Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

SIMULIZI:THE REVENGE OF DERICK 

MTUNZI:WIZZY JOOH 

FACEBOOK:STORY ZA JAY 

 

****SEHEMU YA PILI(2)****

 

ILIPOISHIA 

Mpambano ukaanza huku Derrick akionyesha uwezo mkubwa sana wa kupambana japokuwa Inspector mbogo alijitahidi kumdhibiti Derrick Derrick lakini akajikuta akishindwa kwani Derrick alikua akirusha mateke na ngumi kwa ustadi wa hali ya juu mapigo hayo ya Derrick yakamfanya Inspector mbogo akubari kushindwa na kumfanya Derrick acheke sana kwani baba yake mdogo ajafanikiwa kumgusa na ngumi hata moja

 

SONGA NAYO 

Derrick akampa mkono baba yake mdogo na kumnyanyua chini alipokua ameangukia baada ya kupigwa teke na Derrick 

 

"Wewe mtoto mbona una hatari hivi" aliongea Inspector mbogo huku akimtazama Derrick anayetabasamu tu

 

"Hatari gani mzee" aliuliza Derrick huku akichukua kitaulo kidogo na kujifuta jasho usoni mwake 

 

"Dogo unajua kupigana sana hata mimi siingii ndani" alijibu Inspector mbogo huku akionekana kuukubali uwezo wa Derrick 

 

"Hahaha hamna bwana bamdogo mbona uwezo wangu ni wa kawaida tu" aliongea Derrick huku akiwa anacheka 

 

"Aya bhana ngoja me nikajiandae niende kazini" aliongea Inspector mbogo na akatoka ndani ya chumba hicho cha mazoezi 

 

"Inabidi nianze kufanya uchunguzi wa chinichini ili niweze kumtambua muhusika wa mauaji ya wazazi wangu na mdogo wangu" Derrick aliongea kwa sauti ndogo huku na yeye akitoka ndani ya gym hiyo na kuelekea chumbani kwake

 

⭐⭐⭐⭐

 

Inspector mbogo alimaliza kujiandaa na akanywa chai aliyoandaliwa na mke wake kisha akaondoka nyumbani kwake na kuelekea kazini kwake

 

Alifika kazini kwake na akapaki gari lake eneo la maegesho kisha akaingia ndani ya kituo cha polisi anachofanyia kazi

 

"Mkuu amesema ukifika upitilize hadi ofisini kwake" aliongea askari moja huku akiwa amempigia saluti Inspector mbogo ambaye hakujibu kitu zaidi ya kwenda moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya RPC 

 

Aliingia ndani ya ofisi hiyo kisha akampigia RPC saluti ya kikakamavu huku akiwa amesimama mbele yake

 

"Kaa hapo Inspector" aliongea RPC Nzige huku akimuonesha Inspector mbogo sehemu ya kukaa

 

Inspector akakaa sehemu aliyoambiwa akae na akawa tayari kusikia mkuu wake amemuitia kitu gani 

 

"Inspector nimekuita hapa kuna kitu nataka nikuambie na ninapokuambia hiki kitu usijaribu kukipuuzia kwasababu itakugalimu" aliongea maneno hayo rpc na kumfanya Inspector mbogo astuke kidogo kwani hajamuelewa kabisa RPC ana maana gani kuongea maneno hayo

 

"Mkuu bado sijakuelewa unamaanisha nini" alihoji Inspector mbogo

 

"Ipo ivi kesi ya mauaji ya kaka yako inakubidi uache kuifuatilia yani namaanisha uachane nayo kabisa" aliongea RPC kwa sauti nzito kidogo huku akiwa amemkazia macho Inspector mbogo aliyebaki ameduwaa

 

"Kwa..kwa..Kwa..kwanini mkuu ikiwa hii kesi nilitakiwa niifatilie mimi" alihoji kwa mshangao Inspector mbogo huku akimtazama RPC 

 

"Wewe sasa hivi umebadilishiwa kesi ya kuifatilia kuna genge la wahuni inabidi ukalifatilie na hiyo kesi ya mauaji ya kaka yako itafatiliwa na mtu mwingine umenielewa" aliongea RPC huku akiwa ameyatoa macho yake yanayotisha mithili ya simba aliyekosa kitoweo

 

"Ndio mkuu" aliitikia kwa unyonge Inspector mbogo huku akimtazama RPC huyo

 

"Vizuri! Chukua hili file na ukalisome ili ujue unaanzia wapi kwenye operation ya kuwakamata hawa wauni" aliongea RPC huku akimpa Inspector mbogo file lenye maelezo ya wapi genge hilo la wahuni linapatikana 

 

Inspector mbogo akanyanyuka kwenye kiti alichokalia kisha akampigia tena saluti RPC huyo na akatoka ndani ya ofisi hiyo huku akiwa na hasira kali mno

 

"Bwana mdogo ni Bora ukatekeleza nililokuambia la sivyo maisha yako yatakuwa ni mafupi mno hahahaha" aliongea RPC baada ya Inspector mbogo kutoka ndani ya ofisi hiyo 

 

ITAENDELEA

Previoua Next