SIMULIZI:THE REVENGE OF DERICK
MTUNZI:WIZZY JOOH
FACEBOOK:STORY ZA JAY
****SEHEMU YA TANO(5)****
ILIPOISHIA
"Well well well sawa mr fredrik mbogo tutaona kati ya mimi na wewe nani ni mkubwa kwa mwenzake" aliongea RPC huku akipiga makofi ya kejeli
"Tutaona" alijibu Inspector mbogo na akatoka ndani ya ofisi hiyo ya RPC Nzige huku akiwa na hasira kali sana na mkuu wake huyo
SONGA NAYO
Inspector mbogo alitoka ndani ya kituo hiko cha polisi na akaelekea alipolipaki gari lake akapanda na kuondoka mahali hapo kwa kasi
Safari yake iliishia bunju ilipo nyumba yake akapiga honi na mlinzi akamfungulia geti na akaliingiza gari lake kisha akashuka na kuingia ndani ya nyumba yake
Alimkuta mke wake(Maria) akiwa amekaa kwenye sofa anaangalia TV bila wasiwasi wowote
"Baby jamani mbona umerudi mapema" aliuliza Maria huku akisimama kwenye sofa alilokua amekalia na kwenda kumkumbatia Inspector mbogo
"Nimeamua tu nije nyumbani kupumzika maana kichwa kinauma sana" aliongopea Inspector mbogo huku akiwa bado amemkumbatia mke wake
"Ooh! Pole honey basi ngoja nikuangalizie dawa upunguze hayo maumivu" aliongea Maria huku akijifanya kusikitika
"Aah Usijiangaishe sana hapa nikilala kitakaa sawa" aliongea Inspector mbogo
"Basi sawa twende ukapumzike" aliongea Maria huku akimtazama mbogo usoni
"Sawa hivi Derrick yupo wapi?" Alihoji Inspector mbogo
"Ametoka ila kaniambia atarudi muda sio mrefu" alijibu Maria huku akitangulia mbele kwenda chumba huku Inspector mbogo akifata kwa nyuma na alikua anayaangalia makalio ya Maria yalivyo makubwa na akajikuta akimeza mate ya uchu
⭐⭐⭐⭐
Derrick alifika ununio na alisimamisha gari yake mbali kidogo na jumba lilikokuwepo mbele yake akazima gari hiyo kisha akashuka na kuanza kulisogelea jumba hilo
Alipofika akalitazama geti kubwa la jumba hilo vizuri kisha akayapeleka macho yake juu ya fensi ya nyumba hiyo na akaziona nyaya za umeme akatabasamu kisha akarudi nyuma mita kadhaa na akakimbia kwa kasi alipofika karibu na fensi hiyo akadunda na kuruka sarakasi na akatua ndani ya jumba hilo huku akiwa hajaguswa na nyaya hata moja
Derrick akayaangaza macho yake kushoto na kulia na hakuona mtu yoyote kisha akatazama mbele na kuiona nyumba ya kifahari sura yake ikakunja ndita baada ya kuiona bembea iliyokua eneo hilo
"Nitawaua wapuuzi wote waliodhurumu uhai wa wazazi wangu pamoja na mdogo wangu" aliongea kwa uchungu Derrick kisha akaanza kupiga hatua kuisogelea nyumba hiyo
Alifika hadi mlangoni akataka kushika kitasa lakini akasita na akaitazama mikono yake kisha akatoa groves kwenye mifuko ya Suruali yake na kuzivaa mikononi
Akatoka mlangoni hapo na akalisogelea dirisha kubwa lililopo karibu na mlango akalifungua dirisha hilo la kioo na akaingia ndani ya nyumba hiyo kupitia dirishani hapo
Akayatazama mandhari ya nyumba hiyo na kujikuta akishindwa kuyazuia machozi yasitoke kwenye macho yake
Akaisigelea picha kubwa iliyobandikwa ukutani sebuleni hapo na akawa anawaangalia watu waliokuwepo kwenye picha hiyo kwa uchungu
Kwenye picha hiyo walionekana wazazi wa Derrick wakiwa pamoja na doris na Derrick mwenyewe
"Nisipolipiza kisasi kwa ajili yenu hakika nafsi yangu haitokaa ipate amani milele kwahiyo ni lazima nilipe kisasi na nitawaua wote waliohusika" aliongea Derrick huku akilia kwa uchungu mkubwa sana
ITAENDELEA
Comments