SIMULIZI:THE REVENGE OF DERICK
MTUNZI:WIZZY JOOH
FACEBOOK:STORY ZA JAY
****SEHEMU YA NNE(4)****
ILIPOISHIA
"Hapana muda wake bado haujafika na hata hivyo nataka baba yake mdogo ndio aanze kisha yeye afuatie" alijibu Maria na jamaa wa upande wa pili wa simu akakubaliana nae kisha akakata simu hiyo na kuangua kicheko kikubwa cha kejeli
SONGA MBELE
Derrick alikua ndani ya gari lake akiwa kwenye barabara ya bagamoyo na alikua hana habari kabisa kama mama yake mdogo ametuwatuma watu wamfatilie anapoelekea
Alifika hadi maeneo ya boko chama na hapo akaingia kwenye barabara ya ununio na akaongeza mwendo kasi wa gari yake
Lakini anastukia kuwa kuna gari lina mfatilia kwa nyuma hivyo anaamua apunguze mwendo wa gari yake huku akitaka kuona watu hao ni kina nani na wanalengo lipi?
"Hawa kenge hawanijui vizuri mimi" aliongea Derrick baada ya kuona watu hao wanaomfatilia pia wamepunguza mwendo hivyo anaamua kuongeza speed tena na watu hao nao wakaongeza kasi ya gari yao
"Pumbavu kabisa" aliongea kwa hasira Derrick huku akiligeuza gari lake kwa ustadi mkubwa huku likiwa kwenye kasi yake hiyohiyo na kusababisha rami ichafuliwe na magurudumu ya gari hiyo
"Wait and see the show" aliongea Derrick huku gari yake ikiwa inaangaliana na gari ya watu wanaomfatilia na alikua anawafata kwa mwendo wa kasi huku akiwa hana wasiwasi hata kidogo
Jamaa hao baada ya kuona mtu waliyekuwa wakimfatilia amewageuzia gari na sasa anawafata kwa kasi ya ajabu walijikuta wakipatwa na mshangao mkubwa kwani hawakutegemea kabisa kama mtu huyo atafanya kitu kama hicho
"Mkwepe mkwepee wewe" aliongea moja ya jamaa aliyekuwepo ndani ya gari hiyo na alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana
Dereva aliamua kuingiza gari ndani ya mtaro ili kuepusha ajali iliyokuwa inakwenda kutokea mbele yao
Derrick akafunga breki za gari yake kisha akatoa kichwa kwenye dirisha na kuiangalia gari hiyo iliyoingia mtaroni kisha akatabasamu kwa dharau na akaligeuza gari lake na kuendelea na safari yake ya kwenda ununio
⭐⭐⭐⭐
Inspector mbogo aliingia kwenye ofisi ya RPC na akamkuta anamalizia kuongea na simu
"Vipi una shida gani Inspector" RPC Nzige aliuliza huku akimtazama Inspector mbogo aliyesimama mbele yake
"Mkuu bila kukuvunjia heshima naomba kukuambia kwamba hii kazi uliyonipatia sitoifanya" Inspector mbogo aliongea kwa ujasiri mkubwa huku akiwa amekunja uso wake kwa hasira
"Unasemaaa! embu rudia ulichokisema sijakusikia vizuri" alihamaki RPC huku akisimama kwenye kiti chake
"Nimesema hivi hiyo kazi uliyonipatia sitaifanyaaa" mbogo aliyarudia tena maneno yake huku akimkazia macho rpc
"Naona unajiamini sana mbogo na sijui ni kwanini unajiamini kiasi hiko" aliongea RPC huku akimsogelea Inspector mbogo na akasimama mbele yake wakawa wanaangaliana uso kwa uso
"Nikuambie kitu kimoja mbogo wewe bado ni mdogo sana kwangu mimi na hata cheo chako hunifikii hata kidogo hivyo ninakushauri ukiache hiko kiburi chako unachoniletea maana ukijifanya mjuaji sana itakukosti" aliongea kwa sauti nzito rpc nzige huku akimtazama Inspector mbogo
"Nikuambie ukweli tu bwana nzige mimi sikuogopi hata kidogo na usifikiri unaweza kuniendesha unavyotaka wewe" alijibu Inspector mbogo
"Well well well sawa mr fredrik mbogo tutaona kati ya mimi na wewe nani ni mkubwa kwa mwenzake" aliongea RPC huku akipiga makofi ya kejeli
"Tutaona" alijibu Inspector mbogo na akatoka ndani ya ofisi hiyo ya RPC Nzige huku akiwa na hasira kali sana na mkuu wake huyo
ITAENDELEA
Comments