Reader Settings

Ulinzi kwa malkia.

Regina  uso wake wa kirembo ulifubaa. Hakuwahi  kuona  uvamizi  wa viumbe wa ajabu wa aina hio. Alishawahi kuangalia filamu za mazombi, lakini muda huo kiila kitu kilikuwa ni uhalisia.

“Hamza! Kwanini hajarudi mpaka sasa hivi, yupo sawa?”Aliuliza Regina akimwangalia Asmuntis kwa wasiwasi.                             

Moyo wake ulikuwa ukienda  mbio mno , alikuwa na wasiwasi  Hamza atakuwa kwenye matatizo.

“Shemeji wewe muamini  tu bosi wetu . Uwezo wake  sio wa kutilia shaka. Kwa sasa  tutakuchukua kukutoa hapa”

“Barhams , listen! Protect the queen”Aliongea Azzle akiwaamrisha wanajeshi wake kumlinda malkia Regina.

Asmuntis na yeye alitoa maagizo  kwa maninja wake kuua kila  kiumbe kitakachomsogelea  Malkia.

Ilikuwa ni mara ya kwanza  kwa Regina kuwasikia wakimuita Malkia, yaani mke wa mfalme wa kuzimu.Lakini hata hivyo hakuwa  na muda wa kufurahi wala kuona haya , kwasababu muda huo akili yake ilikuwa  katika hali ya kupaniki. Alikuwa na wasiwasi zaidi juu ya usalama wa Hamza na nini kilichomtokea.

*****

Ukweli ni kwamba Hamza alikwisha kujua  yale maskeletoni yalishafika  muda mrefu. Vita yake na Mr Skelidoni ilichukua zaidi ya dakika kumi.

Kutokana  na ukali wa vita yenyewe , nguvu  kubwa zilikuwa zikitumika kila  dakika inapopotea.

Hamza aliweza kuhisi kabisa , mbinu ya mgawanyiko ilikuwa ikinyonya sana nguvu yake ya mwili  na  spidi yake  kidogo ilianza  kushindwa  kuendana na  uhiari wa  fahamu zake.

Skelidoni nguvu  zake za kiroho zilikuwa zimeshuka  kwa kiasi  na  uwezo wake wa kudhibiti wafu  ulishuka  pia.

Hamza alichokifanya ni kutegemea  mbinu yake ya mgawanyiko , kudhibiti  uchawi  wa kifo ambao  Skelidoni anamtupia , lakini baada ya muda  alianza kuathirika.

Ilikuwa ni kwa bahati nzuri Skellidoni na yeye nguvu zilikuwa zikimwishia. Mara baada ya kutoa mikondo kadhaa ya   roho ya umauti , alijipeperusha angani  kusogelea eneo la makaburi  katikati.

“Lucifer , kama unataka kuendeleza hili pambano na mimi njoo hapa kwenye makaburi”

Hamza hakuwa mjinga , alijua bwana huyo kukaa juu ya makaburi  ni kwa ajili ya kutaka kunyonya  nguvu  kutoka kwa  wafu  ili kurudisha zile alizokwisha  poteza.

Lakini Hamza hakua na mpango wa kuendeleza  pambano ,  mpango wake tokea mwanzo haukuwa kumshinda Skelidoni bali ni kuondoka  katika hilo eneo.

“Tuondoke”

Aliongea Hamza mara baada ya kuona  Skellidoni hana nguavu za kutosha za kumzuia haraka sana alimshika  Black Fog na kuondoka  nae kwa kukimbia.

Licha ya gari waliokuja nayo kuharibika , lakini miguu yao haikuwa  slow kwenye kukimbia. Black Fog  alijua  wanapaswa kuwahi , hivyo alijitahidi kuendana na spidi ya Hamza na  kukimbia kwa   kasi.

Mara baada ya kuona  wanakimbia , Skellidoni aliekuwa akiogelea katika  nishati ya umauti alitoa cheko kubwa.

Black Foig mara baada ya kumwangalia Hamza , aligundua alisharudi katika mwonekano wake   baada ya kuacha kutumia  mbinu ya Mgawanyiko , lakini  alikuwa akitokwa na jasho mno  na kuhema kwa nguvu.

“Bro upo sawa? Unaonekana kuchoka sana” Aliuliza Black Fog  akiwa na wasiwasi.

“Usiwe na wasiwasi , tuharakishe tu kurudi”Aliongea Hamza , ukweli ni kwamba  hio ni mara yake ya kwanza kutumia mbinu ya  Mgawanyiko kwa muda mrefu  na aliweza kuhisi  uhatari  wake.

Unachopaswa kujua ni kwamba nguvu za kimwili za Hamza hazikuwa za kawaida kabisa. Hamza alijihisi katika  historia ya binadamu pengine hakuna binadamu ambae ana mwili  wenye nguvu kama zake.

Lakini kutumia tu mbinu ya Mgawanyiko , ilimchukua dakika kumi tu kuchoka mno  kama vile amefanya kazi ngumu kwa  muda mrefu sana.  Kama isingekuwa   wasiwasi wake juu ya  Regina  na washikaji zake. Angekaa chini na kulala kidogo.

Alishindwa kuelewa  juu ya mtu ambae alitengeneza mbinu ile , alijiuliza  kama mbinu yenyewe inanyonya nguvu ya mwili kiasi hicho , malengo yake ilikuwa ni nini? Au ilitengenezwa kwa ajili ya binadamu wa tofauti na yeye.

Hamza alikuwa na wasiwasi , licha ya kwamba alikuwa akikimbia kurudi  ukumbini lakini  alihofia kama itatokea hali ya kumtaka kutumia nguvu zaidi , je ataweza? Kwa sababu muda huo  alijihisi kuchoka mno.

Lakini kwa hali yoyote ile , Hamza aling’ata meno yake  na kuvumilia  na  waliendelea kuzichanja  mbunga kupita katikati ya msitu  mpaka walipokuja kuona mwanga mbele yao.

*****

Ukumbi wa Baraza la maksi uligeuka na kuwa  kuzimu . Njia zote za kuingilia  zilikuwa zimezibwa na  nguvu kubwa ya umauti  na  maiti za wanajeshi. Ilishindikana kwao kutoka ndani ya eneo hilo baada ya kuumizwa.

Maiti na Maskeletoni ambayo yalikuwa  chini ya utawala  wa kimashambulizi , haikuwa suala tu la kuwashambulia  watu , bali walikuwa pia wamebeba virusi  ambavyo vilikuwa vikisambaa kwa kasi hewani.

Kila ambae alihema  na kuvuta virusi hivyo,  hata wale wazima walibadilishwa  akili zao na kuanza  kushambulia wenzao.

Kwa hali ya kusikitisha ndani ya muda mfupi tu  asilimia kubwa ya  watu wote waliokuwa ndani ya uwanja huo , walishaambukizwa na virusi  na  wengi zaidi waliendelea kuathirika.

Wanajeshi  wakubwa wa ulimwengu wa giza, macho yao yalikuwa yamebadilika rangi. Wengi wao walibadilika na kuanza kung’atana.

Kadri watu walivyozidi  kudondoka chini na kupoteza uhai , eneo hilo liligeuka  mto wa damu.

Moto mkali ulikuwa ukiunguza makundi kwa makudi ya wale  ambao wamekwisha kuambukizwa na kupandwa na wazimu.

Nyakasura  mwili wake wote ulitoa mng’ao wa miale  ya moto , licha ya eneo hilo kuwa na sumu nyingi  na  maambbukizi ya virusi , hakuathirika hata kidogo.

Watu wengi mara baada ya  kuona  moto wa Nyakasura ulikuwa na ufanisi mno kwenye kuwadhibiti  misukule hao,  wale waliokuwa hawajaambukizwa walimsogelea na kumuomba awalinde

“Nyie hebu nipisheni , mnanizuia njia nitaendelea kuwaunguza vipi?”

Yeye peke yake aliweza kuunguza zaidi ya mamia ya maskeletoni  na maiti  lakini kwasababu   mengi yalikuwa yamesambaa kila kona pamoja na  uwepo wa watu wengi , alishindwa  kuyaunguza kwa  haraka.

“Nyakasura , tukiendelea hivi hatuwezi kufanikiwa , tunapaswa kutengeneza njia  watu wakimbie na  ndio namna tunaweza kutumia uwezo wetu wote kuwadhibiti”Aliongea Huge.

“Unadhani sijafikiria hivyo? Unaona kabisa kila njia  za kutokea zimejazana  misukule  na maiti zenye maambukizi , watu  waliopo hapa hawana mafunzo  yoyote , watarukaje  kutoka nje?”

“Kama hakuna jia nzuri , tunaweza kuitengeneza”Aliongea Huge  huku akigeuza uso wake na kumwangalia  Mr Air kwa mbali , ambae alikuwa bize  kuyeyusha maskeletoni.

“Mr Air , unaonaje wewe na  Captain mkisaidiana? Ili mradi tukiweza kutengeneza njia ya watu kukimbilia , tutapunguza wingi wa vifo”

Oleg ambae alikuwa katikati  ya  kazi ya kupasua  maskeletoni  na ngumi na mateke,  mara baada ya kusikia hivyo , alicheka kwa nguvu.

“Kweli wewe ni msomi , akili yako imewaza vyema”

Mr Air na yeye aligeuka  na kumwangalia  Huge  na kisha alitingisha kichwa kumuelewa. Palepale alielea juu angani  na kusambaza mikono yake. Wimbi  kubwa la mkondo wa upepo  lilijitengeneza katika uelekeo mlalo  na kuwa  kama kimbunga.

Upepo ule haukumuumiza mtu , bali ulisafisha njia eneo la katikati, wakati huo  huo  Mr Air aliita elementi za unyevunyevu wa maji  kutoka pande zote na kuzielekezea katika eneo la  katikati.

Ghafla tu  eneo la kati lilifunikwa na maji ambayo ni kama vile hayakuwa yakiathiriwa na  kani mvutano kwa namna yalivyokuwa yakielea

Oleg mara baada ya kuona  maji yale macho yake yalichanua kwa furaha .

“Maji haya yananitosha kabisa , kupambana  nchi kavu bila maji kunachosha mno”

Mara baada ya kuongea hivyo palepale  alichomoa upanga uliokuwa kwenye kiuno chake.

Upanga ule  mara baada ya kuhisi uwepo wa maji  uling’aa.  Ulikuwa ni kama kioo , chenye kutoa mwanga wa kufurahisha macho. Ilikuwa  ni kama Dhana  tofauti na siraha ya kiuungu ambayo inaweza kusabaisha  watu nywele zao kusisimka.

“Upanga mzuri sana!”

“Inasemekana  katika historia ya urithi wa  ukoo wa Viking , upanga ule unaweza kutumiwa na  mbarikiwa wa  bahari pekee “

Watu  walishindwa kuzuia mshangao wao , mara baada ya kuona Capteni Oleg  hatimae ametoa siraha yake  ya uwakilishi.

Oleg alisimama wima na kuondoa ule upanga wake mbali na maji yale yaliokuwa yakielea  na kitendo kile  kilifanya yale maji kusogelea ule upanga kwa kasi  kwa namna  ya kuvutwa kama sumaku.

Muda huo  , Oleg alionekana kuwa wa  kawaida tu . Alikuwa amesimama  kama mwanajeshi ambae anajivunia kile anachofanya huku nywele zake na misharubu ikipeperushwa  na upepo.

Ghafla tu upanga ule uliacha kuvuta yale maji na badala yake  yalimvaa Oleg  na kuanza kumzunguka kwa spidi , kama vile kuna kitu kimeyashikilia.

Mr Air kuona vile aliondoa utawala wake katika maji yale  na   sasa yakawa chini ya Oleg.

Oleg alipiga makelele  kwa namna ya kunguruma na palepale upanga wake aliouelekezea angani ulianza  kurefuka urefu  wake  huku yale maji  yaliokuwa yakimzunguka yakipotea taratibu , ilionekana kama vile  yale maji ndio yanayoongeza upanga ule urefu kwenda hewani.

Ndani ya dakika chache tu  upanga mkubwa wa mita  kadhaa ulionekana,huku ukisambaza  msisimko  na nguvu isiokuwa ya kawaida.

“Ghadhabu ya  mungu wa habari!!”

Baada ya kuongea vile , Oleg aliupigiza chini ule upanga , upanga ule ulikuwa ni kama Nyangumi iliokuwa ikidondoka  na kwenda kukandamiza   vitu vilivyokuwa chini yake na kutengeneza nafasi.

Nishati iliotoka katika siraha ile na maji yalioruka   ilisababisha  uwanja wote kutingishika.

‘Boom!”

Majukwaa ya uwanja yalionekana kushindwa kuhimili  nguvu ile ya mkandamizo  na kutoboka  eneo la katikati na shimo kama  njia lilionekana.

Watu wengi walioshuhudia tukio lile walijikuta wakitetemeka. Ndio sasa waliweza kuamini  juu ya  nguvuya Sea God Blade. Mwanzoni  watu  waliposikia Oleg kumiliki upanga unaotengenisha meli , waliamini ni upanga wa chuma , lakini  muda huo walichoweza kushuhudia ilikuwa tofauti , ulikuwa ni upanga unaoongezeka ukubwa kulingana na  uwepo wa maji.

Mara baada ya  shimo kubwa kuonekana , lenye kuruhusu watu wengi kupita. Rais  Maxim  haraka sana aliamrisha.

“Ondokeni kila mmoja . Liacheni hili eneo kwa ajili ya magwiji kupambana”

Ukweli ni kwamba watu wengi walishajua  uwepo wao ulikuwa ukiwapa shida Magwiji kuonyesha uwezo wao wote. Kama isingekuwa uwepo wa watu maskeletoni hayo yasingechukua muda kudhibitiwa.

Hivyo kila mtu hakutaka kuwa mzigo ndani ya eneo hilo na kukimbia kadri awezavyo kujiokoa.

Ndani ya muda mfupi tu , watu  ambao walikuwa na uwezo wa kukimbia waliweza kutoka  kupitia shimo.

Muda mfupi tu watu ndani ya  ukumbi huo walipungua kwa kiasi kikubwa. Nyakasura  na magwiji wengine  hawakuwa na kizuizi tena cha kupigana.

Maskeletioni baadhi yaliotaka kufuata shimo , waliunguzwa na moto wa Nyakasura  na mwanga wa  nuru wa Mikaeli.

Ndani ya dakika chache tu  Nyakasura na  Mikaeli waliweza kudhibiti hali  kwa asilimia kubwa.

Mara baada ya kuona hali imeweza kudhibitiwa , Maxim  na   viongozi wengine wajuu walijikuta wakipumua kwa ahueni.

“Rais , tunapaswa kuondoka hili eneo  haraka iwezekanavyo , kama  kutakuwa na mlipuko , sumu yake itatuathiri vibaya” Kiongozi mmoja aliongea.

Maxim aliishia kutingisha kichwa na muda huo  ile anataka kutembea aliweza kumuona mtu  alievalia  joho la rangi nyeusi akimsogelea

“Skellidon?!”

Maxim na wengine walionekana kushangaa .  ukweli ni kwamba walijua  Skellidoni  kwa uwezo wake   angeweza  kushuhugulikia hilo suala kwa ufanisi mkubwa. Kuongea na wafu  ilikuwa ni  taaluma yake.

Lakini sasa  tokea kuanza kwa  tukio hilo , Skellidon alionekana kuwa  kimya tu , jambo ambalo lilimshangaza Maxim na wengine.

Muda ule Maxun  mara baada ya kuhisi kitu kisichokuwa kawaida , ghafla tu aliweza kuona  moshi  wa ajabu ukimtoka  katika vazi lake lile  na kusambaa.

“Nini  hiki?”

“Msivute! Ah!”

Viongozi hao hawakutegemea kama Skellidoni angewaambukiza. Ingawa baadhi yao walikuwa wana mafunzoya nishati za mbingu na ardhi lakini  hawakuwa na kinga zidi ya sumu.

Dakika ambayo Maxim alishtuka , alitoa sauti kali  na kuanza kumshambulia Skellidon . Lakini hata hivyo Skellidoni alionekana kutoathiriwa na sauti yake  na kuendelea kusambaza  sumu ya  umauti.

Maxim , alikuwa  ni mzee  , hakuwa kijana . Sauti yake  pia  ilikuwa imepungua makali yake  na mwili umezeeka.

Mara baada ya kuvuta moshi  mwingi wa  Sumu ya  umauti , sura yake  ilibadilika na kugeuka nyeusi   na alianza kukohoa mfululizo huku akitema damu .muonekano  wake ulijawa na   kutokukubali  na maumivu aliosikia yalimzidia na kudondoka chini.

“Rais !”

Kundi la watu wa Set , mara baada ya kuona tukio hilo walipiga makelele kwa mshangao. Hakuna hata mmoja  alieamini kwamba moja ya magwiji kumi, Mr Skellidon, angemuua Rais Maxim waziwazi.

Unachopaswa kujua ni kwamba Set organisation ilikuwa chini ya ulinzi wa  mataifa mengi makubwa duniani . Kumuua kiongozi wake maana yake ni kujitengenezea uadui na  mataifa hayo na sio hivyo tu  kumuua pia ilikuwa ni kukiuka sheria za ulimwengu wa giza maana yake  utapambana na kila mmoja wa ulimwengu huo.

Magwiji wengine hawakutegemea jambo hilo lingetokea . Walikuwa bize kupambana  na  maskeletoni, maiti  pamoja na watu walioambukizwa , lakini  nani angegundua Maxim ndio alikuwa  shabaha  na maskeletoni walikuwa  chambo.

“Pisheni njia!”

Ghafla tu   mwanga wa rangi nyeupe  ulishika kutoka juu , Silvia ambae alikuwa amevalia  gauni lake la rangi nyeupe  alionekana kama malaika  wakati akishuka na kwenda kutua   karibu ya   maiti ya Rais Maxim  akiwa na macho yaliojaa ukauzu.

“Skeletoni pokea adhabu takatifu! Adhabu ya  nuru ya  mungu”

Silvia alifungua  kiganja cha mkono wake  na mpira wa nuru  ulijitengeneza, ulikuwa ni kama  jua  na kuangaza  eneo hilo  wakati huo wa usiku.

Kila mmoja aliebakia eneo la tukio , aliishia kuangalia namna  ambavyo mwanga ule  uligeuka   boriti kama mshale  na  kutupiwa Skeletoni  na kumuunguza.

Msisimko wa   nguvu ya umauti uliokuwa ukimtoka Skellidon ulipotea, mwili wake  ulitingishika kidogo tu na sekunde kumi na tano mbele , mwili wote uliyeyukia hewani  kama  ukungu mweusi . Kitu pekee kilichobakia lilikuwa ni vazi lake la joho jeusi  pekee  na baadhi ya mifupa aliokuwa ameiniing’iniza.

Watu kuona shambulizi lile walionekana kushangazwa na uwezo wa  Silvia, lakini kuna wengine walijawa na shaka.

“Mbona kama naona sio kawaida,  yaani  Gwiji aina ya Skelidoni ameuliwa na shambulizi moja tu?”

Watu  wachache waliokuwepo walibung’aa  mara baada ya kuona  Skelidoni hayupo tena.

Ingawa ni kweli  ufunuo wa nuru  , mbinu anayotumia  Malkia mweupe ilikuwa  na nguvu juu ya aina nyingi za uchawi , lakini watu walishindwa kuelewa imekuwaje  mtaalamu wa juu mwenye cheo cha ugwiji  kuuliwa na shambulizi moja tu.

Magwiji walioshuhudia suala hilo , walionyesha hali ya  kutokuamini pia , walikuwa na shaka  kwenye nyuso zao  kuona ghafla tu  Skelidoni ameuliwa. Hata hivyo hakuna hata mmoja ambae  alitaka kuongelea suala hilo , kwasababu  baada ya kifo cha Maxim  nyaraka aliokuwa ameshikilia imedondoka chini ardhini.

Sebastiani ndio aliekuwa wa kwanza  , kilikuwa ni kivuli chake tu kilichoonekana kikipotea kuelekea eneo nyaraka ile ilipo kuiokota.

“Tena usijaribu !”

Mikaeli ni kama alikuwa kwenye mawazo ya Sebastiani  kwani aliweza kushituka  mapema sana  na  alirusha mkuki wake uliotawaliwa na nguvu ya nuru na kwenda kumkinga Sebastian kwa mbele.

Sebastiani hakuwa na jinsi zaidi ya kusimama , kujiepusha kugusana na nuru ya  mkuki ule.

Muda huo Silvia  ambae alikuwa karibu  na Maxim alichukua nafasi hio  na kuinama chini na kuokota ile nyaraka. Hakuishia kuiokota tu aliinamisha hata kichwa chake kuonyesha ishara ya heshima mbele ya  maiti ya Maxim.

“President, everyone will remember the price you paid for the underground world.”Aliongea Silvia akiwa na  hali ya majonzi usoni.

“Silvia mtawala  wa siku za zama , je bado unapanga kuendelea kushirikiana na  watu wa Madhabahu takatifu?”Aliuliza Sebastiani.

“Prince Sebastian kwanini unaongea hivyo? Tulikuwa  na nguvu kipindi kile  na sikutaka tu  nyaraka hii kuangukia katika mikono ya watu  wabaya. Mpaka sasa hatujajua bado nani  kasababisha haya  mashambulizi , kwanini  tusiwe   makini  kwanza?”

“Mhm! Kwa mtazamo  wangu , wewe White Queen , utakuwa  ndio upo nyuma  ya haya”Aliongea Sebastiani kwa  kejeli.

“Prince , unao ushahidi wa kuongea hayo juu yangu?”

“Your creed of Odd Ones is ’Chos -Forvr’ which  translate chaos will  exist forever. Making this world  fall into  chaos  and war , isn’t  that what you’re after ?”

“Kadri ulimwengu utakavyokuwa   katika machafuko ndio  namna  nyie wote mlivyo na furaha! Kwasasa lazima una furaha baada ya kufa kwa  Rais Maxim  na kuvurugika kwa ulimwengu wote wa giza. Nyie ni tofauti na sisi , ukituongelea sisi tunaishi chini ya sheria ya ‘ Avoiding the world’  kwa zaidi ya miaka elfu moja sasa. Sisi ndio kabila la watu wenye amani  duniani hapa ,  tofauti na  wewe White Queen , kushika hio nyaraka  ya  dawa ya kifo   ni hatari zaidi , hivyo   unaonaje ukinipatia mimi?”

“Kwanza kabisa, licha ya kwamba ni kweli sisi  The Odd ones  tunaamini ukweli wa Chaos , hio ni imani yetu tu pekee . Hatujawahi kuwa na mawazo ya kuiharibu dunia. Pili , sina mpango wa kuishikilia hii nyaraka mimi mwenyewe , tusubiri mpaka hili janga lipite na kisha tutakusanyika pamoja  na kuingalia na kujadiliana namna ya kudili nayo. Si ndio vizuri zaidi kuliko mtu mmoja kuishikilia?”

“Sylvie, you don't need to speak nonsense with these heretics. If you are not of my race, your heart will definitely be different.” Aliongea Mikaeli akimaanisha kwamba Silvia aache kuongea na huyo  mzushi , akiongezea kwa kusema kama sio wa kabila lao basi mioyo yao itakuwa tofauti siku zote.

Wakati huo  wakati wakiendelea  kuongea , Nyakasura alisogea karibu yao na kuwaangalia kwa chuki.

“Hivi nyie! Huu ni muda wa kuendelea kujadiliana kuhusu hio nyaraka? Hebu angalieni kuna maelfu ya watu  wameathirika , ni kipi tunapaswa kufanya?”

Nyakasura alikuwa amechukia mno  kwa namna   watu wengi wasiokuwa na hatia walivyoambikizwa.  Aliona sio vyema kuwaua wote kwa moto.

Viongozi muda huo  ndio sasa waligundua , ijapokuwa viumbe hao wa kutisha  wamekwisha kumalizika , lakini kulikuwa na watu wengi ndani ya tukio ambalo walikuwa na majeraha na kuambukizwa na virusi.

“Jamani   haina haja ya kupaniki , pengine  ufunuo wangu wa uponyaji unaweza  kuondoa sumu  ndani ya miili yao. Nisaidieni kuwakusanya  wote walioumia sehemu moja”

“Kweli  kabisa , nguvu ya uponyaji  ya  Malkia wa nuru  ina uwezo wa kuondoa  nguvu za kichawi”

Viongozi wa  baraza hilo haraka sana waliondoka kwa ajili ya kuweka utaratibu kwa majeruhi kupelekwa katika eneo moja ili kutibiwa.

Silvia aliishia tu kumwangalia  Sebastiani  na macho yaliojaa  ukauzu na kisha akashusha pumzi zake.

“Prince ,  kama hakuna kingine  nadhani tutamalizia  baada ya kutibia majeruhi . Sidhani kuna  kitu muhimu zaidi ya kuokoa uhai wa mtu , au unasemaje?”.

Watu wengi waliosikia  maneno ya Silvia walitingisha vichwa kwa kuona ameongea kwa busara sana. Sebastiani upande wake aliishia kutoa  mguno  tu na kisha akaondoka.

***

Nje ya ukumbi  watu wa Inferno walifanikisha kumtoa Regina nje akiwa salama salimini . Hata hivyo   baadhi ya masenari  walikuwa pia wameambukizwa na moshi wa kifo  na  waliishia kudondoka chini  kwa maumivu.

Wakati kila mmoja akiwaza nini  hatua ya kuchukua , ndio muda ambao Hamza na Black Fog waliweza kufika.

“Bosi! Hatimae umerudi”Aliongea  Mameni.

Hamza aliishia kuangalia  hali ilivyo mbaya katika eneo hilo  pamoja na shimo ambalo limetengezwa kutokea  nje  ya uwanja, aliishia tu kukunja sura kwa jinsi watu walivyokuwa wakiugulia maumivu  , huku wengine wakionyesha ishara za kupandwa na wazimu.

“Wife , unaendeleaje?”

Mara baada ya kuona Hamza amerudi salama , Regina alishikwa na hali ya ahueni  na kutingisha kichwa chake.

“Nipo sawa . Shukrani kwa kila mmoja  hapa  nimekuwa salama , ni kwamba tu baadhi ya watu wameingiwa na sumu”Aliongea Regina na Hamza alitingisha kichwa na kugeuza kichwa chake.

“Wameambukiwa na sumu ya  umauti , wanapaswa kutibiwa haraka iwezekanavyo”

“Inaonekana Silvia  anapanga kuwatibu  watu wote walioambukizwa , anataka tuwakusanye watu wote katika eneo moja”Aliongea Azzle.

“Sawa,  ufunuo wake wa uponyaji  utakuwa na nguvu ya  kutosha”

Mara baada ya  masenari kuchukuliwa , hatimae watu walipata muda wakuongelea kile kilichotokea.

“Bosi , ulikuwa umeenda wapi? Suala kubwa limetokea hapa , kulikuwa na kundi kubwa la..”

“Najua” Hamza aliingilia  na kisha akaendelea, “Nilizuiwa na Skellidoni ndio maana nilishindwa kurudi kwa wakati . Najua ameita kundi kubwa la   wafu , lakini kwa bahati mbaya  hakukuwa na mtandao”

Mara baada ya kila mmoja kusikia hivyo , walijikuta wakishangaa  na kuona ni ajabu.

“Bosi Skeletoni  ameuliwa  na Silvia muda si mrefu”

“Nini!”

“Haiwezekani , Master  huyo aliekufa ni feki , ni skeletoni lililokuwa  chini ya  akili za Skelidoni’Aliongea Black Fog.

Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa baada ya taarifa kutoka pande zote kukinzana.

Hamza aliona suala hilo lilikuwa na ukakasi , hivyo aliamua kusikiliza kile kilichotokea wakati  akiwa hayupo.

Mara baada ya kusikia  kwamba Skelidoni amemuua  Rais Maxim na pia yeye kuuliwa na shambulizi moja na Silvia , alijua fika  huyo ni feki. Hio ni kwasababu Hamza alishaona uwezo halisi wa Skellidon  na kwa namna yoyote ile hawezi kufa kwa shambulizi moja la Silvia  kirahisi.

“Bosi kwahio  kwa maelezo yako unamaanisha ulikuwa ni mtego wa Skellidon na bado yupo hai?”Aliuliza Asmuntis.

“Nina uhakika hajafa ,  lazima sasa hivi atakuwa amejificha”

“Lakini  bosi tatizo ni kwamba  kama unasema  hajafa  na  asipojitokeza , hata uwaambie watu yupo hai , hakuna atakae kuamini”Aliongea Berly.

“Shenzi! Kwanini bosi adanganye? Kwa  ukubwa wa cheo chake  anawezaje kufanya hivyo?”Aliongea  Leviathan.

“Sisi tunaweza kumuamini bosi kwa asilimia mia moja , lakini wengine  sidhani . Isitoshe  kipindi cha vita takatifu tulishirikiana  na   Madhabahu ya Giza. Awamu hii alichofanya  Prince Sebastiani kimefanya watu  kumhisia  kama mhusika  na moja kwa moja lazima  tuunganishwe”Aliongea Azzle.

Hamza alihisi kichwa chake kuanza kumuuma . Alijua kile kilichotokea ni mpango wa Skellidon lakini hakuwa na namna ya  kutoa ushahidi. Na kuhusu Ankh hakuwa na uhakika kama ilikuwa kweli kwasababu  hakuweza kujua ni sababu gani  Dokta Genesha aliamua kuhifadhi kiboksi hicho ndani ya Baraza la maksi.

Haijalishi  Dokta  Tembo alimdanganya  au kulikuwa na sababu nyingine, Hamza hakuweza kupata  kuelewa.Muda huo akiwaza aliwez k usikia sauti ikimwita kutoka nyuma.

“Hey, Ulikuwa umeenda wapi wewe?”

 

Previoua Next