Reader Settings

Unaweza kurudi ulipoishia kupitia Maktaba.

Jimmy aliingia na kupokea ukaribisho kwa ishara ya kutingisha kichwa akionekana ana haraka, hakuwa na muda wa kupoteza

"Vipi bro kuna shida gani mpaka ushindwe kuoiambia kwenye simu?" Cid aloiloza akiwa na shauku ya kujua kilichomleta hapo

"Nahitaji gari lako" Jimmy aliongea

"Hilo tu? Mbona ungesema kwenye simu tu ingeeleweka ningekuandalia mazingira kabla hujafika"

"Haina haja pia nahitaji kingine kutoka kwako"

"Kipi hiko?"

"Nahitaji...... " aliongea Jimmy kwa sauti ya kawaida huku akiiacha sentensi ielee na kufanya ishara flani mkononi jambo lililomshtua Cid

"Bro unataka bastola? Ebu kuwa serious bro kwanza mimi naitolea wapi Usiniambie unataka kufanya uhalifu" 

"Huna haja ya kuwa na wasiwasi siendi kuua mtu ni kutishia amani tu kuna kenge zinaleta mazoea" Jimmy aliongea hakutaka kufunguka sana kuhusu jambo lililomtokea

"Hata kama kuna watu wamekuchokoza hutakiwi kwenda mbali hivyo"

"Kwahiyo unasemaje bro? "

"Hapana bro sio kama nakataa sina hicho unachokitaka mimi ni mfanya biashara na sio polisi" 

"Ishu sio wewe kuwa nayo ishu ni unaipataje"

"Unamaanishaa...." aliongea akiishia njiani baada ya kugundua kitu

"Ndio, hao walinzi weko si wana vibali vya kumiliki siraha ya moto unachopaswa ni kuwaazima tu sidhani kama watakukatalia bwana mdogo" aliongea jimmy akitoa tabasamu

°°°°°°°°°°

Muda mchache baadae Jimmy alionekana ndani ya gari aina ya Range rover jekundu siti ya dereva, akiwa ndani ametulia tuli akisubiria kitu na mara simu ilianza kuita, ilikuwa ni ile simu ndogo aliyoorushiwa na yule ninja mzungu

Aliipokea na kuiweka sikioni akiwa na sura makini isiyo na masihara hata kidogo, alinyamanza kimya akisubiri kusikia sauti upande wa pili nao upande wa pili ukitegemea kusikia sauti kuanza kwake lakini wapii ni sauti ya kiyoyozi cha kwenye gari ndiyo kilisikika zaidi

Upande wa pili aliamua kuvunja ukimya

"Kijana niseme tu umenifurahisha sana sikutegemea kabisa!" ilisikika sauti upande wa pili na ilikuwa ni ya kiume tofauti na alivyotegemea Jimmy kusikia sautki ya mwanamke

"Acha kuzunguka nipe location haraka iwezekanavyo"

"Haha napenda sana watu aina yako kijana yaani ni 'direct' sana hakunaga longolongo"

"Nikuonye tu nikikuta hata alama ya mchubuko kwenye mwili wa ndugu zangu Naapa utakiona kifo ni bora kuliko kuishi"

"Usiwe na wasiwasi kijana japokuwa tumewateka ndugu zako ila tunaheshimu sana wanawake fata location niliyokutumia" aliongea mwanaume wa upande wa pili

"Nataamini vipi kama mpo na familia yangu na kama wako salama?" aliongea Jimmy na kipya kilifata kwa muda kisha sauti yenye ikasikika

"Kaka..... Kaka tumetekwa tusaidi.. ee" ilikuwa ni sauti iliyoambatana na kilio nauoga

"Monica uko sawa? mama yuko sawa?" Jimmy alikurupuka baada ya kusikia sauti ya dada yake na kuuliza maswali

"Niko.... Mama..."

"Hello.... Hello.. Hello??" jimmy aliongea kwa nguvu baada ya sauti ya dada yake kukoma

"Nadhani sasa umeshadhibitisha kile ulichokuwa na shaka nacho" 

"Amini nakwambia wewe mpuuzi umegusa sehemu ambayo hukutakiwa kugusa" Jimmy alifoka kwa hasira na baada ya kumalizia sentensi tu simu ilikata na ujumbe kuingia na baada ya kuusoma ulikuwa ukimuelekeza mahali anapotakiwa kufika huku ujumbe ukisisitiza kwamba anapaswa kwenda mwenyewe vinginevyo hataiona familia yake kamwe

Baada ya kumaliza kuusoma ujumbe huo aliangalia pembeni kwenye siti ya abiria kulikuwa na bastola nyeusi aina ya Glock 17  generation 5,ni toleo la mwaka 2017

Ni siraha inayotumia 9mm bullet(size ya risasi) na inabeba jumla ya risasi 17 ambapo bastola nyingi hazifiki idadi hiyo, kama haitoshi kuna "extended magazines" zenye idadi 33 za risasi. Tukiongelea kuhusu reliability Glock hai-jamm Unaweza kuiangusha kwenye matope, mchanga, hata kwenye maji, na bado itafanya kazi kama kawaida. Ndiyo maana jeshi, polisi, na hata special forces wanaiamini.

Frame yake imetengenezwa kwa "polymer" hivyo kufanya kuwa nyepesi na imara isiyo na uzito wa kukuelemea, kingine ni kuhusu mfumo wake, Glock 17 ina mfumo wa "Safe Action System"  yaani ilimradi unakaza trigger inafanya kazi bila stress ya system nyingine sijui kukoki na risasi husafiri hadi mita elfu moja(1000 meters) 

Jimmy baada ya kuikodolea macho alisafisha koo na kunyosha shingo lake vizuri na kuwasha gari na kuliondoa kwa kasi maeneo hayo

°°°°°°°°°°

MILITARY HEADQUARTERS TPDF (Tanzania People'sDefenseforce))

Makao makuu ya jeshi la taifa nchini Tanzania lipatikanalo maeneo ya Upanga jijini dar es salaam, ndani ya uzio mkubwa wenye ulinzi mkali sana kulikuwa na majengo mbalimbali ya jeshi walionekana wanajeshi wakiwa katika majukumu yao waliyopangiwa

Kwenye jengo moja lenye ulinzi mkali kuzidi maeneo yote,Ndani ya ofisi ya mkuu wa majeshi ya ulinzi alionekana mzee ameketi kwenye kiti cha heshima pamoja na mzee mwingine pia,walikuwa ni majenerali

Ilikuwa ni ofisi kubwa sana yenye kila kinachoitajika ili kuitwa ofisi ya mkuu wa majeshi ya nchi ya Tanzania

Katika kiti hiko cha heshima Aliyeketi alikuwa ni Jenerali John Merizasta akiwa ndiyo mwenye umri kati ya miaka sitini na tano kwenda sitini na nane akiwa amevalia gwanda iliyochafukwa na vyeo vingi pamoja na kofi yenye beji la dhahabu huku upande wa pili uliomtenganisha na meza kubwa ya ofisi aliketi Luteni Jenerali Omary  Mwachitete akiwa wa pili kicheo naye akivalia gwanda lake la heshima lenye vyeo vingi pamoja na kofia yenye beji la dhahabu

Walikuwa katika hali ya utulivu wakizungumza mawili matatu kuhusu mambo ya jeshi na usalama wa nchi kwa ujumla

Wakati wakiwa katika mazungumzo ya kina ghafla sauti ya mlango kugongwa ilisikika na Jenerali Merizesta aliruhusu mgongaji kuingia

Mlango ulifunguliwa na aliingia mwanajeshi wa kiume umri wa makamo aliyevalia kombati mwenye cheo cha kanali, baada ya kuingia alitoa heshima kwa wakubwa zake kupiga salute

"Unaweza kunipatia taarifa kanali" aliongea Jenerali Merizesta alionekana kutegemea ujio wa kanali

"Ndio ndio Mkuu nimefanya kama ulivyoagiza hili ndilo faili lenye taarifa kamili" alijibu kanali huyo na kumpatia Jenerali faili hilo kwa heshima

"Sawa kanali unaweza kwenda" Aliongea Jenerali Merizesta baada ya kupokea na kumpa ishara ya kuondoka. Kanali huyo alitoa heshima yake kwa wakuu na kutoka

Jenerali alifungua faili hilo ambalo ndani yake kulikuwa na picha ya mwanaume kijana na taarifa zake kamili

"Huyu kijana ameikoa familia yangu" aliongea jenerali akimwambia luteni mara baada ya kumaliza kupitia taarifa hizo

"Unamaanisha yule kijana aliyewaokoa wanao kutoka mikononi mwa adui" Luteni jenerali aliuliza

"Ndio ndio lakini inashangaza taarifa zake ni raia wa kawaida tu, anaitwa Jimmy Julian Jairo ana miaka ishirini na mbili(22) amemaliza kidato cha sita mwaka huu na ana subiri kuanza elimu ya Chuo" Aliongea Jenerali Merizesta ilionekana alikuwa amepata taarifa kuhusu tukio la kujaribu kuwauwa watoto wake lakini hakuweza kufika nyumbani kutokana na majukumu ya kijeshi

"Hata hivyo ni Jambo la kushukuru pengine bila yeye wanao wangekuwa marehemu sasahivi"

"Hilo nashukuru sana ila huoni hili jambo lina mashaka ndani yake? Mtu wa kawaida asiye na rekodi yoyote kuweza kudhibiti majambazi wanne wenye siraha ambayo ni kazi ya walinzi wenye mafunzo na uzoefu lakini wameshindwa" aliongea Jenereli akimpatia faili Luteni Jenerali

"Haishangazi sana isitoshe baba marehemu yake pia alikuwa mwanajeshi pengine alimjenga mwanae kwenye mazingira kama haya" aliongea Luteni jenerali baada ya kumalizia kusoma faili na kugundua kitu

"Unataka kusema......." aliongea Jenerali akiishia njiani

"Ndio ukiangalia jina la baba yake unakuta ni Julian Jairo rafiki yetu aliyefariki miaka 15 iliyopita, Unamsahauje mtu muhimu kama yule ndani ya jeshi letu?" aliongea Luteni Jenerali na kumfanya sasa Jenerali kurejewa na kumbukumbu

"Asee uzee unanitafuna vibaya mno mambo ni mengi sana kiasi cha kusahau" aliongea Jenerali

"Unazingua sana mzee mwenzangu bila yeye nadhani tusingefika hapa tulipo" aliongea Luteni Jenerali

"Sema yule muhuni hakutuambia kama ana familia" aliongea Jenerali

"Yeah nilishangaa niliposikia jina lake ila inabidi tupate taarifa pia ili kudhibitisha itoshe kusema alijua kutuficha" Luteni Jenerali alidakia

"Hahaha si alisifika sana kwa kutunza siri ndio maana aliaminiwa sana na wakubwa kipindi kile lakini jambo la kusikitisha hatunaye tena"

°°°°°°°°°°

Muda ulikuwa umeenda sana na mpaka kufikia wakati huo saa ilisoma saa kumi na mbili dakika kumi tano, angani kulikuwa na wingu zito jeusi ikionyesha dalili ya mvua

Lilionekana gari jekunde maeneo hayo ya bagamoyo likikatiza sehemu isiyo na dalili ya watu kuishi wala mnyama kuonekana akipita

Ilikwenda kusimama sehemu yenye uwanja mkuubwaaa na Jimmy alishuka nje ya gari na kwenda kusimama mbele ya boneti la gari mkononi akishikilia kitabu. 
Kwasababu ya giza na eneo hilo kutoonekana nyumba yoyote wala kifaa chochote cha umeme aliacha taa za mbele ya gari kumulika

Sekunde si nyingi zilisikika ngurumo la gari zikikaribia eneo hilo na kweli zilionekana gari nne nyeusi zote zikiwa SUVs na zilikwenda kusimama mbele ya macho ya Jimmy umbali kama wa mita thelathini hivi

Milango minne yote ya magari yale ilifunguliwa na walishuka watu kumi na nane wawili wakiwa ni ndugu zake jimmy mama yake na dada yake wamefungwa kamba mikononi na vitambaa machoni wasiweze kuona, wengine wote walikuwa ni raia wa kigeni wanaume kwa wanawake wakivalia nguo rangi tofaut-tofauti

"BOOM! BOOM... BROOOM!" sauti ya radi pamoja na mwanga mweupe ulimulika na mvua ilianza kunyesha 

"Hatimae umefika kijana, mwisho wa siku udhaifu mkubwa kwa binadamu ni familia" aliongea mwanaume chotara mwenye asili ya kiarabu na kizungu kwa lafudhi mbovu

"Nimeshafanya kama mlivyotaka waachieni ndugu zangu" aliongea Jimmy

"Usiwe na wasiwasi kijana umefanya jambo zuri kuleta hiko kitabu hivyo tukabidhi ndipo tuwaachie" 

"Nitaamini vipi maneno yako kama ni ya kweli naomba muwaachie kwanza ndipo niwape kitabu chenu isitoshe sina mpango wa kutoroka hapa" aliongea Jimmy na kumfanya mwanaume yule kutabasamu

"Kama nilivyosema kabla huwa naheshimu sana wanawake...." Aliongea mwanaume yule akiwapa ishara vijana wake wawili wasogee mpaka karibu na Jimmy wakiwa na ndugu zake kufanya mabadilishano na ndivyo ilivyokuwa Jimmy aliwakabidhi kitabu nao walimkabidhi ndugu zake

Jimmy baada ya kuwapokea mama na dadaye aliwafungua kamba na mikono na mara baada ya mama yake kumuona Jimmy ndiye aliyekuja kuwaokoa alitokwa na machozi ambayo hayakuonekana vizuri kwasababu ya mvua

"Mwanangu.....um..." 

"Hapana mama huu sio wakati sahihi wa kuongea tutaongea tukiwa mahali salama" Jimmy alimzuia mama yake asiongee zaidi

"Monica unaweza kuendesha gari?" Jimmy aliuliza na Monica alitingisha kichwa kukubaliana nae, naye Jimmy alimpatia funguo 

"Ondoka mahali hapa uende mbali na hapa mpaka uhisi upo salama"

"Vipi kuhusu wewe?"

"Wewe fanya kama ninavyokwambia... Ondoka mahali hapa, kuhusu mimi msijali nitatafuta namna ya kutoka hapa" aliongea Jimmy akiwafungulia mlango wa gari nao hawakuwa tayari kuondoka lakini Jimmy aliwalazimisha mpaka kuingia na kuondoka mahali hapo wakimuacha peke yake akiwasindikiza na macho mpaka walipotokomea hapo

"Ooh ni upendo ulioje, Inaonekana tayari ulishajua hatutakuruhusu uondoke hapa haha unanifurahisha sana kijana" aliongea mwanaume yule ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo la watu kumi na tano wanaume kwa wanawake, walikuwa miili iliyoonyesha wamepitia mazoezi makali sana na mafunzo

Jimmy aliishia kutoa tabasamu lenye uovu ndani yake alijiambia leo lazima atoke na roho zao wote, alijiambia kama kuua ni dhambi mbona dhambi anazo nyingi tu, Ieleweke kwamba jimmy katika maisha yake hakuwahi kutoa uhai wa mtu zaidi ya kushuhudia watu wakifa mbele ya macho yake na siku hio ndio ilikuwa mara ya kwanza kwenda kutekeleza mauaji, kama ni kwenda motoni siku ya kihama kwasababu ya hiyo dhambi alishaikubali hatima hio isitoshe hata kama asipoua motoni kunamuhusu kama kawaida. Kuna watu wengine hawafai kuwepo kwenye uso wa dunia ili kutosababisha matatizo zaidi

"wapuuzi kama nyinyi ndiyo mnatusababisha tuingie dhambini baada ya toba ya muda mrefu" aliongea Jimmy ambaye alikuwa ameloa chapachapa macho yake yakiwa serious

Interesting. You’re either fearless… or foolish. I just want to see how you defeated that bitch" aliongea mwanaume yule na kutoa ishara kwa vijana wake tayari kwa pambano

Kufumba na kufumbua maninja hawa hapa mbele ya macho ya Jimmy ulikuwa ni mshikemshike patashika nguo kuchanika, mapambano kwenye mvua weuweeee!! Ilikuwa ni hatari na nusu. Jimmy alikuwa akijitahidi sana kupangua mapigo na kushambulia lakini safari hii haikuwa rahisi kwake maninja hao walikuwa ni wabobezi zaidi ya wale wa mwanzo

Walikuwa wakitumia mbinu ya Shadow step na mbinu nyingine za kininja walikuwa kama wanapoteapotea na kuibuka angle tofauti tofauti kilichomsaidia jimmy ni mafunzo yake ya hisia vinginevyo angekuwa amejeruhiwa vibaya sana

Mapambano yaliendelea ndani ya dakika kadhaa na Jimmy aliona sasa asipofanya kitu muda si mrefu anaenda kuitwa Marehemu.


TO BE CONTINUED...............

Previoua Next