SIMULIZI:THE REVENGE OF DERICK
MTUNZI:WIZZY JOOH
FACEBOOK:STORY ZA JAY
****SEHEMU YA TATU(3)****
ILIPOISHIA
"Bwana mdogo ni Bora ukatekeleza nililokuambia la sivyo maisha yako yatakuwa ni mafupi mno hahahaha" aliongea RPC baada ya Inspector mbogo kutoka ndani ya ofisi hiyo
SONGA NAYO
Inspector mbogo akaelekea moja kwa moja kwenye ofisi yake huku akiwa amelishikilia file alilopewa na RPC nzige na uso wake ulikua umekunja ndita zitokanazo na hasira
Alifika kwenye ofisi yake na akakaa kwenye kiti kisha akaliangalia file hilo kisha akalifungua na kuanza kuangalia ndani kuna kumeandikwa nini
"Fuck fuck fuck" alitukana kwa hasira Inspector mbogo baada ya kuona kesi aliyopewa kuifatilia ambayo iliandikwa ndani ya file hilo
"Yani mkuu amenidharau vipi hadi anipe kesi kama hii" alijiuliza mbogo huku akiendelea kuliangalia file hilo
Inspector mbogo alinyanyuka kwa hasira kwenye kiti alichokua amekikalia na akaamua kurudi ofisini kwa RPC ili amuulize ni kwanini amebadilishiwa kesi kubwa na kupewa kesi hiyo ya kulifatilia genge la wahuni wa mtaani
⭐⭐⭐⭐
Derrick anatoka chumbani kwake huku akiwa amependeza mno na anaonekana kuwa kijana mtanashati
"Vipi Derrick unataka kutoka?" Aliuliza mama mdogo wa Derrick anayejulikana kwa jina la Maria
"Ndio mamdogo kuna naelekea ila sitokaa sana" alijibu Derrick huku akimtazama mama yake mdogo
"Aah! Sawa usichelewe kurudi basi" aliongea Maria huku akiwa anamtazama Derrick kwa macho ya utofauti kidogo
"Usijali mama nitakua hapa muda si mrefu" alijibu Derrick huku akitoka ndani ya nyumba hiyo
Alipofika nje akapanda moja ya gari lililokua kwenye eneo la maegesho kisha akaliwasha gari hilo na kuondoka mahali hapo kwa mwendo wa taratibu na alipofika nje akaongeza mwendo wa gari lake na kutokomea kusipojulikana
⭐⭐⭐⭐
Baada ya Derrick kutoka ndani ya nyumba hiyo Maria anaichukua simu yake iliyokua kwenye kochi kisha anaingia upande wa majina na anatafuta jina la mtu aliyemsevu kisu kisha anampigia
"Nisikilize kisu huyu dogo ametoka hapa lakini hajaniambia anaelekea wapi kwahiyo fanya juu chini ujue anaelekea wapi" aliongea haraka haraka Maria huku akionekana yupo serious
"Nitajie namba ya gari aliyoondoka nayo tahadhari" ilisikika sauti nzito upande wa pili wa simu ya Maria
"T 503 DDM gari ni Crown royal" alijibu Maria huku uso wake ukiwa umetawaliwa na tabasamu pana
"Hesabia kazi imeisha vipi unataka tumuue kabisa au" aliuliza jamaa wa upande wa pili wa simu
"Hapana muda wake bado haujafika na hata hivyo nataka baba yake mdogo ndio aanze kisha yeye afuatie" alijibu Maria na jamaa wa upande wa pili wa simu akakubaliana nae kisha akakata simu hiyo na kuangua kicheko kikubwa cha kejeli
ITAENDELEA
Comments