Reader Settings

SIMULIZI:THE REVENGE OF DERRICK

MTUNZI:WIZZY JOOH

FACEBOOK:STORY ZA JAY

 

***SEHEMU YA KUMI(10)***

 

ILIPOISHIA

Lakini kabla inspector mbogo hajajibu chochote wanasikia milio ya risasi nje ya nyumba yao hivyo kwa pamoja wanakimbilia dirishani na kuchungulia nje

Hapo wanawaona watu saba waliovalia mabushori usoni wakiwamalizia kuwaua mapolisi waliokuja na inspector mbogo

 

SONGA NAYO

Mlinzi anaongea na watu hao na anaonekana kuna kitu anawaelekeza 

 

Baada ya kama dakika mbili za maongezi kati ya mlinzi na watu hao wanaanza kuisogelea nyumba ya inspector mbogo

 

"Derrick tafuta sehemu ujifiche nataka kuwashughulikia hawa watu" inspector mbogo aliongea kwa sauti ya chini huku akimtazama derrick anayelisogelea kabati lake lililopo chumbani humo

 

"Hakuna kitu kama hicho mzee wewe tulia hapa nikuoneshe huu mchezo unachezwa vipi" aliongea kwa kujiamini Derrick huku akifungua kabati lake hilo na kumfanya inspector mbogo atoe macho kwa mshamgao

 

"We..we..we..wewe hizo siraha umezitolea wapi?" Aliuliza kwa mshamgao inspector mbogo huku akizitazama siraha nyingi zilizopo kwenye kabati hilo la Derrick

 

"Maswali baadae huu ni muda wa kazi" alijibu Derrick huku akichukua bunduki mbili ndogo na kuzichomeka kwenye kiuno chake kisha akachukua na visu viwili vidogo (daggers) na akaviweka chini na akachukua shati lake na kulivaa kisha akaviokota visu vyake na kumtazama baba yake mdogo

 

"Vipi mzee" aliuliza Derrick huku akatabasamu na hakutaka kumsikiliza baba yake mdogo atajibu nini akalisogelea dirisha la chumbani kwake na akachungulia nje akaona hali ni shwari hivyo akatoka ndani ya chumba chake kwa kupitia dirisha hilo la kioo lisilo na nondo

 

Derrick alishuka kwa umakini zaidi kutoka katika chumba chake kilichopo ghorofani hadi chini kabisa

 

Akaangaza huku na kule kisha akaanza kuusogelea mlango wa kuingilia sebuleni kwa umakini sana

 

Derrick aliufikia mlango huo na akaukuta upo wazi akachungulia na akawaona watu hao wakipandisha juu ghorofani kwa mwendo wa kunyata

 

Derrick akatabasamu huku akiwasikitikia wavamizi hao kwani kifo atakachokwenda kuwaua kitakua ni kibaya sana

 

Taratibu akaingia ndani na akaanza kuwasogelea watu hao kwa umakini sana 

 

Alipoona amekaa sehemu nzuri ya kuwashambulia akazitoa bunduki zake kiunoni na akazitazama kisha akaangalia SMG walizoshika majambazi hao na akazirudisha bunduki hizo akachomoa visu vyake 

 

Kwa kasi ya ajabu akawakimbilia majambazi hao ambao walijikuta wakipigwa na butwaa baada ya kumuona mtu akitokea nyuma yao na kuanza kuwashambulia kwa kasi ya ajabu 

 

Walijitahidi kumshambulia mtu huyo kwa kutumia bunduki zao lakini wakajikuta wakishindwa kumuangusha kwani mtu huyo alikuwa akihama sehemu moja kwenda nyingine kwa haraka sana hivyo wanajikuta wakishindwa kumuweka kwenye target 

 

Derrick alikuwa akiwashambulia kwa kuwakata kwenye shingo zao majambazi hao na alikuwa anahakikisha akikata basi koromeo nalo linatoka nje ya shingo

 

Derrick aliwaua kikatili majambazi hao na alionekana kuyafurahia mauaji hayo anayoyafanya

 

Alifanikiwa kuwaua majambazi wote na akabaki mmoja tu ambaye alionekana kuwa ndio kiongozi wa watu hao waliovamia kwenye nyumba hiyo ya inspector mbogo

 

Derrick akamuangalia jambazi huyo kwa macho ya dharau sana kisha akasikitika huku akikitazama kisu kikubwa alichokishika jambazi huyo na akavitazama visu vyake vilivyojaa damu kisha akavitupa chini na akaanza kumfata jambazi huyo kwa ajili ya kupambana naye

 

⭐⭐⭐⭐

 

Inspector mbogo alipiga simu kituo cha polisi na kuwaambia kwamba amevamiwa nyumbani kwake na alivyomaliza kuongea na polisi akaikoki bunduki yake na kutoka ndani ya chumba hicho cha Derrick kilichopo ghorofani

 

Alitoka kwa mwendo wa taratibu na akafika kwenye kona ambayo Derrick na kiongozi wa majambazi hao wanapigana na akachungulia 

 

Akamuona Derrick akipambana na jamaa mmoja mrefu aliyevalia bushori usoni 

 

Jamaa huyo alijitahidi kumdhibiti Derrick lakini akajikuta akishindwa kwa mapigo yake kupanguliwa na kushushiwa ngumi nzito mwilini mwake

 

Derrick hakutaka kumuonea huruma kabisa jamaa huyo na alimpiga mapigo ya kumvunja viungo na baada ya muda mfupi jamaa huyo akajikuta akilegea na kudondoka chini asiwe na uwezo wakujisogeza hata kidogo

 

Ving'ora vya gari za polisi zilisikika nje ya nyumba ya inspector mbogo na inspector huyo wa polisi akajitokeza alipokuwa amejificha na akaenda kumzuia Derrick asiendelee kumpiga jamaa huyo

 

Polisi waliingia ndani ya nyumba ya inspector mbogo na wakapanda ngazi kwa umakini wa hali ya juu huku wakiwa wamezitanguliza bunduki zao Mbele tayari kwa mashambulizi

 

Lakini polisi hao wanajikuta wakipatwa na mshangao baada ya kuona maiti nyingi zikiwa zimezagaa chini huku zikiwa zimeuwawa kikatili na inspector mbogo pamoja na Derrick walikuwa wamesimama Mbele ya maiti hizo

 

ITAENDELEA

Previoua