani ya kile  kiboksi kulikuwa na nyaraka ,  hakukua na kitu kingine zaidi.

Maxim aliishia  kutoa nyaraka ile ,  au bahasha  na kuisoma pale juu kwa nguvu; “A, K , H . Hili ndio jina  lililoandikwa hapa juu  , jina la nyaraka” Aliongea na kuweka vizuri  nyaraka ile ili kamera zipige na kuonyeshwa kwenye runinga watu waone.

Maelfu ya watu mara baada ya kuona  kichwa cha nyaraka  ile minong’ono  iliibuka , kila mtu  akionekana kuotea kitakuwa kitu gani.

Nusu ya  wawakilishi  waliokuwepo , pamoja na taasisi kubwa , walikuwa na uelewa kidogo juu ya  dawa ya kifo  na  jina lake  lilivyoitwa iliwafanya wawe na hali ya msisimko wa shauku katika  macho yao.

“ANKH... Cross of Life… hivi ni kweli  itakuwa ni  taarifa za tafifi za Genesha juu ya  dawa ya kifo?”Aliongea Oleg na kumfanya Silvie kumwangalia  Mathias Huge wa jicho la Anga au Binamu.

“Master Huge isije ikawa  kupitia jicho lenu la Anga , mlijua kilichomo ndani ya kiboksi ni  Ankh !Ni kweli?”Aliuliza

“Samahani , siwezi kujibu swali lako”Aliongea Huge m hakuwa na hisia zozote  katika  sura yake, zaidi ya tabasamu hafifu.

“Unavyopenda kujikweza sasa , hata kama una teknolojia ya jicho la Anga huwezi kujua kila kitu. Kama  mngekuwa na uwezo wa kuweza kumfuatlia mwanasayansi mwenye akili nyingi kama Dokta Genesha si  mngeshamchukulia hatua tokea mwanzo?”Aliongea  Mtakatifu Auland.

Auland kama kiongozi wa jamii ya siri ya wanajeshi wa  zama za kale , maarufu kama  Knight Templar au Dragon Knight, hajawahi kuwa  na ukarimu wowote mbele ya watu wa Binamu. Kwasababu  kazi yao kubwa  ilikuwa ni  kufuatilia mambo ya watu  na kila wanapopata taarifa wanauza bila ya kujali  hasara    juu ya  mwenye siri zake. Huge hakuongea neno  zaidi ya kutingisha kichwa chake  na tabasamu.

“Kama kweli kutakuwa na dawa ya kifo , binadamu ataingia  katika  nyakati mpya za  kustaarabika”Aliongea  Vampire Sebastian.

“Sebastian usiwe na wasiwasi , hata kama  itokee  kuwe na dawa ya kifo ,  binadamu  hawatokuua. Isitoshe  tunaweza kuwafanya  wanyama wa maonyesho  kwenye Zoo”Aliongea Mikaeli.

Kauli hio ilimfanya Sebastian kujawa na  hasira na  macho yake kuonyesha nia ya kimauaji lakini licha ya hivyo Mikaeli hakumuogopa na alimkazia macho vilevile.

Muda ule hatimae   nyaraka ndani ya bahasha ilitolewa , na taarifa juu ya dawa  ya kifo  zilimulikwa. Muda huo  magwiji wawili , yaani wa  madhabahu ya Giza na ya Nuru walionekana  kungurumiana.

Sababu ilikuwa nyepesi tu  , kitu pekee ambacho  Strigoi  wanajivunia  nacho ni kuishi  miaka mingi. Strigoi waliamini siri ya ukuu wa binadamu  imefungwa katika uchache wa miaka yake  ya kuishi . Hivyo ikitokea binadamu akapata  dawa ya kuvuka kiunzi   na kurefusha umri wake maana yake kadri atakavyoishi ndio ataendelea kugundua nini kimejificha katika mwili wake na mwisho wa siku watakuwa na nguvu  kubwa kuliko  wao.

Wakati binadamu yeye akitafuta dawa ya kurefusha uhai , Strigoi wenyewe  wanatafuta dawa ya  kuurefusha uhai wao bila ya kulala muda mrefu.

Maana yake ni kwamba  wakati   binadamu wakijiendeleza , wao watakuwa wamelala  pono ili kurefusha   uhai na  kipindi cha kulala  kwao mpaka wanaamka binadamu watakuwa wamepiga hatua kubwa na kama ni hivyo  maana yake ni kwamba kauli ya Mikaeli   kuwageuza  wanyama wa maonyesho   kwenye Zoo  inaweza kuwa na ukweli.

Hivyo  kwa namna yoyote  ile Madhabahu ya Giza hawawezi kuruhusu binadamu kupata  dawa ya kuzuia kifo.

Mara baada ya kuona magwiji wawili  wa  madaraka makubwa  tayari wapo  on fire . Maxim aliona aongee kidogo ili kupoza hali.

“Tafadhari naombeni mtulize jazba! Nyie mnagombanaje  bila ya kujua nini kipo  ndani yake”Aliongea.

“Kama ni hivyo basi tunaomba raisi  utufngulie hio nyaraka  na kila mmoja kuona nini kipo ndani yake”Aliongea Prince Sebastiani  , lakini moyoni alitamani nyaraka  hio isifunguliwe.

“Rais  Maxim huna haja ya  kumsikiliza , hio ni zawadi aliotuachia  Dokta Tembo  kwanini  turuhusu na mavampire  kuangalia?”

“Mikaeli!!” Sebastiani alisimamama huku akiwa amefura mno, “Unadhani siwezi kukufanya chochote kwasababu tupo hapa?”

“Tatizo nini kwani mkubwa , mbona wasiwasi mwingi , mimi sijali kama  utafanya lolote au utakaa na kutulia”Aliongea Mikaeli  huku  akishikilia mpini wa jambia.

“Nyie wawili , acheni basi hayo mnayofanya kwa ajili ya mimi mzee wenu. Madhabahu ya Nuru  na Giza uwepo wenu  ni muhimu sana  kwa ulimwengu wetu  na hata kwa ulimwengu wote . Kama vita ikitokea  kwasababu ya hii nyaraka ambayo haijulikani kilichopo ndani ni nini , basi sidhani  kuna manufaa ya kuionyesha”

“President , sio kama  ni makusudi , lakini nyaraka hio pia ni muhimu sana kwetu Strigoi  na ni matumaini  yangu leo hii nitajua inahusiana na nini”Aliongea Sebastian.

“Nilijua tokea mwanzo kitu  kisichotarajiwa kitatokea  nikifungua hiki kiboksi , lakini Sebastiani nakuomba kwanza ukae chini. Hapa  yapo mashirika mengi   na wawakilishi wengi  ,  kuhusu  chochote kilichopo ndani ya hii nyraka  tutakiangalia wote na kukaa chini kukijadili na kufikia maamuzi”

Sebastiani alisinyaza macho yake na kuangalia chini na ghaflat tu aliinua mkono juu  na mwanga wa rangi nyekundu kama damu ulionekana katika  ncha za vidole vyake , mwanga ule uliambatana na  herufi za  michoro  kama runes hivi.

Ghafla  tu  vidole vile vilifyatua  ule mwanga wa damu  na kutengeneza kitu kama chupa  la rangi nyekundu  ambalo lilipaa angani na kutoka nje  kabisa ya  uwazi wa uwanja na kupasuka  na kusambaza   rangi za herufi angani.

“Sebastiani unafanya nini, ndio unatuma ishara kuwaita wenzako?”Aliuliza Mika.

“Kipi cha kushangaza , mimi pekee ndio  strigoi hapa  , sidhani kama  ni ajabu kuita  watu  wa jamii yangu pia, au  ni kosa?”

“Mh! Bado hata hajasoma nyaraka inasema nini , lakini ushaanza kuogopa vyote hivyo. Inaonekana ulichoweza ni kuishi miaka minigi tu lakini  ujasiri wa kupambana  mwenyewe  huna” Mikaeli alikejeli.

Ilikuwa ni wazi kwamba  Sebastiani alikuwa kama  mwakilishi  wa viumbe vyote vya giza  na kama kweli  binadamu wamepata dawa ya kuzuia kifo, maana yake  wataweka uhai wao rehani  na sio kwao wanywa damu pekee, bali mpaka kwa viumbe wengine wote wasionekana.

Baada  ya  kuona namna ambavyo   watu hao wawili walivyochemka , magwiji wengine waliishia kubakia kimya , wakionyesha nia za kutokuingilia.

Maxim  alijikuta akijutia kufungua kisanduku hicho , hata hivyo aliona kama asipokifungua siku hivo , basi angejiingiza katika matatizo  ya  kisanduku hicho kuibiwa  kwa nguvu na pengine hata kuuliwa.

“Jamani , Muda huu nitawaita  wanasayansi wetu wawakilishi kwa ajili ya kuangalia hii nyaraka inahusiana  na nini  na kisha tatawasikiliza  kile watakachotuambia . Lazima  tuweke misingi ya  amani  hapa”Aliongea Maxim.

Ile anamaliza sentesi yake , sauti za  vilio zilianza kusikika kutoka nje  na ghafla tu vilio hivyo vilipotea.

Malaika wa  nuru ,Mikaeli  ndie wa kwanza kushituka , huku akikunja sura  na kuonyesha mshangao.

“Nahisi nguvu kubwa ya roho ya umauti”

Kauli yake ilifanya magwiji wengine wote kusimama  na kuangaza kila  kona.

Muda ule  kundi kubwa la  viumbe wafu  ,  lilionekana likilazimisha kuingia ndani ya ukumbi huo. Viumbe hao walikuwa   wakishambulia kila kilichokuwa mbele yao na kuua.

Walinzi  na baadhi ya washiriki wenye uwezo mkubwa , walianza kupambana na maskeletoni yale , lakini  ilikuwa ngumu kutokana na kwamba  mengi yalikuwa na siraha aina ya mikuki mkononi , ilikuwa ngumu pia kuwaua  na risasi kutokana na kukosa nyama, hivyo ilihitajika mapigano ya ana kwa ana na kufanya hali kuzidi kuwa ngumu.

Ghafla tu uwanja uliokuwa na ukubwa wa kutosha watu wengi uligeuka na kuwa chumba  kisicho na nafasi, na msisimko wa kifo  kila mtu dhaifu kiroho ulimwingia na nafsi kuanza kufurukuta  na akili yake kuibiwa palepale na hata wengine  kupoteza maisha kabla ya kuguswa.

“Nini kinaendelea , hawa  viumbe wa wito wa kifo wametokea  wapi?” Aliongea Oleg  na  haraka sana aligeukasna kumuangalia Mr Skeletoni

“Skeletoni , wewe ndio umewaita?”

“Captain , Skeletoni alikuwa na sisi muda wote , anawezaje kuwaita?”Aliuliza Silvia.

Skeletoni hakuongea chochote , alikuwa amesimama tu kama sananu.

“Sebastian , itakuwa ni wewe? Mbona mshenzi sana , yaani unatumia wafu kushambulia watu?”Aliongea Mikaeli huku akimnyooshea Sebastiani mkuki wake.

“Nadhani utakuwa na matatizo kwenye akili yako wewe , nimetuma ishara kuita watu wangu na  hawajafika bado. Isitoshe  sisi ni wa damu  safi , hatuwezi kutumia mbinu chafu kama hii  ya kichawi”

“Mhmh! Nyie ndio  wamiliki wakubwa wa  jamii ya wachawi duniani . Kama wewe hutumii uchawi haimanishi wenzako nao hawatumii”Aliongea Mikaeli.

Nyakasura mara baada ya kuona wawili hao wanagombana bila ya kufanya chochote alionekana kuchukia.

“Mnachukiza kweli! Tumalizaneni na hii dharula  kwanza  na ndio mwendeleze  ugomvi wenu kama mnataka”

“Nyakasura yupo sahihi . Tunapaswa kwenda kuua hawa  misukule  kwanza”Aliongea Silvia.

“My fellow countrymen! Tafadhari naombeni msipaniki , tuna  magwiji wataalamu hapa  , tutafanya kazi pamoja kumzima adui yetu”Aliongea  Maxim.

Kabla hata sauti yake haijapotea angani ,  Nyakasura alishachukua hatua  na moto wake wa dhahabu  kwenda kuyaadhibu yale  maskeletoni.

“Haha…  hayawi   hayawi sasa   yametokea yakukutokea , hebu na tufanye jambo  na tusimuache huyu binti kujichosha mwenyewe”Aliongea Oleg na kujivingirisha kama jiwe kutoka jukwaani na kudondokea chini kama furushi.

Haraka sana  Silvia na  moto wake wa nuru alipaa  kushuka jukwaani , Saint Auland  na  Huge  wote waliungana na  watu wao  kusambaa kila kona na  kutoa msaada.

Mikaeli na Sebastiani , waliishia kuangaliana kwa muda na  wakaacha kupigana na kuungana na wengine.

Mara baada ya magwiji wote kushuka jukwaani kwa ajili ya kutoa msaada , Mr Skelletoni ambae amevalia kofia  alitembea  kuelekea  njia ya kutokea. Watu mara baada ya kumuona akielekea uelekeo huo walijua anaenda kutoa msaada , hivyo hakuna aliemtilia shaka.

Watu wa Inferno ,  mara baada ya kuona jambo hilo , walipatwa na wasiwasi moyoni.

“Kuna mtu anapanga  kuiba  urithi alioacha  Dokta Tembo?”Aliongea Berly.

“Nyie mpaka sasa hamuoni ajabu , kwanini bosi na Black Fog hawajarudi?”Aliongea Mameni.

“Bosi wetu atakuwa sawa  , huu ni muda wa kuweka nguvu zetu kumlinda shemeji yetu asipatwe na shida yoyote  na kumuondoa  hili eneo”Aliongea Azzle.

Previoua Next