SIMULIZI:THE REVENGE OF DERICK
MTUNZI:WIZZY JOOH
FACEBOOK:STORY ZA JAY
****SEHEMU YA NANE(8)****
ILIPOISHIA
Derrick ndio alikua akitoka ndani ya nyumba yao ambayo wazazi wake walikua wakiishi na kwenye mkono wake wa kulia alikua ameshika kamera ndogo huku mkono wa kushoto akiwa ameshika file lenye rangi nyeusi
Alitoka ndani ya nyumba hiyo na akapanda gari lake kisha safari ya kurudi nyumbani kwa baba yake mdogo ikaanza huku akiwa hajui kabisa kama bamdogo wake amenusurika na kifo
SONGA MBELE
Derrick alifika nyumbani kwa baba yake mdogo akapiga honi na akafunguliwa geti na mlinzi akaliingiza gari lake ndani na akaenda kulipaki kisha akashuka na akaingia ndani ya nyumba ya bamdogo wake
Sebuleni hakumkuta mtu yoyote yule akaitazama saa yake na akaona ni saa tano na dakika kumi na sita (23:16) akaenda kuizima TV iliyokuwa honi kisha akapandisha ngazi kuelekea kwenye chumba chake kilichopo gorofani na alipofika akafungua mlango akaingia ndani na akajibwaga kwenye kitanda chake kikubwa na usingizi ukampitia
⭐⭐⭐⭐
Maria alikuwa chumbani kwake amekaa kitandani na laptop yake na alikuwa akimtazama Derrick kwa kupitia CCTV Camera zilizokua kwenye jumba hilo
Maria akatabasamu kwa dharau kisha akaichukua simu yake na akampigia kisu na simu iliita kwa muda mfupi na kupokelewa
"Ndio mkuu" ilikua ni sauti ya Kisu iliyosikika upande wa pili wa simu
"Chukua kikosi chako na moja hapa nyumbani huyu mpuuzi kajileta" aliongea Maria kwa madaha
"Dakika sifuri mkuu tutakuwa tayari tupo hapo" kisu aliongea kwa kujiamini na Maria akakata simu hiyo kisha akawapigia watu wake aliowapa kazi ya kumuua Inspector mbogo
"Hawa wapuuzi mbona hawapokei simu aah" alilalamika Maria baada ya kuona simu inaita muda mrefu bila kupokelewa na akaamua kupiga tena
⭐⭐⭐
Inspector mbogo alikua ndani ya difenda ya polisi na walikuwa wakiifata ambulance iliyobeba maiti za watu aliowauwa kwa nyuma
Inspector mbogo yeye ndio alikua amechukua simu ya jambazi aliyejaribu kumuua na akaiweka simu hiyo kwenye mfuko wa mbele wa Suruali yake
"Bosi Marry" Inspector mbogo alilisoma jina la mtu aliyekuwa akipiga kwenye simu hiyo na hakuipokea akaiacha hadi ikakatika
Lakini wakati akiwa anataka kuirudisha simu hiyo mfukoni akasikia tena simu hiyo ikiita hivyo akaghailisha kuirudisha mfukoni na akaangalia jina la mpigaji na akuta ni yule yule boss marry akapokea na kuiweka sikioni
"Nyinyi vipi mbona nawapigia hampokei" ilisikika sauti upande wa pili wa simu ikifoka na sauti hiyo ikamfanya mbogo aduwae sana
"Haloo nyinyi wapuuzi mbona hamuongei" Inspector mbogo aliisikia tena sauti hiyo ya mwanamke akifoka
"Mariaaaaa" aliita kwa kuhamaki Inspector mbogo na simu hiyo ikakatwa haraka sana
ITAENDELEA
Comments