SIMULIZI:THE REVENGE OF DERICK
MTUNZI:WIZZY JOOH
FACEBOOK:STORY ZA JAY
****SEHEMU YA SABA(7)*****
ILIPOISHIA
"Mkuu huyo mtu wako amewasababishia kina shabani ajali na maetokomea kusikojulikana" aliongea kisu kwa ghadhabu kubwa huku akionekana kuwa na hasira na Derrick
"Nini unasema kawasababishia ajali kina shabaniii" alihamaki Maria huku akiwa hayaamini maneno ya kisu kwani yeye alimchukulia Derrick kama kijana asiyejua lolote kuhusu kupigana
SONGA MBELE
"Ndio mkuu huyo dogo amesababisha hadi wenzangu wameumia na sasa hivi wapo hospitali yani nina hasira nae kinoma yani" alijibu kisu kwa sauti yake nzito na ya kutetemesha
"Aarggggg! mtafuteni na mumteke mpeni mateso ya kutosha mbwa huyo" aliongea kwa hasira Maria huku akiwa ametumbua mimacho yake
"Sawa mkuu Hesabia kazi imeisha" aliongea kisu kwa kujiamini na hata asijue huyo mtu anayetakiwa kumteka ni wa aina gani
"Mshenzi kabisa huyu kenge" aliongea Maria huku akiwa ameshaikata simu yake na akaiweka chini
Lakini simu yake inaita tena anaichukua kisha anaangalia jina la mtu aliyempigia na anabofya kitufe cha kupokea
"Shangazi" anaita Maria baada ya kuipokea simu hiyo
"Usiku wa Leo nataka huyo Inspector awe ameshakufa Maria " ilisikika sauti ya madam juliet upande wa pili wa simu ya Maria
"Sawa shangazi" aijibu Maria na simu ikakatwa
Maria akabonyeza namba kadhaa kisha akazipiga na simu ikaita na baada ya sekunde kadhaa ikapokelewa
"Mbogo anatakiwa kuuawa usiku huu kwahiyo andaa watu wako na waingie mtaani kumtafuta maana hapa nyumbani ametoka" aliongea Maria kisha akakata simu hiyo na akairusha kwenye kitanda kisha yeye akaingia kwenye bafu lililopo ndani ya chumba hiko
⭐⭐⭐
Inspector mbogo alikua barabarani kuelekea kwenye klabu moja iliyo maeneo ya boko basihaya na huko alikua akienda kumtafuta Derrick kwani ni sehemu ambayo Derrick alikua akiipenda sana
Lakini akiwa anaendelea na safari yake hiyo anagundua kuwa kuna gari ipo nyuma yake inamfatilia na kabla hajakaa sawa anamuona mtu aliyevalia bushori akijitokeza kwenye dirisha la gari hiyo inayomfatila na akaanza kumshambulia kwa risasi
Hapo Inspector mbogo anaamua kuongeza spidi ya gari yake ili watu hao wasiweze kumdhuru
Watu hao nao wanaongeza kasi ya gari yao na walikua wakiendelea kumshambulia Inspector mbogo kwa risasi mfululizo na walifanikiwa kuitoboa tairi ya gari la polisi huyo
Gari ya Inspector mbogo ikayumba yumba na mwisho wa siku ikaenda kuparamia mti mkubwa uliopo pembezoni mwa barabara
Majambazi hao wanne wakashuka kwenye gari yao na wakaisogelea kwa tahadhari gari na walipoifikia mmoja wao akafungua mlango wa mbele wa dereva
Na akajikuta akitumbua macho kwa mshangao baada ya kutomuona Inspector mbogo kwenye siti ya dereva
Anayaangaza macho ndani ya gari hiyo lakini bado hamuoni polisi huyo ambaye wamepewa agizo la kuuondoa uhai wake ndani ya usiku huu
Anatoa kichwa nje na kuwatazama wenzake wanaomtazama yeye kisha anapeleka kichwa kulia na kushoto akimaanisha kwamba ndani ya gari hiyo hakuna mtu yoyote
Lakini wakiwa wanaendelea kushangaa shangaa ghafla mmoja wao anaanguka chini baada ya mguu wake kuvutwa na mtu aliyekuwa chini ya uvungu wa gari hiyo
Wenzake wanapigwa na butwaa baada ya kumuona mwenzao ameanguka chini kama furushi na kabla hawajajua ni kitu gani kilichomuangusha mwenzao wanashangaa kuona mtu akichomoka Chini ya gari kwa kasi ya ajabu na akaanza kuwashambulia kwa mapigo mazito mazito yaliyowapeleka wote chini kwa dakika tatu tuuu
Inspector mbogo akawatazama majambazi hao kisha akachuchumaa na akawavua mabushori waliyoyavaa na akafanikiwa kuziona sura zao
"Hawa sijui ni kina nani tena" alijiongelea Inspector mbogo huku akiwapiga picha majambazi hao na alivyomaliza kuwapiga picha akalitazama gari lake lililobonyea upande wa kushoto baada ya kujibamiza kwenye mti huo
Akaiangalia simu yake na akapiga simu kituo cha polisi na akawaita polisi waje eneo hilo upesi
⭐⭐⭐
Derrick ndio alikua akitoka ndani ya nyumba yao ambayo wazazi wake walikua wakiishi na kwenye mkono wake wa kulia alikua ameshika kamera ndogo huku mkono wa kushoto akiwa ameshika file lenye rangi nyeusi
Alitoka ndani ya nyumba hiyo na akapanda gari lake kisha safari ya kurudi nyumbani kwa baba yake mdogo ikaanza huku akiwa hajui kabisa kama bamdogo wake amenusurika na kifo
ITAENDELEA
Comments