Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

SIMULIZI:THE REVENGE OF DERICK 

MTUNZI:WIZZY JOOH 

FACEBOOK:STORY ZA JAY 

 

****SEHEMU YA SITA(6)*****

 

ILIPOISHIA

"Nisipolipiza kisasi kwa ajili yenu hakika nafsi yangu haitokaa ipate amani milele kwahiyo ni lazima nilipe kisasi na nitawaua wote waliohusika" aliongea Derrick huku akilia kwa uchungu mkubwa sana 

 

SONGA MBELE 

Derrick akaacha kuitazama picha hiyo na akaelekea kwenye moja ya chumba kilichopo ndani ya nyumba hiyo

 

Alipoingia ndani ya chumba hicho kikubwa akayaangaza macho yake pande zote za chumba hicho kisha akaisogelea picha ndogo ambayo walipiga baba yake na mama yake picha hio ilikua imewekwa kwenye frame na kutundikwa ukutani

 

Derrick alipoifikia picha hiyo akaweka mkono wake kwenye picha hiyo kisha akarudi hatua kadhaa 

 

Derrick baada ya kuigusa picha hiyo eneo la chini vilisikika vyuma vikisagana na baada ya muda mfupi aridhi ilifunguka na likatokea shimo la duara 

 

Derrick akalisogelea shimo hilo na akaanza kuingia kwa kutumia ngazi zilizopo pembezoni mwa shimo hilo

 

Baada ya muda mfupi alifika chini ya handaki hilo ambapo taa kubwa zilikuwa zikiwaka na kutoa mwanga mkali kiasi cha kuvifanya vitu vilivyomo ndani ya handaki hilo kuonekana vizuri kabisa

 

⭐⭐⭐⭐⭐

 

Ndani ya mjengo mmoja mkubwa uliopo maeneo ya ostabay wanaonekana watu watatu wakiwa wamekaa kwenye masofa ya kifahari na wakijadili jambo fulani 

 

"Kwahiyo umesema huyo Inspector wako amesema hatoacha kuifatilia kesi ya mauaji ya afande Frank mbogo" ilikua ni sauti ya mwanamama aliyekuwa amevalia mavazi ya gharama sana

 

"Ndio mkuu Inspector mbogo amegoma kabisa kuacha kuifatilia hii kesi na anaonyesha kujiamini sana na sijui ni kwanini" alijibu RPC Nzige huku akimtazama mwanamama huyo

 

"Inakuwaje unasumbuliwa na Inspector wa polisi bwana nzige" aliuliza mzee mwengine aliyekuwa mahali hapo

 

"Sio kwamba namuogopa mr Alex ila mimi nahisi huyu Inspector kuna mtu mkubwa yupo nyuma yake ndio maana anajiamini kupita kiasi" aliongea RPC huku akimuangalia mzee Alex aliyekaa kimya anamsikiliza kwa umakini

 

"Kuhusu huyo askari wewe Ondoa shaka tutadili nae Sisi wenyewe chamsingi unatakiwa kuhakikisha unaufuta ushahidi wote wa afande Frank kuhusu biashara yetu sisi" aliongea mwanamama huyo anayejulikana kwa jina la madam juliet 

 

"Sawa mkuu nimekuelewa" alijibu Rpc Nzige huku akinyanyua grasi yenye pombe ndani na wote watatu kwa pamoja wakagongesha grasi zao huku wakicheka sana 

 

⭐⭐⭐

 

"Huyu Derrick atakuwa wapi mbona mpaka saa hizi hajarudi na nimempigia lakini simu yake haipatikani" aliongea Inspector mbogo huku akimtazama mke wake na walikuwa mezani wakipata chakula cha usiku

 

"Aah baby na wewe unakua na wasiwasi utafikiri Derrick ni mtoto vile" alijibu Maria huku akiendelea kula pilau lake

 

"Maria hofu ni lazima niwe nayo kwasababu hali ilivyo sasa hivi Derrick hapaswi kukaa nje ya nyumba hadi sasa hivi" aliongea Inspector mbogo huku akinyanyuka kwenye kiti cha mbao alichokalia

 

"Sasa unaenda wapi" aliuliza Maria huku macho yamemtoka kama mjusi aliyebanwa shingo na mlango 

 

"Naenda kumtafuta mwanangu" alijibu Inspector mbogo 

 

"Mhh" aliguna Maria kisha akaendelea zake kula huku asiwe hata na hofu yoyote ile 

 

Inspector mbogo akatoka chumbani kwake huku akiwa ameshika funguo ya gari mkononi na alipofika sebuleni akamuangalia Maria ambaye alikua bize na kutafuna paja la kuku 

 

Alisikitika kwa kutingisha kichwa chake kisha akatoka ndani ya nyumba yake hiyo na akapanda kwenye gari kisha akaingia mtaani kumtafuta Derrick huku akiwa hajui kabisa aanzie wapi

 

⭐⭐⭐⭐

 

Maria baada ya kuona Inspector mbogo ametoka akanyanyuka kwenye kiti kisha akaingia chumbani na akachukua simu yake akaiwasha kisha akabonyeza namba kadhaa na akaipigia bamba hiyo

 

"Vipi kisu mbona hunipi taarifa zozote za kazi niliyokupa au tayari mmemuua" aliongea Maria kwa sauti ya wasiwasi kidogo 

 

"Mkuu huyo mtu wako amewasababishia kina shabani ajali na maetokomea kusikojulikana" aliongea kisu kwa ghadhabu kubwa huku akionekana kuwa na hasira na Derrick 

 

"Nini unasema kawasababishia ajali kina shabaniii" alihamaki Maria huku akiwa hayaamini maneno ya kisu kwani yeye alimchukulia Derrick kama kijana asiyejua lolote kuhusu kupigana

 

ITAENDELEA

Previoua Next